RIWAYA: Msitu wa Solindo

RIWAYA: Msitu wa Solindo

MSITU WA SOLONDO

Mtunzi Richard Mwambe

Sehemu 4



Solondo Solondo
Msitu wa Solondo ni msitu mkubwa wenye miti mingi na wanyama wakali, ndani
yake wanaishi watu wa jamii mbalimbali wenye mila tofauti za kizamani. Watu wengi
waliuogopa msitu huo kutokana na kile kilichosemwa kuwa kuna miujiza mingi, uchawi
na hatari za kila aina pia waliamini kuwa majini na mashetani hutokea katika msitu huo.
Msitu huo ambao wakoloni wa kijerumani na kiingereza walihifadhi mali nyingi sana
uliachwa katika hali hiyo hakuna hata aliyediriki kuingia baada ya kusikia kuwa wapo
waliojaribu kwenda huko hawakurudi wengine waliliwa nyama na kupotelea huko. Kwa
hiyo kila mtu aliogopa hata kuzungumzia. Matambiko na ibada za kijadi zilifanyika
katika msitu huo, katikati ya msitu huo kulikuwa na jiwe kubwa sana jeusi ambalo kwa
kuliona tu linatisha na inasemekana lilikuwa linaongea, hapo ndipo walipotolea sadaka ya
damu jamii walioishi ndani ya msitu huo. Katika jiwe hilo kulikuwa na pango kubwa
ambalo ndani yake kulikuwa na mapango madogomadogo mengi, jamii mojawapo
iliyokuwa inaishi katika msitu huo ambayo iliitwa ‘Gorino’ , gorino kwa lugha yao
ilimaanisha ‘mla watu’ walikuwa wanawakamata watu wanaoingia ndani ya msitu huo na
kuwaficha katika pango hilo ambalo wao waliamini lilikuwa ndio nyumba ya Mungu wao
na kila walipotaka kutoa sadaka walichukuwa mmoja wa watu hao na kutoa sadaka ya
damu, waliwakata vichwa na kuwatoa kafara, nyama iliyobaki ililiwa na vichwa
vilining’inizwa kama mapambo ya eneo hilo hii ilikuwa ni sherehe kubwa sana ngoma
zilipigwa na walicheza, hakuruhusiwa mwanamke kusogea hapo kwani waliamini
mwanamke atamkasirisha mungu wao. Lakini eneo hili ambalo wakoloni walilitumia
kama hifadhi ya mali zao lilikuwa ni lasiri sana kiasi kwamba hata wakazi wa huko na
pembezoni hawakujua ukweli huo, madini mbalimbali yaliyohifadhiwa pangoni humo
miaka ya elfu moja mia nane hamna aliyeyagusa kwa kutokujua, Msitu huo ulibaki katka
hali niyo watu weupe wengi walijaribu kuingia kwa kuwa walijua ni nini kipo huko lakini
nao waliishia uko huko.
Amata alirudiwa na fahamu, akiwa pale chini bado alitazama juu na kuona watu watatu
kati yao alimtambua Golam ambaye alichuchumaa jirani yake pembeni yake kulikuwa na
mwanaume mwingine mwenye asili ya kizungu ambaye hakumjua alimuona mwanamke
mwingine naye alikuwa na asili ya kizungu, Amata alizidi kuchanganyikiwa kwani
hakuwajua hao wote ni akina nani, ghafla alipata mshtuko ambao ulimfanya anyanyuke
ghafla na kushikwa na mshangao kwa kumuona huyu aliyesimama mbele yake sio
mwingine ni Saringo. Huyu alimtambua bila kificho kwani kati ya wote huyo ndiye
aliyemfahamu kwanza, Amata aliwatazama wote mmoja baada ya mwingine ila alimkazia macho sana Saringo ambaye bado alikuwa hamuelewi uhusiano wake na
matukio yote haya.
“Amata, kaa chini tuongee kidogo...” Saringo alimuomba Amata. Amata akaketi na
wengine wote wakafanya hivyo. Wakiwa wamezunguka moto uliokuwa unawake hapo
alfajiri hiyo ili kuidhibiti baridi kali iliyowanyanyasa, kando yao miti mirefu na mikubwa
iliwazunguka, mto mkuwa wa maji mengi yaendayo kasi ulipita eneo hilo, kelele za
ndege wakubwa zilisikika.
“Hawa unaowaona ni rafiki zangu, huyu anaitwa Bw. Stephan Van Leuwen kutoka
Poland na huyu ni rafiki yake kutoka German anaitwa Bi. Hellen Schurman wote ni
wakufunzi katika chuo kikuu cha Heidelberg huko Ujerumani, ni wataalamu wa mambo
ya kale. Huyu mwengine unamfahamu Golam, huyu ni binamu yangu mtoto wa mjomba
wangu, na mimi naitwa Saringo mjukuu wa mzee Koloto.” Saringo alitoa utambulisho
huo, kisha akageukia upande wa pili
“Huyu anaitwa Amata!” alimtambulisha kwa kifupi
“Amata Ga Imba, au mate ya Simba” Golam aliongezea na wote wakatabasamu
Amata bado alimkazia macho binti huyu anayeitwa Saringo ambaye alionekana
mkakamavu akiwa ndani ya jinsi iliyomkaa vizuri na fulana yake nyekundu ambayo kwa
nje aliifunika na kishati cha buluu angavu ambacho hakufunga vifungo ila alifunga fundo
kwa chini, buti kubwa nzuri ya kijeshi aliyoitupia mguuni mwake haikuwa ya kawaida.
Amata bado alikuwa hajaelewa vizuri kinachondelea hapo alipomtazama yule mzungu
ambaye kichwani mwake alivaa kofia kubwa kama ile ya Marlboro akiwa anavuta kiko
yake, mgongoni akiwa na begi la kijeshi na mkononi akiwa na bunduki aina ya ‘rifle’, na
rafiki yake wa kike mwenye macho makali daima litafuna jojo akiwa kavaa jinsi ya kaki
na shati zito pia la kaki, alionekana mtaratibu na mpole kiunoni mwake alikuwa na
bastola mbili kushoto na kulia. Amata aliogopa sana kwakuwa kwanza alizoea kuwaona
wazungu makanisani tu na wakiwa wamevaa makanzu, alizoea kuona bunduki za
kuwindia tu kama gobole ambalo hata yeye aliachiwa na marehemu baba yake. Alikuwa
na mawazo mengi yaliyokuwa yakipita kichwani mwake.
“Tuko hapa kwa nia moja tu, tunakwenda ndani ya msitu wa Solondo, sisi watano, na
wewe tuliona unatufaa, mimi ndiye nilikutafuta kwa gharama kubwa” Saringo
alimuambia Amata. Amata akaendelea kumsikiliza kwa makini, Saringo akaendelea
“Nilikuja kijijini kwenu kumsalimia shoga yangu Chausiku ambaye unamfahamu sana,
nikiwa pale ule ugonvi uliokuhusisha wewe niliuona na nilivutiwa kwa jinsi ulivyompa
mkong’oto yule bwege. Nikafuatilia mwisho wake kuona, nilipojua kuwa umekamatwa
na uko polisi nikaja kukutembelea nilikuja tu kukutia hasira na si kingine lakini nilipanga
wewe ufungwe nikiwa na lengo moja kuwa kule gerezani utakutana na binamu yangu
Golam na kweli ikawa hivyo, Golam nilimpa kazi muda mrefu ya kutafuta mfungwa
mkakamavu, mpiganaji, asiyeogopa kitu na ulivyofungwa wewe nikamwambia Golam
akuchunguze, siku chache tu akanipa taarifa nzuri ya kuwa ulimpiga hata mtu ambaye
wao wote wanamuogopa, ndio hapo tukasuka mpango wa kukutorosha wewe na Golam,
na mpango huo tuliusuka mimi na hawa wazungu kwa kuwa sisi tulikuwa na ramani ya
gereza lile, njia zote za siri ambazo wenyewe wakoloni walizitumia kuwakimbia maadui
pindi wanapovamiwa.” Saringo akakohoa kidogo na kuendelea
“Babu yangu alifanya kazi kama askari wa mkoloni na kituo chake kilikuwa hapo
gerezani, wakati huo ikiwa ngome ya mjerumani kabla ya kuchukuliwa na waingereza, yeye ndiye alibaki na hii ramani, yeye pamoja na wenzake ndio walikuwa wanaenda
Solondo kuhifadhi vitu vingi vya wajerumani, alinipa siri hii miaka mingi sana mpaka
sasa nilikuwa nimeitunza, baba yangu aliniambia siri hii pia, na kabla ya kufa kwake,
babu alifuatwa na watu wengi sana waliodhani kuwa yeye alikuwa anajua zaidi na
amefika huko katika pango la msitu wa Solondo. Kabla hajafa alinipa mkoba wake
mchafumchafu nilipoufungua ndani ndio niliona makaratasi ya kizamani na maandishi ya
ajabu ajabu siyaelewi, nilihifadhi karatasi zile vizuri, na nilipokwenda masomoni Ulaya
ndipo nilikutana na hawa rafiki zangu Mr Stephan akiwa ni mkufunzi wangu, nilipojua
vizuri kijerumani ndio nilipojua maana na siri nzito iliyomo katika makabrasha yale, ndio
hapo tulipopanga kikosi kazi kuukabili msitu huu wa Solondo hadi tuone mwisho,
tukaona wewe pia unafaa kuwepo katika kikosi kazi hiki”.
