Riwaya: Taharuki

gilbert35

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
247
474
SIMULIZI; TAHARURI
Imeandikwa na Halfani Sudy
Whatsapp; 0652212391

Hii ni Sehemu ya Kwanza

Kwa mara ya tatu sasa simu ya Catherine iliyokuwa imelala pweke juu ya kitanda chake ilikuwa inaita. Simu iliita kwa mara nyingine tena mpaka ikakatika, hakukuwa na mpokeaji wa simu ile.

Catherine, alikuwa yupo bafuni mwake, akiipitisha taratibu sabuni yenye manukato mazuri katika mwili wake wa kirembo. Sabuni ilikuwa ikipitishwa na mkono laini maeneo mbalimbali ya mwili huo, huku ikiacha povu lililoambatana na harufu nzuri sana. Hakuwa na haraka, na hii ilikuwa ni kawaida yake siku zote akiingia bafuni.

Alikuwa anatumia zaidi ya dakika arobaini ili kuhakikisha mwili wake mzuri umetakata vilivyo. Baada ya kuhakikisha zoezi lake la kuutakatisha mwili wake kukamilika, alifungulia tena bomba la maji, maji yalikuwa yanatiririka kutokea juu mithili ya mvua za rasharasha, maji yaliyopata bahati ya kudondokea juu ya mwili mzuri sana wa Catherine.

Catherine Simon Madoshi, alikuwa ni msichana mwenye umri wa miaka ishirini na moja. Alikuwa na urefu wa wastani, urefu uliopata bahati ya kuvikwa katika mwili mzuri sana. Alikuwa ni kati ya wasichana wachache tunaoweza kusema kuwa walibarikiwa na Muumba.

Alikuwa na uzuri wa umbo, sura na sauti. Ungelipata bahati ya kumuona ungeliweza sema kuwa kama alipata bahati ya kujichagulia jinsi alivyotaka awe kwa Muumba.

Katika umri huo mdogo, Catherine alikuwa anamiliki maduka matatu makubwa ya nguo za kike, huku brand yake ya Cathy Clothing Line ikiwa inakuwa kwa kasi kubwa sana nchini Tanzania. Catherine, alikuwa ameingia mkataba na msanii maarufu sana wa kike, ambaye alimsaidia sana kuipaisha brand yake ya nguo za kike. Huku Cathirine mwenyewe, akiwa ni mwanamitindo aliyeibuka ghafla na moja kwa moja kukimbilia katika kilele cha uanamitindo.

Wiki moja iliyopita, alikuwa ametoka kukabidhiwa taji kubwa sana la uanamitindo wa Afrika, nchini Afrika ya Kusini. Baada ya kulitwaa taji hilo, jina la Catherine lilipaa mithili ya tiara, na kujaa katika kila mdomo wa mtanzania mpenda mitindo. Catherine ilikuwa ni nyota mpya iliyong’ara katikati ya mzimu wa kushindwa kwa nchi ya Tanzania katika mashindano mbalimbali ya urembo na ulimbwende.

Catherine alitoka bafuni baada ya kumaliza kuoga, akiwa amejifunga kwa taulo jeupe lililopita juu kidogo ya matiti yake madogo. Alifungua mlango wa bafu na kutokea chumbani kwake. Moja kwa moja alielekea mbele ya kabati lake lililokuwa na kioo kikubwa. Macho yake yalikuwa yanautazama mwili wake mzuri kiooni.

Alidumu akijitazama kwa dakika zipatazo tano, kisha alitabasamu mwenyewe, tabasamu ambalo lililoongeza urembo wake maradufu. Alilitoa taulo lake mwilini na kulitupia juu ya sofa pekee lililokuwemo mle ndani. Sasa alibaki mtupu, mwili wake laini usio na doa hata la bahati mbaya ukiwa mbele ya kioo.

Alichukua kopo la mafuta, akalifungua, kisha akatosa kidole chake cha shahada. Kidole kikiwa kinazama taratibu katikati ya mafuta ndipo simu yake iliita tena. Catherine alikitoa kidole katika mafuta na kugeuka nyuma, alielekea mahali kilipo kitanda.

Aliichukua simu yake kwa mkono wa kushoto, alisoma jina la mtu aliyekuwa anapiga,
“Sweetheart..,” alisema kwa sauti ndogo, kisha akaipokea.
“Habari za sahivi mpenzi,” Catherine alisema kwa sauti yake laini ya kudeka baada ya kupokea simu.
“Unaongea na Sauti Simuni, tunamshikilia mpenzi wako, utafuata maelekezo yetu kama unapenda kumwona jamaa yako akiendelea kupumua!”

Sauti kavu, ya kiume ilisema simuni bila ya wasiwasi wowote ule.
Mstuko uliompata Catherine ulikuwa hauna mfano. Alibaki ameganda kama sanamu akiwa mtupu chumbani, mkono wake wa kushoto ukiwa vilevile sikioni, kilichoongezeka ni majimaji laini yakiyoshuka katika mashavu yake, Catherine alikuwa analia.

“Hallo, hallo, bila shaka unanisikia, tutakupa maelelekezo ya nini cha kufanya baada ya dakika tano. Usijaribu kumwambia mtu yeyote juu ya jambo hili, tunaifatilia kila hatua yako.” Simu ikakatwa.

Catherine alibaki kimya, mkono wake wenye simu bado ukiwa sikioni. Lakini ubongo wake ulisafiri mbali sana, aliikumbuka siku ya kwanza aliyokutana na Martin Mbaga.

Sherehe ilikuwa inakaribia kufika tamati. Waalikwa na wageni mbalimbali walikunywa, kula na kusaza, lakini bado vyakula na vinywaji vilibaki vingi sana. Ilikuwa ni katika sherehe ya harusi kubwa sana jijini Dar es salaam. Tajiri namba moja nchini Tanzania, Bilionea Khatibu Zawiya alikuwa anamuoa mtoto wa kike wa waziri wa mambo ya ndani, mheshimiwa Almas Fumbo. Harusi iliyolitikisa jiji la Dar es salaam kwa takribani miezi mitatu leo hii ilikuwa inafikia tamati.

Ndani ya ukumbi kulijaa watu wengi wenye nyadhifa mbalimbali. Kulikuwa na wanasiasa wakubwa sana, wafanyabiashara matajiri na watu maarufu mbalimbali. Miongoni mwa watu maarufu waliopata bahati ya kualikwa katika sherehe hiyo ni Catherine, ikiwa ni wiki moja tu tangu atoke kutunukiwa taji la Mwanamitindo bora wa Afrika.

Catherine alikuwa amekaa upande wa kushoto wa ukumbi wa Mlimani city, sehemu ambayo kulikuwa na watu maarufu mbalimbali, kulikuwa na wanamuziki wakubwa, wachezaji wa mpira wa miguu maarufu na waigizaji mbalimbali wa filamu waliokuwa wanatamba katika kurasa za mbele za magazeti. Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwake kukaa karibu na watu ambao hakuwahi hata kuwaza kama ipo siku atakaa karibu nao kwa kiasi hicho. Mmoja wa watu hao, alikuwepo Martin Mbaga....

Catherine aligutushwa kutoka mawazoni baada ya simu yake kuita, simu iliyokuwa bado imeganda katika sikio lake tangu alivyotoka kuongea na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Sauti Simuni. Aliangalia mtu aliyekuwa anapiga simu ile, ilikuwa ni namba ileile ya Martin. Hofu ilimpanda marudufu, alishuhudia jinsi vidole vyake mwenyewe vilivyokuwa vinatetemeka, huku vikiwa vimeloa jasho. Hali hii ilikuwa inamtokea mara zote anapopatwa na hali ya uwoga kupitiliza.

Aliipokea,
“Ninashukuru sana kwa kufata maelekezo yetu ya kutomwambia mtu yeyote kuhusu simu yangu. Sasa unachotakiwa kufanya ili kuokoa maisha ya mpenzi wako, kwanza vaa nguo zako..” Kauli hii ilimstua sana Catherine, “Inamaana ananiona?” alijiuliza kwa sauti ndogo iliyosikiwa na sikio la Sauti Simuni.

“Hiyo sio kazi yako kujua, nimekwambia fuata maelekezo yangu. Vaa nguo zako zile ulizovaa katika sherehe ya harusi ya Bilionea Khatibu Zawia. Acha simu juu ya kitanda chako. Utatoka nje ya geti lako, utakuta gari ndogo nyekundu imepaki upande wa pili wa barabara, utaenda kupanda katika mlango wa kati. Ukiingia tu gari itaondoka, hutakiwi kuongea kitu chochote kile na dereva wa gari hilo.

Dereva atakupeleka hadi katika nyumba moja, utashuka na kuingia ndani ya nyumba hiyo, katika eneo la maegesho la magari utamkuta kijana mmoja atakayekuwa amevaa kanzu nyeupe na barghashia, utamwambia,
“ Nimefuata mzigo”.

Huyo kijana ataingia ndani na kutoka na begi jeusi. Utachukua begi hilo na kutoka nalo nje. Utakuta gari ya bluu imepaki upande wa pili wa barabara, utaenda kuingia katika mlango wa kati wa gari hilo. Gari itakupeleka hadi uwanja wa ndege, dereva wa hilo gari atakupa nakala zote unazotakiwa kuwa nazo unaposafiri.

Utapanda ndege inayoelekea jijini Nairobi saa mbili asubuhi. Ukifika katika uwanja wa ndege wa Nairobi, kuna mtu atakupokea, atakuwa amevaa fulana nyeupe, kwa mbele imeandikwa kwa maandishi meusi ‘OCAFONA’, utampa hilo begi baada ya kuingia ndani ya gari lake atakalokuja nalo uwanjani, kisha yeye atakupa nakala zote za kukuwezesha kurudi jijini Dar es salaam.

Ukifika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, utapokelewa na mpenzi wako Martin. Na hapo ndipo utakuwa umeokoa maisha ya mpenzi wako. Kumbuka, tutakuwa tunakufatilia katika kila hatua utakayokanyaga. Katika safari hiyo utakuwa karibu na kifo kuliko wakati wowote ule katika maisha yako. Kosa moja tu, liwe la kukusudia ama la bahati mbaya litakupeleka kuzimu! Nakutakia kazi njema mrembo wangu.....” Simu ikakatwa.

Catherine alipumua kwa nguvu, kichwa chake kilikuwa kina mambo mengi sana ya kufikiria, lakini hakukuwa na muda huo wa kufikiria. Ilimpasa kutekeleza maagizo kwa ajili ya maisha yake, kwa ajili ya kumuokoa mpenzi wake.

Je nini kitatokea? Huu ni mwanzo wa TAHARUKI kutoka kwa mwandishi Halfani Sudy. Like na comment
CapaEbook_3cee8ae8-c59a-4bb2-8cd6-e8d13dfeb724.jpg


Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
HALFANI SUDY anaandika TAHARUKI

Whatsapp 0652 212391

Hii ni sehemu ya Pili

Catherine alipumua kwa nguvu, kichwa chake kilikuwa kina mambo mengi sana ya kufikiria, lakini hakukuwa na muda huo wa kufikiria. Ilimpasa kutekeleza maagizo kwa ajili ya maisha yake, kwa ajili ya kumuokoa mpenzi wake
Alisogea katika kabati lake la kisasa la nguo lilikuwa konani mwa chumba chake. Alifungua mlango wa kushoto wa kabati hilo, alitazamana na nguo nyingi sana, kwa pupa alianza kuisaka nguo aliyoivaa katika sherehe ya harusi ya Bilionea Khatibu Zawia. Akaiona. Ilikuwa ni gauni ndefu ya rangi ya njano, iliyonakshiwa kwa rangi ya dhahabu kuzunguka maeneo ya shingo na kwenye pindo za mikono. Aliivaa. Miguuni alivaa viatu visivyo virefu vya rangi ya dhahabu pia, harakaharaka alitoka nje kufuata maagizo.
Upande wa pili wa barabara aliliona gari aliloambiwa na Sauti Simuni. Ilikuwa ni gari ndogo nyekundu, aina ya Starlet. Kwa mwendo wa uwoga, huku akionekana kuwa amejawa na hofu tele, alielekea katika lile gari. Alipolifikia, alisimama kwa sekunde kadhaa kabla hajashika kitasa cha mlango wa kati wa ile gari, akaufungua, nao bila hiyana ukafunguka. Bila ya kufikiria, alijitosa ndani ya ile gari na kuufunga mlango. Moja kwa moja aliyaelekeza macho yake mbele, alichobahatika kukiona ni kofia kubwa la pama, la rangi nyeusi likifunika kichwa cha dereva wa ile gari, pamoja na koti kubwa jeusi likifunika mgongo wa yule dereva. Dereva aling’oa gari sekunde ya nne baada ya Catherine kujitosa mle ndani.
Ilikuwa ni safari ya kimyakimya, huku Catherine akilikumbuka vizuri onyo alilopewa na Sauti Simuni...
” .......Ukiingia tu gari itaondoka, hutakiwi kuongea kitu chochote kile na dereva wa gari hilo.......”
Alichoweza kufanya Catherine, ni kuzungusha tu macho yake mle garini, huku mara chache akiichungulia mitaa ya jiji la Dar es salaam. Walikuwa wanapita katika barabara inayoelekea Kawe.
Gari ilitembea kwa takribani dakika arobaini na saba, ndipo kwa mara ya kwanza alibahatika kuisikia sauti ya yule dereva mwenye kofia ya pama nyeusi na mgongo uliovaa koti.
“Inama chini ya siti..” Ilikuwa ni sauti ya taratibu lakini iliyoonesha hali ya mamlaka ndani yake.
Catherine aliitii ile sauti, alikilaza kichwa chake katikati ya mapaja yake. Sasa hakuwa na ruhusa ya kuona kitu chochote kile kikichoendelea mle ndani ya gari, ama katika mitaa ya jiji la Dar es salaam akiyoiangalia mwanzoni. Safari iliendelea, na alidumu katika hali hiyo kwa dakika arobaini, ndipo gari lilisimama. Catherine akajua amefika mahali alipotakiwa kushuka, aliinuka na kufungua mlango huku maagizo ya sauti ya Simu Simuni yakimrejea kichwani mwake.
“.............Ukiingia tu gari itaondoka, hutakiwi kuongea kitu chochote kile na dereva wa gari hilo. Dereva atakupeleka hadi katika nyumba moja, utashuka na kuingia ndani ya nyumba hiyo, katika eneo la maegesho la magari utamkuta kijana mmoja atakayekuwa amevaa kanzu nyeupe na barghashia, utamwambia,
‘Nimefuata mzigo’.
Huyo kijana ataingia ndani na kutoka na begi jeusi. Utachukua begi hilo na kutoka nalo nje.......”
Catherine alienda moja kwa moja kwenye eneo la maegesho ya magari. Kulikuwa na magari saba ya kifahari yakiwa yamejipanga. Alijaribu kuangalia ‘plate number’ za yale magari, zote hazikuwa nazo. Alipolikaribia gari la sita, ndipo mbele yake alipokutana na kijana mmoja aliyekuwa amevaa kanzu nyeupe, na kofia aina ya barghashia kichwani.
“Nimefuata mzigo” Catherine alisema bila ya salamu.
Yule kijana alimwangalia Catherine kwa sekunde tatu, kisha aliingia ndani na kutoka na begi dogo la rangi nyeusi, akamkabidhi Catherine. Catherine alitoka nje ya nyumba akiwa kalishika lile begi mkononi, alivyofungua tu geti, mbele yake , upande wa pili wa barabara alikuwa anatazamana na gari dogo la rangi ya bluu. Kwa mwendo wa haraka alilifuta lile gari, mapigo yake ya moyo yalimpiga kwa nguvu akiwa hajui kwamba alikuwa anafanya jambo sahihi ama la. Alipolikaribia lile gari mlango wa kati ulifunguliwa, aliingia huku akiwa amejawa na uwoga mkubwa sana. Safari ya kuelekea uwanja wa ndege ilianza.
Ndani ya gari kulikuwepo na dereva pekee, ambaye hakujishuhulisha kabisa na Catherine, Catherine naye alitulia kitini akiwa kalikumbatia lile begi jeusi, akiwa hajui kuna nini ndani yake? Safari iliwafikisha hadi katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na baada ya taratibu zote kukamilika, Catherine alipanda ndege ya shirika la ndege la kimataifa la Kenya airways na safari ya kuelekea jijini Nairobi ilianza, hiyo ilikuwa saa mbili kamili asubuhi. Hali ilikuwa ni ya pilikapilika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenya jijini Nairobi. Abria wengi walikuwa katika harakati za kuingia na kutoka katika uwanja huo mkubwa zaidi nchini Kenya. Wafanyakazi waliovaa sare katika uwanja huo walikuwa bize kuhakikisha wanawahudumia wateja wote waliokuwa wanahitaji huduma mbalimbali. Katika dirisha moja kulikuwa na afisa wa kike kutoka katika jeshi la uhamiaji akiwa anamhudumia kijana mmoja wa makamo.
“Unaitwa nani?” Yule mhudumu wa kike aliuliza huku akiziangalia nyaraka alizopewa na yule kijana.
“Naitwa Ombeni Mleli” Yule kijana alijibu huku akimtazama yule afisa wa kike.
“Weka kidole cha mwisho hapo” Afisa uhamiaji alisema huku akimuonesha Ombeni mahali alipotakiwa kuweka kidole chake cha mwisho. Ombeni aliweka, dakika kumi zilitosha kwa Ombeni kukamilisha taratibu zote za kuingia nchini Kenya.
“Karibu sana nchini kwetu” Yule afisa uhamiaji alisema huku akitabasamu.
“Ahsante sana” Ombeni alisema huku akitabasamu.
Alienda mahali alipoweka mizigo yake na kuibeba, alitoka nje ya uwanja wa Jomo Kenyata kutafuta mahali ambapo atapata usafiri wa kumtoa katika maeneo ya uwanja. Moja kwa moja alielekea mahali alipoona teksi nyingi zimeegeshwa, kabla hajafika madereva wawili walimkimbilia huku mmoja akiliwahi begi moja alilokuwa amelishika mkononi. Ombeni hakupinga, aliufuata uelekeo wa yule dereva.
“Karibu sana Nairobi” Dereva alisema walipoingia ndani ya gari.
“Ahsante....” Ombeni alikatisha kuongea baada ya kumwona mtu aliyekuwa mbele ya gari yao.
“Sijui unaelekea wapi bosi?” Dereva aliuliza akiwa tayari ameshawasha gari.
Dereva alipokewa na ukimya, mteja wake alikuwa kimya macho yake yakiwa yameelekea umbali wa kama mita hamsini kutoka mhali walipokuwa.
“Bosi....” Dereva aliita.
Ombeni bado alikuwa kimya.
“Bosi” Safari hii dereva aliita kwa sauti kubwa huku akimtingisha bega Ombeni. Ombeni alistuka huku akisema, “Naomba uifuatilie ile gari nyeusi, kuwa makini sana wasijue kama wanafuatwa”
“Sifanyi hiyo kazi” Dereva alikataa.
“Nitakupa kiasi chochote cha fedha unachokohitaji” Ombeni alisema kwa sauti ya kusisitiza.
“Naitwa Beka!” Dereva alisema kwa sauti kubwa huku akitia gari moto na kuanza kulifuta lile gari aliloelekezwa na Ombeni. Beka aliendesha gari kwa umakini mkubwa sana, akihakikisha dereva aliyekuwa anaendesha lile gari jeusi aliloelekezwa na mteja wake hagundui kama anafuatwa. Safari yao iliishia katika hoteli ya Khweza, hoteli iliyokuwepo katika barabara ya Ngara.
Beka aliegesha gari nje ya hoteli ya Khweza, “Nadhani nimefanya kazi yako kwa umahiri mkubwa, nilipe ujira wangu nirudi uwanja wa ndege”
“Ahsante sana Beka, wewe ni dereva mzuri sana, naahidi kukutumia nikiwa hapa Nairobi, naomba mawasiliano yako” Ombeni alisema huku macho yake yakiwa eneo la maegesho akiliangalia lile gari walilokuwa wanalifatilia. Beka alimtajia namba yake ya simu Ombeni, Ombeni aliiandika namba ya Beka katika simu yake.
“Sijui imegharimu shilingi ngapi?” Ombeni aliuliza.
“Shilingi elfu tatu” Beka alijibu.
Ombeni alitoa pesa katika pochi yake, kisha alishuka garini. “Tutwasiliana” Beka alisema wakati akifunga mlango. Akawasha gari na kuondoka.
Ombeni akiwa na mizigo yake, kwa umakini mkubwa alielekea katika hoteli ya Khweza.
“Martin Mbaga! Alidhani atanikimbia milele? Sasa leo ninaenda kumtia mikononi mwangu, nitakachomfanya leo, bila shaka maiti yake itakuwa ndio maiti iliyouwawa kinyama zaidi katika historia ya dunia!”

Je nini kitatokea katika TAHARUKI, tuwe wote kesho hapahapa...

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
HALAFANI SUDY anaandika TAHARUKI
Whatsapp 0652 212391
Hii ni Sehemu ya Tatu

“Martin Mbaga! Alidhani atanikimbia milele? Sasa leo ninaenda kumtia mikononi mwangu, nitakachomfanya leo, bila shaka maiti yake itakuwa ndio maiti iliyouwawa kinyama zaidi katika historia ya dunia!”
“Habari dada yangu, nahitaji chumba” Ombeni alisema alipofika mapokezi, alikuwa anatazamana na msichana mmoja aliyekuwa amevaa shati jeupe na sketi ya bluu. Nywele zake zilikuwa zimesukwa kwa mtindo wa kisasa ambao uliongezea kitu katika uzuri wake.
“Karibu sana katika hoteli ya Khweza, chumba umepata kaka yangu” Mhudumu wa kike alimjibu Ombeni huku akimwangalia kwa sura yenye tabasamu.
Ombeni aliitikia kwa kutikisa kichwa huku akiikagua kwa macho ile sehemu ya mapokezi.
“Unaitwa nani?” Yule mhudumu aliuliza.
“Ombeni, Ombeni Mleli” Ombeni alisema huku akimwangalia yule mhudumu.
Mhudumu aliinamia tarakilishi yake na kuanza kubofyabofya, ilimchukua kama dakika tano hivi mpaka kukamilisha alichokuwa anakiandika.
“Sunday” Mhudumu aliita akiangalia ulipokuwa mlango wa kioo wa kuingilia mle hotelini. Kijana mmoja alienda, alikuwa amevaa sare za rangi sawa na alizovaa yule mhudumu tofauti tu ilikuwa yeye alikuwa amevaa suruali.
“Mpeleke mteja chumba namba mia mbili na tano” Yule mhudumu alisema huku akimpa Sunday kadi ya kufungulia mlango.
“Karibu sana katika hoteli ya Khweza, nina imani utafurahia huduma zetu” Sunday alisema huku akimsaidia kubeba begi moja Ombeni.
“Ahsante sana kaka” Ombeni alisema huku mawazo yake yakiwa mbali kabisa. Alikuwa anatafuta namna sahihi ya kumwingia Sunday ili apate fununu kuhusu mtu anayeitwa Martin Mbaga, mtu aliyekuwa anamsaka kwa udi na uvumba.
“Kuna wenzangu walikuwa wametangulia, sijui wamepata chumba namba ngapi?” Ombeni alijifanya anajiongelesha mwenyewe walipokuwa katika Kambarau.
“Hao wenzako wamefika sasahivi?” Sunday aliuliza huku akimwangalia Ombeni.
“Ndio, wamefika kama dakika tatu zilizopita” Ombeni alisema huku akimwangalia Sunday kwa siri.
“Ocafona” Sunday alisema kwa sauti ndogo lakini iliyosikiwa vizuri na Ombeni.
“Ocafona?” Ombeni aliuliza kwa sauti kubwa kidogo, mara Kambarau ilisimama kuashiria walikuwa wamefika katika floo waliyoikusudia, mlango ukafunguka, wote wakatoka nje. Baada ya kutoka katika Kambarau, chumba kama namba tatu hivi ndicho kilikuwa chumba namba mia mbili na tano.
“Karibu sana Khweza Hoteli, hii ni kadi ya kufungulia mlango, na hii ni nywila za WIFI” Sunday alisema huku akimkabidhi ile kadi pamoja na nywila.
“Mbona hujaniambia kitu kuhusu Ocafona? Ni kitu gani?” Ombeni aliuliza baada ya kupokea ile kadi na karatasi.
“Si umesema ni wenzako? Sasa kwanini hujui kuhusu Ocafona?” Sunday aliuliza huku akianza kuondoka. Hapo ndipo Ombeni alilitambua kosa alilolifanya, akamwacha Sunday aende zake.
Alifungua mlango kwa kutumia ile kadi maalum ya kufungulia mlango, mlango ulifunguka, alikuwa anaangaliana na chumba kikubwa na kizuri sana, chumba chenye hadhi ya nyota tano. Moja kwa moja aliweka mabegi yake katika kabati maalum, kisha akaenda kukaa kitandani.
“Ama zangu, ama zako Martin Mbaga” Ombeni alisema kwa sauti ndogo huku akinyanyuka kwenda kuwasha runinga, alirudi tena kitandani akiwa ameshika rimoti mkononi. Akajilaza kitandani.

Chumba cha tatu kutoka chumba cha Ombeni Mleli, ndicho kilikuwa chumba ambacho walikuwa wamefikia kina Martin Mbaga. Martin alikuwa amekaa katika kiti akimwangalia mwenzake ambaye alikuwa amekaa kitandani.
“Robby tumeupata mzigo, imekuwa rahisi sana kuusafirisha huu mzigo kwa kumtumia Catherine, bila shaka hali ingekuwa ngumu sana kama tungekuja nao sisi” Martin alisema huku akimwangalia Robby.
“Ni kweli Martin, ingawa mwanzoni sikukubaliana na njia hii ya kumtumia Catherine lakini niseme tu, imefanya kazi vizuri kwa sana. Umaarufu wa Catherine umewazubaisha maafisa wa uwanja wa ndege na kufanya iwe rahisi kwetu kuuingiza huu mzigo.” Robby alikubaliana na Martin.
“Kilichobaki hapa ni kuwasiliana na Bilionea Zawwiya ili tujue tunaupeleka wapi huu mzigo? Bila shaka atafurahi sana akisikia kuwa tumefanikiwa kuuingiza Nairobi huu mzigo” Martin alisema kwa furaha.
“Mpigie tujue nini kinafuata?” Robby alishauri.
Martin alitoa simu yake ya mkononi katika mfuko wa suruali aina ya dengrizi. Akaanza kubofya simu yake na kuanza kuitafuta namba ya Bilionea Zawwiya. Alipoiona alipiga, simu iliita lakini haikupokelewa.
“Hapokei simu” Martin alisema huku akimwangalia Robby pale kitandani.
“Jaribu tena kumpigia” Robby alishauri.
Martin aliufuata ushauri wa Robby, aliipiga tena namba ya Bilionea Zawwiya, safari hii simu yake ilipokelewa.
“Martin” Sauti ya Bilionea Zawwiya ilisikika simuni.
“Habari za sahivi Bosi, nikitaka nikujulishe kuwa mzigo umefika salama Nairobi” Martin alisema simuni.
“Safi sana Martin, nipo kwenye kikao lakini ninakuandikia ujumbe pa kuupeleka huo mzigo. Nitakupigia nitakapomaliza kikao” Bilionea Zawwiya alisema.
“Sawa Bosi” Martin alijibu, kisha alikata simu.
“Amesemaje?” Robby aliuliza baada ya Martin kukata simu.
“Amesema atanitumia ujumbe kunielekeza mahali pa kuupeleka huu mzigo” Martin alijibu. Mara simu yake ikaingia ujumbe.
“Bila shaka utakuwa ni ujumbe wa maelekezo ya kuupeleka mzigo” Martin alisema huku akiufungua ujumbe kutoka kwa Bilionea Zawwiya. Ujumbe ulisomeka...
‘Peleka mzigo katika klabu ya usiku ya New Bamboo saa sita na dakika sita, ipo maeneo ya Eastleigh, ukifika utaulizia mahali ilipo kasino ya Plus ndani ya hiyo klabu, utauweka mzigo katika kifaa cha kuwekea uchafu kilichopo upande wa kushoto wa maliwato ya Kasino, narudia tena usithubutu kuufungua huo mzigo!’

Je nini kitatokea? LAKO JICHO!

Riwaya hii unaweza kuisoma kwa haraka kupitia page yetu ya riwaya pale Facebook. Unaweza kuitafuta kwa kuandika Simulizi Za Gilbert au bofya hapa chini

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
HALFANI SUDY anaandika TAHARUKI
Whatsapp 0652212391

Hii ni sehemu ya Nne.

“Bila shaka utakuwa ni ujumbe wa maelekezo ya kuupeleka mzigo” Martin alisema huku akiufungua ujumbe kutoka kwa Bilionea Zawwiya. Ujumbe ulisomeka...
‘Peleka mzigo katika klabu ya usiku ya New Bamboo saa sita na dakika sita, ipo maeneo ya Eastleigh, ukifika utaulizia mahali ilipo kasino ya Plus ndani ya hiyo klabu, utauweka mzigo katika kifaa cha kuwekea uchafu kilichopo upande wa kushoto wa maliwato ya Kasino, narudia tena usithubutu kuufungua huo mzigo!’
“Leo saa sita usiku tutaupeleka mzigo katika klabu ya usiku ya New Bamboo” Martin alisema huku akiwa anaiangalia simu yake.
“Haaa itakuwaje sasa, mpango si ilitakiwa Catherine akukute uwanja wa ndege akirudi?” Robby aliuliza kwa mshangao.
“Hivyo ndivyo ilivyotakiwa kuwa, lakini ujumbe kutoka kwa Bilionea Zawwiya unasema hivyo, nitatafuta namna nyingine kwa kuwasiliana na Catherine ili nimtoe wasiwasi” Martin alisema.
“Sawa, kwakuwa yatupasa kusubiri hadi saa sita usiku tunaweza kwenda kupata chochote hotelini” Robby alishauri.
“Sawa” Martin alikubali, akalichukua lile begi lilikuwa na mzigo na kulitupia uvunguni mwa kitanda. Walihakikisha kila kitu kipo sawa mle chumbani na kutoka nje.
******
Wakati wakina Martin wakitoka nje, ndio wakati huohuo ambao Ombeni naye alikuwa anatoka nje ya chumba chake ili aanze kumsaka Martin Mbaga mle hotelini. Alifungua mlango wake taratibu, kwa tahadhari kubwa alitoa kidogo kichwa chake na kuangalia upande wa kulia hakukuwa na mtu, wakati anageuka upande wa kushoto ndipo alipomuona, aliwaona Martin na Robby wakitoka katika chumba chao.
“Martin amekwisha” Ombeni alijisemea kwa sauti ndogo.
Bila kuhisi chochote, wakina Martin walielekea katika Kambarau na kushuka chini mahali ulipokuwa mgahawa wa hoteli. Harakaharaka, Ombeni alirudi chumbani kwake, alielekea katika kabati alipoweka mabegi yake, alilifungua begi moja na kutoa kadi bandia ya kufungulia milango, kadi ambayo kwa ukubwa ilikuwa mithili ile ya hoteli ya Khweza, ingawa yake ilikuwa ya rangi nyekundu. Alisimama wima na kujipapasa upande wake wa kulia, bastola yake imara aina ya Enfield revolver ilikuwa imetulia kiunoni. Alitoka nje akiwa ameishika ile kadi yake mkononi, moja kwa moja alielekea katika mlango wa chumba walichotoka wakina Martin, chumba namba mia mbili na tisa.
Aliangalia pande mbili za shoroba, hakukuwa na mtu yeyote, hakukuwa na lolote la kulitilia shaka, akachanja ile kadi yake katika mlango, bila ajizi mlango ukafunga, Ombeni aliingia mle chumbani kwa tahadhari kubwa sana. Sasa alikuwa amesimama katikati ya chumba walichotoka wakina Martin. Alizungusha macho yake mle chumbani mithili ya Kinyonga, akitafuta lolote lile la kumtilia shaka, lakini hakuona lolote lile. Akiwa anatafakari wapi pa kuanzia, ghafla alisikia kelele za mlango ukifunguliwa, kwa kasi ya ajabu aliviringisha mithili ya tairi la gari na kuingia uvunguni mwa kitanda, na dakika hiyohiyo ndipo Robby alikuwa ameingia mle chumbani huku akipiga mluzi. Robby alienda mezani na kuchukua pochi yake ya ngozi iliyokuwa juu ya kitabu kidogo, kisha alitoka nje.
Kule uvunguni Ombeni alikutana na kitu kigumu zaidi mwishoni mwa uvungu, kutokana na giza lilikuwepo kule uvunguni hakujua ni kitu gani, lakini akili yake ilimtuma akichukue kile kitu, alivyotoka uvunguni ndipo alipogundua kuwa lilikuwa ni begi dogo jeusi ambalo hakujua kuna nini ndani yake.
“Bila shaka hili begi halijawekwa humu uvunguni kwa bahati mbaya” Ombeni alijisemea mwenyewe huku akijaribu kufungua zipu ya lile begi, zipu ikafunguka, ndaniye alikutana na kitu kilichoviringishwa katika mfuko wa nailoni wa rangi ya kijani, nao akaufungua, macho yake yalikutana na kamera ndogo nyeusi aina ya Nikon D75000 Dsir.
Harakaharaka aliirudisha kamera katika ule mfuko wa nailoni, akautosa ndani ya begi lake na kutoka nalo nje ya chumba cha kina Martin, akili yake ilimwambia kwamba kuna jambo la siri ndani ya kamera ile, naye alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kulijua jambo hilo, akidhani kwamba pengine ingekuwa silaha ya kumchapia Martin.

Simu ya Martin ilikuwa inaita kwa mara ya tatu sasa, mara mbili za awali ilipokuwa inaita hakuhangaika kuangalia nani alikuwa anapiga. Alikuwa bize akichanganya wali wake na mchuzi wa nyama. Ilivyoita kwa mara ya tatu, Martin alipangusa majimaji katika mikono yake kwa kutumia tishu na kuitoa simu yake huku akionesha sura ya kukereka, hakupenda kupigiwa simu wakati wa kula. Aliishika na kuangalia nani aliyekuwa anampigia? Alibaki ameikodolea macho simu yake akiwa katika mshangao.
“Nani anapiga?” Robby aliuliza huku akichukua nyama katika bakuli kwa kutumia mkono wake wa kulia.
“Bosi” Martin alisema huku akiipokea simu yake.
“Nilikwambia usifungue mzigo Martin, kwanini umekiuka maagizo yangu!” Bila hata ya salamu, sauti ya ukali kutoka kwa Bilionea Zawwiya ilisikika baada ya Martin kupokea simu.
“Sijafungua mzigo Bosi” Martin alisema kwa sauti iliyoambatana na uwoga, kengele ya hatari iligonga kwa nguvu sana kichwani kwake.
“SITAKI UTANI KATIKA KAZI!” Bilionea Zawwiya alisema kwa nguvu na kukata simu.
“Twende chumbani” Martin alisema huku akinyanyuka kwa kasi na kukimbilia ndani, Robby naye alifuata nyuma, mkukumkuku walielekea chumbani kwao. Walishuka katika Kambarau na kuelekea katika chumba chao. Harakaharaka Robby alichanja mlangoni kwa kutumia kadi maalum ya kufungulia mlango, mlango ukafunguka, walipoingia tu, moja kwa moja Martin alizama uvunguni kwa mtindo wa ajabu. Baada ya sekunde hamsini alitoka huku akiwa amekata tamaa.
“Mzigo umechukuliwa Robby” Martin alisema kwa huzuni huku akimsogelea Robby.
Ombeni ameshaufungua mzigo wa siri, atakutana na nini ndani yake? Je kina Martin watajua aliyechukua mzigo? LAKO JICHO.


Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
RIWAYA: TAHARUKI
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU: 0652 212391

Hii ni Sehemu ya Tano

“SITAKI UTANI KATIKA KAZI!” Bilionea Zawwiya alisema kwa nguvu na kukata simu.
“Twende chumbani” Martin alisema huku akinyanyuka kwa kasi na kukimbilia ndani, Robby naye alifuata nyuma, mkukumkuku walielekea chumbani kwao. Walishuka katika Kambarau na kuelekea katika chumba chao. Harakaharaka Robby alichanja mlangoni kwa kutumia kadi maalum ya kufungulia mlango, mlango ukafunguka, walipoingia tu, moja kwa moja Martin alizama uvunguni kwa mtindo wa ajabu. Baada ya sekunde hamsini alitoka huku akiwa amekata tamaa.
“Mzigo umechukuliwa Robby” Martin alisema kwa huzuni huku akimsogelea Robby.
“Haupo? Nani kachukua mzigo?” Robby aliuliza kibwege.
“Robby, wewe ndiye mtu wa mwisho kuingia humu ndani baada ya kuwa tumesahau pochi yenye hela ya kwenda kulipia kule mgahawani. Robby! Naomba uniambie wapi umeupeleka mzigo?” Martin alisema kwa nguvu huku akimtolea macho Robby.
“Martin, naapa sijauchukua mzigo, nilikuja humu chumbani, nikachukua pochi iliyokuwa juu ya meza na kuondoka, sijauchukua mzigo” Robby alisema huku akirudi kinyumenyume kumkwepa Martin.
“Nani sasa kauchukua ule mzigo ikiwa wewe pekee ndiye mwenye kadi ya kuingilia humu ndani? Na ni wewe pia ndiye mtu wa mwisho kuingia humu ndani. Sasa ni nani aliyechukua mzigo kama si wewe!” Martin alisema huku kwa mikono yake miwili akizishika kola za shati la Robby.
“Nipe sikio lako Martin na ninaomba niamini Martin, siwezi kukuzunguka hata siku moja, ni mimi ndiye niliyekuingiza katika kazi hii, kwahiyo ninaijua thamani ya hii kazi, siwezi kuipoteza imani ya Bilionea Zawwiya kwetu, siwezi kuzikwepa milioni za Bilionea Zawwiya kirahisi hivyo. Imani yangu ni kwamba kuna mtu katuzunguka, na lazima tumsake mtu huyo kwa namna yoyote ile” Robby alisema kwa hisia kali sana.
Martin alimwachia Robby, alirudi kinyumenyume na kujitupa kitandani. Akalala chali.
“Nimekwisha” Martin alisema kwa sauti ndogo.
“Huu sio muda wa kukata tamaa Martin, ni muda sahihi wa kumsaka mtu ambaye ameingia humu chumbani na kuuchukua mzigo.” Robby alisema huku akisogea pale kitandani alipokuwa amekaa Martin.
“Sina wa.....” Wakati Martin akianza kuelezea simu yake iliita, harakaharaka aliitoa simu yake mfukoni, kama alivyokuwa amehisi, simu ilipigwa na Bilionea Zawwiya.
“Martin, wataalam wangu wa teknolojia wamechunguza na kupata jibu. Wamegundua kwamba mzigo upo katika chumba namba mia mbili na tano katika hoteli mliyopo, tumia nguvu na akili zako zote kuhakikisha unaupata huo mzigo, ni muhimu sana” Balozi Zawwiya alisema kwenye simu.
“Sawa Bosi, nafanyia kazi hilo...” Martin alisema harakaharaka na kukata simu.
“Robby, mzigo upo chumba namba mia mbili na tano, tujiandae tukavamie chumba hicho, lazima tuhakikishe tunaupata” Martin alisema huku nguvu zikiwa zimemrejea.
“Atajuta huyo mtu au watu waliojaribu kuingilia anga zetu” Robby alisema huku akiichomoa bastola katika upande wake wa kulia wa kiuno, Martin naye akajipapasa kiunoni, bastola yake ilikuwepo. Hakuitoa.
“Tunaenda kuvamia chumba namba mia mbili na tano” Martin alisema huku akielekea mlangoni, Robby naye alifuata kwa nyuma.
Dakika mbili baadae walifika katika mlango wa chumba namba mia mbili na tano, Martin aligonga mlango kwa kutumia mdomo wa bastola aliyokuwa ameitoa kiunoni, ulipokelewa na ukimya. Aligonga tena kwa nguvu zaidi ya awali, bado ilikuwa kimya,
“Tunafanyaje kuingia humu ndani?” Martin alimuuliza Robby ambaye alikuwa ameshika bastola kwa mikono yake miwili akiielekeza pale mlangoni.
“Jaribu kugonga tena” Robby alishauri.
“Hodiiii...” Safari hii Martin aligonga huku akiita kwa nguvu, bado ilikuwa kimya, mlango haukufunguliwa.
“Hebu sogea nikuoneshe” Robby alisema huku akiusogelea mlango, Martin alisogea pembeni kuona mwenzie alikuwa anataka kufanya nini? Robby alijipekua katika mfuko wake wa nyuma na kutoa vyuma vidogo viwili. Akaanza kucheza na mlango wa chumba namba mia mbili na tano, ilimchukua dakika zipatazo tatu pale mlangoni, akausukuma mlango, ukafunguka.
“Una akili sana Robby” Martin alisema huku akitabasamu, kwa umakini mkubwa waliingia mle chumbani, bastola zao zikitangulia mbele ya vifua vyao.
Ndani ya chumba walipokewa na utulivu mkubwa, ilikuwa chumba mithili hakijawahi kukaliwa na mtu tangu hoteli ifunguliwe. Kwa umakini mkubwa wakaanza kupekua kila mahali mle chumbani. Sauti ya Bilionea Zawwiya ilipita tena kichwani kwa Martin, kwamba Mzigo wao ulikuwa mle ndani. Hii iliongeza juhudi na umakini kwa Martin.
“Huu hapa mzigo” Martin aliisikia sauti ya Robby ikitokea maliwatoni. Kwa kasi Martin alikimbilia kule maliwatoni, alimkuta Robby akiwa amepanda juu ya sinki akiwa kashika begi dogo jeusi.
“Umeukuta wapi?” Martin aliuliza akiwa kasimama katikati ya mlango.
“Aliuficha juu ya dari” Robby alisema akishuka juu ya sinki.
“Ni nani aliyekuja kuuiba huu mzigo kule chumbani kwetu? Na aliingiaje mle chumbani? Anapaswa kulipwa stahiki yake kwa hiki alichokifanya, lazima tuchunguze nani kapanga katika chumba hiki?” Martin alisema huku sauti yake ikionesha kwamba alikuwa amepandwa na hasira,
Martin akatoa mfukoni kinasa sauti na kukiweka chini ya meza. Wakatoka mle ndani wakiacha kila kitu kipo kama walivyokikuta. Walipofika chumbani Martin alimpigia Bilionea Zawwiya.
“Bosi tumefanikiwa kuupata mzigo” Martin alisema baada ya salamu.
“Safi sana Martin, je mmempata huyo mtu aliyejaribu kuuiba mzigo?” Bilionea Zawwiya aliuliza.
“Tumeingia katika chumba ulichotuelekeza lakini hakukuwa na mtu, tumeacha kinasa sauti ili tunase kila kitu kwa atakayeingia mle ndani. Niseme tu huyo mtu kakitafuta kifo chake kwa nguvu!” Martin alisema kwa hasira.
“Martin ninakuamini sana, sijategemea kama utafanya kosa la kizembe kama ulilolifanya leo. Sitegemei hii kutokea tena kwako, sasa peleka mzigo kama nilivyokuelekeza awali. Sitegemei ufanye kosa lengine tena, kosa lengine lolote, hata liwe dogo kiasi gani linamaanisha kifo chako! Nitakuuwa kwa mkono wangu!” Bilionea Zawwiya alisema kwa hasira na kukata simu.
Martin alipumua kwa nguvu, alikuwa anaielewa maana ya kauli ya Bilionea Zawwiya, kama akifanya kosa lengine basi angeuliwa kweli.

Je nini kitatokea? LAKO JICHO!

Note: Hakuna kitu kizuri kama sapoti kutoka kwa wasomaji. Ukimaliza kuisoma Sehemu ya tano ya riwaya hii tuachie maoni yako hapa. Maoni yanaleta motisha kwa mwandishi, acha kusoma bila kulike na kutoa maoni. Au tuikatishe?
Tukutane Tena Kesho

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Weka vitu mzee tukielewa ndo uanze kusuasua
Sasa hata haijaeleweka unaanza kulalama kwanza huwa haumalizi riwaya usitusumbue
 
RIWAYA: TAHARUKI
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0652212391

Hii ni Sehemu ya Sita

“Wamenidanganya, wale watu wamenidanganya, Sauti Simuni amenidanganya, mbona sijamkuta kipenzi changu pale uwanja wa ndege kama walivyoniahidi?” Catherine alikuwa anawaza akiwa amekaa juu ya kitanda chake.
Ilikuwa zimepita saa kadhaa tangu Catherine arudi kutoka jijini Nairobi nchini Kenya alipoenda kupeleka Mzigo asioufahamu ndani yake kuna nini? Aliufikisha salama mzigo jijini Nairobi kwa mtu aliyekuwa amevaa fulana lenye maandishi ya Ocafona. Na huyo mtu alimsaidia kumpa nyaraka ambazo zilimuwezesha kurudi jijini Dar es salaam, lakini cha kushangaza alipofika katika uwanja wa ndege hakumkuta mpenzi wake kama alivyoahidiwa na Sauti Simuni.
“Lazima nifanye kitu kuhakikisha ninamwokoa Martin, nipo tayari kwenda popote pale, nipo tayari kutumia hadi shilingi yangu ya mwisho kuhakikisha ninampata mpenzi wangu Martin” Catherine alikuwa anawaza peke yake. Akachukua simu yake na kuangalia orodha ya majina, aliliona jina alilokuwa analitafuta, ‘Gabriel Thomas, akaipiga namba ya Gabriel.
“Hallo mrembo? Mbona usiku sana, kuna tatizo?” Sauti ya Gabriel ilisikika simuni ikiuliza maswali mfululizo huku ikiwa imeambatana na uwoga.
“Gabriel upo wapi? Nina shida kubwa sana ninaomba unisaidie” Catherine aliongea kwa sauti ya kulalamika.
“Catherine, una shida gani usiku huu?” Gabriel aliuliza kwa sauti ya uwoga.
“Sio suala la kuongelea kwenye simu, niambie wapi ulipo nije nikueleze”
“Unajua ni usiku sana sasa hivi. Ni hatari kwa mtoto wa kike kutembea peke yako usiku kama huu, niambie wewe wapi ulipo nije”
“Nipo nyumbani”
“Sawa, nipo njiani, nitakuwa kwako baada ya saa moja”
“Ahsante sana Gabriel, ninashukuru sana kwa moyo wako” Catherine alisema huku sauti yake ikirejewa na matumaini.
Saa sita na dakika sita usiku mlango wa geti la nyumba ya Catherine uligongwa, Catherine alienda kufungua akijua kuwa aliyekuwa nje alikuwa ni Gabriel, kwa maana waliwasiliana na kumwambia kwamba alikuwa amekaribia nyumbani kwake.
“Karibu sana Gabriel” Catherine alisema baada ya kufungua mlango.
“Ahsante Catherine, simu yako ya usiku imenitisha sana, kuna tatizo gani?” Gabriel aliuliza.
“Karibu kwanza ndani Gabriel, nitakuhadithia kila kitu” Catherine alisema huku akiushika mkono wa Gabriel na kuingia naye ndani. Walienda kukaa sebuleni, katika makochi mawili yaliyokuwa yanatazamana.
“Gabriel, samahani sana kwa simu ya usiku, najua nimekatisha usingizi wako, naomba unisamehe kwa hilo” Catherine alimuomba samahani Gabriel, kisha alimueleza kila kitu kuhusu ile simu ya Sauti Simuni na yote yaliyotokea mpaka alivyoenda jijini Nairobi na kurudi.
“Pole sana Catherine, umepita katika njia ngumu sana ambayo hata siku moja sikudhani kama unaweza kuipitia, pole sana kwa kumpoteza shemeji, lakini mimi ninakuahidi kwamba nipo tayari kuhakikisha shemeji anapatikana kwa njia yoyote ile, lakini kabla sijakushauri naomba nikuulize wewe ulikuwa unafikiria kufanya nini?” Gabriel alimpa pole Catherine na kumuuliza swali.
“Nimewaza na kuwazua, nina saa zaidi ya tano nikiwaza juu ya jambo hili lakini sijapata majawabu, ndio maana nimekuita wewe unisaidie cha kufanya, nilikuwa nawaza kwenda kutoa taarifa Polisi lakini nikikumbuka Sauti Simuni alivyonionya ninahofia sana maisha ya Martin”
“Upo sahihi Catherine, hili suala tukilipeleka Polisi tutamweka katika hali ya hatari zaidi Martin, lazima tufanye kitu ambacho kitalinda usalama wa Martin pia” Gabriel alisema.
Catherine alikuwa anamwangalia Gabriel, “Gabriel......” Catherine alitaka kuongea lakini alikatikatishwa na Gabriel.
“Mimi ninafikiria tutafute mpelelezi wa kujitegemea, yeye ndiye atatupeleka mahali alipo Martin” Gabriel alilitoa wazo lake.
“Mpelelezi wa kujitegemea..” Catherine alisema kwa sauti ndogo.
“Ndio, lazima tutafute mpelelezi mahiri wa kujitegemea na tumkabidhi suala hili, sisi hapa hatuna ujuzi wowote katika masuala ya uchunguzi, hivyo nafikiri tukimpata mpelelezi wa kujitegemea bila shaka atatupeleka kwenye majibu juu ya mahali alipo Martin” Gabriel alieleza kwa kirefu.
“Nashukuru sana Gabriel kwa mawazo yako, ndio maana nikakufikiria wewe katika marafiki zangu wote, ila sasa tatizo linakuja ni mpelelezi gani wa kujitegemea tutamtumia katika kazi yetu, na wapi tutampata huyo mpelelezi wa kujitegemea?” Catherine aliuliza swali.
“Daniel, lazima asubuhi twende katika ofisi ya Daniel Mwaseba, ni yeye ndiye atatupeleka mahali na sababu ya kutekwa Martin na hao watekaji” Gabriel alisema kwa kujiamini.

Gabriel anamshauri Catherine wamtafute Daniel Mwaseba kuwasaidia kumtafuta Martin, je nini kitatokea? LAKO JICHO!

Kama kawaida, sapoti ni muhimu sana baada ya kusoma. Like na toa maoni yako, pia share iwafikie marafiki zako ikiwezekana.

#SimuliziZaGilbert #HalfaniSudy

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
RIWAYA; TAHARUKI
Imeandikwa na Halfani Sudy
Simu 0652 212391

Hii ni sehemu ya Saba

“Ndio, lazima tutafute mpelelezi mahiri wa kujitegemea na tumkabidhi suala hili, sisi hapa hatuna ujuzi wowote katika masuala ya uchunguzi, hivyo nafikiri tukimpata mpelelezi wa kujitegemea bila shaka atatupeleka kwenye majibu juu ya mahali alipo Martin” Gabriel alieleza kwa kirefu.
“Nashukuru sana Gabriel kwa mawazo yako, ndio maana nikakufikiria wewe katika marafiki zangu wote, ila sasa tatizo linakuja ni mpelelezi gani wa kujitegemea tutamtumia katika kazi yetu, na wapi tutampata huyo mpelelezi wa kujitegemea?” Catherine aliuliza swali.
“Daniel, lazima asubuhi twende katika ofisi ya Daniel Mwaseba, ni yeye ndiye atatupeleka mahali na sababu ya kutekwa Martin na hao watekaji” Gabriel alisema kwa kujiamini.
“Daniel Mwaseba, nimewahi kulisikia mara kadhaa mpelelezi mwenye jina hilo, ni mpelelezi maarufu sana hapa Tanzania, umahiri wake unaimbwa hadi nje ya mipaka yetu, lakini mimi sijui wapi tutampata huyo Daniel, na pia sidhani kama nitaziweza gharama zake”
“Ni kweli, Daniel ni kiboko ya madhalimu, mimi ninaijua mahali ofisi yake ilipo, tutaenda kesho asubuhi, na kuhusu gharama usijali, nitalipia gharama zote za uchunguzi” Gabriel alisema.
“Ninakushukuru sana Gabriel. Wewe ni rafiki wa kweli, wazungu wana msemo wao wanasema ‘a friend in need?”
“ ............is a friend in deed” Gabriel alimalizia.

SURA YA SABA

Saa nane kamili usiku, Hatia na Mtumwa walifika nyumbani kwa Meya wa Kimathi, mtaa wa Kimathi karibu na ofisi za magazeti ya Nation. Meya wa Kimathi alikuwa anaishi kwenye jumba kubwa sana la kifahari, jumba lililozungushwa na kuta nene huku kwa juu zikizungushiwa nyaya za umeme ili kuzuia wezi. Ndani ya kuta kulikuwa na maua mazuri yakiyotunzwa na mtu maalum, huku kwa nyuma kukiwa na bwawa zuri la kuogelea, upande wa kulia wa nyumba kulikuwa na maegesho ya magari iliyojaa magari mengi ya kifahari.
Kwa ndani, nyumba ilikuwa na sebule iliyopaswa kuitwa ya kisasa, ikiwa na kila samani ghali. Kwa kutazama muonekano wa nyumba tu ilikuwa inakuonesha ukwasi wa mtu aliyekuwa anaimiliki nyumba hiyo.
Meya wa Kimathi alikuwa ni mwanaume mwenye umri wa miaka arobaini na sita, mwanaume aliyekuwa anaheshimiwa zaidi jijini Nairobi. Alikuwa na ukwasi ambao aliutumia kusaidia kaya masikini nchini Kenya, hali iliyofanya apendwe na wakenya wengi sana, hasa masikini. Kila mwezi Meya wa Kimathi alikuwa anawapeleka watoto watatu nchini India kwa ajili ya kwenda kugharamia matibabu yao, pia alikuwa anaichangia serikali ya Kenya katika mipango yake mingi ya kimaendeleo, hilo lilifanya aheshimike sana na viongozi wa chama na serikali.
Hakuna aliyekuwa hajawahi kulisikia jina la Meya wa Kimathi nchini Kenya, kama si kwa kumuona ana kwa ana basi kwa kumuona hata katika runinga, jina la Meya wa Kimathi lilikuwa halikauki katika midomo ya wakenya.
Pamoja na yote hayo lakini hakukuwa na mtu aliyekuwa anajua wapi Meya wa Kimathi aliupatia utajiri wake, alikuwa ni tajiri aliyeibuka ghafla mithili ya uyoga pori na kuchanua katikati ya msitu mnene. Leo alikuwa masikini wa kutupwa, kesho akabadilika na kuwa masikini, kisha keshokutwa akabadilika na kuwa tajiri na hatimaye akawa tajiri mkubwa sana. Masikini rafiki yake masikini, tajiri rafiki yake tajiri, na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Meya alikuwa na mrafikii wengi sana nchini Kenya, na utajiri wake ulipoongezeka kwa kasi maradufu akapata marafiki nje ya Kenya, na miongoni mwa marafiki hao ni Bilionea Zawwiya kutoka nchini Tanzania.
Urafiki wa Bilionea Zawwiya na Meya wa Kimathi ulianza siku ile rais wa Tanzania, Mheshimiwa Mark Mwazilindi alivyokuwa na ziara ya kiserikali nchini Kenya. Katika msafara wake aliongozana na Bilionea Zawwiya kama mwakilishi wa wafanyabiashara wa Tanzania, na kwa upande wa rais wa Kenya, aliambatana na Meya wa Kimathi kama mwakilishi wa wafanyabiashara wa Kenya. Urafiki wao ulianzia siku hiyo na kukua kwa kasi ya ajabu. Siku Meya wa Kimathi alipoenda nchini Tanzania kwenye harusi ya mtoto wa Bilionea Zawwiya aliyekuwa anafunga ndoa na mtoto wa waziri wa mambo ya ndani, mheshimiwa Almas Fumbo. Baada ya harusi, walikutana nyumbani kwa Bilionea Zawwiya na kuingia mkataba wa siri kati yao.
“Karibuni sana vijana” Meya wa Kimathi alisema wakati akikaa kwenye sofa.
“Ahsante sana Meya wa Kimathi” Hatia na Mtumwa walijibu kwa pamoja.
“Bila shaka mmeniletea mzigo” Meya wa Kimathi alisema huku akiwaangalia Hatia na Mtumwa kwa zamu.
Mtumwa aliliweka lile begi jeusi katika meza ya kioo iliyokuwa katikati ya sebule, “Huu ndio mzigo uliotuagiza Meya” Hatia alisema huku akimwangalia kwa umakini Mtumwa wakati akiuweka ule mzigo.
Kijana mmoja mfupi aliyekuwa miongoni mwa walinzi wa Meya wa Kimathi aliusogelea ule mzingo, kisha akampa Meya, Meya aliligeuzageuza lile begi kisha akalifungua, akakuta kitu kimeviringishwa katika mfuko wa nailoni, akaufungua nao, mikononi mwake alikuwa ameshika kamera.
“Safi sana vijana” Meya wa Kimathi alisema kwa sauti ndogo lakini iliyosikiwa na kila mtu pale sebuleni.
“Robert, njoo uiangalie hii kamera” Meya wa Kimathi alisema huku akigeuka kwa kijana mwengine aliyekuwa mrefu na mweupe aliyekuwa amesimama nyuma yake. Robert alisogea kwa Meya wa Kimathi na kuichukua ile kamera, aliigeuzageuza huku akitabasamu, aliifungua nyuma ya ile kamera, macho ya Meya wa Kimathi yalikuwa katika uso wa Robert, kila sekunde zilivyokuwa zinasogea ndipo sura ya Robert ilikuwa inabadilika, ilikuwa inatoka kwenye tabasamu kwenda katika mshangao.
“Kadi ya kumbukumbu haipo katika hii kamera!” Robert alisema kwa nguvu huku akimtazama Meya wa Kimathi.
“Unasemaje!” Meya wa Kimathi alisema kwa nguvu huku akiinuka katika kochi alilokuwa amekaa.
“Hakuna kadi katika hii kamera” Robert alisema tena huku akimkabidhi Meya ile kamera.
“Nini kimetokea nyinyi vijana? Mmenichezea mchezo?” Badala ya kuipokea ile kamera, Meya wa Kimathi aliuliza huku akimwangalia Mtumwa.
“Bosi, sisi hatujafanya chochote, tumeileta vilevile kama tulivyoikuta ndani ya ndoo ya takataka” Mtumwa alisema kwa sauti iliyotia huruma, Hatia naye alitikisa kichwa kukubaliana na maneno ya Mtumwa.
“Kuna mtu anahisi katuchezea mchezo, lakini kwangu huyo mtu hajatuchezea mchezo ila kacheza mchezo hatari sana wa kifo, na kwa sasa yupo karibu zaidi na kifo kuliko wakati wowote ule katika maisha yake!” Meya wa Kimathi alisema kwa hasira huku akirusha mikono yake hewani kwa nguvu.
Watu wote pale sebuleni walikuwa kimya, wote walikuwa wanamsikiliza Meya wa Kimathi.

Je nini kitatokea? LAKO JICHO!

Sapoti kidogo katika kutoa maoni na kulike itasababisha mwendelezo uje kwa kuchelewa. Tuandikie maoni yako hapa.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
RIWAYA: TAHARUKI
Imeandikwa na HALFANI SUDY
SIMU 0652 212391

Hii ni Sehemu ya Nane

Daniel Mwaseba alikuwa ofisini kwake, siku hii alifika ofisini mapema zaidi kuliko ilivyo kawaida yake. Akiwa nyuma ya meza, juu yake kulikuwa na mafaili mengi. Mbele ya jalada la faili alilokuwa amelishika kulikuwa na maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa wino mwekundu WIZI WA MADINI YA TANZANITE. Daniel alipitia kurasa moja baada ya nyingine ya faili alilolishika. Faili lilikuwa na kurasa ishirini na moja, lilikuwa ni faili la ripoti ya uchunguzi juu ya wizi mkubwa wa madini ya Tanzanite uliotokea huko Mererani katika wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.
Tanzanite ni kito chenye rangi ya bluu, zambarau na kijani. Kito hicho cha thamani kinapendwa sana na mataifa mbalimbali. Kihistoria, kito hicho kiligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1967 katika milima ya Mererani. Kiligunduliwa na mtanzania aitwaye Jumanne Mhero Ngoma.
Miezi mitatu ulitokea wizi mkubwa sana wa madini ya Tanzanite, kiasi cha karati 1000 zilikuwa zimepotea katika ghala la kuhifadhia madini hayo. Karati moja ya madini hayo inacheza kati ya dola 250 hadi 500 za kimarekani, karati moja ni sawa na milligramu 200.
Faili lililokuwa mikononi mwa Daniel lilikuwa limetoka kwa askari polisi mwenye cheo cha Inspekta, kwa majina alikuwa anaitwa Ombeni Mleli, Ombeni ndiye askari aliyepewa kazi ya kuchunguza juu ya wizi huo mkubwa wa madini kuwahi kutokea nchini Tanzania, lakini hadi sasa alikuwa bado hajafanikiwa kuwatia mikononi wahusika wa wizi huo, kikubwa alichofanikiwa kujua ni uhusika wa kijana anayeitwa Martin Mbaga, ambaye alihangaika kumsaka kwa takribani miezi yote hiyo bila ya mafanikio.
“Martin Mbaga” Daniel alisema kwa sauti ndogo huku akilitupa lile faili juu ya meza. Alitoa simu yake mfukoni na kutafuta katika orodha ya majina, akaliona jina la mtu alilokuwa analitafuta, Hannan Halfani. Alibonyaza kitufe cha kupiga simu, simu ilianza kuita.
“Hallo Daniel” Sauti ya kike ya Hannan ilisikika simuni.
“Habari yako Hannan? Upo wapi?” Daniel alisalimia na kuuliza.
“Nipo njiani ninaendesha, ninaelekea ofisini” Hannan alisema.
“Ok, sasa ukifika ofisini ninaomba unisaidie kunifanyia kazi moja” Daniel alisema.
“Kazi gani Daniel?”
“Ninataka umchunguze mtu anayeitwa Martin Mbaga, ninaomba uniambie kila kitu kinachomhusu” Daniel alimuomba Hannan.
“Sawa Daniel, nitaifanya kazi yako pindi tu nikifika ofisini” Hannan alikubali.
“Nashukuru sana Hannan” Daniel alisema na kukata simu.
Daniel aliweka simu yake ya mkononi juu ya meza, akajiegemeza juu ya meza huku akiwaza.
“Ngoja nione kama Hannan yupo imara kama siku zote, nimempa mtihani sawa na niliompa Inspekta Ombeni...” Akiwa katikati ya mawazo mlango wa ofisi yake uligongwa.
“Ingia....” Daniel alisema huku akiangalia juu ya dari.
“Samahani bosi, kuna wageni wako wanaomba kuonana na wewe” Katibu Muhtasi wa Daniel aliyeitwa Merina alisema huku akiwa amesimama kwa nidhamu.
“Wageni gani hao?” Daniel aliuliza akiwa bado ameangalia darini.
“Mmoja amejitambulisha kwa jina moja tu la Gabriel na mwengine amesema anaitwa Catherine Simon” Katibu Muhtasi alijibu.
“Ok, waambie waingie” Daniel alisema, sasa akiwa anamtazama Merina.
Merina alitoka nje, macho ya Daniel bado yalikuwa yameelekea mlangoni ili kuwaona hao wageni watakaoingia. Dakika moja baadae wageni aliokuwa anawasubiria waliingia. Alianza kuingia mwanaume, kisha akafuatiwa na Catherine, sura zao zikionesha kwamba walikuwa wamezingwa na mawazo.
“Karibuni sana” Daniel alisema akinyanyuka kitini, akawaonesha sehemu ya kukaa kwa mkono wake wa kulia.
“Ahsante sana kaka” Catherine na Gabriel waliitikia kwa pamoja huku wakikaa katika sofa la kukaa watu wawili lililokuwepo mle ndani.
“Karibuni tena, sijui niwasaidie nini?” Daniel alisema huku akiligeuza lile faili lilikuwa limelala pale mezani.
“Kaka Daniel, samahani sana kwa kukuvamia katika ofisi yako bila ya taarifa, kwa majina mimi ninaitwa Gabriel Mwazilindi, ni mtoto wa pili wa rais Mark Mwazilindi, huyu mwenzangu ni Catherine Madoshi, ni mlimbwende na mjasiriamali”
“Karibuni sana, kumbe nimevamiwa na ugeni mkubwa sana, eeh niambie dhumuni la ugeni wenu?” Daniel alisema huku akitabasamu, sura yake ikionesha kwamba alikuwa hawafahamu kabisa kina Gabriel.
“Mimi na Catherine tumesoma shule moja, na kusoma huko pamoja kumetengeneza urafiki mkubwa sana kati yetu. Dhumuni kuu la kuja hapa ni kuhusu Catherine, Catherine ana matatizo ambayo tumeona wewe unaweza kutusaidia, kwa kifupi tu Catherine ana mpenzi wake ambaye ametekwa na watu wasiojulikana....”
“Anaitwa nani huyo mpenzi wa Catherine” Daniel aliuliza kwa sauti ya upole.
“Anaitwa Martin Mbaga” Catherine alidakia kwa sauti ya huzuni.
“Martin Mbaga?” Daniel aliuliza kwa sauti kubwa.
Gabriel na Catherine waliangaliana, “Vipi unamjua Martin?” Catherine aliuliza kwa sauti ya uwoga.
“Naomba uniambie namna Martin alivyotekwa?” Daniel aliuliza bila ya kulijibu swali la Catherine.
Catherine alichukua nafasi kuelezea kila kitu kilivyotokea, tangu alivyopokea simu ya Martin iliyopigwa na Simu Simuni akiwa anatoka bafuni kuoga mpaka safari yake ya kuelekea Nairobi kupeleka mzigo asioufahamu.
“Aisee pole sana Catherine kwa yaliyokukuta. Sasa msaada gani mnaoutaka kutoka kwangu?” Daniel aliuliza huku akiwaamgalia kwa zamu.
“Msaada tunaoutaka kutoka kwako, utusaidie kumuokoa Martin kutoka kwa watekaji, tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha” Gabriel alijibu huku akimwangalia Daniel.
“Nitawasaidia” Daniel alisema kwa sauti ndogo,” Sihitaji kiasi chochote cha fedha kutoka kwenu katika kazi hii” Daniel alisema huku macho yake yakimwangalia Catherine.
“Kweli Daniel? Utatusaidia bila gharama yoyote?” Catherine alisema kwa sauti ya kutoamini maneno ya Daniel.
“Ni dhima yangu kuwasaidia Catherine” Daniel alisema huku akiwaangalia Gabriel na Catherine kwa zamu.
“Daniel tunashukuru sana kwa moyo wako, u kijana mwema kama sifa zako zinavyotangazwa siku zote katika majarida mbalimbali ya kipelelezi, nakuachia namba yangu, tutakuwa tunawasiliana kujua utakuwa umefikia wapi katika suala hili la kuhakikisha Martin anarudi nyumbani kwa Catherine” Gabriel alisema huku akimwangalia Daniel kwa jicho la shukrani.
Baada ya maongezi yaliyodumu kwa takriban dakika kumi na tano, wakina Gabriel waliaga na kuondoka.
“Martin Mbaga, umefanya kazi nzuri sana kijana wangu. Gabriel utakuwa ni ufunguo wetu kumfikia rais Mark Mwazilindi..” Daniel alisema kwa sauti ndogo wakati akilifunua tena faili la wizi wa madini ya Tanzanite, akiwa katika kurasa ya tatu simu yake iliita, ilikuwa simu kutoka kwa Hannan.
“Daniel upo wapi? Ninahitaji kuonana na wewe sasa hivi” Sauti ya Hannan iliongea harakaharaka baada tu ya simu yake kupokelewa na Daniel.
“Kuna nini Hannan?” Daniel aliuliza swali badala ya kueleza mahali alipo.
“Ni kuhusu Martin Mbaga..” Hannan alijibu.
“Kwa sasa nipo ofisini kwangu Hannan, ila ninaomba tukutane katika hoteli ya Sea Don baada ya nusu saa” Daniel alisema huku akinyayuka katika kiti.
“Sawa Daniel” Hannan alijibu na kukata simu.
Daniel alitoka nje ya ofisi, alimuaga Merina. Alienda katika maegesho ya magari, alichukua gari yake na kuelekea katika hoteli ya Sea Don kukutana na Hannan.

Martin na Robby bado walikuwa ndani ya hoteli ya Khweza, katika chumba chao, waliporudi kutoka katika klabu ya usiku ya New Bamboo moja kwa moja walienda kuchunguza katika chumba namba mia mbili na tano, chumba ambacho alichopanga mtu aliyeiba mzigo wao lakini hawakumkuta, walikikuta chumba kikiwa vilevile mithili ya walivyokiacha walipoingia na kuuchukua mzigo. Walipolikosa windo lao ndipo waliporudi chumbani kwao.
“Robby, huyu jamaa katuharibia sana kazi, Bilionea Zawwiya atatulaumu sana kwa uzembe tulioufanya, kiukweli nimeanza kufanya kazi na Bilionea Zawwiya kwa mguu mbaya sana” Martin alisema kwa sauti ya majuto.
“Usujilaumu sana Martin, katika hizi kazi vitu kama hivi hutokea, makosa madogomadogo kama haya sio ya kuyaweka kichwani, lakini pamoja na kukosea kidogo lazima tufanye kitu kurekebisha, lazima tuhakikishe tunamtia katika mikono yetu kikaragosi aliyeingia chumbani kwetu na kujaribu kuuiba ule mzigo, lazima tumuoneshe kwa namna gani alifanya kosa, na hii itatusaidia pia kujua alikuwa na lengo gani mpaka kufikia hatua ya kuuchukua ule mzigo? Imetokea kwa bahati mbaya au alikuwa anatufuatilia?” Robby alisema huku akimwangalia Martin.
“Upo sahihi Robby, lazima tufanye kitu, hadi sasa Mvamizi yupo hatua moja mbele yetu, yeye anatujua sisi na pia pengine anajua ule mzigo ni kitu gani? Haikutakiwa hata kidogo kuwa hivi. Sasa Robby naomba tufanye kitu kimoja, kamuhadae yule dada wa mapokezi, ufanye ufanyavyo urudi na jina la mtu aliyepanga katika chumba namba mia mbili na tano, huo ndio utakuwa mwanzo wa kumjua huyo Kikaragosi na lengo lake” Martin alisema.
“Ok sawa, ngoja niende nikaifanye hiyo kazi” Robby alisema huku akielekea mlangoni.
Alivyotoka Robby, simu ya Marti iliita, alikuwa Bilionea Zawwiya, kwa mara ya kwanza Martin aliipokea simu ya Bilionea Zawwiya akiwa anatetemeka.
“Martin umefanya nini? Mbona umekuwa mzembe kiasi hicho?” Bilionea Zawwiya aliongea kwa sauti ya ukali pindi tu simu yake ilipopokelewa.
“Nimefanya nini Bosi, nimepeleka mzigo sehemu sahihi kama ulivyotuagiza” Martin alisema kwa sauti ya wasiwasi.
“Mzigo haujakamilika Martin!” Bilionea Zawwiya alisema kwa nguvu.
“Mzigo haujakamilika? Mbona sikuelewi Bosi? Sisi hatujaufungua mzigo, na tuliupeleka kama ulivyotupa maelekezo” Martin alisema kwa sauti ndogo.
“Martin umechezewa mchezo, mtu aliyeingia chumbani kwenu na kuuiba mzigo ameufungua, niliweka alamu maalum niliyounganisha na simu yangu ya kunijulisha pindi tu mzigo utakapofunguliwa, na ndio maana nilikupigia simu muda mfupi tu baada ya yeye kuufungua mzigo, pamoja na kuufungua lakini huyo mtu amefanya kitu kibaya zaidi, amechukua kitu muhimu sana katika huo mzigo, na hiko kitu ndio chenye thamani katika ule mzigo kuliko mlichopeleka nyinyi katika klabu ya New Bamboo”
“Mfyuuuuu..” Martin alihema kwa nguvu, mkono wa kulia ulioshika simu ulikuwa unatetemeka kwa hasira.
“Martin, ninakupa saa tano za kuhakikisha unamjua huyo mtu, na hakikisha anakupa kadi ya kamera ambayo ina siri zetu za kule Mererani, tusipoipata hiyo kadi siri zetu zitakuwa barazani kwao” Bilionea Zawwiya alisema na kukata simu bila ya kusubiri majibu ya Martin.
Martin alibaki ameganda kama sanamu, huku mkono wake ulioshika simu ukibaki sikioni, Robby aliingia dakika kumi baadae akimkuta Martin akiwa katika hali hiyo.
“Martin” Robby aliita.
Martin alikuwa kimya, akiwa anaangalia kwa umakini mbele lakini ukweli ni kwamba alikuwa haoni chochote.
“Martin!” Safari hii Robby aliita kwa nguvu zaidi huku akiwa kamsogelea Martin, Martin alikuwa kama katoka kuzinduka katika usingizi mzito.
“Robby, tumekwisha......” Martin alisema kwa sauti ndogo. Robby aliuona uwoga mkubwa sana katika macho na sauti ya Martin, hakuwahi kumuona katika hali hii tangu afahamiane naye siku kadhaa zilizopita, kichwani kwake aliamini kweli walikuwa wameisha.
“Kumetokea nini Martin?” Robby aliuliza kwa sauti ya kufadhaika.
“Amenipigia simu Bosi, kumbe jamaa alifungua mzigo. Ule mzigo ulikuwa ni kamera na jamaa amechukua kadi yenye siri za Mererani, ni nani hasa yule jamaa?” Martin alisema huku akiachia swali kwa Robby.
“Anaitwa Ombeni, Ombeni Mleli” Robby alisema huku neno Mleli akijikuta akilitaja sambamba na Martin.
“Unamfahamu?” Robby aliuliza kwa sauti kubwa.
“Ombeni Mleli ni adui yangu namba moja hapa duniani....” Martin alisema kwa sauti iliyoonesha kuwa ilikuwa na mchanganyiko wa hasira na uwoga kwa pamoja.
“Ni nani huyo jamaa?” Robby aliuliza kwa sauti ndogo.

Je nini kitatokea? LAKO JICHO!

Kama bado hujajiunga na group letu la whatsapp bofya hapa kujiunga

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
RIWAYA; TAHARUKI
Imeandikwa na HALFANI SUDY
Whatsapp 0653 212391

Hii ni Sehemu ya Tisa

“Unamfahamu?” Robby aliuliza kwa sauti kubwa.
“Ombeni Mleli ni adui yangu namba moja hapa duniani....” Martin alisema kwa sauti iliyoonesha kuwa ilikuwa na mchanganyiko wa hasira na uwoga kwa pamoja.
“Ni nani huyo jamaa?” Robby aliuliza kwa sauti ndogo.
Mapenzi huanza kwa namna nyingi sana, kuna wakati mapenzi huanza kwa namna ya kushangaza na ajabu. Mfano ni mapenzi ya Martin na Catherine, yalianza kwa namna hiyo inayoitwa ya ajabu. Ilikuwa ni miezi mitatu tangu Martin amalize mafunzo ya ushushushu huko nchini Urusi. Kwa tafsiri nyepesi ushushushu ni taaluma inayohusu ukusanyaji wa taarifa za kiusalama kwa njia za siri. Maeneo makuu ya kazi za idara ya usalama wa Taifa ni kukusanya na kuchambua habari za kiusalama zinazohusiana na ujasusi, uzandiki, uhujumu na ugaidi. Lakini jukumu la idara hii si kukusanya taarifa hizo tu, bali pia kuzuia matukio hayo yanayofahamika kama matishio ya usalama wa Taifa.
Martin Mbaga alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi aliyefuzu mafunzo hayo magumu kwa uweledi mkubwa. Kutokana na ugumu wa zoezi la kukusanya taarifa za kiusalama ndio maana mashushushu wanapaswa kuwa watu wenye akili isiyo ya kawaida, au wenye wenye uwezo mkubwa sana wa kutumia akili. Kikawaida binadamu anakuwa na milango mitano ya fahamu; pua, mdomo, masikio, macho na ngozi. Lakini Martin alikuwa na mlango wa ziada wa fahamu, hisia, na hii ndio sababu ya watu wanaomfahamu walizoea kumuita kwa jina la Martin Hisia. Baada ya mafunzo ya ushushushu, Martin alirudi nchini huku kichwani kwake akiwa tayari kuitumikia kwa umakini na uweledi mkubwa.
Martin Hisia, kijana barobaro ambaye kwa kipindi hiko alikuwa na umri wa miaka ishirini na sita tu, jumatatu moja alienda ofisini kwa mkuu wake ili kupangiwa majukumu yake ya kazi, huko ndipo alipokutana na Catherine Simon Madoshi.
Catherine alikuwa ni mtoto pekee wa kike wa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Simon Madoshi. Siku hiyo ya jumatatu wakati Martin akitoka ofisini kwa mkuu wake ndipo alipokutana na Catherine wakati akiingia ofisini kwa baba yake. Ilitokea kwa bahati mbaya tu, Martin kumgumia Catherine nje ya mlango ya ofisi ya Luteni Jenerali Madoshi. Neno lilitoka katika mdomo wa Martin ni ‘samahani’ lakini mrejesho wake kutokka kwa Catherine ulikuwa ni tofauti. Kibao cha nguvu kutoka katika mkono wa kulia wa Catherine kilitua katika shavu la upande wa kushoto la Martin. Martin aliganda mithili ya sanamu akiwa haamini kabisa kilichotokea.
“We mwanamke kwanini unanipiga?” Martin aliuliza kwa sauti kavu, lakini hisia zake zikimwambia kwamba kuna kitu kisicho cha kawaida kutoka kwa yule mwanamke.
“Ni Catherine huyo, mtoto wa Luteni Jenerali Madoshi” Kabla Martin hajajibiwa swali lake aliisika sauti kutoka nyuma yao, alikuwa ni katibu muhtasi wa Luteni Jenerali Madoshi.
“Kuwa mtoto wa mkuu haihalalishi kufanya hiki alichokifanya” Martin alisema kwa nguvu huku akiishika blauzi nyekundu aliyoivaa Catherine juu ya suruali yake ya dengrizi nyeusi. Ulisikika ukelele mkubwa kutoka katika mdomo wa Catherine akimuita baba yake. Sekunde zisizozidi nne mlango wa Luteni Jenerali Madoshi ulifunguliwa kwa nguvu, alikuwa amesikia ukunga wa sauti ya mwanamke anayempenda zaidi hapa duniani.
“Kuna nini hapa?” Luteni Jenerali Madoshi aliuliza kwa sauti yenye mamlaka.
“Anataka kunipiga huyu kijana..” Catherine alisema kwa sauti ya uwoga huku akimuoneshea kidole Martin.
“Sema kitu kilichotokea we mwanamke, mimi ninataka kuku......”
“Nyamaza Martin, umewezaji kunyanyua mkono wako na kuupiga moyo wangu?” Luteni Jenerali Madoshi aliuliza huku akimsogelea Martin.
Martin alibaki kimya, akiwa haamini kama siku yake ya kwanza kazini imeharibika namna ile.
“Sitaki kusikia chochote kutoka mdomoni mwako, mtafute mtu anayeitwa Daniel Mwaseba atakwambia unatakiwa kupata adhabu gani kwa hiki kitu ulichokifanya leo”.
Martin aliitii kauli ya Luteni Jenerali Madoshi, aliitikia kwa heshima huku akipiga saluti. Siku hiyo ndio alianza safari ya kumtafuta mtu anayeitwa Daniel Mwaseba. Ilimchukua wiki mzima hadi kumpata Daniel, na ilimchukua miezi mitatu kuikamilisha adhabu aliyopewa na Daniel.
Mwanzoni alipoambiwa amtafute Daniel alidhani atapewa adhabu ya nguvu kama wapewazo watu wote wanaokosea kwenye vyombo vya usalama, lakini kwake haikuwa hivyo, Daniel alimpa adhabu iliyomshangaza sana. Kwake aliiona kuwa ilikuwa ni adhabu ngumu lakini hakuwa na nafasi ya kuipinga. Adhabu aliyopewa ilikuwa ni, afanye afanyavyo ajenge urafiki na Catherine Simon Madoshi. Kwa mwengine pengine adhabu hii ilikuwa ni ndogo sana, lakini si Martin, kujenga urafiki na mtu aliyemuonesha dharau kubwa sana siku ya kwanza tu kukutana hakikuwa kitu rahisi.
Pamoja na ugumu wa adhabu hiyo, lakini hakukuwa na namna yoyote ile ya kufanya zaidi ya kujenga urafiki na mwanamke yule aliyemchukulia kama mwanamke mwenye dharau kuliko wanawake wote hapa duniani. Kama Martin alidhani kazi ya kutengeneza urafiki na Catherine itakuwa ngumu, basi alikosea, kazi hiyo haikuwa ngumu bali ilikuwa ngumu sana. Martin alifanya kila namna kutengeneza ukaribu na Catherine lakini alichoambulia ni matusi, kejeri na dharau. Ilimpasa hadi afanye vitu ambavyo si kawaida kufanywa na mwanaume wa kawaida lakini yote hayo aliambulia dharau na matusi. Ilipita miezi miwili na siku ishirini na tisa na alikuwa bado hajaikamilisha adhabu aliyopewa.
Siku moja, majira ya saa nane usiku, Martin alikuwa anatoka katika klabu ya usiku ya Ambiance iliyopo maeneo ya Sinza Afrikasana. Mikono yake yote miwili ilikuwa imeshika imara usukani wa gari aina ya Toyota Mark X, huku mlio wa mluzi ukitamalaki mdomoni mwake ukiufatiza wimbo mzuri wa mwanamziki Keyzah B. Matairi manne ya Toyota Mark X yalikuwa yanatiririka kwa kasi katika barabara ya Shekilango usiku huo wa manane. Wakati macho yake mawili yakiwa yakiwa yanatazama mbele ilipokuwa zinamulika taa za gari yake, ndipo alipowaona vijana watatu wakimsukasuka mwanamke mmoja pembeni ya klabu ya usiku ya San Sirro iliyopo maeneo ya Legal. Kati ya wanaume hao watatu, macho ya Martin yalivutiwa na mwanaume mmoja. Mguu wake wa kulia ulipunguza mwendo wa gari na kwenda kusimama mbele kidogo ya walipokuwa wale wanaume watatu na yule mwanamke. Akashuka garini huku akiuendeleza mluzi wake mdomoni. Aliinama karibu na tairi la mbele la gari yake akijifanya akiliangalia kama limepata tatizo. Ingelikuwa wewe ungedhani macho ya Martin yalikuwa yanaliangalia tairi la gari yake, lakini huyu hakuwa wewe, alikuwa ni Martin Hisia. Macho ya Martin yalikuwa yanawaangalia wale wanaume watatu na yule msichana.
Ilichukua takriban dakika kumi, ndipo wanaume wawili waliingia ndani ya gari baada ya kumsukumia garini yule mwanamke. Mwanaume mmoja alibaki pale, na huyo ndio ilikuwa shabaha ya Martin.
Yule mwanaume aliangalia pande zote kuona kama kuna mtu yeyote aliyeona kitendo walichokuwa wamekifanya muda mfupi uliopita, hakumwona mtu yeyote wa kumtilia shaka, ndipo alioingia katika gari dogo lililoegeshwa pembeni ya barabara na kuliondoa kwa kasi, akiufuata ule uelekeo walioelekea wale wenzake.
“Robby, lazima nikufuate nijue mna mpango gani na huyo mwanamke?” Martin alijisemea kimoyomoyo wakati akiingia katika gari yake, alifuata uelekeo lilipoelekea magari ya kina Robby.
Mara kadhaa Robby alikuwa anageuka nyuma kuona kama kuna mtu yeyote aliyekuwa anamfuatilia, lakini mara zote hakumwona wa kumtilia shaka. Martin alikuwa analifuatilia gari la Martin kwa umakini mkubwa sana, akihakikisha hafanyi kosa lolote lile la kumjulisha kwamba alikuwa anafuatiliwa.
Gari ya Robby ilipofika njiapanda ya Shekilango, ilikata kulia na kuifuata barabara iliyokuwa inaelekea maeneo ya Magomeni, bila kuhisi hata kidogo kuwa kuna mtu alikuwa anamfuatilia nyuma yake.
Gari ya Robby iliishia katika nyumba moja maeneo ya Magomeni Mwembechai. Ilikuwa ni nyumba yenye hadhi nzuri tofauti na nyumba nyingi zilizokuwemo maeneo hayo. Kuta kubwa iliyopakwa rangi ya zambarau ilikuwa imeizunguka nyumba hiyo ya kisasa. Martin alienda kuegesha gari yake umbali mrefu kidogo kutoka katika hiyo nyumba ili iwe ngumu kwake kugundulika.
Kwa umakini mkubwa alishuka katika gari, alitembea taratibu gizani huku mkono wake wa kulia ukigusa mahali alipokuwa ameihifadhi bastola yake, moja kwa moja alielekea katika nyumba lilipoingia gari ya Robby. Alizunguka kwa nyuma huku akitafuta mahali sahihi pa kumwezesha kuingia ndani.
Safari yake ilimfikisha nyuma ya nyumba ambapo ukuta wake ulikuwa mfupi kidogo tofauti na sehemu nyingine alizozipita, akaona pale ndio mahali sahihi pa kumwezesha kuingia ndani ya ile nyumba. Kwa ustadi mkubwa aliuparamia ukuta na kujivuta kwa juu. Kichwa chake kikawa kinachungulia ndani ya kuta wakati sehemu kubwa ya mwili wake ukiwa kwa nje, macho yake yaliliona eneo lote nje ya ile nyumba. Kulikuwa na magari matano ya kisasa, aliyatambua magari mawili, gari aliloingia nalo Robby na lile gari lililoondoka na mwanamke kule katika klabu ya San siro. Lakini kwa bahati nzuri alichokuwa anakitafuta hakukiona, hakukuwa na mlinzi yeyote. Aliuvuta zaidi mwili wake na kuupandisha juu ya ukuta, kisha akajirusha ndani ya nyumba bila ya kutoa ukelele wowote.
Chini kulikuwa na majani madogomadogo na maua yaliyotengeneza bustani ya kuvutia sana. Martin aliichomoa bastola yake kiunoni huku akinyata taratibu kuelekea katika nyumba iliyokuwepo mbele yake.
Usiku huo, hali ilikuwa ya utulivu mkubwa wakati akipiga hatua za kimyakimya kusonga mbele, sasa bastola yake ilikuwa mkononi huku kidole chake cha shahada cha mkono wa kulia kikiwa kimegusa kibonyazio cha bastola.
Dakika mbili baadae, alifika upande wa mbele wa nyumba, maua mengi yaliyotengeneza vichaka vidogo vilimficha mbele ya taa za ulinzi zikizotoa mwanga wa wastani usiku huo. Akiwa ameinama kidogo, aliambaa na ukuta wa nyumba na kufika sehemu lilipokuwa dirisha la sebuleni, hapo ndipo alipoweka kituo. Alijinyanyua kidogo kuchungulia ili kuona kama ataona chochote mle ndani. Macho yake yaliwashuhudia watu sita kila mmoja akiwa amekaa katika sofa lake, kati ya watu hao aliwatambua watu wanne, Robby, yule mwanamke waliyenchukua katika klabu ya San siro na wale jamaa walioingia naye kwenye gari. Watu wawili waliobaki hakuwatambua, walikuwa ni kijana mmoja mrefu, mweupe ambaye alikuwa amevaa suruali yenye mifuko pembeni na fulana ya kijani, mwingine alikuwa kijana mfupi ambaye uso wake ulitawaliwa na ndevu zisizo katika mpangilio maalum, yeye alikuwa amevaa suruali ya dengrizi ya bluu na fulana nyeupe yenye ufito mweupe katika sehemu za kola.
“Tumefanikiwa kumpata Grace, lazima Grace atuambie u wapi mzigo wetu” Yule kijana mrefu na mweupe alisema huku akiwatazama wenzake kwa zamu.
“Jamani kama nilivyowaambia tangu kule kazini, mimi sijachukua mzigo wenu” Mwanamke ambaye kwa sasa Martin alimtambua kwa jina la Grace alisema kwa sauti ya kulalamika huku macho yake yakiwa mekundu mithili ya mtu aliyetoka kuvuta bangi.
“Grace unatulazimisha kukufanyia kitu ambacho hakitasahaulika katika nchi hii, wewe ni mtoto wa kike, si vyema tukakufanyia tunachotaka kukufanyia, sisi ni watu wakarimu sana, lakini tunabadilika pale tu tunapoingiliwa katika anga zetu, una hiyari ya kutuambia mzigo wetu upo wapi kabla hatujakufanya kitu kibaya sana!” Yule mwanaume mfupi alisema huku akinyanyuka sofani. Alijipekua kiunoni na kutoa kisu kirefu kilichokuwa kinang’aa.
Uso wa Martin ulipatwa na msisimuko ulipokiona kisu kile, ujasiri aliokuwa nao awali ulipotea ghafla na kukumbwa na hofu, hofu iliyoonekana dhahiri katika kila kiungo cha mwili wake.
“Nakukata kidole chako! Na nitakukata vidole vyako vyote mpaka utakapojisikia kutuambia mahali ulipouweka mzigo wetu!” Yule jamaa mfupi alisema huku akiwa kaushika mkono wa Grace kwa mkono wake wa kushoto.

Hivi ndivyo mambo yalipoanzia, njoo tena kesho hapa HALFANI SUDY akusimulie hiki kisa kilichozua TAHARUKI kubwa sana.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
RIWAYA: TAHARUKI
Imeandikwa na HALFANI SUDY
SIMU 0653 212391

Hii ni sehemu ya Kumi

“Grace unatulazimisha kukufanyia kitu kibaya ambacho hakitasahaulika katika nchi hii, wewe ni mtoto wa kike, si vyema tukakufanyia tunachofikiria kukufanyia, sisi ni watu wakarimu sana, lakini tunabadilika pale tu tunapoingiliwa katika anga zetu, una hiyari ya kutuambia mzigo wetu upo wapi kabla hatujakufanya kitu kibaya sana!” Yule mwanaume mfupi alisema huku akinyanyuka sofani. Alijipekua kiunoni na kutoa kisu kirefu kilichokuwa kinang’aa.
Nywele za Martin zilisisimka alipokiona kisu kile, ujasiri aliokuwa nao awali ulipotea ghafla na kukumbwa na hofu, hofu iliyoonekana dhahiri katika kila kiungo cha mwili wake.
“Nakukata kidole chako! Na nitakukata vidole vyako vyote mpaka utakapojisikia kutuambia mahali ulipouweka mzigo wetu!” Yule jamaa mfupi alisema huku akiwa kaushika mkono wa Grace kwa mkono wake wa kushoto.
“Nawaambia, nawaambia ukweli” Grace alisema kwa sauti yenye kitetemeshi.
“Upo wapi mzigo wetu?” Yule jamaa mrefu aliuliza huku naye akisimama sofani.
“Mzigo wenu nilienda kuuficha kwa rafiki yangu...” Grace alisema kwa wasiwasi.
“Anaitwa nani huyo rafiki yako?” Yule jamaa mfupi aliuliza kwa sauti yenye matumaini. Grace hakujibu, alibaki akiwatazama tu wale wanaume wawili ambao hawakuonesha hata kidogo sura ya urafiki kwake.
“Hatupo kufanya maigizo hapa!” yule jamaa mfupi alisema kwa nguvu huku akiachia kofi kubwa lililotua upande wa kula wa Grace, Grace alisukumwa kwa nguvu ya kofi lile na kwenda kujibwaga hovyo sofani. Maumivu makali sana yalipita shavuni kwake, lakini hakuipata nafasi ya kuyasikilizia vizuri maumivu hayo, kwani yule jamaa mfupi alimsogelea kwa kasi pale sofani na kumkaba shingoni, kisha akamgeuza na kutazamana naye.
“Nakuuwa!” Jamaa mfupi alisema kwa nguvu wakati sura zao zikiwa zimekaribiana sana.
Martin aliyaona macho ya uwoga kutoka kwa Grace, ghafla akamsikia akisema,
”Mzigo wenu upo kwa Catherine Madoshi!”
Sura za mshtuko zilionekana kwa watu wote waliokuwemo pale sebuleni, lakini mshtuko huo pia ulienda katika sura ya Martin, hakutegemea hata kidogo kama kikao kile cha sebuleni kingemhusisha Catherine, mwanamke ambaye aliyegombana naye siku ya kwanza tu kuonana hapa duniani, mwanamke aliyekuwa na kazi ya kuirudisha amani kama alivyoadhibiwa na Daniel, lakini sasa alipata la nyongeza kutoka katika mdomo wa Grace, Catherine alikuwa na mzigo ambao ulikuwa unahitajiwa na wanaume wale wanne, hakujua ni mzigo ni gani? Wala unahusu nini? Lakini kichwani kwake kilipita kitu kimoja tu ‘Haukuwa mzigo wa kheri’
“Kamfungie kile chumba cha mwisho” Yule jamaa mfupi alisema huku akimwachia Grace, yule jamaa aliyekuja na Grace alimuongoza Grace kumpeleka katika chumba cha mwisho.
“Mbona umemruhusu Grace aondoke kabla hajatuambia huyo Catherine ni nani?” Yule jamaa mrefu aliuliza huku akimwangalia yule jamaa mfupi.
“Namjua Catherine Madoshi” Yule mtu mfupi alijibu kwa kujiamini, “Lazima tuhakikishe tunampata Catherine na kumleta hapa usiku huu!” Yule mtu mfupi alisema kwa sauti yenye mamlaka.
“Robby, tunaingia kazini sasahivi, ninaifahamu nyumba anayoishi Catherine, tunaenda kuivamia na kumteka baada ya kutuambia wapi ulipo mzigo wetu!”
Wote waliitikia, bila ya kuhisi kama kuna macho yasiyohusika yalikuwa yanawaangalia, wote wanne walitoka nje ya nyumba na kuelekea nyumbani kwa Catherine. Martin alipohakikisha wale jamaa wameondoka, alizunguka nyumba na kwenda uwani, alitumia ufunguo malaya kufungua kitasa cha mlango na kuufungua mlango, chumba cha kwanza tu kuingia alijibanza humohumo, kilikuwa ni chumba kidogo kilichokuwa kinatumika kama stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali visivyphitajika kwa muda ule.
“Leo lazima nijue mbivu na mbichi” Martin aliwaza wakati akijificha nyuma ya magunia ya mkaa.
Zilipita takribani saa mbili ndipo aliposikia mlio wa geti kubwa likifunguliwa, kisha akasikia mlio wa gari ukiingia ndani ya uwa. Dakika tano baadae alisikia kelele za mlango wa mbele ukifunguliwa huku sauti ya yule jamaa mfupi ikisema kwa nguvu,
”Catherine utatuambia wapi ulipo mzigo wetu!”
“Mzigo gani?” Martin aliisikia sauti ya Catherine ikiuliza swali ikiwa katika hali ya uwoga.
“Unajifanya huelewi eeeh, leo tutakuonesha kuwa watu unao wachezea sio wa mchezo, leo tutakuonesha kuwa umegusa watu wasiogusika” Martin aliisikia tena sauti ya yule jamaa mfupi.
Martin hakuisikia tena sauti ya Catherine, zaidi ya kusikia sauti ya mafua ya Catherine, alitambua kwamba Catherine alikuwa analia.
“Robby kamlete Grace hapa” Sauti ya mtu mfupi ilisema.
“Inamaana mmemteka na Grace?” Sauti ya kilio ya Catherine iliuliza ikiwa katikati ya kilio.
“Sio tumemteka Grace! Tunakuja kumuua Grace mbele ya macho yako endapo haujatuambia mahali ulipo mzigo, kisha tutakutesa na wewe na kukuuwa, sidhani kama kuna mtu ataitambua maiti yako kwa jinsi tutakavyoifanya” Sauti ya mtu mfupi ilisema kwa majigambo.
Ulipita ukimya wa kama dakika tatu huku zikisika kilio cha kwikwi kutoka kwa Catherine. Mara Martin aliisikia sauti ya Catherine akiwa kule stoo ikiita kwa nguvu.
“Graceeee” Catherine aliita huku akilia.
“Wape mzigo wao Catherine” Grace alijibu kwa sauti ya kuchoka.
“Msimuue Grace!” Mara sauti ya Catherine ilisika kwa nguvu, “Mzigo wenu upo kwa Jordan”
“Ni nani huyo Jordan na anaishi wapi?” Safari hii Martin aliisikia sauti ya mtu mrefu, mweupe.
“Jordan ni mpenzi wangu, anaishi Mikocheni kwa Nyerere, nyumba namba mia mbili na kumi na nne” Catherine alisema kwa sauti ya kitetemeshi, katika akili yake alijua kuwa anamuokoa Grace kwa kusema mahali ulipo mzigo, kumbe alikuwa anajidanganya, alikuwa amemuingiza mpenzi wake Jordan katika hatari kubwa sana, alikuwa anafanya kosa ambalo atalijutia siku zote katika maisha yake.
“Brown na Robby mtaenda kuufata mzigo na kuuleta hapa, hakikisheni hamuachi ushahidi wowote ule” Yule mtu mfupi alisema, hapo ndipo Martin alipogundua kwamba yule mtu mrefu, mweupe anaitwa Brown.
Walivyoondoka wakina Robby nyumba ilikuwa kimya, hadi saa kumi na mbili asubuhi ambapo walirejea. Martin akiwa kule stoo alisikia makelele mengi sana ya furaha, akajua kwamba jamaa walikuwa wameupata mzigo wao. Hamu ya kuujua huo mzigo ulikuwa ni mzigo gani ilimpanda Martin.
“Catherine na Grace tunawaachia huru, sitegemei kama mtamsimulia yeyote hiki kilichotokea usiku wa leo, iwe siri yenu kama bado mnapenda kuishi hapa duniani, mmelewa?” Mtu mfupi alisema kwa ukali.
“Ndio kaka” Catherine na Grace waliitikia kwa pamoja. Kisha ukapita ukimya kabla ya Martin kuisikia sauti ya Brown ikiuliza.
“Hivi tumefanya kitu sahihi kweli kuwaacha huru wale wanawake?”
“Usijali Brown, tumewaachia kimkakati, tutwatumia wale wanawake kuusafirisha huu mzigo kuelekea jijini Nairobi” Mtu mfupi alisema kwa kujiamini.
“Nakuamini sana, ninaiamini mipango yako na haijawahi kufeli hata siku moja” Brown alisema kwa matumaini.
“Hamjaacha ushahidi wowote?” Mtu mfupi aliuliza.
“Kama ulivyotuambia, tumemuua hawara wa yule demu bila kuacha ushahidi wowote ule” Brown alisema bila ya wasiwasi wowote.
“Safi, tumefanya kazi kubwa sana usiku wa leo, sasa ni wakati wa kwenda kujipongeza” Mtu mfupi alisema. Baada ya dakika chache Martin alisikia milango ya nyumba ikifunguliwa na kufungwa, alisikia mlio wa gari ukitokomea nje wa nyumba. Hapo ndipo alipotafuta nafasi ya kutoka nje ya nyumba ile kwa kutumia njia aliyoingilia usiku.
Asubuhi hiyo jiji la Dar es salaam liliamka na habari ya msiba mkubwa sana, Jordan, mtoto wa kwanza wa waziri wa mipango na fedha, Charles Wale alikuwa ameuwawa kwa kupigwa risasi ya kichwa nyumbani kwake. Ulikuwa msiba uliotingisha viunga vyote vya jiji la Dar es salaam. Jordan Wale lilikuwa ni jina lililopata umaarufu kutokana na umahiri wake wa kucheza mchezo wa mpira wa kikapu. Jordan alikuwa mchezaji wa kutumainiwa katika timu ya mpira wa kikapu ya Pazi. Umaarufu wa Jordan uliongezeka maradufu baada ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamitindo anayechipua kwa kasi, Catherine Simon.
Kifo cha Jordan kilimtesa sana Catherine kwakuwa ni yeye pekee ndiye aliyejua nini kilimsibu mchumba wake. Pamoja na kujua lakini hakuthubutu kumwambia yeyote nini kilitokea usiku ule. Askari wa jeshi la Polisi walitumia muda mwingi kumhoji kama anamjua muuaji wa mpenzi wake, lakini Catherine aliufunga mdomo wake kila alivyokumbuka vitisho vya usiku vya kina Brown.
“Catherine na Grace tunawaachia huru, sitegemei kama mtamsimulia yeyote hiki kilichotokea usiku wa leo, iwe siri yenu kama bado mnapenda kuishi hapa duniani, mmelewa?”

Je nini kitatokea? LAKO JICHO!
Usisahau kuwaalika marafiki zako waufollow ukurasa huu kwa riwaya kali kama hizi.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom