Riwaya: Mtoto Wa Shetani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
RIWAYA; MTOTO WA SHETANI
MTUNZI; ALLY AYUBU KATALAMBULA
SEHEMU YA KWANZA
KIGOMA-1999
Wingu zito la mvua lilikuwa limetanda angani,ilisikika ngurumo za radi kila kona ya mji wa kigoma,ilikuwa yapata saa moja na dakika ishirini, giza zito lilienea katika mji,dalili ya mvua kubwa ilionekana waziwazi,
Dakika chache badae mvua ilianza kunyesha.
Ilikuwa ni mvua kubwa ya mawe,epepo mkubwa ulivuma na kubeba takataka nyingi,
umeme wa tanesko tayari ulisha katika saa nyingi,
Sophia mwanamke mwenye muonekano wa kiafrika, alikuwa amejibanza pembezoni mwa ukuta akijikinga mvua kubwa ya mawe, awali mvua haikumfikia likini kadri muda ulivyo zidi kusonga mbele ndivyo mvua ilivyo ongeza kasi ya kunyesha,kwa dakika kadhaa alijikuta amelowa nusu ya mwili wake.
Mwili wake ulitetemeka kwa baridi kali,alikunyata mikono yake kifuani mwake,meno yake yaligongana,hakujua aondoke eneo hilo au abaki,alijiuliza akilini,kabla hajajua amue nini alihisi kuguswa bega lake la kulia,
alipo geuka halmanusra azimie kwa kile alicho kiona
Baba la miraba minne likiwa kifua wazi mkono wa kulia likiwa limekamatilia kisu chenye makali kotekote kikiwa kimetapakaa damu,huku mkono wa kushoto lilishikilia kichwa cha mtu kimechinjwa,
Ajabu kile kichwa kilikuwa kinakapua kope za macho yake huku midomo yake ikiwa inatafuna vitu visivyo julikana . “kwanini unaogopa” kile kichwa kilisema.Sophia hakuwa na la kusubiri alitimua mbio kali huku akipiga makelele ya uwoga,
Kutokana na mvua kunyesha Sophia aliteleza na kupiga mweleka,aliponyanyuka hakuamini alicho kiona
Alionekana yule mtu akiwa mbele yake mkononi akiwa na kisu pamoja na kile kichwa chake kinacho vuja damu.mwili wa Sophia ulikufa ganzi,mapigo ya moyo yalimdunda mithili ya ngoma za kizaramo, mashaka makubwa yalimjaa moyoni mwake.lile baba la miraba minne lilimsogelea,huku likiwa limemkazia macho, nguvu za kukimbia Sophia hakuwa nazo tena, alibaki ameganda kama amepigwa shoti ya umeme.
“mtoto wa Lambulakata ” sauti yenye mkwaruzo kutoka katika midomo ya kile kichwa ilisikika, mvua ya mawe na upepo iliyokuwa inanyesha haikuwa kitu usizuie Sophia kuvuja jasho katika maungo yake, alitetemeka kwa woga, alijuta kujikinga mvua katika kuta za jumba bovu majira yale ya jioni. lile jibaba lenye misuri thabiti halikutia neno lolote, lilisogea karibu kabisa na Sophia likiwa limemkazia macho makali. kwa nguvu lilinyanyua kile kisu chake na kwa nguvu zake zote lilimdunga nacho Sophia kifuani,
Damu zilimiminika kama maji katika bomba, Sophia aliachia miguno mikali ya maumivu, hakujua kwanini yule mtu anamtendea unyama ule alisikia maumivu makali mno,yule mtu hakuishia hapo alichomoa kisu katika kifua cha Sophia na kumdunga nacho tena kifuani,maumivu aliyoyapata Sophia katika mwili wake yalikuwa hayaelezeki, nguvu zilimwishia akajikuta anaelekea chini.mboni za macho yake zilipoteza uwezo wa kuona, giza lilitanda machoni pake,izraeli mtoa roho alimuona waziwazi.Sophia aliona anakufa bila kujua kosa lake la msingi mpaka ipelekee yeye kupewa adhabu kubwa ya kifo kiasi kile..kope za macho yake zilifumba na hakujua kilicho endelea tena.
****************************************
Ta,ta,ta,ta,ta,ta Ilikuwa ni sauti ndogo ya saa ya ukutani, majira ya saa tisa za usiku, katika eneo lenye ukubwa wa wastani mithili ya ukumbi, kulikuwa na ukimya tulivu katika eneo hilo hakikusikika kitu kingine zaidi ya mishale ya saa ndogo ya ukutani,
Mwili wa Sophia ulikuwa umelazwa katikati ya watu takribani kumi na tisa,walio kuwa wameuzunguka, mazingira ya eneo hilo kulikuwa na zulia kubwa jekundu, katika kuta kulikuwa na trei ndogo iliyobeba mishumaa mikubwa yenye kutoa mwanga mwekundu,mahali ulipo lazwa mwili wa Sophia ilikuwa ni katika meza ya kioo yenye ukubwa kidogo kama futi sita au saba,
Wale watu walikuwa uchi kasoro vijichupi walivyo kuwa wamevivaa katika viuno vyao, walikuwa ni mchanganyiko waume kwa wake, vichwa vyao waliviinamisha chini wakiwa wamesimama kwa utiifu mkubwa, ilisikika sauti ndogo ya filimbi ikitokea chini ya meza ambayo alikuwa amelazwa Sophia,
Hilo tukio lilifanya wale watu wainame wakiwa wameelekea katika ile meza ulipo lazwa mwili wa Sophia, walisujudu, kwa nukta kadhaa ile sauti ya kifilimbi ilikata, taratibu waliinua vichwa vyao,
Mzee mwenye mvi nyingi kichwani, mashavu yaliyo nenepeana na mwenye muonekano wa ukali, alisogea mahali ulipo mwili wa Sophia, alivuta sanda nyeupe peee iliyo kuwa imefunika mwili wa Sophia, mwili wa Sophia ulibaki uchi wa mnyama, yule mzee alitizama maiti ile ya Sophia kuanzia unyayoni mpaka kichwani,ajabu mwili wake haukuwa na jeraha la kisu sehemu yeyote, aligeuza shingo yake na kutizama wenzake walio kuwa wamemzunguka, wote walikuwa wamemkodolea macho pasina kuyapepesa upande wowote,
Yule mzee mwenye mvi, alisaula kijichupi chake na kubaki uchi, sehemu zake za siri zilikuwa wima zimekakamaa mithili ya ukuni mkavu, akasogea karibu na mahali ilipo lala maiti ya Sophia,dalili za kutaka kufanya mapenzi na maiti zilionekana waziwazi..
Yule mzee mwenye mvi na mashavu makubwa, hakuwa na woga wala haya kwa wenziwe waliokuwa wamemzunguka, alitanua mapaja ya Sophia huku akiwa ameelekezea jogoo lake katika sehemu za Sophia,
Haikuwa kazi rahisi kuzamisha kwa ndani kama alivyo taka,kwa zaidi ya dakika tatu hadi nne kila alipojaribu ilikuwa ngumu,aliwageukia wenziwe wiliokuwa wamemtumbulia macho muda wote wakitizama kitendo kile huku wakiwa na muonekano wa kukubaliana na jambo lile alilokuwa anafanya mwenzao.
Yule mzee Hakuzungumza kitu aliwatizama wenziwe kwa zamu kisha pasina kutia neno akanyoosha mkono wake wa kushoto kama mwenye kuomba kitu kwa wenziwe alinyoosha mkono kwa sekunde takribani tisa alisogea kijana mrefu wa futi sita na nusu, alikuwa ni yule kijana mwenye misuli mikakamavu ambaye alihusika na kifo cha Sophia kwa kumchoma choma visu kifuani, alimpatia yule mzee kichupa kidogo cheusi.
Baada ya kupokea Yule mzee alisogea tena karibu na mwili wa Sophia kisha akafungua kifuniko cha ile chupa ndogo,alimimina vitu fulani kama mafuta katika kiganja chake kisha akapekecha na kupaka katika jogooo lake kubwa lililokuwa bado limesimama wima.
Alipo hakikisha ameridhika aliweka pembeni ile chupa ya mafuta na kusogea katikati ya mapaja ya maiti ya Sophia aliitanua kama awali, kisha akaanza zoezi lake la kuchomeka lile jogoo kubwa katika maungo ya Sophia.naaam! sasa alifanikiwa kuingiza kwa ndani.alianza kufanya mapenzi na MAITI, alifanya,akafanya tena na tena.kimuonekano hakufanya kwa ajili ya starehe bali kwa ajili ya jambo fulani walilokuwa wamekusudia.
***********************************************************
SAA 2 ASUBUHI; MITAA YA KATUBUKA; KIGOMA MJINI.
Watoto wa shule ya msingi Katubuka walikuwa wengi wamemzunguka binti aliyekuwa amepoteza fahamu, huku nguo zake zikiwa zimelowa kwa matope, mwilini akiwa na michubuko chungu nzima, kadri muda ulivyo zidi kusogea ndivyo idadi ya watu ilivyokuwa inaongezeka eneo lile.
“jamani huyu binti sijui amepatwa na nini” yalikuwa ni maneno yaliyo ulizwa na kila mtu aliyefika eneo lile. “Bado ni mzima au amekufa?” hata sisi hatujui walijibu kwa pamoja wanafunzi kama wanne “wapigieni simu polisi” alishauri mama mwingine.
Haikujulikana ni nani aliye wapa taarifa polisi, ndani ya dakika kumi tayari tenga la polisi na polisi wapatao watano walikwisha fika eneo la tukio,waliuchunguza mwili wa binti yule kwa nukta kadhaa,kisha wakaupandisha katika defender ya polisi, “ni nani anamjua huyu binti” aliuliza askari mwenye cheo cha koplo, huku akipitisha macho kwa halaiki ya watu akitegemea kuona jibu la swali lake. Kuna ukimya ulipita lilikuwa ni jibu kwa yule koplo kuwa hakuna anae mfahamu,
Gari la polisi lilondoka kwa kasi eneo lile akibaki askari mmoja kwa ajili ya uchunguzi,gari lilifunga breki katika hospitali ya Maweni,upesi manesi walimpokea na kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi…
Hakuna mtu aliye amini kwamba yule mgonjwa bado ni mzima!! kwa zaidi ya dakika hamsini na tano, Madaktari walijaribu kuokoa maisha ya yule binti mgonjwa.
Dakika tano baadae mlango wa chumba cha upasuaji ulifunguliwa alitoka nesi akiwa anasukuma kitanda cha wagonjwa juu yake akiwa amelala yule binti.
Kwa zaidi ya masaa tisa dripu za maji zilikuwa zikiingia kwa kasi katika mishipa ya mwili wake, na masaa machache taratibu kope za macho ya yule binti zilianza kufunguka.
“Pole” ilikuwa ni sauti nyororo ya nesi aliyepewa jukumu la kumwangalia binti yule. “ni..ko..wa..pi?” aliuliza yule binti kwa sauti yenye maumivu ndani yake, “hospitali ya Maweni” alijibu nesi huku akimtizama kwa udadisi mkubwa.
“Unaitwa nani jina lako?” nesi alimtupia swali yule binti mgonjwa,, “SO..PHI..A” alijibu “pole sana utapona na kama una aina yoyote ya mawasiliano ya nduguzo nipatie ili niwarifu sababu tangu asubuhi ulipoletwa na polisi hakuna jamaa yako yeyote aliye jitokeza” alisema nesi huku akiandika vitu fulani katika faili lake.
Sophia hakujibu kitu zaidi ya kutikisa kichwa,aliendelea kulala huku akilini mwake aikiwa na mawazo lukuki, kuna kumbukumbu zilipita akilini mwake mithili ya mkanda wa filamu, aliikumbuka siku ya jana jioni wakati anaelekea kwa mchumba wake Ally aliyekuwa anaishi mitaa ya Mwandiga, wakati anakaribia kufika mvua kubwa ya mawe iliaanza kunyesha, Anakumbuka alijikinga mvua katika kuta za jumba bovu, lakini ghafla alitokewa na kiumbe wa ajabu ambapo alichomwa chomwa visu kifuani na hakujua kilicho endelea..
Alijipapasa kifuani mwake lakini ajabu hakuwa na jeraha lolote kifuani mwake. Hii ilizidi kuumiza bongo yake.
Akiwa katika lindi kubwa la mawazo alistushwa na sauti nzito ya kiume. “Habari yako binti” aligeuza shingo kule sauti ilipo sikika, alikuwa ni daktari, alikuwa ni daktari mwenye mvi nyingi kichwani na mashavu makubwa huku katika paji lake la uso kukiwa na mikunjo mikunjo isiyo hesabika, ama unaweza kuiita ndita,
Sophia hakujibu kitu kwa nukta kadhaa alikuwa akimkodolea macho yule mzee huku akijaribu kuvuta kumbukumbu mahala aliko pata kumwona yule mzee.
“Unaendeleaje” aliuliza yule mzee huku akiwa hajali vile Sophia anavyo mtizama kiudadisi. Alisogea karibu zaidi na kitanda cha Sophia kisha akainama na kuweka sikio lake katika tumbo la Sophia, alipo inua kichwa alionekana ni mwenye furaha isiyo kifani,Sophia alizidi kushangaa,alikuwa ni yule mzee aliyeambaka Sophia akiwa mfu..
Furaha ya yule mzee bado ilizidi kumshangaza Sophia, akili ya Sophia haikupata kumbukumbu mahali alipopata kumwona yule mzee daktari.
“Tumbo lako limebeba mkombozi” , Alisema yule mzee huku akimtizama Sophia kwa mapenzi makubwa. Sophia alichanganyikiwa,alihisi kichwa kinauma kwa zile fikra nyingi kichwani mwake, alitamani amuhoji maswali yule mzee ilimradi apatiwe majibu ya fikra zake..
Alijaribu kufungua mdomo wake ili ahoji,,ajabu mdomo wake ulikuwa mzito kabisa hakuweza kuzungumza!.
“usiwe na haraka utafahamu muda ukiwadia” Alisema yule mzee, alikwisha soma mawazo ya Sophia kichwani mwake,
“Kesho asubuhi utaruhusiwa, hakikisha ufikapo nyubani usifungue mdomo wako kumweleza yeyote habari zilizo kukuta jana usiku”.
Moyo wa Sophia ulipiga “paaaaaaa” kengele ya hatari iligonga kichwani mwake,akili yake ilifanya kazi haraka,haraka aliona maisha yake tayari yamekwisha ingiliwa na aina ya jamii nyingine ya kishetani, pia ni kauli hiyo ndiyo ilyo fungua kumbukumbu zake.
Alikumbuka baada ya kudungwa visu kadhaa kifuani mwake alipoteza fahamu,na alipo zinduka alijikuta amezungukwa na watu walio kuwa wamesimama kwa heshima na unyenyekevu wa hali ya juu ilionekana ni kama waliokuwa wakifanya ibada zisizo eleweka, yeye akiwa kalazwa juu ya meza ya kioo,ajabu majeraha yake ya visu hayakuonekana kabisa mwilini mwake.
ITAENDELEA KESHO SAA KUMI NA MBILI JIONI.
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi @Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya Lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO @multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden@bwii ONTARIO Kobe The Vein mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo @shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi DONALD stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny @Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi @Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA Khantwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom