RIWAYA: Siku kabla ya leo

RIWAYA: Siku kabla ya leo

Karefresh bana

Screenshot_20180314-082107.jpg
 
Sehemu ya 12*


Temba alimgeukia koplo Mina akamwambia habari alizopewa na rafiki yake ya kuwa Mbena ameonekana Mwanza ila amezuiliwa kituo cha polisi bila msaada.

Wakapanga kufanya jambo ila kabla halijafanyika hilo jambo ilibidi wamfuate Manyau waliemhifadhi katika moja ya vyumba mle ndani.

****
Macho ya Manyau yalishuhidia watu wawili wakiingia katika chumba kile alichofungiwa,alikuwa ni Koplo Mina na Temba.

Temba alimfuata na kuanza kumuuliza

"Kuwa muwazi Manyau nani amemuua Maiga na kwanini"

Manyau hakujibu alikaa kimya huku macho akiyaelekeza mashariki lakini hayakudumu sana huko yakarudishwa kasikazini haraka kwa konde zito la mkono wa kushoto wa bwana Temba.

Wakawa wakitazamana sawia na hapo Manyau akashuhidia hasira za wazi kwa Temba ila yeye alijua hasira zile si kwa ajili ya kifo cha Maiga,hasira hizi ni kwa ajili ya jambo lingine kabisa,jambo ambalo alilijua yeye na Temba na si Koplo Mina alie pembeni.

"Nakuuliza kwa mara ya mwisho,nani kafanya ujinga ule" aliuliza Temba,mara hii aliuliza kwa gadhabu ya wazi ambayo hata Koplo Mina alielewa na alijua kuna la zaidi baina ya watu wale na hata lile swali halikuwa la kifo cha Maiga lilikuwa swali la kitu kingine.

Koplo Mina akaona atachelewa kuujua ukweli uliojificha na muda unazidi kwenda haraka akampiga kikumbo Temba na akamfikia Manyau na bila kuuliza akashusha mvua ya kipigo.

Haikuzidi dakika tano,tayari Manyau hakuwa yeye,alikuwa karibia ya mfu hata sauti haikutoka vizuri na ilibidi aseme tu kile anachokijua.

"Nilitumwa na Zamda,lakini sikuua mimi,na sasa Zamda yupo Mwanza na hapa wamebaki kina Mafoo na wao ndo wanajua nani mhusika"

Koplo Mina akamgeukia Temba,na kabla hajauliza tayari Temba alikuwa ashasema

"Nawajua" Alisema huku akigeuka na kuanza kutoka ndani ya chumba kile,nyuma alimwacha koplo Mina akihangaika kujiuliza Temba ni nani na kwanini anamsaidia!

***
Walikaa kwenye sebule pana huku kila mmoja akimtizama mwenzie na punde Temba akauvunja ukimya ule.

"Hao watu ni washenzi hujapata ona,na nawajua wote,ila hawa Wafoo nadhani ni Saudi yako,tatizo mtu atakae kuwa nyuma yao ndie tatizo na sijui kama utasalimika"

"Kwa hiyo unanitisha na nani yupo nyuma yao" alisema Mina

Temba akashusha pumzi ndefu kisha akamtazama Koplo Mina na kusema

"Sina hakika ila nadhani ni yeye,japo sitakwambia lakini unapaswa kuwa makini sana katika hatua zako"

Waliendelea kuzungumza zaidi ya dakika kumi na wakapanga kugawana ili wakamilishe miyangisho yao sawa.

Koplo Mina alipangwa kubaki Dar na kushugulika na Wafoo ambao walikuwa ni watu wawili mapacha.

Na Temba alipanga kwenda Mwanza mchana huo kwa ndege binafsi ili apambane na Zamda akisaidiana na Mauna huku akimwahidi koplo Mina wakifanikiwa kuonana salama basi atamsimulia yaliomkuta kutoka kwa watu hao

*/**
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom