Sehemu ya 7*
Mchinjiko alimtazama Mbena,kisha kwa utaratibu akamfuata akamshika mkono na kumwinua alipokuwa amekaa,akamkokota hadi ilipokuwa gari ikiwa imepaki na watu wengine ndani,
Kisha pasipo kuambiwa kitu akabebwa na kutupwa ndani gari lile aina ya toyota Ford,ndani Mbena alikutana na watu wengine wawili waliompokea na kumfunga uso kisha safari ikaanza na hakujua anapelekwa wapi.
Saa 12:38
Muda huu ilimkuta Mbena akiwa kwenye mchanga laini,akasimama akajipapasa akajikuta kama alivyokuwa wakati akitolewa sehemu asioijua na hakujua hata hapo alipo ni wapi,akakumbuka Mara ya mwisho alikuwa wapi,kumbukumbu zilipo mrudia vizuri akakumbuka punde alipotupwa ndani ya gari akafungwa kitambaa,kisha yakafuatia maumivu makali karibu na mkono wake,maumivu ya kuchomwa kama na sindano.
Ajabu alipojaribu kupiga hatua akashindwa,hapo akajaribu kutazama napo akashindwa akajipapasa usoni akagundua bado amezibwa uso,akanyanyua mkono na kukitoa usoni kitambaa cheusi kilichotumika kumfunga usoni.
Akatazama kushoto na kulia akagundua alikuwa ametupwa kando kando ya fukwe za bahari ama ziwa,alijaribu kuvuta taswira maeneo gani atakuwa,hakupata jibu,akajaribu kupiga tena hatua,miguu ikakataa kumpa ushirikiano,si miguu hata mwili ulikuwa hauna nguvu za kufanya lolote.
Mbena alijulikuta akitetemeka mwili mzima,hofu ikamwingia,
Midomo nayo ikamsaliti ikakataa kufumba,akaanza kutokwa na udenda,kila akijaribu kuzuia akashindwa,mikono haikunyanyuka, miguu nayo ikashindwa kuhimili akajikuta akirudi chini bila kupenda na alipojaribu kupiga kelele haikuwezekana,machozi yakaanza kumtoka,na kwa mbali hakuona msaada wowote.
*****
Koplo Mina alipaki pikipiki yake hatua kadhaa kutoka mlango wa kuingilia Lasi Vegas casino,akatazama kushoto na kulia akavuka kijia kidogo na kukifikia kimlango kidogo cha kuingizia kadi ya kufungulia mlango,akazama mfukoni akatoa kadi ile,akapachika kwenye kijimlango kile,punde mlango ukajifungua nae akazama ndani,hatua kadhaa akakutana na mlinzi wa mlango ule akiwa amevalia suti safi nyeusi,wakatazamana kisha bila kusemeshana koplo Mina akatoa kadi nyingene akamnyooshea,hakusubiri aruhusiwe akapiga hatua na kuingia ndani.
Koplo Mina akatua begi mezani bila kukaa akasema na aliemkuta ndani ya chumba kile.
"Kamba nahitaji Msaada!?"
"upi"
"kuna hii chombo hapa nimepora nataka kupata kilichomo"
Kamba akalipekua lile begi,akatoka na kompyuta mpakato,akaitazama kisha akaifungua na na kuiwasha,akainama kidogo akapekua na kutoka waya mrefu akauweka kwenye kitu mfano wa kihifandi umeme au power bank,akatulia kimya kisha akamtazama Mina,akamuuliza
"email au vihadhio"
Mina akajibu "email"
Kamba akazama kupekua kompyuta ile.
Ndani ya dakika kadhaa hakupata kitu akamtazama Mina na kuzungumza
"email nyingi ila kuna Email moja inaonekana iliingia jana na kufutwa, na alieituma inaonekana alitumia utaalamu maana nikiifuatilia ilikotoka haionekani lakini ngoja....."
.akazama tena kupekua hiki na kile punde akatoka na jibu
"inaonekana ujumbe ulitumwa kwa ems kutoka mwanza na hii ilikuwa ni saa tisa na dakika kumi usiku lakini huu ujumbe kutoka mwanza ulipokelewa kabla ya kutumwa kwenye email hii kutokea Dar es laam na huyu alietuma mwanza alikuwa amesimama au alikuwepo kituo kikubwa cha polisi"
Koplo Mina akaguna na hapo akagundua mchezeshaji wa mchezo ule alikuwepo palepale kituoni,akazama kwenye tafakuri akazama mfukoni akatoka na simu akampa Kamba,kamba akaitazama kisha akapachika kwenye kifaa kidogo,hapo akapakua vitu kadhaa kisha akatoka na jibu
"Simu ya mwisho kuingia kwake ilitoka kwa mtu anaetambulika kwa jina Temba,simu hii ilikuwa na ujumbe wa maneno pia yalioonesha walikuwa na makubaliano ya kulipana nyumbani."
Temba pia alifanya mawasiliano akitokea mtaa wa kawe karibu na kituo cha radio,nyumba namba 14
Saa 12:45
Mina alikuwa ameiacha Vegas kasino alikokwenda kukutana na rafiki yake ambae huwa anamsaidia mambo mengi ya mawasiliano na alitoka kuvikagua vifaa vya mwandishi wa habari alieuawa makumbusho.
Na sasa alikuwa njiani kuelekea kawe.
****
Walikaa wawili tu katika ofisi hii,mazungumzo yao waliyafanya kwa sauti ndogo,hata ungekuwa hatua kadhaa nyuma yao asingelisikia,wote walikuwa wanaume,
Mmoja alikuwa mnene mfupi na mwingine alikuwa mrefu mwembamba,wote walivaa mawani......
Asalaam kudo(Bahati Mwamba)