Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Mbwa wa geti

Sehemu ya kumi


Kulikuwa na foleni ya malori mengi yaliohitaji kupima uzito pale na na hivyo watu kadhaa walikuwa wapo chini wakifanya biashara zao,zedi akawatazama watu wale na kisha akatumia kioo cha upande wa dereva kuona waliko wenyeji wake na jambo la ajabu kabisa aliona dereva akiteta jambo na askari maalumu wanaokuwa wanalinda vituo vile,Zedi hakuwa mjinga.


Dereva yule alirudi haraka kwenye gari yake baada ya kuwa watu madereva wengine walikuwa wanapiga honi wakitaka asogeze gari lake.

Alimanusura ashindwe kuiondoa ile gari baada ya kuona mgeni wake hayumo ndani ya gari.

Wahka ukamjaa akawa anasogeza gari huku akiangalia upande wa vioo kushoto na kulia pengine ataona hata nguo ya Zedi.

Utingo wake alirudi nae kwa lugha ya kitaita akauliza alipo mgeni wao,hakupata jibu la maana zaidi ya kuchanganywa tu na majibu ya dereva wake.

Askari aliekuwa anapewa mchongo wa kumkamata Zedi nae akawa amefika huku akiwa ameongozana na askari wengine waliokuwa eneo lile .

Isuzu ile ilipaki pembeni mwa kituo kile baada ya kumaliza kukaguliwa huku dereva na utingo wakiwa hawajui waseme nini mbele ya askari wale waliokuwa na wao wamepiga simu makao makuu ili waongezewe nguvu eneo lile ili wamkamate gaidi kutoka kundi la alshabaab aliesadikika kushiriki kulipua westgate.

Wakiwa wanahaha kuulizia uelekeo alioonekana Zedi akipita mara difenda ya askari wapatao kumi na tano iliingia kwa fujo ndani ya kituo kile na hapo madereva na matingo walipata kuisoma namba,mizigo ya magari yao ilikaguliwa hovyo huku maswali yakiwa ni wapi wameona mtu yule hatari alipoelekea na hakuna aliejibu maana kila mtu alikuwa bize na mambo yake wakati zedi aliposhuka na kujichanganya na wamachinga kisha akatokomea upande wa pili wa barabara.

Zedi alikuwa anatembea kwa kufuata njia ya watembea kwa miguu iliokuwa mbali kidogo na barabara huku wazo lake likiwa ni namna gani ataweza kufika Nairobi salama.

Alivipita vimtaa kadhaa na kisha akaanza kuingia mjini sasa na huko akakutana na mapya mengine

Kila ukuta,kila nguzo ya umeme ilikuwa na sura yake ilionekana kwenye machapisho yaliokuwa yamepambwa kwa maneno kadhaa .

Zedi aliyapuuza na sasa alikuwa ameiacha hiyo njia na alikuwa anapita kufauata reli na tayari giza lilianza kushika hatamu.

Lengo lake alitaka awahi kuvuka stesheni ama kituo kikuu cha treni kisha aingie katikati ya Nairobi kwa kuivuka daraja ya Ahi River

Ni wakati akikaribia kitua cha treni cha Nairobi Railway alipata kuona barabara kadhaa zikiwa zimewekwa kizuizi huku kila gari likakaguliwa na baadhi ya raia waliokuwa wakitembea kwa mguu .

Akapiga hesabu alizozijua yeye ili aweze kuvuka barabara bila kutiliwa shaka hasa aliamini mavazi yake yametangazwa kwa kila askari,mara kwa mbali akasikia treni ikipiga honi kuashiria inaingia jijini Nairobi.

Behewa kadhaa zilimpita na yeye hakuwa na na ujanja zaidi ya kufanya awezavyo kudandia behewa moja wapo na kuingia ndani na hapo akafanikiwa kuingia ndani ya jiji la Nairobi kwa kupitia kitua cha treni na alipokwisha kushuka akaongoza njia na kutoka pale kituoni kisha akafuata barabara ya Nkrumah na kuingia kulia huko akaifuata barabara ya lusula kisha akakunja kushoto na kuingia kwenye nyumba za shirika la nyumba la kenya ndani ya Kaviba streat na hapo akaanza kukagua namba za nyumba lengo likiwa ni kukifikia nyumba namba 150 aliokuwa ameelekezwa na mateka mwenzie ndani ya ngome ya Kabah.

Akili yake tu ndo ilihisi yule mzee alitaka kumwambia kitu cha muhimu ama pengine alihitaji kumwelekeza jambo lenye kuendana na mkasa ule ambao hakujua aupe jina gani.

Aliambaa na giza lile huku macho yake yakijaribu kuzipitia namba za nyumba zilizokuwa eneo lile na hatimae akawa ameifikia nyumba namba 149 ni wakati huo ambapo aliona harakati flani zikiendelea kwenye nyumba iliofuata ambayo aliamini ni nyumba alioihitaji.

Nyumba ile ilikuwa na gorofa moja kwenda juu na wakati alipokuwa akisogea aliona taa za vyumba vya juu zikiwaka lakini gafla tu aliona zikizimwa hadi taa za nje.

Jambo lile halikufanya asite kuendelea kusogea mbele,ni wakati akikaribia zaidi ndipo akapata kusikia geti likifunguliwa na haraka akaona kuna gari iliokuwa imezimwa taa ikisogea pale na kisha kuna watu wawili walikuwa wakitoka ndani ya lile geti wakiwa na wamebeba kitu mfano wa sanduku dogo lakini ilionesha lina uzito kiasi chake.

Watu wale walipokuwa wakikaribia milango ya lile gari mara mmoja simu yake iliita na akashusha chini mzigo ule na kisha akapokea akasikiliza kidogo kisha akawambia wenzie
“Jafo anatuomba tufanye haraka maana kuna kiwingu kinakuja”

Muda huo Zedi alikuwa amewasogelea zaidi hivyo kufanya aweze kuyasikia vizuri maongezi yao na akanasa jina Jafo.

Zedi aliwapita wakati wao wakizidi kufanya jitihada za kuingiza mzigo wao ndani ya gari ni wakati huo Zedi alipata kushuhudia jambo lingine tena.

Aliona kama kivuli tu kikihitokeza kizani na kwa wepesi wa hali ya juu kikaenda hewani na kilipotua kilikuwa juu ya gari ya wale watu na kisha kikashuka na kwa aina nyingine tena ya ajabu na hapo watu wale wakajikuta wakichezea kipigo na wao wakajaribu kujibu lakini hawakuweza kuzuia nguvu ya kile kivuli kilichokuwa kinashuhudiwa na Zedi kutoka kwenye pembe ya kona ya ukuta ya nyumba za upande wa pili.


Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom