Riwaya: UCHU

UCHU

KAZI KWAKO II

Ilikuwa saa tatu na nusu Chifu alipompigia simu
Jack Musoke kule Arusha.
"Naam Chifu. Nilikuwa nasubiri huku kiroho
kinanidunda. Haya nipashe".
"Willy Gamba ndiye mtu wako, mpokee uwanja
wa ndege saa sita na nusu mchana".
Musoke alipigwa na butwa. Hakuweza kujibu
kwa ajili ya furaha na msisimko. Hata Chifu
alipokata simu hakusikia. Utafikiri kapigwa na
radi.
"Willy Gamba! Willy Gamba! Jamani huyu Chifu
nitamfanyia nini kwa kumleta willy Gamba!
Mungu anatupenda sana Waafrika maana sasa
kazi itafanyika", Musoke alijisemea kama kichaa.
Baada ya kuachana na Chifu, Willy Gamba
alikwenda tena kwenye ofisi za Shirika la Ndege
Tanzania ATC kujua kama kutakuwa na ndege
ya kurudi siku ile ile jioni, maana Chifu alimkatia
tiketi ya kurudi kesho yake jioni ambayo
hakuiafiki. Alitaka arudi siku ile ile.
"Kuna ndege toka Kilimanjaro jioni", Willy
alimuuliza kimwana mmoja kati ya vimwana
walikuwa kwenye kaunta wakiwashughulikia
wateja.
"Hakuna ndege jioni, kuna inayoondoka saa tano
na nusu hapa na kuondoka kule saa saba na
dakika kumi basi', yule kimwana alijibu huku
akimrembulia macho.
"Hakuna ndege ya shirika lingine lolote?".
"Hakuna, labda uchukuwe ya kukodi huko
Tanzanair", kimwana alijibu kwa kebehi akijuwa
kuwa Willy hawezi kumudu gharama za kukodi
ndege.
"Unaweza kunifanyia mpango ili hiyo ndege
inichukuwe uwanja wa ndege wa Kilimanjaro saa
kumi na mbili jioni?", Willy aliuliza katika hali ya
kuomba.
"Sisi haturuhusiwi, sisi tunahusika na kuuza
tiketi za ATC tu", yule kimwana alijibu kwa
wasiwasi. Willy alitoa kadi yake, na kumweleza.
"Mimi ni mteja wenu mzuri sana. Nenda hapo
Tanzanair kanikodishie, nitamtuma katibu
mahsusi wangu, atakuja kukuona mkalipe na
kwa kufanya kazi hiyo na wewe utapata
chochote kwani hakuna kazi ya bure siku hizi.
Wewe unaitwa nani?".
Akiwa amepigwa na butwa yule msichana
alijibu. "Naitwa Mariam".
"Oke, Mariam fanya hiyo kazi kungali mapema,
mimi naenda uwanjani kuwahi ndege yenu ya
saa tano. Katibu wangu anaitwa Dudu, atakuja
kumaliza mambo ya malipo na wewe".
Kabla Mariam hajaanza kulalamika Willy alikuwa
amekwisha nyanyuka na kuondoka.
"Wanaume wengine utafikiri wana dawa. Huyu
mwanaume kanitia butwa, sasa itanibidi nifanye
hiyo kazi yake; nimeshindwa hata kupata
mwanya wa kukataa", Mariam alimweleza
mwenzake aliyekuwa amekaa karibu naye.
"Hukuona macho yake! Akikuangalia tu roho
inadunda, hiyo ndiyo dawa yake, ni mwanaume
anayevutia sana, ana sumaku ya kiume,
mwanamke hawezi kumkatalia kitu naye
anajuwa hivyo", Husna alimjibu Mariam.
Mariam aliondoka na kwenda kumtafutia Willy
ndege huku kiroho chake kinarukaruka. "Sijui
nitamwona tena yule mwanaume, kaniachia kadi
yake, ngoja nitamtafuta", Mariam alifikiri huku
akielekea ofisi za Tanzanair.


ITAENDELEA
 
Daaah sasa kazi kwangu iko wapi hapa mkuu
 
UCHU

KAZI KWAKO III

Willy Gamba alipofika ofisini kwake kwenye
jengo la Sukari, Mtaa wa Ohio, ilikuwa saa nne
na robo. Dudu aliangalia saa yake na
kumwangalia Bosi wake kwa macho ya
kumshitaki kuwa kachelewa.
"Shikamoo bosi", Dudu alimsalimia Willy.
"Marahaba, najuwa umeninunia kwani sikuwahi
kutimiza miadi na wateja.
"Kumbe unajuwa, na ukafanya makusudi", Dudu
alijibu.
"Siyo makusudi, ila ndiyo sababu kuna usemi
kuwa, bosi hachelewi kazini, huwa amepita
kwenye shughuli kadhaa wa kadha, nami nilipita
kwenye shughuli kadha wa kadha. Sasa sikiliza,
mimi naondoka kwenda Arusha kwa ndege ya
ATC saa tano unusu, nina muda mfupi sana.
Kumetokea dharura. Nataka nirudi leo jioni,
maana dharura hii inaweza kunifanya nisafiri
kwa muda wa wiki kadhaa nje ya nchi. Kwa vile
ATC hawana ndege kutoka Kilimanjaro jioni,
nimemuomba msichana mmoja aitwaye Mariam
pale kwenye ofisi ya mauzo ya ATC anifanyie
mpango wa ndege ndogo ya kukodi ya
Tanzanair. Hivyo, uende ulipie na ndege iwe
kwenye uwanja wa ndege wa Arusha saa kumi
na mbili jioni, umeelewa?".
"Nimeelewa bosi, naona kweli dharura, mpaka
kukodi ndege, nani atalipia gharama hizi bosi?".
"Nina mteja ambaye atalipia", Willy alijibu.
Dudu alikwisha fanya kazi na Willy kwenye ofisi
yao hii ya watu wawili kwa muda wa miaka
mitatu. Hivyo alikwisha mwelewa vizuri Willy na
alifurahi sana kufanya kazi na mtu sifa na
mwenye roho nzuri kama Willy. Hata siku moja
hakupata ugonjwa wa moyo toka kwa bosi wake
huyu. Alikuwa mtu tofauti sana na watu wengine
ambao Dudu aliwahi kufanya nao kazi.
Baada ya kuacha kazi serikali, ambako alifanya
kazi kama mpelelezi, na akawa mpelelezi wa
kutegemewa si Tanzania tu bali Afrika nzima,
Willy Gamba aliamua kuanzisha ofisi yake
binafsi ya upelelezi, hasa iliyohusu mambo ya
Bima. Aliamua kuacha kazi akiwa na umri
mdogo wa miaka 42 tu. Kwa vile alitaka aoe
kwani kazi yake serikalini ilimfanya asafiri sana
nje, kitu ambacho kilimfanya asioe maana ndoa
yake ingekuwa ya wasiwasi. Hivyo aliomba na
kwa shingo upande na baada ya malumbano ya
muda mrefu na waajiri wake huku akisaidiwa na
Chifu ambaye alikuwa Bosi wake kabla
hajastaafu, alikubaliwa kuacha kazi. Ndipo
baada ya kuacha kazi, akamwoa mchumba wake
ambaye alikuwa amesubiri kwa muda mrefu
huku akimvumilia kwa safari zake nyingi.
Huyu mchumba wake aliitwa Pepe. Pepe alikuwa
mtoto wa watu, msichana aliyeumbika, mzuri
wa sura na tabia, na kwa uzoefu wake mwingi
kwa wasichana, Willy aliamua lazima amwoe
Pepe na kila wakati alimwambia mama yake
ambaye kila siku alikuwa akimpigia kelele aoe,
na asipomuoa Pepe basi hataoa tena.
Mama yake Willy alikuwa na wasiwasi sana na
Pepe, kutokana na jinsi mtoto yule alivyokuwa
mzuri wa sura. Alifikiri kuwa msichana mzuri
kiasi kile hawezi kuwa mke wa nyumbani kwani
lazima atakuwa na maringo. Lakini Mama yake
Willy alikuwa kakosea kabisa. Huyu msichana
alikuwa amelelewa kwao, wazazi wake walimlea
kwa kumtayarisha ili aje awe mke wa mtu.
Walimsomesha vizuri mpaka chuo kikuu, lakini
walihakikisha kuwa Pepe anapata mafunzo ya
namna ya kuishi na watu na maisha ya ndoa
yanapewa kipaumbele. Na kweli pamoja na uzuri
usioelezeka wa maumbile ya Pepe, tabia yake
ilikuwa nzuri isiyoweza kuelezewa vilevile. Hii
ndio inaonyesha kuwa tabia ya mtu haitokani na
maumbile yake, bali zaidi inatokana na malezi.
Hivyo, baada ya kuacha kazi, Willy alifanya vitu
viwili kwa mara moja. Alianzisha ofisi yake
binafsi na akamwoa Pepe. Na hii miaka yao
mitatu ya ndoa ilikuwa miaka mitamu iliyojaa
kila aina ya raha, starehe na mapenzi yasiyo
kifani. Kila mtu aliyewaona na kujuwa
walivyokuwa wanaishi, aliwaonea wivu.
Dudu naye aliajiriwa na Willy alipofungua tu ofisi
yake, Chifu ndiye aliyemtafutia mfanyakazi huyu.
Hivyo hata ofisini kwake kazi zilifanyika vizuri na
kwa uelewano mkubwa. Kweli Willy alikuwa
hatoka nje ya Tanzania kikazi, ila tu kwa
mapumziko ambayo alisafiri pamoja na Pepe
wakitalii nchi nyingi sana, na kumwonyesha
dunia ilivyo.
"Kama ndege inaondoka saa tano na nusu itabidi
uwahi maana siku hizi msururu wa magari
kwenye barabara ya Nyerere ni hatari".
"Kweli kabisa, niitie taksi, AVIS, na uwaeleze
waje wanipokee jioni, kama yule dereva wao
Ismail yupo ningependa aje yeye".
Ofisi za AVIS zilikuwa ofisi mpya jijini Dar es
Salaam na haikuwa mbali na ofisi za Willy.
Tangu ianzishwe ilikuwa na uhusiano wa karibu
na ofisi ya Willy vilevile meneja wao walikuwa
rafiki wa Willy.
"Pepe ana habari", Dudu aliuliza baada ya
kuagiza taksi.
"Hajui, na ndio maana ningependa nirudi jioni ili
kama nitasafiri nje ya nchi nijuwe
nitamwelezaje. Na maelezo ili yaeleweke usiku
ndio mzuri, hasa mkiwa ndani ya shuka".
"Au vipi", Dudu alidakia.
"Hivyo akipiga simu mwambie nitachelewa
kurudi nyumbani, huenda hadi saa mbili usiku.
Pale shuleni kwao kama kawaida ya Dar es
Salaam, simu bado haifanyi kazi".
"Nitamweleza baba, usiwe na wasiwasi".
Taksi ilifika. Willy akachukua mkoba wake tayari
kuelekea uwanja wa ndege.
"Shikamoo", Ismail alimwamkia Willy.
"Marahaba Ismail, maana sasa abiria tayari
wana 'check-in' fanya kila njia sitaki kuachwa
na ndege hii".
"Inaondoka saa ngapi?".
"Saa tano u-nusu".
"Dakika hamsini zimebaki, utawahi acha mimi
nifanye kazi yangu", Ismail alimjibu Willy
wakaondoka.
Kweli Ismail aliijuwa kazi yake maana
walipotoka kwenye jengo la Sukari aliingia Mtaa
wa Ohio ili kukwepa msururu wa magari,
akaingia Barabara ya Titi Mohamed, alipofika
Mnazi Mmoja akaingia Mtaa wa Uhuru, halafu
Lumbumba na kisha Mtaa wa Lindi tukatokea
Ilala na kushika tena Mtaa wa Uhuru, tukaingia
Barabara ya Nelson Mandela. Ndipo akashika
Barabara ya Nyerere kwenye taa za Tazara, na
ndani ya dakika ishirini tulikuwa Uwanja wa
Ndege.
"Asante Ismail", Willy aklimshukuru na
kumkabidhi shilingi elfu moja kama asante.
"Usisahau jioni?".
"Nimeshaelezwa mzee, utanikutwa nakusubiri".
Willy alijulikana sana na wafanyakazi wa ATC na
Dahaco, kwenye kaunta ya kujiandikisha kabla
ya kuondoka na kwa vile alikuwa na mkoba
wake tu walimchukuwa mara moja na kulipia
kodi ya kiwanja na kuelekea chumba cha
kuondokea.
Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania ATC
iliondoka Dar es Salaam saa tano na nusu
kamili. Willy alikuwa na tiketi ya daraja la
kwanza, na alipoingia ndani ya ndege akitafuta
mahali pa kukaa alimwona mwalimu wake, mzee
Petro Magoti, akimchekea.
"Njoo ukae hapa Willy, habari za siku nyingi?".
"Nzuri, shikamoo", Willy alijibu huku akiuweka
mkoba wake chini ya kiti chake.
"Marahaba, nimefurahi kukuona baada ya miaka
kama mitatu hivi".
"Asante mwalimu, unajuwa nilikwambia wakati
tulipoonana Mwanza kuwa nilikuwa natarajia
kuacha kazi ya kuajiriwa ili nijiajiri mwenyewe,
sasa tayari nimefanya hivyo. Na pia sasa
nimeoa.
"Aha, hongera, nimefurahi sana nikisikia
wanafunzi wangu mkiendelea vizuri", Mzee
Magoti alijibu.
Mzee Magoti alikuwa Mkuu wa Shule ya
Sekondari ambako Willy alisoma. Kwa vile Willy
alikuwa na akili nyingi sana darasani, walimu
wengi walimpenda sana na kumheshimu. Hata
wakati matokeo ya mtihani wa Cambridge wa
darasa la kumi na mbili yalipotoka Willy alipata
ushindi wa juu kuliko mwanafunzi mwingine
yeyote katika Afrika Mashariki na hivyo kuiletea
shule ya Mwalimu Magoti heshima kubwa.
Kutokana na matokeo hayo mazuri hata
Mwalimu Magoti alipandishwa cheo hata
kushika nyadhifa mbalimbali katika Wizara ya
Elimu hadi kufikia kuwa Kamishna wa Elimu. Na
alipostaafu walimu walimchagua kuwa
Mwenyekiti wa Chama chao kama miaka miwili
iliyopita.
"Nimekusikia ukiunguruma kwenye magazeti
kuhusu matatizo ya walimu", Willy
alimzungumzia.
Ndege ilikuwa inaweka speed ili iruke. Hivyo
kama ilivyo kwa abiria wengi wakati huu kila
mtu hunyamaza kimya akingojea ndege ipae
ndipo waendelee na mazungumzo.
"Ndio kijana wangu, hali ni mbaya sana
mashuleni mpaka sasa walimu wana mgomo
baridi. Watoto hawasomi kabisa, shule ambazo
zinasemekana zinasoma, hasa zile za Sekondari,
mwalimu anaweza kuingia darasani mara moja
kwa wiki. Sasa utasema huku ni kusoma kweli,
si hatari kwa maendeleo ya hawa vijana wetu
ambao watakuwa viongozi wetu wa baadaye",
Magoti alijibu.
"Lakini mzee, wewe ukiwa kiongozi wa walimu
si uzungumze nao waelewe athari za kufanya
hivyo kwa taifa hili", Willy alimshauri.
"Bwana mdogo, wewe unaweza kumshauri mtu
mwenye njaa! Walimu hawa wote wana njaa,
ndicho kilio chao. Mishahara ya serikali wewe
mwenyewe unaijuwa. Na kutokana na kupanda
kwa gharama za maisha, mshahara wa
mwalimu wa kawaida anaweza kuutumia kwa
siku tatu tu katika mwezi na ukaisha, je, siku
ishirini na saba afanyeje?", Mzee Magoti aliuliza.
"Lakini mzee hii inahusu watu wote walioajiriwa
serikalini. Wote mishahara yao haitoshi", Willy
alijibu.
"Ahaa, sasa unasema. Yote hii inategemea
unyeti wa kazi. Ili watu wajiongezee kipato
wanahangaika na kufanya shughuli nyingine.
Sasa hivi ukienda kwenye maofisi mengi ya
serikali hukuti watu, ukiuliza katoka nje kikazi.
Kweli kikazi, maana anakwenda kufanya kazi
kwenye miradi yake binafsi, iwe kwenda
kukamua ng'ombe wake maziwa au kuwatafutia
majani, au iwe kwenda kununua bia kwenye
kampuni ya bia ili apeleke kwenye kiduka chake
pale nyumbani, yote wanasema kaenda nje
kikazi. Sasa kwa mwalimu hahitaji kutoka. Mimi
nimekuwa mwalimu karibu maisha yangu yote,
ualimu ni kazi ambayo unahitaji saa ishirini na
nne, siyo kazi unayoweza ukafanya na kazi
nyingine, hutaweza kuifanya sawasawa, Saa hii
unafundisha. saa hii unasahihisha kazi za
wanafunzi, saa hii unatayarisha masomo kwa
ajili ya kesho. Kweli kazi ya ualimu ni nyeti
inayohitaji muda wako wote. Sasa walimu nao
wanapofanya kama wafanyakazi wengine na
kuwa na miradi matokeo yake ndio hayo!
wanafunzi hawafundishwi", Mzee Magoti
alieleza.
Mhudumu wa ndani ya ndege alifika na
kuwauliza watakunywa nini.
"Mimi chai", Mzee Magoti alijibu.
"Na mimi chai", Willy naye pia alijibu.
"Msingependelea bia au pombe nyingine kali",
yule msichana aliendelea kuwashawishi.
"Hapana ni mapema mno", Mzee Magoti alijibu
huku Willy akitingisha kichwa kukubaliana naye.
Hata kama Willy angependa bia lakini haikuwa
heshima mbele ya mzee aliyemheshimu kama
huyu kufanya hivyo.
"Haya, chai yenu inatengenezwa.
"Asante", walijibu, tena kwa pamoja. Kisha
wakaendelea na mazungumzo yao.
"Sasa Mzee Magoti, si mmeieleza serikali na
serikali inajuwa tatizo hili, na athari zake kwa
taifa hili! Maana hawa vijana ndio taifa la kesho,
na kama hawasomi ina maana karibuni tu
tutakuwa na taifa la wajinga. Yaani wakati dunia
inaingia kwenye karne ya ishirini na moja, elimu
ndio kitu muhimu kwa taifa lolote, ili liweze
kwenda sambamba na mataifa mengine katika
sayansi na teknolojia: kama maneno unayosema
ni kweli basi tuko hatarini", Willy alieleza
mawazo yake kwa Mzee Magoti.
"Maneno yako ni kweli kabisa kijana. Na hiki
ndicho tunachopigia kelele sisi mpaka sasa
hatuelewani na viongozi wakifikiri tunajaribu
kuwachochea wananchi. Lakini viongozi wetu
hawajali kabisa. Jibu lao kila siku ni kwamba
hali ya uchumi ni mbaya, na serikali haina fedha.
Lakini sababu kubwa kwa nini hawajali. ni kwa
sababu wao na marafiki zao hawaathiriki na
tatizo hili walimu hapa nchini, maana wao
wanasomesha watoto wao nje. Hivyo hawajali
kama watoto hawasomeshwi: wa kwao
wanasoma nje na katika shule za hali ya juu",
Mzee Magoti alijibu kwa uchungu sana.
"Mzee Magoti umegusa kitu cha hatari sana.
Yaani viongozi wetu wamekuwa na ubinafsi.
Kwa vile wao wana pesa, basi wanapeleka
watoto wao nje na hawajali nini kinawapata
watoto wa wakulima na wafanyakazi, ambao
hawana uwezo wa kupeleka watoto wao nje".
"Barabara kabisa Willy, lakini zaidi ya hapo
wanajenga tabaka la watawala na watawaliwa.
Kwa vile watoto wa wakulima na wafanyakazi
ambao ndio wengi katika nchi hii, watapata
elimu duni, basi hawa watoto wa viongozi na
matajiri ambao ni kama asilimia (2%) ya idadi
ya watoto wote wa nchi hii, watarudi na elimu
nzuri na hivyo ndivyo watakavyoshika madaraka
hapo baadaye maana wao watakuwa
wamesoma vizuri, na kama ulivyosema ndivyo
wataenda sambamba na mataifa mengine. Hii ni
hatari kubwa kwa taifa hili", Mzee Magoti alijibu
tena kwa uchungu.
"Ina maana viongozi wetu wanaiachia hali hii ya
kushuka kwa kiwango cha elimu nchini kwa
makusudi kabisa ili wawape watoto wao na wa
matajiri nafasi ya kuendelea kuiongoza nchi hii,
na kuwanyima watoto wa watu wa kawaida
nafasi hii! Kama hii ni kweli, basi tunaelekea
kubaya, maana katika nchi hii tangu uhuru
watoto wa watu wa kawaida, ambao ndio sisi,
serikali ilitupa nafasi nzuri na kutusaidia ili
tuinuke na tuweze kuliondoa taifa katika ujinga
na kuweza kuinua taifa na familia zetu kutoka
katika hali duni", Willy alieleza.
"Nchi imegeuka, ubinafsi umetawala roho za
viongozi wetu, wanajifikiria wao tu. Si viongozi
wa wananchi tena, ila wanatafuta uongozi kwa
faida yao wenyewe. Hata ukiangalia ni viongozi
wachache sana kwa sasa ambao sio matajiri.
Wanaingia katika uongozi wakiwa hawana kitu,
lakini baada ya muda mfupi unawakuta
wamejilimbikizia mali. Afadhali wangefanya hivyo
halafu wakaendelea kuwasaidia wananchi ili na
wao hali zao ziinuke, la hasha, sera zao ni za
kuwadidimiza wananchi wawe masikini pamoja
na vizazi vyao ili wasiwe na sauti kabisa. Sauti
wanataka ibaki yao na vizazi vyao ili wabaki
madarakani kama vile wafalme.
"Sikilizeni... tunakaribia kutua kwenye uwanja
wa ndege wa Kilimanjaro. Mabibi na mabwana,
inuweni viti vyenu wima, fungeni mikanda yenu
ya viti tayari kwa kutua", sauti ya msichana
ilisema.
"Mzee, basi nitakutafuta ili unielimishe zaidi
kuhusu mambo yalivyo katika nchi yetu hii kwa
sasa, maana kwa muda mfupi huu nimeelimika
kwa kiasi fulani", Willy alimweleza Mzee Magoti
maana ndege ilikuwa inaelekea kutua na hivyo
wasingekuwa na muda wa kuzungumza zaidi.
Mzee Magoti alitoa kadi yake yenye anwani na
simu.
"Basi ukirudi Dar es Salaam, nipigie simu
tuonane".
"Asante Mzee".
Ndege ilipogusa chini wote wakawa kimya
mpaka iliposimama kabisa.
"Haya kwe heri Mzee Magoti", Willy alimpa
mkono. Akachukuwa mkoba wake na akawa wa
kwanza kutoka. Alipoiangalia saa yake ilikuwa
saa sita na nusu mchana .
Willy aliposhuka kutoka ndani ya ndege,
alimkuta Musoke anamsubiri.
"Shikamoo".
"Marahaba, habari za siku nyingi, haujabadirika
bado, ila umetia uzito kidogo", Musoke
alimweleza Willy.
"Asante, unajua nimeoa, sasa mapochopocho
yananimaliza". Wote walicheka na kuelekea
kwenye gari ambalo lilikuwa la kukodi lakini
Mzee Musoke alikuwa analiendesha mwenyewe.
"Nimefurahi sana umekubali wito".
"Unajua tena Chifu, ni vigumu sana kumkatalia
kitu, hasa anachokiamini yeye kuwa ni kitu
muhimu".
"Najua, lakini lazima nikushukuru", Musoke
alijibu huku kiroho kikizidi kumdunda kwa furaha
kwa kuwa na uhakika kuwa Willy yuko naye
tayari kwenda kutekeleza kazi hii nyeti, ambayo
inaweza kuleta ufumbuzi mkubwa kwa mataifa
ya Afrika.


ITAENDELEA
 
ndo umemaliza?
Haijaisha mkuu najitahidi kuiandaa ile niimwage yote. Hata mimi najua kiu yenu,najitahidi kadri niwezavyo niiweke yote. Tuwe wavumilivu tu mambo yatakaa vizuri.
 
nilikuwa nimeleta ya

KAZI IMEANZA

IV

Lakini nimegundua bado iko mbali sana maana inaonesha Willy akiwa Rwanda siku ya kwanza.

kidi kudi unatutesa sana
 
nilikuwa nimeleta ya

KAZI IMEANZA

IV

Lakini nimegundua bado iko mbali sana maana inaonesha Willy akiwa Rwanda siku ya kwanza.

kidi kudi unatutesa sana

Daaah kidi kudi tuwekee bas tuvutie usingizi
 
Last edited by a moderator:
UCHU
TAFUTA UKWELI

Ilikuwa yapata saa saba unusu.
Musoke na Willy walipofika
nyumbani kwa Temu. Walimkuta
Temu akitembeatembea mbele ya
nyumba yake katika bustani huku
ameweka mikono yake nyuma.
Kwa vile nyumba ilikuwa juu
kwenye kilima, na wao
walimwona kabla hajawaona
mpaka walipopiga honi ya gari ili
kufunguliwa lango la mbele.
Alipoona ni gari la kukodi la
Musoke, mara moja alikimbia na
kulifungua lile lango hata askari
wake anayelinda nyumba yake
hakuwahi mbio za mzee huyu. Hii
yote ilionyesha shauku aliyokuwa
nayo Temu juu ya suala hili la
Rwanda.
"Shikamoo", Willy alimshalimia.
"Marahaba, karibu".
Temu alipeana nao mikono na
wote na kuwakaribisha kule uani
kwenye bustani ya nyumba.
"Wengine?", Musoke aliuliza.
"Saa nane watafika".
"Vizuri".
Walipokuwa wameketi kule
uawani kwenye kivuli kizuri cha
miti, Musoke alitumia nafasi hiyo
kuwafahamisha.
"Bwana Temu, huyu ni kijana
wetu, anaitwa Willy Gamba, sasa
hivi anafanyakazi za kujitegemea,
lakini alikuwa kwenye idara ya
upelelezi ya Tanzania kabla
hajaamua kuacha kazi ili
ajitegemee. Yeye ameombwa na
marafiki zetu wengine aje
atusaidie kwenye hili tatizo letu",
Musoke alieleza huku Temu
akionekana kushikwa na butwaa.
"Na bwana Gamba, huyu ni mzee
Temu na ndiye Mkuu wa PAM
upande wa Tanzania.
Willy aliinuka na kumpa Temu
mkono.
"Mimi siamini macho na masikio
yangu", Temu aliendelea
kuonyesha kama mtu
aliyeshituka sana. "Hivi kweli
Willy Gamba yupo! na ni wewe!
Hivi ni kweli baba yangu, ni kweli.
Mimi siku zote husikia habari za
Willy Gamba na huamini kuwa ni
hadithi tu, maana mambo
ambayo ameyafanya wakati wa
ukombozi wa nchi zilizo kusini
mwa Afrika tulifikiri ni
propaganda tu ya kamati ya
ukombozi ya OAU. Kumbe mtu
mwenyewe upo na ni kweli. Eehe,
ama kweli kuishi kwingi kuona
mengi. Basi bwana Musoke, kazi
yetu itafanikiwa", Temu alieleza.
"Huyu kijana wetu Mwenyezi
Mungu amemjaalia uwezo
mkubwa sana katika kazi hii ya
upelelezi. Hakuna mtu
unayeweza kumlinganisha naye
hapa Afrika, sijui huko Ulaya,
lakini hata majasusi wa huko
Ulaya ndiye aliyekuwa
akiyakomesha wakati wote huo.
Kwa kweli hata mimi niliposikia
amekubali na ni yeye anayekuja
basi roho yangu ilitulia, najuwa
tutafanikiwa. Hivi kwanini
wamekukubalia kustaafu
mapema hivi?", Musoke
alimuuliza Willy lakini kabla ya
kujibu, mhudumu wa pale
nyumbani alifika na kutaka
kujuwa watakunywa nini.
"Bwana Gamba unataka kunywa
nini?, kunywa kitu kidogo, maana
huko ndani wanatengeneza
chochote cha mchana, sisi
wachaga ndizi ndicho chakula
chetu, sijui wewe utapendelea?",
Temu aliuliza.
"Kinywaji naomba klabu soda, na
nitafurahia sana macharari", Willy
alijibu huku Temu akicheka na
kufurahi kusikia macharari.
"Kumbe unayajuwa eeh basi baba
yangu tutakula hayo maana
wanaandaa. Na wewe mzee
Musoke?".
"Mimi nitakunywa ki-wiski
kidogo, unajuwa sisi wazee
lazima ushituwe damu kidogo
upate joto".
"Sawa kabisa, nenda kalete
haraka", Temu alimwagiza
mhudumu wake.
"Ehe Willy, kwanini umeruhusiwa
kustaafu mapema hivi?, au kwa
sababu ya Afrika Kusini kupata
uhuru?", Musoke aliuliza tena.
"Hapana, mimi niliomba kustaafu
ili niweze kuoa na kuanza maisha
ya kifamilia maana kazi hii haifai
kama umeoa na una familia. Sasa
hivi nimeoa na mke wangu ni
mjamzito. Na hata kazi hii
nimekubali tu, kwanza kwa
sababu na mimi nimeumwa sana
na hali hii ya mauaji ya Rwanda
na pili kwa sababu Chifu alisema
nisipokwenda mimi atakwenda
yeye. Na unajuwa bwana Musoke,
mimi nisingependa hata kidogo
kuruhusu kitu kama hicho".
"Ni kweli kazi hii inahitaji kuweka
mawazo yako pamoja, usiwe na
fikira zingine, lakini ndivyo hivyo,
taifa bado linakuhitaji mara kwa
mara kama hivi, ingawaje si sana
kama ulivyokuwa jikoni", Musoke
alikubaliana na Willy. Mara
wakaona wenzao wengine
wanaingia na wote wakasimama
kuwasalimia.
Temu alichukuwa nafasi ya
kuwafahamishe wenzake kwa
Willy Gamba. "Hawa ni wana
PAM kutoka sehemu mbalimbali
za Afrika. Na wamekuja kwa ajili
ya kikao hiki cha kutathimini jinsi
mambo yalivyokuwa huko
Rwanda. Huyu ni bwana Kimani
kutoka Kenya, huyo ni Abakusi
toka Nigeria, huyu ni Makwega
toka Zambia na huyu kijana
mwenzio ni Malisa kutoka hapa
hapa Tanzania". Kisha akageuka
na kumgusa Willy. "Na huyu
ndiye mgeni tuliyemtarajia kwa
ajili ya kazi yetu. Bwana Willy
Gamba.
Kimanina Malisa waliwahi
kusikia habari zake nao
walishikwa na mshangao kama
wa Temu. Musoko alitumia nafasi
hiyo kunong'ona na Abakusi na
Makwega kuwaeleza Willy
Gamba hasa alikuwa mtu wa sifa
za namna gani. Bila hata kusema
mengi, alipoeleza kazi zake mbili
alizofanya na kuutingisha
ulimwengu kwa kuwazuia
majasusi wa Afrika Kusini tayari
wote wakamtambua na kupigwa
na butwaa vilevile.
"Wakati mwingine binadamu akili
inashindwa kuamini kitu. Mimi
nilisikia jinsi mpelelezi wa Afrika
alivyoyaangamiza majasusi kule
Kinsasa, Zaire, na nikaamini
kuwa zilikuwa hadithi tu. Sasa
namuona hapa mtu mwenyewe,
akili inashindwa kuamini.
Inashangaza", Abakusi alisema.
"Kama Willy Gamba ndiye huyu
kijana, basi mambo yetu
yameiva", Makwega naye alinena
na kutokwa na wasiwasi
aliokuwa nao usiku.
Bila kupoteza muda mkutano
uliendelea huku wakipata
huduma za vinywaji na chakula.
"Nafikiri wasiwasi wetu wote
sasa umepungua baada ya
kumpata kijana huyu?", Musoke
alisema kama vile akitoa maoni
ya mkutano.
Wote walitingisha vichwa kama
ishara ya kukubali.
Kwa vile kijana huyu yuko hapa,
tumpe maelezo tunataka
atufanyie nini. Nafikiri mimi
niendelee na kama mtu ataona
nimepwelea mahala naomba
asisite kuongezea, sawa".
"Sawa", wote walimjibu mzee
Musoke.
"Bwana Willy, wewe mwenyewe
naami unazo habari nyingi
kuhusu matukio ya Rwanda. Ila
sisi, kama wana PAM tungetaka
tupate undani zaidi wa mambo
yalivyotokea huko Rwanda mpaka
yakafikia yalipofikia na watu zaidi
ya milioni moja katika nchi ya
watu milioni tano kuteketezwa
kwa siku kadhaa tu. Kitu hiki
kinatisha na kama hakiwezi
kuangaliwa kwa undani na
kuthibitiwa inaweza kutokea tena
si Rwanda tu bali hata mahali
pengine Afrika. Sijui
unanielewa?", Musoke alimuuliza
Willy.
"Nakuelewa, ila nataka nijie ni
nini hasa mnataka mimi nifanye
maana kule sasa kuna serikali ya
RPF, kuna mashirika ya kimataifa,
kuna mashirika yanayotetea haki
za binadamu, mnafikiri mimi
nitafanya nini zaidi ya watu hawa
na wenye uwezo na mapesa
mengi nyuma yao, maana na wao
wanachunguza kwa kina maovu
yaliyotendeka Rwanda", Willy
alisema akitaka ufafanuzi zaidi.
"Sawa bwana Gamba, kitu
tunachotaka sisi ni uchunguzi
wetu wenyewe. Hawa watu
wengine wote wanaweza kuwa na
nia zao tofauti. Serikali ya RPF ni
mhusika kwa kiasi fulani.
hatuwezi kupata ukweli asilimia
mia toka kwao. Mashirika ya
kimataifa yenyewe yanaweza
kuwa na ajenda tofauti, tena
wanaweza kutoa ripoti kutokana
na ajenda yao. Wanaotetea haki
za binadamu nao wana mtazamo
wao kwa maana ya kuonyesha
kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa
haki za binadamu Rwanda. Sisi
tunataka uende zaidi ya pale,
ujue kama haki za binadamu
zilikiukwa, na kwa nini zilikiukwa,
lazima kuna sababu.
Mauajiyaliyotokea nini kiini
chake, maana yanaonekana
yalikuwa yamepangwa toka
mapema. Na vilevile kwanini
Afrika na dunia kwa ujumla, ikiwa
kimya pamoja na nchi jirani kama
Uganda, Tanzania, Zaire na
Burundi hazikufanya chochote
kuzuia mauaji haya. Tukishajuwa
chanzo na sababu zilizofanya
mpaka binadamu akafikia kuwa
mbaya kuliko mnyama, nafikiri
tutakuwa tumejifunza; na hili
fundisho litatusaidia kuweka
mkakati wa kuzuia kitu kama
hicho kitakapotokea. Vilevile
tujue namna ya kukidhibiti kabla
hakijaleta maafa makubwa kama
haya", Musoke alijibu.
"Oke, nimeelewa nini mnataka,
nitajitahidi niweze kuchimbua
mambo uliyoyataja hapo ili nipate
vyanzo vyake", Willy alijibu.
"Lakini haitakuwa kazi lahisi,
lazima uwe macho maana ukweli
wa mambo haya unaweza kuwa
na athari nyingi kwa watu
mbalimbali ndani ya Rwanda na
pengineko duniani. Kwa hiyo
ikijulikana kuwa kuna mtu
anatafuta ukweli na ikaonekana
kuwa ataupata, basi ujuwe
masiha yako yanaweza kuwa
hatarini maana mpaka sasa
tunaamini kuna watu wanajaribu
kufukia ukweli usijulikane. Na
hawa watu watakuwa watu
hatari. Tafadhali, hadhari ni
lazima", Abakusi alimwasa Willy.
"Nitalitazama hilo", Willy alijibu
na kuendelea, "Na malipo yangu
yatalipwaje, maana sasa ni
mfanyabiashara na si mfanyakazi
wa serikali tena. Kazi hii
nimeichukua binafsi".
"Malipo utalipwa na PAM. Kwa
ajili ya kazi hii PAM iliwaomba
michango wafanyabiashara wa
kiafrika ambao wanaunga mkono
msimamo wa PAM na wametoa
michango mizuri sana na tukitoka
hapa tutapitia hotelini kwangu
nikupatie malipo yako. Sijui
utahitaji kiasi gani?", Musoke
aliuliza.
"Mimi vilevile, kama nilivyosema,
naunga mkono madhumuni ya
PAM, kwani ni mpaka pale
Mwafrika atakapojitambua kuwa
lazima azungumze na Waafrika
wenzake kupambana na ukoloni
mambo leo ndipo atakapokuwa
amejikomboa kutoka katika
umasikini, ujinga na maradh. Kwa
jinsi hiyo na mimi nikiwa
mshabiki wa PAM nitaomba
nilipwe gharama zangu tu
nitakazotumia, lakini utaalamu
wangu nautoa bure".
Makofi na kupeana mikono ya
shukrani vilisikika.
"Sijui hii kazi unafikiri itachukuwa
muda gani?", Kimani aliuliza.
"Mimi nitawafanyia kazi, nipeni
muda", Willy alijibu.
"Wiki mbili?", Makwega aliuliza
pia.
"Nitajitahidi".
"Basi tuonane hapa baada ya wiki
mbili", Musoke aliagiza.
"Sawa".
"Lakini Willy Gamba atakuwa
anawasiliana na mimi Kampala
kwa kila hatua atakayofikia.
Kama ikionekana kazi inakuwa
bado baada ya hizo wiki mbili,
nitawajulisha", Musoke alieleza.
"Sawa".
"Haya, asanteni sana wazee,
tutaonana Mwenyezi Mungu
akitujaalia baada ya wiki mbili.
Sasa hivi ngoja niende na mzee
Musoke akanikamilishie masuala
ya mapesa", Willy aliaga huku
akiwachekesha.
"Nilitaka kusahau. Tumekupatia
nafasi ya kulala Impala, ukienda
tu pale mapokezi watakupa
funguo, tumelipia kila kitu, kazi
kwako. Sijui kama utahitaji usafiri
kesho kukupeleka uwanja wa
ndege?", Temu alieleza na
kuuliza.
"Hapana, nitajitegemea kwenda
uwanja wa ndege".
Musoke alipoangalia saa ilikuwa
saa kumi na nusu. Willy alipewa
mkono wa heri na wajumbe wa
PAM huku kila mmoja
akimwombea mafanikio na
usalama. Willy aliupokea mkono
huo wa heri huku naye
kimoyomoyo akiomba sala zao
ziwe pamoja naye, kwani hawa
walikuwa watu wenye roho za
ubinadamu, ambao walikuwa
wakitumia muda wao kujaribu
kuwasaidia wengine bila malipo
ya aina yoyote. Kweli Mungu
awabariki.
Musoke na Willy aliondoka,
wakaelekea Maunt Meru.
"Kesho umesema ndege saa
ngapi?", Musoke alimwuliza Willy.
"Saa tatu asubuhi".
"Nije nikupeleke?".
"Hapana, nina marafiki wengi
hapa watanipeleka".
"Na leo jioni tunaweza kula
pamoja?", Musoke alimkaribisha
chakula cha usiku.
"Hapana, nitakwenda kwa dada
yangu jioni, alifiwa na mjukuu
wake na nilikuwa sijapata nafasi
ya kumsalimia na hii ndio nafasi
pekee niliyopata".
"Umeua ndege wawili kwa jiwe
moja".
"Bila shaka", Willy alijibu huku
akijuwa kabisa kuwa angeondoka
jioni ile. Willy kama kawaida
yake, aliendelea kuonyesha kama
angelala Arusha. Hii inaonyesha
jinsi ambavyo Willy hamwamini
mtu yeyote mara akishakuwa
kazini.
"Huwezi kujuwa, kikulacho ki
nguoni mwako, uzoefu wa siku
nyingi umenifundisha", Willy
alijisemea moyoni.
Walipofika Hoteli ya Mount Meru,
walikwenda chumbani kwa
Musoke na kuanza kuelezana
tena. Kwa vile Musoke naye
alikuwa na uzoefu wa siku nyingi
na kazi ya upelelezi alijuwa Willy
angetaka nini.
"Bwana Gamba, unajuwa kazi hii
inaweza ikawa ngumu na ya
hatari kuliko hata jinsi
tunavyotegemea. Hivyo,
jitayarishe kwa yote, nadhani
unanielewa?", Musoke
alimwuliza.
"Nakuelewa sana, kazi hii
naichukulia uzito uleule wa
kawaida, sintaipuuza hata
chembe. Kwa kawaida uzoefu
umenionyesha kuwa kwa
kawaida kazi rahisi ndio hugeuka
kuwa ngumu sana".
"Vizuri, mimi ninao wenyeji kule
Rwanda, ambao nafikiri
wanaweza kukusaidia kupata
fununu za awali", Musoke
alisema na kufungua mkoba wake
na kutoa kitabu chake cha
anuani. "Yuko rafiki yangu
ambaye kwa miaka amekuwa
akiipinga siasa ya chama cha
MRND. Yeye ni mwanajeshi.
Alikuwa kamanda katika jeshi la
kumlinda Rais, lakini kwa vile
hakukubaliana na sera yao,
aliacha na kuanza kwa siri
kueneza habari kwa vyombo
vinavyotetea haki za binadamu
jinsi serikali ya Rwanda
ilivyokuwa inavunja haki za
binadamu nchini humo. Wakati
Rais alipouawa Aprili 6, 1994,
yeye alikuwa Nairobi kuonana na
Katibu wa Chama cha kutetea
Haki za Binadamu ulimwenguni.
Hata hivyo, huku nyuma mke
wake na watoto wake sita na
wapwa wake wawili, wote
waliuawa tarehe 7, Aprili. Hii ina
maana angekuwepo Kigali na yey
vilevile leo angekuwa marehemu.
Anakaa Kimihurura nyumba
namba 168. Simu yake kwa
bahati ni moja ya chache
zinazofanyakazi sasa hivi na ni
namba 50486. Yeye ni Mhutu.
"Umeishazungumza naye?", Willy
aliuliza.
"Nitazubumza naye, tuna
uelewano mzuri, na yeye anajuwa
mengi kwa watu wachache
waliokuwa wanaipinga serikali
waliobaki. Na ujuwe huyu mtu
alikuwa karibu sana na serikali
ya Rwanda, na huenda karibu
sana na Rais mpaka kufikia kuwa
kamanda wa jeshi lake. Hivyo,
anajuwa serikali ilivyoondolewa
madarakani na RPF vizuri sana,
na ndio sababu vilevile kumtafuta
ili kumuua ili kuua ukweli wa
mambo".
"Vizuri, nikifika Rwanda
nitamtafuta kama nitamhitaji".
"Tumekupangia kwenye hoteli
iitwayo Des Mille Collines. Hoteli
hii ni maarufu maana wakati wa
mauaji watu wengi, hasa wa
mataifa ya nje, walijificha hapa
na hivyo hata wanyarwanda
waliokuwa wanatafuta ili kuuawa
kati ya walionusurika ni wale
waliobahatika kufika hoteli hapo.
Hivyo, nayo itakupa fursa nzuri
kupata fununu mbalimbali.
Vilevile ningependa umwone
Padre mmoja ambaye
tunafahamiana na yeye
alinusurika kimiujiza baada ya
mapadri, maburuda , watawa na
watu wote waliokuwa kwenye
kituo hicho cha dini kiitwacho
Centre Christus, kuuawa na
Wahutu wenye siasa kali. Padri
huyu anaitwa Jean Marie
Karangwa. Utapata mengi toka
kwake vilevile".
"Bado yuko kwenye kituo hicho?",
Willy aliuliza.
"Ndio yupo, na anajaribu
kukianzisha upya. Na wa mwisho
ambaye ningependa umwone
ikiwa unahitaji msaada, maana
huwezi kujuwa, unaweza kuwa
kwenye hatari ambayo inahitaji
msaada wa kiserikali, hasa
kijeshi. Huyu ni rafiki yangu
saana, tumekaa naye jirani mjini
Kampala na ni mmoja wa
makamanda wa RPF, mtu
shupavu kama wewe na msomi
kama wewe na kijana wa rika
lako. Naamini mkionana
mtashibana tu. ana roho safi
sana. Anaitwa Col Thomas
Rwivanga, namba yake ya simu
60314".
"Asante, nikihitaji msaada wake
nitamtafuta", Willy alijibu.
"Utaondoka lini na kwa njia
gani?", Musoke aliuliza.
"Mimi kesho kutwa nitakutafuta
Kampala nikiwa Kigali
kukujulisha nimefika".
Musoke hakuuliza zaidi maana
alielewa maana yake. Kisha
akatoa bahasha kubwa iliyokuwa
na pesa za dola za Kimarekani.
Idadi yake haikuzungumzwa,
lakini bila shaka ilikuwa maelfu
ya madola.
Baada ya kumpa mzigo huo
walisimama na kuagana.
"Haya, nakutakia safari njema na
kazi njema. Nakuombea heri",
Musoke alimshika mkono
akionyesha uchungu kidogo.
"Asante sana, tuombe Mungu",
Willy alijibu na kuondoka.
Willy alipoachana na Musoke
alikodi teksi pale nje ya Mount
Meru Hotel na kuelekea Impala.
Alipofika Impala alijitambulisha.
"Naamini nina nafasi ya chumba
hapa, naitwa Willy Gamba.
Msichana wa mapokezi aliangalia
kwenye orodha yake ya majina
kisha akaliona jina la Willy
Gamba.
"Ndio baba, chumba 212", alijibu
huku akitoa funguo na
kumkabidhi.
"Una mizigo?".
"Hapana, huu mkoba wangu una
kila kitu".
"Kila kitu?".
"Kila kitu nakuambia, utashangaa
nikiufungua, mrembo zaidi yako
atatokea".
Yule msichana akacheka na Willy
akapandisha ngazi. Alikifungua
chumba na kukuta kidogo lakini
kizuri sana. Aliangalia saa yake
akaona ilikuwa saa kumi na mbili
kasoro robo.
Alikwenda kitandani akatoa
blanketi, akaliweka pembeni na
kufunua shuka na kutengeneza
kama kwamba kulikuwa na mtu
aliyelala pale. Kisha, akauweka
ufunguo kwenye kufuli la mlango
kwa ndani, akachukua mkoba
wake. Akafungua mlango na
kuurudisha bila kuufunga na
funguo kwa vile aliziacha ndani
makusudi na kutelemka chini.
Alipoangalia pale mapokezi na
kuona wapokeaji wapo
shughulini, alichepuka na kutoka
nje. Akelekea kwenye maegesho
ya teksi na kukodi teksi kuelekea
uwanja wa ndege wa Arusha.
Ilikuwa yapata saa kumi na mbili
na robo alipofika uwanja wa
ndege na kukuta ndege imeshatua
tayari. Rubani wa ndege
alimfuata na kumpokea mkoba
wake.
"Habari za jioni?", Rubani
alimshalimia.
"Za jioni nzuri asante".
"Huna mzigo zaidi?".
Sina, ni huo huo".
Rubani aliufungua mlango wa
ndege hii ya Tanzanair, aina ya
Cessina Mark 4, na kumkaribisha
abiria wake huyu mmoja, ambaye
walikaa pamoja kwenye viti vya
mbele, na kisha akawasha injini
za ndege, na kuruka.


ITAENDEA
 
kiporo kama cha J.K kwa mhongo!!! kitachacha kidi kudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…