Tanzania Motorbike Road Trip - Tanga | Safari ya Tanga

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,167
Wakuu Habari zenu, poleni n majukumu.

Ile safari yangu ya Tanga kutumia pikipiki yangu cc110 nimefanikiwa kwenda salama na kurudi salama kabisa.. Mungu ni Mkubwa.

Niliondoka Ijumaa iliyopita, nikashinda jumamosi kwa kufanya Mizunguko ya Town na kulijua jiji pamoja na kwenda kule Amboni kwenye Mapango Ya Amboni.

Katika kuthibitisha hilo nilifunga camera kwenye Helment yangu so each and everything kipo recorded.

Video ya Safari ya kutoka Dar hadi Tanga ipo youtube nimeweka kipande cha kutoka Dar hadi Mkata then nitaedit tena kipande cha kutoka Mkata hadi Point nyingine.

Kwa upande wangu hakuna nilichopoteza, kwanza nimeenjoy road trip, nimeona vitu vingi sana barabarani pia na kunipa udhoefu mkubwa sana wa kuwapa kipaumbele mabasi au gari linalotaka kukupita.

Kiufupi, nimefanya kile moyo wangu unakipenda na hakuna mtu aliyenilazimisha kufanya.

Asante kwa wote walionishauri Service bora ya Pikipiki.



KAMA UNASWALI KARIBU UNIULIZE.

ASANTE.
IMG-20230223-WA0293.jpg
 
1. Bajeti ya mafuta?

2. Ulikuwa unafuata vibao vya spidi?

3. Safari umetumia muda gani?
Maswali Mazuri sana.

1. Kuhusu Mafuta.. Tank langu la Mafuta ni lita 4.8.. wakati nipo Dar niliweka mafuta ya elfu 12000 ambayo nilipata full Tank.. pia ilibeba kidumu cha lita 5 ambacho hicho niliweka mafuta ya elfu 14 ambayo lita kama 4 hivi.

Mafuta yaliyo kwenye tank la pikipiki nimetembea nayo mpaka Mkata (niliposimama chai) nikajaza tena yaliyo kwenye kidumu lita 4.. lita 4 hiyo ikanifikisha hadi muheza ambako kwenye dumu niliweka elfu 13000 na kwenye pikipiki niliweka elfu 9.

Mafuta hayo toka hapo muheza yalinifikisha mpaka kiwanda cha cement kile ndipo nikachukua ya kwenye dumu ambayo niliingiza kwenye pikipki kama lita 2 hivi hivyo mpaka nafika TANGA nilikuwa na Mafuta ya kutosha kwenye pikipiki na kwenye Dumu ambayo niliyatumia kesho yake kwenda Amboni Cave

NB. Sikupenda niishiwe mafuta njiani ndo nijaze.. hivyo nilikuwa nikitembea kilomita kadhaa nasimama najaza

(Kuna mtu aliniambia usisubili mafuta yaishe sababu utakuwa unahalibu kableta (sijui nimepatia jina) ile ya kuvuta mafuta wakati upo safari ndefu

PIKIPIKI YANGU KWENYE SWALA LA MAFUTA INANUSA TU ILA HOFU YANGU NDO ILIYOPELEKEA NITEMBEE NA KIDUMU BUT BILA KUDUMU NINGEFIKA BILA WASIWASI NA MAFUTA (NDO SAFARI YANGU YA KWANZA)
 
1. Bajeti ya mafuta?

2. Ulikuwa unafuata vibao vya spidi?

3. Safari umetumia muda gani?
2. Kwenye Vibao vya Speed nilikuwa makini sana kwenye 50 nilitembea 50 lakini sababu mimi sisafiri kushindana speed yangu kubwa sana ilikuwa 70 na speed ya wastani ni 60 ambayo hiyo nimetembea nayo sanaa hadi nafika Tanga (60 ni speed kubwa kwenye hii pikipiki)
 
1. Bajeti ya mafuta?

2. Ulikuwa unafuata vibao vya spidi?

3. Safari umetumia muda gani?
3. Niliondoka Dar saa 11 asubuhi.. sikumbuki Pale Mkata nilifika muda gani (sikuangalia saa pale ila nahisi ilikuwa kama saa 3 au 2) nilikaa pale kama lisaa limoja kwa ajili ya kuvuta pumzi na kuacha magari ya mikoani yapite kwanza..

Tanga niliingia saa 7 mchana (hapa njiani nilikuwa nasimama sana mara ninywe maji, mara nikute kivutio flani nipige picha so nilikuwa mtu wa kusimama simama hovyo Utalii wa ndani mara nipige na kibao karibu Tanga hope unaelewa )
 
Hako ka mkoba kwenye pikipiki kanapatikana wapi na bei gani? Kazuri sana kwa ruti
Nilinunua kariakoo ilikuwa 95000.. yeah kazuri sana.. humo niliweka:
1. Mswaki
2. Sabuni
3. Nguo za kuvaa
4. Shuka la kimasai (ili nilibeba endapo ikitokea itilafu ya kunifanya nilale polini)
5. Koti la Mvua
6. Sendo/Ndala za kushindia
7. Baadhi ya Documents ya pikipiki
8. Maji na Biskuti

Vyote vilikaa humo.. sema uwe mzuri kwenye kuvipanga, ukipanga vibaya unaweza kuona Truck dogo kumbe ni kubwa sana
 
Ulipita njia ya Bagamoyo,Msata.

Wakati mwingine unaweza kupita Saadani,Pangani ukatokea Tanga mjini. Hii ni shortcut ila bike yako hakikisha tyre zipo vizuri na mafuta ujaze ya kutosha.
Yeah wakati nipo Tanga kuna mtu aliniambia kuna shortcut hiyo uliyosema.. nikamuuliza ni barabara ya rami akasema hapana.. nikasema mmh hiyo hapana ata kama ni shortcut
 
Back
Top Bottom