Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,326
Ni kweli kama walivyosema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria.Haijawahi kutokea huko nyuma, kwa uchaguzi mkuu wa nchi yetu kuingiliwa ki wazi wazi na watu wa nchi za nje wa aina ya akina Robert Amsterdam!
Sijui ingalikuwaje kama kila mgombea wa urais katika uchaguzi huu angalikuwa na Amsterdam wake kutoka mataifa yenye nguvu duniani; yakimprotect mgombea wao na kutishia kuwafikisha kwenye mahakama ya ICC wale wote watakaoonekana kuwa tishio la mgombea wao kupata ushindi.
Fikiria kama Benard Membe naye angalikuwa na Amstedam wake, kwa dhoruba alilolipata, Seif na Zitto wangalikuwa wanasubiri kufikishwa ICC!! Fikiria dhoruba wanayoipata akina Hashim Rungwe kwa kuzuiliwa kutoa ubwabwa kwenye kampeni zao, idadi ya watu wangaliofikishwa mahakama ya ICC wangalikuwa kiasi gani? Fikiria dhoruba wanayoipata akina Lipumba na kadhalika kwa kukosa mafuriko kwenye mikutano yao na kadhalika.
Huko kwa akina Amsterdam nchi nyingine hata kuhisiwa tu kama ilishiriki kuingilia uchaguzi wa nchi yao huwa ni jambo lisilokubalika. Tulishuhudia kasheshe iliyotokea kwa China na Urusi kuhisiwa kusaidia ushindi wa Trump katika uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016. Kasheshe hii hadi sasa haijaisha na wala Trump mambo ya ICC hayamuhusu.
Sasa jee tunaweza kuwashitaki kwenye mahakama za kimataifa hawa akina Robert Amsterdam ambao wazi wazi kabisa wameingilia uchaguzi mkuu wetu? Au sheria za kimataifa zinasema nini juu ya watu kama hawa?