Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Mbwa wa geti

Sehemu ya kumi na moja


Aliona kama kivuli tu kikihitokeza kizani na kwa wepesi wa hali ya juu kikaenda hewani na kilipotua kilikuwa juu ya gari ya wale watu na kisha kikashuka na kwa aina nyingine tena ya ajabu na hapo watu wale wakajikuta wakichezea kipigo na wao wakajaribu kujibu lakini hawakuweza kuzuia nguvu ya kile kivuli kilichokuwa kinashuhudiwa na Zedi kutoka kwenye pembe ya kona ya ukuta ya nyumba za upande wa pili.

Kivuli kile kilichokuwa kimepambwa na barakoa nyeusi kilipiga mbinja na muda mfupi tu kuna gari ilikuja na kwa kasi ikitokea upande wa pili wa nyumba ile namba 150,gari ile ilikuwa ni nyeupe na ilikuwa na namba za usajili K369DLD, na ilipofika haraka wakateremka watu wanne wakiwa wamevaa suti nyeusi na kisha wakateta kidogo na kuchukua kile kisanduku kutoka kwa wale jamaa ambao walikuwa hoi hawajiwezi kwa kipigo kutoka kwa mtu mwenye barakoa nyeusi,kisha wakapanda gari lao na kuondoka eneo lile kwa kasi.

Zedi alitulia kuona kama kulikuwa hakuna mtu mwingine atakae sogea pale ilipokuwa gari nyeusi ambayo aliamini wamiliki wake wamekufa ama wamezimia.

Alipoona kumetulia akaanza kupiga hatua taratibu ili kuifikia gari ile.

Akiwa kabakiza hatua chache tu kuifikia gari ile mara ukasikika mlio wa injini kutekenywa na punde ikawaka na kutimka eneo lile,Zedi akajaribu kuiwahi aone kama atafanikiwa kuwaona waliomo,ikamzidi kasi hivyo akasimama na kupiga hesabau zingine tena.

Dakika tano baadae zilimkuta Zedi akiingia ndani ya nyumba namba 105 ambayo hakubahatika kumjua mmliki wake kwa jina ila alihisi ni yule mzee aliempa maagizo ya kuifikia nyumba ile.

Alitembea kwa tahadhari kuingia ndani zaidi huku akiwa hana hakika na usalama wake hadi muda huo.

Aliufuata mlango wa kuingia ndani ya nyumba ile ambao nao ulikuwa wazi na alipokwisha kuingia haraka akanyata na kujibanza pembeni kidogo ya mlango na kutulia ili kujipa nafasi ya kunasa mjongeo wa kitu chochote ndani ya giza la pale sebleni.

Zikapita zaidi ya dakika kumi bila kusikia chochote na hapo akafanya kunyata tena kuyafikia masofa yaliokuwa yamebebeshwa kuonesha kuna kitu kilikuwa kinatafutwa hapo ndani,alipoyafikia tena akasimama na kusikiliza kidogo huku hesabu zake zikiwa ni kupata japo hata kiberiti ili apate kuona chochote chenye kuweza kumsaidia,aliogopa kuwasha taa za pale ndani maana hakujua lolote kuhusu ile nyumba.

Akazidi kutembea ndani ya sebule ile na punde masikio yake yakanasa sauti ya mdondoko wa kitu ndani ya nyumba ile nae haraka akachumpa na kujibanza nyuma ya kabati iliokuwa ipo karibu na ngazi za kuelekea vyumba vya juu.

Mwanga hafifu kidogo ulitoka kwenye penlight ya mtu aliengia mle ndani na alionekana mwenye haraka na Kama alikuwa anatafuta kitu alichokuwa amekiangusha mle ndani maana alionekana kupekua zaidi chini ya kwenye zulia.

Zedi alimwona kwa kila hatua aliopiga mtu yule na hata alipookota kitu pale chini macho ya Zedi yalimwona pia na akili ya Zedi ikamhitaji mtu yule.

Alitoka alipo kwa kasi na kumpita mtu yule kisha akasimama nyuma yake,mtu yule alisikia akipitwa na kitu karibu yake akasimama wima na akataka kugeuka hapo akakutana na ngumi nzito iliomfanya apepesuke kurudi nyuma na ile kurunzi ya kijasusi ikaanguka mbali kidogo.

Mtu yule nae hakutaka kuwa mzembe haraka akarusha makonde mfululizo na kumpa shida Zedi namna ya kujikinga na hiyo ndio nafasi alioitaka mtu yule kwa wepesi wa karatasi akajirusha nje kupitia mlango uliokuwa wazi na Zedi alipokuwa amepata kusimama vyema akaruka kumwahi mtu yule lakini alichelewa aliishia kuona mlango wa geti ukijifunga kumaanisha kuna mtu kaupita.

Zedi haraka akageuka kurudi ndani na kama mwendawazimua akaipitia kurunzi ile na kuelekea kwenye Kabati alilokuwa amejibanza na hapo haraka akapekuwa kwenye milango ya kabati lile na punde akatoka na kadi mbili za benk akazitia mfukoni na haraka akatoka nje na kutokomea gizani.
*****

Nusu saa badae ilimkuta Zedi akiwa amesimama mbele ya mashine ya kutolea pesa kwenye Bank ya backlays ndani ya mtaa wa Namore.

Aliingiza nywila kama alivyokuwa ameambiwa na mzee Matare na alilifahamu hilo jina kwa sababu ndilo lilikuwa juu ya kadi ile ya Bank.

Akatoa kiasi cha ksh 72000 na kukitia mfukoni na kisha akachukua kadi nyingine tena (visa) akajaribu kutoa pesa lakini hapo akakutana na manaeno yalioonesha akaunti ile imefungwa,

Itaendelea

Operation jicho la paka inaenda kuanza kwenye group leo usiku huku Jicho la kuwadi ikianza kesho

Jiunge nami kwa garama ndogo tu
Whatsapp 0658564341
Text 0758573660

Asalaam kudo
 
Mbwa wa geti

Sehemu ya kumi na mbili


Akatoa kiasi cha ksh 72000 na kukitia mfukoni na kisha akachukua kadi nyingine tena (visa) akajaribu kutoa pesa lakini hapo akakutana na manaeno yalioonesha akaunti ile imefungwa,

Kwanini ifungwe wakati ina pesa na mtumiaji hayupo,hapo akapiga akili mara mbili na kugundua kuna tatizo,haraka akatoka ndani ya kibanda kile cha kutolea pesa kilichokuwa pembeni tu ya mlango wa kuingilia ndani ya bank ile na ulikuwa umefungwa kwa sababu ilikuwa ni usiku.

Akatoka huku akijaribu kuwaza ni wapi atapata duka anunue nguo ili abadili muonekano wa mavazi hasa baada ta kugundua kila askari ameambiwa kuhusu mavazi yake.

Alietembea kwa muda kidogo na kufika hadi eneo la kupaki daladala maarufu kama matatu kwenye mji wa Nairobi,kisha akaita konda na kuuliza yalipo maduka ya nguo mitaa hiyo,akaelekezwa kisha akaelekea huko.
****

Usiku mnene ulimkuta Zedi akiwa amerudi kwenye nyumba ya mzee Matare na kisha akaikagua na kuhakikisha Hakuna mtu au kitu akaamua kwenda kujilaza huku mto aliolalia akiufunga kwa kamba ndefu ilioenda hadi kwenye kitasa cha mlango hivyo kama mtu angeliingia kamba ingelivuta mto na yeye kuamka,alipohakikisha mtego wake akaamua kupumzika ndani ya nyumba alioamini maadui wanaisakama kila muda ila ndo komando yule mzoefu akamua kuweka makazi yake.

Hatari ilioje!!!!

******

Kumekuchwa Dodoma

Lakini kuchwa huku kulikuwa na aina nyingi za mapambazuko.

Ndani ya hotel ya perugina,kulikuwa na tukio la ajabu kidogo na tukio hili lilitokea wakati ambao hakuna alietarajia litatokea ndani ya usiku uliopita.

Askari zaidi ya wawili walikuwa wanagonga vyumba vya wageni waliolala ndani ya Hotel ile na miongoni mwa vyumba vilivyofikiwa na askari wale ni chumba kilichokuwa kimekaliwa na watu wawili waliokuwa wapo kwenye tafakuri maana walikuwa na taarifa ya mauaji yale na hapo walikuwa wanajaribu kupata jibu la nani hasa aliekuwa anavujisha siri kutoka ndani ya idara yao,idara nyeti kabisa.

Ziga na Mina walikuwa wanatazamana wakati waliposikia mlango unagongwa kwa nguvu huku wakisikia sauti za askari wasiofuata misingi ya kazi yao wakikoroma ndani nyuma ya mlango.

Taratibu Mina akasimama na kuuendea mlango,akaufungua na hapo akakutana na tusi zito kutoka kwa askari wale waliokuwa wameshika bunduki zao mikononi.

Ziga akapandwa na gadhabu lakini alipomtizama mpenzi wake akaona ishara ya kumtuliza nae akatii.

Askari wale walikagua kila pahali ndani ya chumba kile na kisha wakauliza maswali kadhaa kuhusu tukio lililotokea usiku ndani ya hotel ile na maswali yote yakajibiwa na Mina aliekuwa anajua nini maana ya upuuzi wa askari wa Tanzania.

Askari wale wakatoka ndani ya chumba kile huku wakiwaacha wapenzi wale wakiwa wanarudi tena kujadili kuhusu kilichotokea.

“waliwezaje kujua kama watu kutoka makao makuu watafikia hapa?! Lilikuwa swali la Ziga kwenda kwa Mina.

“sijui kwa kweli,maana imetokea haraka mno tena wakati ambao hata sisi hatukujua kama wenzetu wapo tayari ndani ya Dodoma” alijibu Mina.

Wakaangaliana bila kusemeshana na Kama aliekumbuka kitu Ziga akanyanyua simu yake na kumpigia Chief.

“nakusikia” ilikoroma sauti upande wa pili

“Kuna kuku anakula mapandio yetu,hivyo naomba msilete tena mbegu nyingine,zilizoko zinatosha” ilikuwa ni sauti ya Ziga akiomba kwa chief kwa lugha ya mafumbo kisha akasikiliza kidogo na kukata simu na bila kusubiri akasimama na kuchukua mabegi yake na mpenzi wake na kutaka kutoka lakini Mina akawahi kumzuia

“ningojee dakika moja tu nakuja” alisema huku akiuendea mlango na kutoka nje.

Baada tu ya kutoka nje ya chumba chao,Mina akakutana na umati wa askari polisi wasiopungua kumi huku wengine wakipiga picha miili ya maiti mbili zilizokutwa ndani ya chumba kimoja.

Mina akataka kukatiza kati yao lakini askari mmoja akamfokea na kumzuia asipite

Taratibu Mina akatoa kitambulisho chake na hapo kilichofuatia ni askari yule kupiga saluti mfululizo kama kinyonga alieona chatu kwenye mti.

Mina hakumjali akasogea hadi ilipo miili ya watu wale,hakutaka kuamini ni watu kutoka kwenye kitengo chao ni watu kutoka kwenye kitengo ndani ya usalama wa Taifa (NSA) National security Agency.

Akawapekua kidogo na hapo akakutana na mchirizi mwekundu kwenye shingo zao,hiyo ikampa maana ya kuwa walinyongwa kabla ya kufa kwao,akatoa simu yake na kupiga picha sehemu kadhaa alizoona zaweza kumpa mwanga kwa aina ya mauaji yalivyofanyika.

Alirudi hadi chumbani kwao na akamkuta Ziga akiwa yupo wima na mabegi yake ikimaanisha hakuwa amekaa tangu Mina atoke mle chumbani.

“Aliefanya mauji hakuwa mmoja,yawezekana ni kikundi cha watu zaidi ya wawili na nilivyoona waliwalazimisha kusema kitu kabla hawajawaua” alisema Mina kisha akanyosha mkono na kumpa Ziga simu aliokuwa ametumia kupiga picha miili ile ya wanausalama wale waliokuwa wameuwawa.

“Walilazimishwa kusema chumba ulichopo…”alisema Ziga huku akiirudisha simu mikononi mwa Mina,hapo Mina akatoa jicho kama kumbikumbi aliebanwa na sisimizi.

“wewe umejuaje”

“Usiku wakati umelala chief alipiga simu kwako,nikaipokea,kisha akanipa maelekezo flani ambayo yalikuwa yanakulenga wewe!”

“Alisemaje!!?”

Alisema popote tulipo tunahitajika kuungana na na vijana waliokufa kutegua mtego unaotegwa hapa Dodoma,lakini kubwa ni kuwa ofisi inajua wewe na wale vijana ndo mlihitajika hapa na mlitakiwa kufikia hotel hii tuliopo”

Mina akakuna kichwa kuweka sawa fikira zake na hapo akakubaliana na Ziga ya kuwa kuna nyoka anawala visigino ndani ya idara yao na kwa hayo machache tu,waliona ugumu wa kazi maana adui anaeza kuwa amekita mizizi yake kila idara ndani ya nchi.

Mina akachukua mkoba wake na kuanza kutoka ndani ya chumba huku nyuma akifuata ziga.

Waliingia ndani ya gari yao na kabla hawajaondoka Mina akauliza

“Twaenda wapi muda huu”

Ziga akamtazama kisha akamjibu

“Sehemu salama ni nyumbani kwa Zedi”alisema hayo huku akianza kuondoa gari kwenye maegesho na kisha akaimakata barabara

“Yah wazo zuri na pia tunaeza mshawishi akatusaidia mawili matatu ndani ya huu mji” aliongezea Mina huku tayari gari yao ikiyapita magari kadhaa kwa mwendo wa kawaida.

Ila ni kwa kuwa hawakujua na laiti wangejua!!!!!!


Itaendelea



Nb: kuna wasiopenda vipande kila siku naomba tuwasiliane kuanzia kesho jioni mzigo wote utakuwa tayari PDF

0758573660 kwa garama ndogo tu

Hapa Jf tutaendelea kama kawaida hadi tamati.
Usisahau ndani ya group kuna riwaya mpya
"Operation jicho la paka"
 
Mbwa wa geti

Sehemu ya kumi na tatu


Ila ni kwa kuwa hawakujua na laiti wangejua!!!!!!

****

Burizozo alikuwa amekaa kwenye sofa akitizamana na Tausi,huku kushoto kwao kukiwa na mtoto mdogo umri wa miaka kama mitano ama sita hivi

Tausi alikuwa akimtizama Burizozo kwa chuki kubwa sana.

Tausi alitaka kusema kitu lakini alikatishwa na sauti ya mtoto aliekuwa karibu yake ,mtoto alilalama njaa ,alitaka kunyanyuka ili ampe walau chai ahsubuhi ile lakini akapata onyo kutoka kwa Burizozo

“usimpe chai ama kitu cha moto,atakufa maana ametoka kutema mzigo sasa hivi….”

Kilifuata kilio kutoka kwa Tausi,alilia kwa kuona mwanae amegeuka kuwa mbeba madawa ya kulevya.

Na hapo akamatazama tena mwanae yule na Kama ndio anamwona kwa mara ya kwanza,akaona vile mtoto amedhoofu,akamfunua shati alilokuwa amevaa na hapo akaona kovu kubwa lililokuwa tumboni kwa yule mtoto mdogo.

Tausi hakutaka kujiuliza lile kovu ni la nini,tayari alishajua hutumika kutolea tembe zinazosalia tumbobi baada ya kushindwa kutoka kwa njia ya haja .

Tausi alilia na kama mtoto mdogo lakini kilio chake hakikufika mbali wala hakikuwa na thamani zaidi kilimwamsha Kabah aliekuwa kalala juu gorofani na akashuka kwa kasi na kipensi tu na kuwakuta Tausi na mwanae wamekumbatiana,hakujali.

Kwa kasi akamfikia Tausi na kumvuta juu na haraka akamchapa makofi kama sita mfululizo na kumchana usoni kisha akamsukuma kwa nguvu na kumtupa juu ya sofa na bila huruma akanyoosha mkono ili amtandike kofi mtoto aliekuwa amesimama kando akitizama mama yake akisulubiwa,lakini konde lile halikufika likadakwa na Burizozo,

“We need him more than you think” alisema kwa lugha ya kusihi na maneno yakamwingia Kabah akagairi kutoa kipigo kwa mtoto aliefanana na Zedi kwa kila kitu.

Hasira zake bado zilikuwa kwa Tausi na akaendelea kumshushia makonde na kufanya damu zijae kwenye sura ya mwanamama yule sura ambayo ilikuwa imeanza kutota kwa utumizi wa dawa za kulevya.

Kabah alipoona roho yake imesuuzika kwa kipigo alichotoa akaanza kumburuta Tausi kuelekea kwenye chumba ambacho huwa hakifunguliwi mara kwa mara na huko akamtupia humo kama mzoga kisha akakifunga kwa nje.

Tausi alijikunyata kama mtoto mdogo huku kilio kikiwa ni kwikwi,alijuta kwa alioyafanya na alijuta kwa kumsaliti mwanaume aliempenda kuliko kitu chochote.

Mara nyingi Tausi akiwa katika hali kama ile hujituliza kwa dozi ya sindano ama mnuso wa cocaine.

Na tayari mwili ulikuwa unahitaji kupata hicho kitu,lakini hakuwa na wa kumpa ndani ya chumba kile cha giza totoro.

Matanio yalizidi uwezo,akanyanyuka,lakini hakupiga japo hatua mbili akawa yupo chini maumivu ya kipigo yalikuwa yapo kila sehemu,tena ni bora angelikuwa amepigwa na mtu kama mimi au wewe ambao hatujui hata silaha inashikwa vipi,lakini huyu alikuwa amepigwa na komando la waasi wa huko Somalia,tangu utoto hadi ujana wake anacheza na roho za watu tu.

Tausi hamu ya kuvuta unga ilimzidia,akajongea hadi kwenye mlango,akaugonga mara kadhaa na punde ukafunguliwa ila alieufungua hakuwa msemaji akafanya alichoagizwa,akamwaga maji ya baridi ndani ya chumba alichomo Tausi kisha akaufunga ule mlango na kumwacha Tausi akiwa anaelea juu ya maji ya baridi.

Kwa kiasi chake ilimsaidia kumwindolea zile hisia za uhitaji wa kuvuta unga,lakini nafuu ile haikudumu kamwe.

Tausi akawa anayapitia mateso ya kujitakia!!!
****
Ziga alikuwa anaikata kona ya nkuhungu chama na akapunguza kidogo mwendo kulingana na ukali wa kona ile.

Safari yao ilikuwa ya ukimya,haikuwa safari ya mbwembwe kama walivyokuwa wamezoea wawapo wa wili ndani ya gari.

Mbele kidogo ya mtaa wa nkuhungu vibandani Ziga alikata kulia na kupita pembeni kidogo ya ukuta wa nkuhungu sekondari kisha akasogea mwendo wa mita mia mbili na kisha akasimisha gari mbele ya geti kubwa jeusi.

Ziga akapiga honi kadhaa lakini hakuna alietoka kufungua,ikabidi Mina ashuke na kulisogelea geti lile na hapo akaona kitu kilichoamsha hisia mbalimbali ndani ya kichwa chake.

Kimuonekano tu ilionekana eneo lile halijakaliwa na watu kwa muda mrefu kidogo.

Mina akalisogelea zaidi lile geti na kujaribu kusukuma na hapo mshangao mwingine ukamvaa geti la nyumba ya Zedi lilikuwa wazi na kwa tahadhari kabisa akaingia ndani ya uzio wa geti lile nako akazidi kupigwa na butwaa.

Palionekana kutofanyiwa usafi kwa muda mrefu hali iliopelekea kuote majani marefu huku uchafu wa kila aina ukiwa umejaa pote .

Mina akazidi kujongea kuingia ndani ya nyumba ya Zedi na huko akapigwa na mshangao ambao hakuutegemea.

Ni wakati anaingia ndani ya nyumba ya Zedi,mlangoni tu akakutana na matone ya damu yalioganda na Kukauka kabisa na yalionesha ni ya muda mrefu kidogo na pia mlangoni kulionesha kumeparazwa na kitu kama risasi hivi.

Akausukuma mlango na kuingia ndani kabisa kwa mwendo wa tahadhari kabisa.

Hakuwa mgeni wa matukio na moja kwa moja akajua kabisa pale ndani palitokea ugomvi wa aina yake na wapambanaji walionesha wanaujua mchezo,Mina akabaki akishangaa na kujiuliza kulikoni kimemkuta nini Zedi.
***
Ziga akiwa ndani ya gari aliona vile Mina alivyokuwa ananyata kuingia ndani na hapo akajua kabisa huko si salama nae akataka kushuka ili aungane na Mina.

Ni wakati alipokuwa akikaribia kufungua mlango wa gari akili yake ikamtuma atazame kwenye kioo na hapo hakuwia kugundua hawapo peke yao pale,kuna macho ya watu wawili yalikuwa yanawatizama,na sio kuwatizama tu yalikua yanawatizama kwa husda.


Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom