asanteelimu2016
JF-Expert Member
- Sep 23, 2016
- 248
- 147
NA Halfani Sudy
Ilikuwa ni siku iliyoisha vizuri ndani ya Mji mdogo wa Kitalii Kilwa Masoko. Hakukuwa na taarifa yoyote kubwa ya kihalifu katika vitabu vya jeshi la Polisi ndani ya Kilwa Masoko. Ni mwaka wa tano sasa mfululizo Mji huu ulitulia.Askari walikuwa wamepumzika, habari za mauaji walikuwa wanazisikia mikoa mingine tu. Kwao kulikuwa shwari.
Ndani ya jumba moja ndani ya Mji wa Masoko kulikuwa na mtu amelala usingizi mzito. Lakini alistuka ghafla kutoka usingizini. Moyo wake uliruka sarakasi ndani ya kifua chake. Alistuka sana. Kupigiwa simu saa 9 za usiku iliashiria hali si shwari.Inspekta Nyange akaangalia kioo cha simu yake tena,namba iliyompigia ilikuwa katika mfumo wa ‘private number’,hali ya wasiwasi ikazidi kumuandama
"Halooo"
“Habari”
“Kuna mauaji!”
“Wapi?”
“Mtaa wa Lumumba,nyumba namba tano!”
Inspekta Nyange hakupata hata nafasi ya kuitikia wala kusaili zaidi. Simu ya mtu yule aliyejiita msamaria mwema ilikatika au tunaweza sema ilikatwa !
Bila kufikiria mara mbili, Inspekta Nyange alivaa nguo zake za Polisi na kuchukua silaha yake,bastola,alitoka chumbani kwake hadi ukumbini,akatoa simu yake ya kiganjani na kupiga .
“Halo ”
“Halo Inspekta ”
“Tukutane mtaa wa Lumumba nyumba namba tano kuna mauaji !, njoo na askari wenzio wanne ”
“Sawa mkuu ”
Alipofika karibu na mtaa wa Lumumba alipokewa na vilio. Vilio vya maombelezo. Ilikuwa yapata saa kumi alfajiri wakati Inspekta Nyange anawasiri eneo la tukio,lakini wingi wa watu wa eneo lile ulimshangaza sana,kulikuwa na umati mkubwa wa watu,wakilia! Wakilia kwa uchungu mkubwa sana !