Rombo wanaume walalamika madume ya nyani kushika shika wake zao

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Wanaume wilaya ya Rombo walalamika madume ya nyani kushika shika wake zao bila ridhaa yao.

Wakuu sikilizeni wenyewe.

=====
Wanaume wanaoishi pembezoni mwa Mto Mlembea, Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro wamelalamika wake zao kuvamiwa na nyani wa kiume na wakati mwingine kuhatarisha usalama wao.

Wamesema nyani hao wamekuwa ni tishio kwa wake zao na watoto na kwamba wakati mwingine huwavamia wakiwa mashambani, kuiba watoto wadogo wa kike na wakati mwingine wakitaka kuwabaka.

Pamoja na uvamizi huo wa nyani, wamesema nyani hao wamekuwa wakiingia ndani na kula vyakula, kula mifugo na hata mazao yaliyopo mashambani hali ambayo imewafanya kutelekeza mashamba yao wakihofia mazao yao kuliwa.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Ijumaa Septemba 29, 2023 katika Kijiji cha Samanga kilichopo kata ya Kirongo Samanga wilayani humo, wananchi hao walimtaka Mbunge wa Rombo, Profesa Adolf Mkenda ambaye alikuwa kwenye mkutano huo kuwaondoa kwenye makazi ya wananchi na kukwepa usumbufu huo.

Akijibu kero hiyo ya wananchi Profesa Mkenda ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia alisema hajaridhika na uondoaji wa nyani katika maeneo ya wananchi kwa kuwa bado ni wengi na wamekuwa kero kwa wananchi.
 
Serikali itangaze wazi kwamba Rombo ni wilaya ya wanawake watupu na itoe ruhusa wanaume twende huko tukanyooshe mambo.

Wanipe kata moja, yoyote alieko ndani ya kata yangu namchakata.

Wanawake wa Rombo wanapata shida sana na changamoto nyingi.
 
Wanatakiwa wawe wanavaa suruali hawa jamaa wa rombo niaje aiseee wanashindwa kushauri wake zao 😄
 
Hao ni nyani tunaowajua au ni kitu kingine? Yaani mwanamke unashikwashikwa na mnyama na umetulia tu
 
Kilimanjaro kuna aina zote za apes. Wapo mbega, kima, tumbili, nyani na sokwe. Kuna shule moja iko moshi vijijini kunapokuwa hakuna wanafunzi shuleni tumbili na nyani wanaingia madarasani kutafuta chochote cha kula walichoacha wanafunzi. Wakikosa cha kula wanachanachana madaftari ya wanafunzi waliyoyaacha darasani. Hawaachi kuja shuleni wananusa na kujua kuna mahindi na maharage yapo stoo, na kama stoo ina dirisha bovu wanashughulika nalo waingie stoo wale mahindi. Ni wabishi balaa
 
Back
Top Bottom