Amata alibaki ameduwaa ‘Msitu wa Solondo!’ alijiwazia aliona kama yuko katika ndoto
labda ataamka lakini haikuwa hivyo.
“Saringo!” Amata aliita na kuweka pozi kabla hajaendelea kuongea “unaujua msitu wa
Solondo au umeusikia tu kama ulivyosema?”
“Sijawahi kuingia msituni ila sasa tumeamua kwenda” Saringo alimueleza Amata
“Msitu wa Solondo sio wa kuuchezea, tutakufa sote hakika, kuna mashetani na viumbe
vya ajabu, kwa nini tuyakatishe maisha yetu tukiwa bado vijana? Kuna nini kule cha
maana? Acheni upumbavu wenu. Golam, ndio hii safari uliyotaka twende?” Amata
alimuuliza Golam.
“Amata! Hii ndiyo safari, usiogope zile ni hadithi tu, wazee hawakupenda twende huko
lakini ni msitu tu wa kawaida. Ujue kila kona sasa unatafutwa mfungwa uliyetoroka
utajificha wapi? Twende Solondo” Golam alijibu na kutoa tabasamu lake la kuvutia
ambalo daima humfanya Amata kucheka.
“Hao wazungu wanaweza kutembea kwa miguu? Maana ni safari ya siku kama saba hadi
tufike.” Amata aliuliza kwa wasiwasi
“Wataweza ndio maana wamekuja.” Saringo alijibu
Amata akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameridhika, akanyayuka akaingia kwenye
vichaka vya karibu akatokomea huko. Saringo, Golam na wenzao walibaki kumsubiri
bila mafanikio.
Walibaki kujadiliana tu nini cha kufanya kwa kuwa hawakujua Amata kaenda wapi na
kwa nini. Wakiwa katika butwa hilo mara walisikia kelele za mnyama mwenye hasira
kutokea porini, wakiwa bado hawapo vizuri mnyama aina ya Ngiri alikatiza kati kati yao
kwa kasi ya ajabu, Bw Stephan alipigwa kikumbo na kudondoka vibaya kwenye mawe
bunduki ikianguka upande mwingine, wengine walikimbia kila mtu upande wake wakiwa
wamechanganyana hawaelewi kilichotokea. Bw Stephan aliumia sehemu ya mkono
alikuwa akivuja damu. Amata akasimama mbele yao
“Nauliza tena! Nyi mnaweza kuingia Msitu wa Solondo? Huyo ni ngiri tu mmekimbiana
hivyo wengine na bunduki zenu mmeshindwa kujipanga kumshambulia, sijui kama
tutarudi mi nina wasiwasi.” Amata aliwaeleza huku akitweta.
“Amata acha ujinga!” Saringo aling’aka
“Sio ujinga mimi nilienda porini kumkurupusha huyo mnyama ili niwapime uwezo wa
kukabiliana na hatari za ghafla, maana huko msituni kuna wanyama wakali, na isitoshe
kuna mashetani ambayo hata uyaoni kwa macho we utahisi unatandikwa bakora tu! Sasa
itakuwaje?” Amata aliwauliza kwa ukaliHaya na tuanze safari mengine tutayaona uko huko!” Saringo aliwaambia wengine.
Safari ya kuingia Msitu wa Solondo ikaanza, Golam akiwa na jisu kubwa kiunoni mwake
aliongoza msafara akifuatiwa na Bw. Stephan na bunduki yake kubwa, Saringo akiwa na
begi lake la kijeshi mgongoni alionesha kutembea mwendo wa kikakamavu haswa,
Bi.Hellen mkimya asiye na maneno mengi aliendelea kuchapa mwendo na bastola zake
kiunoni alionekana amejiandaa haswa katika safari ile ngumu. Walipita katikati ya msitu
ni ndege na wadudu ndio waliokuwa wanawasindikiza, Amata akiwa na uta wake
mgongoni alikuwa wa mwisho katika msafara huo ambao ulikuwa ukiongozwa na Golan
hakukuwa na anayeongea kwa wakati wote huo, walikuwa wakifuata kajia kadogo
kanakoelekea milimani, ilionekana kuwa Golam alikuwa mzoefu wa eneo hilo kwa kiasi
fulani ukiacha Saringo ambaye alikua na karatasi kubwa tu la khaki ambalo ndani yake
kulikuwa na michoro mingi ya ajabu na isiyoeleweka. Amata akiwa hana wasiwasi
nyuma ya wote alivuta hatua uku akiwa na mgagi wake mdomoni, baada ya mwendo
mrefu wa kama masaa matatu hivi walifika mtoni ambako ilibidi wavuke kwenda
ng’ambo ya upande wa pili, maji ya mto yalikuwa yanakwenda kwa mwendo wa wastani,
maji haya yaliyochanganyika na udongo yalikuwa na rangi kama chai ya maziwa.
Wote walisimama kando ya mto huo wakiyaangalia maji kwa makini
“Inabidi tuvuke!” Saringo aliwambia wenzake. Wote wakatazamana na kuanza kujiandaa
kwa kuvuka hakuna aliyejua kina cha mto huo wala hatari yoyote iliyopo hapo, hakuna
aliyeonekana kuogopa bali kila mtu alionesha ujasiri, Amata alionekana kasimama tu
kana kwamba hakuwa mmoja wao katika hilo.
“Kuna kamba? Inabidi mmoja aogelee mpaka ng’ambo akafunge hiyo kamba kwenye mti
ili wengine iwe rahisi kuvuka” Amata alitoa rai. Na kila mmoja kukubaliana na wazo
hilo. Stephan akatoa kamba ndefu ya kutosha Amata akajitolea kuivusha kamba hiyo.
Akaichukua na kujifunga kiunoni tayari kwa kuvuka, aliyaangalia yale maji kwanza kisha
akachukua podo na uta wake na kuuweka mgongoni tayari kwa kuvuka
“Naomba mnilinde” Amata aliwaambia wenzake na kujitoma ndani ya maji aliogelea
kwa ustadi sana kukatisha mto huo, maji yalikuwa magumu kwake katika kuvuka.
Alikotoka wote walikuwa kimya kumuangalia Amata jinsi anavyoyakata maji japo si kwa
ustadi sana wakiwa bado katika kumwangalia mara walimuona Amata akizama kabla
hawajajiweka vizuri waliona mkia wa mamba mkubwa ukitokeza juu ya maji
“Mamba!!!” Golam alipiga ukelele. Amata alibanwa mguu na mamba alijitahidi
kujinasua lakini mamba yule alimzamisha tena, aliipomuibua mara ya pili alichomoa
mshale mmoja kutoka katika podo lake na kumchoma mamba yule jichoni, Mamba
alimuachia Amata na akajigeuza chali Amata kwa ustadi mkubwa alimchoma tena eneo
la kifua mamba yule kisha akajaribu kuogelea kwa kujihami, mamba yule akajinyayua
juu Bwana Stephan kwa ustadi mkubwa alimlenga na kumpiga risasi mbili eneo la tumbo
mamba yule alijibwaga majini... mfu!. Bw Stephan akashusha bunduki yake na kushusha
pumzi ndefu, Amata alifika ng’ambo na kuifunga kamba ile mtini kisa kuwapa ishara
wengine kuvuka, mmoja baada ya mwingine walivuka na hatimaye wote walifanikiwa
kuvuka. Bi Helen aliuangalia mguu wa Amata lakini haukupata majeraha makubwa
alipohakikisha kuwa anaweza kusonga mbele basi safari ikaendelea. Giza lilianza
kuunyemelea msitu
“Hapa tunaweza kulala” Amata alilisisitiza wakakoka moto na kupumzika. Kila mtu
akiwa amejilaza kwa mang’amung’amu. Saringo alilala jirani kabisa na Amata, Hellen akiwa jirani na Stephan, Golam alikuwa mbali kidogo kakaa kaegemea mti peke yake.
Usiku mnene ulifika msitu wote ulitulia, moto uliendelea kuwaka polepole, Golam
alinyanyukla pale alipo na kuja kwa wenzake
“Amata!” akamuamsha Amata kwa upole Amata akaamka, Golam akamuonesha ishara
ya mkono kuangalia upande wa pili, Amata aliona wasichana wawili kwenye kamfereji
wakiwa kama walivyozaliwa, weupe, warembo wana nywele ndefu. Wakiwa
wanatazamana macho na wasichana wale, mara wale wasichana wakaanza kuwaita kwa
ishara ya mkono, Golam alichanganyikiwa akiwa kasimama wima mwili wake
ukionekana wenye hitaji baada ya kukaa gerezani miaka sita bila kuona hata utupu wa
mwanamke alivutiwa na wasichana wale hata kusahau kila kitu na kutamani kwenda.
Amata aliwaangalia kwa makini, akili ikamrudia ghafla ‘msituni hapa wasichana hawa
wametokea wapi?’.
“Golaaammmm” Amata aliita kwa nguvu, ukelele uliowaamsha wengine, Golam
aliendelea kuelekea kwa wale wasichana huku akianza kuvua nguo zake, Golam
aliwafikia wale wasichana nao wakamdaka na kuanza kufanya mapenzi, kelele za
mahaba zilisikika kwa nguvu hata zikageuka kuwa kelele za kutisha za wanyama wa
ajabu lakini pale walipokuwepo hapakuonekana mtu tena.
Amata alibaki kaweka mikono yake kichwani huku akitokwa na machozi, Saringo
Alishindwa kujizuia kulia kwa sauti na uchungu Hellen alimsaidia kumnyamazisha na
kumpa moyo, Stephan alibakia akiangalia kwa mbali japo mkononi mwake alikuwa na
bunduki yake kubwa lakini haikuweza kufanya chochote kwani pale walikutana na
ulimwengu mwingine.
Upepo ulivuma taratibu usiku ule na moto uliendelea kuwaka, wakiwa wameuzunguka
moto huo kila mmoja akiwa kimya akipanga na kupangua yaliyo kichwani mwake
“Msitu umemmeza...” Amata alisema kwa sauti ya upole
“One down, four to go!” Hellen aliongeza huku akirushia vijiti katika moto.
Milio ya bundi na wanyama watawalao usiku vilisikika kutoka ndani kabisa ya msitu huo
“Masikini Golam!” alisikitika Saringo, Amata akamsogeza karibu na kumbana ubavuni
kwake akimpa maneno ya faraja. Hellen aliinuwa mkono wake wa kushoto na kusoma
saa yake iliyokuwa bado inajizungusha kuonesha wakati unavyokwenda, ilitimu saa kumi
na nusu alfajiri, akavuta begi lake na kutoa kijiguduluia kidogo na kutengeneza kahawa
ambayo wote walikunywa na kuchangamka upya.
Alfajiri hiyo ilikuwa tulivu, kibaridi kilipuliza kwa upole, wote wanne walianza safari ya
Solondo kwa siku ya pili,
“Sasa tuwe makini zaidi maana tunazidi kuingia ndani ya msitu wa Solondo na
tunakabiliwa na mauzauza mengi” Amata aliwasisitizia wenzake huku wakiendelea
kukatisha pori lile nene, walikokuwa wakienda wote hawakujui isipokua tu kadiri ya
maelekezo ya mchoro wa kale ambao mara nyingi Stephan na Saringo waliusoma
uliwaelekeza upande Fulani na sasa uliwaekeza kuutafuta mbuyu mkubwa ambao upo
huko ndani ya msitu na kwamba kutoka mbuyu huo ndio hasa atapata maelekezo sahihi
ya wapi waelekee. Waliendelea mbele huku wakitumia panga kukata manyasi marefu
yaliyofanya njia hiyo kuwa ngumu kupita. Amata aliyekuwa mbele alitumia ujuzi wake
wote kukata manyasi hayo ambayo kana kwamba yaliwasihi wasiendelee na safari yao
ngumu. Wakiwa katia mwendo wa tabu sana dhidi ya nyasi ndefu na vichaka vya kutisha, miba mikali iliyowachoma na kuwakwangua kila upande wa miili yao lakini hawakukata
tama hata kidogo, mara wakasikia mvumo kama wa wadudu wengi warukao, Amata
alipoinua macho kutazama juu aliona mzinga mkubwa wa nyuki na wengi
wakirandaranda huku na huko, Amata akawapa ishara wenzake kuonesha wawe watulivu
dhidi ya nyuki hao wenye hasira. Helen alionekana kuchoka sana akiwa kamuegemea
Stephan begani huku wakiendelea na safari yao
“Tupumzike kidogo” Stephan aliomba kwa kutumia Kiswahili chake cha kubabaisha, jua
lilikuwa ni kali mno wakaketi chini ya mti mkubwa na kupumzika wakinywa maji na
mikate waliyobeba.
“Amata, inaonekana safari za msituni unazijua sana eee!?” Saringo alimuuliza Amata
“Niliopokuwa na marehemu baba yangu tulikuwa tukienda kuwinda mara nyingi na yeye
ndiye alinifundisha lugha na tabia ya msitu” Amata akajibu huku akiendelea kula
mabungo aliyoyachuma porini.
“Lugha na tabia ya msitu! Ni vitu gani hivyo?” Saringo aliuliza kwa mshangao, akasogea
karibu na Amata kana kwamba alitaka kujua vizuri juu ya maneno hayo.
“Msitu huongea Saringo, na una tabia pia kama wewe ulivyo!” Amata alijibu
“Msitu una mambo mengi sana, hatari kubwa zipo, vyakula vingi vinapatikana na pia
wanyama wa kuliwa na kula binadamu wapo” akamtazama Saringo aliyeonekena
kuvutiwa na habari hiyo
“Pia msitu hukwambia juu ya hatari ijayo na ya namna gani, baba yangu alinifundisha
haya yote kwa kuwa yeye kalelewa msituni robo tatu ya maisha yake” Amata alimalizia
kusema.
“Ina maana wewe umeshawahi kuja huku Solondo?”Hellen alimtupia swali Amata
“Hapana, ni mara yangu ya kwanza kuja ndani kabisa ya msitu huu, na baba yangu
aliniambia nisije kujaribu kuingia maana msitu huu unaaminiwa unakula watu, sikuwahi
kuelewa kauli ile lakini sasa nimeijua maana yake!” Amata alimjibu Hellen
“Kwa vipi umeijua hiyo kauli?” Stephan alidakia
“Golam! Golam amemezwa na msitu” alijibu na kutikisa kichwa kuonesha masikitiko
yake, kisha akaendelea
“Tunakokwenda hatukujui lakini hatari kubwa iko mbele yetu, kwa kuwa tumeamua
tuendelee, ila tusishangae tutakapopoteana huko mbele” Amata alimalizia kauli yake na
kumtolea tabasamu Hellen, akageuka upande wa pili kwa kuwa daima hakupenda
kumwangalia Amata usoni maana tangu alipomuaona mara ya kwanza kule mtoni mara
baada ya kutoroka gerezani alijikuta moyo wake ukimpenda ghafla kijana huyu, fukara
asiye na dira ya maisha lakini mzuri wa uso na siha ya kiuanaume zaidi ya hapo kwa
ujasiri mkubwa alionao wa kupambana na hatari na kujitolea mhanga, hilo ni swala
ambalo Hellen lilizidi kuongeza mapenzi kwa Amata tatizo tu ni kuwa pale alikuwa na
rafiki yake Stephan hivyo hakuthubutu kabisa kuonesha hali hiyo, na mara nyingi
Saringo alipokuwa jirani na Amata, Hellen alisumbuka sana moyoni.
Stephan aliinuka pale alipoketi na kuchukua kimkoba chake kidogo ambacho ndani yake
kulikuwa na kibuyu kidogo akaenda karibu na kijito kidogo umbali wa kutupa jiwe, kijito
kile kilichosongwa na mitete mingi kilikuwa na maji machache yakitembea kwa taratibu
sana. Alipofika pale alichota maji na kujaza kibuyu chake, kisha akaanza kutoa nguo
zake ili apate kujimwagia maji. Amata akiwa kwenye maongezi na Saringo na hellen
mara Amata akanyamaza ghafla na kutazama kwenye mitete ile akamuonesha ishara
saringo ya kumuomba uta wake, amata aliupokea na kujiweka vyema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom