HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,450
- 6,211
- Thread starter
- #41
MSITU WA SORONDO
Mtunzi Richard Mwambe
Simu 0754740668
Sehemu 5
Nini Amata?” Hellen alimuuliza
“Chatu! Nyoka mkubwa anayeweza kumeza mtu” Amata alijibu. Hellen akajificha
nyuma ya Amata, Saringo alikuwa akiangalia kwa makini lakini hakuweza kuona cha
kufanya alisubiri kuona nini Amata anataka kufanya, kwa upole Amata aliweka mshale
sawia katika uta wake na kuvuta kwa nguvu zake zote, mikono yake iliyojaa misuli ya
nguvu ilituna na kuonesha kiasi gani nguvu alizotumia kuvuta uta huo, huku akiongea
lugha isiyoeleweka akiwa ameuma meno bado hakuachia pigo lake, kilichoonekana ni
jinsi tu alivyoutembeza uta huo taratibu sana kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Kutoka ndani ya mitete ile nyoka mkubwa alifyatuka kwa spidi ya ajabu kuelekea mtoni
alipo Stephan, Amata aliachia uta wake na mchale uliondoka kwa spidi kali kukikabili
kichwa cha nyoka yule, hamad!!
“Stephannnnnnn!!!!!” Hellen alipiga kelele ya nguvu na Stephan alipogeuka alishuhudia
joka kubwa refu lililofungua domo lake likimuelekea, mara alishuhudia kitu kikipita kwa
kasi kati yake na joka lile, ulikuwa mshale wa Amata aliopigwa kwa ustadi lakini
kutokana na ukelele wa Hellen Joka lile liligeukia upande ulikotoka ukelele hivyo
kufanya shabaha ya Amata kuwa ya bure. Joka lile lilijivuta na kuburuzika chini
likijikunjakunja kuelekea walipo akina Amata, Amata alijinyanyua na kujirusha upande
wa pili akimvuta Saringo wakati huo Helleni alijiinua na kujikuta amechelewa, alipigwa
ngwala maridadi sana na joka lile na kupaishwa juu, kabla hajafika chini joka lili
lilimdaka kwa ustadi mkuwa na kujiviriga mwilini mwake, likiwa linadondoka kwa kwa
kasi, Amata alikuwa tayari kesha vuta uta wake na kuuwachia, shabaha ya ajabu! Mshale
ule ulipenya sawasawa karibu kabisa na kichwa cha joka lile, kutokana na maumivu yale
joka lile likamuachia Hellen na kudondoka chini Hellen nae akadondoka juu yake, Joka
lile likajivuta tena kumkimbiza Amata, amata hakukimbia mbali bali aliuzunguka mti ule
waliokuwa wamekaa huku akiweka vizuri mshale wake wa tatu alijikwaa na kuanguka
vibaya, joka lile likamtia mkononi likamviriga vizuri, bahati nzuri mkono mmoja wa
Amata ulikuwa nje ya mvirigo ule
“Amataaaaa....” Saringo aliita, na kumrushia kisu ambacho Amata alikidaka kwa ustadi
mkubwa na bila kuchelewa alididimiza kisu kile kwenye sehemu ya mwili wa joka hilo,
joka likajiinua juu likiwa bado halijamuachia Amata, Amata alisikia mvumo mkali na
alichokishuhudia ni damu iliyoruka kwa matone makubwa makubwa, joka lile halikuwa
na kichwa tena, likaanguka kwa mshindo mkuu, ilikuwa ni risasi kutoka AK 47
iliyopigwa kwa ustadi wa hali ya juu na Stephan na kukitawanya kichwa cha joka lile na
kukichanachana vibaya.
“Nice shot!!” Hellen alimsifu Stephan, wakakumbatiana na kubusiana kama ishara ya
kupongezana. Saringo alimfuata Amata pale alipolala na kumsaidia kujitoa katika joka
lile, haikuwa kazi rahisi kuukunjua mwili wa joka lile kubwa ambao kwa wakati huo
ulikuwa bado umejiviriga katika mwili wa Amata. Helen na Stephan nao waliungana na
Saringo katika kazi hiyo, mara wakafanikiwa na kumnasua Amata ambae uso wake
ulikuwa umechafuka kwa damu ya joka lile, wakamlaza vizuri na kumuosha uso wake.
Mikono laini ya Saringo ilipita usoni mwa Amata, Amata akajitikisa kidogo na kuushika
mkono wa Saringo
“Nini Amata?” saringo alimuuliza
“Mkono wako laini umenisisimua mwili...” Saringo akatabasamu aliposikia maneno hayo
ya Amata Usianze Amata!” Saringo akasisitiza. Amata aliketi na kutazama vizuri huku na huku,
akaokota uta na podo lake akaweka mgongoni... safari inaendelea!
Msitu ulizidi kuwa mnene mbele yao, lakini Stephan aliyekuwa na ramani ya wapi
wanakokwenda alisisitiza kuelekea upande huo hata kama haukuwa na njia, walisonga
mbele, panda milima, shuka, vuka mto pasua vichaka, mvua, jua vyote vilikuwa juu yao,
chakula kikubwa kilikuwa ni matunda ya porini ambayo kwayo walijitosheleza na
kujipatia vitamini za kutosha sio mpaka akuandikie daktari.
Jioni hiyo ya siku ya tatu mvua ilikuwa kubwa sana, radi zisizo na huruma zilipasua anga
lote na kulifanyia michoro ya kutisha, hapakuwa na pa kujikinga wala kujificha, wote
walitota miili hata nguo zao kugandamana na miili yao, walitetemeka kwa baridi kali ya
msituni hata miguu ilishindwa kutoa ushirikiano na mwili mara nyingi ilikataa kusonga
mbele, hakukua na lakufanya isipokuwa ni kujivuta hivyo hivyo, walitamani jua liwake
haikuwa hivyo, walipenda wakoke moto lakini kila kitu kililowana, safari ilizidi kuwa
ngumu kwani msitu wote ulifunikwa na ukungu mzito hata mwanga wa tochi haukufua
dafu. Amata alisimama na kugeuka nyuma akawaonea huruma wenzake maana walikuwa
wakitetemeka kupita maelezo. Saringo alimuendea Amata na kumkumbatia kwa nguvu
huku akitetemeka, vivyo hivyo kwa Hellen na Stephan, walivuta hatua fupifupi japo kwa
shida kujitafutia mahali pa kupumzika.
“Tukae humu mpenzi!” Amata alishtuka kidogo kusikia kauli hiyo toka kwa Saringo,
alibaki kujiulizauliza maana hajawahi kuitwa mpenzi katika maisha yake. Amata
alitazama na kuona pango pembezoni mwa mti kabla hajaamua cha kufanya Stephan na
Hellen wakawa tayari wamejitoma ndani ya pango hilo lenye kiza,
“Amata twende!” Saringo alisema huku akimvuta mkono kuelekea pangoni, Amata
alimvuta Saringo kwa nguvu na kumkumbatia kifuani mwake, akamkazia macho Saringo
alimtazama Amata usoni kwa hasira lakini hakuwa na la kusema alizungusha mikono
yake mgongoni kwa Amata na kuikutanisha kisha kuegemeza kichwa chake kifuani mwa
Amata. Amata alitulia kimya kwa muda akiangalia lile pango waliloingia akina Stephan
“Saringo! Unafikiri hilo ni pango? Isije kuwa mtego tu” Amata alimuuliza Saringo
“Wenzetu wameingia wewe hutaki, Amata una nini twende!” Saringo alisisitiza
“Saringo! Mbona hatumsikii Stephan au Hellen hata kutuita!? Nina wasiwasi hili si
pango la kawaida!” Amata aliposema maneno hayo Saringo akashtuka na kugundua
kuwa ni kweli hawa viumbe wawili wangeshawaita lakini kimya yapata dakika mbili
sasa, Saringo akamuachia Amata, akaokota kipande cha mti kilicho jirani hapo
akakirushia ndani ya pango lile lakini hakusikia chochote hata mdondoko wa kipande cha
mti, Saringo akajishika mdomo na kuanza kutoa machozi.
“Saringo! Hapa ni msituni, usilie, tulia, jikaze kama mwanamke. Kilichobaki hapa ni
kutafuta cha kufanya kwa kuwa sasa tumebaki wawili wenzetu tayari msitu umewameza”
Amata alimbembeleza Saringo
“Hatuna silaha za kutosha itakuwaje kupambana na maadui?” Saringo alimuuliza Amata.
Amata akatazama podo na uta wake akajikuta kabakiwa na takribani mishale kumi na
tano podoni, akatikisa kichwa akaingiza mkono kwa ndani ya suruali yake kama
anayetaka kutoa dhakari ili ajisaidie, Saringo akasogea pembeni kidogo kwa hofu maana
hakujua Amata anataka kufanya nini, alipotoa mkono ukatoka na bastola moja. Saringo
alishangaa
“Umeipata wapi?” Saringo alimuuliza Amata Alinipa Hellen nimuhifadhie” alimjibu Saringo na kumtupia swali
“unajua kuitumia?”
“Ndio!” Saringo akajibu huku akiichukua mikononi mwa Amata na kuigeuzageuza kisha
akatikisa kichwa kuashiria amekubali, akajaribu kama analenga kitu, Amata akampatia
kikasha kimoja cha risasi, Saringo akakipokea na kukihifadhi vizuri...
[emoji814][emoji814][emoji814]
Stephan na Hellen waliingia kwenye kitu kama pango lakini halikuwa pango la
kawaida bali ni kama shimo lakini halikuenda chini isipokuwa lilikuwa na mteremko
mkali sana, hawakuweza hata kufanya lolote bali waliporomoka ndani kwa kasi ya ajabu
na huku kulikuwa na giza nene kuliko giza lenyewe, waliendelea kuseleleka hakuna
aliyepiga kelele kwana kati yao kila mmoja alikuwa akitahamaki. Baada ya kama dakika
tano za mseleleko ule Hellen alijigonga kwenye kitu kama ukuta au jiwe na kupoteza
fahamu, Stephan hakujua afanye nini maana giza ni nene, huku akiwa anavuja damu
mkononi mwake kwa kuwa alichunika vibaya sehemu ya nyuma ya mkono wake, alitoa
kiberiti na kuwasha angalau apate mwanga kidogo, lakini mwanga ule bado haukufua
dafu kwa giza lile. Stephan aliegeme kitu kama ukuta lakini alihisi ulikuwa rafu sana
alijaribu kuvuta hisia na kutega sikio lake kwa makini labda atasikia chochote ama watu
kuongea au chochote, lakini hakusikia kitu, taratibu macho yalianza kupambana na giza
lile na kuanza kuona japo kidogo, akiwa bado katika kutambua kilichopo ndipo aliposikia
kwa mbali mtweto wa mtu anayehitaji msaada, mara moja akagundua kuwa bila shaka ni
Hellen lakini hakujua upande upi hasa yupo akajaribu kuita kwa upole, lakini bado
aliendelea kuusikia ule mtweto ambao kwa sasa ulikuwa wa taratibu lakini ulisikika
kutokana na ukimya wa mle shimoni, alijaribu kupanda taratibu haikuwa rahisi kwa kuwa
hapakuwa na pakujishikia ila tu alisaidiwa na vipande vya mawe vilivyochomoza huku
na huku, mara akamfikia Hellen ambaye alikuwa amenasa kwenye jiwe fulani kumbe
hakuwa mbali na pale alipoangukia Stephan, alijaribu kumnasua pale aliponasa na lile
jiwe likang’oka kumbe lilishikwa tu kwa udongo, wakaporomoka nalo mpaka pale chini.
Stephan alitoa mguno wa uchungu na kishindo kile kilimrudishia fahamu Hellen, Hellen
aliangalia huku na huku na kumgeukia Stephan
“Tuko wapi Stephan? Amata na Saringo wako wapi?” hellen aliuliza huku akionesha
kuweweseka. Stephan alimtuliza akiwa hajui nini cha kufanya zaidi kwa wakati ule
alitazama uku na huku na akagundua kuwa lile shimo lilikuwa linaendelea lakini sasa si
kwa kwenda chini bali tambarare ambapo unaweza kutembea ukiwa wima, bila kupoteza
muda alisimama na kumuinua Hellen, akiwa bado na bunduki yake mgongoni walianza
kutembea taratibu ndani ya shimo lile wakiwa hawajui wapi wanakoelekea,Hellen
alikuwa anamfuata tu akijua labda Stephan anajua chochote, waliendelea kwenda nusu
wakitembea na nusu wakikimbia ili mradi wafike wanakokwenda. Hellen alianza
kushikwa na woga aliushika mkono wa Stephan kwa nguvu zote akiwa anatweta kwa
nguvu, mara Stephan akasimama akainama na kushika magoti yake huku akitingisha
kichwa kwa masikitiko “...tumekwisha! Hellen, sijui hata tuendako”. Alichukua bunduki
yake nakufanya kama analenga kitu lakini hakuna alicholenga akafyatua binduki yake na
ukelele wa bunduki hile ulijirudia mara nyingi kabla hakujakua kimya tena, haja yake
asikie tu kama kuna mlio mwingine utakaosikika zaidi ya huo wa bunduki hiyo. Taratibu
waliendelea kutembea na kutembea mwisho walichoka na njaa iliwashika wakaketi chini
na kila mmoja alipitiwa na usingizi kwa muda wake
Safari ilikuwa ngumu kwa Amata na Saringo, chakula chao kikiwa ni matunda ya
mwituni na maji ya mtoni, waliendelea kwenda wakiwa hawajui hasa ni upande upi
ambao wanatakiwa kuelekea.
“Nahisi tunapotea !” Saringo alisimama na kusema huku kajishika kiuno
“Tufanyeje sasa! Tuendelee mbele labda tutajua la kufanya” Amata akamjibu huku
akimshika mkono akimaanisha safari iendelee. Saringo ambaye wakati huo alioneka uso
wote kusawajika kwa uchovu alijivuta kwa hatua za taratibu na kufuata kule
alikoongozwa na Amata.
“Twende mpaka tupate mahali pazuri pa kupumzika maana jioni nayo imeshakaribia”
Amata alimueleza Saringo huku wakiendelea na safari hiyo isiyo na mwisho bali yenye
hatari na misukosuko mingi. Baada ya kutembea kwa muda walifika eneo moja ambalo
liko wazi sana kama kiwanja cha mpira lakini ilikuwa ni katikati ya msitu, katika eneo
hilo kulikuwa na nyasi nzuri za kijani fupifupi lakini katikati kulikuwa na mbuyu
mkubwa sana mnene ambao juu yake aulionesha wazi kuwa kulikuwa na mibuyu
iliyoning’inia, Amata alisimama kabla ya kuingia katika uwanda ule akatafakari mawili
matatu, akamgeukia Saringo
“Umeona! Umeona mbuyu ule?” alimuuliza saringo ambaye kwa wakati huo alikuwa
kamuegemea Amata begani kwa upande wa mgongo.
“Huu ni uwanja au kitu gani?” Saringo naye alitupa swali kwa Amata,
“Hapana huu si uwanja hapa lazima kuna kitu, Stephan alitueleza kuhusu mbuyu siyo
ule?” Amata alimuuliza Saringo, kwa hamaki kubwa saringo aliutazama mbuyu ule,
kikapita kimya cha dharula. Akatikisa kichwa kwa ishara kuwa amekubaliana na Amata
“Yeah utakuwa ndio wenyewe! Alisema upo katikati ya uwanja, ndiyo nimekumbuka,
ndiyo utakuwa ni huu” saringo aliongea kwa upole sana katika hali ya kushangaa.
“Mbuyu wa Shetani!!!” Amata aliongezea kwa upole uleule
“Unasemeje Amata? Mbuyu wa Shetani?!” Saringo alimwangalia Amata usoni na
kumtupia swali lile.
“Ndiyo Saringo, ule ni mbuyu wa Shetani! Unaitwa Mbuyu Kolo... mbuyu wa maajabu,
babu yangu alinisimulia mengi sana juu ya mbuyu huu” Amata alimueleza Saringo huku
akiwekaweka manyasi vizuri kwa kukaa chini.
“Saringo!” Amata aliita taratibu na saringo alimgeukia “Bee, Amata unasemaje?” huku
akikaa katikati ya miguu ya Amata na kumlalia kimgongo kifuani.
“Ni nini mnakitafuta huku porini? Na akina Stephan?” Amata alimuuliza Saringo.
“Ni stori ndefu sana Amata, ndefu mno” Saringo akashusha pumzi ndefu na kumeza mate
kwa shida kutokana na ukavu wa midomo yake.
“Niambie tu, maana hapa tutalala ili kesho tujue cha kufanya, ila lazima tulale juu ya mti
kuepuka wanyama wakali wenye uchu na nyama tamu yenye chumvi ya Binadamu”
Amata alimueleza hayo saringo huku mikono yake akimzungushia saringo kwa mbele
kwa kuipitisha chini ya makwapa yake, alifikiri atapata upinzani kwa kitendo hicho lakini
la, Saringo aliivuta na kuikutanisha juu ya kifua chake kisha akainamisha kichwa kwa
nyuma na kumuangalia Amata kwa juu “nakupenda Amata!” alimwambia huku
akitabasamu, AmataAmata! Tukimaliza safari yetu tutakuwa matajiri sana, tunakwenda Solondo kuchukua
sanduku kubwa na ndani ya sanduku hilo kuna mali nyingi sana, dhahabu, almasi, yaspi,
lulu za aina mbalimbali, mawe ya thamani tofauti”. Saringo alimwambia Amata, Amata
alimkazia macho saringo
“Nani aliyekwambia Saringo?! Solondo ni msitu wa kifo, msitu unaokuwa hai na kumeza
kila aingiyae...”Amata alieleza lakini saringo alimkatisha “Hapana amata, hizo ni hadithi
za kale, si za kuamini, wazee wetu walitusimulia ili tuogope kabisa kuingia ndani ya
msitu huu lakini ukweli ni kuwa ndani ya msitu huu wajerumani wamehifadhi vitu vingi
sana na babu wa baba yangu alikuwa askari wao amekuja sana huku kuleta vitu
walivyokuwa wakivichimba huku na huko katika nchi yetu! Watu wengi waliuawa na
wajerumani ndio na hawakurudi tena vijijini mwao ndio maana hizo hadithi zenu
zikawepo” saringo aliongea kwa jazba
“...hadithi zenu !!! hadithi zenu!!!” Amata alijiwazia moyoni akijaribu kulinganisha
asemayo Saringo. Amata akashusha pumzi akibaki na maswali mengi kichwani akatoa
pera akaanza kutafuna huku akichezesha kichwa chake kama mtu anayefuatisha muziki
fulani. Wakiwa katika hali ya ukimya sana kila mtu alizama katika mawazo yake ambayo
hakuna mwingine aliyeyajua
“Dunia imekuharibu umesahau mila na desturi za nyumbani” aliropoka Amata
kumwambia Saringo, Saringo alihamaki kwa kauli ya Amata na kumtazama usoni sasa
sio kwa sura ile legevu bali yenye jazba na uchungu
“Unasemaje Amata?!.. wewe unaendekeza ujinga na upumbavu wa kijijini! Hujui hata
dunia upande wa pili inaendeleaje, lazima maisha yabadilike, mimi naishi mjini naelewa
lakini wewe umezaliwa na kukulia huku porini utajua nini, fuata nnayokwambia” saringo
alifoka.
“ Huwezi kuniamrisha kufuata unayonambia wewe ni mwanamke tu, kama mimi
nimekulia huku mshamba wa kizamani kwa nini mlinitafuata katika safari yenu hii isiyo
na miguu wala kichwa, na usomi wenu na maendeleo mliyonayo mngefika wapi?
Stephan yuko wapi , helen yuko wapi? Mbona wamepotea bila kujua, na we bado zamu
yako. Lazima udumishe mila na desturi, asili itabaki kuwa asili tu!” Amata alifoka pia.
“Asili itabaki kuwa asili tu” Maneno haya yalimchoma sana Saringo na yalimrudia mara
kwa mara. Saringo akanyanyuka na kusoge pembeni, akaketi na kuikunja miguu yake
kuelekea kidevuni huku akiwa kaizungushia mikono yake aliinama na kulia kwa
vikwifukwifu.
Giza liliufunika msitu taratibu, sauti za ndege na mbweha zilisikika huku na huko, macho
ya Amata yalikuwa yanapambana na usingizi uliokuwa unayasumbua huku wadudu nao
wakifurahia kuona kiumbe hiko katika makazi yao, hakuona njia nyingine zaidi ya
kutafuna matunda yake aliyoyahifadhi vyema katika mkoba suruali yake ile ya
kimagereza, huku akitumia nguvu nyingi kujaribu kuangazaangaza kuona kama kuna
hatari yoyote inayowakabili, alimwangalia Saringo na kugundua kuwa tayari alikuwa
amelala ‘wanawake bwana!’ alijisemea moyoni huku akitikisa kichwa chake kuonesha
kukata tamaa.
“We mbona unalala kibwege hivyo? Unafikiri uko kwenu hapa!” alimuamsha Saringo
kwa kumtikisa na kumwambia maneno hayo, saringo alinyanyua kichwa na kumtazama
Amata kwa sura yenye mikunjo ya usingizi na uchovu. Amata alitabasamu na
kukumbuka maneno aliyoambiwa na baba yake ‘ukitaka kuchagua mchumba mtazame
anapoamka’ hapo alihakikisha baada ya kuona sura ya Saringo alipotoka katika kipande akapotezea kimtindomtindo.