Rombo: Amuua mkewe na kisha kujinyonga

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mwenyekiti wa kitongoji cha Urua chini, kijiji cha Mfuruashe wilayani Rombo, Agustine Moshi(35) amemuua mkewe, Anastasia Agustine (31) kwa kumkata kata na kitu chenye ncha kali na kisha mwenyewe kujiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mshereheshaji maarufu wilayani humo (MC), anadaiwa kutenda mauaji hayo usiku wa kuamkia leo Novemba 8, 2021.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Novemba 8, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema wawili hao walikuwa na mgogoro wa kimapenzi, ambapo wiki moja iliyopita mke wake huyo alimpeleka dawati la jinsia Rombo.

"Huyu jamaa wiki iliyopita mke wake alimpeleka dawati la jinsia hapa wilayani, walisuluhishwa lakini inaonekana halikuisha na ni suala ambalo inaonekana ni wivu wa mapenzi, hivyo akaamua kuchukua jukumu la kumuua mkewe na kisha kujiua kwa kujinyonga," amesema Kanali Maiga.

Kanali Maiga amesema wanandoa hao wameacha watoto watatu wadogo.

MWANANCHI
 
Taarifa za Jeshi la Polisi na Waandishi waliofukuzwa over vyeti feki, sasa wamerudishwa kwenye ajira. Hakuna anae stop to think kabla hajaweka kitu hewani.

Wivu wa Mapenzi maana yake wanandoa walitakiwa kuacha choyo na ubinafsi na wakubali ku shea viungo vyao na jamii nzima ya Halmashauri ya Rombo ????

Murder weapon ni nini? Eti “kitu chenye ncha kali.” Ni yale mawe waliokuwa wanachonga Zinjanthropus ??? Yani akaua halafu kajichoma na jiwe la Zinjanthropus akavuja damu weeeee mpaka akafa. Kajiua kwa kuji torture!

Una solve vipi murder case kama hujui na hujali kujua murder weapon ni nini wala cause of death wala manner of death?
 
Taarifa za Jeshi la Polisi na Waandishi waliofukuzwa over vyeti feki, sasa wamerudishwa kwenye ajira. Hakuna anae stop to think kabla hajaweka kitu hewani...
Acha kingereza kingi we kijana, kitu chenye ncha kali chaweza kua kisu, panga, mkuki, kijiti, uma wa chakula na vifaa vingine vingi vinavyoweza kutoa uhai.

Vipi kama katia kisu mara kadhaa na kuchomoa na kisu kikatupiliwa mbali, utajua ni silaha gani kati hizo tajwa imetumika. Lakini pia vifu vipi vya aina nyingi sana sana, kuna vikubwa na vidogo.

Acha umuch know.
 
Kama umefanikiwa kupata watoto/ mtoto kabla hujaoa basi usioe lea wanao chapa mbususu maisha yaendelee.

Kama huna mtoto basi tafuta tu mtoto ila achana na mambo ya kuoa.

Ndoa ni moto, kuoa ni kukumbatia moto huku ukijua fika kua ni moto.
 
Daah, juzi kuna mwanamke huko Rukwa sijui, kaua mume wake na kumzika kwenye shimo la mkaa, matukio ya wanandoa kuuana mbona yanazidi..
 
Wanawake wanazidi kuwa vichwa ngumu baada ya kuambiwa kwamba wanaume wanachopaswa kuchangia ni mbegu tu.......kwa hiyo wanaume tujifanye tu maboya angalau siku ipite.
 
Back
Top Bottom