SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 4 : EPISODE 5
“Ruby karibu sana”
akasema Dr Fabian baada ya
Ruby kuwasili ikulu
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akajibu
Ruby
“Gosu Gosu yuko wapi?
“Gosu Gosu nimempangia
kazi nyingine ndiyo maana
nimekuja peke yangu”
“Watu wako wote pale
SNSA wako salama? Akauliza
Dr Fabian
“Tunashukuru wote wako
salama kabisa”
“Nafurahi kusikia hivyo”
akasema Dr Fabian na ukimya
mfupi ukapita
“Nilitaka tukutane ili
unipe ripoti ya kile ambacho
mmekuwa mnaendelea
kukichunguza ndani ya SNSA
lakini kabla ya yote nataka
kufahamu kuhusu Mathew
Mulumbi.Huyu ni mtu wako
wa karibu.Je ulifahamu
kuhusu uwepo wake hapa
Tanzania? Nilikuuliza swali
hili asubuhi kwenye simu
lakini nataka kukuuliza ana
kwa ana”akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo ambalo sikutaka
kulizungumza simuni lakini
kwa kuwa tumeonana ana kwa
ana nitakueleza ila nitaomba
libaki kwako na asifahamu
mtu mwingine yeyote”
“Nieleze tafadhali”
akasema Dr Fabian
akionekana kuwa na shauku ya
kutakakufahamu jambo hilo
“Ni kweli Mathew
Mulumbi alikuwepo hapa
nchini” akasema Ruby na
ukimya ukapita
“Ni kweli alikuwepo hapa
nchini ndiyo maana akalipua
ubalozi wa Marekani lakini je
wewe ulifahamu kama yuko
hapa nchini? Hilo ndilo swali
langu” akasema Dr Fabian
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Alinitafuta na tukaonana”
akajibu Ruby na Rais
akamkazia macho
“Kuna chochote
alikwambia kuhusiana na hiki
alichokifanya?
“Hapana mheshimiwa
Rais hakunieleza kuhusiana na
hiki alichokifanya.Hata mimi
nilistuka sana baada ya kusikia
kwamba ndiye aliyelipua
ubalozi wa Marekani hapa Dar
es salaam”
“Nimesikitishwa sana
Ruby kwa hiki alichokifanya
Mathew.Nimejiuliza maswali
mengi kwa nini aamue
kujiunga na kundi la
kigaidi?Hata hivyo sishangai
sana kwani toka nilipopata
taarifa zake na hata
nilipoonana naye ana kwa ana
sikuwahi kumuamini.Kibaya
zaidi amebadili hadi jina
anaitwa sijui jina gani lile”
“Abu Zalawi” akasema
Ruby
“Ndiyo.Anajiita hivyo.Nani
amemroga Yule jamaa hadi
akafanya maamuzi haya
mabaya ya kujiunga na IS?
Akauliza Dr Fabian
“Tena imekuwa vyema
amebadili jina na uraia wake
na hajulikani kama ni raia wa
Tanzania kwani angetutia aibu
kubwa endapo angejulikana ni
raia wa
Tanzania.Nimemchukia sana
Yule jamaa na ninaomba
afungwe hata maisha huko
gerezani au auawe kabisa !
akasema kwa ukali Dr Fabian
na Ruby akaonekana
kuchukizwa na kauli ile ya Dr
Fabian
“Samahani Ruby hili suala
la Mathew limenikasirisha
sana hadi nikasahau kama
tuna mazungumzo
muhimu.Ulisema kuna jambo
la muhimu unataka kunieleza”
“Ndiyo mheshimiwa Rais
lakini linahusiana na huyo
Mathew”
“Jambo gani hilo?
“Alipofika hapa nchini
alinitafuta na lengo kubwa la
kunitafuta kwake ni kunipa
taarifa muhimu” akasema
Ruby na kumtazama Rais
aliyekuwa akimsikiliza huku
sura yake ameikunja kwa
hasira
“Mathew alinipa taarifa za
watu waliomuua mufti wa
Tanzania na akanielekeza
mahala wanakoishi”
“Aliwafahamu watu
waliomuua mufti wa Tanzania!
DR Fabian akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa Rais
anawajua na alinielekeza
mahala wanakoishi”
“Ulimuamini hicho
alichokwambia? Akauliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninamuamini na tuliifanyia
kazi taarifa yake”
“Ruby usiniambie baada
ya haya yote aliyoyafanya bado
unamuamini Yule jamaa !
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais.Ni
kweli Mathew anashirikiana na
kundi la kigaidi la IS na katika
mazungumzo yetu alikiri hilo
lakini aliniambia ana sababu
maalum ya kushirikiana na
kundi hilo la IS.”
“And you believe
him?akauliza Dr Fabian kwa
ukali
“Yes I do Mr President !
akajibu Ruby kwa sauti ya juu
kidogo
“Ruby siamini kama haya
maneno yanatoka katika
kinywa chako.Unawezaje
kumuamini Yule jamaa wakati
ni gaidi?Zaidi ya watu sabini
wameuawa na idadi inaweza
kuongezeka.Unawezaje
kumuamini huyu muuaji
mkubwa? Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
ninamfahamu Mathew
Mulumbi na nimelazimika
kuamini kile
alichoniambia.Alinipa taarifa
muhimu kwamba IS wako
hapa nchini na ndiyo
wanaendesha mashambulio
mbali mbali ya kuua viongozi
wa dini na kuchochea
vurugu.Alituelekeza mahala
wanakoishi magaidi hao na
tukafanya operesheni ya
kuvamia makazi yao kwa
kuwatumia makomando
tukafanikiwa
kuwakamata.Katika upekuzi
wa makazi yao tuligundua vitu
kadhaa ikiwemo mabaki ya
vifaa vya kutengenezea
bomu.Tunahisi yawezekana
bomu lililotumika kulipua
ubalozi wa Marekani
lilitengenezwa hapo” akasema
Rub na kumtazama Dr Fabian
halafu akaendelea
“Tuliwakamata watu wote
waliokutwa hapo na
tunaendelea kuwahoji.Kuna
mtu ambaye Mathew
alituelekeza tumtafute anaitwa
Assad Ismail ambaye ni
kiongozi wao.Tukimpata huyo
tutafahamu mengi kuhusiana
na hizi vurugu
zinazoendelea.Mheshimiwa
Rais hiki kinachoendelea hivi
sasa kina sababu zake na
ningeomba utupe muda zaidi
wa kuendelea kulichunguza
jambo hili nina uhakika siku si
nyingi tukafanikiwa kujua kiini
cha hizi vurugu.Kama
tukifanikiwa kumpata huyo
Assad Ismal tutamuhoji kujua
nani aliyemtuma afanye
mauaji ya viongozi wa dini na
kuchochea vurugu ?
Mheshimiwa Rais tunaelekea
kuzuri katika uchunguzi wetu”
akasema Ruby
“Ruby umeniweka njia
panda sijui nishike
lipi.Nashangaa kwa Mathew
ambaye amejiunga na magaidi
kuwapa taarifa ambazo
zitawaweka wenzake katika
hatari.Hili haliingii akilini hata
kidogo.Iweje awauze wenzake?
Akauliza Dr Fabian
“Ni kwa sababu Mathew si
gaidi” akajibu Ruby
“Huo ni iongo Ruby.Kama
asingekuwa gaidi asingefanya
shambulio lile baya na kuua
watu.Hakuna sababu yoyote ya
kumtetea mtu huyu ni gaidi na
muuaji!! Akasea Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais, ni
kweli Mathew anashirikiana na
magaidi lakini ni kwa sababu
ya misheni maalum ya siri”
“Alikueleza ni operesheni
ipi hiyo ya siri? Dr Fabian
akauliza
“Hakunieleza lakini …”
“Hakuna lakini
Ruby.Kama hakukueleza basi
ni mwongo.Mathew Mulumbi
amekuwa mnyama na ………”
“Mheshimiwa Rais
nakubali umuite Mathew
majina yote mabaya kwa hili
alilolifanya lakini ningeomba
unisikilize mimi ambaye
ninamfahamu Mathew vizuri
kuliko wewe ! akasema Ruby
kwa sauti ya juu kidogo halafu
wakatazama kwa muda Ruby
akaendelea
“Ninamuamini Mathew na
ninaamini hiki alichokifanya ni
kwa sababu maalum.Hata siku
moja Mathew hawezi
akashirikiana na magaidi
kama hana sababu ya kufanya
hivyo.Tukiweka pembeni
hilo,ni yeye ambaye ametupa
mwanga kuhusiana na hiki
kinachoendelea hapa
nchini.Tulikuwa tumekwama
hatujui tuanzie wapi lakini ni
yeye ambaye ametusaidia na
sasa ninaweza kusema tuna
sehemu ya kuanzia kufahamu
chanzo cha vurugu zilizotokea
hapa nchini” akasema Ruby.Dr
Fabian akamtazama kwa muda
na kusema
“He lied to you ! akasema
Dr Fabian kwa ukali
“Amekudanganya nawe
ukakubali.Anacheza na akili
zenu Yule jamaa na hakuna
chochote cha maana.Kama
kweli watu hao aliowaelekeza
ni magaidi kuna chochote
mmekwisha kipata hadi sasa
kutoka kwao?
“Bado tunaendelea
kuwahoji mheshimiwa Rais
lakini taarifa aliyotupa
Mathew ni ya kweli kabisa na
haina mashaka hata
kidogo.Mheshimiwa Rais
nakuomba uweke akiba ya
maneno kwa sasa kwani
baadae jambo hili
litakapokuwa limefika mwisho
usijilaumu kwa maneno
yako”akasema Ruby
“Usinifundishe nini cha
kuzungumza Ruby.Ni aibu
sana kwa mtu mkubwa kama
wewe kuchezewa akili yako na
mtu kama huyu asiye na hata
chembe ya utu !
“Mheshimiwa Rais
naomba uniamini na uamini
kazi inayofanywa na idara
yangu.Nakuhakikishia
tutaupata mzizi wa hizi
vurugu.Tayari tumekwishapata
mwanga” akasema Ruby na Dr
Fabian akacheka kidogo
“Mwanga ulioonyeshwa na
gaidi? Katu hiyo si taarifa ya
kuamini na sina hakika kama
kweli hao mliowakamata ni
magaidi” akasema DrFabian
“Mheshimiwa Rais
uliniamini na kunipa idara ya
SNSA niiongoze.Sintaweza
kufanya kazi yangu kikamilifu
kama
hautaniamini.Mheshimiwa
Rais kama hauna tena imani
nami kwamba kwa
kushirikiana na wenzangu
tunaweza kulishughulikia
suala hili la vurugu zilizotokea,
naomba uteue mtu mwingine
ambaye unadhani anaweza
akaongoza vyema idara ya
SNSA kama unavyotaka.Mimi
niko tayarikuacha kazi muda
huu huu ! akasema Ruby
akionekana kukasirika
“Ruby huu si wakati wa
kufikiria mambo kama
hayo.Taifa liko kwenye wakati
mgumu mno.Sitaki kusikia
tena ukizungumza au hata
kufikiria kitu kama hicho cha
kuacha kazi.Ninakuamini
ndiyo maana nilikutoa
Uingereza nikakuleta hapa
kufanya kazi hii”
“Kama ni hivyo
mheshimiwa Rais naomba
utuamini mimi na
wenzangu.Nakuhakikishia
mheshimiwa Rais si muda
mrefu kutoka sasa kuna
mambo mengi yatajulikana
kuhusiana na hiki
kinachoendelea.Naomba
uniamini na utupe nafasi”
akasema Ruby na baadaya
muda Dr Fabian akauliza
“Ukiacha hao jamaa
mliowakamata mkidai ni
magaidi kuna mpango gani
mwingine mnao wa
kutuwezesha kufahamu chanzo
cha hizi vurugu?Wale watu
mnaowatafuta mnaohisi wana
mahusiano na hizi vurugu
mmefikia wapi kujua mahala
walipo? Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
mpango tunaoendelea nao ni
kuwahoji wale magaidi
tuliowakamata ili tupate
taarifa za mahala alipo Assad
Ismail ambaye anaweza
akatupa maelezo ya kutosha
kuhusiana na hizi vurugu
kwani ni wao wanaoendesha
mauaji ya viongozi wa dini”
“Mathew Mulumbi again”
akasema Dr Fabian kwa sauti
ndogo
“Ruby nenda kaendelee na
mipango yenu
sintawaingilia.Kama kuna
chochote mtakipata ambacho
unadhani ninapaswa
kukifahamu utanijulisha”
akasema Dr Fabian
“Nashukuru mheshimiwa
Rais nitafanya hivyo” akajibu
Ruby huku akinyanyuka
akaagana na Rais akaondoka
“Sina imani tena na
SNSA.Hakuna chochote
tunachoweza kukipata kutoka
kwao kama tayari
wanaongozwa na akili ya
Mathew Mulumbi.Ningeweza
kumtoa Ruby na kumuweka
mtu mwingine lakini nilimtoa
Uingereza aje aongoze idara
hii na amepitia mambo mengi
mazito hadi kufika hapa ngoja
nimpe muda nione muelekeo
wake.Ameniudhi mno leo kwa
namna alivyomtetea Mathew
Mulumbi eti kitendo
alichokifaya cha kulipua
ubalozi wa Marekani ni moja
ya operesheni zake.Stupid !
akawaza Dr Fabian akiwa na
hasira
VICTORIA – SEYCHELLES
Boti aliyopanda Mathew
Mulumbi iliwasili katika pwani
ya jiji la Victoria nchini Sheli
Sheli.Bado Mathew alikuwa
amevishwa mfuko kichwani
hivyo hakufahamu walikuwa
wapi.Alishushwa kutoka katika
ile boti na kuingizwa garini
milango ikafungwa magari
yakaondoka.Baada ya mwendo
wa takribani dakika ishirini
gari alilopanda Mathew
likapunguza mwendo halafu
likasimama.Milango
ikafunguliwa akashushwa
ndani ya gari akaingizwa
katika nyumba,akahisi kama
vile wanashuka ngazi kuelekea
chini.Akasikia mlango
ukifunguliwa akaingizwa ndani
ya chumba halafu mlango
ukafungwa na watu wote
wakatoka kukawa
kimya.Chumba kilikuwa na
giza nene.
Zilipita dakika kama kumi
hivi mlango ukafunguliwa
tena,taa ikawashwa halafu
Mathew akavuliwa ule mfuko
kichwani.Mtu mmoja
akamsogelea Mathew
akachuchumaa na kumfungua
pingu za miguu na mikono
akamtaka Mathew amfuate
wakaingia katika chumba
kimoja ambamo waliwakuta
watu wanne wakipata chakula.
“Karibu Abu Zalawi”
akasema Yule jamaa
aliyekwenda kumfungua na
Mathew akaketi kitini na
kujumuika na wale jamaa
katika chakula,alihisi njaa
kali.Hakuwa ameweka
chochote tumboni toka
asubuhi.Walikula kimya kimya
bila mazungumzo na baada ya
kumaliza kula mazungumzo
yakaanza
“Abu Zalawi pole sana kwa
safari ndefu”
“Ahsante nashukuru”
akajibu Mathew
“Naitwa Jeffrey,wenzangu
ni Richard,William,Brian,na
Christopher” akasema Jefrey
akiwatambulisha wenzake kwa
Mathew
“Tumepewa maelekezo
maalum na viongozi wetu ya
kuhakikisha misheni yako
inakamilika lakini hapo hapo
jambo hili lisionekane kama ni
tukio la kutengenezwa ndiyo
maana utaona ilitumika nguvu
kidogo wakati wa kukukamata
ili tukio lionekane ni halisi”
akasema Jeffrey na kunyamaza
kidogo
“Muda mfupi ujao
tutakufanyia mahojiano
ambayo yatafuatiliwa moja
kwa moja na makao yetu
makuu Langley.Baada ya
mahojiano hayo tutakupeleka
katika chumba cha mateso ili
kukutesa ufunguke na hapo
utatusamehe kwani tutatumia
nguvu ili ionekane ni jambo la
kweli.Tutafanya namna ili
upoteze fahamu halafu
tutakupeleka katika chumba
walimo wale wanasayansi wa
Iran na utaanza kujenga
ukaribu nao” akasema Jeffrey
na kumuelekeza Mathew
namna mahojiano yao
yatakavyokuwa maswali
atakayoulizwa na majibu
anayotakiwa kuyatoa.Baada ya
mazungumzo yale Mathew
Mulumbi akarejeshwa katika
kile chumba na kufungwa
pingu akavishwa mfuko
kichwani.
Zilipita dakika kadhaa taa
yeye mwanga mkali ikawaka
mle ndani halafu mlango
ukafunguliwa wakaingia watu
wanne mle ndani.Mathew
akainuliwa na kutolewa
akapelekwa katika chumba
kingine akafungwa mikono
katika pingu za mezani halafu
ikawashwa taa yenye
mwangaza mkali na ule mfuko
aliofunikwa kichwani
ukatolewa.Ndani ya chumba
kulikuwa na watu wapatao
nane wakiwamo wale ambao
alikula nao chakula muda
mfupi uliopita.Kulikuwa pia na
kamera imeelekezwa upande
wake.Mbele yake alikaa Jeffrey
akivuta sigara.
“Unafahamu hapa uko
wapi?akauliza Jeffrey
“Nitafahamu vipi wakati
mmenifunika na mfuko
kichwani muda wote? akajibu
Mathew
“Usijali uatafahamu
tu.Hapa ni moja ya sehemu
wanakoletwa watu kama wewe
kwa ajili ya kufanyiwa
mahojiano.Naomba nikuweke
wazi kwamba hapa ni mahala
panapoogopwa mno na mtu
yeyote aliyewahi kupita
mahala hapa ukimwambia
kwamba unataka kumrejesha
hapa ataongea kila lugha
anayoifahamu ili asiweze
kuletwa hapa.Taarifa nyingine
ya mahala hapa ni kwamba
wote waliowahi kuletwa hapa
wote walifunguka na kutoa
ushirikiano.Nikupe mifano ya
watu waliowahi kupita
hapa.Hasan Izz Al
Din,Abdelkarim Hussein Al
Nasser,Jaber Elbaneh,Ali Saed
Bin Ali El Hoorie, na wengine
wengi.Hawa wote ni magaidi
wakubwa na walihusika katika
matukio mbali mbali ya kigaidi
na kuua wamarekani.Wote
walipofika hapa walifunguka
na kutaja mtandao wao
wote.Wapo vile vile ambao
walifikishwa hapa na
hawakutoka hai na wapo
ambao kwa miaka mingi
wameendelea kushikiliwa
sehemu hii kwa kushindwa
kutoa ushirikiano.Hakuna
yeyote kati ya watu wako
anayeweza kukusaidia ukiwa
hapa hivyo ni jukumu lako
kujisaidia wewe mwenyewe”
akasema Jeffrey na kuwasha
sigara nyingine.
“Anza kwa kututajia jina
lako na umetokea wapi”
akasema Jeffrey.Mathew
akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Naitwa Abu Zalawi,raia
wa Saudi Arabia” akasema
Mathew na kunyamaza
akawatazama wale watu mle
ndani
“Abu Zalawi unafahamu ni
kwa nini uko hapa? Akauliza
Jeffrey lakini kabla Mathew
hajajibu akaingia mtu
mwingine akamnong’oneza
Jeffrey kitu sikioni
“Jibu Abu Zalawi
unafahamu kwa nini uko
hapa?Jeffrey akauliza
“Nimelipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es salaam”
akajibu Mathew
“Abu Zalawi nataka
utufahamishe umewahi
kushiriki katika matukio
mangapi ya kigaidi kabla ya
hili la Dar es salaam? Akauliza
Jeffrey
“Mengi” akajibu Mathew
“Unaweza kuyataja?Jeffrey
akauliza
“Nilimuua mkuu wa
Mossad Afrika
Mashariki,nimeshirikiana na
kundi la wanamgambo la
Ammar Nazar Brigades
kufanya mashambulio kadhaa
ndani ya Israel” akajibu
Mathew bila woga
“Sababu gani ilikupelekea
ukalipua ubalozi wetu Dar es
salaam? Akauliza Jeffrey.Sura
ya Mathew ikabadilika na
akaonyesha hasira
“Ni kwa sababu ya
dhuluma na ukandamizaji
kunakofanywa na Marekani
kwa nchi za kiislamu.Marekani
ina chuki dhidi ya uislamu na
ndiyo maana kila uchao
imekuwa ikizikandamiza nchi
za kiislamu na
waislamu.Mfano ni nchi ya
Iran imekuwa inawekewa
vikwazo chungu nzima na
Marekani na kama haitoshi
bado wana mpango wa
kuishambulia kijeshi.Hiki
nilichokifanya ni kuionya
Marekani kwamba waislamu
tutasimama imara kutetea dini
yetu dhidi ya ukandamizwaji
wowote ule ! Hiki kilichotokea
Tanzania kitaendelea sehemu
nyingine mbali mbali duniani
hadi pale nchi yenu
itakapoacha unyanyasaji kwa
waislamu na nchi zao !
akasema Mathew kwa
ukali.Huku akitabasamu
Jeffrey akasema
“Abu Zalawi umejinadi
kwamba ulichokifanya ni kwa
ajili ya kupigania haki za
wasilamu wanaonyanyaswa na
Marekani lakini Marekani
hainyanyasi waislamu na
jambo lingine ni kwamba
Uislamu hauamini katika
ugaidi.Katika shambulio lile
umeua pia waislamu.Hivyo
ndivyo kitabu kitukufu
kinaelekeza kuua watu wasio
na hatia yoyote hata waislamu
wenzako? Akauliza Jeffrey
“Vyovyote mjuavyo ninyi
lakini fahamuni mapambano
haya yataendelea sehemu
mbali mbali duniani ! akasema
Mathew
“Abu Zalawi shambulio lile
ulilolifanya limeua watu zaidi
ya sabini na miongoni mwao ni
wanawake na watoto wapo
waislamu wenzako pia
waliokuwa wamepewa hifadhi
katika ubalozi wetu wakiamini
ni sehemu salama na hii
inaonyesha wazi kwamba
hatuchukii uislamu na
waislam.Damu ya watu hao
wote inakulilia wewe.Wengi
wa watu uliowaua ni waafrika
wenzako na huwezi kujua
yeawezekana katika
mkusanyiko ule wapo pia
ndugu zako.Nafsi yako
haikusuti kwa hiki
ulichokifanya? Akauliza
Jeffrey na Mathew
akawakumbuka wale watoto
aliowakuta ndani ya gari
lililobebab bomu
“Masikini wale watoto
bado wadogo sana sijui kama
walisalimika” akawaza
“Abu Zalawi ukimya huo
unaonyesha wazi kwamba hata
wewe nafsi yako inakusuta kwa
hiki ulichokifanya.Hata
nikiitazama sura yako
haionyeshi ukatili na hii
inanipa picha kwamba
umefanya kitendo hiki bila
ridhaa yako.Nataka utuambie
nani waliokutuma ukafanye
shambulio lile?Nani viongozi
wako? Abu Zalawi tunataka
kuzuia mashambulio ya kigaidi
yasiendelee kutokea na kuua
watu wasio na hatia na wewe
nayo nafasi kubwa kabisa ya
kusaidia hilo
liwezekane.Tuambie nani
waliokutuma ukafanye
shambulio lile? Akauliza
Jeffrey.Mathew akawatazama
kisha akasema
“Tayari nimetimiza kazi
yangu niliyotakiwa kuifanya
hapa duniani hivyo sioni
sababu ya kuendelea kupoteza
muda wenu kunihoji kutafuta
taarifa ambazo hamtaweza
kuzipata. Nipelekeni huko
mnakowapeleka mashujaa
kama mimi mkanitese
mtakavyo na hata ikiwezakana
nichomeni sindano ya sumu
nife kabisa siogopi chochote na
niko tayari kufa hata sasa
kwani naamini kwa
nilichokifanya ninangojewa
kwa hamu peponi ! akasema
Mathew.Jeffrey akamtazama
na kusema
“Abu Zalawi katika
matamshi yako uliitaja nchi ya
Iran kwamba inaonewa na
Marekani.Kuna nchi nyingi za
kiislamu kwa nini ukachagua
kuitaja Iran? Kwa nini isiwe
Iraq,Syria au nchi yoyote
nyingine?akauliza Jeffrey
“Iran ni mfano wa nchi
inayochukiwa na
kukandamizwa na Marekani
lakini zipo nyingi” akajibu
Mathew
“Ulitumwa na serikali ya
Iran kufanya shambulio lile?
akauliza Jeffrey
“Mnapoteza muda wenu
bure hapa na kunichelewesha
kuiona pepo.Niueni haraka
kwani hamtaweza kupata kitu
chochote kutoka kwangu”
akasema Mathew
“Nilikuelekeza hapo awali
kwamba ukiingia mahala hapa
utake usitake lazima
utafunguka lakini wewe naona
bado hujapafahamu vizuri
mahala hapa.Nitakuchukua na
kukutembeza mahala hapa
upafahamu vizuri halafu
tutakuja tena kuzungumza
baadae” akasema Jeffrey na
kuelekeza Mathew afunguliwa
pingu
“Twende tukatembee rafiki
yangu.Usiwe na hofu” akasema
Jeffery kisha akatoka mle
ndani akiwa na Mathew
Walitembea katika
vyumba kadhaa vya jumba lile
huku Jeffrey akimpa Mathew
maelezo na mara wakaingia
katika chumba kimoja
kikubwa chenye vifaa kama
chumba cha mazoezi.
“Abu Zalawi hapa
tutafanya mazoezi kidogo
lakini hautafanya na mimi”
akasema Jeffrey na kugonga
ukuta mlango miwili
ikafunguka wakatokea watu
sita.Ilikuwa ni mijitu ya
miraba minne na yenye sura za
kuogofya
“Hawa ndio utakaofanya
nao mazoezi” akasema Jeffrey
na kuwageukia wale jamaa
“Nimewaleteeni mgeni
anahitaji mazoezi kidogo ili
achangamke” akasema Jeffrey
na kumsukuma Mathew
akaangukia katika mikono ya
mmoja wa wale jamaa
akamdaka na kumuinua juu
juu kisha akamrusha kwa
mwenzake akamdaka na
kumtandika ngumi nzito
ambayo ilimfanya Mathew
aone nyota akapepesuka na
kupigwa teke akajikuta katika
mikono ya mwingine ambaye
alimtandika ngumi akanguka
chini.Akainuliwa na mwingine
akamtandika ngumi Mathew
akaenda chini.Alikuwa
anapigwa kwa zamu.Ndani ya
muda mfupi hakuwa
akitazamaika.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby aliwasili nyumbani
kwa Gosu Gosu akitokea ikulu
alikokuwa na mazungumzo na
Rais.Alipokewa na Gosu Gosu
wakaelekea katika chumba cha
mapumziko
“Mgeni yuko wapi?
Akauliza Ruby
“Yuko chumbani kwake
anapumzika”
“Umezungumza naye
chochote?
“Hapana Ruby
sijazungumza naye
chochote.Uliniambia
nisimuulize chochote hadi
utakapofika wewe mwenyewe”
akasema Gosu Gosu
“Good.Umekuwa naye
toka Arusha unaweza
ukamuelezeaje? Akauliza Ruby
“Hatukuwa na
mazungumzo mengi lakini kwa
haraka haraka anaonekana ni
mjanja na mwenye kuchukua
tahadhari na vile vile hapendi
kuchunguzwa .Nadhani
utakapozungumza naye
tutafahamu mambo mengi
kuhusu yeye.Vipi uko utokako?
“Huko mambo
hayakwenda vizuri na
Rais.Mazungumzo
yalitawaliwa na mtu mmoja tu
Mathew Mulumbi.Rais
alikuwa mbogo akitoa
matamshi makali kumuhusu
Mathew.Nilijaribu kumdokeza
Rais kwa kifupi kuhusu kile
tunachoendelea nacho hivi
sasa ndani ya SNSA
nikamdokeza kwamba
mafanikio haya yote hadi
tukafanikiwa kuwafahamu na
kuwapata magaidi
wanaoendesha matukio ya
mauaji hapa nchini ni kwa
sababu ya Mathew Mulumbi
lakini hatukuelewana pale
nilipomwambia kwamba
Mathew yuko katika misheni
maalum na kile alichokifanya
ni mojawapo ya misheni
hiyo.Kwa ujumla maongezi
yetu hayakwenda vizuri
kufuatia suala hili la
Mathew.Rais ametoa maneno
mengi ya dharau kwetu ilifika
wakati nilitaka kuachana na
kazi hii” akasema Ruby
“Usijali Ruby.Haya yote
Mathew aliyafahamu ndiyo
maana akatutahadharisha
mapema.Sisi tunaoelewa
kinachoendelea tuendelee
kusimama naye.Tuendelee
kupambana kuhakikisha nchi
inakuwa shwari na
tunawafahamu wale wote
waliochochea vurugu hizi”
akasema Gosu Gosu
“Twende tuka zungumze
na Nawal” akasema Ruby na
Gosu Gosu akamuongoza
wakaenda katika chumba
alimo Nawal akagonga na
Nawal akafungua mlango
akawakaribisha ndani.Nawal
alimtazama Ruby kwa jicho
ambalo Ruby alilielewa.Nawal
alikuwa anamtaka Gosu Gosu
atoke mle ndani.
“Usihofu Nawal tunaweza
kuendelea Gosu Gosu
akiwepo” akaema Ruby
“Karibu Tanzania.Pole kwa
safari “
“Ahsante.Poleni na nyie
kwa yanayoendelea hapa
Tanzania”
“Tunashukuru Mungu
mpaka sasa tu wazima”
akasema Ruby na ukimya
mfupi ukapita kisha akasema
“Nawal nadhani ni wakati
sasa wa kuzungumza
kuhusiana na kile kilichokuleta
hapa Tanzania.Mama yako
Habiba Jawad aliponipigia
simu aliniomba nikusaidie
kufika Dar es salaam na vile
vile katika kile kilichokuleta
hapa Tanzania.Tayari
nimekusaidia umeweza kufika
salama Dar es salaam na sasa
ninataka kufahamu kuhusu
kile ambacho umekuja
kukifanya hapa Tanzania”
akasema Ruby
“Kwanza kabisa
nawashukuruni sana Ruby na
Gasu Gasu”
“Gosu Gosu” akasema
Ruby na kumrekebisha Nawal
“Jina gumu linanisumbua
kutamka hata hivyo
ninawashukuruni sana kwa
kuniwezesha kufika salama
Dar es salaam.Kama
ningekuwa mwenyewe
ingeniwia ugumu kuingia Dar
es salaam haraka na kwa
urahisi namna hii.Ahsanteni
na ningeomba nipewe
gharama zilizotumika
kunifuata kule Arusha ili
nizirejeshe” akasema Nawal
“Usijali Nawal.Wewe ni
mgeni wetu hivyo lazima
tuhakikishe tunakuhudumia
kwa kila kitu kama mama yako
alivyompokea na kumtunza
Mathew Mulumbi” akasema
Ruby
“Anaendeleaje Mathew
Mulumbi?akauliza Nawal
“Mathew hatujui kwa sasa
anaendeleaje.Kwani si mko
wote Saudi Arabia? Ruby
akauliza
“Mathew yuko hapa
Tanzania.Hamjaonana bado?
Akauliza Nawal .Ruby na Gosu
Gosu wakatazamana
“Ina maana hajui Mathew
alichokuja kukifanya hapa
Tanzania? Gosu Gosu na nawal
wakaongea kwa Kiswahili na
Nawal hakuelewa chochote
kwani hakuifahamu lugha ya
Kiswahili.
“Twende naye taratibu
tutafahamu kila kitu” akajibu
Ruby
“Ndugu zangu kitu
kikubwa cha kwanza ambacho
nataka mnisaidie ni kuonana
na Mathew Mulumbi.Tafadhali
sana nisaidieni kwa hilo”
akasema Nawal
“Nawal utatusamehe
kwani kwa sasa hatufahamu
mahala aliko Mathew
Mulumbi” akasema Nawal
“Mathew yuko hapa Dar es
salaam.Hamjaonana
naye?Mnafahamu makazi yake
yalipo? Akauliza Nawal
“Nawal tafadhali usitake
kutuchanganya akili zetu.Ina
maana huna taarifa za
alichokifanya Mathew?
Akauliza Gosu Gosu huku
akimtazama Nawal kwa macho
makali
“Gosu Gosu.! Taratibu”
akasema Ruby
“Ruby ni kweli ninahitaji
mno kuonana na Mathew
Mulumbi kabla ya mambo
yote.Kama bado hamjaonana
naye Mathew yuko hapa
Tanzania.Nipelekeni katika
makazi yake yawezekana
akawa huko” akasema Nawal
“Nawal hapa tulipo ndipo
makazi ya Mathew Mulumbi
ila anayeishi hapa kwa sasa ni
Gosu Gosu na sisi tote hapa ni
kama nyumbani kwetu kwani
Mathew ni mtu wetu wa
karibu sana”akasema Ruby
“Ina maana Mathew
hajawasiliana nanyi alipokuja
hapaTanzania? Akauliza
Nawal
“Hapana hajawasiliana
nasi na hatukujua kama
Mathew yuko hapa Dar es
salaam”
“Mathew aliiandika namba
yako katika kitabu chake cha
kumbu kumbu na kwa kuwa ni
namba yako pekee
iliyoandikwa humo tuliamini
wewe ni mtu wake wa muhimu
sana ndiyo maana tutakutafuta
tukijua kwamba unaweza
ukanielekeza mahala alipo
Mathew” akasemaNawal
“Nilipigiwa simu na mtu
aliyejitambulisha anaitwa
Najma ambaye ni mke wa Abu
Zalawi ambaye baadae
niligundua ndiye Mathew
Mulumbi akaniambia kwamba
Mathew alikuwa ananitafuta
simuni.Nimeshangaa
unaponiambia kwamba
Mathew alikuwepo hapa
Tanzania”
“Ni kweli Ruby.Mathew
Mulumbi amekuja Tanzania”
“Amekuja kufanya
nini?Kwa nini amekuja kwa
siri?Hapa ni nyumbani kwake
kwa nini hajakanyaga kama
amefika Tanzania? Ruby
akauliza
“Sifahamu amekuja
kufanya nini lakini najua
amekuja Tanzania”
“Kwa nini unasisitiza sana
kutaka kuonana na Mathew
Mulumbi? Akauliza Gosu Gosu
“Kuna taarifa muhimu
nataka kumpatia”
“Taarifa ipi?
“Ni kuhusu mke wake
Najma.Alijiua kwa kujipiga
risasi baada ya Mathew
kuondoka na hafahamu
chochote juu ya jambo hilo”
“Nini kilisababisha Najma
akajiua?Ruby akauliza
“Inadaiwa ni wivu.Alihisi
labda Mathew ana mwanamke
mwingine na ndiyo maana
Mathew alipoondoka tu Najma
akabaki akajiua” akasema
Nawal
“Anafahamika kama Abu
Zalawi.Wewe umefahamuje
anaitwa Mathew Mulumbi?
akauliza Gosu Gosu
“Niliambiwa hivyo na
mama kwamba jina halisi la
Abu Zalawi ni Mathew
Mulumbi na anatokea
Tanzania ambako
hawalifahamu jina la Abu
Zalawi”akajibu Nawal
“Hapa naona tunacheza
mchezo wa kitoto.Tunapoteza
muda bila sababu ya msingi”
akasema Gosu Gosu kwa
hasira na kuinuka
“Gosu Gosu nini unataka
kukifanya?akauliza Ruby
“Ruby hatuwezi kuendelea
na mchezo huu wa
kipuuzi.Huyu mwanamke
asitufanye sisi wajinga”
akasema Gosu Gosu
“Sikiliza Nawal Mathew
Mulumbi amelipua ubalozi wa
Marekani hapa Dar es salaam
usiku wa kuamkia leo na
asubuhi ya leo amekamatwa
jijini Nairobi na makachero wa
CIA akitafua usafiri wa kumtoa
nchini Kenya ili akimbilie
Somalia na mpaka sasa hatujui
mahala alipo.Nataka utuambie
ukweli hukufahamu alichokuja
kukifanya Mathew huku
Tanzania?akauliza Gosu Gosu
“Naomba mniamini ndugu
zangu sifahamu chochote
kuhusu jambo hilo.Ni Mathew
kweli aliyefanya hicho kitu au
ni mtu aliyefanana naye?
Mathew katu hawezi kufanya
kitu kama hicho” akasema
Nawal na Gosu Gosu
akamtazama kwa hasira halafu
akasema
“Nawal nitazame vizuri”
akasema Gosu Gosu na Nawal
akamtazama bila hofu.
“Gosu Gosu anataka
kufanya nini?akawaza Ruby
“Nimeishi msituni katika
mapigano makali toka nikiwa
na umri chini ya miaka
kumi.Kabla sijawa na maisha
haya unionayo sasa
nilichokuwa nakifahamu ni
bunduki ,risasi na kuua
tu.Muziki wangu ni milio ya
risasi na mabomu.Kwangu
mimi kutoa roho ya mtu ni
kama kunywa maji.Usinione
hivi mimi ni mkatili mno na
usijaribu kuingia katika anga
zangu utajuta na kumlaumu
mama yako kwa nini alikuleta
duniani” akasema Gosu Gosu
na kunyamaza kidogo
“Nimeanza na utangulizi
huo ili ufahamu umekutana na
watu wa namna gani.Mimi na
mwenzangu Ruby tunafahamu
kila kitu kuhusu ninyi.Mama
yako Habiba Jawad ni mfadhili
mkubwa wa ugaidi
duniani.Ndiye anayekifadhili
kikundi cha IS na makundi
mengine
mbalimbali.Tulifahamu hiki
alichokuja kukifanya Mathew
hapa Tanzania.Tulionana naye
akatueleza alichokuja
kukifanya.Tunataka kufahamu
wewe nini kimekuleta hapa
Tanzania?Kuna shambulio
lingine la kigaidi mnapanga
kulifanya Tanzania?Tueleze
tafadhali muda wa michezo
umeisha ! akasema Gosu
Gosu.Nawal akavuta pumzi
ndefu
“Sikiliza Nawal” akasema
Ruby
“Kwanza kuna kitu
ambacho wewe na hata mama
yako Habiba Jawad
yawezekana hamkifahamu
kuhusu Mathew.Amejiunga
nanyi na anafanya mambo ya
kigaidi lakini Mathew si gaidi
ni jasusi.Pili ni kuhusu
sisi.Mimi na huyu mwenzangu
Gosu Gosu ni wakurugenzi wa
idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi ijulikanyo kama
SNSA.Jukumu letu ni
kuhakikisha nchi inakuwa
salama.Tunafahamu wewe
umetoka katika familia ya
kigaidi na umekuja hapa
Tanzania kwa malengo hayo ya
kufanya ugaidi.Nawal kwa
ufupi tu nataka ufahamu
kwamba umeingia katika
mkono wa serikali na
tutakuchukua kwa ajili ya
mahojiano hivyo nakushauri
tueleze kile kilichokuleta hapa
Tanzania.Huna sababu ya
kutuficha kitu kwani
tunafahamu kila kitu kuhusu
Habiba Jawad.Tuanzie hapo
Nawal nini umekuja kukifanya
hapa Tanzania? Akauliza
Ruby.Nawal
akatabasamu.Gosu Gosu
akaonekana kukasirishwa na
kitendo kile cha Nawal
kutabasamu alipoulizwa
swali,akasimama
“Tunachokifanya hapa ni
mzaha?akauliza Gosu Gosu
Ruby akawahi kumshika
mikono kwani tayari mkono
wa kulia ulianza kuinuka
“Jizuie GosuGosu !
akasema Ruby
‘Msinielewe vibaya ndugu
zangu.Nimetabasamu baada ya
kugundua kwamba nimefika
mahala nilipopahitaji mno”
akasema Nawal.Ruby na Gosu
Gosu wakatazamana
“Hatujakuelewa Nawal
unamaanisha nini unaposema
umefika mahala ulipopahitaji?
Akauliza Ruby
“Chloe Bennet.Ndilo jina
langu halisi” akasema Nawal
na kuwasimulia akina Ruby
historia yake hadi alivyofikia
kuolewa na Ammar Nazar.
“Oh my God ! Ama kweli
dunia hii imejaa siri.Kumbe
huyu mwanamke naye ni
jasusi dah ! Gosu Gosu
akashangaa
“Nikiwa kwa Ammar
Nazari ndipo nilipokutana na
Mathew ambaye kwa wakati
huo alikuwa anatumiwa na
Mossad kwa lengo la kumsaka
Habiba Jawad akifahamika
kama Abu Zalawi.Nilijenga
naye mazoea na baada ya
kufahamiana vizuri
nikamfahamisha kuwa mimi
pia ni jasusi na nilikuwa pale
katika misheni maalum”
akasema Nawal na
kuwasimulia akina Ruby
kuhusiana na safari ya Mathew
hadi alipofika pale kwa Ammar
Nazari na kujiunga na kikundi
kile cha wanamgambo.Ruby
alilengwa na machozi baada ya
kuelezwa mambo aliyoyapitia
Mathew
“Sikujua kama Mathew
ameteseka namna hii” akawaza
Ruby
“Israel walifahamu
maficho ya Ammar
wakayashambulia lakini kwa
bahati nzuri mimi na Mathew
tulifanikiwa kutoroka na hapo
ndipo tulipoanza kumsaka
Habiba Jawad.Haikuwa kazi
rahisi kumfikia Habiba”
akasema Nawal na
kuwasimulia akina Ruby safari
ngumu waliyopitia hadi
kumfikia Habiba Jawad.
“Baada ya kufika kwa
Habiba misheni ya kumuua
ikabadilika na tukajikuta
tukiungana naye.Mimi
niliolewa na mwanae anaitwa
Abu Dahir na Mathew
akamuoa mtoto mwingine wa
Habiba anaitwa Najma
ambaye ndiye alikupigia simu
kukuuliza kama unamfahamu
Abu Zalawi” akasema Nawal
“Kitu gani kiliwapelekea
mkabadili misheni mliyokuwa
nayo ya kumuua Habiba
wakati mkifahamu fika ni
mfadhili mkuu wa ugaidi?
Akauliza Gosu Gosu
“Tulipofika kwa Habiba
kwanza tayari alikuwa
anatufahamu sisi ni akina
nani.Kupitia vyanzo vyake
aliweza kufahamu sisi ni
majasusi na lengo letu lilikuwa
ni kumuua.Alitueleza bila
kutuficha kwamba tulikuwa
pale kwa ajili ya kumuua na
akatutaka tusiendelee na
mipango yetu kwani ana
malengo mazuri na sisi na
ndipo misheni ilipobadilika
tukajikuta tukiingia katika
familia yake.Kwa ufupi tu
Habiba Jawad ni tofauti na
watu wanavyomfikiria.Baada
ya kuwa naye karibu tumepata
bahati ya kumfahamu vizuri na
yawezekana msinielewe lakini
ni mtu wa tofauti na wengi
wamjuavyo” akasema Nawal
na sura ya Gosu Gosu
ikaonekana kubadilika
“Mtu wa
tofauti?Anafadhili makundi ya
kigaidi na kuua watu halafu
unatuambia ni mtu wa tofauti?
Habiba ni muuaji mkubwa
kwani bila yeye makundi haya
ya kigaidi yasingeendelea
kuwepo na kustawi ! akasema
Gosu Gosu
“Usemayo ni kweli Gosu
Gosu lakini nina sababu ya
kusema kwamba Habiba ni
mtu wa tofauti na wengi
mnavyomdhania.Niwape
mfano mdogo.Miezi kadhaa
iliyopita mtu mmoja
aliyefahamika kama James
Kasai akishirikiana na kundi la
IS walifanya mauaji makubwa
hapa Tanzania ambapo wake
kadhaa za marais waliuawa.Ni
Habiba Jawad aliyemuwezesha
Mathew kumpata na kumuua
James Kasai.Mnalifahamu
hilo? Akauliza Nawal.Gosu
Gosu na Ruby wakatazamana.
“Naamini hamkuwa
mkilifahamu hilo.Huo ni
mfano mdogo tu kuhusu
Habiba Jawad.Bila yeye
Mathew asingeweza
kufanikisha kumpata James
Kasai” akasema Nawal
“Sasa nimepata picha
kamili.Wakati wa operesheni
ile ya kumsaka James
Kasai,Mathew alikuwa
anazungumza na mtu simuni
kila usiku na kila walipomaliza
mazungumzo yao alikuwa
anakuja na taarifa
mpya.Kumbe alikuwa
anazungumza na Habiba
Jawad.Nadhani ndiyo maana
alinikataza nisimfuatilie ili
nsigundue kama alikuwa na
mashirikiano na Habiba
Jawad” akawaza Ruby
“Habiba Jawad” Nawal
akaendelea
“Anatumika tu kufadhili
makundi ya kigaidi lakini wapo
wahusika wakuu wa ufadhili
huo nyuma yake” akasema
Nawal na kuwapa maelezo
marefu akina Ruby kuhusiana
na idara ile ndogo ndani ya
CIA ambayo ni maalum kwa
mashirikiano na makundi ya
kigaidi lakini akina Ruby
hawakuonekana kushangaa
sana
“Usiku wa kuamkia jana
tulionana na Mathew na
akatueleza kuhusiana na hiyo
idara na mahusiano yake na
hiki kinachoendelea hapa
nchini kwa sasa na akatusaidia
pia kutuelekeza mahala walipo
magaidi wa IS ambao
wanatumiwa kuchochea
vurugu ambao tumewakamata
tunaendelea kuwahoji.Katika
mazungumzo yetu alikwepa
sana kutueleza kuhusiana na
kile alichokuja kukifanya hapa
Tanzania ambacho ni kulipua
ubalozi wa Marekani hadi leo
asubuhi ilipotangazwa
kwamba amekamatwa jijini
Nairobi akituhumiwa kuwa
ndiye aliyelipua ubalozi ule.
Nataka kufahamu ni misheni
gani aliyonayo Mathew hadi
akalipua ubalozi ule wa
Marekani? Akauliza Ruby
Nawal akawaeleza kwa
kina kuhusiana na misheni
ambayo Mathew anaendelea
nayo iliyompelekea alipue
ubalozi wa Marekani.Gosu
Gosu na Ruby wakabaki
vinywa wazi.
“Oh Mungu wangu ! Kwa
nini Habiba akamuhusisha
Mathew katika jambo hili? Hii
ni misheni ya hatari sana na
lengo lake ni ili Mathew auawe
kwani uwezekano wa kumaliza
salama misheni hii ni mdogo”
akasema Ruby
“Nakubaliana nawe Ruby
kwamba misheni hii ni ngumu
na ya hatari kubwa sana
yawezekana ni misheni ngumu
kuliko zote alizowahi kupitia
Mathew na Habiba
analifahamu hilo lakini ilikuwa
lazima Mathew aifanye”
akasema Nawal na kuwaeleza
akina Ruby umuhimu wa
misheni ile anayokwenda
kuifanya Mathew.
“Naamini mmeona
umuhimu wa Mathew
kushiriki katika misheni hii”
akasema Nawal na Ruby
akatikisa kichwa
“Japo ni misheni ya
muhimu sana hasa kwa nchi
yetu na dunia kwa ujumla
lakini ni misheni ya kifo”
akasema Ruby
“Jukumu letu ni
kumuombea ili aweze
kumaliza misheni hiyo akiwa
salama kabisa” akasema Nawal
“Nawal umesema wewe ni
jasusi wa CIA.Unaweza
kuwasiliana na wenzako na
kufahamu mahala alipo
Mathew hivi sasa? Nataka
kujua kama bado yuko Nairobi
ili tufanye mipango ya
kumuokoa kwani misheni hii
ni mbaya mno na tunaweza
kumpoteza” akasema Gosu
Gosu
“Nikurekebishe Gosu Gosu
kwa sasa siko tena
CIA.Nilipoamua kuolewa na
Abu Dahir ulikuwa ni mwisho
wangu na CIA na mpaka sasa
hawajui niko wapi hivyo sina
mawasiliano na watu wa
CIA.Jambo lingine hata kama
ningekuwa bado CIA
nisingeweza kufahamu mahala
alipo Mathew kwa kuwa ni
misheni ya siri kubwa.Tatu
hata kama tungefahamu
mahala alipo hatuwezi kwenda
kumuokoa Mathew kwani yeye
mwenyewe ametaka kuifanya
misheni hii kwa kuelewa
umuhimu wake.Nawashauri
ndugu zangu kitu kikubwa kwa
sasa ni kuendelea kumuombea
tu Mathew ili akamilishe
misheni hii akiwa
salama.Binafsi nina uhakika
kwamba atamaliza na atakuwa
salama.Nawaomba na ninyi
muwe na uhakika huo.Msiwe
wepesi kuamini kwamba
Mathew ni gaidi.Ameingizwa
katika ugaidi kwa malengo
maalum lakini ukweli utabaki
pale pale kwamba Mathew ni
jasusi na hata siku moja
hawezi kuwa
gaidi.Tumeelewana katika
hilo?akauliza Nawal
“Hata yeye mwenyewe
alitueleza hivyo kwamba
tusiamini kile tutakachokisikia
juu yake.Tunamfahamu
Mathew,tumekuwa naye muda
mrefu na
tunamuamini”akasema Ruby
“Vizuri.Huo ni upande
mmoja wa Mathew Mulumbi
ambaye anaendelea na
misheni yake” akasema Nawal
na kunyamaza kidogo
“Watu hawa ambao
wanaichezea dunia watakavyo
bado wana uchu na rasilimali
za Afrika.Ndugu zangu mimi ni
mmarekani lakini nina damu
ya Afrika.Baba yangu asili yake
ni Libya hivyo japokuwa
nimechanganya damu lakini
mimi bado ni mwenzenu mimi
ni mtoto wa Afrika na
dhumuni la kuja hapa ni
kuwasaidia ndugu zangu”
akasema Nawal.Ruby na Gosu
Gosu wakatazamana
wakatabasamu
“Karibu Afrika Ruby bara
lililojaa utajiri lakini likiongoza
kwa umasikini mkubwa kwa
sababu ya kunyonywa na hayo
mataifa makubwa.Madini
yanasombwa tunabaki na
mashimo makubwa,rasilimali
za misitu zinavunwa na utajiri
mwingine mwingi
unachukukuliwa na sisi
tunachoambulia ni misaada
kidogo,mikopo yenye masharti
magumu na silaha ambazo
tunazimia kuuana wenyewe
kwa wenyewe.Libya nchi
alikotoka baba yako amani
imetoweka.Kumekuwa na
mapigano kila
uchwao.Kinachoendelea Libya
kiko sehemu nyingi ya
Afrika.Mapigano ya wenyewe
kwa wenyewe na mingi ya
migogoro hiyo inasababishwa
na wanasiasa wanaogombea
madaraka.Viongozi hawataki
kung’oka madarakani na
mambo mengine mengi.Hiyo
ndiyo Afrika.Lakini mengi ya
haya niliyokueleza
ukichunguza chanzo chake ni
mataifa makubwa” akasema
Gosu Gosu
“Uko sahihi Gosu Gosu.
Mataifa makubwa yamekuwa
ni chanzo cha migogoro mingi
inayoendelea barani
Afrika.Nchi za kiafrika
hazikupaswa kuwa na
umasikini mkubwa kama
uliopo sasa” akasema Nawal
na Gosu Gosu akaingilia kati
“Tazama nchi kama
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo ni nchi yenye utajiri
mkubwa wa madini na
rasilimali nyingine lakini
imekuwa ni nchi masikini
kutokana na migogoro
isiyokwisha.Kila uchao
makundi ya waasi
yanaibuka.Ukijiuliza
yanatokea wapi? Wanatoa
wapi silaha ? Utapata jibu
kwamba kuna nguvu kubwa
kutoka nje ya Afrika” akasema
Gosu Gosu
“Mfano mwingine ni haya
machafuko yaliyotokea hapa
Tanzania na
Uganda.Yametengenezwa kwa
kusudi maalum.Wakati ninyi
mkigombana wao wanapata
nafasi ya kujipenyeza na
kuchukua kile wanachokihitaji
na sasa wanayabeba mafuta ya
Uganda mapipa kwa mapipa
bila kujali damu ya watu
inayoendelea kumwagika.Huu
ni ukatili mkubwa na aibu kwa
nchi kubwa kama Marekani na
ndiyo maana niko hapa”
akasema Nawal na kunyamaza
kidogo
“Baada ya mpango wao wa
kupata mafuta kufanikiwa sasa
wamenogewa na wanataka
kwenda mbali zaidi ya
mafuta.Wanataka kuingia
katika rasilimali nyingine
kama vile madini na mazao ya
misitu.Ili kulifanikisha hilo
lazima vikosi vya Marekani
vilivyopo hapa Tanzania
viendelee kuwepo kwa muda
mrefu na ikiwezekana
viongezwe zaidi hivyo basi
wameamua kuja na mpango
mwingine na safari hii
wanataka kuja kusambaza
kirusi hatari kitakacholeta
maangamizi makubwa”
akasema Nawal
“Kirusi?! Akauliza Ruby
kwa mshangao
“Ndiyo wanataka
kusambaza kirusi hatari
ambacho kiko kwenye
maandalizi hivi sasa”Nawal
akawaeleza kwa kina
kuhusiana na mkakati ule wa
kusambaza kirusi nchini
Tanzania halafu akainuka
akaenda katika sanduku lake
akalifungua na kutoa faili dogo
akatoa picha akampatia Ruby
“Anaitwa Sattar Sayf Al
Din” Akasema Nawal.Ruby
akazitazama picha zile halafu
akampa Gosu Gosu naye
akazitazama
“Ni nani huyu
mtu?akauliza Gosu Gosu
“Huyu anatokea kundi la
IS na ndiye anayekuja
kusambaza kirusi hicho hapa
Tanzania.Hivi sasa tayari yuko
Marekani akiandaliwa kwa
kazi hiyo” akasema Nawal.
“Hiyo ndiyo misheni
iliyonileta hapa
Tanzania.Nimekuja
kuhakikisha kwamba mpango
huo haufanikiwi na Tanzani
ainaendelea kuwa sehemu
salama.Kwa mara nyingine
tena ni Habiba Jawad ambaye
amenituma nije kutekeleza
mpango huu kwa siri.Nadhani
sasa mtaweza kuona ni kwa
nini hata Mathew aliamua
kushirikiana na huyu
mama.Hayakuwa maamuzi
rahisi kuamua kushirikiana
mtu ambaye kwa muda mrefu
tumekuwa tukiamini ni
mfadhili mkuu wa ugaidi
duniani”`
“Kwa nini Habiba anauma
na kupuliza? Akauliza Gosu
Gosu
“Nimekwisha waambia
sababu ya Habiba kufanya hivi
anavyofanya ni kwamba
anataka kukimaliza kikundi
kile kidogo ndani ya CIA
ambao wanasababisha haya
yote kutokea.Watu hao wasio
na huruma hata chembe ndio
ambao Mathew Mulmbi
amechagua kupita njia ngumu
yenye mateso makali ili
kuwafikia na kuwamaliza.Kwa
hili nathubutu kumuita Habiba
Jawad ni shujaa kwani
angeweza kuacha wakaendelea
na mipango yao na watu wengi
wakapoteza maisha lakini
amekataa kuendelea kuwa
mtumwa wa hawa watu,hataki
tena kuendelea kufadhili
mauaji ya watu wasio na hatia
na ndiyo maana anatutumia
mimi na Mathew
Mulumbi.Ndugu zangu
ninataka tushirikiane katika
hili.Peke yangu sintaweza”
akasema Nawal.Ruby
akamgeukia Gosu Gosu
“Gosu Gosu
unasemaje?Unamuamini huyu
mtu? akauliza Ruby kwa
Kiswahili
“Ruby nadhani
tungejadiliana kwanza
pembeni kabla ya kumpa jibu”
akasema Gosu Gosu
wakamtaka radhi Nawal
wakatoka mle ndani wakaenda
kusimama katika varanda.
“Umemsikiliza vyema
maelezo
yake.Umemuamini?akauliza
Ruby
“Kwa maelezo aliyoyatoa
kuna kitu kinaniambia
nimuamini japo lazima tuwe
na tahadhari sana
tunaposhirikiana na watu
kama hawa ambao wametoka
katika mzizi wa ugaidi”
akasema GosuGosu
“Nini ushauri
wako?Tushirikiane naye
au?akauliza
Ruby.Walijadiliana kwa muda
wa dakika kama tano hivi
kisha wakakubaliana
kushirikiana na Nawal halafu
wakarejea ndani
“Nawal tumekubaliana
kushirikiana nawe.Kama
nilivyokueleza awali kwamba
sisi ni viongozi wa idara
inayoshughulika kwa siri na
usalama wa ndani wa
nchi.Tunazo rasilimali za
kutosha kutuwezesha
kutekeleza hicho ulichokuja
kukifanya.Tunataka kujua je
huyu mtu anayeleta kirusi
anakuja lini?Anafikia wapi?
Tukifahamu hayo itakuwa
rahisi kwetu kufanya
maandalizi” akasema Ruby
“Kwa sasa bado sina
taarifa zozote lakini nategemea
kupata taarifa kutoka kwa
Habiba Jawad.Yeye anafuatilia
kila kinachoendelea kuhusiana
na mpango huo wa
kukisambaza kirusi.Kitu cha
kanza ninachohitaji ni kupata
mawasiliano ili niwasiliane na
Habiba Jawad” akasema
Nawal
“Mawasiliano
utapata.Lakini tungetaka
kufahamu kuhusu huyo mtu
anayekuja kusambaza kirusi
anakuja kwa kutumia njia
gani?Atakuja lini? Akauliza
Ruby
“Kama nilivyosema
kwamba ninategemea kupata
taarifa zote kutoka kwa Habiba
Jawad.Hatua ya kwanza
ilikuwa ni mimi kufika Dar es
salaam halafu nitawasiliana
naye na atanipa
maelekezo.Nisaidieni niweze
kuwasiliana naye na kama
tayari anazo taarifa
atanijulisha” akasema
Nawal.Ruby akampa Nawal
simu yake ili awasiliane na
Habiba Jawad.Nawal
akafungua sanduku lake
akatoa kijitabu kidogo
akaandika namba za Habiba
katika simu akapiga simu
ikaanza kuita baada ya muda
ikapokelewa
“Hallo”akasema Habiba
“Mama Habiba ni mimi
Nawal”
“Ouh Nawal.Nimefurahi
kusikia sauti yako.Tayari
umefika Tanzania? Akauliza
Habiba
“Ndiyo mama.Tayari
nimekwisha fika Tanzania na
tayari nimefika Dar es salaam
na tayari nimeonana na
Ruby”akasema Nawal
“Nafurahi kusikia hivyo
Nawal.Hautaweza kuonana na
Mathew kwani tayari
amekwisha anza misheni
yake.Jana usiku alilipua
ubalozi wa Marekani na leo
amekamatwa jijini Nairobi
hivyo kwa sasa mpango ule wa
kumpeleka Iran
unaendelea”akasema Habiba
“Tayari nimekwisha zipata
taarifa hizo mama.Imekuwa
bahati nzuri kwangu kwani
Ruby ni mkurugenzi wa SNSA
idara ya usalama wa ndani ya
nchi hivyo tutasaidiana katika
hilo zoezi”
“Ouh kweli ! Habiba
akashanga
“Ndiyo mama”
“Vizuri sana .Basi
saidianeni kuhakikisha
kwamba mnaokoa raia wa
Tanzania na dunia kwa ujumla
kwani kirusi hicho endapo
kikisambazwa basi kinaweza
kuvuka mipaka ya Tanzania na
kusambaa hadi sehemu
nyingine za dunia”
“Sisi hapa tuko
tayari.Kuna taarifa zozote
umezipata tayari kuhusiana na
Sattar Sayf Al Din?akauliza
Nawal
“Taarifa nilizo zipata ni
kuwa kirusi kinachotarajiwa
kuja kusambazwa Tanzania
kiko tayari lakini tatizo lililopo
ni kwamba wanasayansi bado
hawaja pata kinga
yake.Mpango ulikuwa kabla ya
kusambaza kirusi hicho lazima
iwe imepatikana kinga yake ili
kuwakinga wanajeshi wa
Marekani walioko Tanzania na
vile vile kuwakinga
wamarekani endapo kirusi
hicho kitavuka mipaka ya
Tanzania”
“Kwa hiyo
wameahirisha?akauliza Nawal
“Hapana
hawajaahirisha.Mpango uko
pale pale.Kwa mujibu wa
taarifa nilizozipata ni kwamba
kwa sasa vurugu zinaonekana
kupungua na hii imewapa hofu
hivyo wameamua kukisambaza
kirusi hicho hivyo hivyo bila
kinga yake kuwa tayari”
akasema Habiba
“Dah ! akasema Nawal
“Nawal kwa namna yoyote
ile hakikisha kirusi hiki
hakisambai Tanzania au katika
ardhi ya Afrika.Watu wengi
watakufa kwani hakina kinga
bado”
“Nakuhakikishia mama
kwamba kirusi hicho
hakitasambazwa hapa
Tanzania.Mipango yao ikoje?
Sattar Sayf Al Din anakuja lini
Tanzania? Akauliza Nawal
“Bado sijajua anakuja lini
lakini kwa taarifa nilizozipata
ni kwamba atakapofika
Tanzania Sattar atapokelewa
na mtu anaitwa Assad
Ismail.Huyu anaishi Mombasa
Kenya lakini nimetaarifiwa
kwamba kwa sasa yuko hapo
Tanzania na ndiye
atakayemsaidia Sattar katika
zoezi hilo la kusambaza hicho
kirusi.Ili kuweza kumpata
Sattar lazima umpate kwanza
Assad”akasema Habiba
“Umesema anaitwa Assad
Ismail?akauliza Nawal
“Ndiyo Assad Ismail”
akajibu Habiba na Nawal
akamgeukia Ruby
“Andika katika karatasi
Assad Ismail” akasema Nawal
“Huyu Assad nitampata
vipi hapa Dar es
salaam?Anaishi wapi?akauliza
Nawal
“Bado sijapata taarifa
kamili za mahala alipo lakini
hadi kufikia kesho mchana
nitakuwa nimejua wapi
unaweza ukampata”
“Mama ahsante kwa
taarifa hizi nitazifanyia kazi
kwa kushirikiana na wenzangu
niliowakuta hapa” akasema
Nawal
“Sawa Nawal.Naomba uwe
makini sana unapolishghulikia
jambo hili kwani ni mpango
wa siri wa taifa kubwa hivyo
lazima watakuwa wamechukua
kila aina ya tahadhari
kuhakikisha mpango wao huo
haukutani na vikwazo vya aina
yoyote.Nawal katika misheni
hii hakuna kitu kushindwa
umenielewa? Akasema Habiba
“Nimekuelewa mama”
akasema Nawal na kuagana na
Habiba.Nawal akawaeleza kile
alichoelezwa na Habiba
“Huyu Assad Ismail
Mathew alikwisha tupa taarifa
zake na tayari tumeanza
kumsaka.Huyu ndiye ambaye
amekuwa mchochezi mkuu wa
vurugu zinazoendelea.Kwa
kushirikiana na wenzake
wamekuwa wakiendesha
mauaji ya viongozi wa dini kwa
lengo la kuwafarakanisha
waumini wa dini
kushambuliana.Tayari tunao
watu wanaoshirikiana na
Assad unaendelewa
kuwahoji”akasema Ruby
“Mmekwisha pata taarifa
zozote za mahala alipo
Assad?akauliza Nawal
“Hapana.Tumewahoji
watu wale na mpaka sasa bado
hatujapata
chochote.Wamekuwa wagumu
sana kusema chochote.Kuna
mtu anaitwa Marwan ambaye
Mathew alituelekeza kwamba
ndiye anafahamu mahala alipo
Assad.Tayari
tumempata.Tumemfanyia
mahojiano lakini bado
hajafunguka” akasema Ruby
nawal akashusha pumzi na
kusema
“Nimeishi na magaidi kwa
miaka kadhaa ninawafahamu
vyema.Naweza kusema
kwamba tayari wameharibiwa
akili zao na wako tayari kufa
muda wowote.Kupata taarifa
kwa hawa watu si jambo la
mchezo inahitaji kutumika
nguvu kubwa.Kuwahoji
magaidi si sawa na kuwahoji
wahalifu wengine wa
kawaida.Magaidi ni watu
wanyama sana na
unapowahoji unapaswa nawe
uwe kama wao nadhani
mmenielewa ndugu zangu ”
akasema Nawal na Gosu Gosu
akamtazama Ruby
“Ruby nafahamu mimi si
mtanzania na wala si mtu wa
idara yenu lakini ni
mwenzenu.Nina ombi moja
kwako”akasema Nawal
“Omba Nawal”
“Ninataka kumuhoji huyo
Marwan ambaye Mathew
alielekeza kwamba ndiye
anayefahamu mahala alipo
Assad” akasema Nawal sura ya
Ruby ikaonyesha
kutokukubaliana na wazo la
Nawal
“Nawal yuko
sawa.Nilikwambia jambo hili
toka awali Ruby.Watu hawa
wanapaswa kuhojiwa tofauti
na watu wengine.Tupe nafasi
mimi na Nawal tuwahoji tena
wale jamaa.Nina uhakika kuna
kitu tutakipata kutoka kwao”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu sipendi
namna ulivyomfanyia
Marwan.Si…..”
“Ruby hii ni vita.Kila
mbinu lazima itumike kupata
taarifa.Tafadhali kwa mara ya
kwanza Ruby fumba macho
kuwa na moyo wa jiwe.Ruhusu
nguvu itumike kuwahoji hawa
magaidi ili tuweze kumpata
Assad ambaye lazima tumpate
kwa gharama yoyote” akasema
Gosu Gosu.
“Gosu Gosu kanuni za
idara haziruhusu matumizi ya
nguvu katika kuwahoji
watu.Ulichokifanya ni
kinyume na kanuni
zetu.Lazima tufuate maelekezo
yaliyotolewa katika kufanya
mahojiano na kupata taarifa
kutoka kwa watu tunaowahoji”
“C’mon Ruby.Huu si
wakati wa kufuata hizo kanuni
ambazo hazitoi
matokeo.Tazama kwa kufuata
kanuni hizo hizo mpaka leo hii
hakuna tulichokipata kutoka
kwa wale magaidi ! akasema
Gosu Gosu kwa sauti ya juu
kidogo
“Gosu Gosu mimi ndiye
kiongozi wa idara na ndiye
mwenye maamzi ya mwisho
hivyo siwezi kuruhusu
matumizi ya nguvu kubwa
kama ulivyofanya kwa
Marwan.Sikufurahi hata
kidogo kwa kile ulichokifanya !
Ruby naye akajibu kwa sauti
ya juu
“Kuna nini ndugu
zangu?akauliza Nawal baada
ya kuona Gosu Gosu na Ruby
wakibishana kwa kutumia
kiswahili
“Hakuna tatizo” akajibu
Gosu Gosu
“Kama hakuna tatizo
nadhani mmenielewa ombi
langu la kutaka niwahoji hawa
jamaa mliowakamata kwa
maelekezo ya Mathew.Si kazi
nyepesi kupata taarifa kutoka
kwa magaidi kama
nilivyowaeleza na wakati
mwingine inalazimu kutumia
nguvu kubwa”akasema Nawal
“Hapo ndipo kuna tatizo
Nawal.Idara yangu hairuhusu
matumizi makubwa ya nguvu
katika kuwahoji watu
tunaowashikilia”akasema
Ruby na Nawal akamtazama
kwa macho ya mshangao
“Ruby ni kweli hapo kuna
tatizo.Tazama” akasema Nawal
“Mimi si mtanzania lakini
nimekuja hapa kuwasaidia
watanzania na janga kubwa
linalowakabili.Katika
kulitimiza jukumu langu hilo
sintahitaji vikwazo vya aina
yoyote ile.Kirusi hicho
kikisambaa hapa Tanzania
halitakuwa janga la kwenu
pekee bali la kidunia hivyo
nalazimika kutumia kila njia
kuhakikisha kwamba mpango
huo wa kusambaza kirusi
haufanikiwi.Naomba
tushirikiane Ruby.Nafahamu
kila idara ina kanuni zake
lakini huu si wakati wa kufuata
hizo kanuni.Haya ni
mapambano ya kufa na
kupona.Lazima tuwe na
kanuni zetu wenyewe aidha
gaidi atoe siri au afe ! akasema
Nawal na kwa mbali Gosu
Gosu akatabasamu
“Nimempenda
Nawal.Huyu ndiye anayenifaa
kufanya naye kazi ! akawaza
Gosu Gosu
“Ruby kuna tatizo lolote
katika suala hilo? Akauliza
Nawal
“Hakuna tatizo lakini
itabidi tutafute sehemu
nyingine kwa ajili ya
kuwafanyia mahojiano hao
jamaa.Hatuwezi kutumia ofisi
za SNSA kwa jambo hilo”
“Hakuna tatizo.Tunazo
nyumba tatu kwa ajili ya kazi
hiyo hapa Dar es salaam
tutatumia moja wapo”
akasema Gosu Gosu
Kwa shingo upande Ruby
akiongozana na Nawal na Gosu
Gosu wakaondoka kuelekea
ofisi kuu ya SNSA
VICTORIA – SHELI SHELI
Mathew alianguka chini na
kupoteza fahamu kufuatia
kipigo kikali
alichopewa.Hakuwa
anatazamika usoni, alikuwa
amechafuka damu.Yote haya
yaliyokuwa yanaendelea
yalikuwa yakifuatiliwa na
viongozi wa CIA nchini
Marekani.Baada ya kupoteza
fahamu maelekezo yakatolewa
kwamba wampumzishe hadi
baadae.Mathew akaburuzwa
na kutolewa ndani ya kile
chumba akashushwa chini
zaidi na lango la chumba
kimoja likafunguliwa na
Mathew akarushiwa ndani ya
kile chumba akiwa bado
hajitambui kisha lango
likafungwa.Ndani ya kile
chumba kulikuwa na watu
sita.Watu wale walionekana
wachovu na waliokata
tamaa.Walikuwa na ndevu
nyingi na nguo chafu.Watu
wale sita kila mmoja alikuwa
amelala juu ya godoro dogo na
chumba kilikuwa na
mwangaza hafifu.Pembeni ya
kile chumba kulikuwa na
mlango wa choo na
bafu.Kulikuwa na meza ya
chakula iliyokuwa na viti
sita.Pembeni ya chumba
kulikuwa na meza ya kusomea
yenye viti viwili na juu yake
kulikuwa na vitabu vitatu vya
quran.
Baada ya Mathew kutupwa
mle ndani wote waliinuka
kutoka katika magodoro yao
wakamkazia
macho.Hawakumfahamu ni
nani.Mmoja wa wale jamaa
akainuka na kwenda
kumgeuza akamtazama na
kutikisa kichwa wa masikitiko
kutokana na hali aliyokuwa
nayo.Uso wake ulikuwa
umevimba na kuchafuka damu
“Hawa watu ni wanyama
sana” akasema huku akimvua
Mathew shati alilokuwa
amevaa wale wengine nao
wakainuka wakamfuata
“Ni mzima? Akauliza
mwingine
“Hana fahamu amepigwa
mno”
“Ni nani huyu
mtu?Amefanya nini? Kwa nini
aje aunganishwe nasi?
Mwingine akauliza
“Tumsaidie aweze
kuzinduka halafu atatueleza”
Haraka haraka wakaanza
jitihada za kumsaidia Mathew
aweze kurejewa na fahamu.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby akiwa na Gosu Gosu
na Nawal waliwasili katika
makao makuu ya SNSA
wakashuka garini na kuelekea
ofisini kwa Ruby ambaye
aliwataka Gosu Gosu na Nawal
wabaki mle ofisini yeye
akaelekea katika idara ya afya
kutazama maendeleo ya
Marwan.
“Idara kubwa sana hii na
nyeti kwa nchi.Haipaswi kuwa
na kiongozi mwoga
anayeogopa kufanya maamuzi
magumu” akasema Nawal
baada ya Ruby kutoka mle
ofisini
“Usijali Nawal.Tutapata tu
kile tunachokitafuta” akajibu
Gosu Gosu
“Sifahamu lugha yenu
mnayozungumza lakini wakati
mkizungumza niliona kama
vile Ruby anaonyesha wasi
wasi” akasema Nawal
“Ruby anajaribu
kuzingatia kanuni lakini kwa
hatua hii tuliyofika kanuni
hazina nafasi.Nakubaliana na
ushauri wako kwamba tuwe na
kanuni zetu wenyewe gaidi
aidha aseme ukweli au ateseke
hadi kufa” akasema Gosu Gosu
“Uliniambia kwamba
ulikuwa mwanajeshi? Akauliza
Nawal
“Ndiyo.Nilikuwa
mwanajeshi wa kikundi kimoja
cha waasi waliokuwa
wakipigana vita na serikali ya
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Nimekaa msituni toka
nikiwa mdogo kabisa
nikipigana vita”
“Ouh kumbe asili yako ni
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo?
“Ndiyo.Lakini kwa sasa ni
raia wa Tanzania” akajibu
Gosu Gosu na mlango
ukafunguliwa akaingia Ruby
“Marwan anaendelea
vizuri.Nimekwisha elekeza
apakiwe katika gari maalum
yeye na wenzake wawili kisha
tutawapeleka katika moja ya
nyumba zetu kwa ajili ya
mahojiano” akasema Ruby
“Ahsante sana Ruby kwa
kukubali kufanya maamuzi
haya magumu” akasema
Nawal.Gosu Gosu akatoka mle
ofisini na kwenda kukusanya
vifaa kwa ajili ya kuwasaidia
katika mahojiano yao na
kuvipakia garini.Marwan na
wengine wawili wakaingizwa
katika gari kisha wakaondoka .
“Gosu Gosu anafurahi kwa
kumpata mwenzake ambaye
anaonekana anapenda
matumizi ya nguvu katika
kutafuta taarifa.Sifurahi hiki
wanachokwenda kukifanya
kwani ni kinyume na kanuni
zetu na hata haki za
binadamu.Si kila wakati njia
ya mateso inakuwa na
manufaa.Watu kama hawa
kuna njia za kuwahoji kwani
tayari wamekwisha haribiwa
kisaikolojia hivyo inabidi
kuanza kwanza kuwarejesha
katika maisha ya kawaida
ndipo hapo unaweza ukapata
kile unachokihitaji kutoka
kwao.Sina hakika kama nguvu
itafanikisa kupata chochote”
akawaza Ruby wakiwa garini.
Iliwachukua dakika
hamsini na mbili kuwasili
katika nyumba ambayo
wangeitumia kuwahoji wale
magaidi.Nyumba ilikuwa giza
na walinzi walikuwa
wamejificha kwa ndani.Ruby
akawapigia simu akawajulisha
kuwa tayari wamefika na geti
likafunguliwa.Marwan na wale
magaidi wenzake wakaingiza
katika chumba wakiwa
wamefungwa vitambaa usoni
na mikono yao ikiwa
imefungwa pingu.Ruby
akaelekeza jenereta liwashwe
na maandalizi yakaanza.Nawal
na Gosu Gosu wakafanya
maandalizi ndani ya chumba
watakachokitumia kuwahoji
wale magaidi na walipokuwa
tayari magaidi wote watatu
wakaletwa ndani ya kile
chumba wakafunguliwa
vitambaa walivyokuwa
wamefungwa usoni .
“Hello Marwan ! akasema
Gosu Gosu baada ya
kukutanisha macho na
Marwan ambaye alionyesha
hofu kubwa
“Tumekutana tena siku ya
leo.Tutaendelea pale
tulipoishia siku ile” akasema
Gosu Gosu na kumuinua
Marwan akampeleka katika
kiti.Ruby hakuwemo ndani ya
kile chumba alikuwa
anafuatilia kinachoendelea
akiwa katika chumba kingine
“Huyu ndiye Marwan”
Gosu Gosu akamwambia
Nawal
“Asalaam alaikum
Marwan” Nawal akamsalimu
Marwan ambaye sura yake
ilionyesha hasira kubwa baada
ya kusalimiwa na Nawal
“Hata kama usipojibu
lakini tutaelewana tu” akasema
Nawal kwa lugha ya
kiarabu.Marwan kwa dharau
kubwa akamtemea mate.Gosu
Gosu aliyekuwa karibu
akainua mkono wake na
kumnasa Marwan kofi zito
“Taratibu Gosu Gosu.Hizi
dharau ni za muda tu
zitakwisha” akasema
Nawal,Gosu Gosu akamuinua
Marwan akamketisha kitini
“Marwan,naomba nianze
kwa kujitambulisha
kwako.Naitwa
Nawal.Nimekuwa katika kundi
la Ammar Nazari brigades
kama mke wa Ammar Nazari
naamini umewahi
kumsikia.Leo hii niko hapa
Tanzania kuzungumza
nawe.Kuna kitu kimoja tu
ambacho nakitaka kutoka
kwako.Wapi alipo Assad
Ismail? Akauliza Nawal kwa
lugha ya kiarabu.Marwan
akamtazama kwa hasira na
kusema
“Shetani wa kike
wewe.Kwa nini umetusaliti
kiasi hicho na kuungana na
hawa viroboto wasio na
thamani yoyote?
Nakuhakikishia utajutia hiki
ulichokifanya ! akasema
Marwan kwa hasira naye
akitumia lugha ya kiarabu
“Marwan ninarudia
tena,ninataka kufahamu
mahala alipo Assad
Ismail”akasema Nawal
“Fanya chochote
ukitakacho lakini siwezi
kukueleza chochote msaliti
mkubwa wewe ! akafoka
Marwan
“Gosu Gosu tuanze kazi
hadi atakapokuwa tayari
kusema ! akasema Nawal.Gosu
Gosu akamuinua Marwan
kutoka kwenye kiti
akampandisha katika kitanda
akamfunga vizuri kwa
mikanda mikononi na miguuni
“Hakuna mateso yoyote
mtakayonitesa
yatakayonipelekea nikafungua
mdomo wangu na kuwapa kile
mkitakacho ! akasema Marwan
“Usimjali Gosu Gosu
atasema tu ! akasema Nawal
kisha Gosu Gosu kwa nguvu
akaupanua mdomo wa
Marwan na Nawal akaingiza
mpira halafu akafungulia maji
na tumbo la Marwan likaanza
kujaa maji.Baada ya muda
akafunga maji na kuuchomoa
ule mpira.Marwan alikuwa
anaweweseka
“Wapi alipo
Assad?akauliza Nawal lakini
Marwan hakujibu.Nawal
akampa ishara Gosu Gosu
ambaye aliuinua mguu wake
wa kulia akaushusha katika
tumbo la Marwan ambaye
aliyatapika yale maji
yaliyokuwa tumboni.
“Tunaanza upya hadi
utakaposema mahala alipo
Assad ! akasema Nawal na
zoezi lile likaendelea
Mara nne tumbo la
Marwan lilijazwa maji na
kutapishwa lakini hakusema
chochote.
“Sijawahi ona mijitu
migumu kama hii ! akasema
Gosu Gosu
“Usichoke Gosu Gosu
atasema tu” akasema Nawal
kisha akaelekeza Marwan
atolewe pale kitandani
wakamfunga katika chuma
maalum kilichotengenezwa
mfano wa goli la mpira wa
miguu.Marwan alining’inizwa
akiwa mtupu .Alikuwa
amechoka mwili wake
haukuwa na nguvu
“Marwan kabla
hatujaendelea na zoezi la pili
nataka utueleze mahala alipo
Assad ! akasema Nawal lakini
Marwan hakufumbua mdomo
wake kusema chochote.Gosu
Gosu akapanga vipande vya
mbao chini ya miguu ya
Marwan akamwagia mafuta
“Mara ya mwisho
Marwan.Wapi alipo
Assad?akauliza Nawal lakini
Marwan aliendelea kutoa
matamshi kwa lugha ya
kiarabu.Nawal akampa ishara
Gosu Gosu akawasha kiberiti
na kutupia katika zile mbao
moto ukalipuka na kufikia
miguu ya Marwan ambaye
alishindwa kuvumilia akaanza
kupiga kelele kubwa kwa
maumivu makali aliyoyapata
baada ya moto kuanza
kuunguza miguu yake.
“Assad yuko wapi?akauliza
Nawal lakini Marwan hakujibu
aliendelea kulia
“Gosu Gosu akalegeza
mnyororo na Marwan
akashuka chini akiukaribia
zaidi moto ambao uliendelea
kuwa mkali.Kilio kikazidi
“Nitasema alipo Assad !
Mmoja wa wale magaidi
waliokuwamo ndani ya kile
chumba akasema baada ya
kuona mateso yale makali
aliyopewa Marwan.Gosu Gosu
akageuka na kumtazama kwa
hasira
“Tafadhali msiendelee
kumtesa Marwan nitawaeleza
kila kitu kuhusiana na mahala
alipo Assad ! akasema Yule
jamaa na Gosu Gosu
akapunguza ule moto.Bado
Marwan aliendelea kupiga
kelele za maumivu na sauti
ilielekea kumkauka
“Haya tueleze haraka alipo
Assad ama nitakupandisha
wewe kukuchoma na moto ule
! akafoka Gosu Gosu
“Nitawaeleza jamani
naomba msiendelee kumtesa
Marwan namna hii ! akasema
Yule jamaa ambaye alionekana
kuwa na umri mdogo tofauti
na wenzake
“Unaitwa nani? Gosu Gosu
akamuuliza
“Naitwa Jabir Hafidh”
akasema Yule jamaa
“Jabir una miaka
mingapi?akauliza GosuGosu
“Nina miaka ishirini na
mbili”
“Ana miaka ishirini na
mbili” GosuGosu akamwambia
Nawal kwani hakuelewa lugha
ya Kiswahili
“Kijana mdogo sana kwa
nini akaingia katika makundi
haya ya kigaidi” akasema
Nawal
“Jabir tueleze alipo Assad
na ninakuonya kama
ukitudanganya basi mateso
utakayoyapata ni makubwa
kuliko haya ya Marwan !
akasema Gosu Gosu
“Nitawaeleza ukweli”
akasema Jabir
“Mimi si mwenyeji wa Dar
es salaam lakini kuna sehemu
inaitwa Sarara.Pale kuna hoteli
moja ambayo bado
haijafunguliwa hapo ndipo
anapoishi Assad”
“Umewahi kufika mahala
hapo?akauliza GosuGosu
“Ndiyo nimewahi kufika
hapo nikiwa na Marwan kuna
vitu tulikwenda kuchukua kwa
Assad” akajibu Jabir.Gosu
Gosu akamweleza Nawal kile
alichoambiwa na Jabir
“Unamuamini?akauliza
Nawal
“Anaonekana anasema
ukweli” akajibu Gosu Gosu
“Sawa mshushe huyo
gaidi” akasema Nawal.Gosu
Gosu akazima ule moto halafu
akamshusha Marwan.Mlango
ukafunguliwa akaingia Ruby
moja kwa moja akaenda
kumtazama Marwan
“Ameungua vibaya mno
miguu yake” akasema Ruby
huku Marwan akiendelea
kugugumia kwa maumivu
makali
“Hakuna dawa yoyote ya
kumpunguzia huyu mtu
maumivu makali?akauliza
Nawal
“Hatuna dawa yoyote kwa
hapa hadi makao makuu ndiko
kuna kitengo cha tiba”
akasema Ruby
“Kwa hapa
tumemaliza.Tayari tumepata
kile tulichokuwa
tunakihitaji.Turejee makao
makuu tumuwahishe huyu
jamaa akapate matibabu”
akasema Gosu Gosu.Ruby
akawaita walinzi wa nyumba
ile wakambeba Marwan na
kumuingiza garini
wakaondoka kurejea makao
makuu.Safari ilikuwa ya kimya
kimya
“Japo tumefahamu alipo
Assad lakini hiki kilichofanyika
ni ukatili mkubwa
sana.Sijawahi kushuhudia
mateso ya namna hii yaani
mtu anachomwa taratibu
anaungua kama nyama.Dah !
akawaza Ruby
“Hawa jamaa wamekutana
wote wakatili.Gosu Gosu
namfahamu ni mkatili sana
lakini sikutegemea na huyu
mwanamke naye awe na
ukatili kama wa Gosu
Gosu.Nadhani ndiyo maana
yeye na Mathew walielewana
sana kwani hata Mathew naye
aina yake ya kufanya kazi ni
hivi hivi kutumia mateso
makali.Yawezekana labda
mambo haya ninayaona
mageni kwangu kwa sababu
mimi si jasusi lakini kwa hawa
waliosomea kazi hii kwao
wanayaona ni mambo ya
kawaida sana.Naanza kufikiria
labda na mimi yanipasa
kusomea mambo haya kwani
nimeingia kuongoza idara hii
nikiwa sina ujuzi mkubwa wa
mambo haya ya kijasusi.Baada
ya suala hili la vurugu
kumalizika nitaangalia kama
nitaweza kwenda kusomea
masuala haya ya ujasusi na
kuwa mjuzi kama huyu Nawal”
akawaza Ruby
Walifika katika ofisi zao na
kwa haraka Marwan
akashushwa akakimbizwa
upande wa afya ili kuanza
kupatiwa matibabu kwani hali
yake ilikuwa mbaya.Hakuweza
kuongea zaidi ya
kukoroma.Wale magaidi
wengine wakaenda kufungiwa
katika vyumba maalum vya
kuhifadhia
watuhumiwa.Ruby,Gosu Gosu
na Nawal wakaelekea katika
ofisi ya Ruby ambaye alikaa
katika kiti chake akainamisha
kichwa
“Ruby samahani kwa kile
ulichokishuhudia mle ndani
lakini ilibidi kutumia njia ile ya
mateso ili kuwafungua hawa
jamaa.Mambo kama yale ni ya
kawaida sana katika shughuli
hizi.Wakai mwingine inabidi
kujitoa ubinadamu ili kupata
taarofa za
muhimu.Utatusamehe kama
tuliku…...”
“Hakuna tatizo.Kitu
kikubwa ni kuwa tumepata
taarifa za muhimu
tulizozihitaji sana.Nini
kinafuata baada ya kupata
taarifa hizi?Tunavamia hoteli
hiyo alipo Assad?akauliza
Ruby
“Hapana.Hatuwezi
kuvamia hoteli hiyo hadi pale
tutakapojiridhisha ni kweli
Assad anaishi hapo.Hawa watu
si wa kuwaamini asilimia mia
moja” akasema Nawal
“Sawa.Kwa sasa ni usiku
hivyo zoezi la kufuatilia
nyumba ile kujua kama Assad
yuko mle ndani litaanza
asubuhi.Tunazo drone kubwa
ambazo huzitumia kufuatilia
mambo mbali mbali hapa Dar
es salaam tutaelekeza moja
katika nyuma ile na
kuchunguza kila
kinachoendelea lakini ushauri
wangu kama huyo jamaa
anayekuja kusambaza kirusi
anamtegemea Assad
kumsaidia kusambaza kirusi
hicho basi hatuna sababu ya
kumkamata Assad.Tuendelee
kumfuatilia Assad kimya
kimya na pale tukihakikisha
tayari amekwisha onana na
Sattar basi utakuwa ni wakati
wetu wa kuwatia nguvuni wote
wawili na kuchukua kirusi
hicho” akasema
“Hilo ni wazo zuri sana
Ruby.Tutafanya hivyo lakini
nina ushauri.Hili suala la
virusi liwe ni siri yetu sisi watu
watatu.Wasifahamu watu
wengine ili kuzuia kutokea
taharuki” akasema Nawal
“Ushauri mzuri.Gosu Gosu
mpeleke Nawal nyumbani
akapumzike.Amesafiri
kilometa nyingi na anahitaji
kupumzika.Kesho asubuhi
tunakutana hapa kuendelea na
kazi” akasema Ruby
“Vipi kuhusu wewe?
Akauliza Gosu Gosu
“Usihofu kuhusu mimi
.Nikimaliza kazi zangu
nitakwenda kupumzika pia”
akasema Ruby akaagana na
Nawal ambaye aliondoka na
Gosu Gosu