Nilimuamini rafiki yangu kageuka kaanza kuingiza gia kwa mpenzi wangu

Friday Malafyale

JF-Expert Member
Jan 18, 2017
1,808
2,911
Habari wana MMU, nina rafiki yangu mwenye jina la J kwa sasa yupo mkoni huko. Aliyonifanyia sikuamini.

Mimi nina mpenzi wangu ambaye alikuwa akisoma chuo fulani ambacho kipo Mbeya kwa sasa kamaliza 2016. Mapenzi yetu yalianza 2014 nikiwa namalizia chuo masomo yangu mwaka wa tatu kiukweli huyu binti ni wa Kyela nami ni wa huko huko.

Basi mapenzi yetu yalinoga sana sana, yaani sijawahi kupendwa na mwanamke kama huyu, nikienda kwake kumtembelea nilikuwa naenjoy sana sana sana alikuwa akifanya shopping za maana kwenye misosi, matunda n.k tulipendana sana of course sitaki nimkosee Mungu katika hilo.

Basi nikirudi wilayani kwangu nje na mkoa wa Mbeya ni mishe busy na kazi zangu basi naye akija kwangu kusalimia alikuwa anapika yaani anachukua majukumu kama mke wa ndoa, usiku mambo ya wakubwa.

Story isiwe ndefu sana, kuna binti anaitwa Esta ni mfano sio jina lake halisi nilitokea kumtamani sana basi nikatupa ndoano akakubali.

Maisha yakaendelea nikaomba game nikala la pili nikala pia, sasa hiki kipindi niko na huyu Esta (Jina la mfano) mawasiliano nikawa napunguza ama akipiga namwambia nimechoka ama niko bisy nicheck badae mara nyingi nilikuwa kwenye mishe na huyu jamaa yangu J alijua kinachoendelea, na anajua siri zangu nyingi (ikiwemo ya kuwa na watoto wawili mama tofauti) hili nilimficha huyu mpenzi wangu yule wa Kyela.

Basi muda umeenda enda wee! Kuna siku huyu binti wa Kyela akaomba aje atembee kwangu akaja kusalimia akakaa siku tatu, hapo alipokuja akakuta sms kwenye simu yangu ambayo haikumpendeza sana na ilikuwa ya yule Esta, basi nikaomba msamaha yakaisha (wanawake wanahuruma waacheni tuu) Basi kesho yake mchana akawa anapekua pekua laptop yangu akakuta kuna picha za kimahaba ambazo zilipigwa tukiwa na Esta kupitia webcam ya kwenye .

Akalia sana why nimfanyie vile nikaomba msamaha sana sana akalia sana akajutia kuwa nami (kwa kweli nilimkosea sana) Usiku tukalala sikumgusa nikahofia ataninyima game, kesho yake akaja yule jamaa yangu nikamwomba aniombee msamaha mwishowe binti akanisamehe.

Kitu kilichokuja kutibua sasa.
Siku ya tatu yake (hii ni real story sio maigizo) akaja Esta asubuhi sana sana, muda kama kumi na mbili na nusu na muda wote huo niko na mtoto wa kinyakyusa line ya Vodacom niliiweka offline kwa hyo alikuwa akinitafuta hanipati. Basi ile asubuhi nastuka tuu mlango unagongwa ngo ngo ngo!!! Mmh nikastuka mara ya tatu nikauliza we nani akakaa kimya, mara ya nne nikaona ninyanyuke kufika mlangoni ni yule Esta.. Akili ikahama ghafla nikajua tayari nishafumaniwa. Nikamuuliza "Umefuata nini" wakati mara zote anapokuja huwa simuulizi hivo akashangaa sana why namuuliza vile, hapo nikawa nabana asiingie ndani, akaniuliza huniruhusu niingie ndani nikajibu kuna jamaa yangu kalala vibaya so vizuri kumuona, akachungulia kwenye bawaba za mlango akaona kwamba kuna mtu anapita hivi akaforce aingie ndani.

Tukio lilikuwaje.


Baada ya kufika ndani nikapanic akanambia nimekuja kuchukua ipad yangu, kulikuwa na ipad aliacha mbovu ilibidi ampatie mdogo wake anayeenda nchini Zanzibar. Basi haraka haraka nikampa, huku mwili unanitetemeka. Lakini kabla hao wadada ndani walisalimiana vizuri tuu.
Baadaye Esta akaaga anaondoka sikumsindikiza kabisa kitu ambacho sio kawaida yangu.

Mawazo nani nimwache na nani nibaki naye.

Ilibidi alobaki ndani ndio nianze kubembeleza sasa. Binti wa watu akalia sana sana akaniambia Desh desh...umeniumiza sana kuniletea mwanamke ndani kwa macho yangu nimeona, Nikajaribu kumuomba msamaha akahoma hakunywa chai, akaniomba tuu nimwitie taxi imbebe mpaka stendi aondoke kwenda Mbeya mjini. Nikafanya hivyo kama alivyotaka.
Akaondoka njiani akawa anani update kafika wapi. Kwa hayo nilomfanyia nilijuta sana sana, akanambia nimemshusha sana thamani yake sana.

Msamaha.
Wanawake wana roho nzuri sana ukiendana nao licha ya yale makosa yangu akanisamehe tukaendelea, na yule Esta nae nikamwomba msamaha kwa kudanganya lakini.

Jamaa yangu ananiharibia.
Jamaa yangu mwenye jina la J. Akaanza kuwasiliana na yule demu wangu kama shemeji yake lakini baadaye akawa anaanza kuharibu kumwambia mambo yangu yoote hata habari za watoto wangu wawili nilionao, mabinti niliotembea nao kitu nilichoshangaa huyu binti wa Kyela akanambia kila kitu kuwa alonambia yote haya ni jamaa yako, kila mwanamke alokuja hapo nilitonywa na jamaa yako huyo huyo. Akasema baadae alipoharibia akaanza kunitongoza kuwa achana na jamaa hakufai wala nn, achana naye kuwa na mimi. Nikawaza kuwa huyu jamaa yangu ndio mnafiki wa aina hii?

Anaharibia anataka tena aanze kumla alokuwa shemeji yake, bahati nzuri yule binti akanambia kila kitu, ila jamaa mpaka sasa nimempotezea nikaona nisigombane na rafiki yangu kwa ajili ya mwanamke. Kuweni makini na jamaa au mashosti zenu mnaowapa taarifa na habari zenu. Samahani kwa story ndefu imenitokea mimi mwenyewe.

Asanteni
 
Pole sana. Mkuu nikuulize kitu.
Huyo mnyakyusa amegundua hayo yote na tukio la kufumaniwa kwako na mwnamke alimuona anaingia ndani ...je alikutamkia kua MUACHANE??
au alionyesha tu kuumia na ulichomfanyia
 
Mkuu we ni kiwembe daah

Watoto wawili mama tofaut,.plus mnyaki na esta na wengine ambao hujawataja kwenye story yako
 
Pole sana. Mkuu nikuulize kitu.
Huyo mnyakyusa amegundua hayo yote na tukio la kufumaniwa kwako na mwnamke alimuona anaingia ndani ...je alikutamkia kua MUACHANE??
au alionyesha tu kuumia na ulichomfanyia
Hilo fumanizi na ambayo ameambiwa na jamaa
 
Of course mwanamke ananipenda sana kwa sura mimi ni Handsome sana na najua kuvaa kitandani niko vizuri labda mapungufu mengine. Hajawahi nitamkia hayo
Kwaio amekufumani live, amejua una watoto wa mama wawili tofauti, na amejua na mengine mabaya aliyoambiwa na rafik yako, LAKINI HAJAKUTAMKIA KUA MUACHANE! Is that it??
Anaonesha kuumia tu, kusononeka, kulaumu, si ndio mkuu?
 
Of course mwanamke ananipenda sana kwa sura mimi ni Handsome sana na najua kuvaa kitandani niko vizuri labda mapungufu mengine. Hajawahi nitamkia hayo
Bas mkuu kama hajakutamkia, asante kwa jibu, kuna utafit wang wa mahusiano naufanya...
anyway back to topic, anakupenda huyo mdada sema unachukulia upendo wake for granted kwamba unaweza fanya lolote na asikuache kabisa, hata kukutamkia hajafanya hivo sabab anakupenda kwa dhati na still ana hope maybe utabadilika. Wanawake wa aina hio ni wachache, so thamin.ulichonacho(mnyakyusa)na thamini unachopewa (upendo).
 
Shyeeeh...!!! Hivi nchini Zanzibar naweza fika kwa gari moshi baada ya siku ngapi? Kuna njaa pia huko?
 
Huyo dada ni fala kaambiwa maovu yako badala auchune achunguze aweze kuamua anakuambia tena? acha ajibebee zigo jinga
 
Bas mkuu kama hajakutamkia, asante kwa jibu, kuna utafit wang wa mahusiano naufanya...
anyway back to topic, anakupenda huyo mdada sema unachukulia upendo wake for granted kwamba unaweza fanya lolote na asikuache kabisa, hata kukutamkia hajafanya hivo sabab anakupenda kwa dhati na still ana hope maybe utabadilika. Wanawake wa aina hio ni wachache, so thamin.ulichonacho(mnyakyusa)na thamini unachopewa (upendo).
Wanawake wa aina hii ni wabaya kupindukia.
 
Back
Top Bottom