Kalamu Yangu
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,110
- 1,077
NITARUDI ARUSHA
Matukio ya siku ile yalimfanya aanze kuamini zile tetesi za kuwa wazazi wake wanafanya biashara haramu.Zile alizoziona kama tuhuma zilizotokana na wivu wa watu juu maendeleo ya wazazi wake zilianza kupata maana kichwani mwake na kuendea kumchanganya akili.Akiwa katikati ya lindi la mawazo hayo Alice alishtushwa na mlio wa kengele ambao ulionekana ulikuwa umeenza muda sana kusikika lakini kutokana na mawazo aliyokuwa nayo hakuusikia tangu mwanzo.
Alikurupuka na kuelekea mlangoni ambako alikutana mama yake akiwa na wadogo zake, walisalimiana na wakamtaka waende wote nyumbani kwa wazazi wake.Baada ya kutoa sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na uchovu alikubaliwa kuachwa pale nyumbani kwake kwa makubaliano kuwa angeenda kuwatembelea siku iliyofata.
Mahakamani, ndio ni mahakamani yupo pale kama watu wengine walioamua kuhudhuria hukumu y kesi ile iliyokuwa imevuta hisia za watu wengi sana.Hakujua ni nani alikuwa akihukumiwa siku ile kwani kila alipokuwa akiwatazama wale waliokuwa wamekaa pembeni yake walikuwa wakimtazama kana kwamba ndiye aliyekuwa akihukumiwa siku ile.Kamera za waandishi wa habari vyakitaifa na kimataifa zilikuwa zikimuelekea kila baada ya dakika chache.
Anaamua kugeuka nyuma nako anawaona wadogo zake wakiwa watokwa machozi wakimtazama kwa macho yaliyokosa tumaini,anawatazama nao wanainuka kutoka pale walipokuwa wamekaa na kwenda kukaa pembeni yake kushoto na kulia wakimkumbatia.Anawatazama wamekosa, wanaonekana wamekata tamaa lakini yeye bado haelewi nini kilichokuwa kikiendelea kilichowafanya wadogo zake walie.
‘’Dada tutawaona wazazi wetu tena?’’ Mdogo wake aliyekuwa amekaa kushoto kwake alimuuliza na akimtazama.
‘’Tutawaona si wale pale’’Alimjibu wakati huo mama yake alikuwa akionekana kizimbani akieleza maneno kadhaa kwa akiwakama anamsujudia hakimu.
‘’Dada huna uchungu na jambo hili, mbona kama unaona ni jambo la kawaida sana?’’ Mdogo wake wa mwisho aliyekuwa upande mwingine alimuuliza kwa sautiya kunong’ona.
‘’Nina uchungu wadogo zangu hili jambo tumwachie Mungu’’Alijibu kwa kifupi na kusikiliza kwa makini sauti ya baba yake aliyekuwa akiongea maneno ya kuusisimua moyo wake.
Wadogo zake walimtazama kama wakimwambia kuwa yeye ndiye tegemeo lao, hapo nafsi yake ikaiona kazi iliyokuwa mbele yake.Si kwa sababu ya kukosa pesa, pesa walikuwa nazo tena za kutosha tatizo lilikuwa upendo.Upendo wa baba na mama, kitu ambacho ni bahati kukipata, naam nao walikuwa wameipata nahati hiyo kwa muda mrefu na walikuwa wameshaizoeana ilikuwa ikienda kuzima kama mshumaa uliowaka kucha.
Akajikuta kwa mara ya kwanza akikumbwa na huzuni kubwa ingawa mwanzoni alikuwa akijiona shujaa kwa kufanikisha kile kilichokuwa kikitokea.Akataani kusimama atoke nje lakini miguu ilikuwa mizito aitamani atoe machozi lakini machozi yaligoma kutoka.Donge la uchungu lilimkaba shingoni na akaona wote waliokuwa mle ndani wakimsuta, kama vile nafsi yake ilivyomsuta.Akaona kukaa pale ni kujiba maumivu zaidi, maumivu ambayo hayakuvumilika, maumuivu malipo ya usaiti wake kwa kujivika ushujaa ambao aliona hauna maana tena maishani mwake kwani umempa maumivu ambayoanaona hayatapoa hadi siku ya kifo chake.
Ndiyo ni kifo chake ndicho kitakuwa mwisho wa maumivu yake ambayo ni malipo ya usaliti wake, wale waliokuwa wakimsifia mwanzoni kwa kulifanikisha hilo aliona wakimzomea na kumcheka kwa kumwingiza mkenge.Mkenge wa maana haswaa, ndiyo ameingizwa mkenge na watu ambao wao walikuwa wakiusaka umaarufu na pesa.Akajitahidi kusimama lakini miguu ilikuwa mizito akahisi wadogo zake wamemkanyaga lakini haikuwa hivyo nafsi yake ilikuwa nzito kumruhusu asimame , ilitaka ashuhudie hadi mwisho kile kilichokuwa kikitokea.
Akafanikiwa kusimama huku kamera za waandishi wa habari zikielekea kwake, hakuzijali akatoka kwa mwendo wa haraka, akiwaacha wadogo zake ambao kama walitaka kumfuata lakini waliahirisha na kubaki wamekaa kumtazama baba yao aliyekuwa akiendelea kuongea.Kichwani mwake alikuwa amekusudia jambo moja kujiua, kifo ilikuwa njia pkee ya kuikabili aibu ambayo aliona alikuwa ameitengeneza, hakujali maisha yakeningedharaulikaje alichokuwa akikijali wakati huo ni kuikwepa aibu akiwa hai.Kutoka pale alipokuwa amekaa hadi njea ya ukumbi ule alihisi nkama ni sehemu ya umbali wa maili nyingi sana kwani macho ya watu yote yalielekezwa kwake kana kwamba walikuwa wakimsuta.
Alipofika nje akaingia garini na kutoa gari kwa kasi ya ajabu, kasi ambayo alijua lazima angeipata ajali ambayo ingemtoa uhai.Aliingia barabara kuu kwa mwendo ule ule, hakufikisha hata mita mia gari iliacha njia na kugonga nyumba iliyokuwa pembeni mwa barabara.liutoa ukulele wa mshutuko akijishika kifuani pake ambapo usukani ulikuwa umembana.
Alice alishtuka usingizini akitokwa jasho huku bado mikono yake ikiwa kifuani, ilikuwa saa tisa usiku.Alitetemeka kwa hofu akiwa haamini kama ile ilikuwa ni ndoto.Akatoka na kwenda bafuni ambako aliamua kuoga ili apooze ile hofu aliyokuwa nayo lakini hata baada ya kuoga bado uoga uliotokana na ndoto ile mbaya ulizidi kuongezeka.Alijaribu kupata tafsiri ya ndoto ile lakini kila alichokuwa akibashiri aliona kinazidi kumwogofya.
Ingawa hakuwahi kuzichukulia ndoto kama kitu kinachoweza kutokea ama kuwa na maana yoyote lakini ndoto ile aliiona ikiwa na maana fulani kwake.Alijaribu kulala tena lakini bado maluweluwe ya ndoto ile yalibaki kumsumbua na kumnyima usingizi.Alijaribu kuchukua kitabu cha hadithi kukisoma lakini akaona kila kitabu kinaandika kugusia kile alichokuwa akikiota.Akaelekea sebuleni na kunywa maji , akaka kwenye sofa kivivu akiiangalia sebule ya nyumba yake iliyokuwa umejaa upweke hapo pia akamkumbuka Joseph.Mpenzi wake ambaye katika ndoto ile alionekana kumwingiza kwenye janga kwa ushauri wake mbovu.Akajikuta ameirudia ile ndoto mbaya, akasimama na kuwasha televisheni lakini bado akili yake haikuhama.
Akaona bora aondoke na kwenda wa wazazi wake, akaliendelea gari lake na kulitoa hadi nje safari hii akiendesha taratibu mawazo ya ajali ya ndotoni yalimtisha na kuamua kuendesha gari taratibu akielekea kwa wazazi wake.Zikiwa zimebaki nyumba kama tatu aifikie nyumba yao, aliona kundi la watu waliokuwa wamevaa makoti marefu wakitokea upande wa nyumbani kwao.Hakujua ni watu gani lakini alivyowakaribia na kuwamulika vizuri na taa za gari aliwaona wakiwa na silaha mabegani,chini mabuti yao yakikanyaga tope lililokuwa limetokana na mvua iliyokuwa imenyesha usiku ule.
Askari!
Akaropoka akikumbuka ile ndoto yake mbaya.
Wale waskari walipomfikia akapunguza mwendo ili asiwarushie tope lililokuwa palekwenye barabara nyembamba.Walionakena hawana habari naye kwani hakuna aliyeonesha umakni kumtazama, akashusha pumzi kwa nguvu na hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa akitetemeka mikono na jasho la uoga lilikuwa likimvuja makwapani na mfereji wa katikati ya mgogo ulipitisa jasho jembamaba la uoga licha ya baridi kali la usiku ule.
Alifika nyumbani kwa wazazi wake na kupiga honi kwa fujo akiamini mlinzi wao alikuwa katopea usingizini kama ilivyo kawaida yake, lakini ziku ile tofauti na siku nyingine.Yule mlinzi alichungulia kupitia kitundu kidogo na kulitambua lile gari kabla ya kufungua geti kwa tahadhari.
‘’We vipi mbona usiku hivi?’’ Aliuliza kwa wahka yule mlinzi wakati akifunga geti.
‘’Kuna tatizo mie kuja kwa wazazi wangu muda huu?’’Alice alimjibu kwa swali akielekea ndani.
‘’Kuja hapa si tatizo, tatizo kuja na nguo za kulalia’’Aliongea yule mlinzi akimkodolea macho kifuani yule binti mbichi.
Alice alijitazana na kuamini alichokua ameambiwa na yule mlinzi na kumgeukia yule mlinzi.
‘’Hayakuhusu’’Aliongea kwa kifupi na kuelekea ndani.
Alienda moja kwa moja hadi chumbani kwake, chumba ambacho alikuwa akikitumia akiwa hapo kwao.Huko akabadili nguo na kurudi sebuleni ambapo alikutana na macho mazito ya mama yake aliyekuwa usingizini akiwa amekaa kivivu kwenye sofa.
‘’Enhee vipi usiku usiku si ulisema ungekuja kesho’’Mama yake alimuuliza mwanaye ambaye naye alikuwa amekaa kwenye kochi lililokuwa likitazamana na lile alilokuwa amekaa mama yake.Wakati huo huo baba ayke alikuja sebuleni na kukaa pembeni ya mama yake.
Akamsalimia na kumgeukia mama yake kana kwamba anasubiri ruhusa ajibu swali lile aliloulizwa likiwa na chembechembe za shutuma, hofu na mshangao.
‘’Ndoto mama’’Alice alijibu kifupi.
‘’Ndoto imefanyaje?’’ Wazazi wake wakauiza kwa pamoja.
Alice aliisimulia ile ndoto yake iliyomtisha na kupelekea kufika pale nyumbani kwa wazazi wake usiku ule.Wakati anasimulia ile ndoto Alice alionekna akiogopa na kuna sehemu alikuwa kitokwa na machozi kabisa, baba yake ambaye alikuwa amekaa na mama yake akaenda kukaa pembeni yake alimzungushia mkono wake begani kwa namna ya kumpunguiza ile hofu yake.
Alice alimalizia na utata alioupata jioni ya siku ile akioneshwa kufadhaishwa na wazazi wake kumweleza uongo, akikumbushia vitisho vya yule askari mlevi.
Wazazi ake wakamtoa hofu na kumweleza kuwa ile ilikuwa ni ndoto tuu, na kumtaka akalale jambo ambalo kwake nalo lilikuwa mtihani kwani uoga bado haukumtoka na alijihisi kuwa na wazazi wake ni usalama wa pekee kwa wakati ule.
Wakaamua kuwasha televisheni na kuangalia hadi kulipopambazuka ambapo wazazi wake waliingia chumani kwao wakimwacha akianza kufanya kazi za mbalimbali za usafi pale nyumbani na wadogo zake wakiungana naye wengi wakishangaa dada yao kuwa pale alfajiri ile.
Baadaye wazazi wake wakamweleza Alice kuwa ajiandae kwa safari, naye akafanya hivyo na ilipotimu saa nne, watu a tatu walikuwa garini wakielekea Duruti.Walikuwa wakielekea ziwa, ambao Alice aliambiwa kuwa anapelekwa kwenda kutuliza akili, lakini Alice alihisi kulikuwa na kitu tofauti juu ya safari yake kwani ilikuwa kawaida wanafamilia wote kwenda huko ingawa aliambiwa, eti anafidia wenzake walivyoenda jana yake.
Alice aliwatazama wazazi wake ambao licha ya kuonekana kuwa na tabathamu na kuongea njia nziama juu ya uzuri wa sura ya Tanzania walionekana walikuwa na kitu kingine cha ziada kilini mwao.
Walifika ziwani na baada ya kutimiza taratibu zote, walienda kukaa mahali ambapo hapakuwa na harakati za binadamu pakiwa na ule upweke waliouhitaji wazazi wake kukaa wakiangalia majini ya ziwa huku wakila hiki na kile kunogesha mazungumzo yale mazito.
‘’Alice mwanangu’’Mama yake alimshtua baada ya dakika kadhaa za kila mmoja kufikiri alilooona linapaswa kufikiri, wakati wazazi wake wakifikiri namna binti yao atakavyolipokea jambo lile yeye alikuwa akifikiri jambo ambalo alikuwa akienda kuelezwa na wazazi wake jambo ambalo alikuwa na uhakika lilikuwa zito kulipokea akilini mwake na bila shaka lilikuwa ni jambo lililotisha.
‘’Abeeh mama’’
‘’Najua una maswali mengi kichwani mwako kuliko majibu, na tumekuja hapa kukupa majibu ambayo tuna hakika yatakupa maswali mengine ambayo bila shaka majibu yake ama utayapata ama yatakosekana ila tuna hakika yatapatikana yote’’ Alieza kwa kirefu mama yake ambaye hakuwahi kumwona akiwa katika hali ya umakini namna ile.
‘’Kwa hiyo yale niliyoota yalikuwa ya kweli?’’ Aliuliza Alice kwa wahka.
‘’Achana na ndoto zako wewe, hizo ndoto huwa zinakuja kama una tabia ya kushindia na kulalia chipsi kuku, ungekuwa unakula ugalia au mtori wala usingeota upuuzi huo’’ Aliongea baba yake na kuwafanya wote wacheke. Alice alikuwa wa mwisho kumaliza kicheko chake kwani alikumbuka hata jana yake mchana alikuwa amekula chipsi huku akisahau hata mara ya mwisho kula ugali.
‘’Turudi kwenye jambo letu, ni kwamba tumekutafutia nafasi ya kwenda kujiendelea kimasomo Australia……’’
‘’What? ‘’Alice aihamanika na kuongea kimombo akimkatika mama yake hata kumalizia kauli yake.
‘’Ndiyo, ni Australia mji nchi uliyokuwa ukiiota siku zote’’Mama yake aliongeza.
‘’Lakini mama……’’
‘’Lakini nini, kila kitu kipo tayari na kila kitu kipo tayari una wiki moja ya kujiandaa’’’Mama yake akamkatisha.
‘’Kazi?’’Aliuliza Alice.
‘’Kwa hiyo leo unaitamani sana kazi yako kuliko hamu yako ya Australia?’’Mama yake akamsuta kiaina.
‘’Hapana mama ni ghafla mno’’
‘’Siyo ghafla sema umejiingiza kwenye mahusiano hivyo unaona hatari ya kumpoteza, hilo si tatizo tunamfanyia mpango wa kumleta huko msome wote’’
Alice alishindwa afurahi, aone aibu ama asikitike, akabaki hajui aseme ama asiseme awaze ama asiwaze alibaki kama mtu ambaye akili yake imeganda kwa nukta kadhaa.
‘’Mbona unaonekana huamini, ndo hivyo tumeamua kutokuharibia furaha yako mwanetu’’Aliongeza baba yake amabaye alikuwa kimya kwa muda mrefu.
‘’Na ile ndoto?’’ Alijikuta ameropoka Alice.
‘’Na wewe mwanangu, umeanza kuziamini ndoto? , Kama unaziamini basi amini kuwa zilikuwa zikikutabiria kitu kizuri’’Aliongea baba yake akiokota jani lililodondoka kutoka kwenye mti walikuwa chini yake na kulitupia majini.’
‘’Hapana baba, ndoto hii imenitesa tofauti na ndoto zote nilizowahi kuota kwenye maisha yangu’’
‘’Kama imekutesa bali ilikuwa ikikuonea wivu kwa bahati hii iliyokuwa mbele yako’’ Baba yake akaingiza utani.
‘’Asanteni wazazi wangu kwa zawadi hiyo nzuri, asanteni sana lakini mie sipo kwenye mahusiano hivyo hilo suala la kwamba mtamleta na mwenzangu nisome naye linanichanganya’’Hatimaye Alice aliongea, na ni kama alikuwa amewatekenya wazazi wake, kwani walicheka hadi kufikia kutoa chozi.
‘’Sisi ni wakubwa zaidi yako, mwanetu’’Aliongea mama yake akimalizia kicheko.
‘’Kwa hiyo?’’ aliuliza kwa jazba kidogo.
‘’Tunajua mnapendana na Joseph’’
Moyo wa Alice kama ulitoka na kurejea mahali pake alipotajiwa jina hilo, mshtuko alioupata baada ya wazazi wake kumtajia jina la mtu aliyekuwa akimpenda kwa dhati na wazazi wake.Alijua wazazi wake wanajua mengi kuhusu Joseph.Alijua kuwa walikuwa wanajua kuhusu ukaribu wake na Japhet binamu yao ambaye kwa wazazi wake ni kama chui na mbuzi.
Hapo kichwa chake kikaanza kuyatafsiri yale maneno kwa namna tofauti na alivyokuwa akiyasikia, ni Australia kweli aliyoifahamu ama ni kifo?
Akaamua kujikausha na kuliweka kawaida.
‘’Asante sana wazazi wangu, asante kwa upendo huo’’Hatimaye akasema kwa furaha.
‘’Asante mwanetu, wewe ni faraja kwetu’’ Aliongea mama yake akitabathamu.
Baadaye wakaongea mengi wakala na kufurahia madhari ya Duruti na kurejea mjini.Alice alikaa pale kwa wazazi wake kwa siku kadhaa wakati huo akijiandaa kwa safari ya kwenda masomoni huko Australia, ikiwa ni pamoja na kuomba ruhusa huko kazini ambako kutokana na jina la baba yake haikuwa kazi kuipata.
Kilichomtia hofu hata siku tano baada ya ndoto ile ni kule kutojua lolote juu ya mipango ya mpenziwe Joseph kwenda naye masomoni.Hilo ndilo lilimfanya aende Moshi siku ile, na alipompigia simu na kuelezwa kuwa alikuwa Arusha ndipo alipoamua kumwambia Arusha si mahali salama kwake kwani alikuwa na kitu kilichomthibitishia hilo.
Alipata kujua hilo baada ya kufanikiwa kunasa mazungumzo ya baba yake na mgeni mmoja ambaye kwa familia ile hakuwa mgeni.Hakuwa mgeni kwani walikuwa ni watu waliokuwa kama ndugu.Hakuwa mwingine bali Daktari Mshana wanafamilia ile wakipenda kumwita Anko Mshana, mazungumzo hayo aliyasikia siku ile alipoenda kwa wazazi wake bila kuwataarifu na kwenda chumbani kwake.Akiwa chumbani nyumba ikiwa pweke alisikia gari likiingia pale nyumbani kwao na kwa kuwa hakuwa amenda na gari, haikujulikana kwa yule mgeni na baba yake kujua kulikuwa na mtu mzingine pale ndani zaidi yao wawili na mlinzi ambaye wakati Alice anaingia pale ndani alkuwa ameenda msalani.Kwa kuwa mwenyeji ambaye hakuwa na gari ilikuwa si lazima asubiri mtu wa ndani amfungulie ,hivyo Alice alijikuta pekee ndiye ajuaye uwepo wake pale ndani, hakufanya vile kwa lengo la kuchunguza ila ilitokea kama bahati ikawa siri na akapata kitu kilichomsaidia.
‘’Vipi twende ofisini ama hapa ni salama?’’ Daktari Mshana au Anko Mshana aliuliza akitazama huku na huko.
‘’Hapa ni salama hakuna kiumbe mwingine zaidi ya yule mjusi ambaye nadhani kapotea njia’’
‘’Kwa hiyo tumwamini yule mjusi?’’ Daktari Mshana aliuliza akimwangalia mjuzi aliyekuwa juu ya malango wa kuelekea jikoni.
‘’Unamwogopa?’’
‘’Kidogo’’
‘’Ngoja nikamuue’’Aliongea baba yake Alice na kwenda kumuua na kumtupia kwenye kasha la taka.
‘’Hapo salama, enhee nipe habari’’Alianza Daktari Mshana.
‘’Sina habari mpya ujio wako najua una habari ndiyo ninayoisubiri’’
‘’Okey, ni kuhusu yule mjusi ambaye naona kama amejiingiza kwenye jivu akidhani moto umezima kumbe anaelekea kwenye gogo lenye moto mkali’’
‘’Naam kaendeleza chokochoko zake tena?’’Aliuliza baba Alice aliyeelewa mjusi aliyekuwa akizungumziwa kitu ambacho hakukijua ni kwamba nyuma ya ukuta uliokuwa nyuma yake kulikuwa na kiumbe ambaye alikuwa akisikiliza kile kilichokuwa kikizungumzwa kwa umakini mkubwa.
‘’Naona anacheza ngoma asiyoijua, amejipeleka kwa yule nyoka aliyeng’olewa meno bila kujua yakiota anaweza kuja kumgeuka na kumgeuza mlo’’
‘’Unadhani anaweza kuja kuota meno?’’Baba Alie aliuliza.
‘’Nitamwotesha ili amgeuz…..’’Alianza kueleza Daktari Mshana lakini hakufanikisha kumalizia sentensi yake kwani alikatishwa na sauti iliyojaa mshangao mkubwa kutoka kwa rafiki yake ambaye ni baba Alice.
‘’Utamwotesha katika wakati hana kinywa?’’
‘’Ndiyo yataota tuu na yatakuwa na sumu kali sana ambayo bila shaka kila atayekutana naye kama hatokufa basi atageuka kuwa nyoka mkali zaidi yake’’Alifafanua kwa fumbo lililoeleweka kwa mlengwa.
‘’Ni hatari kwetu lakini’’Baba Alice aliongea Kinyonge.
‘’Kivipi?’’ Daktari alitumbua macho kushangaa ubaridi uliomwingia ghafla mwenzake.
‘’Huyo nyoka anaweza kugeuka na kuja kutushambulia’’
‘’Kivipi?’’ Aliendelea kushangaa Daktari Mshana.
Alice alishindwa kuelewa mazungumzo ya wale watu wawili aliokuwa akiwaheshimu daima lakini siku ile alijikuta akiwaogopa ghafla. Alitamani awafuate na kuwaambia kuwa wapunguze mafumbo ili naye aelewe lakini hakuwa na uwezo huo.Alibaki akiumiza kichwa akijaribu kuelewa kile kile kilichokuwa amekisikia kutoka kwenye vinywa vya wawili wale waliouwa sebuleni.Alijua kilichokuwa kikizungumzwa si tuu kilikuwa siri bali alihisi kilikuwa ni haramu kwani licha ya kuhakikisha hata mjusi alikuwa ameuawa waliamua kuendelea kuongea kwa mafumbo.
‘’Sijui wanawaficha wale samaki kwenye jokofu?’’ Alinong’ona kwa hasira Alice kule chumbani.
Wakati Alice akimiza kichwa kujua maana ya mijuzi na nyoka waliokuwa wakizungumzwa , baba yake aliinuka na kwenda kuchukua chupa ya mvinyo na bilauli mbili kisha akaijaza kwenye hizo bilauli na kumpa moja yule mgeni wake na nyingine akiinywa mwenyewe huku akikaa pale alipokuwa amekaa awali.Daktari Mshana akagundua kuwa kulikuwa na jambo kubwa ambalo ambalo mwenyeji wake alitaka kumweleza.
Kule ndani Alice alichukia ukimya wa wale wawili ambao aliamini wangeendelea kuongea basi angeweza kubahatisha kujua maana ya wale mijusi na nyoka wasio na kinywa.
‘’Daktari, huo mjusi umeshaingia kwenye nyumba yangu na ukigeuka nyoka utaweza kuharibu kila kitu’’Baba Alice alisita na kunywa funda moja la mvinyo kabla ya kuongeza mwingine kwenye ile bilauli kabla ya kuendelea.
‘’Ni hatari sana kama atageukia nyoka kwenye nyumba yangu kama atowaua wanafamilia basi atawageuza nyoka na wanitishie hata kuniangamiza’’
‘’Kama yupo ndani ya nyumba yako si rahisi tu kumwangamiza kama ulivyofanya kwa yule mjusi ambaye sahizi yupo kwenye kundi la taka nyingine?’’ Alihoji Daktari Mshana.
‘’Si rahisi kama unavyodhani, dokta’’Aliongea kwa unyonge na kuinua bilauli ya mvinyo na kuuunywa mvinyo uliokuwa umebaki na kuibamiza ile bilauli juu ya meza na kumshtua Alice kule chumbani ambaye nusura atoe sauti ya uoga.
‘’Kwa hiyo tufanye nini?’’
‘’Australia’’Alice alijikuta akitoka pale mlangoni alipokuwa amekaa kutega sikio na kwenda kitandani kwake akitetemeka huku akiuhisi mstari wa jasho uliokuwa ukipia kwenye makwapa yake.
‘’Atapelekwa lini, maana ameshakuwa hatari sasa kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya habari vinavyoniambia’’Aliongea baada ya kimya kifupi kidogo tangu baba Alice alipotoa wazo la Australia kwa hiyo mjusi ambaye kama angeachwa angeweza kuwa nyoka mkali mwenye sumu.
‘’Binti yangu akienda tuu masomoni mitafanya hivyo’’
‘’Lini anaondoka?’’
‘’Ana siku chache sana hazifiki tatu’’
‘’Si useme lini ama huniamini hata mie nduguyo?’’ Daktari Mshana aliuliza akimtazama rafiki yake usoni kwani aliona kama haaminiki.
‘’Mbona una mawazo hayo ndugu yangu mie nimekueleza siku hizo kwani najua uamuzi wa siku gani aondoke katika hizo siku tatu nimwachie mwenyewe katika kujenga Imani yake kwetu ili hata tukifanya chochote sije akatuhisi’’Alieza baba Alice akaeleweka, tofauti ni kwama hakujua kuwa si yule aliyekuwa mbele yake pekee ndiye aliyekuwa ameelewakile alichokieleza bali kulukuwa na mtu mwingine wa tatu ambaye aliyasikia na kuyaelewa yale maelezo yake.
Huyo mtu wa tatu alikuwa ni bintiye mpenzi Alice aliyekuwa nyuma ya ukuta ule uliokuwa umegusana na sofa alilokuwa amelikalia, tofauti na ilivyokuwa mwanzo wa mazunguzo yao yaliyokuwa yamejaa mafumbo ambayo bintiye alikuwa amesimama akiwa ametega sikio kwa makini safari hii alikuwa amejibwaga pale chini kama gunia lisilo na mzigo huku akibubujika machozi ya uoga na uchungu mkubwa.
Alikuwana haki ya kutoa machozi na kuwa na hofu kubwa, machozi yaliyotoka baada ya kuelewa kile alichokuwa hajakielewa mwanzoni.Hapo akaiona sura halisi ya moyo wa baba yake, ilikuwa imetawaliwa na ukatili na unyama tofauti na upole na upendo uliokuwa ukionekana kwenye macho ya wengi kupitia sura na matendo yake ya mwangani.Alice alifanikiwa kujua nyuma ya sura ile na matendo ya mwangani kulikuwa na roho katili na matendo mabaya ya gizani.
Alichoka.
Alitamani iwe kama ile ndoto ya na mwishowe aamke na kukimbilia kwa wazazi wake ambao wangemthibitishia kuwa iliuwa ni ndoto tuu na haingekuwa na maana , lakini haikuwa hivyo , ilikuwa si ndoto ya kutisha wala kusisimua bali ulikuwa ukweli uliotisha.Alijua kuujua ule ukweli mchungu uliomuumiza mtima wake.Ingawa aliwahi kusikia ubaya wa baba yake lakini hakuwai kuuamini alijua ni gere tu za wasakatonge wavivu na wenye husda juu ya familia yao, hapo zile tetesi za matendo mabaya ya wazazi wake zikarejea kichwani kwake kama mkanda uliokuwa ukikimbizwa na kuanza kuamini kila baya ambalo lilimhusisha baba yake kwani kitendo cha kupanga mauaji ya mpenzi wake ambaye alijua kabisa kuwa anampenda ilikuwa ni zaidi ya unyama.
‘’Ina maana na mama anayajua haya?’’ Aliwaza Alice.
‘’Huenda hajui, naomba iwe hivyo mama yangu mpenzi asiwe na roho hiyo ya kishetani ‘’Aliendelea kuwaza wakati huo aliwasikia wale wawili pale sebuleni wakiogea kama wakiagana.
Baadaye alisikia mlio wa magari mawili yaliyotanguzana yakitoka, hapo akajua kuwa baba yake alikuwa ametoka na yule mgeni.Alijitahidi kuinua miguu yake iliyokuwa imekosa nguvu na kufanikiwa kuchungulia kule getini alimwona mlinzi akifunga geti na kuzunguka upande ambao kulikuwa na choo na Alice hakutaka kupoteza muda aliinuka na kutoka nje kwani alishajua kilichokuwa kikimpeleka kule chooni yule mlinzi ni kuvuta bangi kwani ukimyana upweke wa nyumba ili ulimpa nafasi ya kuvuta bangi.
Aliwahi kumfuma mara mbili akivuta bangi, mara ya pili aliomba msamaha na kumweleza kuwa kwa kazi yake ya kukesha akilinda ilimbidi awe anavuta ili kuweza kukesha.Hivyo Alice alitoka nje ya nyumba ya wazazi wake na kuelekea barabarani ambako alikodi teksi kuelekea nyumbani kwake akiwa na hofu na uchungu mkubwa huku akijipa jukumu la kumwokoa mpenziwe, Joseph aliyejulikana kama mjusi mbele ya baba yake na Anko Mshana.
_______
Akiwa garini kuelekea kwake, Daktari Mshana amabaye alikuwa akifanya kazi katika hospitali ya Mount Meru jijini Arusha, alikuwa akiutafakari mpango ambao alishauriwa na Baba Alice ama Mzee Temu kama wengi walivyokuwa wakimwita.Ulikuwa ni mpango uliokuwa ukikinzana kabisa na mpango wake, mpango ambao alikuwa ameusuka siku nyingi tangu alipomwona Joseph kwa mara ya kwanza miaka mitatu iliyopita.Kwa kumtumia mwanaye Ludovick alifanikiwa kujua mengi kumuhusu kijana huyo na kusuka mpango ambao sasa ulikuwa katika hatua za mwisho kukamilika, mpango ambao ni yeye pekee alikuwa akiujua huku mwanaye akijua sehemu tuu ya mpango huo na aliyemwita ndugu yake mzee Temu na mkewe wakija kujua mwishoni alipoamua kuwashirikisha pale alipoona panafa tena ikionekana kama nasibu tuu.
