Poleni watu wa Zimbambe kwa kifo cha Cde Robert Mugabe.
Ukizungumzia Uhuru wa Zimbambwe toka kwa Wakoloni bila ya kumtaja Robert Mugabe basi maelezo yako yatakuwa na kasoro, Robert Mugabe mchango wake ulikuwa mkubwa sana katika kupigania uhuru wa Zimbabwe mpaka Aprili 1980 Zimbabwe ilikuwa Taifa huru.
Ni kwa kawaida wana diplomasia Wa Kiafrika kuto kosoana katika masuala ya uongozi au uchaguzi mkuu,,Changamoto la utawala Mugabe lilianza Rasmussen mwaka 1999 wakati Chama kikuu cha upinzani cha MDC chini ya Morgani Tsangirai kilipo anzishwa , Na pia kundi kubwa la war veterans walipo anza vita ya kutwaa ardhi ilio kuwa inamilikiwa na wazungu.
Chimbuko la MDC likuwa changamoto kubwa sana katika utawala Mugabe Hugo akiwatuhumu kuwa wana fadhililiwa na Mataifa ya nchi za nje ili kuendeleza ukoloni mamboleo.Katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi inasadikiwa kuwa watu zaidi ya 20,000 walipoteza maisha yao wengi wao toka upande WA upinzani .