Roho inaniuma mpenzi wangu anataka tuachane kwa sababu hayaelewi maisha yangu

Ila kakwambia ukweli asee..
Ila mwanaume akiwa hana kitu anatia huruma balaa

Cheki hapo unavyoongea kiupole ngoja uzipate sasa ni mwendo wa kubadili mademuz

Makiseo

Simara
 
Ah kirikata mama eh
Ah dance for mama eh, papa eh
Na kama akiringa achana naye
Utapata mwingine baadaye 🎶🤸🕺
 
Kipindi nina mgogoro na mpenzi wangu niliomba ushauri humu JF kutokana na tabia za mpenzi wangu wengi walinishauri nijaribu kukaa naye chini na kuzungumza nae kiupole hatimaye nimefanikiwa na tumezungumza .

Katika mazungumzo aliniambia kiustarabu anaona bora tuachane au tuvunje uhusiano kwa sababu zifuatazo

1. Haoni future nzuli na Mimi hivyo anaona kama nampotezea muda

2. Maisha yangu hayaeleweki nimekuwa mtu wa kubangaiza ninaishi maisha ya kubahatisha hivyo bado sijasimama

3. Amejitahidi kuvumilia hali yangu ya maisha lakini uvimilivu unamshinda kwani Miaka yote haoni mabadiliko kila siku niko vile vile haoni hatua yoyote nilioipiga Katika maisha haya.

4. Finally akaniambia amenipa muda anataka kuona maisha yangu yanabadilika anataka kuona natoboa Katika maisha haya

Ila alichoniambia Kikubwa tuvunje uhusiano kama sitoweza kutimiza Yale anayoyataka yeye nimuache aendelee na maisha yake
Kwa ukweli huyo binti hana upendo na wewe, upendo hauna masharti, hana uvumilivu atakusumua mbeleni kubali kuumia kwa sasa ila baadaye utapata wa kukupenda, mwache aende
 
Kwa ukweli huyo binti hana upendo na wewe, upendo hauna masharti, hana uvumilivu atakusumua mbeleni kubali kuumia kwa sasa ila baadaye utapata wa kukupenda,mwache aende
Usimtie moyo huenda hatapata wa kumpenda.
Hivi ni kweli upendo haunaga vigezo?
Hebu tuwe wakweli.
1. Kama wewe unapenda aina flani ya mtu awe mpenzi wako hiyo sio kigezo?

2. Ikiwa muda wote amemvumilia huo sio upendo?

3. Je mwanamke hupenda au hupendwa naye hutii na kujifunza kukuzoea hatimaye upendo?

Tuwe na mjadala wa kweli na sio blabla
 
Upendo ni tabia ya Mwenyezi Mungu nasi viumbe vyake tumeridhi kutoka kwake. Kwa tabia ya asili Upendo hauna vigezo ndiyo maana soma 1 Korinto. 13 hapo utaona upendo hauna vigezo, waingereza unconditional love. Ila zipo sifa za watu wanaopendana kama ukweli, uaminifu, msamaha, kushirikishana au kusaidiana ,n.k ndiyo maana mwanaume anapotaka kuoa anabidi aombe kwa Mungu ampe mke mwema, kwani Mungu aliahidi nitakupa wa kufanana nawe.

Kwenye pointi ya pili kuvumiliana wote mnavumiliana siyo upande mmoja kwamba nimekuvumilia weweunatakiwa ufanye hivi hapana. Wote mnashirikiana kwa kila kitu. Swali la tatu wote mnatakiwa mpendane ila Mwanaume anakuwa kiongozi mwanamke ana nafasi ya kuwa msaidizi au mshauri, Tito 3.4 ili wawatie wanawake vijana akili wawapende waume zao. Mwanaume tumeambiwa tuwapende wanawake kama Kristo Yesu alivyolipenda kanisa lake efeso 5.25.
 
Laiti wanawake wote wangekua kama huyo binti! Kumpata mtu anaekupa changamoto za maendeleo sio jambo rahisi. Tuweke hisia na mihemko pembeni, huyo binti anachotaka ni uhakika wa future. Ndio maana anamwambia baharia ajitahidi kukaza kidogo kuingia uchumi wa kati ili waende sawa.

Kuna movie sikumbuki vizuri lakini kama sikosei inaitwa "The Diary" jamaa alidhalilika na kudharaulika kisa ufukara, hii ilimpa ari na nguvu akafanya mabadiliko makubwa sana.
 
Maisha yangu yalikuwa kama yako , ex wife akaniambia tuachane nikagoma akaniambia "UNANING'ANG'ANIA NGA'ANG'ANIA KWANI MIMI MAMA YAKO?"
Hahahaaaa mkuu live real life ACHA KUYAZUIA MAFANIKIO YAKO KWA AJIRI YA HISIA ZAKO.
 
Laiti wanawake wote wangekua kama huyo binti! Kumpata mtu anaekupa changamoto za maendeleo sio jambo rahisi. Tuweke hisia na mihemko pembeni, huyo binti anachotaka ni uhakika wa future. Ndio maana anamwambia baharia ajitahidi kukaza kidogo kuingia uchumi wa kati ili waende sawa.

Kuna movie sikumbuki vizuri lakini kama sikosei inaitwa "The Diary" jamaa alidhalilika na kudharaulika kisa ufukara, hii ilimpa ari na nguvu akafanya mabadiliko makubwa sana.
Ndugu huwezi kuishi na mtu mwenye kukupa mashinikizo huku hakuonyeshi ushirikiano wowote wa wote kuvuka kwenda uchumi wa kati, hiyo ni dhana potovu, wakae pamoja wapange mipango na washirikiane pamoja. Uchumi ukipanda si ni wa familia kwani ni wa mwanaume mwenyewe.
 
Yani kama ni mtu mzima na unajua kuchanganua mambo mpaka hapo situation ilipofikia inaonesha mwanamke wako hana mapenzi kabisa na wewe afu pia yuko kimasilahi zaidi ndo maana anahitaji utengeneze mafanikio yako ila kiuhalisia angekua anakupenda mngetafuta mafanikio pamoja na yeye
 
Huo ndiyo ukweli hamna kuficha mwanamke maslahi huyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom