SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 5: EPISODE 1
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Msafara wa mke wa Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Millen Kelelo
uliwasili katika ukumbi
ambao mkutano mkubwa wa
wake za marais duniani
utafanyikia.Alipokewa na
meneja wa ukumbi ule kisha
Millen na ujumbe wake
wakaingia ndani kukagua
shughuli za maandalizi ya
ukumbi
zinavyokwenda.Walizunguka
sehemu mbali mbali za
ukumbi na kwa kiasi
kikubwa maandalizi
yalikuwa
yanaridhisha.Millen akatoa
maelekezo kadhaa kwa
meneja wa ukumbi ule
halafu yeye na ujumbe wake
wakaondoka wakaelekea
Swala hoteli moja kati ya
hoteli kubwa ya nyota tano
ambayo baadhi ya wageni
ambao ni wake za marais
watafikia.Hapo napo Millen
alipokewa na meneja wa
hoteli na kutembezwa
sehemu mbali mbali za hoteli
kujionea namna
walivyokuwa wamejiandaa
kuupokea ugeni ule mkubwa
kabisa.Maandalizi yalikuwa
makubwa na ya
kuridhisha.Millen na ujumbe
wake walizungukia baadhi
ya mahoteli mengine ili
kujiridhisha na maandalizi
na kikubwa hasa
walichokuwa wakikitazama
ni suala la usalama wa
wageni wawapo katika hoteli
hizo.Baada ya kumaliza
kuzungukia mahoteli,Millen
na msafara wake wakaeleka
katika soko kuu la bidhaa za
kiutamaduni ambako wageni
wanatarajiwa kupelekwa
hapo ili kutazama bidhaa
mbali mbali za utamaduni
wa mtanzania.Millen
alizungumza na
wafanyabiashara katika soko
hilo na kuwataka wajiandae
vilivyo kwa ugeni ule
mkubwa wa wake za marais
ambao watakwenda
kutembelea soko hilo na
kununua bidhaa mbali
mbali.Toka hapo sokoni
Millen alielekea moja kwa
moja katika ofisi za taasisi
yake ambako alikuwa na
mkutano na waandishi wa
habari.Kabla ya kuingoa
katika ukumbi kuzunguza na
wanahabari aliingia kwanza
ofisini kwake na baada ya
dakika kadhaa akajulishwa
kwamba kila kitu kiko tayari
na akatoka kwenda
kukutana na wanahabari.
Ukumbi wa mikuano ulio
katika jengo zilimo ofisi za
taasisi yake ulijaa waandishi
wa habari waliokuwa tayari
kusikiliza na kuwafikishia
wananchi kile ambacho mke
wa Rais alikusudia
kukisema.Kama kawaida
yake Milleen ambaye
tabasamu huwa halikauki
usoni akatoa kicheko kidogo
na kusema.
“Samahani sana kwa
kuwachelewesha ndugu
zangu” Wanahabari walitikia
lakini hawakusikika nini
walikiongea kwani walikuwa
wanazungumza kwa sauti ya
chini y kunong’ona.Millen
akaendelea
“Ndugu wanahabari
nimewaiteni hapa leo ili
kupitia kwenu watanzania
waweze kupata taarifa za
kile kinachoendelea
kuhusiana na maandalizi ya
mkutano mkubwa wa
kimataifa wa wake za marais
wa dunia unaotarajia
kufanyika hapa nchini mbili
zijazo.Mkutano huu ni
mkubwa na wa kipekee mno
ambao ni mara ya kwanza
unafanyika barani afrika na
utafanyikia hapa kwetu
Tanzania.Karibu wake za
marais wa nchi zote za dunia
wamepelekewa mwaliko wa
kuhudhuria mkutano huo na
asilimia themanini tayari
wamekwisha thibitisha
kushiriki katika mkutano
huo.Tunaendelea
kuwasiliana na wale
waliobaki ili kupata uhakika
kuhusu ushiriki wao lakini
naamini asilimia tisini na
tisa ya wake za marais
watahudhuria mkutano huo
mkubwa.
Ndugu wanahabari lengo
kuu la kuandaa mkutano
huu mkubwa hapa kwetu
Tanzania ni kujadili kwanza
mwanamke na mabadiliko ya
sayansi na teknolojia,pili
mwanamke na mabadiliko ya
tabia nchi na tatu ni
ongezeko la vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia kwa
wanawake.Kama wote
tunavyofahamu kumekuwa
na mabadiliko makubwa na
ya kasi ya teknolojia hivyo
tunataka kujadili tuone
katika mabadiliko hayo
mwanamke anasimama
wapi? Mwanamke anawezaje
kunufaika na mabadiliko
hayo ya teknolojia? Athari
zipi hasi anakumbana nazo
kufuatia mabadiliko hayo?
Ndugu wanahabari kuhusu
mwanamke na mabadiliko ya
tabia nchi naamini nyote
mnafahamu kuhusu
mabadiliko makubwa ya
tabia nchi yanayoendelea
kutokea sehemu mbali mbali
duniani na kwa kiasi
kikubwa kupelekea mfumo
wa maisha
kubadilika.Tutajadili kwa
kina changamoto anazopata
mwanamke katika
mabadiliko haya ya tabia
nchi na kutafuta majawabu
nini kifanyike na wake hawa
wa marais watakaporejea
katika nchi zao ambako
karibu kila mmoja anayo
taasisi yake watakwenda
kujikita katika kutoa elimu
katika yale ambayo
tutakuwa tumekubaliana
katika mkutano huo.Hayo ni
machache tu ambayo
tutayajadili katika mkutano
huo lakini mada ni nyingi na
tumewaawalika pia watu
kutoka mashirika mbali
mbali ya kimataifa
watahudhuria pia.
Ndugu wanahabari
itoshe tu kusema kwamba
mkutano huu ni mkubwa na
wa kipekee kabisa kuwahi
kufanyika nchini kwetu
hivyo ninapenda kuchukua
nafasi hii kuwaomba
watanzania tujiandae kwa
ugeni huu mkubwa unaokuja
nchini kwetu.Ukiacha faida
kubwa zitakazopatikana
kutokana na maazimio
yatakayotolewa na mkutano
huo lakini kuna faida
nyingine kubwa za
kiuchumi.Mkutano huo
utasaidia katika kuitangaza
nchi yetu kimataifa.Katika
kipindi chote cha mkutano
huo macho yote ya dunia
yataelekezwa Tanzania.Hiyo
ni fursa yetu ya kukuza
utalii kwa kutangaza vivutio
vilivyopo nchini
kwetu.Katika hilo wageni
hawa watakapomaliza
mkutano wao watapelekwa
kutembelea vivutio mbali
mbali vya kitalii vilivyopo
hapa nchini.Wengine
watapelekwa mbuga ya
Serengeti na wengine
watakwenda Ngorongoro na
katika sehemu nyingine
mbali mbali.Wakitoka huko
watakuwa ni mabalozi
wazuri wa kutangaza vivutio
vyetu na tunategemea idadi
ya watalii wanaotembela
hifadhi zetu kuongezeka
baada ya mkutano huo.Faida
nyingine ni kwamba wageni
hawa kila mmoja atakuja na
ujumbe wake hivyo wenye
mahoteli watafaidika.Ugeni
huu mkubwa pia
utatembelea sehemu mbali
mbali kama vile soko la
bidhaa za utamaduni pale
watanunua bidhaa mbali
mbali mbali za
wajasiriamali.Hizo ni faida
chache tu ambazo nimeweza
kuzielezea zitakazopatikana
kutokana na mkutano huu
lakini faida ziko nyingi hivyo
nawaomba watanzania hasa
wana Dar es salaam
muupokee ugeni huu
mkubwa na muhakikishe
mnanufaika na uwepo wa
wageni hao hapa Dar es
salaam.
Ndugu wana habari leo
nimefanya ziara ya
kuzungukia kutazama
maandalizi ya mkutano huu
yanavyokwenda na
nimeridhishwa na
maandalizi
yake.Nimezungukia ukumbi
utakaotumika kwa mkutano
na mikutano mingine midogo
midogo,nimezungukia pia
mahoteli ambako wageni
wetu watafikia na sehemu
nyingine mbali mbali na
kuridhika na maandalizi
mazuri yanayofanyika.Kwa
ujumla kila sehemu
wamekwisha jiandaa
kikamilifu kwa ugeni
huu.Naamini ndani ya siku
chache zijazo maandalizi yote
yatakuwa yamekamilika
Ndugu zangu lengo kuu
la kuwaiteni hapa leo ni
kuwapa taarifa hiyo
kuhusiana na maandalizi ya
mkutano huo mkubwa wa
wake za marais duniani na
ninaomba kupitia kwenu
taarifa ziwafikie wananchi
na muwaelemishe juu ya
faida zitakazopatikana
kutokana na mkutano huo
mkubwa.Nawashukuru sana
ndugu zangu kwa kufika
kwenu na ninawaomba
muendelee kuitika wito kila
pale tutakapowahitaji kwani
ili kufanikisha mkutano huu
tutawahitaji sana.Ahsanteni
sana ndugu zangu na
mchana mwema” akasema
Millen na kusimama kwa
ajili ya kuondoka lakini
mwandishi mmoja wa habari
akapaza sauti akitaka
kuuliza swali.Millen
akatazama saa ya mkononi
halafu akasema
“Ndugu zangu najua
mnayo maswali mengi
mnataka kuuliza lakini kwa
siku ya leo muda
hauniruhusu kwani nina
kikao tena sehemu nyingine
muda mfupi ujao.Nawaahidi
kwamba tutaandaa tena
mkutano mwingine na
nitajibu maswali yenu yote”
akasema Millen
“Mama naomba nikuulize
swali moja tu ! akaendelea
kusisitiza Yule
mwandishi.Millen
akatabasamu na kusema
“Sawa nitaruhusu swali
moja tu kwa niaba ya wote”
“Ahsante sana mama”
akasema Yule mwandishi wa
habari huku Millen akiketi
kusikiliza swali
“Mama umetutuma
tufikishe taarifa kwa
wananchi kuhusiana na
mkutano huo mkubwa na sisi
tutaifanya hiyo kazi kwani
kwani ni jukumu letu
kuhabarisha umma.Swali
langu ni hili.Miezi michache
iliyopita kulitokea matukio
ya mauaji ambayo
yalisababisha nchi za umoja
wa Ulaya kuwatahadharisha
raia wao wasifike au
wachukue tahadhari wawapo
hapa nchini.Wageni
wanaokuja ni wake za
marais nataka kujue je
serikali ya Tanzania
imejiandaa vipi kiusalama?
Akauliza Yule mwandishi
“Swali zuri sana ndugu
yangu.Ni kweli kulitokea
matukio kadhaa hapo siku za
nyuma ya mauaji ambayo
yalipelekea nchi yetu
kuchafuka kimataifa hata
hivyo serikali ya Tanzania
imechukua kila aina ya
tahadhari katika
kuhakikisha kwamba wageni
wote watakapofika hapa
nchini kuhudhuria mkutano
huo mkubwa wanakuwa
salama.Siwezi kuingia ndani
zaidi katika masuala hayo ya
kiusalama lakini itoshe tu
kuwathibitisha wananchi
kwamba nchi iko salama na
wageni wetu wote
watakaokuja watakuwa
salama wao na ujumbe wao
hadi
watakapoondoka.Nawaomba
vile vile ndugu watanzania
ulinzi wa amani yetu ni wetu
sote hivyo kama kuna mtu
atakuwa na taarifa za mtu
au kikundi chochote cha
watu watakaotaka kuvuruga
amani watoe taarifa mara
moja kwa vyombo husika ili
hatua stahiki ziweze
kuchukuliwa na kwa
haraka.Ahsanteni sana
ndugu zangu” akasema
Millen na kuinuka akatoka
huku akiwaacha waandishi
wa habari wakiwa bado na
kiu ya kutaka kuuliza
maswali.
Baada ya kumaliza kikao
na waandishi wa habari
Millen aliingia garini
akaondoka kurejea ikulu
“Mwandihishi Yule wa
habari ameuliza swali
muhimu sana.Usalama ni
kitu kinachopewa
kipaumbele kikubwa mno
katika mkutano huu ambao
lengo lake kuu ni
kuidhihirishia dunia
kwamba Tanzania ni nchi
salama kuishi,kuwekeza na
hata kutembelea.Serikali
imekwisha chukua kila aina
ya tahadhari katika
kuhakikisha mkutano huu
unafanikiwa lakini bado nina
hofu.Japo mambo yametulia
hivi sasa lakini naamini nchi
zile ambazo tuliingia katika
msuguano nazo hazitapenda
kuona mkutano huu
ukifanikiwa.Nchi hasa zile za
umoja wa Ulaya zikiongozwa
na Ufaransa ziliwatangazia
hadi raia wao wasifike
Tanzania au kuchukua
tahadhari za kiusalama
wawapo hapa,hawatapenda
kuona mkutano huu
ukifanyika na kufanikiwa
hivyo watafanya kila aina ya
juhudi kuhakikisha
hatufanikiwi.Huwa naingiwa
na wasiwasi sana nikiliwaza
hilo lakini Rais amekwisha
nihakikishia kwamba
usalama ni mkubwa na wa
kutosha kabisa.Ameniahidi
nisiwe na wasiwasi hivyo
lazima nimuamini” akawaza
Millen
Alifika katika makazi yao
ikulu na kuungana na mume
wake Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr
Fabian Kelelo katika chakula
cha mchana
“Vipi mambo
yamekwendaje huko
ulikotoka? Akauliza Dr
Fabian
“Mambo
mazuri.Maandalizi
yanakwenda
vizuri.Nimekagua ukumbi
ambao umekarabatiwa upya
na kwa asilimia tisini
umekamilika kuna sehemu
chache tu za kumalizia pia
nimetoa maelekezo ya
sehemu za
kurekebisha.Nimekagua pia
baadhi ya hoteli ambako
wageni watafikia kote kuko
vizuri wamejiandaa vya
kutosha.Nikatoka hapo
nikaenda kukagua soko la
bidhaa za utamaduni
ambako wageni watakwenda
kutembelea nako huko
maandalizi yako vizuri baada
ya hapo nikarejea ofisini
kuzungumza na wanahabari
nikawataka watoe elimu kwa
wananchi kuhusiana na
mkutano huu na umuhimu
wake.Kwa ujumla naweza
kusema kwamba kwa kiasi
kikubwa maandalizi
yanakwenda vizuri sana.Kila
idara inatekeleza majukumu
yake vizuri.Fabian
tumekaribia sana kuitimiza
ndoto yetu ya kuihakikishia
dunia kwamba Tanzania ni
sehemu salama” akasema
Millen
“Nashukuru kama kila
kitu kinakwenda
vizuri.Kama kuna chochote
kitakwama nieleze mara
moja” akasema Dr Fabian
“Kuna mwandishi mmoja
aliniuliza swali akitaka
kujua kuhusu usalama wa
wageni akitolea mfano
matukio yale ya mauaji
yaliyotokea wakati
ule”akasema Millen
“Ulimjibu nini?akauliza
Dr Fabian
“Nilimtaka
akawahakikishie wananchi
kwamba usalama ni mkubwa
na wasihofu”akajibu Millen
“Ulimjibu vizuri.Usalama
ni mkubwa sana.Kila aina ya
tahadhari imechukuliwa
katika kuhakikisha kwamba
kila mgeni atakayekuja
nchini kwetu kuhudhuria
mkutano huo anakuwa
salama.Vyombo vyote
vinavyohusika na ulinzi wa
taifa viko macho kuhakikisha
hakuna kitisho chochote cha
usalama kabla na baada ya
mkutano huo.Kwa sasa kila
siku jioni wakuu wa vyombo
vyote vya ulinzi hukutana na
kubadilishana taarifa za siku
nzima kuhusiana na
usalama.Kuhusu hilo usiwe
na wasiwasi wowote”
akasema Dr Fabian
Baada mapumziko ya
mchana Rais alirejea ofisini
kuendelea na majukumu
yake na mara tu alipofika
ofisini akampigia simu
Edwin Mbeko ambaye ndiye
aliyekuwa akikaimu nafasi
ya ukurugenzi wa idara ya
siri ya usalama wa ndani wa
nchi baada ya kifo cha Tamar
Axon
“Mheshimiwa Rais”
akasema Edwin kwa adabu
“Edwin habari za
mchana”
“Nzuri kabisa
mheshimiwa rais”
“Edwin,mke wangu
ametoka kufanya ukaguzi wa
maandalizi ya ule mkutano
mkubwa wa wake za
marais.Kwa ujumla
maandalizi yanakwenda
vizuri lakini nimekupigia
kukupa msisitizo uongeze
nguvu zaidi katika kubaini
kama kuna kitisho chochote
cha usalama kabla ya
mkutano huo.Vyombo vyote
vya ulinzi na usalama hivi
sasa macho yao
vimeyaelekeza katika
kuhakikisha mkutano huo
unafanyika kwa amani na
idara yako pia inaendelea na
jukumu hilo kwa siri lakini
nataka nguvu iongezwe
zaidi.Kipaumbele kikuu cha
idara yako kwa sasa kiwe ni
mkutano huu
mkubwa.Umenielewa Edwin?
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais”
“Ahsante sana” akasema
Dr Fabian na kukata simu
PARIS – UFARANSA
Devotha Adolph akiwa na
gari lake la kifahari
akiendeshwa na dereva wake
huku mbele kukiwa na gari
la walinzi wake aliopewa na
Rais Michale Weren
wamlinde,aliwasili katika
jumba kubwa anakoishi
Theresia Muganza ambaye
kwa sasa anajulikana kama
Melanie Davis.Mmoja wa
walinzi wake akawahi
kushuka katika gari na
kumfungulia mlango
akashuka akavaa kofia yake
nyeupe ya mduara akaanza
kutembea kuelekea ndani.
“Haya ndiyo maisha
ninayoyataka.Nataka
niheshimiwe,nataka niwe na
sauti nataka niwe na nguvu
ya kumuamrisha mwanaume
atii kile ninachokitaka.Huu
ni mwanzo tu,harakazi zangu
hazitakoma hadi nihakikishe
siku moja ninaingia katika
lile jumba jeupe pale Dar es
salaam.Lazima siku moja
niwe Rais wa Tanzania.Hii ni
ndoto yangu ya muda mrefu
na ninaamini siku moja
itatimia.” akawaza Devotha
wakati akipanda ngazi
kuingia ndani huku walinzi
wa jumba lile wakiwa
wamesimama kwa adabu
wakati akipita.Aliingia ndani
na kupokewa kwa furaha na
Melanie.
“Karibu sana
Devotha”akasema Melanie
na kumkaribisha Devotha
chumbani kwake
“You look tired”akasema
Devotha
“Sijui hata niseme nini
lakini toka nimekutana na
Gosu Gosu hakuna
kulala.Yule jamaa ana
minguvu kama
nyati.Akikukamata huwezi
kufurukuta hata kidogo”
akasema Melanie huku
akitabasamu
“Kuwa makini sana na
Gosu Gosu.Kama
nilivyokueleza kwamba he’s
a killer.Si mtu wa kuamini
wala kumfanyia masihara
anaweza akakutoa roho
sekunde yoyote” akasema
“Niko makini sana”
akasema Melanie
“Vipi muelekeo wake
hadi sasa?Unaweza kuwa na
uhakika kwamba tayari
umemuweka
mikononi?akauliza Devotha
“Naweza kukuhakikishia
kwamba tayari ameingia
mtegoni na amenasa.Hawezi
kutoka tena.Kwa yeye
kunipata mwanamke kama
mimi ni kama kuokota gari
lililojaa dhahabu.Mpaka sasa
haamini kama ameweza
kulala nami”akasema
Melanie
“Safi sana.Gosu Gosu ni
mtu muhimu sana katika
mpango huu.Lakini
hakikisha asifahamu kama
mimi na wewe tuna
mawasiliano.Hatakiwi
kabisa kujua kama niko hapa
Paris.Akijua kama tuna
mawasiliano mimi na wewe
kila kitu kitaharibika hivyo
kuwa makini sana”
“Mmewahi kuwa na
mahusiano?akauliza Melanie
“Hapana sijawahi kuwa
na mahusiano naye ila mimi
naye tumewahi kushiriki
katika misheni fulani na
hapo ndipo
nilipomfahamu.Sitaki
kueleza zaidi lakini siku zote
kumbuka huyu mtu ni hatari
na ukikosea kidogo tu
atavuruga kila kitu lakini pia
ni mtu muhimu sana
kwetu.Anao marafiki zake
wengine ambao unapaswa
kuwa muangalifu sana
nao,mmoja anaitwa Austin
January.Huyu ni mkuu wa
kikosi cha jeshi
kinachoshughulika na
operesheni maalum.Naye pia
ni mtu hatari.Kaa naye
mbali kabisa.Kuna mwingine
anaitwa Ruby.Huyu ni
mwanamke hatari.Si muuaji
bali anaitwa mchawi wa
kompyuta.Ana uwezo
mkubwa sana wa kucheza na
kompyuta.Huyu makazi yake
ni nje ya Tanzania hivyo si
mtu wa kuhofia sana lakini
ni hatari.Uwezo wake katika
masuala haya ya
mawasiliano unashangaza
mno.Hawa wote kiongozi wao
anaitwa Mathew Mulumbi”
akasema Devotha na
kunyamaza picha ya Mathew
Mulumbi ikamjia kichwani
akashusha pumzi na kusema
“Mathew Mulumbi ni
mtu mbaya mno lakini kwa
bahati nzuri kwa sasa
hayuko Tanzania na
hatarejea tena Tanzania na
yawezekana tayari
amekwisha fariki huko
mahala alikokuwa,hivyo mtu
wa kuchunga sana ni Gosu
Gosu.Anaweza kuwa na faida
kwetu lakini tukikosea
anaweza akawa na hasara
kubwa.Jitahidi sana kumpa
mapenzi mazito ili
achanganyikiwe” akasema
Devotha
“Usihofu kuhusu
hilo.Gosu Gosu hawezi
kufurukuta tena
kwangu.Ndani ya sku hizi
mbili nimekwisha maliza kila
kitu”akajigamba Melanie
“Good.Nimepokea taarifa
kutoka Tanzania kwa mtu
anaitwa Edwin Mbeko
ambaye ni mkuu wa idara ya
serikali inaitwa
SNSA,amenijulisha
maandalizi yote
yamekamilika”akasema
Devotha
“SNSA ni nini? Akauliza
Melanie
“Secret National security
agency.Hii ni idara ya siri ya
serikali ya Tanzania
inayojishughulika na
usalama wa ndani wa
nchi.Mimi ndiye
niliyeianzisha na ndiye
niliyekuwa mkurugenzi wake
wa kwanza.Baada ya mimi
akafuata Kaiza akaja Tamar
na sasa ni Edwin
Mbeko.Utakapofika
Tanzania umeandaliwa jina
lingine ambalo utakuwa
ukilitumia ambalo
litakutambulisha kama
mtanzania na utajulikana
kama Melanie Chuma.Hivyo
utakuwa na majina
mawili.Melanie Davis raia
wa Ufaransa na mwekezaji
aliyenunua mali zilizokuwa
zinamilikiwa na Mathew
Mulumbi ambaye amefariki
dunia,Vile vile kuna Melanie
Chuma ambaye ni mtanzania
mfanya biashara.Kutakuwa
na tofauti kati ya Melanie
Davis na Melanie
Chuma.Unapokuwa Melanie
Davis unakuwa kawaida
kama ulivyo sasa lakini pale
utakapohitaji kuwa Melanie
Chuma utafanya mabadiliko
kidogo katika mwonekano
wako.Kuna ngozi ndogo
imetengenezwa ambayo
utaibandika chini ya jicho
lako ikiwa na kidoti cheusi
halafu kuna ngozi nyingine
utaibandika pembeni ya
kidevu ikiwa na alama kama
kovu lililotokana na
kidonda.Vile vile kuna ngozi
utabandika katika vidole
vyako ili kubadli alama za
vidole kama kuna mtu
atahitaji kuchukua alama”
akasema Devotha na kutoa
mkebe kutoka katika mkoba
wake akaufungua.Ndani ya
ule mkebe kulikuwa na ngozi
hizo
alizozisema.Akamuonyesha
Melanie namna ya
kuzibandika
“Unapokuwa Melanie
Davis jitahidi sana
kuzungumza kifaransa kila
wakati na ikikulazimu
kuzungumza Kiswahili
utazungumza Kiswahili
kibovu ukidai kwamba bado
unajifunza.Ukiwa Melanie
Chuma utazungumza
Kiswahili safi kama
mtanzania.Kitu pekee cha
kuchunga ni Gosu
Gosu.Huyu amekufahamu
kama Melanie Davis na
kamwe asikutambue kama
Melanie Chuma hivyo basi
Gosu Gosu hapaswi hata
itokee nini kuingia ndani ya
chumba chako na wala
usimkaribishe katika
nyumba yako.Wafanyakazi
wako wa ndani watatoka
hapa hapa Ufaransa na si
wafanyakazi tu bali ni
majasusi ambao wamepewa
mafunzo maalum kukusaidia
lakini vile vile ni kuongeza
ulinzi kwako kuhakikisha
unakuwa salama na una
kamilisha kazi
uliyotumwa.Jambo lingine ni
kama alivyokueleza Rais
kwamba kuna watu ambao
watakuwa wakikulinda bila
ya wewe
kujua.Hawatajionyesha
kwako lakini fahamu kila
uendako watakuwa
wakikulinda.Utalindwa
angani na ardhini.Kila
unakoenda utaonekana na
utafuatiliwa.Mambo yote
kuhusu ulinzi umekwisha
elekezwa hivyo sitaki
kurudia tena.Tofauti
nyingine kuhusu Melanie
Davis na Melanie Chuma ni
makazi.Melanie chuma
atakuwa na nyumba
nyingine ambayo
imeandaliwa.Edwin
atakuelekeza kila kitu kwani
mambo hayo yote amekwisha
yashughulikia.Yatakuwepo
magari ya Melanie Davis na
Melanie chuma lengo kuwa
likiwa ni kuwatofautisha
watu hawa wawili.Hayo ni
machache tu ambayo
nimekuja kukukumbusha
kabla hujaondoka hapo kesho
mengine tutaendelea
kuelekezana pale
utakapokuwa Dar es
salaam.Kumbuka kujielekeza
katika misheni yako
uliyotumwa ambayo ni
kuhakikisha kwamba Afrika
Mashariki inasambaratika
na nchi ya Congo inabaki
peke yake ili iweze kuwa
rahisi kuliondoa genge la
watu wachache wanaotafuna
rasilimali za nchi hiyo vile
vile usisahau kwamba
misheni hizi zinajielekeza
moja kwa moja kwa
watawala wa nchi hivyo basi
ni misheni hatari sana na
ndiyo maana tumetumia
gharama kubwa kuziandaa
hivyo umakini mkubwa mno
unatakiwa lakini usihofu kila
hatua unayopiga sisi tuko
nyuma yako.Usisahau vile
vile kwamba watawala hawa
tunaowalenga ndio
waliowaua wazazi wako
hivyo hakutakuwa na hata
chembe ya huruma kwao”
akasema Devotha na Melanie
akashusha pumzi halafu
akasema
“Ni jukumu zito lakini
nitalifanya kwa ajili ya
wazazi wangu.Niliweka
ahadi kwamba hakuna
aliyehusika katika vifo vya
wazazi wangu atakabaki
salama lazima wote walipe
uovu wao.Hata hivyo nataka
kufahamu nini hatima yangu
mwisho wa misheni
hii?akauliza Melanie.
“Mwisho wa misheni hii
ni wewe kukalia kiti cha
urais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya
Congo.Unachokwenda
kukifanya hivi sasa ni
kutengeneza njia ya kuelekea
huko hivyo kaa ukijua
kwamba siku moja utakuwa
mtawala wa Congo na
utazitimza ndoto za mama
yako” akasema Devotha
“Sihitaji urais na
nimekwisha mueleza hata
Rais Michael.Sitaki kuwa
mwanasiasa” akasema
Melanie
“Nina uhakika maneno
hayo yatabadlika siku
moja.Hata mimi niliwahi
kuwa na mawazo kama hayo
wakati fulani nilichukia
siasa na wanasiasa lakini
kwa sasa nahitaji sana kuwa
Rais wa Tanzania”
“Unataka kuwa Rais wa
Tanzania? Melanie
akashangaa
“Ndiyo Melanie.Nataka
kuwa Rais wa Tanzania na
mipango hiyo
inaendelea.Pale jumuiya ya
Afrika mashariki
itakapovunjika basi
nitachukua urais wa
Tanzania.Wakati mimi
nikiwa Rais wa Tanzania
wewe utakuwa unaandaliwa
kuwa Rais wa Congo”
akasema Devotha huku
akitabasamu
“Kwa nini unataka kuwa
Rais wa Tanzania? Huogopi?
Akauliza
“Mimi siogopi kitu.I was
born a leader.Hii ni ndoto
yangu na lazima niitimize
kwa namna yoyote ile”
akasema Devotha
“Lakini Devotha kwa
haya unayoyafanya endapo
yakigundulika yatakuharibia
safari yako ya kuelekea ikulu
kwani utaonekana msaliti
kwa nchi yako”akasema
Melanie na Devotha
akacheka kidogo
“Kwanza hakuna
atakayefahamu.Mambo haya
ni mipango mikubwa na
ninaungwa mkono na nchi
kubwa za Ulaya.Ngoja
nikufahamishe kitu Melanie
Davis.Bara la Afrika ni tajiri
mno.Mungu ametupa mali
nyingi kuanzia mwanzo wa
bara hadi mwisho wake.Kila
sehemu ni utajiri aidha wa
madini ama wa vitu
vingine.Nchi zilizoendelea
kiviwanda kwa kiasi
kikubwa zinategemea
malighafi kutoka nchi za
Afrika ndiyo maana japo nchi
nyingi za Afrika zinajitawala
zenyewe zinafanya uchaguzi
wa viongozi lakini ukiangalia
wengi wa viongozi wa sasa
wanaochaguliwa katika bara
la Afrika kuna nchi tajiri
ziko nyuma yao ambazo
ziliwawezesha wakashinda
uchaguzi.Mimi ninaungwa
mkono na nchi kubwa za
umoja wa Ulaya hivyo
uhakika wa kuingia
madarakani ni
mkubwa.Siasa za Afrika
bado zimetawaliwa na nguvu
kubwa kutoka nje ya bara la
Afrika” akasema Devotha
“Endapo nchi za ulaya au
yoyote kubwa itakusaidia
ukaweza kuingia
madarakani hudhani
kwamba wanafanya hivyo
kwa ajili ya wewe
kuwasaidia kupata kitu
Fulani
wanachokihitaji?Hudhani
huo ni usaliti kwa nchi
yako?akauliza Melanie
“Umesaidiwa kupata
madaraka hivyo lazima kuwe
na malipo and I don’t
care.Ninachohitaji mimi ni
kitu kimoja tu ambacho ni
kupata madaraka” akasema
Devotha
“Sasa nimejua kwa nini
nchi nyingi za bara la Afrika
ni masikini japo Mungu
amezipa utajiri
mkubwa.Tatizo ni viongozi
wetu ambao wengi waliingia
madarakani kwa nguvu ya
mataifa makubwa ambayo
yanachohitajini kuchota
rasilimali huku nchi
zikiendelea kubaki
masikini.Hii ni laana na
ndiyo maana sipendi kuwa
mwanasiasa” akasema
Melanie
“Huyu mjinga anaongea
nini tena?Mbona anaanza
kubadilika? Akawaza
Devotha akichukizwa na
maneno yale ya Melanie
“Sikiliza Melanie.Hiki
kitu kilikuwepo,kipo na
kitaendelea kuwepo.Hata
mama yako kama angekuwa
Rais wa Congo zipo nchi
tajiri ambazo zilikuwa
nyuma yake na mojawapo ni
Ufaransa.Tuachane na hayo
masuala ya kisiasa
tujielekeze katika jukumu
kubwa lililoko mbele
yako.Fahamu umebeba
jukumu kubwa ambalo
mwisho wake ni kuisaidia
nchi ya Congo.Nenda
katimize ndoto za mama
yako ambaye alitaka kuiona
siku moja Congo ikinufaika
na rasilimali zake ilizojaliwa
na Mungu” akasema Devotha
“Nimekuelewa
Devotha,usiwe na hofu
yoyote.Kila kitu kitakwenda
kufanyika kama
kinavyotakiwa” akasema
Melanie
Walikuwa na
mazungumzo marefu
yaliyohusiana na operesheni
anayokwenda kuifanya
Melanie Afrika
Mashariki.Baada ya
mazungumzo yao Devotha
akaaga na kuondoka kwa
miadi ya kukutana tena siku
inayofuata ambapo Melanie
atakuwa akiondoka kuelekea
Tanzania
“Ama kweli maisha
yanaweza yakabadilika
ndani ya sekunde
chache.Sikuwahi kuhisi
kama siku moja ningeweza
kufikia hatua hii.Ndoto
yangu kubwa ilikuwa ni
kuwa mwanasayansi
mkubwa na nililenga siku
moja kufika hadi anga za juu
lakini leo hii niko hapa
nikiandaa mpango mzito wa
mauaji tena ya watu
wakubwa.Sikutaka kufikia
hatua hii lakini
nimelazimishwa niwe
hivi.Watu waliowaua wazazi
wangu wamenilazimisha
niwe mkatili na lazima niwe
mkatili.Hawakuona huruma
kutoa uhai wa wazazi wangu
na mimi sintaona huruma
kutoa uhai wao.Walikosea
sana kuniacha hai kama
wangejua wangenipiga risasi
ya kichwa nife pale pale”
akawaza Melanie na picha ya
tukio la mauaji ya wazazi
wake ikamjia
“Naamini huko waliko
waliopanga mauaji ya wazazi
wangu wametulia wakiamini
mambo yamekwisha bila
kujua kuna ziraili
anayeziwinda roho zao
anakuja.Narudia tena kuapa
hakuna aliyeshiriki katika
mauaji ya wazazi wangu
atakayebaki salama.”
akawaza Melanie
RIYADH – SAUDI ARABIA
Mathew Mulumbi
alifumbua macho baada ya
kusikia mlango wa chumba
alicholala
ukigongwa.Akainuka pale
kitandani na kuelekea
mlangoni akiwa katika
tahadhari kubwa.Hakuwa na
bastora hivyo ilimlazimu
kujihami kwa kutumia
mikono yake.Alipoufungua
mlango akakutana na jamaa
aliyekuwa na bunduki
akamsalimu na kumtaka
ajiandae kuna sehemu
wanaelekea.
“Nawal yuko
wapi?akauliza Mathew
“Yuko katika chumba
kingine.Yuko salama
usihofu” akajibu Yule jamaa
mwenye bunduki.
Mathew na Nawal
wakiwa wameongozana na
Fatma waliwasili katika jiji
la Riyadh Saidi Arabia
wakitokea Ramallah saa tisa
za usiku na moja kwa ,moja
wakaletwa katika nyumba
hii na kutokana na uchovu
waliokuwa nao Mathew
alijitupa kitandani na kulala
kama chatu aliyemeza mbuzi
hadi alipoamshwa na hodi ya
mlinzi aliyekuja kumuamsha
akimtaka ajiandae.
Mathew akaenda
dirishani akachungulia nje
walikuwa juu
ghorofani.Ilikuwa ni nyumba
nzuri yenye mandhari ya
kuvutia.Chini aliwaona
walinzi wanne karibu na geti
na wawili kati yao walikuwa
na bunduki
“Yawezekana hii ikawa
ni mojawapo ya nyumba za
Habiba Jawad.Ni nyumba
nzuri na ina ulnzi mkubwa”
akawaza Mathew na kuingia
bafuni akaoga.Baada ya
kuoga akakaa kitandani
akisubiri kile kitakachofuata
“Ammari Nazari tayari
ameondoka na sasa
anayefuata ni Habiba
Jawad.Haitakuwa kazi
nyepesi kumuua Habiba
lakini lazima auawe au
akamatwe.Baada ya hapo
nitaanza tena mpango mpya
wa kunirejesha Tanzania
nikaanze maisha mapya.Kwa
miaka hii mitatu nimepitia
mambo mazito mno ambayo
sijawahi kukutana nayo kwa
kipindi chote ambacho
nimekuwa katika kazi ya
ujasusi hivyo basi ni muda
wangu kuachana na kazi
hizi.Kwenye soka mtu
anapotaka kustaafu wana
msemo wao wanasema
anatundika daruga.Nataka
kutundika daruga ili nianze
maisha mapya na familia
yangu ambayo bado
wananihitaji sana.Watoto
wangu,mke wangu……”
Mara alipomkumbuka
Peniela akaikumbuka ile
picha aliyoiona Peniela
akiwa chumbani na Nahum
wakifanya mapenzi
“Picha ile itanitesa sana
kwa miaka mingi lakini
siwezi kumlaumu Peniela
kwa kuwa mimi ndiye
niliyesababisha haya yote
yakatokea.Kama
nisingekubali kuendelea na
kazi hii hivi sasa ningekuwa
karibu na familia yangu na
Peniela asingekuwa na Yule
mwanaume.Simlaumu kwa
kuwa anaamini tayari
nimekufa na sintoweza
kurudi tena ndiyo maana
ameamua kuendelea na
maisha yake.Ni vipi pale
atakapojua kwamba niko
hai?Atanipokeaje?Watoto
wangu watanipokeaje? Dah !
sifahamu nini kitatokea
lakini naomba Mungu
anisaidie waweze kunipokea
na kunikubali” akawaza
Mathew na kuinamisha
kichwa akisikitika.
“Ukitafuta mzizi wa
mimi kufika hapa ni
Peniela.Nilijikuta katika
misheni ya kumuokoa Olivia
ambaye nilikuwa natoka
naye kimapenzi kwa
siri.Lakini kwa nini nikatoka
na Olivia? Ni kwa sababu
Peniela ambaye ni mke
wangu alikuwa mbali
nami.Kwa muda mrefu
kumekuwa na tatizo la
umbali kati yetu.Peniela
amechukua uraia wa
Ufaransa na mimi siko tayari
kuukana uraia wangu wa
Tanzania na kuchukua uraia
wa nchi nyingine hiki
kimekuwa ni kigezo cha
kutufanya tuishi mbali mbali
kwa kipindi kirefu na ndiyo
maana nikajikuta
nikianzisha mahusiano na
Olivia.Kama Peniela
angekubali tukaishi
Tanzania haya yote
yasingetokea lakini haitaki
nchi yake alikozaliwa na
mimi siwezi kuwa raia wa
nchi nyingine kwani hakuna
sababu yoyote ya kunifanya
niukatae uraia wangu.Swali
linakuja kama nitafanikiwa
misheni yangu ya kumuua
Habiba Jawad na kurejea
nyumbani nini kitatokea?Je
mfumo wa maisha yangu
utabadilika?Je Peniela
atakubali kuishi Tanzania au
bado ataendelea na msimamo
wake wa kuishi Ufaransa?Ni
vipi kama akikataa kuishi
Tanzania nitalazimika
kubadili uraia na kuifuata
familia yangu Ufaransa?
Haya ni mambo ambayo
lazima niyatafutie
majawabu.Kama
hakutakuwa na muafaka
katika suala hili sijui nini
kitatokea” akawaza Mathew
na kuondolewa mawazoni
baada ya mlango kugongwa
akainuka akaenda
kuufungua.Alikuwa ni Yule
mlinzi akamtaka waelekee
katika chumba cha chakula
kwa ajili ya kupata kifungua
kinywa.Dakika mbili baada
ya kuingia katika kile
chumba akaingia Nawal
“Abu Zalawi” akasema
Nawal
“Nawal unaendeleaje?
Akauliza Mathew
“Ninaendelea vizuri.Vipi
wewe hali yako?
“Mimi niko vizuri ni
uchovu tu wa safari.Ilikuwa
ni safari ndefu sana ile”
akasema Mathew.
Walipata kifungua
kinywa kimya kimya wakiwa
wamesimamiwa na walinzi
wawili na baada ya kumaliza
Nawal akawaomba walinzi
wale kama watawaruhusu
waende wakapumzike juu ya
lile ghorofa.Walipanda juu ya
ghorofa lile na
wakaishuhudia mandhari
nzuri ya jiji la Riyadh kwani
jumba lille lilijengwa
kilimani.Hata wakiwa kule
juu ya ghorofa bado walinzi
wale wawili waliendelea
kuwalinda lakini walikuwa
mbali kidogo na kuwapa
uhuru wa kuzungumza
mambo yao
“Mathew katika chumba
nilimolala nimegundua kuna
kamera ya siri
imetegwa.Naamini hata
katika chumba chako
ulicholala ni hivyo
hivyo.Hawa jamaa
wanatutazama.Wanachungu
za kila tunachokifanya”
akasema Nawal
“Bado hawatuamini
ndiyo maana
wanatuchunguza.Safari ya
kuelekea kwa Habiba Jawad
bado ndefu.Fatma yuko
wapi?akauliza Mathew
“Fatma sijamuona toka
nilipoamka.Inaonekana
hakulala hapa alipotufikisha
akaondoka zake” akajibu
Nawal.
Ukimya ulipita Mathew
akiwa ameyaelekza macho
yake kutazama namna watu
walivyokuwa wakiendelea na
shughuli zao za kawaida
“Abu uko mbali sana
kimawazo.Unaogopa? Nawal
akauliza
“Hapana siogopi kitu”
“Nini kinakupa awazo
hayo mengi? Akauliza Nawal
“Nimeona namna watu
wale kule chini
wanavyoendelea na
majukumu yao ya kawaida
nikawaonea wivu.Natamani
sana kuishi maisha ya
kawaida kama wale watu
kule chini.Wana furaha na
amani wanaendelea na
maisha yao kama
kawaida.Tazama sisi hatuna
furaha hata kidogo.Tuko
hapa hatuko huru
tunalindwa na bunduki
kama wafungwa.Hatujui nini
hatima yetu,hatujui kama
tutaamka salama siku ya
kesho.Tunaishi maisha ya
mashaka.Kama Mossad
wasingweza kupata namba
yako ya simu wakakuonya
kuhusu mashambulio yale
waliyoyafanya katika kambi
ya Ammar hivi sasa
tungekwisha kuwa majivu
.Nimechoshwa na maisha ya
namna hii.Natamani kurejea
maisha yangu ya kawaida”
akasema Mathew
“Nimechoka
kabisa”akasema Mathew
akisikitika na kuinamisha
kichwa chini.Ulipita muda
kidogo Nawal akasema
“Wakati ninakuganga
majeraha yako nilisoma
maandishi uliyoyaandika
katika mgongo
yanayosomeka”People sleep
peaceably in their beds at
night only because rough
men stand ready to do
violence on behalf” akasema
Nawal na kunyamaza.
“Naamini ulikuwa na
sababu maalum ya
kuyaandika maneno yale.Sisi
ndio wale uliowataja ambao
hatulali ili kuhakikisha
wengine wanakuwa salama”
akasema Nawal
“Kinachonisikitisha zaidi
hakuna anayejua mateso
tunayoyapitia.Kwa mfano
hivi sasa hakuna anayejua
kama siku chache zilizopita
tumenusurika na mabomu ya
Israel.Hakuna anayejua
kama tuko hapa tunalindwa
na askari wenye
bunduki,hakuna oh Mungu
wangu..! akasema Mathew
na kuinamisha kichwa
akisikitika
“Zipo kazi nyingi ambazo
tungeweza kuzifanya lakini
tulichagua kazi hii kwa ajili
ya kuhakikisha nchi zetu na
ndugu zetu wanakuwa
salama.Watu ambao
tumeyatoa maisha yetu
kuwalinda hawapaswi kujua
kile tunachokifanya wala
kukipitia katika kuhakikisha
wao wanakuwa salama.Ni
Mungu pekee ambaye
anaona kile tunachokipitia
na atatulipa kwa mazuri
tunayoyafanya kwa nchi
zetu”akasema Nawal
“Nawal una bahati walau
nchi yako
inakuthamini.Mimi hakuna
anayenijali wala hakuna
anayesumbuka
kunitafuta.Inaniumiza sana
hasa nikiifikiria familia
yangu amabo hivi sasa
wanaamini tayari
nimekwisha fariki” akasema
Mathew
“Una familia? Nawal
akauliza
“Ndiyo nina mke na
watoto wanne”
“watoto wanne?
“Ndiyo” akasema Mathew
“Kwa nini basi
ukaendelea kujishughulisha
na shughuli hizi wakati
tayari una familia kubwa
namna hiyo? Akauliza Nawal
“Nilikwisha achana na
hizi kazi lakini kazi hii bado
iko damuni kwani kila mara
ninajikuta tena katika
misheni mbali mbali
zinazohusiana na nchi.Kwa
mfano kama ilivyoanza
misheni hii sikutegemea
kama leo ingenifikisha hapa”
akasema Mathew
“Nini kimekufikisha
hapa?
“Rafiki yangu alitekwa
nyara na kilichoniponza ni
kuamua kuacha shughuli
zangu na kumtafuta.Mambo
yote yalianzia hapo.Huwa
najilaumu sana kama
nisingekutana na Olivia
yasingenikuta haya
yaliyonikuta”
“Mkeo anaitwa Olivia?
“Hapana.Olivia ni rafiki
yangu wa kawaida lakini
nilikuwa natembea naye na
hii ilisababishwa na umbali
uliopo kati yangu na mke
wangu”akasema Mathew
“Uliponiambia kwamba
uliamua kuacha kila kitu
kwa ajili ya kumtafuta rafiki
yako aliyetekwa nilikuwa
najiuliza ni rafiki gani huyo
anayeweza akakufanya
ukajitoa namna hiyo kumbe
ni mtu wa karibu zaidi”
akasema Nawal huku
akitabasamu
“Vipi kuhusu wewe una
familia? Mathew akauliza
“Niliwahi kuwa na
mpenzi lakini ni mimi
niliyemuomba tuachane
kwani kwa kazi yangu hii
nisingeweza kuwa karibu
naye muda wote na sikutaka
kumkwaza hivyo basi
nikamuomba tuachane na
toka wakati huo sijawahi
kuwa na mpenzi hadi
nilipoingia katika ndoa na
Ammar Nazari”akasema
Nawal
“Unaweza ukanieleza
namna ulivyofika kwa
Ammar hadi ukaolewa
naye?akauliza Mathew na
Nawal akazama mawazoni
“Sipendi sana
kulizungumzia hilo jambo.Ni
moja kati ya mambo ambayo
yananiumiza sana kwamba
nilikubali kuwa mke wa mtu
katili na muuaji.Mke wa
gaidi.Lakini nilifanya hivyo
kwa ajili ya nchi
yangu.Haikuwa rahisi kuishi
ndani ya kundi la magaidi
ambao kila siku
wanachokipanga ni kutoa
roho za watu.Halikuwa
jambo rahisi kuishi na watu
ambao una hakika kwamba
wanaweza wakakugundua
muda wowote na pindi
wakikugundua basi adhabu
yake ni kifo.Nikiwa pale
tayari nilikwisha weka
sahihi ya kifo kwani nilijua
nikikosea kidogo
nitauawa.Haikuwa rahisi
kuishi bila kujua kama
utaiona kesho.Haikuwa
rahisi kumvulia nguo yangu
Yule gaidi ambaye hajui
mapenzi hata chembe.Ni
maisha ambayo sitaki
kuyakumbuka na
ninamshukuru sana Mungu
kwa kuniwezesha nimetoka
pale salama” akasema Nawal
“Pole sana Nawal”
akasema Mathew.
“Chloe ! akasema Nawal
na Mathew akageuza shingo
akamtazama.
“Chloe Bennet ndilo jina
langu.Nina damu ya kiarabu
mama aliniambia kwamba
baba yangu alikuwa na asili
ya Libya.Katika shambulio
lililofanywa na Abdul Yasin
Al Nasser baba yangu ni
mmoja wa watu waliouawa
ndio maana kwa kila namna
lazima nihakikishe
nimempata” akasema Nawal
na kunyamaza kwa muda
“Kama wewe
ulivyonikataza nisikuite
Mathew Mulumbi naomba
nawe usiniite Chloe
tafadhali.Endelea kuniita
Nawal” akasema Nawal
“Sawa ntafanya hivyo”
akajibu Mathew na wote
wakawa kimya kila mmoja
akiendelea kutazama watu
wakiendelea na maisha yao
ya kawaida mitaani
“Nini mpango wako
baada ya kukamilisha
operesheneni hii ngumu
uliyonayo? Akauliza Mathew
“Abu maswali yako
magumu.Sina mpango
mwingine.Nitaendelea
kufanya kazi hii ya ujasusi
kwani ndiyo kazi
ninayoipenda”
“Hujawahi kufikiria
kuachana na kazi hii na
kuwa na familia yako siku
moja? Akauliza Mathew
“Sina uwezo wa kuzaa
hivyo sifikirii kuwa na
familia.Niliomba kuondolewa
kizazi kwa kuhofia nisije
nikabeba mimba ya Yule
gaidi na kama nlivyokuwa
nimewaza ndiyo
ilivyokuwa.Kikubwa
ambacho Ammar alikuwa
anakihitaji sana kwangu ni
kuzaa naye
mtoto.Amejitahidi sana ili
niweze kubeba mimba bila
mafanikio na haifahamu siri
hii.Kwa upande mwingine
nawashukuru Israel kwa
kumuua kwani alikuwa
amepanga mwezi ujao
twende hospitali nikapimwe
kwa nini sipati
mimba?Angegundua siri
yangu angeniua.Ammar ni
mkatili mno zaidi ya
unavyofahamu” akasema
Nawal
“Kwa upande wangu
mimi kinachoniumiza kichwa
ni namna familia yangu
watakavyonipokea kwani
wanaamini tayari
nimekwisha
fariki.Wamekwisha endelea
na maisha yao na mke
wangu tayari ana mpenzi
mwingine.Ninawaza nini
kitatokea pale
nitakapojitokeza?Naamini
nitaharibu kabisa maisha
yao.Haitakuwa rahisi
kunikubali.Naamini watoto
wanaweza wakafurahi
kwamba nimerejea na
ninaweza nikawaeleza
kwamba taarifa ya kifo
changu haikuwa sahihi
lakini kwa mke wangu
haitakuwa rahisi.Hata kama
atanielewa maisha yetu
hayatakuwa kama zamani”
akasema Mathew na Nawal
akamtazama kwa huruma
“Tuachane na hayo kwa
sasa tujielekeze katika
misheni yetu.Katika simu
yako ulikumbuka kufuta zile
picha ulizopiga za
Ammar?akauliza Mathew
baada ya kumuona mmoja
wa wale walinzi wawili
akiwasogelea
“Niliwatumia CIA kisha
nikazifuta katika simu”
akasema Nawal.Yule mlinzi
akawataka warejee ndani
kila mmoja akatakiwa
kuingia katika chumba
chake.Akiwa ndani ya
chumba chake mlango
ukafunguliwa wakaingia
watu wawili,Mathew
akatakiwa kunyoosha
mikono yake akafungwa
pingu halafu akafunikwa
mfuko mweusi kichwani na
kuinuliwa akatolewa mle
chumbani
“Mnanipeleka
wapi?akauliza Mathew lakini
hakuna
aliyemjibu.Alishushwa ngazi
taratibu na kuingizwa katika
gari ambalo hakujua ni la
aina gani akasikia mlango
ukifungwa na gari
likawashwa
likaondoka.Hakujua
anapelekwa wapi.
“Nawal aliniambia katika
vyumba tulivyolala kulikuwa
na kamera za siri hawa
jamaa walikuwa
wanatuchunguza.Lakini hata
kama wakinichunguza
hawataweza kugundua
chochote kama mimi ni jasusi
badala yake watakutana na
taarifa kwamba mimi ni
gaidi niliyetoroka gerezani
nikiwa na Ammar Nazari
ambazo zimewekwa na
Mossad.Nadhani kuna
mahala ninapelekwa.Vipi
kuhusu Nawal?Kwa nini
yeye ameachwa?akajiuliza
Mathew
“Hii ni sababu kwa nini
Israel mpaka leo
wameshindwa kumpata
Habiba Jawad.Si rahisi
kumfikia.Kama ili kumfikia
inakupasa upitie taratibu
hizi basi hataweza
kupatikana.Nashukuru
walau nimepiga hatua katika
kufahamu mahala alipo
Habiba Jawad.Aombe kwa
miungu yake yote
anayoifahamu kwani siku
zake zinahesabika.Labda
niuawe kabla sijafanikiwa
kuonana naye” akawaza
Mathew Mulumbi huku gari
lilkienda kwa kasi.
Ilichukua mwendo wa
kama saa mbili gari lile
alilopanda Mathew
likasimama mlango
ukafunguliwa Mathew
akashushwa.Bado alikuwa
na mfuko
kichwani.Alichokuwa
anakisikia ni milango
kufunguliwa na kufungwa na
mwishowe akakalishwa
katika kiti mikono
ikafunguliwa pingu na
kufungwa kwa kamba nyuma
ya kiti halafu akasikia
mlango ukifungwa kukawa
kimya
“Nadhani wamenileta
hapa kwa mahojiano.Ee
Mungu nisaidie”akawaza
Mathew
Zilipita dakika kumi
akasikia hatua za mtu na
mlango ukafunguliwa
wakaingia watu zaidi ya
mmoja mle ndani.Akasikia
viti vikivutwa halafu sauti
ikaamuru avuliwe ule mfuko
kichwani.Mathew akajikuta
katika chumba kikubwa na
watu watano walikuwa
wamejipanga kuzunguka
meza kubwa.Pembeni
kulikuwa na walinzi wawili
wakiwa na bunduki
wakimlinda.
“Abu Al Zalawi assalamu
alaikum wa
rahmatullahi wa barakatuh”
akasema jamaa aliyejifunga
kilemba kichwani
akionekana ndiye mkuu wa
jopo lile.
“Wa alaykum s salam wa
rahmatullahi wa barakatuh”
akajibu Mathew
“Abu Zalawi karibu sana
Riyadh.Pole kwa safari ndefu
ya kufika hapa na pole sana
kwa yote
yaliyowapata.Utatusamehe
pia kwa namna
tulivyokuchukua na
kukufikisha hapa.Hizi ni
taratibu zetu za kawaida za
kuchukua tahadhari”
akasema Yule jamaa
“Jina langu naitwa Abdel
Fattah Sarraf” akasema Yule
jamaa aliyekuwa kiongozi wa
jopo lile.Mathew alikuwa
kimya akiwatazama
“Abu Zalawi tunaomba
utueleze wewe ni nani,
umetokea wapi na kwa nini
uko hapa?akauliza Abdel
Fattah
“Ee Mungu nisaidie huu
usiwe mtego nimewekewa na
hawa jamaa ili waweze
kunipima kama ninasema
kweli” akawaza Mathew
“Naitwa Abu Al
Zalawi.Ni mtoto wa Khalid
Al Zalawi na Dalia Sultan
ambao wotre tayari
wamekwisha tangulia mbele
za haki.Baba yangu Khalid
alikuwa ni mmoja wa
viongozi wa kundi la Abu
Hafs Al Masri,kundi
lililokuwa na mafungamano
na kundi la Alqaeda na
lilikuwa pia likisaidiana na
baadhi ya makundi ya
wanamgambo wa kipalestina
katika harakati za kudai
haki ya ardhi yao ndipo
alipouawa na vikosi vya
Israel.Kitendo cha baba
yangu kuuawa na Vikosi vya
Israel kilinipelekea na mimi
niingie katika vita dhidi ya
Israel.Nilikwenda Kenya
ambako ni asili ya mama
yangu nikaishi huko na
ndiko nilikoanzia harakati
zangu za kupambanana na
Israel.Nilimuua mkuu wa
Mossad Afrika mashariki
aliyeitwa Avi na majasusi
wengine wawili.Nikiwa
nchini Kenya nilifahamiana
na mtu anaitwa Rashid
ambaye alikuwa ni mfuasiwa
kikundi cha IS.Siku moja
Rashid aliniomba
nikamsaidie kufanya
mabadilishano kati yake na
vikosi vya serikali ya
Tanzania kwani IS walikuwa
wamemteka mtoto wa Rais
wa Tanzania na serikali ya
Tanzania nao kuna mtu
walikuwa wanamshikilia
ambaye IS walikuwa
wanamuhitaji.Rashid
aliniambia kwamba mtu
huyo ambaye anashikiliwa
na serikali ya Tanzania
anaitwa Edger Kaka na ni
mtu muhimu na wakaribu
mno kwa Habiba Jawad”
Mathew akanyamaza na
kuwatazama watu wale
wakiwa kimya kabisa
wakimsikiliza.Akaendelea
“Mabadilishano
yalifanyikia sehemu ya
mpakani mwa Tanzania na
Kenya na wakati
mabadilishano hayo
yakifanyika lilitokea
shambulio kubwa la
ghafla.Tulishambuliwa
kutoka kila upande na mimi
nilipigwa risasi tatu
sikuweza tena kukimbia
nikatekwa na watu hao
ambao walikuwa
wamefunika sura zao
nikapelekwa katika pango
lililokuwa karibu na mahala
pale.Nilipokuwa mle ndani
ya pango aliingizwa pia
Edger kaka ambaye ndiye IS
walikuwa
wanamuhitaji.Nilichomwa
sindano ya usingizi na
nilipozinduka nilijikuta
katika chumba chenye giza
na baadae nikagundua tayari
nilikuwa nimepelekwa nchini
Israel.Niliteswa sana
nikitakiwa kukiri kumuua
mkuu wa Mossad Afrika
Mashariki na kutaja
mtandao wa kigaidi
ninaoshirikiana nao.Miaka
mitatu ya mateso makali
lakini sikuweza kufumbua
mdomo wangu kuzungumza
chochote.Baada ya kuona
wameshindwa kunifanya
niongee waliamua kunifunga
gerezani wakanipeleka
katika chumba ambamo
kulikuwa na mtu
mmoja.Nilikuwa katika hali
mbaya nilikuwa na vidonnda
mwili mzima.Mtu Yule
aliyekuwa amefungwa ndani
ya kile chumba alinisaidia
nikaweza kupata nafuu na
ndipo nilipomfahamu mtu
Yule kama Ammar
Nazari.Nilitokea kuelewana
sana na Ammar na ndipo
tulipoanza harakati za
kuandaa mpango wa
kutoroka gerezani na
tukafanikiwa.Wakati
tukitoroka Ammar alipigwa
risasi mbili lakini sikuweza
kumuacha nilimbeba
tukatoka mle gerezani.Baada
ya kutoroka gerezani sikuwa
na sehemu ya kwenda
Ammar akanikaribisha
katika kundi lake nikajiunga
nao na tukaendeleza
harakati za mapambano
dhidi ya Israel.Mimi ndiye
niliyelipua lile bomu katika
kituo cha treni jijini
Jerusalem na kuua watu
wengi.Ammar aliandaa
sherehe kubwa kujipongeza
kwa ushindi ule dhidi ya
Israel lakini wakati sherehe
zikiendelea ndipo
tulipovamiwa na vikosi vya
Israel na kitu cha kwanza
alichokifanya Ammar ni
kuhakikisha familia yake
inakuwa salama.Alinitaka
mimi niondoke na Nawal na
kuhakikisha anakuwa
salama.Nilimchukua Nawal
na kumuondosha eneo lile
huku mashambulio ya
mabomu mazito ya Israel
yakiendelea.Nilimficha
Nawal ndani ya handaki
mlimani na mashambulizi
yalipokoma ndipo tukatoka
na akaelekeza twende
Ramallah kwa mtu aliyeitwa
Fatma ambaye alikuwa na
ukaribu mkubwa na
Ammar.Wakati nikiwa bado
gerezani ninateswa kule
Israel,niliwahi kupoteza
fahamu nikapelekwa katika
hospitali kubwa ya gereza
kutibiwa na huko
nilionyeshwa Edger kaka
akiwa katika chumba
maalum hana fahamu
amewekewa mashine za
kumsaidia
kupumua.Nilimueleza
Ammar kuhusu Edger kaka
akasema kwamba
tutakapotoka gerezani
atatafuta nafasi ya kukutana
na Habiba Jawad ili tuweze
kumpa taarifa hiyo kuhusu
Edger Kaka.Lengo kuu la
kumfuata Fatma ni
kumuomba atusaidie tuweze
kuonana na Habiba Jawad ili
nimpe taarifa za huyo mtu
wake muhimu Edger
Kaka.Nawal yeye alihitaji
msaada wa kutafutiwa
hifadhi baada ya mume wake
kuuawa.Fatma alitutafutia
hati za kusafiria na ndiye
aliyetufikisha hapa
Riyadh.Hiyo ndiyo historia
yangu kwa ufupi hadi
nimefika hapa kwenu”
akasema Mathew
“Abu Zalawi ahsante
sana kwa kutupa historia
yako ambayo inakuonyesha
wewe ni mtu shujaa.Hongera
kwa kulipua bomu lile juzi
katika kituo cha
treni.Hongera pia kwa
kufanikisha kumtoa gerezani
Ammar Nazari.Pamoja na
hayo yote uliyotueleza bado
kuna maswali machache
tungependa
kukuuliza.Umesema
kwamba uliwahi kujiunga na
kundi la Abu Hafs Al Masri
na…” Abdel Fattah
akakatishwa na Mathew
“Si mimi bali ni baba
yangu Khalid Al Zalawi
ndiye aliyekuwa mmoja wa
viongozi wa kundi hilo”
akasema Mathew.Abdel
Fattah akafungua moja ya
faili lililokuwa mezani
akasema
“Hili faili mbele yangu ni
la kikundi cha Abu Hafs Al
Masri brigades.Majina yote
ya viongozi wa kundi hilo wa
sasa na waliopita yamo
humu lakini sijaliona jina la
Khalid Al Zalawi” akasema
Abdel Fattah
“Yawezekana kuna
makosa katika hiyo orodha
lakini Khalid Al Zalawi
alikuwa mmoja wa viongozi
wa kundi hilo na aliuawa na
vikosi vya Israel.Kutakuwa
na makosa katika uandishi
wa orodha hiyo ya viongozi
kwani haiwezekani baba
yangu asiwemo katika
orodha hiyo” akasema
Mathew
“Orodha hii nimeipata
kutoka katika ofisi kuu ya
Abu Hafs Al Masri brigades
na hawamfahamu mtu huyo
anayeitwa Khalid Al Zalawi”
akasema Abdel Fattah
“Mambo yameanza
kuharibika.Nilipewa taarifa
hizi na Israel nizitumie na
wala mtu huyo Khalid Zalawi
simfahamu,hata historia
yake.Hawa jamaa
wanaonekana wanalifahamu
kundi hili vizuri na leo hapa
ninaumbuka.Lakini Israel
wasingeniopa taarifa zile
nizitumie kujiiunga na
magaidi bila kuzifanyia
kwanza
utafiti.Ninachohitajikukifany
akwa sasa ni kuwa na
msimamo
mmoja.Nikitetereka kidogo
hawa jamaa
watajuaninadanganya na
wataniua.Ee Mungu
nisadie”akawaza Mathew
“Abu Zalawi hebu tueleze
kidogo kuhusu baba yako
Khalid Al Zalawi,maisha
yake kabla hajauwa,mlikuwa
mkiishi wapi nchini
Misri?Marafiki zake wakuu
walikuwa akina nani?
Akauliza Abdel
Fattah.Mathew
akatabasamu kidogo na
kuuliza
“Nini maana
yake?Hamniamii hadi nitoe
maelezo hayo yote?
“Jibu swali uliloulizwa
Abu Zalawi” akasema Abdel
Fattah na Mathew
akachukau sekunde kadhaa
kuyakumbuka maelekezo
aliyopewa na Israel
“Khalid Al Zalawi
marafiki zake wakubwa
ninaowafahamu ni
Mohammed Atef kwa jina la
utani Hafs,vile vile alikuwa
na urafiki na Ayman
Mohammed Rabie al
Zawahiri.Marafiki zake
walikuwa wengi sana na
wengine siwafahamu kwa
majina.Khalid alishiriki
katika mashambuluo kadhaa
yaliyotekelezwa na kikundi
hicho cha cha Abu Hafs Al
Masri brigades kwa mfano
shambulio katika ofisi kuu za
umoja wa mataifa Baghdad
Iraq mwaka
2003,mashambulio ya
mabomu katika sinagogi
nchini Uturuki mwaka
2003,shambulio la bomu
katika hoteli jijini Jakarta
Indonesia 2003 na
mashambulio mengine
kadhaa” akasema Mathew
“Abu umejitahidi kutoa
maelezo lakini maelezo hayo
uliyotoa yanahusiana na
kundi la Abu Hafs Al Masri
brigades na si Kahlid Al
Zalawi ambaye unadai ndiye
baba yako.Huna maelezo ya
kumuelezea baba
yako?akauliza Abdel Fattah
“Nini mnakitafuta
kwangu?Hamniamini haya
niliyowaeleza? Mathew
akawa mkali
“Abu Zalawi,si kwamba
hatukuamini lakini tunataka
kujiridhisha na taarifa
uliyotupa kwani jina la
Khalid Al Zalawi halipo
katika orodha ya viongozi wa
kundi la Abu Hafs Al Masri
brigades hivyo tunapatwa na
wasiwasi kuamini kwamba
kweli wewe ni Abu Al
Zalawi”
“Mimi ni Abu Al Zalawi”
akasema Mathew
“Jina lingine la baba yao
alitwa nani?
‘Hakuwa na jina
lingine.Jina lake ni Khalid Al
Zalawi”akajibu Mathew
“Abu Zalawi hatuwezi
kukuamini kabisa kwa kuwa
mtu unayesisitiza ni baba
yako hatambuliki na
hajawahi kujiunga na kundi
la Abu Hafs Al Masri
brigades.Umetudanganya”
akasema Abdel Fattah kwa
ukali
“Sijawadanganya
nimewaeleza ukweli”
akasema Mathew.
“Umetudanganya”
akasema Abdel Fattah na
kufungua faili lingine
akamuonyesha Mathew
“Huyu mtu katika hili
faili ndiye Abu Al
Zalawi.Umechukua jina la
mtu mwingine.Ulidhani
hatutagundua?akauliza
Abdel Fattah kwa ukali
“Hapana
sijawadanganya.Jina langu
ni Abu Zalawi ! akasema
Mathew
“Umetudanganya.Abu Al
Zalawi si wewe bali ni huyu
ambaye faili lake tunalo
hapa.Abu Zalawi wa kweli
hahusiki katika masuala
yoyote ya ugaidi.Tunataka
utueleze wewe ni nani?
Akauliza Abdul Fattah
“Mimi ndiye Abu Zalawi”
akasema Mathew
“Abu tunataka utueleze
ukweli wewe ni
nani?Tunafahamu wewe si
Abu Zalawi hivyo tunataka
kujua wewe ni nani? Sema
ukweli”akasema Abdel
Fattah
“Mimi ni Abu
Zalawi.Sina jina
lingine”Mathew akaendelea
kusisitiza
Abdu Fattah akainuka
na kuwapa ishara wale
walinzi wawili wamtoe
Mathew mle
chumbani.Akavishwa mfuko
ule mweusi akatolewa mle
ndani na kuingizwa katika
chumba kingine mikono
ikafungwa katika pingu
zilizounganishwa na meza
nzito ya chuma mfuko
ukatolewa kichwani.Mathew
akakitambua kile chumba
kilikuwa chumba cha mateso
“Abu chumba hiki
nichumba cha mateso na
mara chache sana watu
hutoka salama
humu.Tunataka utueleze
ukweli wewe ni nani?
Ukisema ukweli wako
tunaweza kufikiria kukupa
adhabu nyingine kuliko ile
ambayo unastahili kuipata
kwa
kutudanganya.Tunauthamini
mchango wako kwa kulipua
lile bomu kwenye kituo cha
treni hivyo basi hatuoni
sababu ya kukutesa na
unaweza ukawa na msaada
mkubwa kwetu lakini endapo
utaendelea kusisitiza
kwamba wewe ni Abu Zalawi
wakati siye utaniudhi na
nitaamrisha nguvu itumike”
akasema Abdul Fattah
“Mimi ni Abu Zalawi”
akasema Mathew
“Nakuuliza kwa mara ya
mwisho wewe ni
nani?akauliza Abdul Fattah
“Mimi ni Abu Al Zalawi”
Mathew akaendelea
kusisitiza na mara mmoja wa
walinzi aliyekuwa
amesimama nyuma ya
Mathew akakishika kiganja
chake cha mkono akakiweka
mezani na kuzamisha kisu.
“Aaaaghhh !! Mathew
akatoa mguno wa maumivu
“Wewe ni nani?akauliza
Abdel Fattah
“Abu Zalawi ! akasema
Mathew kisu kikiwa bado
kimezama katika kiganja
chake cha mkono.Yule jamaa
akachomoa kile kisu na
damu ikaanza
kumwagika.Mathew akahisi
maumivu makali
“Wewe ni nani? Tueleze
ukweli ! akafoka Abdel
Fattah
“Nimekwisha waambia
mimi ni Abu Zalawi !
akasema Mathew damu
ikiendelea kutoka katika
kiganja chake cha mkono
mara akapigwa ngumi nzito
shavuni kabla hajakaa sawa
akapigwa tena ngumi
nyingine na damu ikaanza
kumtoka mdomoni
‘Tueleze wewe ni
nani?akaliza Abdel Fattah
“Mimi ni Abu Zalawi !
akasema Mathew kwa ukali
Mmoja wa wale jamaa
waliokuwa wakimtesa
Mathew akachukua kichupa
kidogo akakishika kiganja
cha mkono ule uliochomwa
kisu akamimina kimiminika
mahala penye jeraha na
Mathew akafumba macho
akigugumia kwa ndani
maumivu makali aliyohisi.
“Maumivu ni makali
lakini lazima nivumilie kwa
kutokuonyesha udhaifu
wowote” akawaza Mathew
“Jina lako nani?akauliza
Abdel Fattah
“Abu Zalawi ! akajibu
Mathew.Mkono wake wa
kushoto ukakamatwa kwa
nguvu na kuwekwa mezani
na Yule jamaa mwenye kisu
akakizamisha katikati ya
kiganja cha mkono.
“Wewe ni nani?akauliza
Abdel Fattah
“Abu Zalawi ! Mbona
hamnielewi ng’ombe ninyi?!!
Akasema Mathew akiwa
amepandwa na hasira huku
akihisi maumivu
makali.Kimiminika kutoka
katika kichupa kidogo
kikamiminwa mahala
alipochomwa kisu na
maumivu aliyoyapata
hayaelezeki lakini aliendelea
kuvumilia.
“Wewe ni nani?Sema
ukweli ili mateso haya
yamalizike” akasema Abdel
Fattah.
“Endeleeni kunitesa
lakini jina langu ni Abu
Zalawi ! akasema Mathew
Abdel Fattah akatoa
maelekezo mengine na
Mathew akavuliwa nguo na
kwenda kufungwa katika
wavu maalum.Akamwagiwa
maji na kisha Abdul
akashika nyaya za umeme
akazigusanisha zikatoa
cheche
“Tueleze wewe ni
nani?akauliza
“Abu Zalawi ! akasema
Mathew.Abdel akazigusisha
nyaya zile katika kile chuma
na Mathew akapitiwa na
chaji za umeme.
“Aaaagghhhh !!
akagugumia kwa maumivu
“Wewe si Abu Zalawi
tuambie wewe ni
nani?akauliza Abdel
‘Mtaniua jamani mimi ni
Abu Zalawi ! Mathew
akaendelea kusisitiza na
Abdel akagusisha tena nyaya
zile kwenye chuma na
kumuuliza tena Mathew jina
lake lakini aliendelea
kusisitiza yeye ni Abu
Zalawi.Akaamuru
afunguliwe akaenda
kufungwa katika meza na
ndoo ya maji
ikaletwa.Alifahamu kile
wanachokwenda kukifanya.
“Tueleze wewe ni
nani?Mateso haya
yataendelea hadi pale
utakaposema ukweli au la
utakufa !
“Mimi ni Abu Zalawi sina
jina lingine” akasema
Mathew na Abdel Fattah
akafanya ishara mateso
yaendelee.Mathew
akafunikwa na taulo usoni
halafu akaanza kumwagiwa
maji.Alihangaika kutafuta
hewa halafu taulo lile
likatolewa akakohoa
mfululizo
“Jina lako nani?
“Abu Zalawi ! akasema
Mathew na zoezi lile
likaendelea hadi ndoo nzima
ya maji ilipomalizika lakini
Mathew hakulegeza
msimamo wake aliendelea
kusisitiza yeye ni Abu
Zalawi.Abdul Fattah akatoa
tena maelekezo
mengine.Mathew
akachukuliwa na kufungwa
mikono nyuma kwa pingu
halafu akaenda kuwekwa
katika pipa,maji baridi
yakafunguliwa na kujazwa
hadi usawa wa kifua kisha
kukamiminwa dawa yenye
kuwasha na pipa lile
likafunikwa na mfuniko
uliokuwa na sehemu ndogo
ya kupitisha hewa kisha
watu wale wakaondoka
wakimuacha Mathew
akiwashwa mwili mzima
“Ee Mungu naomba nipe
nguvu ya kuhimili mateso
haya makali.Kama nitafariki
kabla sijatimiza malengo
yangu naomba unisamehe
makosa yangu yote,unifutie
adhabu zake na unikaribishe
katika ufalme wako.Najua
nimekukosea
sana.NImetenda dhambi
nyingi.Nimevunja amri
zako.Pamoja na yote
niliyokukosea lakini kuna
jambo moja tu ambalo
naamini nimelifanya kwa
ukamilifu mkubwa
nimeipenda nchi yangu ya
Tanzania kwa moyo wangu
wote sijawahi kuisaliti”
akafanya maombi ya kimya
kimya na kushindwa
kuendelea baada ya
muwasho kuzidi huku
akishindwa kujikuna kwa
kuwa mikono ilikuwa
imefungwa kwa nyuma.
“Je ni kweli Khalid
Zalawi hakuwahi kuwa
kiongozi katika kundi la Abu
Hafs Al Masri brigades?
Akajiuliza akia ndani ya maji
“Mossad ndio walionipa
taarifa zile nizitumie je
walinipa bila kufanya
uchunguzi na kuwa na
uhakika nazo? Hapana
wasingeweza kunipa taarifa
ambazo hawana uhakika
nazo.Naamini kabla ya
kunipa taarifa zile nizitumie
lazima walishafanya
uchunguzi wa kutosha
kujiridhisha kuhusu Khalid
Zalawi.Kama ni hivyo kwa
nini hawa jamaa
wanaendelea kusisitiza
kwamba mimi si Abu
Zalawi?Yawezekana kuna
kitu tayari wamekigundua
ndiyo maana wanataka
kufahamu mimi ni
nani.Nimejileta mimi
mwenyewe katika mdomo wa
Mamba.Sielewi yupi ni
mkweli kati ya Mossad na
hawa jamaa.Kitu cha
muhimu ni kuendelea na
msimamo wangu ule ule hata
wakinitesa vipi au hata
kama wakitishia kuniua
lazima niendelee kusisitiza
kwamba mimi ni Abu
Zalawi.” akawaza Mathew
“Watu hawa ni akina
nani?Fatma yuko
wapi?Nawal yuko wapi?
Akaendelea kujiuliza
maswali
Wakati Mathew akiwa
katika pipa lililojaa maji ya
baridi yenye
kuwasha,upande wa pili wa
nyumba ile Nawal naye
alikuwa katika mateso
makali pia.Mwili wake
ulikuwa umechafuka
damu.Wanawake watatu
wenye sura za kikatili
walikuwa wanaongoza
mateso yale.Alikuwa
amevuliwa nguo zote na
kubaki mtupu.
“Kwa nini lakini
mnanitesa namna
hii?akauliza Nawal
“Tunataka kujua Israel
walifahamu vipi mahala
alipo Ammar Nazari?Kwa
miaka mingi wamekuwa
wakimtafuta Ammar lakini
walishindwa kugundua
mahala anapoishi hadi baada
ya shambulio lile la bomu
jijini Jerusalem” akauliza
mmoja wa wale wanawake
aliyeongoza mateso.Alikuwa
na mikono iliyojaa na sura ya
kikatili.
“Nimekwisha waeleza
sifahamu walifahamuje
kuhusu Ammar” akajibu
Nawal
“Nawal umetueleza kuwa
umeishi kwa muda wa miaka
kadhaa na Ammar Nazari
lakini kwa muda huo wote
uliokaa naye Israel
hawakuweza kutambua
mahala alipo Ammar lakini
amekuja huyu mtu Abu
Zalawi na Ammar
ameuawa.Tueleze ukweli
kuhusu huyu mtu kwani sisi
tayari tumekwisha fahamu
kuwa jina analotumia si jina
lake halisi”
“Sikuwahi kuwa katika
ngazi zozote za uongozi wa
Ammar Nazari brigades
hivyo siwezi kufahamu
chochote kuhusu huyo mtu
mnaye
msema.Nilitambulishwa
kwake kama Abu Al Zalawi
kama ana jina lingine siwezi
kujua” akasema Nawal
“Baada ya kunusurika
katika shambulio lile la
Israel kwa nini ulimpeleka
Abu Zalawi kwa Fatma?
“Abu Zalawi aliniokoa na
alihitaji kuonana na Habiba
Jawad.Sikufahamu mahala
ninakoweza kupata taarifa
za Habiba Jawad ndiyo
maana nikaenda kwa Fatma”
“Ulifahamuje kama
Fatma anamfahamu Habiba
Jawad?akauliza Yule
mwanamama
“Mimi na Ammar tulifika
nyumbani kwa Fatma mara
kwa mara na hata Fatma
alikuwa akifika katika
makazi yetu na nilianza
kuhisi labda wana
mahusiano ya kimapenzi na
niliwahi kumuuliza akasema
kwamba Fatma humletea
maagizo kutoka kwa Habiba
Jawad ndiyo maana
nikaenda kwake nikijua
lazima atakuwa akimfahamu
Habiba Jawad na anaweza
akatusaidia kufika kwake:”
“Nawal hukuwa na
sababu yoyote ya kutaka
kuonana na Habiba bali
huyu jamaa Abu Zalawi
ndiye aliyekupa shinikizo la
kutaka umsaidie aweze
kuonana na Habiba
Jawad.Huyu mtu taarifa
alizozitoa kwamba anaitwa
Abu Zalawi si taarifa za
kweli hivyo nataka utueleze
ukweli huyu mtu ni nani?
Kwa nini akakuokoa wewe
peke yako? Kama aliweza
kumtoa Ammar Nazari
gerezani kwa nini alishindwa
kumuokoa kutoka katika
shambulio la Israel? Tueleze
ukweli tafadhali ama sivyo
mateso yataendelea hadi pale
utakaposema ukweli”
“Sifahamu chochote
kuhusu Abu.Sifahamu kama
amedanganya jina lake”
akasema Nawal.Yule
mwanamke akamnong’oneza
mmoja wa wale wanawake
aliyekuwa naye mle
ndani,akatoka na baada ya
dakika chache akarejea
akiwa na mbwa mkubwa.
“Nawal huyu mbwa
amepewa mafunzo maalum
na nitakapompa maelekezo
ataanza kukuingilia.Naamini
hutapenda kitu kama hicho
kikutokee na hata sisi
hatupendi kukufanyia kitu
hicho lakini kwa kuwa
umeshindwa kuonyesha
ushirikiano kwetu basi
hatuna budi kutumia njia
hii.Nitakutaka kwa mara ya
mwisho utueleze kuhusu
huyu mtu anayejiita Abu
Zalawi ni nani? akauliza
Yule mwanamke.
“Ninaomba tafadhali
msinifanyie hivyo
jamani.Mimi ni mwanamke
mwenzenu.Nimekwisha
waeleza kuwa huyu mtu
mimi simfahamu
vyema.Nilitambulishwa
kwake kama mtu
aliyemsaidia Ammar kutoka
gerezani na toka hapo
tulimfahamu kama
mwenzetu.Sifahamu
chochote kama jina hilo si
lake” akasema Nawal na
kutandikwa kofi kali kisha
mwanamke Yule
akawaelekeza wale
wanawake wengine wawili
wamshike vyema Nawal
wakamuinamisha tayari
kuingiliwa na Yule mbwa.
“Nafasi ya
mwisho.Tueleze kuhusu Abu
Zalawi ! akafoka Yule
mwanamke.Nawali alikuwa
anamwaga machozi.
“Jamani msinifanyie
ukatili wa namna hii”
“Nitahesabu mpaka tatu
na kama bado hautakuwa
tayari kutueleza chochote
nitaamuamuru mbwa huyu
akuingilie”akasema Yule
mwanamke
“Moja ! akaanza
kuhesabu na Nawal ambaye
alikuwa mtupu alikuwa
ameshikwa barabara huku
akilia..
“ Mbili ! akaendelea
kuhesabu
“Tatu ! akasema na
kukunja sura akamshika
shika Yule mbwa akampa
maelekezo na
kumuachia.Yule mbwa
ambaye alimrukia Nawal
kwa nyuma na kabla
hajafanya chochote Nawal
akalia kwa sauti
“Nitasema ! Nitawaeleza
kila kitu ! akasema Nawal na
Yule mwaname akamuondoa
Yule mbwa.Nawal alikuwa
analia huku akihema kwa
kasi
“Haya tueleze ! akasema
Yule mwanamama.
“Tafadhali muondoeni
huyo mbwa haraka humu
ndani ! akasema Nawal huku
akitetemeka.
“Haondoki humu
ndani.Utakaposhindwa
kueleza ukweli kuhusu Abu
Zalawi ataendelea na kazi
yake ! akasema Yule
mwanamama na Nawal
akavuta pumzi ndefu mara
mlango ukafunguliwa na
jamaa mmoja akaingia
ndani.
“Amefunguka? Akauliza
Yule jamaa
“Bado ila anataka
kutueleza ukweli”
“Abdel amesema mpeni
mapumziko kwa
muda.Mlowekeni katika maji
hadi baadae” akasema Yule
jamaa.Nawal akachukuliwa
na kuingizwa katika pipa la
maji yanayowasha kisha
mfuniko ukafunikwa na watu
wale wakatoka wakamuacha
Nawal akiwashwa ndani ya
maji.
PARIS – UFARANSA
Ndani ya chumba
kikubwa chenye kuta
zilizopamba kwa nakshi za
kupendeza,Devotha Adolph
alikuwa amekaa sofani huku
katika meza ndogo mbele
yake kukiwa na chupa ya
mvinyo na mkononi alikuwa
na sigara inayotoa
moshi.Alivuta mkupuo
mmoja wa sigara akapuliza
moshi halafu akainua glasi
akanywa funda moja la
mvinyo
“Lazima nijipongeze kwa
kazi kubwa niliyoifanya hadi
sasa.Haikuwa kazi nyepesi
kuandaa mpango wa
kuisambaratisha Afrika
Mashariki.Kila kitu kimekaa
sawa na kesho Melanie Davis
anaingia Tanzania tayari
kuanza kufanya kazi.Kwa
mbali naanza kuhisi harufu
ya ikulu.Dunia itashangaa
sana pale nitakapotangazwa
Rais mpya wa
Tanzania.Nitaibuka kutoka
kusikojulikana na kuingia
ndani ya jumba lile.Hii
imekuwa ni ndoto yangu ya
muda mrefu na lazima
niitimize” akawaza Devotha
akavuta mkupuo mkubwa na
kupuliza moshi mwingi na
kumbu kumbu ikamjia
kichwani
DAR ES SALAAM
TANZANIA MIAKA
MITATU ILIYOPITA
Gari aina ya Landcruiser
V8 liliwasili katika makazi
ya Devotha likafunguliwa
geti na kuingia
ndani.Devotha ambaye usiku
huu alikuwa amependeza
vilivyo akatoka ndani na
kuingia katika gari lile
likaondoka.Kutoka katika
makazi yake safari iliishia
katika makazi ya balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania
Rafael Berger.Gari
lilisimama karibu na
kibaraza cha nyumba ile na
balozi Rafael tayari
alikuwepo nje ya nyumba
yake kumpokea
Devotha.Mlinzi
akamfungulia Devotha
mlango akashuka na balozi
akampokea
“Devotha karibu sana”
akasema balozi Rafael
“Nashukuru sana
mheshimiwa balozi” akasema
Devotha.Balozi alimuongoza
hadi ndani akamtambulisha
kwa familia yake.Baada ya
dakika ishirini akawasili
tena mtu mwingine ambaye
alitambulishwa kwa Devotha
kama Emmanuel
Antoine.Wote wakaungana
pamoja kwa chakula cha
usiku kisha balozi,Devotha
na Emmanuel wakawa na
mazungumzo hivyo
wakaenda bustanini.Bila
kupoteza muda balozi
akafungua mazungumzo
“Devotha ninashukuru
kwa kukubali mwaliko
wangu na kufika hapa”
akasema
“Hata mimi ninashukuru
kwa kunialika hapa
kwako.Ni mara ya kwanza
tunakutana mimi na
wewe”akasema Devotha
“Ni kweli ni mara ya
kwanza kukutana.Hata hivyo
mimi si mzungumzaji
nitamuachia bwana
Emmanuel aweze kuendelea”
akasema balozi Rafael
“Jina langu kama
nilivyotambulishwa ninaitwa
Emmanuel Antoine
ninatokea Ufaransa na
nimekuja hapa mahsusi
kuzungumza nawe Devotha”
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Kwa miaka mingi
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo ilikuwa katika
mapigano
yasiyokwisha.Vikundi vya
waasi vilikuwa vikiibuka kila
uchao na kupambana na
majeshi ya serikali.Kulikuwa
na makundi mengi kama vile
Alliance of Democratic Forces
for the Liberation of
Congo,Armed Forces of the
Congolese People , Bana
Mura ,Bundu dia
Kongo,Congolese National
Liberation Front,Forces for
Renewal,Mai-Mai,March 23
Movement,Movement for the
Liberation of the
Congo,National Congress for
the Defence of the
People,Patriotic Forces for
the Liberation of
Congo,Patriotic Resistance
Front of Ituri,Popular Front
for Justice in the Congo,Rally
for Congolese
Democracy,Rally for
Congolese Democracy–
Goma,Resistance Patriots of
Congo,Revolutionary
Movement of the
Congo,Union of Congolese
Patriots.Haya ni makundi
machache ambayo nimeweza
kuyataja lakini yalikuwa
mengi.Kwa sasa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo
imetulia na hakuna tena
makundi ya waasi wala
vita.Hata hivyo umewahi
kujiuliza kwa nini makundi
yote haya niliyoyataja
yalikuwa yakitokea nchini
Congo? Kundi moja likipotea
basi liliibuka kundi
lingine.Jibu ni jepesi tu
kwamba makundi haya
yalikuwa yanaanzishwa kwa
malengo maalum na
kinachosababisha haya yote
kutokea kwa sababu nchi ya
Congo ina utajiri mkubwa wa
madini adimu kabisa duniani
ambayo yanahitajika mno
katika viwanda.Karibu
makundi yote
yanayoanzishwa ili
kupambana na serikali
hudhaminiwa na mataifa ya
nje na kupewa silaha na zana
za kijeshi na wanufaik
ahuwa ni viongozi wa
makundi hayo huku
wapiganaji na wananchi
wakibaki masikini.Ziko faida
ambazo zinapatikana
kutokana na mapigano hayo
yanayoendelea huko
Congo.Nchi zinapata masoko
ya kuuza silaha na vile vile
kujipatia malighafi kama vile
madini adimu,maliasili za
misitu nk.Nataka nikiri nchi
yetu pia ni moja ya nchi
ambazo zimefaidika sana na
uwepo wa migogoro
isiyokwisha katika nchi ya
Congo” akatulia kidogo
halafu akaendelea
“Rais Patrice Eyenga
ambaye ameingia
madarakani mwaka uliopita
amefanya kitu ambacho
dunia haikuwa
imekitegemea.Mara tu baada
ya kuingia madarakani Rais
Patrice amekuwa na
mazungumzo na makundi ya
waasi na kwa pamoja
wamekubaliana kuweka
silaha zao chini,kuacha
mapigano na kuijenga upya
nchi yao.Mabadiliko
makubwa yamefanyika
nchini Congo.Makampuni
mengi yaliyokuwa
yamewekeza nchini Congo
katika sekta ya madini
yamefurushwa na
wametafutwa wawekezaji
wengine wapya.Kiujumla
nchi ya Congo imeanza
kupiga hatua
kiuchumi.Kupatikana kwa
amani na mabadiliko
makubwa yaliyofanyika
katika kusimamia rasilimali
za Congo zimetuathiri sisi
mataifa makubwa ambao
kwa kiasi kikubwa tulikuwa
tukitegemea rasilimali hizo
kutokana na mapigano ya
serikali na vikosi vya waasi
na sasa mshirika mkubwa
wa Congo ni China na ndiye
anayeuziwa madini muhimu
yanayohitajika sana katika
utengenezaji wa vifaa mbali
mbali vya kielektroniki”
akanyamaza kwa muda
akamtazama Devotha
“Tunajitaji malighafi kwa
viwanda vyetu vya
kutengeneza vifaa vya
kielektroniki ambayo ni
madini.Ni China pekee
ambayo inapata kiasi
kikubwa cha madini hayo
kutoka Congo hivyo tunataka
kutafuta njia ya
kutuwezesha kupata tena
madini hayo kutoka
Congo.Njia pekee inayoweza
kutuhakikishia kupata tena
mafuriko ya madini ni kwa
kuanzisha tena
machafuko.Pale amani
itakapopotea ndipo nasi
tutaingia na kupeleka vikosi
vya kulinda
amani.Tutawezaje kuivuruga
amani ya Congo? Hilo ni
swali ambalo limenileta
hapwa kwako kutafuta
majibu” akasema Emmanuel
na kunyamaza
“Mimi ninahusiana nini
na suala hilo?Mimi si raia wa
Congo.Sina mahusiano
yoyote na Congo” akasema
Devotha
“Nimekuja kwako kwa
sababu tuna mpango kubwa
wa kuvuruga amani na
kuleta machafuko tena
Congo na wewe ndiye
utakayeongoza mpango huo”
akasema Emmanuel na
Devotha akapatwa na
mshangao
“Mimi?! Akauliza
Devotha
“Ndiyo.Wewe ndiye
ambaye tumekuchagua
uongoze harakati hizo za
kuleta tena machafuko
Congo”
“Emmanuel nadhani
umekosea kunichagua mimi
niwafanyie kazi hiyo.Mimi
sina uwezo wowote wa
kuweza kuvuruga amani na
kuleta machafuko nchini
Congo” akasema Devotha
“Devotha Adolph
sijakosea kuja kwako na
wala hatujakosea
kukuchagua.Tulihitaji mtu
ambaye anaweza akaifanya
kazi hiyo kwa ufanisi na
wewe umetokea kuwa na sifa
za mtu
tunayemuhitaji”akasema
Emmanuel
“Sifa zipi?akauliza
Devotha
“Tumefanya utafiti wetu
na tukagundua historia yako
inaonyesha uliwahi
kulipukiwa na bomu nchini
Kenya na kupoteza familia
yako ukapelewa nchini
Marekani ambako ulipatiwa
matibabu na baadae ulipata
mafunzo ya kijasusi ulifanya
kazi na idara ya kupambana
na ugaidi Marekani na
rekodi zinaonyesha ulifanya
vizuri sana na baadae ulikuja
Tanzania na taarifa tulizo
nazo ni kwamba unaongoza
idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi” akasema
Emmanuel na Devotha
akabaki ameduwaa
“Tuishie hapo Devotha
tunafahamu kila kitu kuhusu
wewe hivyo tunataka uandae
mpango ambao utaifanya
nchi ya Congo iweze kuzama
tena katika machafuko na
vile vile mpango ambao
utaweza kuisambaratisha
jumuiya ya Afrika
mashariki”
“Emmanuel
hapana.Siwezi kufanya
hivyo”akasema Devotha
“Unaweza
Devotha.Nisingeweza kuja
kwako kama sina uhakika
unaweza kufanya jambo
hilo.Usihofu tunajua kitu
tunachokutaka ukifanye ni
cha hatari kubwa lakini
malipo yake ni makubwa
pia.Umeandaliwa jumba
kubwa la kifahari jijini
Paris.Kiasi kikubwa cha
fedha ambacho kinaweza
kukuwezesha ukaishi
kifahari miaka kumi na tano
bila kufanya kazi
yoyote.Kama haitoshi kila
mwezi utakuwa ukipokea
asilimia mbili ya madini
yatakayokuwa yakipatikana
kutoka nchini Congo.Hayo ni
machache tu ambayo tuko
tayari kukupatia lakini yako
mengine mengi” akasema
Emmanuel na Devotha
akabaki kimya kwa muda wa
dakika tatu hadi Emmanuel
alipomstua
“Devotha nahitaji kusikia
maoni yako” akasema
Emmanuel
“Sihitaji hivyo vyote
ulivyovitaja” akasema
Devotha na Emmanuel
akashangaa
“Devotha wewe ni
binadamu wa kwanza
kukataa utajiri mkubwa
kiasi hicho” akasema
Emmanuel
“Nahitaji kitu
kingine”akasema Devotha
“Nini unahitaji?akauliza
Emmanuel.
“Ndoto yangu kubwa ni
kuingia katika siasa.Nataka
nishike madaraka
makubwa.Nataka niwe Rais
wa Tanzania.Kama mnaweza
mkanisaidia katika hilo mimi
pia nitakuwa tayari
kuwasaidia katika mpango
wenu” akasema Devotha na
Emmanuel akatabasamu
“Devotha u mwanamke
wa kipekee
kabisa.Wanawake wengi wa
aina yako wangechagua pesa
na mali nyingi lakini wewe
umekataa hivyo vyote na
umechagua
madaraka.Ninakupongeza
sana kwa hilo.Nikuweke
wazi kwamba asilimia kubwa
ya siasa za bara la afrika
zina shinikizo kutoka
nje.Nchi nyingi za magharibi
kwa sasa zinawekeza katika
siasa za bara la Afrika kwa
kutafuta wagombea wao na
kuwasaidia kuwaweka
madarakani ili wawe na
manufaa kwao.Wanafanya
hivyo kutokana na utajiri
mkubwa wa bara
hili.Kumekuwa na wimbi
hivi sasa la mapinduzi barani
Afrika unadhani ni kweli
wananchi ndio wanaoanzisha
mavugu vugu hayo ya
kuwatoa viongozi
madarakani?La hasha.Wapo
watu ambao huanzisha
vuguvugu hizo na
kuwashawishi wananchi kwa
ahadi ya maisha bora kama
wangefanikiwa kuwatoa
viongozi wao madarakani na
wananachi kwa kutokujua
kwao kilicho nyuma ya pazia
huingia mitaani
kuandamana na lengo lao
hutimia lakini hakuna
mabadiliko yanayotokea
katika maisha yao kama
walivyoahidiwa.Sitaki
nikupe mifano wewe
mwenyewe unafahamu
kinachoendelea barani Afrika
hivi sasa.Nimekwambia hayo
ili upate picha kwamba siasa
za bara la Afrika
zimetawaliwa na nchi kubwa
na wao huamua nani awe
Rais.Vyama pinzani hupewa
sapoti kubwa kwa kuanzisha
vurugu,kuwahadaa
wananchi waione serikali yao
haifai na mambo mengine
mengi.Devotha itoshe tu
kusema kwamba sisi mataifa
makubwa tunalitawala bara
la Afrika lakini si moja kwa
moja kama ilivyokuwa enzi
zile za ukoloni bali
tunatawala kwa kuwatumia
waafrika wenyewe tena
wazawa wa nchi hiyo
hiyo.Kujibu ombi lako sisi
hatuna tatizo na ombi
lako.Tanzania ni moja kati
ya nchi ambazo bado siasa
zake hazijaweza kuingiliwa
na mataifa ya nje kiasi cha
kuthubutu kuwachagulia
nani awe rais wa nchi lakini
kwa kuwa umeliomba
tutaanza kulifanyia kazi
kwani uwezo huo
tunao.Nitaliwasilisha ombi
lako kwa wenzangu tutaanza
kulifanyia kazi.Halitakuwa
jambo la haraka kwani
lazima kwanza tuanze
kujipenyeza taratibu katika
siasa za nchi hii” akasema
Emmanuel
Kumbu kumbu ile
ikamfanya Devoitha
atabasamu akamimina
mvinyo na kunywa
“I chose power over
money.Hivi sasa ningekuwa
mtu tajiri mno kwa ahadi zile
ambazo niliahidiwa lakini
mimi ndoto yangu kubwa ni
siku moja kuingia ndani ya
lile jumba jeupe pale kandoni
mwa bahari.Nataka niwe
kiongozi wa watu zaidi ya
milioni hamsini.Nataka
niheshimike nataka watu
hasa wanaume
wanaowadharau na kuwaona
wanawake ni viumbe dhaifu
waione nguvu ya mwanamke
pale nitakapotwaa
madaraka.Nafurahi baada ya
maandalizi ya muda mrefu
kupanda na kushuka kwingi
lakini sasa mipango imeanza
kwenda vizuri na ninaelekea
katika kuitimiza ndoto yangu
na siku moja nitaitwa
mheshimiwa Rais Devotha
Adolph” akawaza na uso
wake ukajenga tabasamu
kubwa akainua glasi yake
akanywa tena funda lingine
kubwa halafu akasimama
“Sipati picha siku hiyo
nimeshika kitabu cha dini
kati kati ya maelfu ya watu
uwanjani nikiapa kuwa Rais
wa Tanzania.Mimi Devotha
Adolph naapa
kwamba…”akatolewa
mawazoni simu yake
ilipoita.Akaichukua na
kutazama aliyempigia
alikuwa ni Edwin Mbeko
akaipokea haraka
“Hallow Edwin” akasema
Devotha
“Madam habari za huko?
“Huku kwema
kabisa.Unasemaje?
“Nimekupigia
kukujulisha kwamba leo
nilikuwa na mazungumzo na
Rais.Kikubwa alinisisitiza
kwamba kipaumbele cha
SNSA kwa sasa ni
kuhakikisha mkutano wa
kimataifa wa wake za marais
unafanyika kwa amani na
utulivu.Nimemuhakikishia
kwamba hakutakuwa na
tatizo lolote” akasema Edwin
“Safi sana Edwin kwa
kunipa taarifa.Melanie
anatarajia kutua kesho hapo
Tanzania hivyo basi
hakikisha kila kitu
kinakwenda vizuri.Wewe
ndiye utakayekuwa
msimamizi wake mkuu kwa
upande huo na kama kuna
chochote kitashindwa
kwenda vizuri basi lawama
zitakuwa juu yako”
“Usijali madam
maandalizi ni makubwa na
hakutakuwa na tatizo
lolote.Kila kitu kiko vizuri”
akasema Edwin
“Edwin operesheni hii ni
muhimu sana na hakuna
makosa yanatakiwa
kufanywa.Kila kitu kiende
kama kilivyopangwa.Liweke
hilo katika akili yako na
uliimbe kila siku katika
mdomo wako.Umenielewa
lakini?
“Nimekuelewa madam
usihofu”
“Kuna shida nyingine
yoyote,fedha au kitu
chochote?
“Hakuna madam.Kila
kitu kipo na kama nikihitaji
kitu nitakujulisha”
“Ahsante Edwin”
akasema Devotha na kukata
simu