RIWAYA: Siku kabla ya leo

RIWAYA: Siku kabla ya leo

Nadhani ukitizama kule inakoruka Kikosi cha pili utaona lengo langu la kuachia riwaya zote mbili hapa,so usiwe na Shaka zitaisha zote,ila inategemeana na kuruka kila siku maana kuna siku nitakwama kupata bando,ila likiwepo kila siku mzigo utakuwa hewani
ishu hapa sio bando kwani jamii forum IPO free basic! Umakini is everything big brother
 
ishu hapa sio bando kwani jamii forum IPO free basic! Umakini is everything big brother
Unamaanisha nini labda unamaana hata bila bando itafunguka? Au Mimi ndo sijakuelewa au ulimaanisha nini chief
 
Sehemu ya 4*


Saa 10:10 ahsubuhi

Muda huu ulimkuta Mbena na machaguo mawili ya mtu yule mrefu mwembamba au yeye mwenyewe Mbena alimuita Mchinjiko.
Chaguzi zenyewe zilikuwa ni Mbena abakwe na mijibaba huku akirekodiwa video au akubali kwa mdomo wake alishiriki kumuua Maiga.
Mchinjiko alimuahidi ya kuwa akitekeleza moja kati ya hayo basi watamwacha aende zake na maisha yake na hawatamsumbua.

Mbena akalia kwa huzuni huku akiomba huruma kwa bwana Mchinjiko ila huruma hiyo ilikuwa mbali na mtu huyo ambae haijulikani ni kwanini alikuwa ameamua kumteka Mbena na kumshurutisha akubali mauji ya mpenzi wake waliependana kwa moyo wa dhati kabisa.

Kila alivyomsihi bwana Mchinjiko ilishindikana.Mbena akadiriki kumwahidi pesa nyingi bwana yule ila ilikuwa ni kazi bure,
Mchinjiko akamwambia amelipwa pesa nyingi kushigulikia mpngo huo na hana tabia ya kukiuka makubaliano hata kama amelipwa senti moja hatoweza kuikacha kisa atapewa milioni kumi.

Mchinjiko akaona Mbena haelekei kukubali hivyo kutopoteza muda akawaamuru vijana wake wambake Mbena.
Mbena akiwa bado amezubaa akajikuta akibebwa mzobemzobe na kutupwa chini kama mzigo,wakati akiugulia maumivu ya kiuno jibaba moja likamfikia na kumkamata mkono kisha likaingiza mkono katikati ya miguu ya Mbena na bila ustarabu likaivuta kufuli ya Mbena,.
Wakati matukio yote yakiendelea Mchinjiko alikuwa anarekodi kwa kamera yake kubwa,alifurahi pale alipoona Mbena akijaribu kujinasua Mikononi mwa mabaunsa wale huku akiacha hazina yake iliokuwa imeanza kuotesha majani meusi ikiwa nje baada ya kuvuliwa hifadhi yake....

*******

Saa 10:30

Muda huu ulimkuta koplo Mina akiwa makumbusho zilipo ofisi za kampuni ya Lengo Media wachapaji wa gazeti la Mwasema.
Akazitazama ofisi zile kisha kama mgonjwa akavua kofia yake ngumu akauendea mlango wa kuingilia ofisini pale.
Wakati anaingia akatazama kulia na mazingira ya ofisi ile kiujumla,ambapo kulia kwake kulikuwa na binti mmoja aliekuwa anaandikisha wageni wanaoingia na kutoka ofisini pale,akamfuata na kumuuliza zilipo ofisi za mhariri mkuu wa gazeti lile,yule binti akamuomba Mina ajiandikishe kwanza kwenye kitabu cha wageni nae akatii.
Ofisi za mhariri mkuu zilikuwa upande wa kushoto ukiwa kama unaingia kisha utaifuata korido ndefu upande huohuo wa kushoto hapo utakutana na mlango umeandikwa mhariri mkuu,.Yalikuwa ni maelezo ya mwelekezaji kwenda kwa Mina yakijirudia kichwani wakati akiifuata korido ile,punde alijikuta akitazamana na mlango ulioandikwa Mhariri Mkuu.

Alikuwa amekaa nyuma ya kiti cha kisasa cha kuzunguka,huku macho yake makubwa akiwa ameyaficha nyuma ya mawani ya macho,alimtazama tena binti mrefu kiasi,mwenye midomo ya ahueni ya moyo,kifua kidogo,rangi kama papai bivu liliojuu ya mti,mapaja manene kiasi huku pembeni kukiwa na muundo flani wa kuficha kitu,akiwa amevalia suruali ya kitambaa na blauzi safi kabisa huyu alikuwa ni Koplo Mina mbele ya macho ya mhariri Mgimba Wangwe.

Wakati akimtazama kwa matamanio akajikuta akitazamana na kitambulisho cha koplo Mina,hapo bwana Mgimba akapata kigugumizi na mstuko wa wazi kabisa.
Mstuko huo uliashiria kitu cha tofauti kwa koplo Mina,akamkazia macho ya shari mhariri yule ambae wakati huo alikuwa anajaribu kuuficha mstuko wake kisha kwa ujasiri wa kununua akamuuliza

"nikusaidie nini?"

"naomba kufahamu chanzo cha habari ya mauaji mlioandika kwenye gazeti lenu"

"Aaah sio utaratibu huo"

"Basi sawa naomba mwandishi wa habari hiyo"

"Aaah bado sio utaratibu ila.."

Akaiacha kauli yake ikiambaa hewani huku akinyanyuka mle ofisini na kumwahidi koplo Mina anaenda kumuita mwandishi wa habari ile.

Wakati bwana Mgimba akiiacha ofisi ile koplo Mina hakutaka kumwamini bwana yule nae kwa taratibu akaanza kumfuata kwa nyuma kisha akajibanza mwisho mwa korido na kutizama kule aliko bwana magimba alieonekana kuhangaika kupiga simu,hapo koplo Mina akajua mchezo ushaiva,haraka akarudi ofisini na kukaa kimya.

Bwana Mgimba alimpa habari ya kuwa mwandishi wa habari ile kaomba dharura amerudi nyumbani kwake anawageni.

Koplo Mina hakuwa mjinga aliuliza jina la mwandishi yule na makazi yake na hii ni wakati akisaini kitabu cha wageni,.Alipokwisha kufahamishwa na Dada yule akaondoka na kudandia pikipiki yake kuitafuta mwenge karibu na kiwanda cha dawa nyumba namba kumi na nne.

Ilikuwa ni nyumba kubwa huku nje kukizungushwa geti la kisasa kabisa,akalipita na kwenda mbele kulikuwa na kituo cha taxi nae akaacha pikipiki yake pale kisha akaanza kurudi nyuma kwa tahadhari kuifuata nyumba ya mwandishi yule ni wakati akiukaribia mlango akapishana na mtu akitoka kwa kasi ya umeme na wakati akishangaa ikaja pikipiki nyingine kwa kasi na yule mtu aliepishana na koplo Mina akadandia na wakatokomea,

Akili ya koplo Mina ikacheza hakuna usalama pale ndani akapita kwenda ndani kwa kasi akakutana na mlango ukiwa wazi,akausogelea bila tahadhari akazama ndani hapo akakutana na damu mbichi ikimwagika kutoka kwenye mwili wa mtu alielala chini huku tundu za risasi zikiwa upande wa kushoto wa moyo wake.

Wakati akishangaa akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti,
Koplo Mina akajilaumu kutokuwa na tahadhari hadi anaingizwa mtegoni kirahisi vile....



Asalaam Kudo(Bahati Mwamba)

Ahsanteni kwa mnaochangia mungu awabariki kwa ambae bado naomba ufanye hivyo maana kutoa ni moyo bandugu

0758573660
0658564341
0624155629
 
Sehemu ya 5*

Mbena koo lilimkauka na hakuwa na cha kufanya japo hakuwa tayari kuingiliwa kimwili na watu wale asiowajua.
Akaona kupiga kelele hakutomsaidia,njia pekee ni kukubali yeye ndie mhusika katika mauji yale,akapaza sauti kwa nguvu,sauti ile ikamfikia Mchinjiko,akasitisha zoezi la kurekodi,akawaamuru mabaunsa wale wamwache Mbena.
Walimwacha huku wakiwa na uchu wa ngono kwa binti Mbena aliekuwa kanawiri kwa wingi wa uzuri ulioanza kufifia baada ya kukutana dhahama asiojua mwisho wake.

Mchinjiko akawaamuru mabaunsa wale watoke,kisha akambeba mbena na kuingia nae chumba cha pili kilichokuwa maalumu kwa usafi wa mwili wake,akaoga kisha akaamuliwa kujiweka katika muonekano wa mtu ambae yupo huru.

Alipokwisha kuwa tayari akaletwa mbele ya kamera kisha akawekewa ubao mbele yake akaambiwa asome maelezo yale,.
Yote yalikuwa yakiendelea wakati ambao Mchinjiko alikuwa akirekodi kila kitu,na alikuwa mbele yake Mbena na ubao wenye maandishi.

*****
Koplo Mina hakuwa na ujanja mbele yake alisimama mwanaume shababi asie na mzaha na ni mtu anaeonekana kuwa kuua ni jambo jepesi,.
Akamwamuru koplo Mina aweke silaha yake chini,nae akatii,yule bwana alishindwa kuelewa jambo moja,hakuna silaha mbaya duniani kama mwanamke,na ndio yaliomkuta.
Kwa uzuri aliouona kwa Koplo Mina ukampagawisha kabisa akaona asimuue kwanza askari yule,akamletea mzaha,mara amkebehi,mara amtomase maziwa kwa mdomo wa bastola,akaona haitoshi akamsogelea karibu zaidi
Kwa mkono ulioshika bastola akaelekeza kwenye paji la uso,akashuka hadi kifuani kwa Mina,hapo akatulia kidogo akampekenyua blauzi yake,alipoona haimpi ushirikiano wa kuacha matiti wazi akazidi kushuka,hadi alipogusa kitovu.

Wakati yule bwana akifanya udhalilishaji ule hakujua hila za koplo Mina wakati gani atazifanya,yeye akazidi kushuka,akafika eneo la makutano ya maungo ya wanadamu,hapo koplo Mina akatoa mguno hafifu huku akirudisha kiuno nyuma,yule bwana akiwa kazubaishwa na mguno akastukia korodani zikiwaka moto wa pekecha,lilikuwa ni pigo mujarabu kutoka kwa koplo Mina,.
Pigo lile halikumwacha yule bwana na urijali wake,isipokuwa likamfanya awe mdogo kifikira na hakuwa na mbinu mbadala ya kukabiliana na maumivu yake zaidi ya kuweka mikono yote huko angalau azifunde mkononi korodani zake.
Hakujua ni kosa akakutana na mapigo mawili ambayo hakujua ni kutoka katika aina gani ya mapigano,mwili ukaaga roho na roho yake dhalimu ikaenda kukutana na adhabu ya milele.

Koplo akaanza kupekua nyumba ile iliokuwa na maiti mbili,hakukuta cha maana zaidi alikutana na kompyuta mpakato pamoja na simu,akavitia kwenye begi dogo lililokuwa pembeni hapo,hakuwa na la zaidi isipokuwa kupiga simu polisi ili wafike eneo lile kuendelea na utaratibu zaidi.

*****
Saa 11:07 ahsubuh
20/07/2017

Video ya mtoto wa waziri wa Afya Mbena Mnuo kujirekodi na kukiri kuhusika na mauji hayo,kisha kutumia simu yake kurusha mtandaoni ilisambaa kama moto wa kifuu na karibia robo ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walikuwa wameiona video hiyo,huku kisa cha yeye kuua akisema Maiga hakuwa mwaminifu na alimfuma akimsaliti na kahaba vyooni.

Watu wengi walionesha kusikitishwa na taarifa ile,huku wanafunzi wengi wa vyuo mbalimbali wakilaani vikali tukio lile,ilifikia hatua hata ndugu wa pande zote mbili kuanza kurumbana kila upande ukimtuhumu mwenzie,.
Wakati hayo yakiendelea IGP alitoa tamko rasimi kwa vijana wake Mbena atafutwe na akamatwe mara moja kwa kuhusika na kifo cha mtoto wa waziri wa kilimo na rais wa serikali ya wanafunzi dar es laam,..
Vijana wakaingia kazini rasimi wakitumia magari na hata mtandao kumsaka binti yule alieaminika amejificha mahali.

*****
Taarifa zote zile kuna mtu alikuwa anazifuatilia kwa makini sana.
Kisha akachukua simu akapiga mahali,punde upande wa pili ukaitikia na yeye akasema

"Imekuwa kama tulivyotaka"

Kisha akasikiliza upande wa pili kidogo akakata simu na kuiweka mfukoni na akatoka nje ya eneo alilokuwa akatokomea anakokujua.

*****
Yote hayo yalipokuwa yakiendelea Koplo Mina yeye alikuwa ndo anarikabia lango la ofisi za Lengo media,akiwa na shauku ya kukutana na mhariri wa gazeti lile akiamini atampa taarifa muhimu anazozihitaji,akapita kwa pupa hadi mlangoni,na bila kufuata utaratibu akazama ofisini kwa mhariri bastola yake mbele,akapigwa na butwaa hakutarajia kukiona alichokiona mbele yake,bwana Mgimba alikuwa amekaa kwenye dimbwi la damu huku ikionesha risasi zaidi ya tatu zikiwa zimezama kifuani pake.....



Nb:Napenda kuwakumbusha kwa mwenye nia ya kuniunga mkono ili nipige zaidi hatua na Mimi basi nakuomba nichangie kupitia no hizi

0758573660
0658564341
0624155629

Asalaam Kudo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom