Rombo: Mwili wa Kijana Godwin Massawe wakutwa msituni ukiwa hautoi harufu. Wakutwa ukiwa na Rozari na Biblia

Duh humu naona kupinga tu. Kwangu mimi namuona shujaa japo mimi ni Muislam. Mungu ampe pepo. Hii ndio mifano ya kuiga. Aliipa mgongo dunia na kuipenda akhera yake (hereafter). Apumzike salama Godwin. I believe hie is in heaven gate smilling.

Unaiga nini kwa mtu kama huyu? Unaiga kusali muda wote bila kufanya kazi au kitu kingine? Huu ni uzwazwa, huyu bwana alikua na matatizo ya akili na extremist
 
Nimesoma post ya mleta mada pekee ...inawezekana hili limeshaulizwa ! Naomba kujua ni Bbilia gani hiyo yenye KITABU CHA SIRA,ambacho Marehemu alikuwa anasoma!
 
Imani nyingine ni matatizo matupu! Kwa maoni yangu kijana huyu alikuwa na matatizo ya kisaikolojia. Wahusika mtanisamehe kama nakosea kwa kusema hivi, lakini kuna kila dalili kuwa Godwin alikuwa na tatizo zaidi ya imani kali. Hakuna sehemu Mungu ameagiza tukafie porini kwa kusali, hata Yesu mwenyewe alipanda mlimani na kushuka kuendelea na shughuli nyingine.
...angalia hiyo nyekundu! ...Yesu alikuwa anafanya shughuli gani nyingine !Ushahidi?
 
Comments zinazotoka kwenye hii thread inaonyesha ni kwa kiasi gani hii dunia ya sasa inaelekea kizazi kile cha sodoma na gomora...hivi with all due respects...wagonjwa wa akili wangapi tunaona wanaishi na kusali na kwenda kanisani..toka tumezaliwa tuna mental cases ngapi wanafanya vitu kama hivyo...hata kama sio imani yako naamini wote kwenye hii thread mliodhihaki mna adhabu yenu kwa Mungu...this goes in the same way kama ambavyo unavyodhihaki imani kwa kukanyaga biblia au hata quran...you cant be so spoiled mnacomment vitu vya kipuuzi kama hivyo.....uhai ni zawadi ya Mungu hata kifo anapanga Mungu kwa kifo chake kwam kimetufundisha kitu fulani sisi binadamu kwamba kuna watu wenye imani dhabiti historia ya huyo dogo haionyeshi kuwa na ugonjwa wa akili amefanya hivyo akiwa shule mpk hizi sehem zote alizopita. Mwenyezi Mungu awape laana wote mliodhihaki hili fundisho la imani. Hebu nendeni mkatafute hao vichaa au mental retards wanaofunga na kuomba in this manner.
 
Kitabu cha SIRA ni kipi.

Tatizo la watu kujilinganisha na Bwana Yesu au Musa, hawa walikuwa wanahudumiwa na Roho Mtakatifu.

Funga huku unakula hata mara.moja , ukiamua kufunga kavu siku ziwe chache.

Going too soon. Pumzika,
 
Kitabu cha SIRA ni kipi.

Tatizo la watu kujilinganisha na Bwana Yesu au Musa, hawa walikuwa wanahudumiwa na Roho Mtakatifu.

Funga huku unakula hata mara.moja , ukiamua kufunga kavu siku ziwe chache.

Going too soon. Pumzika,
Kitabu cha Sira pia kinaitwa kitabu cha Hekima ya Yoshua Bin Sira. Ni moja ya vitabu 14 vya deuterokanoni (kutoka Kigiriki "deuteros" = ya pili na "kanon" = orodha) ni maandiko ya Agano la Kaleyanayotazamwa na Wakatoliki, na baadhi ya Waorthodoksi na ya Makanisa ya Kale ya Mashariki kama sehemu kamili ya Biblia.

Wayahudi na Waprotestanti wengi huviita apokrifa na kuvitazama kama vitabu vinavyostahili kuheshimiwa lakini si sawa na Biblia yenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Nimesoma post ya mleta mada pekee ...inawezekana hili limeshaulizwa ! Naomba kujua ni Bbilia gani hiyo yenye KITABU CHA SIRA,ambacho Marehemu alikuwa anasoma!
Tafuta biblia yenye vitabu 72 au biblia ya kikatoliki.
 
Back
Top Bottom