KICHUNA CHANGU
Member
- Feb 5, 2016
- 16
- 4
RIWAYA: ANGAMIZO
MTUNZI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
WHATSAPP 0757633010
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA JANA
"Tunaweza kuonana baadae sehemu tofauti na hapa?"
"Bila shaka"
WalibadiLishana namba zao za simu palepale kwenye foleni. Zoezi la usajili lilichukuwa saa zipatazo tano.
Hatimaye Abdul akasajiriwa kama mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha udaktari Arusha.
SASA ENDELEA...
Kuwa Daktari ilikuwa ndoto yake ya siku nyingi sana. Alikuwa anajua masomo ya msingi ili awe daktari. Alikazana sana katika masomo hayo. Alijitahidi sana katika somo la Kemia. Alijitahidi sana katika somo la Fizikia, alijitahidi pia katika somo la Baiolojia. Alifanikiwa kupata alama nzuri katika masomo hayo matatu pale Bagamoyo Sekondari. Alikuwa anapenda awe daktari ili aje kusaidia wananchi maskini wanaoteseka kwa kukosa pesa za matibabu. Siku zote alikuwa anajisemea mwenyewe.
"Mimi ndiye daktari pekee nitakayekuwa mkombozi kwa maskini wote wanaoteseka kwa maradhi mbali mbali kwa kukosa pesa za matibabu"
Baada ya kusajiriwa, Abdul alienda katika Hosteli za chuo kupumzika. Alijilaza kitandani huku akikumbuka misukosuko ya safari yake ya kusaka elimu. Alikumbuka alivyoteseka kipindi kile anatafuta hela ya ada pamoja na ya matumizi ili aende kusoma shule ya Sekondari Ndanda. Alienda kuomba serikalini lakini hawakumuelewa. Alienda kuomba kwa Mbunge wake naye hakumuelewa . Hakupata hela ya ada, hakupata hela ya nauli. Bado alikuwa na elfu kumi ndani, chini ya mto wake wa kulalia. Ilikuwa bado wiki moja ili shule ifunguliwe. Na Abdul akaanze kidato cha tano. Sasa ndoto yake ilikuwa inaanza kuyeyuka. Hakuwa na njia ya mkato ya kumpeleka shule.
" Si ruhusa kukata tamaa katika maisha ukiwa bado unaishi.." Kauli ya mwalimu wake ilijirudia tena katika kichwa chake.
"Sasa kwanini mimi naruhusu kukata tamaa nikiwa bado ninaishi. Tena na afya tele. Haiwezekani. Lazima niende Mtwara nikasome "
Usiku wa siku ile alipata wazo. Wazo ambalo lilipewa baraka na kichwa chake. Aliamua kwenda Mtwara kwa miguu! Alikuwa ameamua hivyo. Usiku ule ule aliweka vitu vyake vyote sawa. Tayari kwa safari.
Asubuhi aliwaambia wazazi wake.
"Baba na Mama mimi leo naenda shule "
"Umepata ada mwanangu ?" Mama yake alimuuliza kwa sauti yake ya upole.
" Hapana"
"Sasa utaenda vipi shule ?" Baba yake alimuuliiza nae.
" Kwa miguu"
"Miguu ?"
"Ndio wazazi wangu. Lazima niende Mtwara kusoma. Na nimeamua kwenda Mtwara kwa miguu !" Alisema akiwa anajiamini sana.
"Hivi Abdul unaujua umbali wa Mtwara kutoka hapa ?"
"Siujui, lakini nitafika "
"Ni mbali sana Mtwara, huwezi kwenda kwa miguu Abdul " Mama yake alimwambia kwa sauti yake ya upole.
"Nimeshafunga kila kitu changu. Ilibaki kuwaaga nyinyi na ndugu zangu. Nakubali Mtwara ni mbali. Lakini bila elimu safari yetu ya kuelekea kwenye mafanikio inazidi kuwa mbali. Bora niumie kwa kutembea kwa miguu kuisaka elimu. Kuliko kuumia kwa umaskini huu uliotukuka. Umaskini umeweka kambi nyumbani kwetu. Hautaki kutuacha hata kidogo. Na kitu pekee kinachoweza kuufukuza umaskini huu kipo Mtwara. Lazima niende Mtwara "
"Tufanye utaenda Mtwara kwa miguu. Je hela ya ada utaitoa wapi ?" Baba alimtupia swali zito.
Alifikiria kidogo akajibu. "Nitajua huko huko Mtwara. Lakini lazima nifike Mtwara kwanza. Mambo mengine yatajijibu huko huko."
Wazazi wake hawakuwa na jinsi. Walimruhusu aende Mtwara . Mama yake alikuwa analia machozi kwa kumuonea huruma Abdul. Baba yake alikuwa anamhurumia pia. Abdul alikuwa jasiri na imara katika msimamo wake. Alidhamiria kwenda kusoma Mtwara kwa njia yoyote ile . Baba aliwaita ndugu zake wote. Akawaambia juu ya safari ya Abdul ya kwenda shuleni Mtwara, tena kwa miguu. Ndugu zake wote walisikitika sana. Kila mmoja aliingia ndani na kutoa akiba aliyojiwekea na kumpa. Abdul alianza safari yake ya kutoka Bagamoyo kwenda Mtwara akiwa na elfu ishirini tu. Familia nzima aliiacha kwenye majonzi makuu. Hakujari. Hakusikitika. Alidhamiria kwenda kusoma. Alidhamiria kweli kwenda Mtwara kwa miguu.
....Abdul alikuwa katikati ya mawazo, simu yake iliita. Aliangalia kwenye kioo cha simu yake, alikuwa Mayasa. Aliipokea na kuanza kumsikiliza.
"Hallo"
"Mambo Abdul "
"Safi Mayasa, nambie"
"Nipo tu, nilikuwa na ombi moja Abdul "
"Nakusikiliza"
"Naomba nikualike chakula cha usiku leo"
"Haina shida, wapi ?"
"Tukutane Tengeru hoteli saa mbili usiku"
"Sawa Mayasa "
"Sawa baadae"
Simu ikakatwa.
Abdul alipoambiwa habari ya chakula cha usiku. Alikumbuka kitu. Alimkumbuka Raiya. Mwanamke aliyesoma nae shule ya Msingi kule Bagamoyo, na kuja kukutana nae kama bahati jijini Dar es salaam. Alikutana nae kama bahati siku ile anatembea kutoka Bagamoyo kuelekea Mtwara kwa miguu.
Siku ile alitembea kweli kwa miguu kutoka Bagamoyo hadi Dar es salaam. Alipofika Mwenge ndipo alipokutana na Raiya akiwa anauza duka la simu pale Mwenge. Ni Raiya ndiye aliyemuona na kumwita Abdul.
"Mambo Abdul ?"
"Safi Raiya, za siku ?"
"Nzuri, vipi mbona na begi mkononi, unaenda wapi ?"
"Mtwara "
"Mtwara utapata gari sahivi. Saa saba hii Abdul ?"
"Naenda kwa miguu " "Miguu ?!!!"
"Ndiyo Raiya"
Abdul alimsimulia kila kitu Raiya kuhusu maisha yake. Alivyofika mwisho aliukuta uso wa Raiya hautamaniki. Umelowa kwa machozi. Alimuonea huruma, na kuahidi kumsaidia.
"Ngoja nikupe hela hii ukapumzike Hotelini. Halafu kesho nitakusafirisha Mtwara. Na pesa ya ada nitakupa"
"Ahsante sana Raiya yaani sijui nikushukuru vipi dada yangu."
"Jioni nikifunga hapa nitakupigia simu tukapate chakula cha usiku sehemu"
"Sina simu Raiya" Raiya alitoa simu moja iliyokuwa kwenye droo pale dukani na kumkabidhi.
Kwa siku ile alimuona Raiya Mungu mtu. Alienda kutafuta chumba cha kupumzika. Kebby hoteli lilikuwa jibu lake. Akaingia ndani na kukaa kitandani. Aliitoa ile simu aliyopewa na Raiya na kuichaji Kebby hotel ilikuwa hoteli nzuri ya kisasa yenye gharama nafuu iliyokuwa Kijitonyama. Ilikuwa na kila kitu ndani. Kwa Abdul Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala kwenye hoteli kubwa kama ile. Siku ile ilikuwa ni moja ya siku aliyokuwa na furaha sana. Ndoto yake ya kusoma ilikuwa inaenda kutimia. Tena inatimizwa na mtu ambaye hakutegemea kabisa. Kweli usimdharau mtu yeyote duniani. Ingawa yeye na Raiya hawakuwa marafiki kipindi wanasoma, lakini walikuwa wanaheshimiana sana. Heshima ile bila shaka ilimpa moyo Raiya wa kumsaidia leo hii.
Saa moja kamili walikutana na Raiya pale Kebby hoteli. Kulikuwa na mgahawa mzuri wa kisasa mbele ya hoteli ile. Walikaa na kupata chakula cha usiku. Wakati wanakula waliongea mambo mengi sana na Raiya. Raiya alimsimulia mambo mengi sana Abdul kuhusu maisha yake. Kumbe kwa sasa Raiya alikuwa mke wa mtu. Alimsimulia mateso aliyokuwa anayapata toka kwa mumewe. Mumewe hakuwa anampa vizuri haki yake ya ndoa .
" Sasa Abdul mimi nitakupa hela" "Nitashukuru sana yaani dada yangu"
"Lakini kwa sharti moja tu"
"Nipo tayari kufuata sharti lolote Raiya"
"Kweli ?"
"Kweli nakwambia"
RAIYA YUPO TAYARI KUMSAIDIA ABDUL LAKINI KWA SHARTI MOJA TU, NI SHARTI GANI HILO, SEHEMU YA TATU YA RIWAYA HII YA ANGAMIZO NDIO INA JIBU...TUKUTANE TENA HAPA KESHO ASUBUHI MUNGU AKIPENDA....