Riwaya/tamthiliya iliyonigusa zaidi, wewe je?

tisa desemba

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
434
114
Haijalishi ulisoma enzi za mwalimu, mzee ruksa, ben au braza jk sote tumesoma vitabu vya riwaya/tamthiliya mbalimbali za waandishi wetu wa nyumbani.
katika kusoma huko naamini ipo riwaya/tamthiliya iliyokugusa zaidi ambayo hadi leo unaikumbuka zaidi hasa kwa kuangalia dhamira ya mwandishi (mfano:-umaskini, rushwa, haki, mapenzi, ulevi nk) ukihusianisha yanayotendeka sasa katika maisha yako ya kila siku, kwa mantiki hiyo tutajie ni riwaya/tamthiliya ipi iliyokugusa zaidi.

kwa kuanzia mimi mwenyewe riwaya ya "watoto wa mama ntilie" ilinigusa sana hasa ninapopita dampo na kuwakuta watoto wa wazalendo wakiokota vitu, inanikubusha zitta na peter watoto wa yule mama ntilie wa manzese, wewe je.....
 
Nazipenda riwaya zote za Willy Gamba. Mtunzi alikua anaonesha jinsi taasisi za kiserikali hasa hasa usalama wa taifa ulivyokua ukiongozwa na uzalendo katika kutetea maslahi ya taifa. Pia riwaya hizo zilikua zinaonesha mapambano dhidi ya udhalimu wa kibepari ndani ya afrika na mapambano ya uhuru wa kweli kwa afrika.
 
"Pesa zako zinanuka" riwaya hii ilizungumzia tamaa, rushwa. Jamaa alikuwa anapata kipato kidogo lakini alikuwa happy! Alipoonja rushwa, ikamuharibu, akawa fisadi, akaiba hata kile kidogo kilicholetwa kuwasaidia wanyonge! Mwishowe mwanae alikufa kwa palala alipokosa dawa aliyoilangua yeye mwenyewe ili aiuze wakati ilikuwa ya kutoa bure. UKISOMA KITABU HIKI, UKILINGANISHA NA TANZANIA YETU, IMESADIFU MBAYA. Ni kipengele kimoja tu cjajua km wamama wa kitanzania wako wa hvyo kwamba; mke wa fisadi huyo alimwamuru mumewe arudishe pesa yote na ajisalimishe police. I wonder wake wa KAGODA, EPA, MEREMETA wataweza hilo? Kitabu kimeonesha, wanawake wakiamua, wanaweza kukomesha ufisadi. Ebu Tz tujaribu kuwatumia...ila wasiwe km Makinda ya ndege...eeh jama!
 
hapana! Kama mchambuzi wa kazi za fasihi, kazi za Willy Gamba zinaingia kwenye kundi la riwaya chuku, ambazo huwa na visa vya kusisimua vinavyoambatana na mapenzi, wakati mwingine kundi hili huiwa romansia. Mara nyingi, riwaya hizi huwa na malengo ya kibiashara zaidi na si kulenga jamii kama riwaya za dhati. Msanii wa Kizazi kipya, Erick Shigongo ni mmoja wa waandishi wa kisasa wa riwaya chuku!
 
'Kuna kitabu cha riwaya asilia ambacho si wengi wanakijua kinaitwa 'Utotole' kilitungwa na GW Mtendamema. Ni classic, kingeandikwa kwa kizungu kingeweza kabisa kuvipiku 'Things fall apart' cha Achebe na 'The Concubine' cha Amadi.
Nadhani kilichapishwa 1978 ila mimi nilikisoma kwenye 80s.
Halafu piga ua, maneno hayatoshi kukielezea 'Dunia uwanja wa fujo' cha E. Kezilahabi
 
Riwaya iliyonigusa ni KIU YA HAKI.Na nikiiangalia nchi yangu inavyoenda na nikifananisha na hiyo riwaya naona kabisa wa2 walioko selikarini walivyokuwa hawana hata chembe ya ku2pa haki ye2.
 
aisee utotole? Umenikumbusha mbali sana nlikisoma miaka ya 90! Nkiwa primary huku nikilia hasa ile safari ya pango la ulili! Nakumbuka hadi zile nyimbo alizokuwa anaimbiwa utotole wakat anamtafta ndugu yake! "kalumbu kukutula kamkana ng'o" daah ni ktb kizur sana.
 
"Pesa zako zinanuka" riwaya hii ilizungumzia tamaa, rushwa. Jamaa alikuwa anapata kipato kidogo lakini alikuwa happy! Alipoonja rushwa, ikamuharibu, akawa fisadi, akaiba hata kile kidogo kilicholetwa kuwasaidia wanyonge! Mwishowe mwanae alikufa kwa palala alipokosa dawa aliyoilangua yeye mwenyewe ili aiuze wakati ilikuwa ya kutoa bure. UKISOMA KITABU HIKI, UKILINGANISHA NA TANZANIA YETU, IMESADIFU MBAYA. Ni kipengele kimoja tu cjajua km wamama wa kitanzania wako wa hvyo kwamba; mke wa fisadi huyo alimwamuru mumewe arudishe pesa yote na ajisalimishe police. I wonder wake wa KAGODA, EPA, MEREMETA wataweza hilo? Kitabu kimeonesha, wanawake wakiamua, wanaweza kukomesha ufisadi. Ebu Tz tujaribu kuwatumia...ila wasiwe km Makinda ya ndege...eeh jama!

hivi hiki ndo kile kitabu kinachomzungumzia adili mtoto fukara na yule dorah mtoto wa mwalimu? Nakumbuka adili alivyobadilika na rushwa...kweli kitabu hiki kinafaa kipelekwe mashuleni! Wanawake kama akina dorah hawapo tena zama hizi.
 
Riwaya iliyonigusa ni KIU YA HAKI.Na nikiiangalia nchi yangu inavyoenda na nikifananisha na hiyo riwaya naona kabisa wa2 walioko selikarini walivyokuwa hawana hata chembe ya ku2pa haki ye2.

wazee kama mzee toboa mambo hawapo tena nchi....!
 
A beatfully once are not yet born.ni riwaya iliyonigusa na kunipa mwangaza kuhusu viongoz we2 kwamba hata kije chama gan, nia yao ni 1, kunyonya,ukandamizaj,uwiz,matumizi mabaya ya vyeo na mal za umma,wizi.
 
Kabwe Makanika, cha Zahir ALLY na Ama Zangu ama Zao cha Hammie Rajab, Kwa miaka ile kabla ya RUNINGA vilikuwa Kiboko.
 
KIBANGA AMPIGA MKOLONI. Moja ya chapter kwenye kitabu cha Jifunze Lugha Yetu,darasa la nne.
 
Kabwe Makanika, cha Zahir ALLY na Ama Zangu ama Zao cha Hammie Rajab, Kwa miaka ile kabla ya RUNINGA vilikuwa Kiboko.

Tunatizama watunzi bingwa wa zamani. Kuna haja ya kuangalia watunzi wapya waliopo sasa wanafanya nini kwa ajili ya vizazi vijvyo. Wengi hawana mwelekeo, hadithi mbovu zisizo na mafunzo waka mwelekeo tofauti na watunzi wa zamani. Hawalingani kabisa, nimesoma riwaya nyingi. Njama Musiba, Zawadi ya ushindi Mtobwa nk..Nawatizama leo wawili au watatu ambao inatakiwa watizamwe kwa darubini kali. Hussen Tuwa, Beka Mfaume na Juma Kidogo. Hivi ni vichwa pekee vyenye uwezo mkubwa wa kufanya yale yaliyofanywa na watunzi wa kale.
 
Vipi kuhusu Amri Bawji na Eddie Ganzel?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom