Road to The Throne

Road to The Throne

Somaiyo

Senior Member
Joined
Jul 1, 2022
Posts
103
Reaction score
187
Denis ni kijana mwerevu mwenye uwezo mkubwa wa kuamua na kutenda mambo mbali mbali kwa hali
ya juu sana. Ni kijana ambaye amelelewa na familia ya Mr John Kapinga waziri mkuu wa nchi ya
KONGOA.

Mnamo mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 25 jijini London alitunukiwa shahada yake ya
kwanza ya masuala ya komputa akiwa kama mwanafunzi wa kwanza mwenye ufaulu mkubwa sana
kupita wote kwa mwaka huo akiwa na G.P.A ya 5.0 na kuweka historia ya kuwa mwanafunzi wa kwanza
kutoka nchi za kiafrika kufanya vizuri zaidi katika masomo hayo ya computa ndani ya chuo hicho kikuu
cha Oxford.

Alisomea maswala ya mtandao yaani (networking), ni mtu hatari na mbobezi aliyekuwa na uwezo wa
kukusanya taarifa mbalimbali za kiusalama kwa kuingia kwenye kifaa chochote cha mawasiliano na
kupakua taarifa zake na kuzitumia atakavyo bila kujulikana.

Aliporudi KONGOA aliendelea kuitumikia
nchi yake ya kongoa kama afisa usalama mbobezi katika maswala ya mtandao. Usoni mwa watu, Denis
alijulikana kama mtumishi wa kampuni ya simu ya AMATEL Kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu
nchini Kongoa.

Alikuwa akiamka hasubui kama watumishi wengine na kuelekea kazini kama watumishi
wengine, na alionekana kama akifanya shughuli za kawaida pale AMATEL kama watumishi wengine
kumbe yeye alikuwa pale kama undercover agent ambaye alikuwa na ofisi yake ya siri ndani ya jengo
hilo kwa ajili ya kuratibu taarifa mbalimbali za nchini Kongoa.

Denis hakuwahi kumfahamu baba yake mzazi, alichukuliwa na familia ya Mr John Kapinga akiwa na umri
wa siku moja hapa duniani, alikuja kufahamu kuwa Mr kapinga sio Baba yake mzazi alipofikisha umri wa
miaka 16 akiwa anahitimu elimu yake ya sekondari ya kidato cha nne kwenda kidato cha tano baada ya
Mr Kapinga kuamua kumweleza ukweli kuhusu historia yake.

Siku hiyo Mr Kapinga baada ya kutoka shuleni kwenye mahafali alimuita na kumweleza Denis kuwa,
aliokotwa barabarani siku ya jumapili mwaka 1989 karibu na geti la Mr kapinga na familia yake wakiwa
wanatoka kanisani na alikuwa amewekwa kwenye boksi jeupe ambalo ndani yake palikuwa na
maandishi yaliyoandikwa “AM SORY” (samahani).

Kwa ushahidi zaidi Mr Kapinga alilichukua boksi lile
alilokuwa amelitunza ndani mwake na karatasi ile aliyoikuta kwenye boksi na akampatia Denis aione,
denis ambaye wakati huo alikuwa anatetemeka huku machozi yakimtiririka kwa mshtuko wa taarifa zile
alipokea vitu vile huku akilia akiwa haamini kile alicho kuwa anaambiwa.

Hakuamini kwa kuwa alijua kabisa Mr Kapinga ndiye baba yake, na mrs kapinga “JULIETH” ndiye mama
yake, kwani ni watu waliomlea vizuri toka hajitambui mpaka kufikia umri wa kujitambua, alijua Kenedy
mtoto wa kwanza wa mr Kapinga ni kaka yake na Poul mtoto wa mwisho wa familia ile ni mdogo wake.
Hakuwahi kuwaza wala kufikiria kabisa kuwa yeye si mtoto wa familia ile kutokana na malezi yaliyo
tolewa kwa upendo mkuu na familia ile.

Zilipita dakika kumi za kulia na kutokuamini alichoambiwa, Alikuwa na maswali mengi sana kwa Mr
Kapinga. Mojawapo ni pale alipomuulliza kuhusu familia yake. Aliuliza kama familia yake ya sasa iliwahi
kufuatilia kama wazazi wake walikuwa ni akina nani alitaka kujua kwanini walimtelekeza, neno AMSORY
lililokutwa limeandikwa kwenye karatasi ile ndani ya boksi lilikuwa na maana gani na Alitaka kujua je ni
baba au mama yake ndie aliyemtelekeza pale nje getini na pia kutaka kujua ni kwa nini walimtelekeza.

majibu aliyoyapata yalizidi kumuumiza zaid Denis kwani alielezwa kuwa mpaka wanafanya mazungumzo
yale taarifa walizo kuwa nazo nikuwa Baba na mama yake wanasadikika walisha fariki dunia na chanzo
cha kifo chao hakikuwahi kujulikania na hivyo hawakuwahi kujulikana wanatokea upande gani mwa nchi
ya KONGOA.

Taarifa za uhakika walizozipata nikuwa alizaliwa katika hospitali ya Mtakatifu John na
ilijulikana hivo baada ya Denis kuokotwa, alipelekwa hospitalini kumuangalia kama anatatizo loloe la
kiafya na yupo nesi aliyemfahamu denis akiwa mchanga kwani nguo alizokuwa amevishwa wakati
anaokotwa ni yeye aliyezitoa kwa mama yake na niyeye aliyemfunga bangili yenye jina lake mkononi
kabla ya kuwaruhusu denis kichanga na mama yake kuondoka.
*************************************************************************************************
 
*****************************************************************************
“Mr Kapinga”, tuna tatizo….. Mh rais amewaelekeza vijana wake kukusanya taarifa zote kuhusu wewe,
amemuagiza Tobi ahakikishe kuwa anajua kila unachofanya ama kutenda, wamepanga kuweka vinasa
sauti nyumbani kwako, hii ni baada ya wewe kuwa nampango wa kugombea urais baada ya yeye
kumaliza awamu yake hii ya pili na ya mwisho. Mr kapinga alipokea taarifa ile kwa kunogonezwa na
bwana Mpambije class mate wake, wakiwa wamekaa kwa karibu meza kuu wakimsubiri Mh Rais mr
John Balikenga aliyekuwa njiani kuelekea mahala hapo kwa ajili ya maadhimisho ya sikukuu ya
wafanyakazi duniani mei mosi. Mr kapinga alicheka sana na kwa kujiamini sana alimjibu Mr Mpambije,
msimamizi mwandamizi wa masuala ya usalama kitengo cha ikulu “I know Mpambije, this isn’t the
right place, tutaongea” mpambije alibaki na mshangao akamuuliza what do you mean Kapinga?
(unamaanisha nini kapinga) akiendelea kucheka ili kuonesha kama hakuna linaloendelea pale meza kuu
bali anafurahia ngoma ya kisukuma iliyokuwa ikiendelea mbele yao mr kapinga alimjibu mpambije, “I
told you this isn’t the right place, we will discuss this matter soon” (nimekwambia hapa sio mahala
sahihi, tutaongea) “sawa” alijibu mpambije akiwa bado anashauku ya kujua tarifa zile mr kapinga
amezipataje.


John balikenga, rais wa KONGOA, rais anaeyeogopwa na kipenzi cha wengi alikuwa njiani akielekea
uwanja wa mkoa wa kanda ya kusini kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani. Alifika mkoa ule kwa
ziara ya siku tatu, na moja ya kazi alizopaswa kufanya ni kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo.
Akiambatana na mkewe Maria, wakiwa kwenye special presidential limosine, Mr john alikuwa mwenye
mawazo. Alikuwa akiwaza ni nini anakwenda kuwaambia watumishi wake. Kwani Katika miaka yake 8 ya
utawala wake, hakuwahi kuwapa nyongeza ya mshahara wala promosheni za vyeo kama alivyo wahi
kuwaahidi miaka 8 nyuma alipokuwa akiwaomba ridhaa. Watumishi hawa walikua na malalamiko mengi
sana, kama vile viongozi na wanasiasa wa vyama kuingilia majukumu yao ya kila siku, kudhalilishwa na
hata kuondolewa kazini bila kufuata utaratibu wa sheria

Wengi walikuwa wamekata tamaa ya maisha, walifanya kazi kwa kutawaliwa na sio kuongozwa, hata
siku hiyo wengi wao walitishiwa kufika eneo la tukio na walipaswa kumshangilia Mr John balikenga rais
wa KONGOA kwa kila atakaloongea. Hawakuwa na furaha. watumishi hawa waliandamwa na makato
mengi kwenye mishahara yao, ivyo kuwalazimu kuishi kwa kukopa kopa kusukuma siku zao za kuishi.
Wakiwa kwenye gari, Maria alimuangalia mmewe kwa haraka nakugundua kuwa hayupo sawa, yupo
kwenye msongo mkubwa wa mawazo, akaamua kumsogelea na kusogeza mkono wake mpaka kwenye
kiganja cha mkono wa kulia wa mumewe, “Baby Are you okey?” (mpenzi uko sawa?) John anashtuka
kidogo, “Yeah am Fine”. (ndio niko sawa) “Usijali…….., evrything will be fine. Stop thinking, by the way
you should remember that, you have done as much as you can so far for these people and the country”
(acha kuwaza sana, kumbuka umeshafanya mengi sana kwa watu wako na taifa). Kwa sauti laini na
yakuvutia Maria alimweleza mumewe.


Mr john alitikisa kichwa chake kukubaliana na aliyoelezwa na mkewe. “I love you; you know that, the
thing is Mr kapinga is one who is stressing me out, how can he plan to take over me after everything I
have done for him? How?” (Nakupenda, na naamini unajua hivyo, kitu kimoja tu kinaniwazisha hapa
kwanini Mr Kapinga anataka kuniondoa madarakani haswa baada ya mimi kumfanyia yeye mambo
mengi tena mazuri tu, kwanini?) John ali ng’aka. Akimshika taratibu mabegani kwa kutumia kiganja cha
mkono wake laini wa kushoto maria anampapasa mabegani na kumtuliza mmewe anatambua kuwa
hayuko sawa. “My love i know it is very full stressing, but let us done with this event, I know you’re my
lion, you will win this battle so take it easy and smart”. (mpenzi najua inachanganya lakini hemu
tumalizane na hili tukio la leo, najua wewe ni simba na utawashinda nenda tu taratibu na kwa umakini)
Mr john alisuuzika kidogo kwa mkewake kumpa moyo. Alimshika mkono na kumpa busu shavuni kama
ishara ya kupendezwa na lichosikia. Kidogo alipata faraja ya muda


Body gurd wa Mh Rais alitoa ishara kwa Mh Rais kuwa sasa wanaingia uwanjani na kwa kutumia kifaa
chake cha kisasa kabisa cha mawasiliamo aliwasiliana na wanausalama waliokuwa nje “number one is
here” (namba moja yuko hapa). Watu walikuwa wa mejaaa uwanjani, wanafunzi raia na watumishi wa
kada mbali mbali, hakukuwa na shamra shamra za kutukuka kama ilivyokuwa imezoeleka awamu za
nyuma, mh rais alishuka kwenye gari yake nakuwapungia mkono wana nchi akielekea jukwaa kuu huku
makofi na nyimbo za kumsifu zikiendelea kupigwa.
**********************************************
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom