RIWAYA: Siku kabla ya leo

RIWAYA: Siku kabla ya leo

Sehemu ya 10*


Manyau alikuwa akilifunga geti la nyumba yake huku mkono mmoja ukiwa umeshika simu na kuiweka sikioni.
Alipomaliza akageuka ili aondoke kulifuata gari lake lakini hakupiga hata hatua hata moja akajikuta akitazamana na mwanadada mzuri mithili ya mke wa sita wa mfalme mswati.

Hakuwa peke yake mwanadada yule,nyuma yake alisimama mwanaume wa shoka akimtizama Manyau.

Manyau alipagawa wazi wazi,kuonekana kwa Temba machoni pake ilikuwa ni ishara mbaya kwake,akapanga kujinasua ili asiingie mikononi mwa mtu yule,alimjua nje ndani na alitambua pasipo juhudi za ziada basi atapotea.

Akamtazama koplo Mina aliekuwa mbele yake akiwa katulia tu kama hanae shida,akamtisha kidogo ila ajabu hakuona japo hata mtikisiko wa kope kutoka kwa koplo yule,akapeleka mikono yake imara ili amdake na kumgeuza kama ngao yake,akajikuta akikutana na hewa,akajipanga upya akaweka mkao wa uzoefu katika mapigano,akatupa mbili tatu zote zikaambulia patupu ila alipokuja kupigwa yeye hakuamini kama bado nchi hii inawanawake kama wale na bila kupenda alijikuta yupo chini huku Koplo Mina akiwa kasimama imara kama nguzo ya nyumba na alipotizama pembeni hakumuona tena Temba.

Baada ya kumlainisha Manyau koplo Mina alimbeba begani mwanaume yule ambae hakuwa haba kwa nyama mwilini mwake.
Koplo Mina alimtupia nyuma ya viti na yeye kukaa karibu yake kisha Temba aliekuwa dereva akaliondoa gari eneo lile huku wakiwaacha watu wakistaajabu walioyaona ndani ya dakika mbili.

***
Ukimya ulikuwa umetawala ndani ya gari ila Temba aliamua kuuvuja ukimya ule.

" Najua unajua Manyau yalionikuta,lakini hujaridhika ukaamua kuniingiza upya kwenye hili dili tata kwa kumweka demu wangu,Manyau uchungu wangu namalizia kwako mbele ya huyo askari wa kike"

Manyau akastuka kusikia yule mwanamke aliekaa karibu yake ni askari,ajiuliza itawezekana vipi asimkamate Temba? Tafakari yake haikufika mwisho akasikia honi zikipigwa kuashiria mwisho wa safari yao.

Ni kweli baada ya muda gari likikuwa linaingia ndani ya uzio wa nyumba kubwa ya kisasa na punde ikasimama akaanza kushuka Temba akafungua mlango wa upande wa kulia na kumtoa Manyau kwa kasi ya ajabu,kisha kikafuatia kipigo cha nusu dakika lakini ilihitaji utumie kompyuta kuiweka mjongeo wa taratibu ili ujue alitumia mtindo gani kumwadhibu Manyau na ndani ya dakika ile uso wake ulikuwa hautamaniki.

Wakati haya yakiendelea Jijini Mwanza Mbena alikuwa kituo cha polisi akihojiwa kwa yaliotokea...

***


Tukutane kwenye group la whatsapp kwa riwaya zingine kwa garama ya Tsh 2500/=

Asalaam kudo.
 
Haya jaman mliopo WhatsApp mtatuambia wengine hatutumii
 
SEHEMU YA 11*


askari polisi wa kituo kikuu cha polisi jijini Mwanza,walikosa majibu ya maana kutoka kwa Mbena.

Kamanda mkuu wa mkoa alikuwepo pia wakati mahojiano yale yasiokuwa na majibu sahihi yakiendelea kwa mtoto yule wa waziri wa Afya.

Ajabu walioiona askari wengine mbali ya kuwa walikuwa wanamhoji mhusika wa kwanza wa mauaji ya Maiga mtoto wa waziri pia,lakini ilikuwa wazi kwao ilihitajika binti yule apelekwe hospitali kwanza maana hali yake haikuwa nzuri.

Mbena alikuwa akitoa udenda kila dakika huku ulimi ukiwa mzito kusema na hata alipoomba kalamu aandika alijikuta anashindwa maana mikono ilikuwa kama mtu aliepooza au kwa lugha nzuri mtu aliugua kiharusi.

Mbena aliwatazama maaskari waliokuwa wamemzunguka,aliwatizama kwa ishara ya kuomba msaada wa matibabu angalau kidogo apate ahueni,lakini hakuna aliemwelewa na hakuna aliejali hasa kamanda yule ambae vijana wake walikuwameshatoa pendekezo la kupelekwa hospitali kwanza ila aligoma kwa sababu anazozijua yeye.

***

Mauna Seko alikuwa akibalizi upepo wa ziwa viktoria ndani ya fukwe za Tunza jijini mwanza.

A
Mawazo yake yalikuwa mbali wakati huo huku kitu pekee kikiwa ni bukta nyepesi iliokuwa mwilini mwake.

Ilikuwa ajabu ahsubuh kabisa kumkuta mtu analipia kwenda fukweni,lakini yeye alikuwa na sababu za kufanya hivyo.

Alikuwa pale kuweka sawa akili yake baada ya kumfumania mpenzi wake akiliwa uroda na mwanaume mwingine ndani ya gari yake alionunua na kumpa mwanamke yule zandiki.

Mawazo yalimjaa pasipo kifani na hakuwa na kuyapunguza zaidi tu aliamua kutafuta pahali tulivu wakati huo na sehemu pekee ilikuwa ni hiyo.

Wakati akijaribu kurusha vimchanga viliwili vitatu ndani ya maji,alihisi harufu katika mwili wake,akageuza shingo ili atizame eneo gani lilikuwa likitoa harufu ile.

Akageuka upande wa bega la kushoto hakuona kitu,akageuka upande wa kulia akajikuta akitoa tusi zito la nguoni huku akifanya jitahada za kujifuta,alikuwa ni ndege aliemwangushia kinyesi chake.

Akiwa kamaliza kujifuta,akili ikamkaa sawa,akakumbuka kitu.

Wakati anageuka upande ule wa kulia, aliona kitu kwa mbali na hapo akageuka tena,ni kweli aliona kitu kikiwa umbali fulani kutoka pale alipo,na bila kutarajia akajikuta miguu ikiwa tayari imeanza kujongea kuelekea kule.

Alistaajabu kumkuta binti akihangaika kusimama,kwa kumtazama alikuwa akipitia mateso makali muda ule.

Haraka akarudi kule hotelini na kuita kiongozi wa Hotel ile akampa taarifa,yule aliepewa taarifa akapiga simu kituo cha polisi.

Kulingana na hali aliokuwa nayo binti Yule, Mauna Seko akaamua kuchukua jukumu la kumwahisha hospitali.

Kama ilivyokawaida ya hospitali zetu na hali aliokuwa nayo ikabidi waombe PF3 kwanza na kweli Mauna akapiga kona kugeuka ili amwahishe kituo cha polisi cha karibu hilo likawa kosa.

Alipofika tu kituoni wakaanza kumhoji huku mgonjwa akizuiliwa kupelekwa hospital.

Mauna hakuwa na namna hasa aliposikia yule aliemsaidia ndie muuaji wa Maiga akagwaya.

***
"Inawezekana vipi hii"Mauna alijiwazia mwenyewe akiwa ndani ya gari akielekea kwa mwanasheria flani ili aende kusimama kumtetea binti yule apewe matibabu.

Licha ya kupeleka mwanasheria lakini bado jitihada zake zikagonga ukuta na akabaki hana la kufanya na imani yake ikamwambia kuna la zaidi katika hayo,akachukua simu yake akzitafuta namba flani kisha muda mfupi alikuwa hewani.

Alikuwa anampigia Temba rafiki yake wa muda wote,usiku na mchana,iwe jua iwe mvua lazima watasaidiana.

Upele ukapata mkunaji,Mauna alipomaliza kuongea na simu akapiga ngumi hewani kama ishara ya ushindi baada ya kuambiwa na Temba nae yupo kwenye harakati hizohizo.

***

Asalaam Kudo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom