Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

kidi kudi

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,528
Reaction score
2,188
Nchi zilizo msitari wa mbele katika Ukombozi Kusini mwa Afrika zimetendewa mambo mengi maovu na Utawala dhalimu wa Makaburu... Hata hivyo halikupata kutokea tishio zito la kutisha kama hili, ambalo linakaribia kutokea.

Tukio la kutatanisha ambalo linawatoa machozi wananchi wa nchi mbalimbali za kiafrika. Wanajitokeza mashujaa na kwenda Afrika Kusini, ili kulikabiri tishio hilo lakini kila aendaye huko harudi na roho yake. Inspekta Kombora nchini Tanzania jasho linamtoka.

Anawatambua na kuwakumbuka mashujaa wengi lakini anamtambua shujaa mmoja. Joram Kiango. Jambo la kusikitisha ni kwamba sasa hivi Joram Kiango ni mtumiaji mzuri ambaye sasa anatembea kutoka jiji moja hadi lingine akiwa na yule msichana wake mzuri Nuru kwa ajili ya kustarehe.

Juhudi za Kombora kumsihi Joram arejee kazini hazifui dafu. Badala yake Joram anafanya maajabu mengine ambayo yanalichafua jina lake hapa nchini Tanzania na kote duniani. Wakati huo siku ambayo utawala wa makaburu umeweka ili kuachia pigo lao la mwisho inazidi kukaribia. Sasa yamebaki masaa...


**************** ************** BEN R. MTOBWA. ************** ************* *************

SURA YA KWANZA

Kama maji ya Bahari ya Hindi yangekuwa na hisia, basi yangejisikia fahari sana kupata fursa nyingine ya kuburudisha miili ya viumbe hawa wawili ambao walikuwa wakiogelea kando ya ufuko huu wakicheza na kucheka. Walifanya picha ya kuvutia sana hususan sura zao zuri zilipoibuka kutoka majini na kumezwa na tabasamu ambalo lilisababishwa na mizaha waliyokuwa wakifanyiana chini ya maji.

Baada ya kuogelea kwa muda mrefu walirejea nchi kavu ambako walijitosa juu ya mchanga na kuruhusu joto likaushe maji miili yao. Ufuko pia ungekuwa na kila sababu ya kusherehekea fahari ya kulaliwa na viumbe kama hawa. Kwani walioana kimaumbile kama pacha, ilihali hawakuwa mtu na dada yake. Walikuwa kama pea ya kiatu cha kiume kwa cha kike.

Mwanamume hakuwa mwingine zaidi ya yule kijana mwenye umbo refu, mkakamavu, aliyekaa kiriadhariadha na sura nzuri, yenye dalili zote za hekima, ushujaa na ucheshi. Kwa jina anaitwa Joram Kiango. Naye msichana alibahatika kupewa umbo lenye kila kitu ambacho msichana anahitajika kuwa nacho, wakati huohuo akiwa na kila ambacho mvulana legelege asingekuwa nacho, ni yule ambaye akutazamapo ungependa aendelee kukutazama, achekapo utafarijika, atembeapo unaburudika.

Yule ambaye kuna madai kwamba alikuja duniani kwa makosa baada ya kuumbwa ili awe Malaika. Madai ambayo kama si ya kweli basi yako mbali sana na uongo. Hata jina lake halikutofautiana sana na sura yake. Wanamwita Nuru. Baada ya kuhakikisha kuwa miili yao ilikuwa imekauka, walijifuta vizuri kisha wakazichukua taulo zao na kuondoka wakaifuata gari yao.

Macho ya watu wengi, waswahili kwa watalii ambao walikuwa katika ufuko huo, hayakukoma kuwafuata. Kutazamwatazamwa, hasa wanapokuwa pamoja halikuwa jambo geni tena kwao. Mara kwa mara macho ya kiume yalikuwa ya yakimwandama Nuru huku macho ya kike yakimfuata Joram kila mahali walipopita.

Walijifunza kuzoea hata wakaanza kusahau kuwa wanatazamwa. Hivyo, walipolifikia gari lao waliingia, Joram akalitia moto wakaondoka kwa mwendo usio wa haraka. Hawakuwa na sababu yoyote ya kufanya haraka. Ratiba yao ya starehe ilikuwa ikielekea kwisha mapema zaidi ya walivyokusudia.

Walikuwa wamekubaliana wakae katika miji yote mashuhuri hapa nchini kwa muda wa wiki nzima kwa kila mji. Lakini hii ilikuwa wiki ya pili tu na tayari walikuwa wameishi Zanzibar, Moshi, Arusha, Dodoma, Mwanza na kujikuta wamerejea Dar es Salaam. Kila mji waliuona unakinaisha baada ya siku mbili tu.

Maisha ya mahotelini waliona yanawafaa watu wavivu, nazo mbuga za wanyama ziliwasisimua watalii, ilihali miji iliwaridhisha wenyeji, na safari za hapa na pale zilikinaisha. Hivyo ingawa walirejea Dar es Salaam na kuendelea na starehe zao wakiishi katika hoteli ya Kilimanjaro, ingawa waliendelea kucheza na kucheka, ingawa hakuna aliyetamka neno lakini bado haikuwa siri tena kuwa maisha ya Kula, kulala...kula, tena, kulala tena", yalikuwa yameanza kuwachosha.

Maisha hayo yalikuwa yameanza usiku ule ambao Joram Kiango asingeweza kusahau. Usiku hadi leo bado unamtia maumivu moyoni, kila anapokumbuka alivyozulumiwa haki na wajibu wake wa kuitia risasi katika kichwa cha Proper, yule katili ambaye pamoja na kuwaangamiza watu wengi ambao hawakuwa na hatia, alikuwa amemuua Neema Iddi kinyama. Ni siku hiyo ambayo Joram alitupa bastola yake na kuamua kuishi kivivu kama wanavyoishi watu wengine.

Msichana huyu Nuru alikuwa amehusika sana katika mkasa huo ambao tayari mtu alikuwa ameuandikia kitabu na kukiita Salamu Toka Kuzimu. Kamwe Nuru alishindwa kuachana na Joram na asingeweza kusitahimili kumwona Joram akiteseka na msiba huo peke yake. Alimfuata na kumsihi hata kulipopambazuka wakajikuta wako pamoja juu ya kitanda kimoja. Tangu hapo hawakuachana, Joram hakuwa mtu aliyeweza kuachwa kirahisi.

Naye Nuru kadhalika alitofautiana sana na wale wanawake wazuri ambazo uzuri wao ni pindi wanapokuwa wamevaa nguo tu. Alikuwa na mengi ambayo alikuwa ameyatenda kwa nia moja tu - ya kumfariji Joram, naye Joram alijikuta akianza kujisamehe. Lakini asingeweza kusahau.....

****************************** ************** **************

Walipowasili chumbani katika hoteli ya Kilimanjaro, walijipumzisha vitandani mwao kwa muda huku wakilainisha koo zao kwa viwanyaji vitamu. Kisha walifuatana bafuni na kuyaondoa maji ya chumvi miilini mwao kwa kuoga vizuri kwa sabuni.

Baada ya hapo waliekea kwenye chumba cha maakuli ambapo walikula na kujiburudisha kwa vinywaji vikali na maongezi laini. Joram akiwa katika vazi lililomkaa vema, suti ya kijivu iliyooana na viatu vyeusi kama kawaida, alikuwa tishio kubwa kwa wanaume waliokuja na wasichana wao. Hata hivyo, walijifariji kwa kujua kuwa asingekuwa mwendawazimu wa kuvutwa na yeyote kwani aliyeketi nae hakuwa msichana wa kawaida.

"Kwanini wanaishi hapa bongo watu kama wale", mtu mmoja alimunong'oneza jirani yake. "Tazama wanavyopendeza, wangeweza kwenda zao nje na kutajirika sana endapo wangecheza mchezo mmoja tu wa sinema", alidakia mwingine. "Kweli kabisa", aliungwa mkono. "Hata maumbile yao yanafikiana.

Yule dada anatosha kabisa kumtia mwanaume yeyote wazimu kiasi cha kumfanya auze hata nyumba yake. Maongezi hayo hayakumfikia Joram wala Nuru. Lakini alikwisha zoea kuyasoma katika macho ya watazamaji wao. Hivyo, alitabasamu kidogo na kuagiza kinywaji kingine.

Nuru alikuwa akiongea neno. Joram aliitika bila kumsikia. Waliendelea kunywa kwa muda hadi walipoamua kuwa wametosha ndipo walipofuatana katika ukumbi wa muziki ambapo walisikiliza muziki na kucheza kwa masaa kadhaa. Walipokinai walikiendea chumba chao ambacho kiliwalaki na kuwapa usiri. Katika usiri huo, kwa mara nyingine miili yao iliburudika na kusherehekea afya zao. Kesho yake baada ya kufungua kinywa walitazamana katika hali ya kuulizana waitumie vipi siku hiyo.

Nuru aliweza kuzisoma dalili za kuzikinai ratiba zao ambazo zilikuwemo katika macho ya Joram. Ingawa walikuwa wakistarehe na kujiburudisha furaha ilikuwa dhahiri kuwa burudani hizo zilikuwa zikiuburudisha mwili wa Joram kamwe hazikuwa zikiburudisha akili yake. Ingawa uso wake ulikuwa ukitabasamu mara kwa mara, roho yake ilikuwa ikiwaka kwa hasira kali dhidi ya adui zake. adui wa taifa na maendeleo ya jamii.

Adui ambao walikuwa wamefanya maovu mengi yasiyokadilika na kumtia lile donda la rohoni kwa kumuua kikatili msiri wake mkuu Neema. Nuru kwa dhamila ya kumsahaurisha Joram na uchungu huo ndipo akajitoa kwake mwili na roho. Lakini ilikuwa dhahili kuwa jeraha hilo lilikuwa bichi katika roho ya Joram, na lisingepona kabisa isipokuwa kwa dawa moja tu kulipiza kisasi.

Hayo alikuwa akiyaona wazi katika macho ya Joram ingawa alijisingizia kufurahia starehe zao. Iko siku Nuru aliwahi kumwambia. "Sikia Joram. Huonekani kufurahia lolote tunalofanya. Kwani usirudie ofisi yako na kuendeleza harakati zako, nitakuwa kama alivyokuwa Neema. Nitakusaidia kwa hali na mali. Joram alicheka na kumjibu Nuru. "Mara ngapi nikwambie kuwa nimeacha shughuli hizo. Nitaendelea kustarehe hadi nitakapoishiwa senti yangu ya mwisho.

Ndipo nitakapotafuta kazi na kuifanya kwa utulivu kama vijana wenzangu". "Kwanini lakini, kifo cha msichana mmoja tu kinakufanya usahau wajibu wako". "Sivyo Nuru. Isieleweke kuwa nimechukia kwa kufiwa na Neema. Yeye ni mmoja tu kati ya wasichana wanaouawa kwa dhuluma na ukatili aina kwa aina ulioko duniani.

Ni mmoja tu kati ya maelfu ya vijana wanaoteseka kwa shida ambazo wanazipata kwa makosa ya watu wengine. Ni mmoja tu kati ya mamilioni ya binadamu wanaoumia kwa umasikini ambao hawakuomba na dhiki ambazo hazina umuhimu wowote". "Sidhani kama nimekuelewa Joram, unazungumza kama mshairi". "Labda.

Ninachotaka kusema ni kwamba bastola yangu haitoshi kukomesha maovu yote yanayotendeka hapa duniani. Kote Afrika na duniani binadamu hawako sawa kiuchumi. Wako wanaoshinda njaa na kuna wanaomwaga chakula. Kama kweli nakusudia kuondoa dhuluma na ukatili kwa nchi dhidi ya nchi nyingine, basi sina budi kuukomesha pia ukatili dhidi ya mwingine.

Maadamu hayo yako nje ya uwezo wangu naona sina budi kusahau yaliyopita na kuanza kula na kunywa kama vijana wenzangu". "Hasira hizo Joram. Upende usipende ukweli ni huo huo. bastola yako haiwezi kuwaelekea viongizi wazembe na wenye choyo ambao wanasababisha hali ngumu kwa wananchi.

Lakini inawajibika kuwakomoa maadui ambao dhamila yao ni kuhakikisha hatulifikii lengo letu la kujenga taifa ambalo rais wake wanafaidi matunda ya uhuru wao. Unafahamu fika kuwa wanatunyima nafasi ya kufanya hayo"... Maongezi hayo yalikuwa yamefanyika siku chache zilizopita.

Nuru alikuwa ameyakumbuka tena leo baada ya kuziona dalili za kukinai katika macho ya Joram. Alijua na kuamini kama wanavyoamini watu wote wanaomfahamu Joram kuwa starehe yake kuu ni pindi anapopambana na adui na burudani yake ni hapo anapowashinda.

Vinginevyo Joram alikuwa akijisingizia starehe. "Leo wapi mpenzi", Nuru aliona amchokoze Joram. "Leo najisikia kulala tu". "Kulala mchana, tangu lini umeanza tabia hiyo ya kulala mchana". "Tangu nilipoacha kuwa Joram Kiango na kuwa kijana mtumiaji anaitwa Joram Kiango". "Nilijuwa utachoka Joram. Kwanini usirudi ofisini na kuanzia leo?". "Sikia Nuru. Usianzishe tena ubishi ambao siupendi. Kweli nitakuwa hapa nikiendelea kutumia tu na si vinginevyo". "Sidhani kama unasema ukweli. Huonekani mtu wa kustarehe maishani". Joram hakumjibu.

Alijilaza kitandani na kujisomea gazeti. kisha jirani yao chumba cha pili aliingia akiwa katokwa na macho. Hakujali kupiga hodi. Wala macho yake hayakuvutwa kuhusudu uzuri wa Nuru kama ilivyokuwa kawaida yake. badala yake alimwendea Joram kitandani akasema, "Hujasikia, Samora Machel amefariki, ndege yake imeanguka huko Afrika Kusini". "Amekufa", Nuru alidakia na kuuliza kwa mshangao.

"Amekufa, na hii siyo bure. Iko namna haiwezi kuwa ajali ya kawaida". "Afrika Kusini, alienda kufanya nini huko", Joram aliuliza kwa utulivu. Hata hivyo macho yake yalikuwa yakiwaka kwa hasira, ingawa hakupenda kujidhihilisha wazi kwa Nuru.

"Siku hizi hata taaifa za habari husikilizi Joram?", Nuru alimuuliza. "Samora hakwenda Afrika Kusini. Alikuwa akitokea nchini Zambia ambako alikutana na rais Mobutu Seseseko wa Zaire na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Robert Mugabe kutafuta suruhisho na mbinu za kuiwekea Afrika Kusini vikwazo zaidi vya uchumi".

"Wanasema chanzo cha ajali hakijapatikana. Bila shaka watakuwa waliosababisha ajali hiyo kwa njia moja ama nyingie", alisema kwa masikitiko. "Nadhani wamezoea kutuangamiza wapendavyo. Kwao sisi ni sawa na vifaranga wanaofugwa. Yeyote ambaye hawampendi wanamponda kwa urahisi. Jambo la kusikitisha ni kwamba sisi hatuwezi kufanya lolote baya dhahiri ni kwamba tutaendelea kuuawa mpaka lini.

Kwanza walimuua Mondalane. Sasa wamemuua mrithi wake Samora na siyo hao tu. Viongozi wengi wa Afrika wamekuwa kama mifugo yao. Tunaorodha ndefu ya viongozi wetu wanaouawa ama kupinduliwa kwa matakwa yao. Tutaendelea kuvumilia mpaka lini", Nuru alikuwa akizungumza kama peke yake.

Lakini macho yake yalikuwa yakimtazama Joram. Alitamani aone kitu katika macho yake. Hakukiona. Jambo ambalo lilimfanya ainame chini na kuruhusu matone kadhaa ya machozi yamdondoke. Yalikuwa machozi ya hasira zaidi ya hudhuni.

****************************** ************** ***************

Kifo hiki cha kijana shujaa aliyeheshimiwa kote dunia, aliyependwa na wapenzi wake na kuogopwa na adui zake, kilifuatiwa na minong'ono mingi kote dunia.

Watu walisema hili na lile, wakipingana na kuafikiana. "Walimuua au...". "Bila shaka". ..."Njama za Afrika Kusini". "Na vibaraka vyao". Siku chache baadae maongezi yalibadilika. "Umesikia Makaburu wanadai kuwa wataendelea kuwaadhibu viongozi na wananchi wa nchi zote za mstari wa mbele ambao wanajifanya vichwa ngumu?". "kweli?, washenzi sana wale. Wanaweza kufanya lolote".

Na baada ya siku chache mambo yakaanza kutokea. Magazeti na vyombo mbalimbali vya habari duniani viliandika habari za kusikitisha. Watu mia nne wamefariki dunia, mia tisa kujeruhiwa vibaya na wengine maelfu kuponea chupuchupu kufuatia ajali isiyokuwa ya kawaida iliyotokea katika jiji la Lagos Nigeria. Watu hao walikuwa katika uwanja wa mpira wakati wa mchezo kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Zaire.

Dakika chache kabla ya mchezo huo kwisha, moto mkali umelipuka na kubomoa uwanja na kusababisha maafa hayo. Wachunguzi wa mambo wanahisi kuwa huenda utawala wa Afrika Kusini unahusika. Kabla watu hawajasahau habari hiyo, ilifuatia taarifa nyingine ya kutisha vilevile. Harare, Zimbabwe Maghala manane ya serikali yaliyokuwa yakihifadhi chakula yameungua moto kwa pamoja. Chanzo cha moto huo hakijajulikana. Jambo la kushangaza ni jinsi maghala hayo yalivyoungua kwa pamoja wakati yako katika wilaya mbalimbali za nchi hiyo. Kuna mashaka kuwa tukio hili kwa njia moja ama nyingine linahusiana na maafa ya Nigeria.

Na baada ya siku chache Dar es Salaam, Tanzania Katika matukio ya kutisha na kushangaza yanayoendelea kutokea katika nchi zenye msimamo wa kimapinduzi za Afrika leo asubuhi, Tanzania imepata pigo kubwa la kusikitisha. Jengo la Benki kuu ambalo lilikuwa likikamilisha marekebisho baada ya ule moto wa awali limeungua tena. Safari hii haielekei kuwa kutakuwa na matengenezo yoyote yanayoweza kulilekebisha zaidi ya kujengwa upya. Chanzo cha mto huo hakijafahamika.

Habari hizi zilitisha Afrika na kuishangaza dunia. Kila mtu aliyezisikia radioni na kuzisoma magazetini alishangazwa na matukio haya ambayo mfano wake haukupata kutokea katika historia ya Afrika na dunia. Ajali ni jambo la kawaida. Kadhalika kuna watu wanaoamini kuwa kuna kitu kinachoitwa mkosi, na bahati mbaya, lakini mikosi mingi kiasi hiki na bahati mbaya kuziandama nchi chache za Afrika zenye msimamo mmoja katika suala la ukombozi ni jambo ambalo lilisababisha nyongeza katika fikra za wasomaji na wasikilizaji wa vyombo vya habari.

Kitu kinachoitwa roho mbaya, kilipenya katika fikra hizo, ingawa hakukuwa na hakika katika mawazo hayo. Baadhi hata waliwahi kutamka hadharani kuwa kuna mkono wa mtu katika matukio hayo. Mawazo hayo yalifuatiwa na hofu katika mioyo ya wananchi na serikali zao walipojiuliza.

Kipi kingefuata, "Joram, tutakaa kimya kusubiri maafa zaidi", Nuru alikuwa akimuuliza Joram baada ya kusoma habari za tukio la benki kuu katika gazeti. Alikuwa amejitahidi kustahamili kutosema lolote aliposoma matukio ya Lagos na Harare. Lakini hili la nyumbani lilimgusa zaidi Nuru. "Aibu iliyoje", aliendelea Nuru. Tuendelee kustarehe kwa vinywaji na muziki huku tukisubiri maafa mengine yatatokea, haiwezekani Joram. Lazima tufanye jambo".

Ndio habari hizo hazikuwa zimempendeza Joram. Hata hivyo alikuwa amezisoma kama raia wengine bila kudhihilisha dalili yoyote ya nia ya kufanya lolote kama alivyokuwa awali. Jambo ambalo lilimfanya Nuru atokwe na machozi. "Serikali inao polisi na wapelelezi wake, ambao inawalipa pesa nyingi", Joram alisema. "Mimi ambae nimeacha shughuli hizo nitasaidia nini?". "Huwezi kusema hivyo Joram. Siamini kama moyo wako wa uzalendo umedidimia kiasi hicho". "Haujadidimia, uko palepale kama ilivyo mioyo ya wazalendo wengine". "Lakini wewe si mzalendo wa kawaida Joram.

Taifa linakuthamini na kukutegemea. Huwezi kulisalti kiasi hicho bila sababu ya kuridhisha. Lazima ufanye jambo. "Ndio. Nitafanya jambo. Nitastarehe na kuendelea kustarehe kama wanavyofanya vijana wenzangu. "Njoo kitandani Nuru. Tafadhali. Njoo tustarehe acha wenye shibe waendelee kulinda shibe yao. Wewe na mimi tuna nini katika nchi hii". "Joram...". "Nuru njoo tafadhali.

Na kama umenichoka sema nimtafute Nuru mwingine ambaye hachoshwi na starehe. Nuru angependa kukataa. Lakini asingeweza. Akamfuata Joram kitandani na akajilaza kando yake kitandani huku machozi yakimtoka kama kondoo anayesubiri kuchunwa.

****************************** ************** ************** ITAENDELEA *
 
SURA YA PILI
Kati ya watu ambao wameisumbukia sana
nchi hii, wakiziweka roho zao katika
minada ya maafa na kwato za mauti
wakiilinda nchi isimezwe na jangwa la
misukosuko inayosababishwa na
majasusi hatari wa Afrika, ni Mzee huyu
Mkwaju Kombora.
Tangu utoto wake baada ya kumaliza
kidato cha sita, alijikuta akitoka chuo hadi
chuo, huku akifundishwa mbinu
mbalimbali za kupambana na adui. Baada
ya kuhitimu vizuri alijikuta akivaa
magwanda ambayo mabega yake
hayakukoma kubadilikabadilika hadi
alipojikuta Inspekta wa kikosi hiki
maalumu. Kupanda kwake ngazi mara
kwa mara kulitokana na moyo wake wa
kishujaa na juhudi zisizo kifani katika
kuwakabili adui wa nchi. Mara kwa mara
alikuwa akiwashinda adui zake isipokuwa
safari chache ambazo alielekea kukata
tamaa. Hata hivyo asingekosa
kumshukuru Mungu kwani nyakati hizo
alitokea kijana yule ambaye alisaidia
kuwanasa adui kwa hila zake za
kutatanisha. Kijana ambae jina lake
lisingeweza kumtoka akilini, huyo ni
Joram Kiango.
Kombora asingesahau mchango wa
kijana huyu katika mikasa ile ambayo
Mswahili mmoja ameamua kuandika
vitabu ili apate chochote kile na kuviita
Dimbwi la Damu, Mikononi mwa Nunda,
Nasikia kuua tena na Salamu kutoka
Kuzimu. Hata hivyo, kama polisi wengine,
Kombora asingeweza kutamka hadharani
kuwa Joram alifanya lolote la haja
isipokuwa alibahatisha na kuhatarisha
maisha yake. Lakini leo Kombora
alitamani kumbembeleza Joram, hata kwa
kumuangukia miguuni, endapo ingebidi,
amsaidie katika kuutatua mkasa huu
ambao ulikuwa ukimtoa jasho yeye na
polisi wenzake wote wa nchi zilizo mstari
wa mbele kwenye ukombozi Kusini mwa
Afrika.
Yalikuwa yakitokea mambo mengi.
Mambo mazito na ya kutisha zaidi ya
walivyoyafahamu wananchi wa kawaida
ambao wanategemea gazeti, radio na
televisheni ziwape habari. Kila mmoja
alikuwa ameshika mikasa ya kuteketea
kwa mamia ya maisha ya watu
wasiokuwa na hatia ambao walipata ajali
ya kutatanisha katika uwanja wa mpira
huko Nigeria. Pia ni wengi waliosikia juu
ya kuungua kwa maghala ya chakula bila
sababu mahususi inayoeleweka huko
Harare. Zaidi, hakuna mtanzania ambaye
hakupata kusikia kuungua tena kwa jengo
la Benki kuu ambalo lilikuwa likijengwa
upya.
Hayo ni maovu ambayo yalisikika katika
vyombo vya habari na mitaani.
Hayakumtisha sana Kombora. Lakini
kulikuwa na haya ambayo yalikuwa bado
siri mioyoni mwa wakubwa wa idara ya
usalama wa taifa. Haya ambayo
hayasemeki wala kutangazwa.
Viongozi wanane wa vyama kadhaa vya
wapigania uhuru wa Afrika Kusini na
mwakilishi wa PLO hapa nchini ambao
walikuwa wakikutana kwa faragha katika
jengo moja jijini Dar es Salaam walikuwa
wamefariki ghafla katika moja ya ajali
zisizoeleweka. Hakuna anayefahamu
kikamilifu chanzo cha vifo hivyo,
isipokuwa kwamba walikufa kwa kuungua
moto uliolipuka ghafla katika chumba
chao cha mkutano. Juhudi zote za
kutafuta chanzo cha moto huo
hazikufanikiwa.
Zaidi ya hao, kuna wale mawaziri wa nchi
zisizofungamana na upande wowote
ambao walinusurika kufa katika ajali
ambayo haikutofautiana na hii ya Dar es
Salaam. Mkutano wao ulikuwa
umeandaliwa kufanyika katika chumba
fulani katikati ya jiji la Lusaka. wakati
wakijiandaa kwenda huko lilitokea suala
jipya ambalo lilichelewesha msafala wao
zaidi ya nusu saa hivi. Kuchelewa huko
kuliyaokoa maisha yao. Kwani chumba
hicho kililipuka kwa moto na kupoteza
maisha ya wafanyakazi wawili wa
chumba hicho na kuharibu vifaa vyote.
Kama awali, chanzo cha moto huo
hakikupata kufahamika mpaka leo.
Hayo ni baadhi tu ya mambo yaliyotokea.
Kulikuwa na hisia kuwa mkono wa
makaburu wa Afrika Kusini ulikuwamo
katika vitendo hivyo. Lakini hisia hizo
hazikuwa na uhakika kamili sasa baada
ya ushahidi mdogo ambao ulikuwa
ukielekea kutoweka kwa njia nyingine ya
kusikitisha.
Ushahidi huo ulikuwa ukielekea kuchipuka
baada ya ule moto ambao uliteketeza
benki kuu. Yuko askari mmoja ambaye
alisema aliamini moto huo ulisababishwa
na mtu mmoja ambaye alifika katika jengo
hilo usiku na kujiita kuwa ni mmoja kati
ya mafundi ambao walikuwa
wakishughulikia jengo hilo. Jengo lilikuwa
chini ya ulinzi mkali wa askari huyo
ambaye alimwamru mtu huyo kusimama
na mikono yake iwe juu. Mtu huyo alitii
amri na kumsihi askari kwa maneno
mengi kuwa amesahau kitu cha muhumu
sana kwake katika jengo hilo, jambo
ambalo lilimfanya askari amruhusu
kuingia ndani baada ya kumpekua kwa
umakini mkubwa. Mtu huyo aliingia
harakahara na baada ya dakika kadhaa
alirudi huku akiwa ameshikiria hirizi
mkononi na kusema kwa furaha.
"Nilikuwa nimesahau hii, ndugu yangu.
Bila kuwa na hii mfukoni siwezi kuishi
zaidi ya masaa ishirini na nne", mtu huyo
alisema akimuonyesha yule askari ile
hirizi.
Askari huyo hakuwa amemwamini sana
mtu huyo, kutokana na jinsi alivyomuona
mkakamavu maana hata alipoelekezwa
mtutu wa bunduki hakuonekana
kubabaika. Hivyo jengo hilo lilipolipuka
moto masaa kadhaa baadaye, askari
huyo alilieleza tukio hilo kwa wakubwa
zake ambao walimweka kati ya watu
ambao walilazimika kuongea na Kombora
ana kwa ana. Baada ya kumsaili kwa
mapana na marefu, Kombora alielekea
kuamini kuwa mtu huyo aliyeingia katika
jengo hilo usiku alihusika kwa njia moja
au nyingine katika janga hilo. Lakini pindi
walipobuni mbinu za kuanzisha msako wa
kumtafuta mtu huyo, askari huyo ambaye
ni mtu pekee aliyewahi kumuona mtu
huyo, alikutwa akielea baharini pwani ya
Magogoni akiwa maiti. Hakuna aliyeweza
kueleza kilichomtoa kwake Magomeni
Mikumi na kuja kuogelea kwa mara ya
mwisho Magogoni.
Ilikuwa dhahili kuwa askari huyo aliuawa.
Jambo ambalo lilimfanya Inspekta
Kombora na wenzake wazidi kuamini
kwamba kulikuwa na namna katika ajali
hizo zilizotokea katika miji mbalimbali ya
Afrika huru. Juhudi zao za kutafuta
chanzo na watendaji wa maafa hayo
hazikuelekea kuzaa matunda yoyote zaidi
ya hisia tu, kwamba Afrika Kusini
ilihusika. Hisia ambazo ziliongezewa
uzito na vitisho ambavyo vililetwa kwa
njia mbalimbali zikitishia uhai wa maisha
ya watu na nchi ambazo eti zingeendelea
na msimamo wao wa kuibana Afrika
Kusini. Vitendo ambavyo, licha ya
kusababisha hofu na mashaka,
vingeweza kupunguza hamasa za moyo
wa kimapinduzi katika fikra za mashujaa
endapo zingeachiwa kuendelea. Ni hapo
ndipo Inspekta Kombora alipozikumbuka
silaha zote na kutamani zielekezwe Afrika
Kusini. Ni hapo pia alipowakumbuka
mashujaa wote na kutamani waelekee
Afrika Kusini. Na kati ya mashujaa hao
jina la Joram Kiango lilitangulia kumjia
rohoni.
Hiyo ilikuwa baada ya kuwasiliana na
wakuu wa vikosi vyote maalumu vya
upelelezi katika nchi zote zilizokwisha
husishwa na maafa hayo ya kutatanisha.
Walishauriana kuwa kila nchi ifanye juu
chini kuhakikisha kisa cha maafa hayo
kinafahamika na ikiwezekana maafa hayo
yakomeshwe. Ndipo Inspekta Kombora
alipoanza kufanya kila juhudi. Tumaini
pekee ambalo lilielekea kumpatia walau
fununu, yaani yule askari mlinzi wa benki
kuu alikuwa sasa ameuawa kwa hila.
Harakati za kupeleleza nani alihusika
katika kumuua askari huyo hazikuwa
zimezaa matunda yoyote. Hivyo Inspekta
Kombra alijikuta hajapiga hatua yoyote
katika jukumu hilo. Badala yake alijiona
kama kiwete ama mtu aliyepooza ambaye
anasubiri maafa ya moto unaomjia kasi.
"Joram lazima ashirikishwe", Kombora
alifoka kimoyomoyo.
Alikuwa na habari zote za Joram, kuwa
tangu baada ya mkasa wa salamu toka
kuzimu alikuwa ameiacha ofisi yake na
kuanza maisha ya kiupuuzi ya kustarehe
katika mahoteli na mabaa akijistarehesha
na yule msichana mzuri wa Arusha
aitwaye Nuru.
"Yeye si mtu wa kuupoteza muda wake
katika mabaa. Kipaji chake kinahitajika
sana katika vita hii. lazima apatikane",
Inspekta Kombora alisema huku akiinuka
kutoka kitini.
Alimtuma mtu ambaye alizunguka katika
mahoteli makubwa na kumpata Joram.
Lakini, kama Inspekta Kombora
alivyotegemea, majibu ya Joram yalikuwa
ya kijeuri kiasi kwamba mtu huyo alijiona
mjinga na kurudi kwa Inspekta Kombora
akiwa amechukia. Jambo ambalo
lilimfanya jioni hii Inspekta Kombora
mwenyewe ayavue magwanda yake na
kuvaa mavazi ya kawaida, kisha akajitosa
katika ukumbi wa Embassy ambao
aliambiwa kuwa Joram alikuwemo
akistarehe.

ITAENDELEA
 
SURA YA PILI--
II
Joram alikuwa ni mtu ambaye halewi kwa
urahisi, tunaweza kusema kuwa alikuwa
amechangamka pindi Kombora alipokuwa
amekaribia meza yake na kuketi.
"Karibu sana Inspekta, karibu uketi",
Joram alisema kwa uchangamfu huku
akimwita muhudumu wa hoteli hiyo. "Leo
naweza kusema kuwa ni siku tukufu sana
kwangu kutembelewa na Inspekta Mkuu.
Habari za siku nyingi mzee?".
"Polepole kijana", Kombora alisema.
"Wanasema siku hizi hata kuta zina
masikio".
"Kwani kuna lolote la siri tunaloongea
hapa mzee?, Siku hizi mambo yote ya siri
nimeachana nayo mzee. Nimeamua kuwa
raia mwema na mtulivu kama ulivyokuwa
ukinitaka niwe", Lilikuwa jibu la Joram.
Kombora hakutia neno. Akamgeukia Nuru
na kumsalimu, "Bila shaka huyu ndiye
yule dada ambaye alikuwa na balaa la
kulazimishwa kushirikiana na yule mwuaji
ambaye alikusudia kuangamiza viongozi
wengi wasio na hatia?", Joram na Nuru
waliitika kwa vichwa. "Ni msichana shujaa
sana. Msichana wa kawaida angeweza
kupoteza kichwa chake mara baada ya
kukabiliwa na mkasa mkubwa kama ule",
alimaliza na kupokea kinywaji chake
akaanza kunywa.
"Sivyo mzee", Nuru alijibu. "Kila nikifikiria
kile kitendo naona aibu kubwa sana.
Nisingestahili kukubali kulazimishwa
kushiriki katika mauaji ambayo
yangekuwa ya kinyama kama yale.
Ingawa yule jasusi Proper alikuwa
kanilaghai kuwa ungekuwa mzaha wa
kawaida bado sikustahili kuafikiana naye.
Uzalendo wangu ulitiwa dosari na kitendo
kile. Najaribu kutafuta nafasi ya
kuudhihilishia moyo wangu lakini
sijafanikiwa...".
"Joram ananinyima nafasi hiyo", Nuru
aliongeza baada ya kusta kidogo.
"Ni hilo tu ulilotaka kusema Nuru", Joram
alidakia. "Nadhani hata Inspekta amefuata
kujadili hilo, au sivyo mzee.
"Inspekta Kombora aliimeza bia iliyokuwa
kinywani mwake. Kisha alijibu.
"Kiasi ni kweli niko hapa kujadili hilo, kiasi
siyo kweli". Alisita kidogo na kuendelea.
"Unajua hatujaonana kwa muda mrefu?
Tangu ulipoondoka Arusha kwa hasira
baada ya kuitupa bastola yako
hatujaonana tena. Nilifika katika chumba
cha dada huyu nusu saa baadaye na
kuukuta ubongo ule na bastola. Nilidhani
umemuua wewe. Lakini bastola yako
haikuwa imefyatuliwa walau hata risasi
moja. Mara kikatokea kile kitabu ambacho
kilinifanya nielewe yote yaliyotokea. Ndipo
nikaelewa kwanini umekasirika na
kuamua kuwa mnywaji".
"Niite mlevi Inspekta, vyovyote sijali".
"Hapana. Wewe si mlevi na wala huwezi
kuwa mlevi. Ni mnywaji tu. Mnyaji
ambaye hanywi kwa ajili ya kupenda
kunywa, isipokuwa kwa hasira baada ya
kunyang'anywa fursa ya kukitia risasi
kwa mkono wako kichwa cha yule
mshenzi. Sivyo Joram?" Kombora alitulia
akimtazama Joram. Mara Joram
akakumbuka kuwa hajavuta sigara kwa
muda mrefu. Alitoa sigara moja na
kuiwasha baada ya kuwataka radhi jirani
zake.
"Kuacha hadhi yako ipotee kwa sababu
ya kukosa kumuua mtu mmoja tu
duniani!", Kombora aliendelea, "Sioni
kama ni haki. Ziko nafasi nyingi za
kufumua vichwa vya watu wenye haki
kabisa ya kufumuliwa. Hati maalum
inatayarishwa ambayo itakuruhusu
kufanya lolote kama afisa yeyote wa
usalama mwenye jukumu maalumu. Zaidi
kimetengwa kifungu maalumu cha fedha
ambacho kitaingizwa katika akaunti yako
ili pesa zisiwe kipingamizi..."
"Taratibu Inspekta", Joram alimkatiza.
"Vipi, mbona mema mengi hivyo, kama
sikosei unachotaka kusema ni kwamba
unaniomba nishiriki katika kutafuta kiini
cha maafa haya yanayotendeka katika
nchi za mstari wa mbele. Na kama
sikosei nadhani mtu uliyemtuma kwangu
amekupa majibu yangu rasmi. Msimamo
wangu ni uleule. Na utaendelea kuwa
uleule. Kama mngefahamu Joram ambaye
alikuwa mpenzi wa Tanzania na Afrika
kwa ujumla, lazima muelewe kuwa Joram
huyo amekufa. Aliyeko hai mbele yako, ni
Joram mpya. Joram ambaye hana na
wala kiu ya kushiriki kwa njia moja ama
nyingine katika masuala yoyote ya nchi.
Aliyeko mbele yako ni Joram wa
mastarehe, Joram wa kutumia. Hata dada
yangu Nuru hapa nadhani anaelewa".
Ndipo Kombora alipoona ugumu wa kazi
iliyoko mbele yake. Kumshauri Joram
ilikuwa sawa na kulilazimisha jabali lielee
juu ya maji. Akiwa mtu ambaye hakuzoea
kuwabembeleza binadamu wengine, hasa
wanaume, Kombora alisema kwa sauti
ambayo ilificha hasira na unyonge.
"Pengine unajua unachokifanya. Lakini
nadhani hujui ni kiwango gani cha
madhara yanayolikabiri taifa hili endapo
tutashindwa kuukomesha uovu huu
unaotunyemelea. Niruhusu nikusimulie
mambo ya kutisha ambayo hayajavifikia
vyombo vya habari".
"Haitasaidia", Joram alimjibu Inspekta
Kombora, "Utaupoteza bure muda wako.
Ninachohitaji kusikia ni habari za
burudani tu. Kama kuna burudani mpya
ambayo sijaiona, kinywaji kipya ambacho
sijakinywa au muziki mpya ambao
sijausikia, nitafurahi endapo utanisimulia.
Juu ya vifo vya marais na raia wasio na
hatia na wenye hatia, si kazi yangu tena".
"Hata hivyo sauti yako haifanani kabisa
na madai yako Joram. Kuna watu ambao
silika yao ni kukesha katika mabaa na
kwenye madansi, wewe si mmoja wao.
Kuna wanaostarehe kusubiri maafa ya
kusikitisha, wewe si mmoja wao Joram.
Kuna wanaofurahia radha ya pombe na
utamu wa muziki zaidi ya kazi na
ushujaa, wewe si mmoja wao vilevile".
"Zamani, Inspekta. Sasa hivi mimi ni
mmoja wao. Na kama huna maongezi
mengine zaidi ya hayo mzee, nitashindwa
kuendelea kukusikiliza", Joram alimaliza
na kutoa sigara yake na kuiwasha.
Kombora hakuona kama angeweza
kufanya lipi la kumshawishi Joram.
Alimtazama Nuru kama aliyehitaji
msaada wake. Akayaona macho yake
mazuri yaliyojaa uzuri katika hali yake ya
kukata tamaa. Hilo kiasi lilimfariji
Kombora. Alifahamu kuwa anaye msaidizi
ambaye angesaidia katika juhudi zake za
kumrejesha Joram Kiango katika dunia ya
Joram Kiango. Kombora hakuwa mgeni
katika dunia hii alijua kuwa mwanamke
mzuri ni silaha. Hivyo akamtupia Nuru
jicho la kumtaka aelewe kuwa
anautegemea msaada wake. Kisha
aliinuka na kuaga bila ya kumaliza
kinywaji chake.
"Hukufanya vizuri, Joram", Nuru
alimwambia.
"Mfuate mkazungumze vizuri".
"Hivyo tu, sikia...".
Nuru akavunjika moyo. Uchungu
ukamwingia rohoni. Alijilazimisha
kuendelea kunywa pombe, lakini
haikumuingia. Baada ya jitihada nyingine
alimtaka Joram radhi, akaondoka
kutangulia chumbani.
"Samahani, naweza kuketi hapa", alisema
mtu mmoja akimsogelea Joram baada ya
Nuru kuondoka.

ITAENDELEA
 
kumekucha tena kidi kudi endeleza burudani mkuu
 
mkuu kidi kudi weekend kimya tupu hofu imenijaa!
 
busara zako muhimu hapa jamvini kidi kudi tupe uhondo
 
daa asee af hizi riwaya ndio zilinifanya niamin bongo hatuwezekan katka nyanja ya ujasusi.
 
Poa kidi kudi nakufuatilia kwa ukaribu kiongozi
 
Last edited by a moderator:
SURA YA TATU
Alikuwa mtu wa umri wa kati. Sura yake
ilionyesha dalili zote za kutocheka,
macho yake yakionyesha dalili ya
kuelemika. Kiasi alionekana kama pombe
ilianza kumshinda nguvu, japo alitembea
kwa uhakika.
Joram alimtazama kwa makini kabla ya
kumjibu, "Una haki ya kukaa popote. Nchi
huru hii".
"Asante", alijibu mtu huyo huku akijiweka
kitini. Baada ya dakika mbili tatu za
kunywa na kuvuta kwa utulivu alimgeukia
Joram na kumwambia, "Samahani. Sina
budi kulitoa dukuduku langu. Siku zote
nimekuwa na hamu ya kuipata fursa hii
ya kuketi nawe. Kama sikosei u Joram
Kiango".
Joram alimtazama kwa makini mtu huyo.
Alipochelewa kumjibu mgeni wake
aliendelea.
"Tumekuwa tukikutana mara kwa mara
katika majumba ya starehe.
Kilichonifanya nikufahamu ni huyu
msichana mzuri unayefuatana nae. Kwa
kweli sina budi kukupa pongezi zako.
Wazuri nimewaona na aina yake lakini
huyu sijapata kuona. Ulimpataja yule dada
Joram". Jambo moja lilikuwa limemvuta
Joram katika kumsikiliza mtu huyu.
Jambo la pili lilijitokeza. Sauti. Ilikuwa
sauti ya kawaida, ikizungumza kiswahili
cha kawaida katika masikio ya watu wa
kawaida. Lakini katika masikio ya Joram
Kiango, Joram ambaye alikuwa sasa
amekaa chonjo, sauti hiyo ilificha uhalisia
fulani.
"Unadhani una haki gani ya kunifahamu,
na kumfahamu msichana wangu wakati
mimi binafsi sikufahamu hata kidogo",
Joram alimuuliza. Kama ambaye
alilitegemea jibu lile yule mgeni alijibu
mara moja japo kwa kusitasita.
"Mimi kwa jina naitwa ISmail Chonde. Ni
mfanyabiashara wa siku nyingi.
Nimezaliwa na kukulia hapahapa ingawa
siku hizi naishi Nairobi".
"Na unawezaje kunifahamu kwa urahisi
kiasi hicho?".
"Nasoma vitabu, nasoma magazeti.
Hakuna asiyekufahamu Joram". Sauti
iliendelea kuwa na walakini katika hisia
za Joram.
"Inaelekea bado huna maswali ya
kuniuliza bwana Chonde. Nataka
kumuwahi huyo msichana unayemwita
mzuri".
"Kweli. Inaonyesha aliondoka hapa akiwa
amechukia", Joram alitabasamu.
"Naona umeona mengi zaidi ya hilo".
"Ndio, nimeona na kusikia mengi. Kwa
kweli endapo utaniona mlevi,
nilichokusudia kuongelea ni yule mzee
aliyekuacha muda. Nafahamu yule ana
madaraka makubwa serikalini. Kama
sikosei alikuwa akikushawishi utoe
mchango wako katika kupeleleza kuhusu
matukio haya. Na niliona akiondoka bila
furaha. Inaelekea umemkatalia. Hivi kweli
umekataa katakata", Joram alimtazama
kwa makini zaidi.
"Sielewi maswali yako yanaelekea wapi?",
alihoji Joram.
"Inashangaza", Chonde aliongeza. "Joram
ninayemfahamu mimi hawezi kuipoteza
nafasi nzuri ya kuonyesha ushujaa wake.
Afrika iko katika mashaka makubwa. Watu
wanakufa hovyo. Majumba yanalipuka
hovyo. Bara zima la Afrika liko
mashakani. Joram ninayemfahamu mimi
angetoa hata roho yake kupambana na
hali hii", Joram alisikia na kupima sauti
ile, akiilinganisha na uso wa msemaji.
Ingawa aliongea kama mtu mwenye
uchungu wnchi na hisia ya bara lake,
bado hisia fulani zilimfanya Joram aone
kitu kama kebehi katika macho yake.
Kana kwamba alikuwa na hakika kuwa
Joram na U Joram wake asingeweza
kufanya lolote. Wazo hilo lilimuongezea
Joram hamu ya kuendelea kumsikiliza.
"Bado sijaelewa unachotaka kusema",
Joram alichochea.
"SIdhani kama wewe ni mzito wa kuelewa
kiasi hicho", wakatazamana. Kila mmoja
akimsoma mwenzake. Kisha Chonde
aliangua kicheko kirefu kilichomwacha
Joram akitabasamu. Baada ya kicheko
hicho aliongeza, "Samahani endapo
umeniona mhuni au mlevi. Sikuwa na nia
mbaya zaidi ya kuzungumza nawe na
kufahamiana. Kwa kheri". Aliinuka na
kuondoka akielekea maliwatoni. Mwendo
wake ulikuwa wa kilevi zaidi ya sauti
yake.
Joram aliendelea kunywa taratibu.
Alipomuona rafiki yake huyo mpya
anayeitwa Chonde akitoka nje ya hoteli na
kusikia mlio wa gari ukiondoka, Joram
alielekea mapokezi ambapo alimsalimu
tena msichana aliyekuwa hapo na
kumuuliza kwa upole, "Samahani dada.
Hivi huyu bwana aliyetoka sasa hivi
anakaa katika hoteli hii?".
"Yule, hakai hapa. Huwa anatokeatokea
tu. Kila mara huja na msichana wake. Leo
ndio kwanza nimemuona akiwa peke
yake. Sijui wamekosana nini na msichana
huyo. Maana huyu bwana inaonekana
pesa si moja ya matatizo katika maisha
yake", msichana huyo alieleza.
"Pengine hawajakosana", Joram
alimchokoza.
"Wamekosana. Bila hivyo
asingenikonyeza mara mbili", Joram
alicheka. Maongezi yao yalikatishwa kwa
simu ambayo msichana huyo alikuwa
akijibu. Alipotaka kuanza tena maongezi
iliingia simu nyingine. Hii msichana huyo
alionekana kuifurahia zaidi. Alizungumza
kwa furaha huku akitabasamu. Baada ya
kutoa chombo cha kuongelea alimgeukia
Joram na kusema.
"Unaona, nimekwambia leo hana mtu.
Ananiambia nikimaliza kazi nimkute hoteli
ya New Afrika, chumba namba 104".
"Ndipo anapokaa?", Joram alihoji.
"Bila shaka".
Baada ya mazungumzo hayo Joram
aliirudia meza yake na kuendelea kunywa.
Mawazo yake yalikuwa yakimfikiria mtu
huyo Chonde. Hakuelewa nini hasa
ilikuwa dhamira ya maongezi yake yale.
Alishuku kuwa pengine alikusudia kupata
undani wa Joram na uamzi wake.
Kwanini?, zaidi Joram alishuku kuwa mtu
huyo hawakukutana kuzungumza
kiajaliajali, bali alikuwa akimfuata yeye au
Kombora kwa ajili hiyo. Juu ya yote hayo
hisia za Joram kuhusu mtu huyo zilizidi
kujiimarisha akilini. Aliona kama
ulikuwemo walakini fulani katika sauti ya
kiswahili chake ambayo iliutia dosari
Utanzania wake. Hayo na kile alichoona
katika macho ya mtu huyo zilimtia Joram
hamu ya kumfahamu mtu huyo zaidi.
Hivyo dakika tano baadaye alijikuta
mitaani akielekea New Afrika. Alipofika
hapo alimwendea mfanyakazi wa
mapokezi na kuzungumza naye hili na lile
huku macho yake yakiwa kazini kutazama
kama funguo namba 104 ulikuwepo.
Aliuona akauliza juu ya mtu wa chumba
fulani ambacho aliona ufunguo wake
haupo.
"Yuko ndani, ameingia sasa hivi".
"Ngoja nikamuone", baada ya kwenda
chumba hicho, Joram alipanda ghorofani
hadi chumba namba 104 ambacho
kilikuwa kimefungwa. Kuacha kwake tabia
ya kutembea na bastola hakukuwa
kumemfanya aache kutembea na vifaa
vyake vidogo vidogo kama funguo malaya
ambazo hazishindwi kulifungua kufuli la
aina yoyote. Hivyo kitasa hicho cha
mlango wa Chonde kilimpotezea nusu
dakika tu.
Chumbani humo, Joram aliurudisha
mlango na kuufunga kwa ndani. Kisha
aliangaza huku na kule kwa makini.
Kilikuwa chumba cha kawaida kama
vilivyo vyumba vingine vya hoteli. Hivyo
Joram hakuwa na kazi kubwa ya
kupekuwa magodoro na viti. Hakuna
chochote. Ndipo alipoliendea Kabati na
kulifungua. Ndani ya kabati hilo kulikuwa
na sanduku kubwa ambalo Joram
alilifungua. Kulikuwa na pesa za kutosha
pamoja na mavazi. Vitu hivyo
havikumvutia Joram. Macho yake
yalivutiwa na nyaraka mbalimbali ambazo
alizipekua kwa umakini. Mengi yalikuwa
makaratasi ya kawaida yaliyomuonyesha
kuwa aliitwa Afith Chonde. Baada ya
kupekuwa zaidi aliipata hati yake ya
kusafiria. Aliifungua haraka haraka huku
akianglia mihuri iliyogogwa katika nchi
mbalimbali ambazo Chonde alikuwa
amezitembelea. Alikuwa anatembea sana.
Mihuri ya Nairobi, Lagos, Lusaka, Harare,
London, New York, Hong Kong, Tripol na
nyinginezo ilikuwa ikionekana waziwazi.
Hilo lilimfanya Joram azidi kuvutiwa na
mtu huyo. Hakuonekana kama
mfanyabiashara mkubwa kiasi hicho.
Zaidi ya vipindi alivyokuwa akitumia
kutoka mji mmoja kwenda mwingine kwa
muda mfupi, hivyo Joram alimshuku kuwa
hakuwa mfanyabiashara wa kawaida.
Hivyo akaongeza umakini katika upekuzi
wake.
Kama alivyotegemea Joram aligudua
mifuko ya siri katika begi hilo. Mifuko
ambayo maafisa wa forodha wasingeweza
kuiona bila ujuzi maalumu. Katika mifuko
hiyo, Joram alikuta bastola moja aina ya
Rivolver, maandishi mbalimbali ambayo
alipojaribu kuyasoma hakuweza kwani
yalikuwa yameandikwa kimafumbo
mafumbo kwa hali ya kijasusi kamili,
pamoja na kijaruba kimoja cha chuma
kilichokuwa kimefungwa kwa ufunguo.
Kijaruba hicho kilimvutia zaidi Joram.
Alihisi kuwa kilikuwa kimeficha mengi
zaidi ya yale aliyokuwa ameyaona. Hivyo
alianza kujaribu funguo zake malaya.
ilimchukua dakika kadhaa alipogundua
kuwa asingeweza kukifungua kisanduku
hicho. Kilitengenezwa maalumu
kufunguliwa na mtu mwenyewe. Kiu ya
Joram juu ya kumjua mtu huyu ikazidi.
"Vipi awe na kisanduku kama hicho,
kimeficha nini, na maandishi haya ya siri
yanasema nini?, siyo bure. Liko jambo",
Joram aliropoka.
"Ndio. Kuna jambo", sauti ilizungumza
nyuma ya Joram. akageuka hima na
kukutana na uso wa Chande akimtazama
kwa kebehi. alikuwa kaketi juu ya kochi.
alivyoingia chumbani kwa ukimya kama
jini na kuketi kwa utulivu kipindi chote ni
jambo ambalo lilimuongezea hofu Joram
akaamini kuwa yule hakuwa binadamu wa
kawaida. Akageuka kumtazama Chonde
huku akiruhusu tabasamu zake kishujaa.
Tabasamu ambayo ilifuatwa na sauti yake
tulivu.
"Tumesema nimefumaniwa".
"Ndio umefumaniwa. Na bahati mbaya ni
kwamba umefumaniwa na kifo. Binadamu
hanichezei mimi na akaendelea kuishi",
Chonde alisema huku akiinuka taratibu
kutoka kitini. "ulijifanya umeacha mambo
yako ya kuingilia mambo yasiyokuhusu.
Kumbe ulikuwa ukijiburudisha kwa
kujidanganya mwenyewe. Umekosea
sana".
"Huwa nafurahia zaidi kuwaua watu
wangu kwa mikono yangu", alisema
Chonde akizidi kusogea.
Mzaha haukuwemo katika macho na sauti
ya Chonde kisha alionekana ni mtu
anayejua nini anachofanya. Jambo
ambalo lilimfanya Joram asogeze mkono
kuiendea ile bastola iliyokuwa imelala
kando yake. kama alikuwa ameuhisi
wepesi wa Chonde basi alikuwa hajauona.
Mara tu mkono huo ulipoifikia bastola
mguu wa Chonde ulitua juu ya mguu huo.
Wakati huo huo Joram alipokea ngumi
mbili nzito zilizomfanya Joram asahau
bastola. Chonde hakuwa na roho mbaya
kiasi hicho. Alimpa muda wa kujiandaa.
Joram akavuta pumzi kwa nguvu na
kuanza kumwendea Chonde. Alimshitua
kwa mkono wa kulia, Chonde aliudaka na
wakati huohuo akamkata Joram judo ya
mgongo na kumfanya aanguke kifudifudi.
Alipoinuka Chonde alikuwa akimsubiri
huku akicheka.
"Wanasema Tanzania kuna mtu mmoja tu
wa kujihadhari nae, ambaye anaitwa
Joeam Kiango. Niko naye chumbani, sioni
ujoram wake".
Maneno hayo yalimuuma Joram zaidi ya
kipigo alichopokea. Akainuka ghafla na
kumwendea Chonde akitumia mitindo na
mbinu zake zote za kupigana. Vipigo
kadhaa alimpata Chonde. Lakini kwa jinsi
vipigo hivyo alivyompiga kwa hasira
havikuwa na madhara kwa Chonde dakika
chache baadae Joram alijikuta yuko chali
sakafuni kasalimu amri. Chonde
akaendelea kutabasamu.
Sasa Joram alimtazama Chonde kwa
mshangao zaidi ya hasira. Ni mtu wa aina
gani anaweza kumwadhibu kama
mwanae, bila shaka si mtu wa kawaida.
Amejifunza mengi kama anavyoonekana
kujua mengi. Pamoja na kwamba kipindi
kirefu kilikuwa kimepita bila Joram
kufanya mazoezi ya viungo na akili,
pamoja na kule kuzoea starehe za
mahotelini na ulevi mwingi, bado hakuna
kama binadamu yeyote angeweza
kumfanya kama Chonde alivyokuwa
amemfanya.
Ile hamu iliyokuwa imelala usingizini
ikaibuka upya katika moyo wake. Hamu
ya mapambano, vitisho, maafa, damu, na
mikasa, hamu ya kuwatia adabu watu
ambao wanependa kuwafanya vibaya
binadamu wenzao. Chonde alionekana
kama mmoja wao. Joram alimtazama
tena na kutabasamu kwa uchungu huku
akisema, "Haya umeshinda.
Kinachofuata?".
"Ni kifo chako", Chonde alijibu kijeuri.
"Siwapendi vijana watundu kama wewe.
Kufa huna budi.
"Kosa langu".
"Unapenda kufa?".
Joram alifikiri kwa makini lipi angefanya
kuahirisha hukumu hiyo ya kifo. Alihitaji
muda ili ikiwezekana itokee njia moja ama
nyingine ya kuyaokoa maisha yake.
Akaanzisha maongezi kwa sauti ambayo
aliifanya dhaifu kuliko alivyokuwa
akimuuliza Chonde hili na lile. Chonde
alikuwa mgumu wa kutoa habari kama
jabali. Kati ya maneno ya kashfa na
matusi kwa Joram, nchi na bara zima la
Afrika hakutamka neno lolote
litakalomfanya Joram ajue kuwa yuko
katika ulimwengu wa ujasusi.
Alichoambulia ni zile hisia tu kuwa
Chonde hakuwa raia wa kawaida tu.
"Umeahirisha sana kifo chako", Chonde
alisema baadae kama aliyekuwa
akizisoma fikira za Joram. Sasa iliyobaki
ni kazi ndogo ya kukutoa uhai. Nitakuua
kwa mkono wangu wa kushoto. Maiti
yako itaokotwa kesho ikiwa
imevunjikavunjika kama mtu aliyeanguka
kutoka ghorofani. Kwa jinsi ulivyobadilika
kitabia hakuna atakayejuwa kuwa
umeuawa", baada ya maneno hayo,
Chonde aliinuka na kumwendea Joram
kama alivyofanya awali, lakini macho
yake yalitangaza kitu kimoja tu, kifo.
Joram alijiandaa. Akijua kuwa vita
vilivyokuwa mbele yake vilikuwa vita
vikubwa pengine kuliko alivyowahi
kupambana navyo. Vita vya kuitetea roho
yake. Akaikusanya akili yake yote na
kumsubiri Chonde kishujaa.
Mara mlango ukagongwa.
Chonde aligutuka kwa mshangao na
kuutazama mlango. Joram hakuipoteza
nafasi hiyo. Aliruka na kuufanya mguu
wake utue katika shingo ya Chonde.
Lilikuwa pigo ambalo Chonde
alilitegemea. Akalihepa na kuachia judo
ambalo Joram aliikinga. Papo hapo
mlango ukagongwa tena na kufunguka na
kuruhusu msichana mzuri kuingia.
Alikuwa yule msichana wa mapokezi pale
Embassy hoteli. Alitokwa na macho ya
mshangao kuona miili yenye jasho,
michubuko na damu, ya wanaume hawa,
ilikuwa tayari kuvamiana. Wote
walimtazama msichana huyo. Chonde
akimlaani, Joram akishukru. Akiwa kama
hajui lipi la kufanya msichana huyo
aliduaa mlangoni, Midomo wazi.
"Karibu ndani. Tulikuwa tukifanya mazoezi
ya viungo na huyu rafiki yangu", Chonde
alimwambia yule msichana huku akivaa
tabasam ambalo lilificha kabisa tabasam
la mauaji. "Karibu ndani. Na wewe ndugu
yangu nenda zako sasa. Tutakutana siku
nyingine".
Joram hakuamini, aliyarekebisha mavazi
yake na kutoka chumbani humo taratibu.
Hakuwa amesahau kumwachia msichana
huyo tabasam la shukrani.
********************************************
*****************
ITAENDELEA
 
SURA YA TATU
II

"Nadhani hakuna njia nyingine zaidi ya
kumlazimisha Joram", Kombora alikuwa akifoka
wakati wa kikao cha dharura kilichofanyika
usiku huo ofisini kwake. "Hawezi kuachwa
aendelee kustarehe katika mabaa huku taifa na
bara zima likiwa mashakani. Mchango wake
unahitajika".
Kikao hicho kilikuwa kimehudhuriwa na viongozi
wa ngazi za juu kutoka idara zote za usalama.
Kiliitishwa ghafla baada ya kuokotwa barua
moja ya vitisho katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Barua ambayo iliandikwa kwa ufupi sana kuwa
ajali za kimiujiza zingeendelea kuipata Tanzania
na nchi zote zilizo mstari wa mbele, endepo
serikali haitachukua hatua za haraka kukomesha
msimamo wake wa kupinga utawala wa kibaguzi
wa Afrika Kusini. Barua hiyo iliongeza kwamba
safari hii moto ungeiteketeza Hospitali ya
Muhimbili, Hoteli ya Kilimanjaro, Jengo la
Kitega Uchumi na baadae Ikulu.
Aliyeiokota barua hiyo na kuisoma aliwaonyesha
wakubwa zake nao baada ya kuisoma waliikabidhi
kwa Waziri Mkuu. Yeye pia, baada ya kuisoma
alienda Ikulu ambapo alimpatia Rais.
"Upuuzi ulioje huu. Hatutaacha kuwatetea ndugu
zetu wanaoteswa bila makosa kwa ajili ya
vitisho hivi. Havikuanza leo. Wala haviwezi
kwisha leo. Tutapigana hadi mtu wetu wa
mwisho katika kuilinda hadhi ya mtu mweusi
katika bara letu hili la Afrika". Pengine Rais
alijibu hivyo akifoka kwa hasira.
"Barua hiyo wakabidhi watu wa usalama. Nadhani
hawatakubali kuendelea kuchezewa kiasi hicho.
Waambie kwamba hatutaki upuuzi wowote
ulioandikwa katika waraha huo haramu utokee".
Huenda Rais aliongeza hayo.
Hakuna aliyeshiriki katika maongezi hayo ya
faragha, isipokuwa hisia hizo zinakuja kutokana
na jinsi Waziri Mkuu alivyomwita Inspekta
Kombora na kumkabidhi barua hiyo. Baada ya
Kombora kuisoma kwa umakini Waziri Mkuu
alimwambia: "Ni barua ya hatari sana. Na
imeandikwa na watu hatari. Watu wenye kichaa.
Kufuatana na hali ilivyo hatuwezi kukubali kuwa
mateka ama watumwa wa Makaburu kwa kuhofia
vitisho vyao. Lazima tupambane nao ana kwa
ana kama tunavyopambana nao kwenye uwanja
wa mapambano. Tuliwashinda Msumbiji, Angola na
Zimbabwe. Kwa nini tusiwashinde Namibia na
Afrika Kusini, tutawashinda. Wao wanajua hivyo,
ndio sababu inayowafanya wakimbie uwanja wa
mapambano na kuja huku kupigana kiuoga".
"Kama tulivyoshuku kitambo, mikasa hii haikuwa
ya kawaida. Kulikuwa na mkono wa mtu. Mkono
wa mtu huyu ambaye ameandika barua hii na
kuthubutu kuipenyeza katika ofisi yangu. Ingawa
haijafahamika wanatumia mbinu gani kuanzisha
mioto hii, nadhani hutashindwa kufanya juu chini
ili ugundue na kukomesha kabisa upuuzi huo".
Kombora akijua uzito wa jukumu hilo ndipo
aliporudi ofisini na kuitisha kikao hicho
kilichokuwa kikiendelea. Walikuwa wamejadiliana
kwa mapana na marefu kuwa nini hasa kilikuwa
kikitokea na majumba yaungue moto wakati
uchunguzi unaonyesha hakukuwa na kasoro
yoyote ya umeme. Hawakupata jibu. Walikuwa
wamejaribu kuzijumuisha taarifa zote za
upelelezi juu ya nani anaweza kuwa alihusika
katika kusababisha mioto hiyo: bado hazikuwepo
dalili zozote za matumaini. Wakapanga mipango
mipya wakaandaa wapelelezi na vyombo kadha
wa kadhaa katika majumba yaliyotajwa.
Wakawekwa watu katika mahoteli, viwanja vya
ndege na vituo vyote vya usafiri kuchunguza
nani anaingia nchini, nani ametoka na ameleta
nini zaidi ya yote hayo ndipo lilipotolewa
pendekezo la kumshirikisha kila mtu mwenye
uwezo wa kuchangia katika upelelezi. hapo
ndipo jina la joram lilipowatoka midomoni.
Ikawashangaza wajumbe kusikia kuwa hata baada
ya kuombwa na Kombora alikuwa amekataa
katakata kushiriki katika kazi hiyo. Joram
waliyemfahamu alikuwa hangoji kuombwa au
kutumwa bali alijituma. Vipi Joram huyu.
Ndipo mzee Kombora alipoibuka na uamziwa
kumshurutisha.
"Lazima tumlazimishe. Alirudi kama ameacha
upelelezi kwa ajili ya mwanamke basi atarudia
upelelezi kwa ajili hiyohiyo ya mwanamke. Yote
hayo niachieni mimi", Inspekta Kombora
aliwaambia.
Baada ya kikao hicho, Kombora alimchukua
msaidizi wake na kumpeleka chemba. "Sikia",
akamweleza, "Nakutaka uwe msiri wangu wewe
peke yako. Unaweza kutunza siri".
"Na bila shaka. Isipokuwa ya wizi na mauaji tu".
"Hii si ya mauaji wala wizi. Nataka unisaidie
kumteka mtu nyara".
"Kuteka mtu nyara, hiyo mbona haiko mbali sana
na wizi, na kama sikosei ni hatari zaidi ya wizi".
"Ndio. Lakini mtu tutakayemteka atafurahi sana.
Bado ni msichana mzuri sana", Kombora alivuta
pumzi kwa nguvu kisha akaongeza.
"Nataka tumteke yule msichana wa Joram. Hiyo
ndiyo njia pekee ya kumlazimisha".
Baada ya kujadiliana kwa muda walielewana.
Wakaandika barua ambayo ilikusudiwa kuwa iwe
imetoka kwa mtekaji nyara akidai kuwa
amemteka msichana huyu na angemuua endepo
Joram angethubutu kujihusisha na upelelezi
unaoendelea nchini dhidi ya maafa ya
kutatanisha. Licha ya barua hiyo waliandaa damu
ambayo ilipatikana kwa msaada wa Daktari
mmoja wa Hospitali ya Ocean Road ili
waidondoshe chumbani humo ili ionekane kuwa
kulikuwa na mpambano uliosababisha kudondoka
kwa damu ya Nuru.
"Tunacheza mchezo mchafu sana. Mchezo wa
aibu. Lakini hatuna budi", Kombora alisema baada
ya matayarisho wakaelekea Embassy Hoteli
katika chumba cha Joram.
Uchunguzi ulikuwa umewapa fununu kuwa Joram
Kiwango alikuwa akiishi katika Hoteli hiyo ya
Embassy. Habari za mwisho usiku huo zilieleza
kuwa Joram alipoachana na Inspekta Kombora
usiku huo alikuwa peke yake akinywa bia wakati
msichana wake alipoondoka kwenda chumbani. Na
kwamba baada ya muda mrefu Joram alionekana
akitoka nje na hadi sasa hajarudi. Kombora
alitegemea kuwa muda huo ulitosha kumfikia
msichana huyo, kumshawishi na akikataa,
wamlazimishea kuondoka nae kwa siri kabla
Joram hajarudi. Walifanya hivyo.
Walifika haraka Hotelini na kukiendea katika
chumba chake kwa siri kubwa. Mlango ulikuwa
wazi haujafungwa. Waliusukuma baada ya kuingia
wakaufunga nyuma yao. Macho yao yalivutwa na
dalili za vurugu katika chumba hicho, vitu
vilikuwa vimetupwa hovyohovyo, matandiko
yalikuwa yamepinduliwa na masanduku
kufunguliwa. Juu ya meza kulikuwa na karatasi
yenye damu. Upande wa pili wa karatasi hiyo
kuliwa na maandishi ambayo ilikuwa baraua ya
wazi kwa Joram Kiango, barua ambayo haikuwa
tofauti na ile ambayo Kombora alikuwa nayo.
Ndugu Joram,
Tunayo furaha kukufahamisha kuwa tumemchukua
msichana wako Nuru na tutakuwa nae hadi hapo
tutakapomaliza shughuli zetu na kujiridhisha. Hii
ni kwa ajili ya kukusihi kuwa usithubuti kabisa
kujiingiza katika upelelezi wa mambo
yanayoitokea nchi hii. Endapo utakuwa mtoto
mtiifu kama ulivyo siku hizi, hatadhurika. Nawe
utakuwa salama. Vinginevyo utakipokea kichwa
cha Nuru kwa njia ya posta na kisha kitafuata
kifo chako. Asante.
Amri
Kombora alisema tena barua hiyo, kisha
akamgeukia msaidizi wake na kumnong'oneza,
"Tumechelewa sana. Wenzetu wametuwahi",
akampatia msaidizi wake barua hiyo ili nae
aisome.
"Sasa tutafanya nini", alihoji askari huyo baada
ya kuisoma barua hiyo.
"Rudisha kila kitu kama kilivyokuwa. Fanya hima
tuondoke hapa haraka", Kombora alimhimiza
msaidizi wake huku wakianza kusogea mlangoni.
"Nilidhani tungemsubiri Joram".
"Hakuna sababu. Akirudi atajua cha kufanya",
wakatoka na kuifuata njia ya kawaida wakiwa
katika mavazi ya kiraia, watu wachache sana
waliwatupia macho zaidi ya mara moja.
"Jambo moja la kupendeza ni kwamba", Kombora
alikuwa akisema. "Wamemchokoza Joram.
Hawamfahamu vizuri. Wataujutia uamzi wao".
ITAENDELEA
 
SURA YA TATU
II

"Nadhani hakuna njia nyingine zaidi ya
kumlazimisha Joram", Kombora alikuwa akifoka
wakati wa kikao cha dharura kilichofanyika
usiku huo ofisini kwake. "Hawezi kuachwa
aendelee kustarehe katika mabaa huku taifa na
bara zima likiwa mashakani. Mchango wake
unahitajika".
Kikao hicho kilikuwa kimehudhuriwa na viongozi
wa ngazi za juu kutoka idara zote za usalama.
Kiliitishwa ghafla baada ya kuokotwa barua
moja ya vitisho katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Barua ambayo iliandikwa kwa ufupi sana kuwa
ajali za kimiujiza zingeendelea kuipata Tanzania
na nchi zote zilizo mstari wa mbele, endepo
serikali haitachukua hatua za haraka kukomesha
msimamo wake wa kupinga utawala wa kibaguzi
wa Afrika Kusini. Barua hiyo iliongeza kwamba
safari hii moto ungeiteketeza Hospitali ya
Muhimbili, Hoteli ya Kilimanjaro, Jengo la
Kitega Uchumi na baadae Ikulu.
Aliyeiokota barua hiyo na kuisoma aliwaonyesha
wakubwa zake nao baada ya kuisoma waliikabidhi
kwa Waziri Mkuu. Yeye pia, baada ya kuisoma
alienda Ikulu ambapo alimpatia Rais.
"Upuuzi ulioje huu. Hatutaacha kuwatetea ndugu
zetu wanaoteswa bila makosa kwa ajili ya
vitisho hivi. Havikuanza leo. Wala haviwezi
kwisha leo. Tutapigana hadi mtu wetu wa
mwisho katika kuilinda hadhi ya mtu mweusi
katika bara letu hili la Afrika". Pengine Rais
alijibu hivyo akifoka kwa hasira.
"Barua hiyo wakabidhi watu wa usalama. Nadhani
hawatakubali kuendelea kuchezewa kiasi hicho.
Waambie kwamba hatutaki upuuzi wowote
ulioandikwa katika waraha huo haramu utokee".
Huenda Rais aliongeza hayo.
Hakuna aliyeshiriki katika maongezi hayo ya
faragha, isipokuwa hisia hizo zinakuja kutokana
na jinsi Waziri Mkuu alivyomwita Inspekta
Kombora na kumkabidhi barua hiyo. Baada ya
Kombora kuisoma kwa umakini Waziri Mkuu
alimwambia: "Ni barua ya hatari sana. Na
imeandikwa na watu hatari. Watu wenye kichaa.
Kufuatana na hali ilivyo hatuwezi kukubali kuwa
mateka ama watumwa wa Makaburu kwa kuhofia
vitisho vyao. Lazima tupambane nao ana kwa
ana kama tunavyopambana nao kwenye uwanja
wa mapambano. Tuliwashinda Msumbiji, Angola na
Zimbabwe. Kwa nini tusiwashinde Namibia na
Afrika Kusini, tutawashinda. Wao wanajua hivyo,
ndio sababu inayowafanya wakimbie uwanja wa
mapambano na kuja huku kupigana kiuoga".
"Kama tulivyoshuku kitambo, mikasa hii haikuwa
ya kawaida. Kulikuwa na mkono wa mtu. Mkono
wa mtu huyu ambaye ameandika barua hii na
kuthubutu kuipenyeza katika ofisi yangu. Ingawa
haijafahamika wanatumia mbinu gani kuanzisha
mioto hii, nadhani hutashindwa kufanya juu chini
ili ugundue na kukomesha kabisa upuuzi huo".
Kombora akijua uzito wa jukumu hilo ndipo
aliporudi ofisini na kuitisha kikao hicho
kilichokuwa kikiendelea. Walikuwa wamejadiliana
kwa mapana na marefu kuwa nini hasa kilikuwa
kikitokea na majumba yaungue moto wakati
uchunguzi unaonyesha hakukuwa na kasoro
yoyote ya umeme. Hawakupata jibu. Walikuwa
wamejaribu kuzijumuisha taarifa zote za
upelelezi juu ya nani anaweza kuwa alihusika
katika kusababisha mioto hiyo: bado hazikuwepo
dalili zozote za matumaini. Wakapanga mipango
mipya wakaandaa wapelelezi na vyombo kadha
wa kadhaa katika majumba yaliyotajwa.
Wakawekwa watu katika mahoteli, viwanja vya
ndege na vituo vyote vya usafiri kuchunguza
nani anaingia nchini, nani ametoka na ameleta
nini zaidi ya yote hayo ndipo lilipotolewa
pendekezo la kumshirikisha kila mtu mwenye
uwezo wa kuchangia katika upelelezi. hapo
ndipo jina la joram lilipowatoka midomoni.
Ikawashangaza wajumbe kusikia kuwa hata baada
ya kuombwa na Kombora alikuwa amekataa
katakata kushiriki katika kazi hiyo. Joram
waliyemfahamu alikuwa hangoji kuombwa au
kutumwa bali alijituma. Vipi Joram huyu.
Ndipo mzee Kombora alipoibuka na uamziwa
kumshurutisha.
"Lazima tumlazimishe. Alirudi kama ameacha
upelelezi kwa ajili ya mwanamke basi atarudia
upelelezi kwa ajili hiyohiyo ya mwanamke. Yote
hayo niachieni mimi", Inspekta Kombora
aliwaambia.
Baada ya kikao hicho, Kombora alimchukua
msaidizi wake na kumpeleka chemba. "Sikia",
akamweleza, "Nakutaka uwe msiri wangu wewe
peke yako. Unaweza kutunza siri".
"Na bila shaka. Isipokuwa ya wizi na mauaji tu".
"Hii si ya mauaji wala wizi. Nataka unisaidie
kumteka mtu nyara".
"Kuteka mtu nyara, hiyo mbona haiko mbali sana
na wizi, na kama sikosei ni hatari zaidi ya wizi".
"Ndio. Lakini mtu tutakayemteka atafurahi sana.
Bado ni msichana mzuri sana", Kombora alivuta
pumzi kwa nguvu kisha akaongeza.
"Nataka tumteke yule msichana wa Joram. Hiyo
ndiyo njia pekee ya kumlazimisha".
Baada ya kujadiliana kwa muda walielewana.
Wakaandika barua ambayo ilikusudiwa kuwa iwe
imetoka kwa mtekaji nyara akidai kuwa
amemteka msichana huyu na angemuua endepo
Joram angethubutu kujihusisha na upelelezi
unaoendelea nchini dhidi ya maafa ya
kutatanisha. Licha ya barua hiyo waliandaa damu
ambayo ilipatikana kwa msaada wa Daktari
mmoja wa Hospitali ya Ocean Road ili
waidondoshe chumbani humo ili ionekane kuwa
kulikuwa na mpambano uliosababisha kudondoka
kwa damu ya Nuru.
"Tunacheza mchezo mchafu sana. Mchezo wa
aibu. Lakini hatuna budi", Kombora alisema baada
ya matayarisho wakaelekea Embassy Hoteli
katika chumba cha Joram.
Uchunguzi ulikuwa umewapa fununu kuwa Joram
Kiwango alikuwa akiishi katika Hoteli hiyo ya
Embassy. Habari za mwisho usiku huo zilieleza
kuwa Joram alipoachana na Inspekta Kombora
usiku huo alikuwa peke yake akinywa bia wakati
msichana wake alipoondoka kwenda chumbani. Na
kwamba baada ya muda mrefu Joram alionekana
akitoka nje na hadi sasa hajarudi. Kombora
alitegemea kuwa muda huo ulitosha kumfikia
msichana huyo, kumshawishi na akikataa,
wamlazimishea kuondoka nae kwa siri kabla
Joram hajarudi. Walifanya hivyo.
Walifika haraka Hotelini na kukiendea katika
chumba chake kwa siri kubwa. Mlango ulikuwa
wazi haujafungwa. Waliusukuma baada ya kuingia
wakaufunga nyuma yao. Macho yao yalivutwa na
dalili za vurugu katika chumba hicho, vitu
vilikuwa vimetupwa hovyohovyo, matandiko
yalikuwa yamepinduliwa na masanduku
kufunguliwa. Juu ya meza kulikuwa na karatasi
yenye damu. Upande wa pili wa karatasi hiyo
kuliwa na maandishi ambayo ilikuwa baraua ya
wazi kwa Joram Kiango, barua ambayo haikuwa
tofauti na ile ambayo Kombora alikuwa nayo.
Ndugu Joram,
Tunayo furaha kukufahamisha kuwa tumemchukua
msichana wako Nuru na tutakuwa nae hadi hapo
tutakapomaliza shughuli zetu na kujiridhisha. Hii
ni kwa ajili ya kukusihi kuwa usithubuti kabisa
kujiingiza katika upelelezi wa mambo
yanayoitokea nchi hii. Endapo utakuwa mtoto
mtiifu kama ulivyo siku hizi, hatadhurika. Nawe
utakuwa salama. Vinginevyo utakipokea kichwa
cha Nuru kwa njia ya posta na kisha kitafuata
kifo chako. Asante.
Amri
Kombora alisema tena barua hiyo, kisha
akamgeukia msaidizi wake na kumnong'oneza,
"Tumechelewa sana. Wenzetu wametuwahi",
akampatia msaidizi wake barua hiyo ili nae
aisome.
"Sasa tutafanya nini", alihoji askari huyo baada
ya kuisoma barua hiyo.
"Rudisha kila kitu kama kilivyokuwa. Fanya hima
tuondoke hapa haraka", Kombora alimhimiza
msaidizi wake huku wakianza kusogea mlangoni.
"Nilidhani tungemsubiri Joram".
"Hakuna sababu. Akirudi atajua cha kufanya",
wakatoka na kuifuata njia ya kawaida wakiwa
katika mavazi ya kiraia, watu wachache sana
waliwatupia macho zaidi ya mara moja.
"Jambo moja la kupendeza ni kwamba", Kombora
alikuwa akisema. "Wamemchokoza Joram.
Hawamfahamu vizuri. Wataujutia uamzi wao".
ITAENDELEA

asanteeee.
 
kazi ndo imeanza kwa Joram Kiango,nakucheki Kila time kidi kudi
 
Back
Top Bottom