Riwaya: Penzi chungu

Riwaya: Penzi chungu

RIWAYA; PENZI CHUNGU
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010


Suto Sutani ni msichana ambaye hakuwahi kupendwa na mvulana yeyote katika maisha yake, kutokana na ubaya wa sura na ngozi yake. Lakini kwa maajabu anajikuta anaangukia katika dimbwi la mapenzi kwa kijana mtanashati Bruno Michael.

Penzi linalopitia katika visa na mikasa ya kutisha sana! Penzi linaloondoka na roho za watu kadhaa. Penzi linalomfanya Suto Sutani ageuke mkimbizi ndani ya nchi yake. Penzi linalomfanya Suto Sutani lazima auwe ili aweze kuishi. Penzi linalomfanya mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba kuingia kazini kumsaka Suto Sutani.

Je nini hatma ya Penzi hili Chungu? Je mpelelezi Daniel Mwaseba atafanikiwa kumkamata Suto Sutani na kujua kiini cha Suto Sutani kufanya mauaji? Nini itakuwa hatma ya Suto Sutani?
Mpigie wakala wa mkoa wako upate nakala ya Riwaya hii kali.

Wakala wa Kariakoo
Jina : Abrassa
0773985828 mkunguni na livingstone

DODOMA WAKALA
JINA KAVISHE
ST Mwanza avenue karibu na TRA
Phone 0654 070 744

KILWA MASOKO
JINA FATUMA
Muuza magazeti karibu na By night bar.
SIMU! 0656634642

Musoma wakala.
Jina Novanus Amiani
Barabara ya mkendo kubwa jengo la Embassy Hotel
Phone 0754 468 964

Moshi Wakala
Jina Osca Mmasy
Yupo jengo la seven eleven , barabara ya chagga
Phone 0769 483 595

Wakala Lindi
Jina Said Watanga
Yupo Stand ya mabasi inatizamana na NMB BANK
Simu 0718 689 619

Wakala Zanzibar
Jina Walid Salim
Yupo mbweni
Contact: 0789369601
0778828989.

Wakala Arusha
Jina Goodluck Mariki
Yupo barabara ya makongoro inatizamana na jengo la CCM mkoa.
Phone 0756 296 443

Wakala Kigoma
Jina Michael
Yupo Kigoma mjini opposite na EXIM bank
Phone 0755 823 527

Wakala Upanga
Jina Fahad Said
Yupo Gold Fashion
Contact: 0686821502

Manzese wakala
Kambangwa
Yupo opposite na JM hotel
O784508250/0763218019

Wakala Iringa
Jina Abel Kisimba
Yupo Uhuru road ,nyuma ya ukumbi wa Highland Hall

Mwanza wakala
Jina Mpombo
Yupo lwempisi house , mtaa wa Liberty
Phone 0756 348 074

Temeke wakala
Jina Hashimu mapengo
Tandika magorofani
Simu- 0714526379
 
Picha cover kitabu penzi chungu
 

Attachments

  • 1424888312400.jpg
    1424888312400.jpg
    52.5 KB · Views: 453
Huyo wa kwenye cover pic kama Mkurya halisi
 
MAWAKALA WA KITABU CHA PENZI CHUNGU.

Wakala wa Kariakoo
Jina : Abrassa
0773985828 mkunguni na livingstone

DODOMA WAKALA
JINA KAVISHE
ST Mwanza avenue karibu na TRA
Phone 0654 070 744

KILWA MASOKO
JINA HADIJA
Swanaha. Com..karibu na By night
Simu; 0652283663

Musoma wakala.
Jina Novanus Amiani
Barabara ya mkendo kubwa jengo la Embassy Hotel
Phone 0754 468 964

Moshi Wakala
Jina Osca Mmasy
Yupo jengo la seven eleven , barabara ya chagga
Phone 0769 483 595

Wakala Lindi
Jina Said Watanga
Yupo Stand ya mabasi inatizamana na NMB BANK
Simu 0718 689 619

Wakala Zanzibar
Jina Walid Salim
Yupo mbweni
Contact: 0789369601
0778828989.

Wakala Arusha
Jina Goodluck Mariki
Yupo barabara ya makongoro inatizamana na jengo la CCM mkoa.
Phone 0756 296 443

Wakala Kigoma
Jina Michael
Yupo Kigoma mjini opposite na EXIM bank
Phone 0755 823 527

Wakala Upanga
Jina Fahad Said
Yupo Gold Fashion
Contact: 0686821502

Manzese wakala
Kambangwa
Yupo opposite na JM hotel
O784508250/0763218019

Wakala Iringa
Jina Abel Kisimba
Yupo Uhuru road ,nyuma ya ukumbi wa Highland Hall

Mwanza wakala
Jina Mpombo
Yupo lwempisi house , mtaa wa Liberty
Phone 0756 348 074

Temeke wakala
Jina Hashimu mapengo
Tandika magorofani
Simu- 0714526379

Mbagala, Vikindu, Mwandege na Mkuranga
Simu; 0687 028898

Wakala wa mbeya
Jina zuberi marijani
Mobile 0763218014

Wakala morogoro
Faisal Nassoro
Mobile 0715 978 711
0779780355
 
SIMULIZI; PENZI CHUNGU
MWANDISHI; HALFANI SUDY


Cha ajabu na kushangaza wote watatu walikuwa wanakoroma. Mikoromo mikali sana. Kila mmoja alikuwa anakoroma huku anatabasamu. Alikuwa anajua kuwa anamdanganya mwenzake. Nani wa kumdanganya mwenzie kati ya watu wale watatu. Wote walikuwa mashujaa katika nyanja yake.

Mikoromo bandia ya watu wale ilivuka mipaka. Sauti za mkoromo zilipita mlangoni na kutokea jikoni. Pale alikolala Suto Sutani awali. Sauti hazikukomea hapo, zilisafiri na kutoka nje ya kibanda kile. Kule nje sauti ilisafiri kwa kasi zaidi ikisaidiwa na upepo na kufika katika sikio la mnyama mkali zaidi porini, Simba!
Simba yule jike nae hakuidharau sauti ile ya mkoromo, alianza kuifuata.
Ndio! Sauti ilimfikisha mpaka nje ya kibanda walicholala kina Mzee Mapengo.

Alipofika pale nje Simba alitulia, ghafla hakuisikia tena ile mikoromo, ilikata ghafla. Simba alikaa pale nje kama dakika mbili, hali ilikuwa shwari. Simba alikizunguka kile kibanda mara tatu, alivyomaliza akatulia katikati ya mlango. Akatoa muungurumo mdogo na kuamua kuingia ndani. Mlango ulikuwa mkubwa na uko wazi, hakukuwa na zuio lolote, aliingia ndani kwa madaha makubwa sana. Alipofika pale jikoni alisita kidogo, akabadiri mtindo, sasa alikaa kitayaritayari kupambana na chochote mbele yake. Aliunguruma muungurumo mkali, akiwa katikati ya mlango wa chumba walicholala Daniel Mwaseba, Suto Sutani na Mzee Mapengo.
Alipofika pale mlangoni, macho ya Simba yaliangalia haraka haraka na kuwaona maadui zake watatu..

JIPATIE KITABU CHA PENZI CHUNGU KWA SH 8000 TU...PIGA SIMU NO 0687028898 KAMA UNAKIHITAJI.
 
TANGAZO

Napenda Riwaya sasa iko WhatsApp..Ukitaka kuungwa Tuma Niunge kwenda
0757 633010
0714 526379
Ni 2000 kila mwezi mpaka mwisho wa riwaya mbili kali.
Majina ya riwaya ni
Biashara ya Kifo-asubuhi
FARIDA -jioni
Usipitwe na uhondo huu
Tunaanza kurusha riwaya jmosi..utaratibu ni kulipa elfu mbili ktk hizo numbers ukirusha tu..unamwambia ulie mrushia atakuadd. ...
Ila ukiwekwa Kwa group shart kubwa ni kwamba hutakiwi utume msg yeyote...ukituma chochote unajiondoa mwenyewe..
 
SIMULIZI YA MAPENZI; FARIDA
Imesimuliwa na Halfani Sudy
SIMU; 0674 395733

Sehemu ya Kwanza

Kilwa Masoko...mwaka 2014

Alikuwa ni mwanamke mzuri sana. Mwanamke mrefu, urefu usiochukiza. Alikuwa na sura ya duara. Nywele zake alikuwa amezikata vizuri ndogondogo. Alikuwa na umbo zuri lililotenganeshwa na kiuno chembamba. Kifuani, alibeba maziwa madogo ya duara. Tumbo dogo, yale wayabebayo walimbwende. Chini, alikuwa na mapaja ya haja. Mapaja manene yanayojaa vyema katika suruali. Alikuwa na miguu minene. Miguu iitwayo ya bia. Alikuwa anatembea kwa mwendo wa madaha. Huku akiacha mwili wake unatikisika vizuri sana kwa nyuma.

Hizo ni sifa chache sana za mwanamke niliyokuwa namsubiri. Sikuwa na miadi nae. Nilikuwa namsubiri apite tu ili nimuone.
Hakuwa mpenzi wangu.
Sikuwa namjua kwa jina.
Sikuwa najua anapokaa.

Sikwenda kazini ili nimuone mwanamke ambaye nilitokea kumhusudu sana. Mwanamke aliyetokea kuuteka moyo wangu ghafla. Kuzimeza fikra zangu.
Cha ajabu. Saa saba sasa hakuwa amepita. Alikuwa na kawaida ya kupita kila siku, saa tatu asubuhi, leo hii saa saba alikuwa bado hajatokea.

"Amepatwa na nini? Mbona mpaka sasahivi hapiti? Au anaumwa? Au amesafiri?
Au leo amepita asubuhi sana..

Siku yoyote atakayopita lazima nimueleze jinsi ninavyoumia juu yake. Nimueleze nia yangu ya dhati ya kutaka kuwa nae. Awe wangu. Nimueleze kama ninampenda kuliko mwanamke yeyote yule hapa duniani. Nimueleze kuwa nataka kuishi na yeye milele. Nataka kuwa sehemu ya maisha yake, awe sehemu ya maisha yangu. Nataka anikaribishe katika moyo wake, niweke kambi. Tena kambi ya kudumu..."

Nikiwa katikati ya mawazo mara nilimuona akija. Moyo uliniripuka kwa furaha.
Alikuwa amependeza kuliko siku zote.

Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya pinki. Blauzi nzuri yenye mistari meupe na meusi, rangi iliyofanana na mnyama pundamilia. Mkononi alikuwa amebeba kibegi kidogo cheupe. Alikuwa anatembea kwa madaha kuja pale nilipokuwa nimekaa.

Nilinyanyuka huku nikisema "Samahani dada"

Alisimama huku akiuliza kwa sauti ndogo " Unaniita mimi?"

Nilianza kumsogelea taratibu huku nikijibu "Ndio"

Leo ndio nilipata nafasi ya kuisikia sauti yake. Alikuwa na sauti nzuri mno. Sauti isiyo kera masikioni. Ilikuwa mithili ya sauti ya ndege chiriku.

Alisimama akiwa ananisubiri. Nilimsogelea taratibu. Kichwani mawazo mengi yakishindana kichwani kwangu.

"Samahani tena dada. Kabla sijakwambia sababu ya kukusimamisha hapa, naomba tufahamiane, mimi naitwa Nassib Omary"

Aliniangalia kwa tuo. Alinipandisha chini-juu. Kama alikuwa anathaminisha thamani ya kila kitu nilichovaa. Akabinua mdomo kidogo kwa juu. Akasema " Naitwa Farida.."
Akaanza kuondoka.

Nilimshika mkono. " Sasa mbona unaondoka Farida. Nilisema tutambuane kisha ndo nikueleze sababu ya kukusimamisha. Samahani sana lakini"

Farida alisema huku akifanya harakati wa kutoa mkono wake nilioushika imara "Nimechelewa sana leo. Naomba nitafute muda mwengine"

Niliendelea kumshika " kwani unaenda wapi? Unajua kila siku nakuona unapita hapa, unaenda wapi?"

"Subiri nikupe business card yangu. Nimechelewa sana yaani kaka. Tutawasiliana."

Aliutoa mkono wake niliokuwa nimeushika. Akafungua zipu ya pembeni ya mkoba wake. Akatoa 'business card'. Alinikabidhi.
"Tutawasiliana Nass" alisema kwa lafudhi tamu sana. Sauti itokayo puani. Zaidi, nilifurahia sana kwa jinsi alivyofupisha jina langu.

Alianza kuondoka kwa maringo. Niligeuka kumwangalia jinsi alivyokuwa anaondoka.

Nilikili kimoyomoyo " Farida alikuwa ni bonge la mwanamke"
Nilitabasamu.

Nilirudi kukaa kitini. Nilianza kuisoma 'business card' aliyoniachia Farida.

Kulikuwa na majina yake kamili. Namba yake ya simu. Barua pepe. Jina la sehemu anayofanyia kazi na mambo mengine kadhaa.

Nikaichukua ile namba ya simu na kuinakili katika simu yangu.
Niliiangalia jinsi namba ya Farida ilivyotulia katika simu yangu. Nilitabasamu tena.

Nilienda kazini. Mimi nilikuwa ni daktari katika hospitali binafsi ya Bakwata. Mwaka wa pili sasa tangu nihitimu masomo yangu ya fani ya utabibu katika Chuo kikuu cha Muhimbili.

Nilipomaliza masomo mwaka 2012 niliamua kurudi nyumbani ili kuwasaidia watu wa nyumbani kwetu. Nilifika ofisini na kuegemeza kichwa changu katika meza. Nikimuwaza Farida.

Nikiwa katikati ya mawazo. Ghafla nilistuka baada ya mlango wa ofisi yangu kusukumwa kwa nguvu.
Alikuwa nesi Rehema.

Kwa sauti kubwa alisema " Ajari! Dokta kuna mgonjwa kapata ajari ya bodaboda. Yaani ameumia sana Doktaa"

Sikumjibu. Nilibeba vifaa vyangu vya kazi harakaharaka. Nikaelekea chumba cha mapumziko. Nesi Rehema alikuwa mbele akikimbilia huko. Nami nilikuwa namfuata nyuma kwa kasi.

Tulipofika tu chumba cha mapumziko. Nilimuona. Nilichanganyikiwa sana...

ITAENDELEA... COMMENTS ZENU MUHIMU SANA ILI IENDELEE..
 
Back
Top Bottom