Kama siasa zenyewe ndizo hizi za kutishiana, angalieni msije kuwaponza hao mnaowategemea kuchukua nchi 2015, wazee wa kazi wasije wakawapotezea into thin air kabla ya 2015!. Si niliwawekea hapa kisio la chini la utawala wa CCM kwa nchi hii ni miaka 100!, hansini iliyomalizi na sasa bado 50 mingine!. Kumbukeni hamwezi kugombea kisu, mwenzako ameshika kwenye mpini, kabla kisu hujakishika, unaana kumtishia atakiona cha mtema kuni!, unajua anaweza kukasirika na kuamua sio tuu kukushikisha kwenye makali, bali kukukata nacho!.
Hakuna ubishi Chadema ndicho chama chenye matumaini makubwa sana kwa sasa, lakini watakaokiponza Chadema, ni watu wenye mawazo kama haya!, mtanisamehe kusema watu wenye mawazo kama haya, hawana akili timamu japo sio lazima mpaka waokote makopo!, hawa ndio ma hate preachers ambao Chadema inapaswa kuwashughulikia kwanza wasije wakakitibulia ushindi laini wanao uotea!.