‘’Yaani anadhani hadi leo sijui kuwa alikuwa nyuma ya mpango wa kumfanya mwanangu kipenzi kuwa mraibu wa madawa? Basi anajidanganya anacheza na mtu hatari sana’’ Aliongea kwa sauti ya chini Daktari Mshana na kutabathamu kisha kumaliza kwa kukunja moyo na sura yake kwa hasira.
Aliujua mwisho wa mwanaye utakavyokuwa, alijua ule unadhifu wa mwili na akili ya mwanaye ulikuwa na mwisho wake mwisho amabao utafunua upande wa pili na upande halisi wa uraibu wa madawa ya kulevya.Aliuogopa upande huo halisi kwani alikuwa ameshaushuhudia kupitia vijana wengi.Lakini alijikuta akitabathamu baada ya kujua kuwa mpango wake unaenda kupunguza machungu ambayo kwa namna ambayo itamfanya awe mshindi.
Wakati Daktari Mshana akifurahia mpango wake huo, upande mwingine Mzee Temu alikuwa akifikiri namna binti yake mpenzi atakavyoumia kumpoteza mwanaume wake aliyekuwa amempenda.hapo akakumbuka tukio kama hilo lililorudisha fikra zake mbali sana.
____
Ndani ya viunga vya chuo kikuu kimoja maarufu kilichopo kanda ya ziwa Viktoria, wanafunzi wawili wenye asili ya mkoa wa Arusha wamekaa wakiongea hili na lile kuhusu masomo yao.Ni mvulana na msichana.Hawa wamefahamaiana kwa bahati , ilikuwa ni wakati wanaatafuta mahali pa kwenda kufanya ‘field work’ katika taaluma zao.
Mvulana alikuwa aliyekuwa akisomea shahada ya Mahusiano kimataifa na msichana alikuwa akisoma ya Uhasibu.Walikuwa wamepata nafasi ya kufanya mazoezi kwa vitendo kwenye ofisi za Jumuhiya ya Afrika mashariki pale Arusha.Baada ya salamu na utambulisho wa hapa na pale huku kilia mmoja akionekana kutomwamini mwenzake moja kwa moja wakapeana namba za simu na kuanzisha mawasiliano ambayo yalidumu hata walipokuwa katika mafunzo yao kwa vitendo pale
Mawasiliano kwa njia ya simu na kuonana kazini pekee havikuwatosha vijana hao wasomi hali iliyopelekea kuwa na ‘mitoko’ mbalimbali katikati nan je ya jiji hilo maarufu kwa biashara na Utalii nchini.Hawakuishia hapo walifikia kutambulisha kwenye familia zao na hilo likawa kosa kubwa lilillokuja kubadili kila kitu kwenye historia ya maisha ya wazazi wao bila wao kujua.
Mzee Temu hakufurahishwa na ujirani wa bintiye na mtoto wa rafiki yake ambaye alimjua zaidi ya umma ulivyokuwa ukimjua.Hakua na Amani siku ile amlipotambulishwa na Alice bintiye mpenzi kuwa mtoto wa rafiki yake Daktari Mshana kuwa ni rafiki yake wa kiume na bila shaka walikuwa wapenzi.
Hilo lilimtia kiwewe kwani alijua ilikuwa ni mbinu na mpango wa Daktari Mshana kutumia mahusiano hayo kama karata ya kumpiku kwenye biashara zake ikiwezekana hata kwa mbinu ya kumwingiza bintiye kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.
‘’Ujanja ni kumuwahi’’ Hilo lilikuja akilini mwake na aliona ni jambo sahihi.
Hakuonesha kupingana na urafiki ama mahusianoano ya bintiye na mtoto wa Daktari Mshana mfanyabiashara mwenzake kwenye biashara haramu na hatari.Lakini akili yake ilikuwa ikihangaika kupanga mpango kabambe ambao ugetumika bila kuacha alama yoyote na kuleta matata zaidi.
Kama ambavyo Mzee Temu alivyoshtuka siku alipogundua kuwa kijana wake na binti wa rafiki yake wanaukaribu akahisi kuwa ulikuwa ni mpango wa mzee mwenzake kumharibia kijana wake na hatimaye biashara yake haramu.Naye bila kuchelewa akaamua kufanya kitu kabla ya mwenzake hajakifanya.
Siku ya mwisho wa mafunzo yao kwa vitendo ilifanyika shrehe ndogo ya kuwaaga na hilo Mzee Temu alilijua na akafanya kile ambacho alikipanga.Ilikuwa saa mbili na nusua ambapo Alice na mtoto wa kiume wa Daktari Mshana walikuwa nadani ya gari wakielekea kwenye hoteli moja iliyokuwa nje ya jiji la Arusha.Ilikuwa ni hoteli ghali sana ambayo ni nadra sana kwa vijana wa kitanzania wasiokuwa na kazi kupata nafasi ya kupata huduma zake.
Wengi waliokuwa wakitumia ni wazee kadhaa wakwasi waliokuwa ama na wake zao kwsa nadhra na agharabu walikuwa ana vimada , mabinti wabichi kabisa walishindwa kuzuia tamaa za pesa au wakitoa rushwa ya ngono ili wapate kazi Fulani waliyokuwa wameziomba.Pia kulikuwa na wazungu na watalii wengine kutoaka nchini waliokuja kutalii kwenye vivutio vingi vilivyokuwa mkoani hapo mkoa maarufu kama ‘Geveva ya Afrika’.
Wakiwa garini pombe walizokuwa wamezinywa kwenye sherehe iliyokuwa imeisha muda mfupi uliopita ziliwaondolea ile aibu waliyokuwa nayo kabla na kuwaongezea hamasa ya ngono.Alice alikuwa haishi kumsifia mpenzi wake huyo na kueleza jinsi alivyokuwa akimpenda huku mikono yake ikiupapasa mwili wa kijana yule ambaye licha ya kuwa alikuwa akiendesha gari lakini hakushindwa kujibu kwa maneno na mara nyingine kwa mabusu.Sauti ya muziki uliokuwa ukisikika kutoka kwenye spika za redio ya gari iliwaburudisha sana na kuwaongezea hamu ya tendo ambalo kwa Alice ilikuwa ni mara ya kwanza anaenda kulifanya kwenye hoteli aliyokuwa ameilipia kwa pesa nyingi alizokuwa amepewa na mzazi wake kwa ajili ya matumizi ya huko chuoni ambako alikuwa amebakiza siku mbili tuu kwenda..Hakusikitika kutoa hela ile kulipia kule hotelini kwani aliona ni heshima kuutoa usichana wake kwenye hoteli ghali na maarufu tena akitolewa na mtu aliyekuwa akimpenda sana na aliyeamini alikuwa mumewe mtarajiwa.Alijisahaulisha kabisa ule ushauri wa kufanya hivyo siku ikiwadia, siku atakayokabidhiwa rasmi kwa mumewe akiwa mke, alisahau ama alijisahaulisha au aliamua kupuuza hilo halikuizuia azma yake ya kufanya kile walichopanga kukifanya na yule kijana.
Upendo wa wazazi wake kwa kijana yule aliyempenda ilikuwa ni kama tiketi ya kumpenda, huku kupokelewa vyema na wazazi wa yule kijana kukimfanya ajione mwenye bahati sana.
Wakati Alice akiwaza hayo kwa kiwango kikuu cha upendo kwa upande wa yule kijana alikuwa mbali kiakili ingawa mwili uliitikia yale matendo yaliyokuwa yakifannyika ama kwenda kufanyika.Akili yake ililiwaza pendo pendo la msichana ambaye walipendana tangu wakiwa kidato cha tano na wakati huo alikuwa akisoma chuo kikuu cha tiba Mhimbili.Likizo ile ilikuwa ni likizo iliyoumiza moyo wa msichana huyo mvumilivu sababu ikiwa ni kijana kuingia kwenye penzi jipya lililokuwa limejaa mbwembwe za kila aina ya starehe.
Aliyakumbuka maneno aliyomtolea msichana huyo mbele ya rafiki zake kuwa hakuwa akimwitaji tena na wakati wake ulikuwa umeisha.Alizidisha maumivu ya msichana huyomrembo alipomwambia kuwa hakuwa na chochote kilichomvutia , si sura na tabia ile ya unyenyekevu alidai ilikuwa inatokana na umasikini wake hivyo alimbana ili tuu ‘amchune’ apate za kuilea familia yake na mama yake‘kikongwe’ ambaye si kwamba alikuwa ni kikongwe kweli bali ulemavu ndio uliomfanya aonekane kikongwe, maneno yale ndiyo yaliyomvunja moyo Grace aliyekuwa mpenzi wake.Na sasa ndani ya gari yalikuwa yakimrudia kijana yule kama vile alikuwa akiangalia sinema moja ya usaliti kwenye mapenzi.
Lakini kama wengi walivyosema, ‘’Ni vema akili kuuendesha mwili kuliko mwili kuiendesha akili’’ kwa kijana yule utundo na uchokozi wa kimahaba aliokuwa akifanyiwa na Alice ulbadilisha akili yake na sasa mwili wenye mhemko na uliochemka kwa mahaba uliendesha akili yake.Hakuwaza linguine zaidi ya ngono na baadaye mwili iliojaa hamu ukaamrisha akili yake kusimamisha gari pembeni.Macho yaliona haikuwa ni njia yenye harakati nyingi hivyo uliiamrisha akili kukubaliana na ulichokuwa umeamua.Alice alishtuka lakini akaelewa kile ambacho kilimfanya mpenzi wake asimamishe gari.
‘’Mpenzi sib ado kidogo tu tunafika hotelini?’’ Aliongea akisitisha harakati za mpenzi wake.
‘’Nimezidiwa laaziz nipunguze kidogo’’ Aliongea yule kijana kwa kubembeleza.
‘’Hapana si unajua sijawahi kufanya nitaumia sana twende tuu hotelini’’
‘’Unasema?’’ Aliuliza yule kijana kwa msahangao.
‘’Hujanisikia love jamani’’ Aliongea kwa kuchombeza Aloce huku akimwita mpenziwe kimombo.
‘’Siamini mpenzi’’Yule kina aliongea akimtazama, hakuamini kama msichana yule aliyekuwa amefikia ngazi ya chuo kikuu bila kufanya mapenzi.
Hakuamini kama wengi ambavyo hawaamini kwa dunia ya leo vijana kutojihusisha na mapenzi hadi umri huo wengi huanza michezo hiyo wakiwa sekondari hivyo kusikia kulikuwa na mtu aliyefikia chuo kikuu bila kufanya mambo hayo alihisi palikuwa na tatizo.
‘’Huamini nini bado dakika chache tuu utaamini mpenzi’’ Alice aliongea lijua mpenziwe hakuwa akiamini na sasa alianza kuamini kwani kila alipokuwa akimwambi hapo awali alijua ni kawaida kamaw alivyo wengi na siku ya siku huja na sababu kibao.
‘’Sawa ngoja nipunguze maji maana zile pombe ni hatari’’Aliongea yule kijana akifungua mlango wa gari lile ghali la baba wa mpenziwe alilokuwa akiliendesha.
Hakufanikiwa kumaliza kufungua mkanda wa suruali yake ili akojoe kwani alishtukia akiguswa na ubaridi wa chuma sehemu mbili za kichwa chake, juu ya masikio yake mawili na akipewa amri ya kutulia na kutosema chochote.
Kilichofuata ni yeye na mpenzi wake kufungwa Kamba ngumu na kuingizwa kila mtu kwenye gari lake.Hkaujua kilichofuata hadi baada ya wiki moja alipojikuta akiwa katika hali ambayo hakuwahi kuwaza kuwa angeweza kuwa nayo kwenye maisha yake.
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kufanyika kwani ndani ya dakika mbili kila nkitu kilikuwa kama kilivyokuwa awali.Alice alikuwa akilia tangu pale alipokamatwa kwa nguvuna mtu aliyeingia kupitia mlango ambao dakika moja mpenzi wake aliutumia kutoka.Mwanzoni alijua ni mpenzi wake ameamua kutumia nguvu kupooza hisia zake lakini halikudumua kilini hata kwa nukta mbili kwani aliona hata mpenzi wake amewekwa chini ya ulinzi na mabazazi wale wasio na chembe ya huruma na kuingizwa kwenye gali linguine lililosimama mbele nyuma ya gari lako na kuelekea walikotokea huku yeye akiendeshwa na mmoja wao na kuelekea kule walikokuwa wakielekea.Dakika chache baadaye gari aliliopanda Alice lililikaribia lango la hoteli ile ghali ambayo Alice na mpenziwe waliakuwa wamepanaga kwenda kuitumia kwa ajiri ya kuburudisha nafsi na miili yao lakini safari hii alikuwa Alice na vijana wawili watekaji , alifunguliwa kamba alizokuwa amefungwa na kupewa maelezo kuwa alitakiwa kutulia na alitakiwa kuongoza huko.
‘’Mmejuaje kama tulichukua chumba hapa hotelini?’’ Aliuliza akitetemeka.
‘’We fuata maelezo ukileta upumbavu nafumua ubongo wako’’Aliongea yule mtu kwa sauti ya chini lakini yenye ukali.
Alice hakuongea kitu zaidi ya kufuata maelezo akili yake ilimwambia huenda ni mpango wa baba yake ambaye huenda hakupenda mahusiano yake na yule kijana lakini wazo hilo alipingana nalo kwani baba yake hakuwahi kuonesha hilo.Walitembea kulekea hotelini wakipita kwenye viunga vya hoteli ile ghali iliyopambwa kwa maua na taa za kuvutia usiku ule.Yule mtu mwingine aligeuza gari na kutoka nje ya eneo la ile hoteli na kuzidi kumchanganya Alice.
Lakini wazo la kuwa mpenzi wake kaamua kumfanyia mchezo na kumpora gari lile la thamani lakini upendo kwa yule kijana ulilipinga hilo pia akaamua kuachana na mawazo hayo na kufikiri namna ya kujinasua na janga lile.Walionekana kama wapenzi huku mkono wa Alice ukilazimishwa kuwekwa kwenye bega la yule kijana ambaye kwa sasa suti yake nadhifu na sura ya kuvutia vilionekana vema.Huku mkono wa yule mwanaume mtekaji ukikishika kiuno cha yule binti mbichi aliyekuwa akitetemeka ndani kwa ndani kwa uoga lakini hilo halionekana kwa yeyote hata walipokuwa wakipishanana na watu wawili waliokuwa wakitoka kwenye lifti iliyokuwa ikiwapeleka kwenye chumba namba 107 kilichokuwa kwenye ghorofa ya nane na ya mwisho ya jengo lile la hoteli hawakuweza kugundua kuwa hawakuwa mtu na mpenziwe bali ni mtekaji na mateka wake.
Walitoka kwenye lifti na kutembea kufuata korido ndefu iliyowafikisha pale ambaoo Alice na mpenziwe walipanga kwenda kupumzika wakati ule.Yule mtekaji alitoa kadi maalum na kufungua mlango wa kuingilia pale ndani, hilo lilimwacha kinya wazi Alice kwa mshangao.
‘’Ina maana walikuwa hata na kadi ya kufungua hapa chumbani?’’ Alijiuliza Alice kimya kimya wakati huo alikuwa ameshasukumwa ndani ya kile chumba na mlango ukafungwa.Akaingizwa chumbani na baada ya kudhibitiwa wa kufungwa kambana kufungiwa mle ndani kisha yule mtekaji akarudi palipokuwa kama sebule ya kile chumba kilichokuwa na kama kaunta ya baa kutokana na kuwa na vinywaji vya kila aina.
Yule mtekaji alikuwa akitathimini cha kufanya baada ya kumfikisha Alice pale kwani kwa maelezo wangemteka yue mpenzi wa Alice akiwa mle ndani kisha kumtisha hata kumtegua Alice na kumpa majeraha kisha waondoke na yule kijana.Sasa mambo yalikuwa tofauti na walivyotegemea kwani walipata upenyo wa kuwateka wakiwa barabarani ambako waliona palikuwa mahali salama.Alitamani ampigie aliyewapa mpango huo ambao walikuwa wameshapokea nusu ya pesa kwa ajili ya kazi ile.
‘’Ngoja nipige pombe za bure bwana kazi imekuwa rahisi sana’’Aliwazana kuinuka kuchukua chumba mbili za pombe kali na kuanza kuzinywa kwa pupa huku akipuuza hata bilauli zilizokuwa zikimtizama mezani.
Baada ya kama nusu saa tangu waingie pale hotelini, yule mtekaji alikuwa ameshaanza kuelemewa na kilevi na kama ilivyokuwa kawaida kwake ulevi ulikuwa ukiambatana na hamu ya ngono.Akafikiri wapi angeipooza ile hamu akakumbuka kuwa kulikuwa nab inti mbichi aliyekuwa mateka chumbani hivyo angeipooza hapo.Wazo la kwenda kumwingilia Alice lilipita bila kipingamizi.
Aliingia chumbani na kumkuta Alice akiwa ameangukia chini, bila shaka katika harakati zake za kutaka kujitoa kwenye Kamba ambazo alikuwa amefungwa mikononi na miguuni na yule mtekaji kabla hajatoka na kwenda kubwia pombe ambazo hakuzitolea jasho.Purukushani za kutaka kujiokoa bila mafanikio ziliikusanya sketi yake fupi na kuonesha sehemu kubwa ya mapaja yakelicha ya taa ya rangi iliyokuwa imewashwa na yule mtekaji wakati anaingia mle ndani uzuri wenye kutamanisha haukuweza kujificha.Alice aliona aibu kuwa vile mbele ya mwanaume yule kwenye ile hali lakini hakuwa na namna ya kuificha aibu ile.
Yule mtekaji mlevikwa pupa akamfungua zile kamba na kurarua kile kisketi kifupi alichokuwa amekivaa yule binti na kumzidishia hamu iliyokuwa imechochewa na pombe alizokuwa amezinywa.Alikifuta na kile kikoti cha suti nyeusi iliyokuwa imevaliwa juu ya kiguo chepesi cheupe kilicoendana na viatu vya yule binti mrembo ambaye saa chache zilizopita alikuwa miongoni mwa wanadamu waliokuwa na furaha duniani.Matiti ya yule binti yalimoa mate yule Mtekaji na kumfanya apaparike kufungua mkanda wa suruali yake nadhifu mwa mkono mmoja huku mkono mwingine ukiwa umelekeza bastola kwa Alice aliyekuwa akitetemeaka kwa uoga.
‘’Hivi naenda kubwakwa na huyu mjinga, Mungu wangu naomba nisaidie’’Aliongea alice kwa uoga huku akili yake ikidhani alikuwa amewaza tuu bila kutamka.
‘’Nani mpumbavu we Malaya?’’ Yule mwanaume aliongea kwa hasira akimnyanyua kwa kumshika shingoni kwa mikono yake mikubwa na yenye nguvu na kumtupia kitandani na kuivuta nguo ya yule binti na kuitupia pembeni.
Alice alitetemeka kwa uoga kwani mwanaume yule alionekana kumzidi nguvu na alikuwa na uwezo wa kutekeleza kile alichokuwa amedhamiria.Pombe zilizokuwa kichwani kwa Alice wakati yupo na mpenziwe saa chache zilizopita zilikuwa zimeshaisha na akili yake ilionekana kuchoka kwa mbali.Alijilazimisha kufikiri kwa haraka na akili yake ikakubali kufikiri haraka ikikwambia kuwa muda huo nguvu ilitakiwa kutumika zaidi tatizo likawa kuwa nguvu zake zilikuwa zinedhibitiwa.
Yule mwanaume alikuwa akihangaika kuuweka mwili wa Alice vizuri ili apate nafasi ya kufaya kile alichodhamiria kumfanyia na pale miguu ya Alice ilipoonekana kukosa nguvu na kukubali kuwekwa vile alivyotaka mbakaji yule jambo moja lilifanyika na kunfanya asitishe kile alichokuwa amekifanya.Ilikuwa ni sauti ya king'ora cha usalama kilichokuwa ukutani kimebonyezwa kwa bahati mbaya na mguu wa Alice uliokuwa umetupwa kwa nguvu.Hiyo ilikuwa ni nafasi kubwa kwa Alice ambaye alishika sehemu za siri za yule mtekaji na kuzivuta akimwachia maumivu makali yule mtekaji mbakaji.
Wakati yule mtekaji amejikunja pale kitandani akipata maumivu makali Alice alitumia sekunde tano kubonyeza kile king'ora cha hatari ambacho kilileta taharuki na purukudhani kwenye yumba mbali mbali ya hoteli ile.
Alichukua mkoba wake na kutoka pale chumbani akinfungia yule bazazi mle chumbani.Alice alitumia muda mfupi sana kutoa kanga mbili alizokuwa ameziweka kwenye mkoba wake mdogo na kuzifanya vazi lake na mbio mbio akatoka nje ya kile chumba apishana na watu waliokuwa wakihangaika huku na huko kuangalia pakitokea.
Wafanyakazi wa hoteli waliwataka watu kutulia na kushuka kwa itaratibu wakiwazuia kutumia lifti kwa kuhofia madhara zaidi kwani king'ora kilichosikika kilikuwa ni tahadhari ya uwepo wa moto.
Alice alijua kuwa hakukuwa na moto hivyo hakuwa na wasiwasi alipishana na watu waliokuwa wakikimbia huku na huko.Akaingia kwenye lifti iliyomchukua peke yake hadi chini ambako alimpigia simu baba yake kuwa alikuwa hatarini.Dakika chache baadaye baba yake alifanya mawasiliano na watu wa hoteli na kupata gari moja lililomtoa Alice hapo hotelini hadi nyumbani.
Baada ya kujieleza huku akificha baadhi ya mambo na kisa kilichomfikisha huko hotelini, kitu ambacho hakujua kuwa baba yake alijua kila kitu Mzee Temu na mkewe wakampa pole wakimuuliza kama kulikuwa na tatizo lolote apelekwe kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.Lakini Alice alidai yupo salama licha ya wazazi wake kung'ang'ana sana juu ya kuangalia afya yake.
Maelezo ya Alice yalimpa mwanga Mzee Temu juu ya kilichotokea na kitu cha kwanza alichokifanya ni kutuma watu wake waliokuwa pale hotelini kwenda kumtoa yule mtekaji na kumfutilia mbali kukwepa ushahidi, pia aliwaagiza aliowapa kazi ya kuingilia mawasiliano ya kamera za ulizi kuyarudisha kwenye hali ya kawaida baada ya kutoa mtu huyo hapo hotelini.Ambacho hakukijua Mzee Temu ni kuwa mtekaji yule rijali alikuwa kilometa moja kutoka eneo la tukio kwani wakati Alice akishuka na lifti yeye alikuwa upande wa nyuma akishuka kwa kamba huku akiamini hakukuwa na kamera ya kuinasa sura yake kwani alijua hakukuwa na kamera ikiyorekodi chochote kati ya zile purukushani.Alipofika chini alitoka kama watu wengine waliokuwa wametaharuki kwa hofu na kutembea hadi mahali walipoweka pikipiki kwa ajili ya dharula na kuiondoa kwa kasi kuelekea Moshi.
Alijua kwa kosa alilokuwa akitaka kulifanya ama alishalifanya kwa namna alivyojua aliwapa ile kazi angetafsiri lazima kifo kingekuwa kikimfuata.Hivyo aliamua kukikimbia akielekea Moshi kisha aende Rombo na baadaye avuke kupitia Tarakea kuingia Kenya ambako alihisi kungekuwa salama.Lakini alikuwa amekosea sana badala ya kukikimbia kifo mtekaji yule mpenda ngono baada ya kubwia pombe alikuwa kikifuata kifo kwani vijana kadhaa walitumwa kutokea Moshi naalipofika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA alipata ajali mbaya sana kwa kugongogwa na roli tupu la mizigo na habari zake ziliishia hapo huku mabaki ya mwili wake yakipelekwa kwenye hospitali ya wilaya ya hai kuhifadhiwa , mabaki ya pikipiki ile ya wizi yakiwekwa kwenye kituocha polisi cha Bomang’ombe.
Kule nyuma Alice na yule mtekaji waliacha kizaazaa cha uwepo wa moto ambapo baada ya hali kutulia ilikuja kujulikana kuwa king’ora cha tahadhari kilikuwa kimeminywa kwa bahati mbaya.Wateja waliombwa msamaaha kwa tukio hilo huku wakitoa ofa mbalimbali kama sehemu ya kufidia kosa hilo.Kama ilivyokuwa kawaida kuna wale wasiopenda usumbufu ambao waliona palikuwa na namna nyingine ya kuuzuia , walizipuuza ofa hizo na kuhamia hoteli nyingine ya hadhi hiyo iliyokuwa na kiwango cha juu kama hiyo zaidi ama iliyokaribiana na hiyo, na hao walikuwa wachache hawakuzidi watano.
Taarifa ya taharuki ile pale hotelini hazikufika mbali hasa kutokana na kutokuwa kwenye ‘changanyikeni’ ambako waandishi wa habar wasio rasmi huwa amkini muda wote hata iwe saa nane za usiku kupata na kusambaza habari hasa zile mbaya.
Siku iliyofuata akiwa na mawazo mengi juu ya alikokuwa amepelekwa yule mpenzi wake Alice alikuwa safarini kuelekea Mwanza chuoni.Alijaribu mara kadhaa kumtafuta simuni mpenzi wake mpya hakupatikana mara zote alizokuwa akimpigia.
Wiki moja baada ya kufika Mwanza Alice alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa alikuwa ni Daktari Mshana.
‘’Haah!hii namba sikuwa nayo vip habari za huko Kenny bado hajaonekana?’’ Aliuliza Alice akimuulizia Kennedy ambaye walizoea kumwita Kenny.
‘’Amepatikana, na kakuulizia sana na keshokutwa ataweza kuja ila sahizi anapata matibabu’’
‘’Matibabu walimuumiza jamani?’’
‘’Hapana hakuumizwa sana si unajua huyu mwenzako mayai sana kwa hiyo karudi kajilegeza mwe yewe na huko ndani sijui hata mkivamiwa nani sijui atamwokoa mwenzake’’Aliongea Daktari Mshana na kucheka akimfanya Alice naye acheke.
‘’Hapana walitufunga zile kamba watakuwa walimuumiza’’Alimalizia kicheko na kuongeza Alice.
‘Kwa wewe mwanamke sawa lakini ye mtoto wa kiume inabidi ajikaze’’
‘’Sawa baba naweza kuongea naye nimsalimie?’’ Alice aliongea kwa wahka, wiki nzima alikosa Amani kutojua alipokuwa mpenzi wake huku akijiona mwenye hatia kwenda kuchukua chumba kwenye ile hoteli ambayo hakujua kuwa baba yake alikuwa na hisa nyingi.
‘’Amelala akiamka atakupigia’’
‘’Nitafurahi sana kumsikia ’’Aliongea Alice bila kujua simu ilikuwa imeshakatwa.
‘’Mungu umlinde mpenzi wangu Kenny awe salama’’Aliongea na kushusha pumzi ndefu Alice ambaye alijikuta akiwa na furaha.
Kujua kama mpenziwe alikuwa salama ilikuwa habari njema kwake iliyokuwa na maswali mengi juu ya wapi alipopelekwa mpenzi wake mpya kwa muda wote wa juma zima.Mtu pekee wa kujibu maswali yake ilikuwa ni Kennedy ambaye aliambiwa alikuwa amelala na baada ya siku moja angekuwa karibu yake wakiongea hili na lile.Lakini hadi usiku unaingia hakupokea simu yoyote kutoka kwa Kenny wala baba yake ambaye Alice alikuwa akimwita Anko.
Siku ya pili nayo ilipita bila simu wala taarifa yoyote, siku ya tatu ambayo alitegemea angemwona Kenny nayo ilipita ikiwa na ukimya uliomnyong’onyesha Alice.
Siku ya nne, juma la kwanza, la pili, la tatu , mwezi na baadaye miezi mitatu iliyohitimisha muhula wa wa masomo kwa mitihani iliisha bila taarifa zozote kutoka kwa Kenny ama baba yake.
Aliporudi Arusha akiwa na hamu kubwa ya kujua kilichomsibu Kenny Alice alikutana na taarifa iliyomnyong’onyesha akili yake.
Baada ya tukio lile ambalo kwa wengi lilifanywa siri Kennedy ama Kenny kama alivyokuwa akiitwa na wengi alipelekwa nje ya nchi.Ilikuwa ni safari maalum na ya siri ya wanafamilia wachache ambao wengi wao waliambiwa kuwa ilikuwa ni baada ya kijana huyo kupata ufadhili wa kwenda kusoma huko.
Taarifa hiyo ilikuwa mbaya kwa Alice ambaye alijua ulikuwa ni mwisho wa penzi lao changa ambalo licha ya kudumu kwa muda mfupi sana lilikuwa na ishara njema huko mbele.Lakini penzi hilo lilififia na kupotea kwa kasi kama moshi wa sigara upoteavyo kwenye uwazi.Kitendo cha Kenny kuondoka bila kumuaga kilikuwa kimemuumiza sana na ilikuwa ni kama ishara ya kuwa penzi lao lilifika mwisho.
Hakutegemea kama kulikuwa na chembechembe za upendo kutoka kwa kijana yule ambaye alijua kuwa alikuwa mume bora mtarajiwa na baba bora wa wanawe Mungu akiwabariki hilo.Alianza kumhusisha na tukio lile akihisi kuwa huenda alishiriki kusuka mpango ule na kupoteza hisia hizo akaamua naye aonekana kuwa alitekwa na kuteseka zaidi na baadaye angepata mgao baada ya kuuza gari.Aliamini hivyo kwani hakujua kuwa ile gari ilikuja kukutwa imetelekezwa kwenye nja moja iliyokuwa ikielekea Arumeru na baba yake akaamua kuliuza.
Hilo Alice hakulijua si kwamba hakujua kwa kuwa hakutaka kujua bali hakupata nafasi ya kujua hilo jambo ambalo liligubikwa na usiri mkubwa.Hivyo akajikuta aimchukia Kenny na kumwona kama mwanaume mwenye roho mbaya na tamaa ya kupata kile ambacho hakukitolea jasho.Taratibu jina la Kenny likimtoka moyoni mwake na akaanza kuyachukia mapenzi.
Kitu ambacho hakikujua ni kwamba nyuma ya tuki lile kulikuwa na mtu mmoja ambaye aliupanga mpango na kuratibu utekelezaji wake na ukafanikiwa kutekelezwa kwa asilimia zaidi ya tisini.
_________
Baada ya Daktari Mshana kujua mahusiano ya kijana wake na binti wa mzee Temu ambaye nje ya shughuli zake rasmi na biashara halali alikuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa baishara ya madawa ya kulevya kama alivyokuwa yeye.Walikuwa na urafiki wao ambao uliunganishwa na baishara hiyo ambayo walikuwa wameanza kuifanya muda mrefu wakitumia watalii ambao nao walihusika na biashara hiyo wakiziunganisha nchi mbalimbali walizokuwa wakitalii kusambaza na kuukuza mtandao wa biashara hiyo haram.
Hawa walikutana kwa bahati sana tangu wakiwa vijana, wakati Mzee Temu kipindi hicho akiwa kijana alikuwa akimiliki kampuni la kusafirisha watalii na kuwapeleka kwenye vivutio mbalimbali vya utalii vilivyokuwa mkoani Kilimanjaro na Arusha.Mtaji wa bishara hiyo aliupata kutoka kwa dada yake ambaye alikuwa pia mfanyabiashara mkubwa wa nafaka soko lake kubwa likiwa Kenya na Ethiopia ambayo kwa kipindi hicho ilikubwa na Ukame.
Wakati ukame wa Ethiopia ukiwa ni janga wa watu na serikalai yao kwa dada yake Temu ilikuwa neema kubwa iliyomtengenezea faida kubwa ambayo ilimfanya ampe mdogo wake ambaye alikuwa mmoja wa wafanyakazi wake mtaji wa kuanzisha biashara yake.
Wakati Temu akikamilisha taratibu za kuanzisha kampuni yake ya kusafirisha watalii kuwapelekea kwenye vivutio mbalimbali vilivyokuwa vikivuta wageni wengi kutoka Ulaya na Marekani, kijana mmoja msomi wa Udaktari katika chuo kikuu kikongwe cha afya cha Pavia kilichoko kwenye mji wa Pavia nchini Italy alikuwa kwenye mipango ya kurudi likizo nchini Tanzania.
Kijana huyo wa Kipare ambaye uwezo wake mkubwa darasani na urafiki wa baba yake na padre mmoja wa kanisa la waadventisti vilimfanya apate bahati ya kwenda kusoma kwenye moja ya vyuo vikongwe kabisa duniani katika tasnia ya utabibu aliiandaa safari yake hiyo akiwa na rafiki zake wengi ambao walikuwa wanachuo wenzake kutoka nchi mbalimbali duniani.
Marafiki hao waliokuwa wakitamani kwenda kutalii nchi nyingine za Afrika lakini kwa ushawishi wake alifanikiwa kuwafanya waje Tanzania kutalii kwenye vivutio vingi ikiwa ni pamoja na mlima mrefu barani Afrika uliokuwa na theluji, mbuga kubwa ya wanyama ya Serengeti,hifadhi ya Arusha Manyara ,Ngorongoro na bonde ambalo lilisadikiwa kuwa kulikuwa na fuvu la binadamu wa kale zaidi ulimwenguni la Olduvai.
Wiki moja baadaye walifanikiwa kuingia nchini Tanzania wakifikia kwenye uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro.Kama bahati kampuni ya bwana Temu ilipata watalii hao ambao walikuwa na safari ndefu ya kutalii kwenye vivutio vilivyokuwa kaskazini mwa Tanzania tena wakianzia Mapango ya Amboni , Tanga.Kwa kuwa aliikuwa mtu aliyependa kuingiza pesa kwenye kila fursa halali ilipopatikana baada ya kukamilisha taratibu zote Kijana Mshana aliamua kujifanya msaidia mizigo wa wale wanafunzi wenzake hivyo alikuwa akilipwa pesa yake kama mpagazi huku akiendelea kutalii kwenye vivutio vingi ambavyo licha ya kuwashawishi wenzake waje kuvitembelea alikuwa amepata sifa hizo kwa simulizi na kusoma tuu vitabuni.
Safari hiyo iliyoburudisha nafsi za waliosafiri ilikuwa ni mwanzo wa urafiki wa Mshana na Temu kwani wakiwa kwenye maandalizi kupanda mlima Kilimanjaro walikutana na Mzee mmoja ambaye aliwaunganisha na kuwana urafiki wao ulioudumu miaka mingi.
Ilikuwa jioni moja wakiwa kwenye kambi ambapo alfajiri ya siku iliyofuatza wangeianza safari ya kupanda mlima huo mrefu mzee huyo aliwafuata Mshana na Temu ambao walikuwa wakiongea mawili matatu wakati huo wale wazungu wakiwa wametingwa kupiga picha za machweo yaliyopendezeshwa na uwanda wenye ukijani chini ya Mlima Kilimanjaro.
‘’Habari zenu vijana’’Aliwasalimia vijana hao ambao walishtuka walipomuona mzee huyo.
‘’Shikamoo mzee, hivi tungekupita tuu si unajua wengine lugha ngumu sana tungejua we ni wa huko huko’’Alisalimia na kutia utani kwani yule mzee alikuwa si mwafrika lakini aliongea kwa Kiswahili sanifu akionekana kuwa hakuwa mgeni wa lugha hiyo tamu.
‘’Mie mwenzenu huu uzungu tuliupata tuu kwa wazazi wetu lakini mazingira yametupa lugha tamu kabisa,kuna mshairi alisema ‘Titi la mama ni Tamu’’
‘’Hahaaaa! Mzee una maneno wewe hadi mashairi unyafahamu maana mie kwa mara ya kwanza nilijua ni titi kweli’’Alidakia Msha ambaye alikuwa hajazungumza tangu asalimie.
‘’Kumbe ni Kiswahili? Mie hadi dakika hii kabla hujaongelea hilo suala nilikuwa nikisikia kauli hiyo nilikuwa najua ni msemo tuu waswahili wakilisifia titi la mama kumbe ni ushairi wa kukisifia Kiswahili , kweli elimu ufunguo’’Aliongea Temu kwa kirefu akijilaumu kutosoma sana kwani alipojua kusoma na kuandika tuu aliachana na kitu kilichoitwa shule na kuhangaika huku na kule akifungua biashara mbalimbali zilizoinuka na kufa hadi pale alipoamua kushirikiana na dada yake ambaye hatimaye alikuja kumpa mtaji wa biashara.
‘’Ufunguo wapi ona we unavyotukamua pesa kisa akili uliyonayo kufungua biashara?’’ Aliongea yule mzungu akicheka.
‘’Haa ni kuhangaika tuu hatuna chetu wenye biashara zao wamepumzika sie tunakuja kupigwa na baridi’’Alijitetea Temu ambacho hakukijua ni kuwa Mzee yule alikuwa akijua mengi kumhusu.
‘’Hata hivyo mnatupiga siye tunaokuja kushangaa mnavyoviona vya kawaida’’
‘’Wapi wazungu wenyewe mmekuwa mabahili sasa kama wewe nitakudanganya nini unajua kila kitu hadi Kiswahili’’Mshana aliongea na kuwafanya wacheke.
Baadaye ukimya ulifuata hadi pale mzungu yule alipouweka wazi mpango wake akiwashawishi kuwafanya mawakala wake wa biashara ya madawa ya kulevya huku kila mmoja akimpa ahadi za kutajirika na kuwa mfanyabiashara mkubwa sana.Mwanzoni walionekana kupingana na jambo hilo lakini baada ya kupewa mpango kamili jinsi biashara itakavyofanyika wakihakikishiwa ulinzi wao na kutobainika walikubalina naye na mipango kadhaa ikasukwa.
Mshana alikuwa wakala mkubwa huko Italia na nchi nyingine za Ulaya akiwaunganisha wasafirishaji mbalimbali waliokuwa chini ya mzungu yule mwenye Asili ya Colombia aliyejulikana kwa wengi kama mlowezi wa Kiingereza kama bwana Adrian Austin.
Kwa bwana Temu aliongezewa mtaji wa akifungua makampuni kadhaa ya kusafirisha watalii kwenye nchi mbalimbali za Afrika huku kwenye nchi kama Morocco na Afrika Kusini zilizokuwa vinara kwa utalii akiingia ubia na kampuni za usafirishaji katika kujenga ule mtandao wa baishara hiyo.Watalii wale walikuwa ni mawakala wa biashara hiyo haramu wakisambaza madawa ya kulevya sehemu mbalimbali duniani.
Hapo ndipo walipokutana Temu na Mshana ambaye kwa kuitembela Arusha alijikuta akijiapiza kuwa angerudi Arusha baada ya masomo yake na kazi angefanyia hapo na ndivyo ilivyokuwa.Alimkuta rafiki yake Temu akiwa amejijenga na kuweka mizizi hapo.
Waliiendeleza biashara yao wakiwa chini ya bwana Adrian Austin hadi pale alipofariki na kumwachia uongozi swahiba wake mkubwa ambaye alikuwa akiishi nchini Malawi bwana Leonardo Cesar ambaye baadaye aliwagawia faida waliyoipata na kuwaacha wafanye biashara kivyao akiwaahidi kuwasaidia kila watakapokwama.Aliamua kuwagawia kwani hakutaka kujishughulisha na baishara hiyo tena , akijikita kwenye shughuli nyingine zilizokuwa zimemuweka hapo Malawi.
Baada ya miaka kadhaa ya urafiki wa Mshana na Temu wakifanya biashara hiyo kwa siri na urafiki mkubwa uhasama unaibuka miongoni mwao kila mtu akitaka kuwa zaidi ya mwenzake na wakajikuta wakiingia kwenye ushindani wa chini chini, ushindani huo ulisababisha waanze kuwindana.Waliendelea kutafutana hadi pale kila mmoja kwa wakati wake akakumbuka mbinu ya kummaliza mwenzake, kitua ambacho kilikuja kubadiisha maisha yao.
Ilikuwa ni mbinu ya hatari na iendayo kinyume na miiko ya biashara yao, mbinu ya kumwingiza mtoto wa mwenzake kwenye utumiaji wa mihadarati.Ni mbinu iliyotumiwa na washindani wakubwa wa biashara hiyo duniani mbinu ambayo rafiki yao Austin aliwaambia ndiyo iliyomfanya aondoke kwao na kuja barani Afrika.
Adui na mshindani wake mkubwa alimfanyia kisa hicho cha kuiingiza familia yake kwenye matumizi wa mihadarati.Kwa wazalishaji na wafanyabashara wakubwa wa madawa ya kulevya ni haramu kwa mwanafamilia , ndugu ama yeye mwenyewe kuyatumia madawa ya kulevya kwani licha ya kuharibu afya zao bia huharibu ufanyaji wa biashara hiyo.
Wauzaji na watengenezaji wanajua ubaya wa madawa hayo kiafya tena wanayajua kiundani kabisa na ndiyo maana nchi mbalimbali huzalisha madawa ya kulevya na kuweka sheria ya kuyazuia kuyauza nchini humo na wakiituia kama mbinu ya kwenda kudhoofisha mataifa mengine shindani na yale ambayo yana manufaa kwao kama.
Nchi zinazoendeea zimekuwa soko kubwa la madawa hayo kwani mataifa makubwa yamekuwa yakitumia mbinu hiyo kuharibu vijana na kuzifanya serikali zitingwe na vita dhidi ya madawa huku zenyewe zikinufaikana na biashara hiyo kwa kuyauza pia kuchukua rasilimali mbalimbali.Kwa kuharibu nguvukazi ya mataifa hayo pia hunufaika kwa kuuza bidhaa walizozizalisha kwani uzalishaji unakuwa umepungua kwenye nchi zinazoendelea.
Kanuni nyingine ni kutowahusisha ndugu hasa watoto kwenye biashara hiyo kwani ni kama kumtengenezea janga huyo ndugu.Lakini pia ilikuwa ni haramu kwa wafanyabiashara hao kuyabeba madawa hayo wenyewe badala yake watumie watu wengine ili hata wakija kukamatwa nayo liwe zigo lao ndiyo maana licha ya kukamatwa kwa watumiaji wengi wa madawa ya kulevya inashindikana kuufuatilia mnyororo huo.Hii inatokana na mbinu ya muuzaji wa mwisho kutojua mtu wa juu kabisa ambaye ndiye mnufaika mkubwa.
Licha ya miiko hiyo yote kujulikana kwa Temu na rafiki yake Mshana, tamaa na husda miongoni mwao ikawafanya kila mmoja atamani kumshusha mwenzake.Uhusiano wa Alice na Kenny uliamsha hisia kuwa kila mmoja alikuwa ameamua kumwangamiza mwenzake kwa kumwingiza mtoto wa mwenzake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa lazima na kumshusha mwenzake kwa kumharibia mtoto wake.
Hilo likamfanya kila mmoja atake kumuwahi mwenzake.Wakati Mshana akipanga kumwingiza Alice kupitia mahusiano yake na Kenny kijana wake kuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya Temu naye aliwaza kinyume chake.Tofauti na Mshana aliyetaka kupitia watu fulani waliokuwa kwenye kundi lake watumie mwanya wa mahusiano hayo kumteka Alice akiwa chuoni Mwanza na kumvutisha ‘unga’ kwa nguvu kisha kupitia Kenny awe anayapata madawa hayo kwa urahisi.
Mzee Temu alikuja na mpango kabambe wa kumwingiza Kennedy kwenye matumizi ya madawa ya kulevya , tofauti na mwenzake aliyepaga kulitekeleza hilo wakiwa Mwanza Temu aliamua kulifanya kabla hawajaiacha Ardhi ya Arusha huku akipanga kila kitu kiutalam kabisa.Na ndiye aliyepanga mpango wa kutekwa kwa Kenny akiwa hotelini na Alice tofauti na alivyopanga kabla mwanya ulipatikana kabla hawajafika hotelini.
Ni Temu ambaye aliratibu mpango mzima, tangu ajue mwanaye alikuwa amechukua chumba kwenye ile hoteli ambayo naye alikuwa akiimiliki alipanga mpango wa kuzizuia kamera za usalama kufaya kazi kwenye maeneo ambayo walijua utekaji ungehusika nalo.Kuanzia chumbani hadi pale mapokezi ambapo watekaji walikuwa wamechukua kadi ya akiba ya kufungulia mlango wa chumba alichokuwa amelipia mwanaye.
Baada ya utekaji huo ilipangwa kuwa Alice aonekana naye kutekwa na kufungwa kitambaa kizito usoni kama ambavyo Kenny angefanyiwa na baada ya hapo Alie ngechukuliwa na kupelekwa hadi nyumbani kwa Temu amabye ni baba yake na kuinginzwa kwenye chumba cha siri kilichopo chini ya nyumba yao.
Ni nyumba chini ya nyumba ambako ni kama ofisi ya baba yake ya baishara zake haramu , huko Alice angewekwa huko kwa wiki nzima akitishiwa maisha huku mzee Temu akipigiwa kuwa alitakiwa atoe kiasi kikubwa cha fedha na kuwaweka kwenye akaunti ya benki ya feki iliyokuwa na jina na taarifa za mwanaye.Kisha Alice angekuja kutupwa mtaroni baada ya baba yake kuweka pesa kwenye akaunti hiyo na kuja kuokotwa na askari akiwa amedhoofu.
Kwa Kenny ilipangwa baada ya kutekwa apelekwe kwenye bonde moja liliokuwa katikati yam situ mmoja huko Rombo mkoa jirani wa Kilimanjaro.Bonde hilo ambalo liliupendezesha msitu uliouzunguka kwa ukijani usioisha lilikuwa ni kituo kikuu cha uzalishaji wa pombe haramu kama gongo lingekuwa ni sehemu sahihi ya kumhifadhi Kenny katika wiki nzima ya umateka wake. Huko baba yake angelazimishwa kutoa pea kama ilivyopangwa kwa Alice lakini tofauti yao Alice asingefanyiwa unyama ambao Kenny angefanyiwa.
Unyama ambao huhitaji roho ngumu isiyo na huruma kuagiza ufanyike ama kuutekeleza, lakini Temu alikuwa na hiyo roho ngumu iliyotokana na tamaa huku pesa ikiitoa ile huruma ndogo waliyobakiwa nayo wale watesi ambao kwao madawa ya kulevya na pombe haramu vilikuwa ni wenyeji wa akili zao.Walifanya unyama waliotakiwa kuufanya, Kenny angeingiliwa kimwili kwa zamu kila ilipofika usiku ka idhini ya kupata madawa ya kulevya ambayo yangekuwa yamempa ‘arosto’ baada ya siku moja tuu ya kuvutishwa.
Tofauti ni kwamba mpango wa Alice haukwenda kama walivyopanga lakini kwa Kenny kila kitu kilienda hivyo na wiki moja baadaye Kenny alikutwa akiwa taabani karibu na nyumbani kwao alfajiri.Kenny aliyatamani madawa ambayo yaliuzoea mwili wake lakini hakujua pa kuyapata.
Kwa kuw baba yake alijua adhari za madwa yale yakiingia mwilini nbaada ya matibabu ya awali ndipo alipoamua kumpeleka Afrika kusini ambako alienda kufanyiwa matibabu ya kuacha madawa hayo akiwadanganya wengine kuwa alikuwa masomoni.Wakati baba yake akijua tatizo lilikuwa madawa pekee , tatizo ambalo lilimalizwa alipokuwa akipatiwa tiba hiyo hakujua kuwa mwanaye alikuwa na kilema kingine, mwanaye alikuwa shoga,tena shoga aliyekubuhu na huko Afrika kusini ni kama alienda kukutanishwa na masoga wabobezi ambao walimfanya mke.
Hata aliporejea nchini na kwenda kuanza chuo kikuu cha Dar es Salaam aliendelea na tabia yake ya ushoga.Alipolizoea jiji la Dar baba yake akataka kutanua soko la biashara yake ya madawa ya kulevya naye kwa hasira za kufanyiwa kitendo cha kuvutishwa unga kwa lazima alijikuta akikubaliana na baba yake na aliifanya biashara hiyo kwa ustadi mkubwa.Wanaume aliokuwa akilala nao nao aliwaingiza kwenye uraibu huo haramu na kuwa na wateja wengi jambo ambalo lilimfanya baba yake ampende sana.Siku ile alikuwa amefanikiwa kumfanya Stella kuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya baadaya azazi wake kuondoka pale nyumbani.
_________________
Baada ya tukio lile la kutekwa Kenny mwanaye Daktari Mshana alifanya uchunguzi wa hisia zake juu ya kuhusika kwa rafiki yake kwenye tukio lile katika kutaka kuiangamiza familia yake.Baada ya kufanikiwa kumpata mmoja wa watekaji wa mwanaye akijaribu kuwapeleleza wale ambao alihisi lazima walikuwa wametumika alifanikiwa kuujua ukweli.Kikawaida alijua lazima hasimu wake angekuwa amewatumia majambazi wa kutoka mbali na mkoa wa Arusha kutekelza unyama huo lakini kwa kadiri mpango huo ulivyoenda alijua lazi kuna wenyeji waliokuwa wakihusika na tukio hilo hasa baada ya kuambiwa na mwanaye kuwa alikuwa amepelekwa kwenye bonde refu lilokuwa karibu na msitu na kwa kadri alivyolijua bonde lile hakukuwa na mtu wa wan je ya Arusha na Kilimanjaro alilolijua bila msaada wa mwenyeji.
Kwa msaada wa maelezo ya mwanaye alifanikiwa kumgundua mmoja wao, alikuwa ni jambazi sugu mwenyeji wa Songea Mkoani Ruvuma.Huyo alikuwa ni jambazi aliyeshindikana na jeshi la polisi kwani licha ya kuaminika kuwa alikuwa akitumia ushirikina wa kutoa kafara ya damu ili kuifanya hirizi yake ili aishi na kukwepa mitego mbalimbali ya polisi na akipona kwenye vipigo vya wananchi wenye hasira kali pia alikuwa na mtandao wake kwenye vyombo mbalimbali vya usalama ambako alipata taarifa mbalimbali ziliohatarisha usalama wake.
Alijua kuwa mtu huyo alikuwa ni hatari na mwenye mipango iliyokamilika lakini alikamilisha mipango vyema palipokuwa na pesa ya maana.Hivyo alifanya mipango ya kumtafuta lakini kama bahati ilikuwa kwake kwani alipofanikiwa kumpata kupitia watu wake alikuta jambazi huyo hatari akiwa na jambo ambalo lilimfanya waungane.
Ni baada ya kufanikisha mpango wake kwa kutumia mtandao mwingine aliokuwa ameupanga mzee Temu alikuwa amepanga kuwaua wote waliokuwa wamehusika kwenye tukio lile ili kupoteza masalia ambayo yangemfanya rafiki yake ajue kuwa ndiye aliyeratibu mpango huo.
Ambalo hakulijua ni kuwa mmoja wa watu aliokuwa amewaweka kuwaua watu wa kwanza alikuwa mfuasi wa jambazi huyo kutoka Songea hivyo baada ya tukio lile kutekelezwa Jambza huyowa Songea akiwa njiani kuelekea Malawi alikopata mpango mwingine alipigiwa simu na mtu huyo na jamaa huyo kuahidi kurudi Arusha na akiwa kwenye mpango wa kurudi Arusha alipewa kazi nyingine ambayo aliona itakuwa imemfanya atoe onyo kwa mtu aliyeagiza kuwa auawe.
Hilo ndilo lililokuwa kuharibu maisha ya familia nyingine ambayo hata haikujua nini kilikuwa kikiendelea.