RIWAYA: Msitu wa Solindo

RIWAYA: Msitu wa Solindo

MSITU WA SOLONDO

Mtunzi Richard Mwambe

Sehemu 12

upande wa kerume kuna kibuyu kikubwa ambacho kimefungwa juu ya miti miwili, bila
kuchelewa alikifumua kwa risasi moja tu na kibuyu kile kilitawanyika vipandevipande
kitu kama mafuta ymazito yalimwagika na kufanya mlipuko mkubwa wa moto eneo lile,
Kerume alipiga mbinja moja kali na kutoka ndani ya pango lile joka kubwa likatoka,
Gorino walimkamata Amata na kumtupa chini kwa nguvu joka lile likatambaa kwa kasi
na kumfikia Amata pale alipolala, kutahamaki Amata alivingirishwa na joka lile na
kuondoka nae, “Amataaaaaaa!!! “ Hellen aliita kwa uchungu huku akijiweka sawa na
kufyatua risasi moja lakini shabaha haikuwa sawa, wakati huo gorino walikuwa
wamechachamaa wengine wakizima moto na wengine wakijaribu kumfikia Hellen. Mara
upepo mkali ukazuka eneo lile vumbi lililowafanya gorino wasiweze kuonana sawasawa
lusiku ule, kweli ilikuwa patashika nguo kuchanika, Kerume alifichwa katika pango
maalum na gorino sita walikaa mbele ya pango hilo kulinda usalama. Hellen hakuweza
kuona sawasawa katika vumbi lile alikimbia upande mwingine ambapo angeweza kuona
vizuri, alipopita eneo lile alilokuwa Amata alikiona nisu cha Amata na uta wake vikiwa
chini havina kazi, haraka aliokota kisu na kwa kuwa joka lile lilikuwa bado halijaisha
kuridi pangoni, Hellen aliruka samasoti kama nne mfurulizo na alipotua alijikuta juu ya
mikono ya Gorino badala ya kuliwahi joka lile huku jisu lile likimtoka mkononi na moja
kwa moja likatua hatua chache mbele ya mateka aliyekuwa akifuata kwa zamu ya
kutolewa kafara. Bila ajizi, aliokota kisu kile na kukata kamba ya mwenzake kwanza
maana yeye alifungwa mikono yote, alipofanikisha basi wote walisaidiana na kubaki huru
lakini hakuna aliyesubutu kutoka pangoni pale. “Heeeelllllppppp!!!!” Hellen alipiga
ukelele, mmoja wa wale mateka hakuona haja ya kukaa pangoni mle alijitoma nje na
jambia lake mkononi kabla hajashambulia alikutana na jiti la uso ambalo lilirushwa
kutoka kwa mmoja wa Gorino aliyekuwa akielekea pangoni huko kwa kasi lakini sasa
akiwa mikono mitupu kuliwahi jiti lake tayari kwa mapambano alijikuta akipaa hewani
na kujibwaga juu ya jiwe baada ya bastola ya Hellen kufanya kazi yake sawasawa.
Kimbunga kile kiliendelea kwa fujo lakini cha kushangaza moto haukuzimika ila
uliongezeka. Akiwa bado akijiweka sawa Hellen alimuona Bundi mkubwa akipita eneo
lile lakini alizungukazunguka tu hakuweza kutua. Hakuwa na lakufanya joka lile
lilikwishapotea pangoni likiwa na Amata, Hellen aliishiwa nguvu hakuwa na la kufanya
Gorino walizidi kuongeza nguvu. Hali ilizidi kuwa mbaya eneo lie wale mateka walitoka
wote wakiwa na majambia yao mikononi pamoja na kukaa mateka siku zote Gorino
hawakujua kuwa majambia yaliyofungwa viunoni mwa mateka wao ni silaha tosha.
Bundi lile lilipita tena eneo lile hali ni ilele halikutua popote likadondosha kitu kama
chupa nyeusi ambayo ilidondokea karibu na Hellen, kwa kuwa muda huwo Hellen
alijikuta akichoka ghafla aliiokota ile chupa na kuitumia kama silaha aliirusha Gorino
mmoja aliijua chupa ile alikimbi pembeni ikadondoke karibu kabisa na mlango wa pango
alilmohifadhiwa Kerume. Moshi mzito ulitoka ndani ya chupa ile uliwafanya Gorino
wale waanze kupoteana na kuweweseka wakikohoa na kuanguka ovyo hii ilikuwa nafasi
nzuri ka Hellen aliweza kuangusha mmoja baada ya mwingine.
Amata alirushwa nje ya pango na kufuatiwa na joka lile, alijikwaa na kuanguka
‘unapokuwa na shida piga mbinja hii... utapata msaada’ sauti ya marehemu baba yake
ilimrudia kichwani bila kuchelewa akakunja mikono yake na kupiga mbinja kali, Hellen
alisikia mbinja ile ikijibiwa msituni, punde si punde Kingusu mzimu wa kina Amata
ukaanza shughuli, mshale wa kwanza ulipiga katikati ya paji la uso la mlinzi wa Kerumehakuomba maji, Kingusu alishuka toka juu ya mti na kujificha mahali aliona jinsi lile
joka lilivyokuwa tayari kummaliza Amata, mshale wa pili ulichana sehemu ya mwili wa
joka lile kubwa, likaanguka na kutapatapa, Hellen alimrushia Amata uta wake ukadakwa
vizuri sana na aliyekusudiwa.
Nguvu ya Gorino ilipungua kwa kasi kutokana na moshi ule ambao ulitoka ndani ya
chupa ile ya ajabu, ulikuwa ukiwafanya wakose nguvu, mmoja wa Gorino aliingia ndani
ya pango lile na kutoka na kitu kama chupa ya mtindo ule ule naye aliipasua kwa kuipiga
katika jiwe moshi mweupe ulitawanyika na kuwarudishia uhai Gorino wale walioanza
kuchoka.
[emoji814][emoji814][emoji814]
Kiumbe cha ajabu kilimtokea Saringo katika maficho yake, Saringo ambaye wakati
huo hali yake ilizidi kuwa mbaya kwa kupoteza damu nyingi alikuwa ametulia kimya
hana la kufanya na alikuwa akiangalia tu nini kitatokea. Alitamani sana kwenda
kuwasaidia wenzake kwa kuwa aliona jinsi walivyobanwa na Gorino katika mapambano
yale lakini alishindwa kabisa. Alijikaza lakini alikuwa anaogopa mno jinsi kiumbe kile
kilivyoonekana, kilisimama mbele ya Saringo na kumwangalia kisha kikamsogelea na
kunyoosha mkono wake kuelekea jeraha la Saringo. Kiumbe kile kilikuwa na vidole
virefu na kadiri ya umbali vilikuwa vikirefuka kuelekea kwa saringo na alimpogusa
jeraha Saringo alihisi ganzi mwili mzima na kuzirai.
Bibi kizee alikuwa akipita eneo la mapambanao kwa umbo la Bundi lakini alishindwa
kabisa kutoa msaada wowote ka Amata na Hellen, hakuwa mbali kwa kuwa kile
alichokubaliana na Amata kilikuwa bado hakijatimia. Katika eneo lile ilikuwa vigumu
kwake kujigeuza na kuwa katika umbo lingine kutokana na uchawi wa hali ya juu ambao
Gorino waliuweka eneo lote la tambiko, hivyo ilikuwa ni vigumu kwa viumbe vingine
kutawala eneo lile au hata kupita ilikuwa ni vigumu kwao. Na katika pambano la Gorino
kumuondoa bibi kizee na wasichana wake eneo lile ilikuwa kazi ngumu kwa kuwa kila
mmoja alikuwa na zindiko lake mahali pale, lakini Kerume kwa kutumia uta wake wa
kichawi aliweza kuwashinda bi kizee na wasichana wake ambao hata wao miaka mingi
nyuma walikuwa wakifanya matambiko yao hao, na humo ndani ya pango walihifadhi
vitu vyao vingi ambavyo Kerume alipowashinda alifunga kwa kuzindika na nguvu zake
za kichawi hivyo bi kizee na wasicana wake wakawa kama watumwa wa Gorino. Bibi
kizee alimuomba Amata Roho ya Kerume akimuahidi kumpatia kila atakachopata.
Saringo alikimbia taratibu kuelekea eneo la mapambano alimuona Hellen alipokuwa
akipambana na Gorino wale kwa kutumia bastola yake ambayo ilikuwa karibu na kwisha
risasi. Amata akiwa na uta wake mkononi sasa lengo lake lilikuwa ni kumtafuta Kerume
lakini katika pango aliloingia kulikuwa na walinzi watano baada ya mmoja kuuawa,
akiwa katika mwendo wa kuchechemea alijaribu kukwepa vishale vya Gorino ambavyo
vingi vilimwandama yeye.
Hellen hakuamini kumuona Saringo eneo lile, Saringo aliingia katikati na mkononi akiwa
na kitu kama mfupa ambao aliutumia kama silaha kwa kuwapigia Gorino wale lakini
alichoshangaa ni kuwa kila aliyempiga nao hakuweza kupona, aliendelea kupambana na
Gorino waliosalia eneo lile kwani wengine wlitawanyika hawakuonekena ila walijificha kwa kuwa hawakujua la kufanya. Kingusu aliwaandama walinzi wa Kerume kwa kupiga
mishale kwa ustadi mpaka walipoukiambia mlango wa pango aliloingia Kerume, Amata
alipotaka kuingia alihisi kitu kumpiga kichwani akarudi nyuma na kuangalia juu mmoja
wa Gorino alimpiga Amata kwa kutumia kitu kama nazi, Amata alipanda juu ya jiwe na
kumrushia kisu kilichompata sawia kifuani. “Amataaaaaaaaa!!!!!” sauti kali ya Saringo
ilimfanya Amata ageuke nyuma kitendo hicho ndicho kikamfanya apone kutoka katika
msahale uliopigwa kutoka pangoni, mshale wa Kerume mshale wa kichawi usiokwepeka
na binadamu, Amata alipepesuka na kuanguka chini, alimuona Kerume akitoka Pangoni
na kuja nje, Amata alijiinua haraka na kusimama kidete uso kwa uso na Kerume. Kerume
alimvamia Amata kwa nguvu Amata akaepa upande na kumpiga ngwala lakini Kerume
aliruka na kusimama sawia, akageuka na kumpiga Amata na kikoto cha mfupa Amata
aliyumba na kuanguka karibu na mlango wa pango, Kerume alimfuata akiwa na hasira
lakini kabla hajamfikia Amata, Kingusu alifyatua mshale uliopita mbele ya uso wake pale
alipoukwepa, Kerume aligeuka na kutazama juu ya mti akamuona nyani mkubwa “Beselo
sito!” akimaanisha ‘huu ni mwisho’ akachukua mchanga na kuupulizia kule alipo nyani
yule punde si punde nyuki walijaa eneo hilo na kuanza kuuma kila aliyekuwepo. Hellen
na Saringo walilala chini lakini haikusaidia, nyuki walimzingira Hellen aliyekuw
akijaribu kukimbia kutafuta pa kujificha, Hellen aliumwa na nyuki wnegi waliompelekea
kukosa nguvu na kuanguka chini, Saringo hakuwa na la kufanya juu ya nyuki wale
wakali.
Amata alipata muda wa kunyanyuka na kuegemea jiwe, Kerume alinyanyua jiti lake na
kumchoma Amata kifuani lakini Amata alibonyea chini na jiti lile likapiga kenye jiwe,
Amata alipita katikati ya miguu ya Kerume na kutokea nyuma yake aliruka teke la
kusukuma na kutua mgongoni mwa Kerume ambaye aliyumba kwenda mbele na kabla
hajageuka mshale wa Amata ulikuwa njiani alipogeuka tu uso kwa uso na mshale ule
lakini Kerume aliudaka kwa mdomo wake akaugeuza na kuurusha kwa mdomo na
mshale ule ulichomoka kwa kasi ya ajabu, Amata alishindwa afanyeje lakini kabla
hajaamua jambo mshale ule ulikosa nguvu na Amata akaudaka kwa mikono yake.
Kerume kwa kutumia kikoto chake cha mfupa alimpiga Amata mapigo ya kifo lakini
Amata alikwepa yote kwa ustadi huku akirudi nyuma mwisho Kerume alirusha kikoto
kile Amata alikwepa, Hellen alikuwa anajaribu kunyanyua uso wake ndipo alipohisi
maumivu makali katika paji la uso, kikoto cha mfupa kilichorushwa na Kerume kilitua
usoni kwa Hellen, Hellen aliona giza kuu likiyavamia macho yake, kutoka pale
alipodondoka wakati akishambuliwa na nyuki alijilaza tena.
Amata alipigwa kichwa na Kerume, alijitoa kwenye mikono ya Kerume na kurusha
ngumi mfululizo ambazo zilimpata Kerume lakini hakutetereka hata kidogo. Amata
alijifanya kukimbia kuelekea kwa Saringo na Kerume alimfuata, Saringo alimrushia
Amata ule mfupa na Amata alipoudaka tu aligeuka na kumtandika Kerume kichwani,
Kerume aliyumba na kabla hajatulia Amata alimpiga tena kichwani pigo ambalo
lilimpeleka chini Kerume hakiwa hajiwezi, akiwa anatambaa kujisogeza na Amata
alikuwa akitembea kumwangalia, akamkanyaga kichwani na kukishindilia kichwa kile
katika mawe. Upepo mkali ukaanza kuvuma miti yote ikawa ikiyumba kwa kasi ya ajabu,
vumbi lilitimka eneo lote. Amata aliona mwanga wa ajabu uliong’aza eneo lote, mwanga
wa rangirangi za kumetameta, Amata akanyanyua uso wake kuangalia mbele na juu ya
jiwe lile alimuona Saringo kasimama akiwa na upanga mkononi, upanga uliokuwa ukitoa mianga ya ajabu na mkono wake wa pili ameshika kichwa cha chui.
“Saringo!” Amata aliita huku akiondoa mguu wake pale alipomkandamiza Kerume.
“Mimi sio Saringo” alisema mwanamke yule huku akishuka mpaka pale chini alipolala
Kerume, sasa akiwa uso kwa uso na Amata. Akampa Amata kile kichwa cha chui kisha
akanyanyua upanga wake juu kwa mikono miwili. Kelele zilisikika msituni za watu
wakilia na kuomboleza, upepo nao aulizidi kuvuma eneo lote, Saringo bandia akashusha
upanga na kukata Shingo ya Kerume, kichwa chake kiliachana na kiwiliwili lakini cha
kushangaza kiwiliwili kile hakikutoa hata tone la damu. Saringo bandia akakitupa kichwa
cha Kerume katika moto uliokuwa ukiwaka eneo lile kisha akachukua kichwa cha chui
kutoka kwa Amata na kukisemea maneno fulani ambayo Amata hakuyaelewa na
kukipachika kile kichwa cha chui katika kiwiliwili cha Kerume na muda huo huo Kerume
akageuka Chui mkubwa wa kutisha, Saringo bandia aliongea maneno fulani na Chui yule
akakimbilia msituni.
Amata alibaki mdomo wazi huku akionekana na sura ya woga, akageuka nyuma na
kumuona Hellen akiwa kalala chini akamfuata na kumtazama alionekana kama hana uhai,
aliyageuza macho yake na kuona tayari ni mfu. Amata alidondosha chozi, mara akasikia
kama kundi la watu likija mahali pale alipogeuka aliona kundi la Gorino likiwa
limesimama nyuma yake.
“Usiogope Amata” yule Saringo bandia alisema
“Hao wote ni mateka wangu, hawana nguvu tena kwa kuwa Kerume zindiko la kichwa
cha chui amerudi alikotoka” aliendelea
“Hapo unapowaona hawajaja wenyewe wamekamatwa na kuletwa. Tumerudi kwenye
himaya yetu ya Msitu wa Solondo, katika pango la Mtukufu Baghoza hakuna aliye juu
yetu ila wote wako chini yetu, na sasa ni zamu yetu kutoa kafara kwa Baghoza” Saringo
bandia aliongea na Amata wakati Amata akiwa bado kamshika Hellen ambaye tayari
mwili wake ulikuwa wa baridi kabisa.
“Amata, umefanya kazi tuliyokuwa tumeishindwa kwa karne na karne, unastahili zawadi
kubwa kuliko unavyofikiria.” Saringo bandia alimwambia Amata
“U nani wewe? Mbona unafanana na Saringo?” Amata aliuliza
“Mimi ni Baghoza, kinara wa roho zisizoonekana. Unisamehe Amata, nilimkuta Saringo
anakata roho nikauchukua mwili wake lakini hapa tunavyoongea ameshakufa” Saringo
bandia aliinamisha kichwa kuonesha masikitiko
“Baghoza!” Amata alitamka na kupiga magoti mbele ya Saringo bandia, akaendelea
“Kuliko kunipa zawadi yoyote, naomba nirudishie uhai wa watu wangu”
“Ha ha ha ha ha haaaaaa, Baghoza hata kama ndiye mleta mauti na mtoa uhai, siwezi
kukutimizia hilo kwa sababu moja” akatulia kidogo kisha akaendelea “Solondo si eneo la
kuishi ninyi binadamu, kama sisi hatuji kwenu na sisi hatupendi mje kwetu. Mnafata nini
huku?” Saringo bandia aliendelea kumwambia Amata
“Wewe hukutaka kuja huku, hata hujui huku kuna nini, ila hawa wenzako wana tamaa ya
mali na utajiri hata ijapokuwa wanajifanya wanafanya utafiti, sisi tuna uwezo wa kuona
fikra zenu. Amata kumbuka tamaa mbele mauti nyuma, kwa tamaa yao wote wamekufa
na hawataamka tena. Ila wewe kwanza umetusaidia kurejesha himaya yetu hatuna budi
kukupa zawadi, na ukishaondoka hapa sisi tutaendelea na ibada yetu ya kafara” Saringo
bandia alisema hayo huku akiwa na upanga wake mkononi. Aliunyoosha upanga wake na
ukaanza tena kutoa ile miale ya mwanga iliyoangaza eneo lote pale katika jiwe, mara
upepo ukaanza tena kama mwanzo sasa ulikuwa wa kuzunguka na ukakusanya vumbi kubwa kisha katikati ya upepo ule Amata aliona kama mtu kasimama na ulipotulia
alimuona bibi kizee kasimama pale na hakumuona tena yule Saringo bandia. Yule bibi
kizee akamsogelea Amata, akainua mkono wake na kutoa pete iliyokuwa iking’aa sana
iliyowekwa jiwe la yaspi safi na kwa ndani ilikuwa na madini kutoka sayari ya Uranus.
Amata akaipokea na kuigeuzageuza ilikuwa ikitoa rangi nyinginyingi.
“Vaa katika kidole cha kati mkono wa kushoto” bibi kizee alitoa maelekezo. Amata
akavaa na alipomaliza aliona mji mkubwa sana mbele yake majengo marefu marefu na
wanawake wazuri warembo wa kuvutia wenye nywele ndefu, hakika mji ule ulikuwa ni
wa kipekee, cha ajabu aliona wanawake tu na ailipogeuka nyuma yeke alijikuta
kazungukwa na wadada wengi sana, Amata alistaajabu aliyoyaona hapo, akanyanyua
mkono wake na kuitoa pete ile kidoleni, akajikuta yupo palepale msituni na mbele yake
bibi kizee akimwangalia, aligeuka nyuma na kuona hakuna wale wasichana isipokuwa
Gorino walioletwa pale.
“Vaa katika kidole cha shahada mkono wa kushoto” bibi kizee alimwambia Amata.
Amata akavaa pete ile katika kidole cha shahada, mbele yake aliona moto mkubwa
ukiwaka katika shimo, cheche kubwa za moto zilikuwa zikiruka na kurudi shimoni,
alisikia vilio vya watu wakilia kwa maumivu makali na kusaga meno, Amata aliangalia
vizuri na kuona watu wengi wasio na idadi. Amata akatoa machozi akalia kwa
vikwifukwifu kwa kuwa aliwaona Hellen, saringo, Stephan na Golam wote wakiwa
katika mateso hayo. Aliivua pete ile na kuishika mkononi. Alijikuta tena na bibi kizee.
“Bibi kwanini rafiki zangu wapo huku?” Amata aliuliza
“Watu wote wenye tamaa ya mali huishia huko, huwezi kuingia Solondo ukafika kwenye
jiwe hili kama una tamaa ya mali. Hizi mali ni zetu, kila penye madini na sisi tupo na
tunayalinda sana. Hawa Gorino walitufukuza hapa na kuchukua wao, wakamuweka huyo
nyoka wao wa ajabu, huyo hakuwa nyoka wa kawaida, mshale wa Kingusu ndiyo
umemmaliza huyo Nyoka.” Bibi kizee alimueleza Amata na kisha akanyanyua kichwa
chake kuangalia angani akaendelea kusema
“ Mwezi umekuwa mpevu, huu ni muda wetu. Amata naomba tuagane, pete hiyo utaivaa
kila utapoitaji kuonana na sisi, utaivaa kidole cha kati kisha utaigonga kwa kwenzi mara
tatu utafunguliwa mlango, ukigonga mara nne utaomba chochote tutakupa. Tahadhali,
usiigonge mara moja wala usiigonge mara mbili.” Bibi kizee alimuasa Amata
“Sasa pita katikati ya hilo pango kubwa, huko chini utakuta mambo mengi sana usiogope
utakutana na viumbe wa ajabu usiogope, teremka chini mpaka ngazi ya kwanza kutoka ya
saba utakuta milango imejipanga nenda mlango wa kwanza kutoka wa tano fungua uingie
pale utakuta vitu vingi sana chagua kadiri ya uwezo wako uende zako” bibi alimaliza
kuongea
“Bibi, nitajuaje njia ya kwenda kwetu? Hata nilivyokuja sijui” Amata aliuliza tena
“Amata muda umeisha tunataka tuanze kazi yetu, nenda sasa ingia haraka kimbia,
imetosha, tena usigeuke nyuma kabisa” sauti ya bibi ilianza kuwa ya kutisha yenye
mwangwi wa ajabu. Amata aliiuacha mwili wa Hellen na kuingia pangoni kwa kasi,
nyuma yake alisikia radi kali na ngurumo za ajabu.
[emoji814][emoji814][emoji814]
Giza nene lilitanda kila kona ya pango lile, Amata hakuweza hata kuona wapi
anaelekea, alivuta hatua fupifupi kwa kuwa alihisi kama akiteremka ngazi, nyuma yake
alisikia tu kama vitu vikianguka na watu wakipumua kwa nguvu alitamani kugeuka lakini alikumbuka maneno ya Baghoza, alijikaza na kusonga mbele, alizidi kuteremka chini
zaidi huku akipapasa kwa kuwa hakuweza kuona hata umbali wa urefu wa mkono wake.
Woga ulimtawala, nguvu zilimpungua alihisi akikosa hewa ya kutosha, akiwa bado
anaendelea kuteremka alihisi amekanyaga kitu, akarudisha mguu kisha akakanyaga tena
akuhisi kile kitu, akaendelea kuteremka ndipo alipohisi mguu wake ukishikwa na kitu
kama mikono akaanza kusikia sauti kama ya siafu wengi waliokuwa wakitembea, Amata
alifikiri kurudi nyuma lakini alikumbuka maneno ya Baghoza, moyo wake ulikosa la
kuamua akanyanyua mguu kwa nguvu lakini bado hakuweza ndipo alipoinama kushika
kilichopo mguuni alijikuta akipigwa kofi la utosini lililompelekea kudondoka katika
ngazi zile na kuviringika kuelekea chini zaidi. Alisikia sauti za vicheko zikimsindikiza na
alipofika chini kabisa utulivu ulirejea kama mwamnzo, sasa hakuweza kusikia vya nje
wala vya ndani. Amata alinyanyuka na kuketi, kila mara mwili ulimsisimka lakini
hakuweza kuona chochote katika pango lile. Alipokumbuka maelekezo aliyopewa na bibi
kizee Amata alihisi kupata ganzi kani hakukumbuka kuhesabu ngazi alizoshuka hivyo
hakuweza kujua yuko ngazi ya ngapi, alijishika kichwa na kujilaumu nafsi yake kisha
akasimama na kuendelea kushuka lakini hakukuta ngazi za kushuka bali ukuta ulimkinga
hakuweza kusonga mbele, aliposhika kushoto na kulia kote aliona vivyo hivyo, hakuwa
na budi zaidi ya kurudi nyuma ili aweze kuhesabu ngazi zile. Lakini akiwa katika
kutafakari afanyeje maana aliambiwa asithubutu kugeuka nyuma, aliikumbua pete yake
aliyopewa na bibi kizee aliunyanyua mkono wake na kuigonga kwa kutumia kwenzi mara
nne pete ile ikabadilika na kuwa ya buluu,
“Ninaomba msaada nimepotea pangoni na kuna giza sana” Amata alimaliza kusema
kisha kutulia kama sanamu. Upepo mwanana ukaanza kuvuma katika pango lile mara
Amata aliiona mienge iliyotundikwa pembeni ya ukuta ule ikiwaka mmoja baada ya
mwingine, baada ya muda mfupi pango lile lilikuwa linang’aa, Amata alichomoa moja ya
mienge ile na kuanza kupanda ngazi zile kwa kurudi nyuma bila kugeuka. Aliendelea
taratibu mpaka alipofika mahali alipoelekezwa, pale akakuta kuna lango kubwa bila
kuchelewa na mwenge wake mkononi akaingia na kuvuta hatua chache alihisi kuna
viumbe vikipita mbele na nyuma yake vikiwa katika shughuli mbalimbali lakini
hakuweza kuviona kwa macho. Pango lilijawa na nyzi nene za buibui kila kona
zikiashiria kuwa humo ndani ni muda mrefu hakujaingiwa na mtu. Katika kutazama uku
na huku akaona milango kadha wa kadha imejipanga na kuwekwa makufuli makubwa.
Alihesabu milango ile lakini ilikuwa ngumu sana kwa kuwa aliona kama inamzunguka,
alikata tamaa mara akakumbuka maelekezo ya bi kizee akaaza kuhesabu tena sasa
akaupata mlango aliyouhitaji, mlango mkubwa wenye kufuli nene akajaribu kutoa yale
mabuibui na kuufikia. Mlango ule ulikuwa na picha ya kichwa cha nyoka mkubwa sana,
Amata aliusogelea na akaona kichwa kile kinapata uhai na kufungua mdomo wake tayari
kutema mate, Amata aliogopa na kurudi nyuma, alipojaribu kusogea tena ikawa vilevile.
Amata akanyanyua mkono wake akaigonga pete yake mara nne “fungua” akatamka neno
hilo. Mara aliona kufuli lile likifunguka kana kwamba kuna mtu aliyefungua na mlango
ukajisogeza kwa ndani, Amata akajitoma ndani, chumba kilikuwa ni kitupu pembeni
kabisa kulikuwa na jeneza lililochongwa michongo ya ajabu ajabu. Amata alisimama na
kuliangalia jeneza lile lililojaa vumbi akalishika kufungua, alipoondoa mfuniko wake
alipigwa na bumbuwazi, kulikuwa na ngazi zikishuka kuingia shimoni, Amata aliingia na
kufuata ngazi zile kuteremka chini kabisa ya shimo lile, ndani ya shimo lile mlikuwa na
giza nene, Amata alishuka taratibu akisaidiwe na ule mwenge alioushika mkononi mwakealipokaribia chini alianza kuona vitu viking’aa kutokana na ule mwanga wa mwenge
alioushika. Amata alitabasamu alipoona vitu vile vilivyojawa vumbi na buibui kufanya
makao yake, sahani, vikombe, vitu mbalimbali vya thamani vilivyotengenezwa kwa
madini ya dhahabu, almasi, vito vya madini mbalimbali kama yaspi, quartz, marmar.
Amata alibakia kaduwaa hajui wapi shike wap aache, alipouona mkufu alimkumbuka
rafiki yake Chausiku ‘huu utamfaa’ alijiwazia. Alizunguka huku na huku na hakujua
afanye nini. Alibaki kufikiria hatima ya maisha yake na mawazo yake yalisafiri dunia
nyingine akimkumbuka Chausiku binti Saidi ambaye ni muda mrefu hakumuona.
HATIMA
Amata akiwa juu ya jiwe kubwa alikuwa na furaha sana alipomuona mtoto wake
akicheza na mama yake Chausiku binti Saidi, alitabasamu alipowaona wakikimbizana
pale katika nyasi za kijani sana zilizojawa kila aina ya rutuba.
Moyo wake uliridhika na ulijawa na furaha alipotazama nyumba yake nzuri kijijini pale,
mashamba makubwa aliyokuwa akimiliki, sasa hakuwa mkulima wa jembe la mkono bali
alikuwa akimiliki trekta kubwa, mifugo iliyokuwa hapo ilizidi kupendezesha eneo kubwa
lililomilikiwa na kijana Amata.
Amata alikuwa akiangalia picha alizotengeneza kutoka katika kamera ile ndogo
aliyoichukua kwa Stephan, picha za kutisha, picha za Solondo.
Aliteremka kutoka katika jiwe lile na kuungana na familia yake katika mchezo ule mzuri,
walicheza na kufurahi pamoja Amata, Chausiku na mtoto wao. Hakika Chau alikuwa ana
haki ya kuwa na furaha kwani alikataa wanaume wengi sana ili kumsubiri Amata atoke
gerezani hakujua hata kidogo masaibu yote yaliyomkuta katika safari yake ya hatari.
Alijawa na furaha tu alipomuona kijana huyu yupo pale kijijini lakini sasa akiwa mtu
tofauti sana, alimkumbatia kwa furaha zote na baada ya muda mfupi wawili hawa
walifunga ndoa na kuishi pamoja na kujenga familia yenye furaha.
Na hapa msemo wa wazee ulitimia...

‘Ridhiki ya Mbwa iko miguuni mwake’
MWISHO MWISHO
 
Kulubule baada ya kutoka msitu wa Solondo tunaelekea wapi tena?
 
Asante kulubule barikiwa mpaka ushangae
Pia shukrani kwa mtunzi [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] Mungu ambariki@amata gaimba
 
Mkuu kulubule nimepita kwenye page ya mtunzi. Kakupost kwamba una copy hadithi zake hafu huweki jina lake kama mtunzi pia hujamtaarifu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom