Riwaya: UCHU


Scofield soma kasheshe xiv
 
SURA YA KUMI NA MOJA
KAMPALA

JKS aliamka mapema asubuhi huku roho
yake ikiwa na furaha nyingi sana. Sasa
hivi alikuwa akielekea benki kwa ajili ya
kuchukua pesa zake. Hisia za urais wa
Tanzania zilimjia katika mawazo yake,
akatamani kuwa kiongozi wa Tanzania ili
atimize ndoto yake ya kuwa mheshimiwa
rais wa Tanzania.
Baada ya kustafutahi kwa chai nzito,
alipiga simu kwenye benki yake hapo
Geneva na kuuliza mahali ilipo. Baada ya
kupata maelekezo sehemu na mtaa
ambao benki ipo, alipiga simu mapokezi
na kumuomba mhudumu amletee teksi
saa tatu kamili ili impeleke benki.
Baada ya kujiweka sawa, alitelemka chini
taratibu ilikuwa majira ya saa tatu kamili,
akiwa amebeba mkoba wake wa ngozi ya
mamba mkononi aliokuwa amepewa
kama zawadi na rafiki yake Jean.
Alipofika chini alikuta teksi inamsubiri
mbele ya hoteli. Alifungua mlango wa
nyuma kama VIP akaingia, akampa
dereva anuani ya benki, baada ya
kuthibitisha ni eneo gari dereva aliondoa
gari huku mawazo ya JKS yakiwa juu ya
baraza lake la mawaziri baada ya
kuukwaa urais.
Jean alikuwa amempa jina la meneja wa
benki na kumweleza kuwa akifika benki
amwone meneja huyo. Alipofika benki
alitelemka na kumwambia mwenye teksi
amsubiri akaingia ndani ya benki na
kuelekea mapokezi. alimwonyesha yule
msichana wa mapokezi jina la meneja.
Asubuhi ile meneja alikuwa bado hana
watu wengi, hivyo akamkaribisha vizuri
sana.
"Karibu Mheshimiwa, nikusaidie nini?",
meneja wa benki aliuliza JKS baada ya
kuingia ofisini kwake.
"Asante", JKS alijibu na kutoa bahasha
yenye maelezo yake yote. Meneja
aliipokea kwa tabasmu na kuifungua
bahasha na kuanza kusoma. Alivuta
Kompyuta yake na kuanza kushughulika.
Meneja, akiwa anatabasamu tena
alimgeukia JKS na kumweleza,
"Samahani, hii akaunti imefungwa jana na
aliyeifunga ametoa pesa zote na kusema
mtu yeyote akifika hapa kuuliza juu ya
akaunti mwenye kitambulisho namba hii,
aelezwe kuwa akaunti hiyo imefungwa
maana mkataba umeisha. Samahani sana
mheshimiwa, nina wateja wengine
wananisubiri".
JKS alichanganyikiwa. Aliinuka, mara
akamuona yule meneja wa benki anakuwa
mkubwa zaidi na yeye JKS anakuwa
mdogo na chumba kinazidi kuwa kidogo,
akasikia anakosa pumzi halafu giza nene
likamuingia mara akaanguka chini na
kupoteza fahamu.
ITAENDELEA
 
Yaaaap,kidikudi njoo tens haraka,jks kauza madini feki kapewa hela feki patamu hapo!!!
 
Kidi kudi ua yote mzee, dah halafu tusha msahau jks
 
kidi kudi huyooo! asante sana and then ona uwezekano wa kurusha kingine.
safi sana! hii ndiyo dawa murua kwa walioficha fedha uswisi.
 
Jamani nikumbusheni JKS ni nani tena nlishasahau
 
dereva aliondoa

gari huku mawazo ya JKS yakiwa juu ya

baraza lake la mawaziri baada ya

kuukwaa urais."



Nimecheka sana. Lol!😂
 
Jamani nikumbusheni KBS ni nani tena nlishasahau

JKS ni mtanzania na ni waziri. alikuwa anawarubuni kambi ya wapigania uhuru akidai serikali inataka kufaham nn kinaendelea kumbe akipata taarifa anawajulisha akazu.

ni huyu JKS alipanga njama za kumwangamiza Willy akiamini kifo cha will kitasaidia yeye kuwa rais wa Tanzania.

alikuwa analipwa hela nyingi na Jean akiamini ndo atafanyia kampeni. sasa kaenda kuchungulia salio kakuta jean kakausha kila kitu ndo huyo kazimia
 

Asante kwa kunikumbusha
 
SURA YA KUMI NA MOJA

KAMPALA
-
II

Ilikuwa yapata saa moja asubuhi Willy
aliposhituka kutoka usingizini baada ya
kuota ndoto mbaya ya vita ambayo aliota
Bibiane akipigwa risasi sita kifuani na
kupoteza maisha, alipotaka kupiga kelele
alishituka kutoka usingizini, akamwona
Bibiane amemlalia kifuani wakiwa
kitandani akakumbuka kuwa kumbe
walikuwa Hoteli ya Sheraton, iliyoko mjini
Kampala, baada ya kuletwa hapa jana
jioni kwa ndege ya serikali ya Rwanda
baada ya kuchukuliwa na helikopita ya
jeshi ya akina Col. Rwivanga kutoka kule
porini Kibumba walikolala baada ya usiku
wa kasheshe walipofanikiwa kuiteketeza
ngome ya Akazu. Taratibu Willy
alimwondoa Bibiane kwenye kifua chake
na kumlaza kwenye mto. Alichukua
chombo cha kuwashia televisheni ili
kusikia taarifa ya habari ya saa moja.
Baada ya kuwasha televisheni mtangazaji
alisoma taarifa ifuatayo.
"Zaire. Vikosi vya wapinzani wa serikali
ya Zaire, vikiongozwa na mpinzani mkuu
Bwana Mpinda vimeanzisha mapigano
makali dhidi ya serikali hiyo vikisaidiwa
na vikosi vya waasi wa kabila la
Banyamulenge vikiongozwa na Meja Tom
Kabalisa Mubanyamulenge, aliyeasi
kutoka jeshi la Zaire. Bwana Mpinda
amekaririwa na vyombo vya habari kuwa
nia yao ni kuuondoa utawala wa kidikteta
wa serikali iliyoko madarakani Kinshansa.
Wamejigamba wakisema usiku wa
kuamkia jana walishambulia kambi
kubwa ya kivita iliyoko Kibumba, karibu
na Goma na kuteketeza silaha nyingi,
vikiwemo vifaru, ndege za kivita, mizinga
mkibwa na midogo na kuua askari
wapatao elfu kumi".
"Pamoja na kwamba habari hizi
hazijathibitishwa na vyombo vingine vya
habari vya ndani na nje, raia wa sehemu
hiyo wamethibitisha kutokea kwa milipuko
mkubwa ya ajabu ambayo hawajawahi
kuisikia katika kambi hiyo. Na wanasema
wanajeshi karibu wote na silaha
zilizokuwa kwenye kambi hiyo
zimeteketezwa kwa milipuko hiyo
iliyosikika mpaka Gisenyi na Goma".
"Habari zilizotufikia hivi punde katika
chumba chetu cha habari zinasema waasi
tayari wamekamata miji wa Goma na
Bukavu na bado wanasonga mbele
kuchukua maeneo mengine. Vilevile, kuna
habari ambazo hazijathibitishwa kuwa
vikosi hivyo vya wapinzani vinasaidiwa
na vikosi vya jeshi la RPF la Rwanda".
"Hii ina maana kuwa wapinzani
wamekusudia kuung'oa utawala wa sasa
ambao umedumu madarakani kwa zaidi
ya miaka thelethini sasa ambao
wameupachika jina kuwa utawala wa
mabavu, unyanyasaji uliojaa rushwa na
udikteta. Bado hakuna taarifa yoyote ya
kukanusha habari hizo kutoka kwa
serikali ya Zaire, mji Kinshansa".
"Na huko Jijini Dar es Salaam, Tanzania
kuna habari kuwa waziri wa ngazi ya juu
nchini humo kwa jina maarufu la JKS
amefariki dunia akiwa katika benki moja
huko Geneva, Uswisi baada ya kupatwa
na shinikizo la damu. Kiongozi huyo
aliondoka nchini Tanzania siku mbili
zilizopita na kuelekea London kwa ajili ya
matibabu ya moyo, bado haijabainika
kwa nini alikwenda Geneva, na alifuata
nini kwenye benki hiyo. Waziri huyo ndiye
aliyekuwa akitegemewa kuwania urais wa
Tanzania baada ya rais wa sasa kumaliza
muda wake".
Willy alitabasamu baada ya taarifa hii
iliyonoga. Kisha, akachukua simu na
kumpigia Mzee Musoke na kumwomba
waonane mchana kama walivyokuwa
wamepanga wakati akiwa mjini Kigali ili
ampatie ripoti ya kazi yake aliyoifanya
kwa mafanikio.
"Nimefarijika kusikia kazi yako kwenye
taarifa ya habari ya asubuhi hii, wewe ni
mwanaume wa shoka", Musoke alimsifu
Willy.
"Asante mzee, tutaonana hiyo saa nane",
Willy alimjibu Musoke na kukata simu.
Kisha akapiga simu nyingine.
"Pepe mpenzi".
"Uko wapi", Pepe aliuliza.
""Niko Kampala narudi kesho".
"Ooh Mungu wangu, toka umeondoka
sijapata usingizi. Njoo mume wangu nina
hamu sana na wewe, nakupenda sana".
"Na mimi zaidi, kesho mama, kwaheri",
Willy akakata simu.
Bibiane alikuwa akisikia lakini alijifanya
kama hamsikii alimgeukia Willy na
kusema. "Uko wapi Willy?, njoo ulale,
najua siku yangu ni leo tu, hivyo lazima
niitumie siku hii kikamilifu".
"Katika nafsi yangu hupenda mtu
anayeelewa mambo kama wewe", Willy
alijibu huku akirudi ndani ya shuka na
kumkumbatia Bibiane.

MWISHO
 
hope uchu umewaisha sasa. nawashukuru kwa uvumilivu wenu tangu mwanzo mpaka hapa tulipofikia. waliokwazika poleni sana tusameheane tusonge mbele naimani mambo mazuri mengi yanakuja.
 
asante kidi kudi, shukrani sana pia wote waliodhirikiana na wewe hakika imekuwa burudani sana. Kwa niaba ya wengine wote nakuomba sana uanze uzi mwingine wa riwaya nyigine ya Msiba au Joramu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…