Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki, ameibuka hadharani akilalamikia kile alichokiita uvunjifu wa sheria za hakimiliki baada ya kuona mdundo wake (beat) ukitumika katika mikutano ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila ruhusa yake.
Kupitia andiko lake kwenye mitandao ya kijamii, Roma alionyesha hasira na kusisitiza kuwa anahitaji kulipwa stahiki zake kwa mujibu wa sheria, akisema: “Mnatumia beat yangu kwenye mikutano yenu ya kampeni bila idhini yangu!! Hilo ni kosa kisheria (copyright). Nahitaji kulipwa stahiki zangu tafadhali sana!!”
Roma ameeleza kuwa si mara ya kwanza kushuhudia nyimbo zake au midundo yake ikitumika bila ridhaa, jambo analolitafsiri kama dharau kwa kazi za wasanii. Aidha, alibainisha kuwa licha ya kuwepo wasanii wengi ndani ya chama hicho, bado nyimbo zake ndizo zinazotumika bila makubaliano yoyote.
Amesema kwa unyenyekevu mkubwa anatafuta mwanasheria wa kumsaidia katika hatua za kisheria ili kupata haki yake. “Ni kosa kisheria kutumia kazi ya msanii hadharani bila makubaliano ya kimaandishi. Lazima niokote, sikubali,” alisema Roma.
Aidha, alimalizia kwa kuhoji kwa nini chama hicho kinashindwa kutumia kazi za wasanii wake, huku wakitumia kazi zake bila ruhusa: “Wasanii wote wa nchi nzima mnao kwenye chama chenu, si mtumie beat zao? Au hawana midundo mikali?”