RIWAYA: Siku kabla ya leo

RIWAYA: Siku kabla ya leo

Hii hadithi huwa inatungwa na kuwekwa hapa au ilishatungwa tayari!
 
sehemu ya 13*

“Mambo si mambo huko koplo,unatafutwa kila pahali,naASCP Odeni kacharuka,yaani kifupi huko hakukaliki” alisema konstebo Tito huku akimgeukia koplo Mina aliekuwa amekaa kwa kuuegemea usukani.

ukapita ukimya wa nusu dakika,koplo Mina kashusha pumzi nyingi kisha akema bila kumgeukia konstebo Tito.

“unahisi hizo hekaheka hapo kituoni ni za kweli?”

Ikawa ni zamu ya konstebo Tito kufikiri kidogo kisha akaja na jibu lililomsisimua mwili koplo Mina

“Mawazo yako yapo sahihi lakini hadi sasa sijajua ni kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hicho kukuzuia wewe na mimi na huwezi amini nimepangiwa kazi nyingine na sijui kwanini mkuu anatetemeka bila kujua chanzo ni nini lakini pia nadhani tu kashindwa cha kufanya maana yawezekana kuna nguvu kubwa kutoka wakubwa zake na nimeshangaa zaidi umezuiwa kuwepo kazini hasa baada ya ugeni wa waziri mkuu kutoka [pale kituoni ahsubuhi ile na hapo ndo kila kitu kilibadilika’

Alimaliza kusema konstebo tito lakini hata kabla hajamaliza kumeza mate likaibuka jambo pale walipokuwa wamepaki gari huku wakijadili.

Ilikuja gari kwa nyuma yao na kuwagonga kisha hata kabla hawajajua wafanye nini kwenye ile gari ya nyuma wakatoka watu wawili wakiwa wameziba nyuso zao huku mikononi wakiwa wameshika bastola na kitendo bila kuuliza wakaanza kushambulia gari lile alilokuwamo kplo Mina na konstebo Tito.

Wa kwanza kutoka ndani ya gari ile alikuwa ni koplo mina,ni baada ya kuona watuwale wakishuka kishari hivyo akawahi kujitupa pembeni ya barabara akiucha mlango wazi.

Tito nae alipona vile akafungua mlango haraka na kujitupa upande wa pili kulikokuwa na gari kadhaa zimepaki huku nyuma akikwepamna na risasi kadhaa zilizoishia kutoboa magari yale.

Wavamizi wale lengo lao lilikuwa ni koplo mina,hivyo wote kwa pamoja mashambulizi yao wakyaelekeza kwa kule alipodondokea mwanamke yule ambae tayari alikuwa kasha chukua nafasi sehemu nyingine na kujificha huku akiwa nae katoa bastola yake lakini akiwa kachelea kushambulia kwa kuwa hakuipata nafasi ile.

******

Konstebo Tito aliinua kichwa kidogo na kutazama wavamizi wale na hapo akafanya jambo,akanyanyua bastola yake na kumlenga mmoja wa wavamizi wale na kumpiga risasi ya mbavu na kudondoka chini,akiwa anaitafuta shabaha nyingine ili ampige aliebaki akashuhudia jambo gumu kuamini,alimshuhudia koplo mina akiwa hewani huku miguu yake akiwa ameitanguliza kwa mbele na miguu ile ikamkita mvamizi aliesalia kifuani na kumdondosha mbali kabisa na koplo mina akisalia amesimama huku akiwa amejiweka fiti kabisa kwa pambano linguine.

Konstebo tito hakutaka kuonekana mzebmbe nay eye alitoka alipokuwa na kuyaruka magari kadhaa na kumfikia koplo Mina huku mtutu wake ukiwa mkononi kwa lolote na lipomtazama bwana yule



asalaamu kudo
 
Sawa BT unakuwa ni ngumu mno kuiunganish story coz unakuwa umesahau hata ulikomea wapi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom