Robert Amsterdam unayaona yanayotekea Marekani?

Kejuu

JF-Expert Member
May 20, 2020
645
904
Ndugu zangu kheri ya Mwaka mpya?

Walimwengu wanafuatilia kwa ukaribu sana uchaguzi wa Marekani na their transfer of power, sasa najiuliza vipi hali hii iliyofanywa na wafuasi wa Trump Jana, ambayo imepelekea watu wa 4 kufariki; ingetokea katika nchi zingine, kama za kiafrika au Latin America, akina Mike Pompeo na kiherehere chao kama malecture wa democracy, si kungekuwa na matamko chungu nzima? Nashangaa hata balozi za nchi mbalimbali, ziko kimya tu hata kukemea Hakuna kama wafanyavyo mabalozi wa USA around the world.

Ni wakati muafaka sasa wa Robert Amsterdam kumpeleka Trump Zehegi yao badala kupoteza muda mwingi kudeal na Tanzania, ambapo uchaguzi ulikuwa huru na haki and there was a peaceful transfer of power.
Jamaa wanafiki sana halafu ni double standard balaa.

Kejuu
 
Duniani hakuna haki, wanaopigania haki duniani huishia kuumia wao wenyewe na uzuri Mungu alishaliweka wazi, tatizo watu tuna vichwa vigumu, alishasema Kama unataka haki fight kwenda mbinguni, duniani huku ni sarakasi mwanzo mwisho na hyo ipo approved na mbingu
 
Marekani wananyooshwa na nguvu ya uimara wa taasisi zao tofauti na hapo tramp asingeachia madaraka
Uko sahihi mkuu, halafu alikuwa anamshinikiza kweli makamu wake wa raisi kwenye show hii ya mwisho
 
Na sisi tulijitoa baada ya kuona anayejiita baba wa democracy amejitoa, hivyo na sisi sio wanachama wa hiyo ICC, UPOOO!!
Mkuu sisi tulijitoa kwenye ile mahakama ya Afrika inayojishughulisha na masuala ya haki ya za binadamu. ICC bado tupo labda tuanze mchakato leo wa kujitoa huko.
 
Duniani hakuna haki , wanaopigania haki duniani huishia kuumia wao wenyewe , na uzuri Mungu alishaliweka wazi ,tatizo watu tuna vichwa vigumu , alishasema Kama unataka haki fight kwenda mbinguni ,duniani huku ni sarakasi mwanzo mwisho na hyo ipo approved na mbingu
Mbingu gani ina haki? Hebu tuondolee ugaidi wako humu
 
Natamani ubalozi wetu nchini marekani watoe waraka wa kulaani matumizi ya nguvu dhidi ya waandamaji.
 
Huyo Jamaa Robert Amsterdam nilianza Kumuona si tu Mpuuzi bali pia ni Mnafiki zamani sana ninashangaa baadhi yenu leo ndiyo mnamuelewa.
 
Back
Top Bottom