Sehemu ya 9*
Koplo Mina hakupata kauli kwa dakika moja nzima,alikuwa akitazamana na Temba,mtu asie ogopa kuua wala kufa,sehemu yoyote ukimtuma anaenda na kurudi akiwa na taarifa njema kwako.
Temba alikuwa kimya kabisa akijaribu kuusoma uwezo wa pili wa kiumbe wa kike wanaetazamana,hakutaka kumdharau kiumbe yule ila alimhurumia maana aliamini uwezo wake kuliko wa mtu mwingine yeyote,aliamini mungu kamuumba peke yake mwenye uwezo wa kufanya lolote kwa kutumia mwili wake.
Akaishusha bastola yake kisha akaipata sauti yake.
"unajua kwanini nimemuua nimpendae?"
Hakupata jibu kutoka kwa Mina,nae hakuwa akilihitaji akaendelea..
"Huwa sipendi mtu atumie nguvu nyingi kuliko akili na huwa sipendi mtu mwenye nguvu napenda mtu mvivu mwenye sifa kama zangu,ninauwezo wa kukuua kwa sekunde zisizo pungua kumi ila naogopa laana ya mume mwenzangu anaekupenda kwa dhati vile atakavyoumia akikuona ndani ya sanda"
Temba alizungumza huku akijitupa kwenye sofa moja wapo na kumtazama Mina aliekuwa kimya akimtazama.
Temba akazidi kuongea....
"Sijui jina lako ila naamini ni wewe uliezuiliwa kuendelea na kesi hii,na kwa ushauri wangu mdogo ni heri uache kabisa hili suala litakupoteza kabla ya usiku wa kesho na ili uone kwamba hili suala ni gumu kwako hata nikifanikiwa kuwa chini ya miguu yako nitakwambia simjui alienyuma ya hili na ukinibana sana nitakwambia nilipokea oda tu ya kuisambaza video ile kwa mtu nisie mjua alidai yupo mwanza na Mimi nilipokea kutoka kwa mtu nisie mjua usiku ule na hapa nina pesa tu ya kazi hiyo"
Akanyamaza huku akiwa anamtazama Koplo Mina usoni,koplo Mina nae akazungumza
"Kwanini unayasema yote hayo kwangu"
"Kwa sababu nataka uniache na kazi zangu na huo ndio ukweli wangu lakini kubwa niache nimzike mpenzi wangu niliemuua mwenyewe sitaki unipe mzigo wa kuwazika nyinyi nyote"
"Sawa,na wewe kwanini ulikubali kupokea oda kwa mtu usiemjua"
"Kazi yangu ni kupokea oda na ofisi yangu ni mwili wangu,lakini hii kitu sijatumia mwili nimetumia mdomo na pesa kidogo na moja ya kazi za ajabu kwangu,lakini nikwambie kitu sijamuua huyo dada sababu yako,nimemuua kwa sababu tulikuwa na ugomvi mkubwa na...."
Hakumaliza sentesi yake akajikuta akivurumishiwa risasi nyingi alizozikwepa kwa ustadi wa hali ya juu,alipotizama upande aliokuwa Mina hakumuona ila alipata kushuhidia wanaume wawili wakiwa na silaha zao mkononi wakivurumsha risasi na kutoka pale alipo akajaribu bahati yake akamlenga mmoja ila bunduki haikuwa na kitu ilikuwa tupu,akapiga hesabu nyingine,akairusha ile bastola yake juu na wale wavamizi wakahadaika kuitazama.
Kutoka pale alipo,Temba akapaa juu kama anaeifuata bastola ile kisha kiajabu kabisa akajikunja na kuachia mikono yake yote miwili na kuikamata bastola bunduki ya mvamizi mmoja na kuivuta upande wake,miguu yake ilitua chini na kumfanya apate egemeo vizuri na kumfanya mvamizi yule awe kama anamparamia hivi kwa kukosa mhimili na kujikuta akidondokea mikononi mwa Temba Misha akapigwa na bega lililoshiba na kumrudisha nyuma na kujikuta hana silaha ipo mikononi mwa Temba.
Wakati Temba akifanya maajabu yale Mina nae akaitumia fursa vizuri kutoka nyuma ya jokofu alikokuwa amejificha alitoka kwa kasi ya umeme wa radi na kumtandika mvamizi aliebakia ngumi ya shavu iliomfanya ayumbe kwa kihoro,kisha pasipo kutarajia Koplo Mina akaachia teke safi kabisa lililolenga usawa wa mbavu na kumfanya mtu yule atetemeka kama kaumwa na siafu makalioni na akiwa na mtetemo huohuo akadakwa koromeo na hakusema kitu tena labda siku ya kiama.
Temba alibaki akitazamana na mvamizi alie hai huku akiwa kamwelekezea bunduki ya Vita,pembeni alimwona koplo Mina akiwa amesimama nyuma ya mateka wao,akatabasamu kisha akamwagiza koplo Mina.
"Ingia chumbani kwangu kwenye mlango uliowazi hapo utakuta vinavyokufaa njoo navyo usijali kuhusu huyu rafiki utamkuta akiwa hai"
Koplo Mina akafanya kama alivyoagizwa huku akiwa na mashaka na Temba,hakutaka kuamini usaidizi wake,na alibaki na swali moja tu huyu Temba ni nani mbona kama anaonesha hahusiki na mpango huu,lakini mbona alikiri mwenyewe,hakuishia hapo akajipa swali kwanini alimuua mpenzi wake na kwanini yeye binafsi anajikuta akianza kumwamini mtu yule anaeonesha ukatili wa wazi kabisa.
Mina mawazo yake yalikoma alipojikuta katikati ya chumba kipana na safi,alipoangaza kushoto kulia hakuona kitu ila pembeni kidogo ya kitanda kulikuwa na kabati kubwa la nguo,akaliendea na kuligungua akapigwa na butwaa,halikuwa kabati la nguo ila ni kabati lililopangiliwa vyema na kubeba silaha mbalimbali za kisasa.
Mbali na silaha pia kulikuwa na vitu vinavyotumika kutesea watu,hapo akapata akili ni kwanini alitumwa kule chumbani,akabebelea vitu vilivyofaa kumtemesha mtu hadithi yote alizomeza,kisha na yeye akabeba silaha moja alioamini itamfaa na kuisunda kiunoni maana hakutaka kumwamini Temba.
****
Koplo Mina alitokeza sebuleni,tofauti na mwanzo muda huu alimkuta Temba kakunja nne kwa lugha rahisi alikaa kwenye sofa na kubebanisha miguu huku chini kukiwa na watu watatu wamelala.
Mmoja ni yule mwanamke alieuwawa na Temba na mwingine ni mwingine no yule aliemuua yeye na watatu ni mateka aliemwacha na Temba muda mfupi uliopita.
Mina akatazama vizuri Temba wala hakuwa na wasiwasi,kisha akahamishia macho alipolala yule mvamizi akamwona anahema kwa mbali na ametapakaa damu usoni kama mtu aliepitia mateso ya wiki nzima.Koplo Mina akastaajabu uwezo wa kupiga wa bwana Temba na pasipo kusema kitu akasogea alipobwana yule alielala na kumwinamia na kabla Mina hajasema chochote Temba akasema
"Alileta jeuri kidogo huyo bwana ako nikamwonyesha kwanini msukuma haendi jando,ila usijali bado anaweza kusema"
Kisha akanyanyuka na kumsaidia koplo Mina kumsimamisha bwana yule na wakaanza kumhoji.
Mwanzo bwana yule alikuwa ngumu kusema chochote ila hakujua anacheza na watu wa aina gani.
Temba akasimama akachukua zana mbili alizoona zinamfaa,akamfikia bwana yule kisha taratibu bila kumsemesha akatoa kifaa kidogo mithili ya sindano na kuanza kumchoma choma miguuni.
Licha ya kutokwa na damu nyingi na maumivu lakini hakusema anachokijua jambo lile lilimkasirisha bwana Temba akamkaba kabali ya shingo kisha akaomba kamba.
Alijuta kufungwa kamba maana muda huo meno yalikuwa yameshangolewa kama mawili hivi tena kwa chuma ya kusafishia kucha,hakuwa na namna ilibidi tu aseme aliemtuma na hapo akalitaja jina la Manyau.
Temba akamwambia Mina anamfahamu mtu huyo ila hakumwambia anamfahamu vipi,koplo Mina hakusema kitu alibaki akishangaa uwezo wa ajabu wa Temba.
saa nane na nusu mchana iliwakuta Koplo Mina na Temba wakiwa kama mke na mume ndani ya gari wakiiacha Kawe kuitafuta Temeke anakoishi huyo Manyau huku Temba akiwa mbali kifikira alikuwa analiwaza jambo,jambo ambalo koplo Mina hakulijua japo ndilo alitaka kulijua kutoka kwa Temba.
*****
Asalaamu kudo
Note:kuna riwaya zinaendelea kwenye group la whatsapp ukitaka kujiunga kuna kiingilio kidogo tu
0658564341.
Hiyo ni kwa whatsapp tu
0758573660 kwa mawasiliano mengine, text and calls