Roma bado inatawala dunia

Roma bado inatawala dunia: ingawa ilianguka mwaka 476 AD ila athari zake zilikula dunia yote, ndo maana primary tulisoma no. za Kirumi na hata saa na Kalenda tunatumia za Kirumi na mataifa mengi yana sheria za Roma mpaka lugha zao tunazitumia. Roma haikuanguka kama inavyosemwa bali ilisambaratika na kuwa nchi za Ulaya ambazo zilikuja kuwa zenye nguvu na kutawala karibu dunia yote na kusambaza utamaduni wao. Mfano Uingereza imetawala bara Asia mpaka bara Arabu, hata ufalme wa Yordan, Saudia, Qatar zimewekwa na Uingereza. Kwaiyo ukisikia jumuiya ya madola tambua hizo ni nchi zilizotawaliwa na the greater Britain. Na Ufaransa, Spain, Portugal nazo hivo hivo.
Ulaya(Roma ya zamani) bado ina mkono mkubwa juu ya nchi za dunia hii. Ndo maana wameweka mahakama yenye sheria za Roma(The hague) ambayo daima ikiwahukumu viongozi wa nchi maskini, utake usitake ukiitwa hapo utaenda tu, na ukibisha utatolewa kwa bunduki.
Nabii Daniel alisema hivi juu ya Roma.
23 Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. Daniel 7
Huu utawala wa Roma utadumu mpk Kuja kwa Yesu. Roma imeathiri dunia kisiasa, kidini, kisheria na kitamaduni na nchi yeyote inayokataa hoja za Roma lazima iangamizwe. Sadamu, Gadafi waliangamizwa sababu walipingana na utawala wa Roma, na sahivi Assad anakinywea kisha # Iran itapotezwa. Nabii aliona jinsi wana wa Ishmael(waarabu) wanavyopinduliwa na Roma maana hao waliifukuza Roma karne ya 7 na Roma ikajirudi tena kwa namna ya kuwaweka vibaraka wao ktk falme za Kiarabu kama ufalme wa Saudia, Qatari, UEA na Jordan hao wote ni puppet wa Roma. Na wote watakao pinga watafanyiwa hivi:-
Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. Daniel 11:42
Utawala wa Roma utaziangusha nchi zote pinzani zikiwemo nchi za Kiarabu na dunia itamstajabiwa mnyama yule(ufalme huo) na kuufata. Ufunuo 13:3 NIV
ROMA itatengeneza utawala wa dini na kulazimisha dunia yote kufata dini hiyo na watakao pinga watauawa.
Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Ufunuo 13:5
Roma haitaangushwa na wanadamu......
......wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Ufunuo 13:4
Roma itaangushwa na Mungu tu.
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu. Ufunuo 18:8
Take care usije anguka na Roma

a1175df048e7c5de0a0fe3db44ef801f.jpg
Naomba, kuelimishwa kwa nukuu moja ya bibilia iliyo badilishwa na papa, aliyesema hakosei n nani ktk roma, pia thibitisha.
Hiyo Ufu:13 ni muham mad ibn abd allah..

Ilipoandikwa MNYAMA WA NNE , UFALME WA NNE. hizo nne zinamaanisha nini?. yaani 1,2,3 ni wakina nani hadi kufikia roma 4 ? Tuanzie hapo
 
Nithibitishe nini..?!
Ulicho kisema, shika bibilia yako vizuri na uisome usiokote vipeperushi ukatupia alafu ukashidwa kiuitetea.
Ni kweli!; ndio sababu waisilamu wanasali ijumaa wakisherehekea kwamba Yesu kafa...wasabato wanasali jumamosi wakifurahia Yesu yupo kaburini...Wakristo tunasali JPili tunasherehekea Bwana wa Mabwana kashinda kifo ni limbuko letu
 
Naomba, kuelimishwa kwa nukuu moja ya bibilia iliyo badilishwa na papa, aliyesema hakosei n nani ktk roma, pia thibitisha.
Amri ya 4 ya Mungu inasema "Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote. Lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku 6 Bwana alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hio Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa. Kutoka 20:8-11.
Hio ni amri ya Mungu iliopindishwa na papa... Kanisa Katoliki hawaisomi jinsi ilivyo ktk Biblia Takatifu
 
Kwanza niseme kwamba mimi siyo Msabato. Mimi ni mkristo ninasali kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG).
Umande fungua Biblia yako kitabu cha Danieli 2:29-45.
Aya hizi zinaonesha dola kuu ambazo zimetawala dunia tangu wakati huo (Nebukadreza alipoota ndoto hiyo) na zitakazotawala duniani hadi dunia hii itakapoondolewa. Falme hizi (dola kuu) zilikuwa na mamlaka kamili dunia nzima (serikali zote duniani zikiwa zinafuata amri kutoka dola hizo kuu). Ikumbukwe kwamba kabla ya Nebukadreza (Babeli) kulikuwa na falme kuu 2 zilizokuwa zimetawala dunia hii, nazo ni Misri na Ashuru. Ukisoma aya hizo utaona kwamba zenyewe hazikuzungumzwa:
Hizo dola kuu 4 tangu ndoto ya Nebukadreza zilizoitawala dunia yote ni kama ifuatavyo:
1. Dola ya Babeli - Kichwa cha dhahabu (Danieli 2:36-38) tangu mwaka 612KK hadi 539KK (Kabla ya kuzaliwa Kristo - KK)
2. Dola ya Umedi na Uajemi - Kifua na mikono ya fedha (Danieli 2:39) tangu mwaka 539KK - 333KK
3. Dola ya Uyunani - Tumbo la shaba (Danieli 2:39) tangu mwaka 333KK hadi 146KK
4. Dola ya Rumi - Miguu miwili ya chuma (Danieli 2:33, 40) tangu mwaka 146KK
Utawala wa dola ya Rumi uligawanyika sehemu mbili:
a. Rumi ya magharibi (Western Roman Empire) ambayo mji wake mkuu ulikuwa Roma (tangu mwaka 146KK hadi 476BK - (BK-Baada ya kuzaliwa Kristo)
b. Rumi ya Mashariki, mji wake mkuu ulikuwa Constantinople (tangu mwaka 146KK hadi 1453BK)

Dola 4 tayari zimekwisha itawala dunia yote, bado dola ya 5 ambayo ni "nyayo" (Danieli 2:33, 42,43). Dola hii ya 5 itakuja kuondolewa na ufalme mwingine utakaotawala milele na milele ambao mtawala wake hatakuwa mwanadamu (Danieli 2:44-45).
Swali; dola ya 5 ni mfalme wa dola gani?
Huyo mfalme atakayeondoa utawala wa dola ya 5 kisha kutawala milele na milele ni
nani?
Tutumie Biblia kudadavua hii mada muhimu! Karibuni.

Uongo mtupu. Hii ni tafsiri inayotokana na fikra za waliotafsiri hivyo kwa kufananisha matukio, hakuna uthibitisho wowote hata kwenye Biblia yenyewe. Natoa sababu zifuatazo:
1. Miaka yote hii uliyorodhesha kwenye maelezo yako haijaandikwa popote kwenye Biblia.
2. Isipokuwa tu kwa dola ya Babeli, nyingine zote ulizoorodhesha hazizungumziwa kwenye Biblia.
3. Unapotaja dola zilizotawala dunia wakati Nebuchadnezzar alipoota ndoto yake, unamaanisha dunia ipi? Unazungumziaje Ancient China (600BC), Ancient India (ambayo ilikuwa na strong urban kingdoms tangu 700BC), Falme za Mesoamerica na himaya staarabu za Maya, America Kusini (tangu 7,000BC)? Hao unaowataja walitawala himaya hizi pia? Kumbe si kweli, dunia unayozungumzia ni ya eneo la mashariki ya kati, sehemu kiasi ya ulaya na afrika ya kaskazini. Dola unazotaja hazikutawala dunia, zilitawala maeneo hayo machache.
4.Sehemu ya dunia unayokwepa kuizungumzia (Uchina, Japan, Korea, na mashariki ya mbali) ndiyo yenye mifumo tofauti ya kiutamaduni na kimaendeleo inayoshindana sana na ya kimagharibi. Haiko kwenye maelezo yako kwa kuwa umejikita kwenye 'dunia' ndogo ya mashariki ya kati.

Bisha.
 
utawala wa nyayo ni utawa wa humanoid under alliens ...

alliens wameshaanza kutengeneza human hybrid ambao ni half human na halfu alliens na hao ndo wanakuja kumonopolise this universe...ndo mana Nchi kibwa kama japan,america,uingereza na zingine zimeanza kutengeneza robot wenye ngozi kama binadamu kabsa na hao robot wana uwezo wa kupiga stori na mwanafamu wa kawaida kabsa bila kumshtukia ...
kwa hiyo binadamu wa kawaida have to be perished away kwa kasi ya ajabu snaa ili kuacha universe hii ndani ya mikono ya wengine....
inshot ndo mana sumu nyibgi zinatengenezwa ili kufupisha life span ya mwnadamu halisi....

it is a battle btn God and satarn let' s enjoy it...hakika wanajuana malengo yao ni nini sio sisi tunaochezeshwa kama mazombi....

Typical paranoia. Usijichanganye ndugu. Hivi kweli unaamini kuwa Mungu anayetajwa kuwa mwenyezi, mwenye uwezo wote, aliumba kiumbe (shetani) halafu akakipa uwezo wa kushindana naye kwa kiwango cha vita hizi mnazosema hapa? Kwamba Mungu mwenye uwezo wote anaumba kiumbe halafu kinamgeuka na kumsumbua kiasi hiki? Hujamwelewa Mungu.
 
Mackie nimetambua kwamba mimi na wewe tupo kwenye spiritual horizons 2 tofauti. Kwangu mimi biblia inajitosheleza, ni kila kitu. Kwa hiyo mjadala na wewe nimefunga. I have nothing any more to debate with u!
Another confused poor soul. Unamaanisha kuwa Mungu ni mdogo kiasi cha habari zake zote kutoshea kwenye kitabu kidogo kama Biblia? Fani yako uliyosomea peke yake ukikusanya vitabu ulivyosoma shahada ya kwanza tu mkusanyiko utazidi ukubwa wa Biblia mara nyingi. Na unajua kuwa fani yako uliyosomea haiwezi kumzidi Mungu, sasa vipi maelezo ya Mungu yatoshe kwenye Biblia pekee? Unazungumziaje watu walioishi kabla Biblia haijakusanywa (rejea historia ya Biblia ujue ni lini vitabu hivyo vilikusanywa katika mfumo unaouona sasa), hiyo habari ya "Biblia ni kila kitu" iliwahusuje, au walikuwa na Mungu mwingine? Na je waumini wa Buddhism na Hinduism ambao vitabu vyao vina umri mrefu kuliko Biblia, wanahusikaje na kauli yako ya 'Biblia ni kila kitu', au nao wana Mungu wao? Na wewe hiyo dini ya "Biblia ni kila kitu" ulizaliwa huko au uliitafuta kwa bidii mpaka ukaipata? Najua mlio wengi mlizaliwa katika dini zenu, inabidi tu mzitetee maana huwezi kukana identity yako, ni kama kabila lako au utaifa wako, lakini kumbuka hakuna aliyechagua kuzaliwa Macca (kwa waislamu) au Roma (kwa wakatoliki) au India (kwa wahindu) au Japan na China (kwa wabuddha), walijikuta huko na wakajifunza tamaduni hizo zilizowalea, sasa huwezi kubeza yote hayo unless unataka tuamini kuwa wote hao katika tofauti zao kila mmoja ana mungu wake tofauti na huyo wa kwako wa "Biblia ni kila kitu".

Mwisho, napenda nikubaliane nawe kuhusu msimamo wako, kwa matarajio kuwa nawe pia utaheshimu misimamo ya wengine. Na kama unaheshimu hivyo, basi usipinge wanachoamini wenzako. Ukitaka kufahamu ni sawa, lakini huna haki ya kukosoa kwa sababu huna objective reference ya kilicho sahihi dhidi ya kisicho sahihi. Fuata yako, waache wenzio pia wafuate yao. Tutofautiane hivyo.
 
Kaka nashukuru sana kwa maelezo mazuri, ila kwa kuongezea ni kwamba.

Kumbuka biblia imesema kuwa rumi ya kimwili haiondoki kabisa. Ni kweli rumi yenyewe iliyokuwepo mwanzo iligawanyika Mara kumi, na mpaka sasa hayo mataifa yaliyounda rumi ya kale yapo kasoro mawili yaliyoharibiwa kabisa kwa maksudi na utawala wa papa.

Na tunaambiwa katika biblia kwamba kuna rumi nyingine ya kiroho, ambayo ilikuwa imepata jeraha baadae na likapona ( huo ni upapa) kumbuka upapa ulikuwa umeshaondolewa hapo mwanzo katika mapinduzi ya ufaransa, papa aliuwawa na mamlaka yake yakaondolewa kabisa.

Lakini tunakuja kuona baadae mfalme mwingine wa ufaransa anakuja kumrejeshea tena mamalaka na kupewa tena kipande cha nchi( Vatican) kwa hiyo yule mnyama mwenye kunena kakufuru aliyekuwa amepata jeraha la mauti hatimaye jeraha hilo likapona akaendelea kunena maneno makuu ya makufuru na mataifa yote wakampa nguvu zao, akapata kazidi kutawala na kunena makufuru.

Kumbuka papa anaposema kwamba hakosei na wala hawezi kukosea, hiyo ni kufuru, pia wanasema kwamba papa anachukuwa nafasi ya mungu hapa duniani, papa amebadili amri kumi za mungu ( na bilbia inaongelea habari za hiyo myama kubadili sheria za mungu, majira na nyakati) kwa mujiba wa mwandishi mmoja wa kikatoliki ni kwamba papa ana uwezo wa kubadilisha maandiko ya biblia, na tayari wamekisha Fanya hivyo. Hiyo yote ni kufanya kinyume na maagizo ya mungu (kukufuru).

Hivyo basi bila kumungunya maneno mnyama anayefuatia ni upapa dunia ianafanya maandalizi ya kukabidhi mamlaka na madaraka yote kwa papa. Kutakuwepo na Dino moja na selikali moja duniani na maandalizi hayo yalikwishaanza kitambo.

Kuna mnyama anayetoka katika nchi yaani marekani ndiye atakayemkabidhi papa mamlaka, kumbuka marekani imetabiriwa ndani ya biblia.biblia ikisema mnyama anatoka baharini au maji mengi ina mahanisha kwamba ni mtawala mwenye nguvu kutoka miongoni mwa nchi yenye watu wengi, lakini ukisoma biblia kuwa mnyama anatoaka katika nchi, maana yake ni kuwa mtawala huyo anatokea sehemu isiyokuwa na watu kidogo sana UA hakuna kabisa, kumbuka na taifa la marekani lilianzishwa na wazungu, ndio waliolivumbua hilo bara akina kolumbas hapakuwepo na watu wengi mpaka wlipokuja kuchukuwa waafrica kuwafanya watumwa. Nchi ya marekani watu wanaokaa himo aslimia 99.999 wote ni watu wa kuja, taifa hilo liliundwa na wageni.

Hivyo unabii wa biblia unatimizwa bila shaka. Na tumeambiwa mpinga kristo na nabii wa uongo wote watatoka rumi ( miongoni mwa nchi za ula ya) kumbuka rumi ya zamani iliundwa na nchi kumi za ulaya, watu wengine udhani kuwa rumi ni Italy pekee. Rumi ya mwanzo ilikuwa ni pamoja na
1 ujerimani
2 uingereza
3 ufaransa
4 Hispania
5 Italy
7 Swiss land
8 ureno na mataifa mengine mawili yaliyoondolewa kama vile wavandali na waostigos.

Duh! Vituko vitupu! Kwa kujitungia udaku tu hujambo! Kwahiyo haya yote yako kwenye biblia ipi? Au na wewe umeandika ya kwako?
Na hiyo biblia unayosoma wewe, unajua ilikotoka? Ni Mungu aliiandika, eti? Hebu tafiti kidogo tu kuhusu maana na asili ya biblia (Biblia ni nini, ilianzaje, ikakua vipi hadi kufikia hiyo unayokariri?)
 
Duh! Vituko vitupu! Kwa kujitungia udaku tu hujambo! Kwahiyo haya yote yako kwenye biblia ipi? Au na wewe umeandika ya kwako?
Na hiyo biblia unayosoma wewe, unajua ilikotoka? Ni Mungu aliiandika, eti? Hebu tafiti kidogo tu kuhusu maana na asili ya biblia (Biblia ni nini, ilianzaje, ikakua vipi hadi kufikia hiyo unayokariri?)
Mkuu! Unapoteza muda wako...wote hao na mpeleta mada ni vi.laza....hakuna wanachojua
 
Sasa Mimi nilikua mroma roma sugu familia nzima ...kanisani nilikua nakaa karibu na padri nadhan mnaelewa ....,....ila nilisikia tu habari ya siku ya ibada ni IPI ???? nikaanza kusoma maandiko na kuuliza baadhi ya watu wadini ...lakini kila nilipokua nikimuuliza padri Wangu alikua akinambia nitakujibu jumapili ijayo hatimae nikaanza kukata tamaa nikawa sionekan tena pale mbele ...Kwa kusoma na kudadisi Nikagundua kua Sabato ya Mungu ni Juma mosi ...Nabiblia pekee ndio inayotoa jibu ....nampaka sasa Familia nzima tu wasabato kasoro Baba yangu lakini naye nikipata muda narudi huwa nazidi kumpa somo ..naniaamini mauti hayatomfika kabla naye hajawa msabato.

Somen Biblia mjue ukuu Wa Mungu ...ujanja na porojo zakubisha bisha alafu biblia hujawahi hata kuigusa pengine hujui inauzwa shilingi ngapi no way zaidi ya kupotea tu.
Propaganda ya anayejifunza propaganda. Eti ulikuwa mroma (sijui ndio kabila gani hii inaitwa hivi), halafu eti ukasikia habari ya "siku ya ibada ni ipi", kwani huko ulikosema kanisani ulikuwa unakaa karibu na padri (kwanza hakuna seat ya namna hiyo katika makanisa yenye mapadri) siku ya ibada haikuwepo? Kwa hiyo ulikuwa unaenda kufanya nini kanisani? Acha uongo ndugu. Amini unachoamini, ni hiari yako, lakini acha uzushi.
Na hiyo biblia uliyosoma ikakueleza kuhusu sabato, uliipata wapi? Unajua historia yake? Kariri tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom