Riwaya/tamthiliya iliyonigusa zaidi, wewe je?

Riwaya/tamthiliya iliyonigusa zaidi, wewe je?

mfadhili
kilio chetu
kiu ya haki
vuta ni kuvute
nguzo mama
rwanda magere
a man of the people
dahhh viko vingi yan
 
mfadhili, nagona, dunia uwanja wa Fujo na betrayal in the city
 
Dunia uwanja wa fujo
kichwa maji
Rosa Mistika
Kilio cha haki
Natala
Haini
Vuta Nkuvute
Kuli
Nyota ya Rehema
Kasri ya Mwinyi Fuad
Shida
Simu ya kifo
Kisima cha giningi
Ahsante mkuu, Je una copy ya nyota ya rehema, kisiwa cha giningi,au Rosa mistika???na je ushawahi Kusoma kitabu kinaitwa ikibidi kufa nife??
 
Ahsante mkuu, Je una copy ya nyota ya rehema, kisiwa cha giningi,au Rosa mistika???na je ushawahi Kusoma kitabu kinaitwa ikibidi kufa nife??

mkuu sina copy yoyoyte
 
Musiba ,ganzel na hammie rajabu ah hawa watu walikuwa wanaijua kazi yao kwa kizazi hiki beka mfaume ninamkubali khasa kwenye "mzee beka na mary 'nadhani hiyo story ya hussein pweza iliitwa hivyo.
Kizazi hiki bado hawajafikia ueledi wa wakongwe kitabu kingine ni allan quartamain na wenzake duh humo mzee mwenye shoka mkuu wa kikosi cha nkomabakosi alifanya yake wakati anasema wanizike kwa desturi za kikwetu wauelekeze uso wangu kuelekea nchi ya uzulu.
 
-Dar es salaam usiku,
-salamu kutoka kuzimu,
-Ngoswe penzi kitovu cha uzembe pamoja na
-Alfu lela ulela.
Dah hivyo vitabu vilinifanya nitafute hela kwa kila namna kuvinunua japo sikuwa na ajira miaka hiyoo.
 
kuna riwaya inaitwa UTENGANO ya MAOHAMED SAID ni nzuri sana km kuna mwenye soft copy yake atuwekee
 
Go read James Hadley Chase's works, recommendations: "The things men do" and "Sucker punch". Zipo loads of softcopies humu. Novel za huyu mtu ni masterpiece, so thrilling walitengeneza about 20 movies from them, ni pure talent this writer!

Umenigusa..usisahau HIT and RUN..
 
The girl who loved a black, mahali maiti zilipo,
Zote zilizotungwa na E. Musiba na Ben Mtobwa.
The river between E.t c
 
Mtambo Wa Mauti- Ben Mtobwa
Vuta n'kuvute - Shafi A. Shafi
Tutarudi na Roho zetu -Ben Mtobwa
Rosa Mistika- nimemsahau mwandishi
Rais anampenda Mke Wangu- Eric Shigongo
 
Hiki cha mtambo wa mauti nakihitJi nitakipata wapi wakuu
 
Kiu,
A man of the people,
Walenisi,
Kitumbua kimeingia mchanga,
_nilitahiniwa nikiwa high school!
 
'Kuna kitabu cha riwaya asilia ambacho si wengi wanakijua kinaitwa 'Utotole' kilitungwa na GW Mtendamema. Ni classic, kingeandikwa kwa kizungu kingeweza kabisa kuvipiku 'Things fall apart' cha Achebe na 'The Concubine' cha Amadi.
Nadhani kilichapishwa 1978 ila mimi nilikisoma kwenye 80s.
Halafu piga ua, maneno hayatoshi kukielezea 'Dunia uwanja wa fujo' cha E. Kezilahabi
Emmanuel Kezilahabiahabi pia aliandika riwaya za "Nagona" na "Mzingile", nilizisoma nikashindwa kupata maudhui yake miaka ya 90s. Mwenye ujuzi wa mambo haya, na ambaye alishazisoma anisaidie tafsiri kwa muhtasari

Hiyo Utotole niliisoma pia miaka ya 80s, sema ilinitisha na visa vyake maana nilikuwa bado mdogo kwa hiyo nilikuwa nawaogopa sana akina Ngoko!

Nawakumbuka wahusika wakuu: Kiselema na Manywele, a.ka.. Utotole na Upendo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom