Riwaya: Nitakufa Nae

Riwaya: Nitakufa Nae

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
522
STORY: NITAKUFA NAE
MTUNZI: JK Mdharuba
+255 718 274 130
+250 726 023 140
mdharuba@gmail.com

SEHEMU YA KWANZA

★★★★★★★★★★★

"Sikiliza Jeff, pamoja na maneno yote uliyoongea, bado sijashawishika kuachana na Jk, sijui kanipa nini yule mwanaume, naomba mniache tu" Aliongea Merry huku machozi yakimbubujika wakati huu,, maneno haya aliyaongea huku kamasi zikimtoka. Jeff alishamthibitishia kuwa Jk hakuwa mkweli kwake, lakini bado alitamani saaana kuendelea kuwa na Jk, licha ya kuwa na uhakika wa asilimia mia kuwa Jk hakuwa mume bora.

Ila, Jeff alithibitisha haya yote kwa Merry akiwa na lake kichwani, ingawa Merry alimuona ni mtu mwema tu. Kusikia majibu haya, Jeff alianza kung'aka, na kuropoka, "Na tutaona mtafika wapi na huyo ms**ge wako Jk, unajifanya unajua kupeeendaa,, ila kitu ntakachomfanya hutaweza kuamini" Aliongea Jeff kwa hasira na kuondoka pale baa akimsukumia meza Merry bila kujali kama ataumia au laa...

Baada ya Jeffy kuondoka mahala pale, Merry alitoa simu yake iliyokuwa kwenye mkoba na kubofyabofya kisha akaweka sikioni, haikuhitaji PhD kujua kuwa alikua akimpgia Jk, mwanaume wa maisha yake, aliyempenda kwa moyo wake wote.

"Baby, uko wapi Laaziz wangu?" Aliongea kwa sauti laini bi Merry baada ya simu yake kupokelewa.
"Nipo hapa Kwa Aziz Ally ndo nasubiri daladala nielekee nyumbani"
"Mi natangulia basi baby huko nyumbani, maana kuna mtu kanitibua sana leo"
"Poa My love tutaongea vizuri nikifika huko, nakupenda sana"
"Nakupenda pia Jk wangu" Alisema Merry na kukata simu.

★★★★★★★★★★★★

Merry Hassan, binti wa kinyamwezi kutokea mkoani Tabora, anajikuta ghafla sana amezama kwenye penzi zito la Jumaa khatib maarufu kama ‘Jk' mtoto wa kitanga, kule Mahaba yalipozaliwa. Licha ya msimamo aliokua nao tangu anakua kuhusu wanaume, lakini alijikuta ghafla sana anazama katika penzi zito la kijana mmoja mtanashati ambaye alikua ni Mwalimu wa shule moja ya Sekondari Jijini Dar..

Wakware mbalimbali walikua wakimtolea macho Merry kutokana na jinsi Mungu alivyomtengeneza vizuri, lakini wala Merry hakujali akiamini wanaendeshwa tu na tamaa zao za kimwili..

Katika harakati zake za kila siku ndipo siku moja alikutana na kijana wa kitanga, mwenye umbo la wastani, mcheshi, akajikuta moja kwa moja anaukabidhi moyo wake kwake, tena mzimamzima..

Moja kati ya watu waliokua wasumbufu sana kwa Merry ni bwana Jeffy John, mfanyabiashara maarufu jijini Dar, alijaribu kutumia pesa zake kadri alivyoweza ili kumshawishi Merry aachane na Jk na awe na yeye lakini juhudi zake ziligonga mwamba. Licha ya kuwa na mkewe, Jeffy bado alionekana kuwa na hamu sana na penzi la Merry,, yeye akiamini Merry alimstahili mtu kama yeye kwa kuwa alikua na pesa na umaarufu!! Jambo ambalo Merry halikumuingia akilini, alimpenda Jk kwa moyo wake wote, licha ya kuwa Jk alikua na maisha ya kawaida saana..

Aliridhika kuwa nae, wakipata dagaa wanakula pamoja kwa amani, wanasikilizana, wanasaidiana kazi, na mambo mengi wakifanya pamoja kama watoto mapacha. Habari za kitandani ndo usiulize, kwani Merry alikua akipewa raha mpaka zinapitiliza, akiwa anatamani saa zote awe na Jk kitandani akiunyanyasa mwili wake..

"Jk, nakupenda saana, naomba usinisaliti, ntalia". Ni maneno ya kila siku yaliyokuwa yakisikika masikioni mwa Jk kutoka katika kinywa cha Merry..

★★★★★★★★★★★★

"Jk Mume wangu, yule Jeffy bado anaendelea sana kunisumbua, leo nilivyokwambia naenda kule Magomeni, basi mda ule wa mchana nilienda pale kwenye ile pub tunayokuwaga mara nyingi, akaja sijui katokea wapi akaanza kunambia eti ooh sijui ww una michepuko, sijui nini, basi akaongea weee mpaka mwisho nikamwmbia uniache tu na Jk wangu, akakasirika akanambia eti atanionyesha, na atakufanyia kitu kibaya" Alieleza Merry akiwa ameweka kichwa chake katika mapaja ya Jk huku mikono ya Jk ikishikashika uso wake laini, ilihali mikono ya Mwery ikiwa imezunguka kiuononi mwa Jk.

Baada ya maelezo haya Jk alitoa tabasamu pana, na kusema maneno machache "Watu wengine bana wana matatizo sana,, haya bana" kisha akaanza kuyatomasa matiti ya Merry yaliyokuwa yamefunikwa na khanga iliyokua imeishia kifuani hapo, taratiiib akaanza kuyapa tabu matiti yale huku mkono mmoja ukitambaa na mwili wa Merry taratiib, maisha ya usiku yakaendelea..
*********************
Asubuhi kabla Jk hajatoka kwenda kazini Merry aliamua kumuuliza Jk kuhusu jambo lile la Jeffy amelipokeaje..
"Jana ulikaa kimya baada ya kukueleza vile, sielewi ulichukuliaje mume wangu"
"Aaah achana nae huyo, hajielewi" Jk alijibu kifupi, akanywa chai kisha akatoka..

*******************************

"Wewe ukifika pale usiulize, fumua risasi moja ya kichwa akafie mbele bata yule" Jeffy alikua akimpanga kijana wake wa kazi kutekeleza agizo la kumuua Jk..hakuwa na huruma hata kidogo, alitaka Jk afe ili aone kama Merry ataendlea kuwa na maringo tena.
"Sawa mkuu nimekuelewa" Alisema kijana yule mwenye umri kati ya miaka 24 hadi 27 akionyesha kuyaelewa vizuri sana maelekezo ya Jeffy John..

*************************

Saa 7:30 mchana simu ya Merry iliita, ilikua ni namba ngeni, simu yake ilishaita kama mara 4 yeye akiwa jikoni, mara hii ya 5 ndo alipokua ameingia chumbani na kuskia simu yake ikiita, akapokea..

"Haloo, nadhani naongea na Merry mke wa Jk" ilisikika sauti ya upande wa pili..
"Ndio mimi, vipi kwema??" Aliuliza Merry akiwa anatetemeka, alishaanza kuhisi kuna ktu kibaya kimetokea sababu ya vile vitisho alivyopata kutoka kwa Jeffy juu ya mumewe Jk..
"Hapana, sio kwema, kuna tatizo.." Ilisema sauti upande wa pili na kumfanya Merry azidi kuchanganyikiwa..

★★★★★★★★★★★★★

Itaendelea....
 
zile hujamaliza umeanzisha mpya jaribu kubadilisha na majina ya wahusika kila story jk yupo inapunguza radha
 
zile hujamaliza umeanzisha mpya jaribu kubadilisha na majina ya wahusika kila story jk yupo inapunguza radha

Kama ulikuwepo akilini mwangu. Uyo JK tumemchoka bwana Mdharuba, hata kma ni ww ila imekuwa too much baba. All in all bado nitabaki kuwa mtumwa wako
 
zile hujamaliza umeanzisha mpya jaribu kubadilisha na majina ya wahusika kila story jk yupo inapunguza radha

Nina wasiwasi kama hii nayo itaisha...au tutaimalizia clouds fm
 
zile hujamaliza umeanzisha mpya jaribu kubadilisha na majina ya wahusika kila story jk yupo inapunguza radha

Kama ulikuwepo akilini mwangu. Uyo JK tumemchoka bwana Mdharuba, hata kma ni ww ila imekuwa too much baba. All in all bado nitabaki kuwa mtumwa wako

Story zote zitaisha..waswas wenu tu..
Afu nilisema mtu anayetaka nimuandike anifuate inbox au anitext majina yake, hamkufanya hvyo..acha nijiandke mwenyew..sbb kila jina unaloliona katika story ni jina halisi la mtu na mwenyew ametoa idhini nitumie jina lake
 
Stori inaponoga ndo mtunzi huwa anakatisha nina wasiwas na hii kukatishwa itaponoga
 
Hata mie naona afanye hivyo
Tumalizie kwanza ile nyingine

Mi nilikuwa naona tungemaliza kwanza zle mbili then hii ndo ikafata au unaonaje mkuu.

Mimi naona niendelee kutangaza biashara kwanza..

Nitapost nyingine ya nne usiku huu..

N.B.
No free lunch, kwahiyo ndoto za story kumalizikia hapa Jf sidhani kama zitatimia..
 
Mimi naona niendelee kutangaza biashara kwanza..

Nitapost nyingine ya nne usiku huu..

N.B.
No free lunch, kwahiyo ndoto za story kumalizikia hapa Jf sidhani kama zitatimia..

aya mdharuba tunyanyase.
 
RIWAYA: NITAKUFA NAE
MTUNZI & MWANDISHI: Jumaa Khatib Mdharuba
+255718274130

SEHEMU YA PILI
★★★★★★★★★★★★★★★
Ilipoishia...
Merry amepokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu akimuuliza kama yeye ndio mke wa Jk, akauliza kama kwema, akaambiwa si kwema kuna tatizo..jambo linalomfanya Merry achanganyikiwe kwani alishapokea vitisho kutoka kwa Jeffy kuwa lazima atamdhuru mumewe..
Sasa endeleeaaa...
“Mumeo amepata ajali, amegongwa na pikipiki wakati akivuka barabara hapa Uhasibu” ndivyo alivyoendelea kutoa maelezo mpigaji yule wa simu..
“Uuuwiiii...mamaawweeee jaammaaniiiii...aaa..meee..pona..laa..ki..ni..mume..wa..ngu..?? Merry aliuliza kwa sauti ya kwikwi maana alishaanza kulia kilio kikubwa mno..
“Ameumia kidogo mno, ila tu alizimia kutokana na mshtuko, lakini wamemfanyia vipimo wanasema hajaumia ndani..na nje ana majeraha mawili madogo tu usoni” Alifafanua msamaria yule na kumfanya Merry kidogo ashushe pumzi..kisha akamuelekeza hospitali mumewe alipo. Dakika 30 tu baada ya simu hii Merry alikua eneo la Hospitali tayari, akitafuta wodi aliyolazwa mumewe.
Wakati yuko njiani kuelekea wodini, akakutana na mtu ambaye alionekana kumfahamu vizuri Merry, ila yeye (Merry) hakumfahamu mtu yule.
“Habari yako dada Merry?”
“Safi tu za kwako?”
“Nzuri, haya mbona hapa saa hizi, kulikoni?”
“Nakuja kumuangalia mume wangu, amepata ajali, amelazwa hapa”
“Duuh Jk amepata ajali?”
“Samahani kaka, unatufahamu mimi na mume wangu?”
“Sasa kwanini nisiwafahamu, hebu tuongozane, yupo wodi namba ngapi?” Mtu huyu ambaye alimuonesha Merry uchangamfu wa hali ya juu, aliongozana nae mpaka alipolazwa mumewe..Jk, wodi #3 katika hospital ile iliyokuwa maeneo ya Kwa Aziz Ally.. Mitaa maarufu sana kwa Jk kwani ilikua karibu na shule anayofundisha. Licha ya kuongozana nae hadi kwa mgonjwa, lakini Merry alimtilia mashaka sana mtu yule, hakuwa anamjua, na Jk alikua akijitahidi kumtambulisha kwa kila mtu.
“May be ni rafiki yake, anamfahamu yeye Jk atakua” Aliamua kujiridhisha hvyo katika moyo wake, ila bado alikuwa na maswali kichwani.
“Bro, pole sana..ndo nimekutana na shem hapo nje kanambia kuwa umelazwa hapa, nikashangaa sana ikabidi nimwambie anilete..pole sana kaka..” Ndivyo alivyoanza mtu yule baada tu ya kumuona Jk.
“Nashukuru sana ndugu yangu..asante sana” Jk alijitutumua kujibu faraja ile aliyopewa.
“Wamekufanyia vipimo?”
“Yaah..wamenambia nisubiri kidogo ili waweze kuniruhusu..”
“Oooh..wamesema watakuruhusu leo?” Aliuliza mgeni yule ambaye alionekana kushangaa kidogo kuhusu ruhusa ya Jk, alionekana kutamani kumuona Jk hospital
“Daah..afu nimekuja kumuona mgonjwa hata matuunda..ila ni kwa sababu sikujiandaa..kaka ngoja nkakuchukulie japo machungwa mawili hapo na maji nakuja sasa hivi” Alijisemea yule jamaa na kabla Jk hajajibu chochote alishaondoka kwa kasi sana akielekea nje..
Akatoka mpaka nje ya lile jengo, akatoa simu yake na kupiga.
“Boss, mission impossible, Jk yupo hosptal..mi nimeenda hadi wodini kumuona. Kwahiyo nimeamua kutumia 'alternative way' ” Ndivyo alivyotoa maelezo kijana yule baada ya simu yake kupokelewa na Jeffy John.
“Be careful” Alijibu Jeffy kisha simu ikakatwa.
Akaelekea dukani na kununua maji, kisha akaelekea kwenye kibanda kidogo kilicho karibu na geti la hospitalin pale na kununua machungwa matano.. Safari ya kurudi wodini ikaanza.
*************
“Mume wangu, hivi unafahamiana na huyu kijana?” Merry alimuuliza Jk mara tu kijana yule alipoondoka pale wodini.
“Hapana, simfahamu..labda ni katika watu wanaonifahamu, kama unavyojua tena, mimi ni mwalimu, nimefundisha watu wengi pengine ni mzazi wa mtu niliyemfundisha, au hata anaweza kuwa nilimfundisha yeye pia..”
“Tatizo lako ni hilo tu mume wangu, kila kitu unakichukulia simpo..hilo ndo tatzo..tangu jana mimi nina wasiwasi na usalama wako, lakini wewe unaonekana hata hujali kabsaaa..” Merry alikua anatimiza jukumu lake ipasavyo haswa kama mwanamke. Kitendo cha Jeffy kumpa vitisho kuhusu Jk kilikua na kila sababu ya Merry kuhofia kuhusu Jk. Ila Jk mwenyewe hakuonekana kujali sana.
“Watu wananipenda mke wangu, ndo maana ukimwambia mtu naumwa haachi kuja kuniangalia..yaani ni muda mfupi tu uliopita nimepata wageni hapa mpaka nikashangaa wamezitolea wapi hizi taarifa? We acha tuu..” Jk hakuonekana kumuelewa Merry hata kidogo..
*************
“Haya shem, matunda haya na maji pia haya kwa ajili ya Bro Jk hapa..vitu muhimu sana hivi kwa mgonjwa..” Alijisemea jamaa yule baada ya kurudi tena pale wodini.. Merry alikua anamuangalia tu bila ya kumjibu chochote..
“Asante sana bro, Mungu akubariki” Jk aliona aitikie yeye na kufanya macho ya Merry ambayo yalikua yakimuangalia yule kijana wakati huu, yageuke kwa Jk..akamuangalia sana kisha akarudisha tena macho yake kwa kijana yule ambaye saa zote alionesha uchangamfu.
“Kunywa maji haya bro, ni muhimu sana maji katika mwili wako kwa sasa..” Alisema kijana yule huku akikata 'seal' ya nailon iliyokuwa kwenye chupa ile kubwa ya maji ya lita 1.5, kisha baada ya hapo akamkabidhi Jk chupa ile ambaye aliipokea na kuamua kukaa ili ayanywe vizuri maana bado alikua amelala pale kitandani.
Lakini kabla hajafikisha chupa ile mdomoni, Merry aliikwapua na kunfanya Jk ahamaki.
“Vipi tena mke wangu, nini tatzo?”
“No Jk, usinywe haya maji mume wangu”
“Kwaninu sasa nisinywe?”
“Nimesema usinywe maji..wee vipii?” Merry alifoka kwa sauti na kufanya watu wa karibu waliokuwa vitanda vya jirani na wagonjwa wao washtuke na kuanza kumuangalia kwa jicho la hasira. Ndio, aliwapigia kelele wagonjwa wao.
“Shika chupa yako, hebu anza wewe kwanza kunywa haya maji halfu utampa na mume wangu anywe” Merry alimwambia kijana yule ambaye alikuwa bado amesimama pale pasipo kuongea chochote.
“Shika kunywaa..” Merry tayari alikua mkali.
Kijana yule akachukua chupa ile ya maji, akaishika kwa mkono wake wa kulia..pamoja na ujasiri alioonyesha kuwa nao, lakini kwa mbaali Merry na Jk walimshuhudia akitetemeka.
“Kunywa sasa hayo maji ambayo unataka mume wangu anywe..kunywaa..” Merry alianza kuwa mkali, alishaisoma saikolojia ya yule jamaa tangu mwanzoni. Akaamua amkomalie..
Wakati kijana yule akigwaya pale, Merry alitumia nafasi ile kuandika ujumbe mfupi kwa mkuu wa kituo cha polisi cha pale kwa Aziz Ally..alikuwa akifahamiana nae vzuri, na namba yake ya simu ya mkononi alikuwa nayo mbali na ile 112 namba ya dharura ya polisi.
“Ulitaka kumpa sumu mume wangu afe si ndio?” Merry alimuuliza kijana yule ambaye wazo lake kichwani lilikua ni kukimbia eneo lile kabla hajatiwa mikononi mwa polisi. Merry alishakua na uhakika kuwa hata huyu kijana akitoka hawezi kufika mbali atakamatwa tu na polisi..kwani alishawaelekeza vizuri na Mkuu yule wa kituoa alishajibu sms yake kuwa vijana wake wanakuja.
“Samahani dada..naomba unisamehe..” Akili ya haraka ya kijana yule ilimtuma aombe msamaha..hapa ndipo Jk alipopigwa na butwaa kwa kuamini kuwa kweli kifo chake kilikaribia leo.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Itaendelea..

Kwa story zingine tamu, follow instagram: @jk.stories
 
Mkuu Mdharuba ungeufanyia kazi ushauri wa hapo juu ingekuwa poa sana wa kumaliza zile mbili kwanza japo unasema biashara ni matangazo,
sijui unajua tena na hizi mb 8.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mdharuba ungeufanyia kazi ushauri wa hapo juu ingekuwa poa sana wa kumaliza zile mbili kwanza japo unasema biashara ni matangazo,
sijui unajua tena na hizi mb 8.

Daah..kaka naomba nisisitize kuwa there is no free lunch.. Story naziuza hizi..siwezi kuzimalizia hapa Jf..
Acha tu niendelee halafu nitatoa utaratibu wa namna ya kupata mwendelezo wake na malipo yatakuaje..
MB 8 sio tatizo langu mkuu, sidhani kama linanihusu..
Asante.
 
Last edited by a moderator:
Ndo maana sisomagi story Kama hii sijaanza hata. Yaani naona kichwa cha habari AF naona last text ni mtumaji anasema hataimalizia!!! Haya sisomi na nakupigia kura upigwe ban
 
Back
Top Bottom