Riwaya: "Mkuki wa Mapenzi" (Love Spear)

Xav Emmanuel

JF-Expert Member
Jul 12, 2018
214
315
RIWAYA: LOVE SPEAR 01

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email: xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------

UTANGULIZI;

MAPENZI
ni moja kati ya njia ambayo kila binadamu anapaswa apitie. Ni njia ambayo haina muonekano halisi ambao unajulikana. Kila mtu anaonja radha yake katika njia hii. Achana na wale wanaoyaona kuwa ni shubiri na hawa wengine wanasema mapenzi ni asali ya kujazia uhai. Kwamaana usipofanya chochote kuhusu mapenzi, unaweza kudhoofika kiuhai.

Hata mimi nimeshindwa kabisa kuyazungumzia mapenzi kwa mapana Zaidi. Kwa maana niliyopitia mimi si hayo tu nawe umepitia.. bali nawe unaweza ukawa na nyongeza au kunipa kitu kipya kabisa amabacho umekutana nacho kwenye njia hii ya Mapenzi pasi mwingine kupitia au kukiona.

ROYSON JOHNSON aliyapa mapenzi alama nyingi sana katika udanganyifu na kutoaaminika. Hatimaye anapata moja kati ya Spea ambayo inamfundisha nini maana ya Mapenzi. Anamfunza ni maana KUPENDA. Hatimaye REHMA AYOUB anakuwa Spea ya mapenzi kwa ROY. Anatoa vilivyoaribika na kudhorota na kuweka vifaa vipya kabisa.. njia hii inakuwa faida na hasara kwa pande zote mbili..

TIRIRIKA NAYO

-------------------------------

KIPANDE CHA 1;

CHUO KIKUU CHA ELIMU DAR ES SAALAM kilikuwa katika harakati zake za kila mhura wa masomo katika kuhakikisha wanakimbizana na muda kwa kumaliza kila kitu kinachohusu mtahara katika ufunzaji wa wanafunzi waalimu ambao wanatumika na wanaendelea kutumika katika Nyanja zote za elimu na taasisi duniani kote.

Pilikapilika zilikuwa moja kati ya vifungu vya sharia mama za chuo. Hakuna katiba wala kipande cha karatasi chochote ambacho kiliandika kuteseka au kusoma kupita maelezo katika chuo hiki. Sharia ya maangaiko ilipitishwa punde tu mara baada ya kupokelewa sifa za chuo kuwa kinadhalisha Uma wa waalimu ambao kwa takwimu ni bora katika utawala na ufundishaji kwa ujumla. Hivyo wanafunzi waalimu walizidi kuchilimika tu kutofuta uhalisia wa chuo hicho wa tangu na tangu.

Waliopishana katika kumbi za kusomea; walipishana. Waliopigana vikumbo kutoka na kuingia getini nao walifanya hivyo. Watu walikuwa wamezagaa kila kona ya chuo. Msururu wa wanafunzi walimu ulikuwa mkubwa mno kiasi cha wengi kukosa hata sehemu ya kukaa.

“Wazee.. njaa imekaza sana kwa upande wangu leo… mniache nipumue basi wakuu!.” Moja ya wanafunzi katika kundi alitoka nje ya mada katika mjadala na kuingiza uchosho kwa wenzake.

“Mwanangu! mi mwenyewe naona kuna wadudu wapo kando.. kwa kona hii wananibinya kinoma yani.. yani kama wanacheza Football tumboni” Mwenzake alidakia na kufanya kundi nzima kukenua meno yao. Walicheka kwa jitihada bila kuachiana nafasi. Wakajikuta wanafunika mada iliyowakusanyisha pale na wote kuikimbilia kwa hamu mada mpya ya njaa.

“Kud*d*ki..!, ko wajuba mnakazaa kuingiza madesa bila mlo?, mimi nilikuwa nawachora tu!. Hakuna nililoshika hata moja. Ukicheki mida inaruhusu kabisa kula..” Mwengine naye akajinyooshea njia kujipa faida. Wote walivamiana kwa kejeli. Walionyesha kufahamiana sana. Walikuwa jumla ya wanaume watano.

“Ohp!, afu ROY anazingua ujue. Toka afike hajaongea kabisa yani. Anatushangaa tu hapa. Haya mada yako ya njaa hiyoo imefika.. changia sasa.” Yule aliyeongea mwanzo akamgeuzia kibanzi mwenzake wa pembeni. Alikuwa naye karibu mkono wa kushoto.

“Brother! Njaa haina mwenyewe!. Kwani kuwasilisha swali si Alhamisi?.. tunakaza leoo da hahhahaha.. tutakutana bhana, kwani imebaki sehemu ndogo!.” Mwingine alimtetea Roy na kutoa ushauri uliofanya mmoja wao kufunga kitabu na kukikumbatia kifuani.

“Aaah!, semeni tu hivyo. Kikubwa kila mtu achukue pati yake hapa. Ngoma itakuwa rahisi Zaidi…”

“Poa,.. We KELVIN tutakutana Whatsapp. Tutachagua kulekule vipengele. Au sio..” alisema yule wa mwanzo na kunyanyuka pale. Alionekana mwongeaji sana.

ROY aliyekuwa kimya toka mazungumzo yanaanza, alichukua kitabu chake na kukifunua hadi katikati kama mtu anayehesabu pesa hivi. Alipofika kati alikomea hapo. Macho yake yakaangaza sehemu ya kitabu aliyofungua na kuipitia kwa macho yake.

… If you bring us all this way for nothing I shall beat sense into you…. I have told you to let her alone.i know to deal with them, said Okagbue…” alisoma na kisha kutabasamu. Alionesha maneno hayo yamemgusa vilivyo. Akakifunga kitabu hicho na kusoma jina la jarada la kitabu.

THINGS FALL APART” alihamasika sana baada ya kusoma maneno hayo ya lugha ya kiingeleza. Akayasoma tena kuhakiki kama atakuwa alipatia lakini mwishowe alijikuta anaachia tena tabasamu. Roy alikuwa anaongea na nafsi yake.

“It’s true!!. all things falling apart..” alijisema kimoyomoyo na kutabasamu tena. Alimalizia kusoma na jina la mwandishi wa kitabu hicho. Bado alikuwa anakitazama tu kitabu. Sio kwamba hakuwai kukiona kitabu hicho mwanzo, hapana. Ila ugeni wa kitu ambacho kipo moyoni kilimfanya kila kitu anachokiona kiwe kipya tena. Alikuwa anatabasamu tu mwenyewe akigeuza geuza kitabu hicho kilichoandikwa na Mbaba nguli wa Fasihi Afrika; Chinua Achebe.

“We taila, mbona unajichekesha chekesha sana!..” Kelvin alikuwa tayari kumkabili Roy ambaye alionekana kuwa na furaha ya aibu. Kwani mwanzo hakuionesha kabisa. Ila baada ya wenzao kutawanyika, Roy aliamua kujichekesha chekesha ovyo.

Roy akatazamana na rafiki yake huyo bila kupepesa macho. Roy alikuwa kama mtu ambaye amenyweshwa pombe inayonoga kwa masaa matatu ya nyuma, alikuwa na hali tofauti siku hiyo kwani baada ya kumjibu rafiki yake huyo alianza tena kutabasamu. Alikuwa kama kindele; yaani mtu aliyechukuliwa msukule na kurudishwa tena uraiani.

“Bro! usiniaminishe kama lile dili limetiki!!.. akii nitakupa heshima yako. Sio kazi rahisi kwa yule mtoto..” Kelvin alianza kutiwa shaka na mpango ambao waliapiana hapo mwanzo. Alihama upande na kumfuata Roy upande aliokaa.

“Enhe.. niambie kabla Tumbo halijatoboka hapa.. nina ubao kish*nzi sana yani..” alidadavua kutaka kujua kile walichoahidiana.

“Wooooooohps!... we unaongelea nini kwani!” Roy alimtoa maana mwenzake kwa kutoelewa kitu ambacho alikuwa anamuuliza.

“Mtoto Scola!... Umbwa wewe!. Unajichekesha tu hapa.. vipi ulimaliza jana hilehile au?” sasa alikuwa muwazi Kelvin.

“Hahahahaha!, we taila sana ujue!. Scola ndo kidudu gani. Bila shaka nilimaliza jana sa tatu tu. Sa tano nikamrudisha kwake. Hana jipya yule… hana tofauti na wengine. Hana makali, hana show, hana mbwembwe, hana lolote. Umbwa wewe… hahhahaha ulimsifia bure tu. We fala macho sio kigezo cha kuwa mzuri kitandani! Hahahahaha!..” alicheka Roy na kumwacha Kelven kwenye hali ya sintofahamu.

“Kwahiyo umepiga?” aliuliza tena kwa kutoamini.

“Ee, nimepiga na kukata.. hahahaha nilikuwa sina salio.. haha!” alijibu Roy na kucheka kwa sauti. Alisahau kabisa kama yupo chuo.

“Daah, we sio poa asee!. Ee kituo kinachofuata ni wapi sasa!”aliuliza Kelvin kumaanisha baada ya Scola nani anafuata.

“Aah!, Ebu achana na hawa watotowatoto.. nina kitu kipya.. bro… kipya!” aliongea Roy na sasa hakuonesha kucheka. Alikuwa muwazi katika sura yake na kuonesha kuwa alikuwa makini na anachokisema.

“Ee!” aliitika kwa utayari Kelvin na kumwacha Roy kuendelea.

“Bro.. naomba niwe serious kwa hili!.. sina utani kabisa.. hapa unaponiona viungo vyangu vya mwili vyote vimeseparate!. Vimetawanyika yani..” Aliongea Roy

“Vimetawanyika!,!” alishaangaa Kelvin na macho yake yakatua hadi kwenye sehemu ya uume wa Roy ambao umefichwa na kitambaa cha kaki. Alikuwa anahakikisha ni kiungo gani kilichotawanyika kwa Roy. Akaganda kutazama hapo.

“We kweli F*l*..!, Umbwa wewe, hahahaha..” alimshika kichwa Kelvin na kumuinua hadi kutazamana. Wote wakacheka. Walikuwa wanajuana kwa vilemba vyao.

“Brother!, nimetoka lecture leo ahsubui ile ya 1 hadi 2 kasoro 5 ile. Huwezi amini ile korido ya kwenda Room B... ule upande wa Wajawazito.. kuna mtoto nimemuona.. I Swear!. (naapa) sijawai kumwona mtu huyo katu… Bro nimeshindwa hata kupokea salamu yake. Nimejikuta namtazama tu hadi anapotea!.. aki! Kelv. DUCE hii sijawai penda kabisa… ila sasa naona kabisa ndio muda wangu huu!” aliongea kwa msisitizo.

“Nyooo!!!! wewe huyo? Hahhaha. We umbwa unaharibu tu watoto wa wenzako. Upende wapi wewe!!” alimshushua jamaake bila kumwonea aibu. Roy alitazama chini na kuwa mpole. Akainuka.

“Bro. ninachokuambia nakiamini kutoka moyoni. Nimempenda yule dada kwa asilimia zote za hapa duniani. Na nina hakika nitampata… kila gharama nitatumia.. nitampata tu, na nina hakika kuwa… yani Bro nakuhakikishia!. Nikimpata tu basi naacha umalaya. Natulia kaka aki tena” Roy leo alikuwa makini sana kwa aliyokuwa anaongea, hakuwa na utani hata kidogo. Hali hiyo ilimshitua kabisa rafiki yake na kushindwa kumwamini moja kwa moja.

“Sina hakika na ahadi yako. We mtafuta huyo mdada.. mchafue.. mwache.. mimi nishakuzoea mbona!” Bado Kelvin alikuwa mbishi kukubali. Roy alimtazama tu rafiki yake huyo na kutomjibu chochote. Alikusanya kila kilichochake na kuachana na rafiki yake huyo. Kila mtu akaendelea na majukumu yake..

INAENDELEA…..
 

Attachments

  • 1LOVE SPEAR.jpg
    1LOVE SPEAR.jpg
    22.9 KB · Views: 17
RIWAYA: LOVE SPEAR 02

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email: xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------

ILIPOISHIA..

“Bro. ninachokuambia nakiamini kutoka moyoni. Nimempenda yule dada kwa asilimia zote za hapa duniani. Na nina hakika nitampata… kila gharama nitatumia.. nitampata tu, na nina hakika kuwa… yani Bro nakuhakikishia!. Nikimpata tu basi naacha umalaya. Natulia kaka aki tena” Roy leo alikuwa makini sana kwa aliyokuwa anaongea hakuwa na utani hata kidogo. Hali hiyo ilimshitua kabisa rafiki yake na kushindwa kumwamini moja kwa moja.

“Sina hakika na ahadi yako. We mtafute.. mchafue.. mwache.. mimi nishakuzoea mbona!” Bado Kelvin alikuwa mbishi kukubali. Roy alimtazama tu rafiki yake huyo na kutomjibu chochote. Alikusanya kila kilichochake na kuachana na rafiki yake huyo.. kila mtu akaendelea na majukumu yake..

KIPANDE CHA 2;

--- UPANDE WA PILI ---

Sauti ya kiwambo cha chini ya miguu ilisikika tokea pande moja ya darasa na kuelekea sehemu nyingine. Bado kwato za miguu ya mtu huyu ziliendelea kulisumbua sakafu kwa hatua ndogondogo azimegazo. Alizisungua sakafu zilizo pigwa deki mda mchache na kuziachia nakshinakshi zake zilizoanguka kutoka usoni.

Alikuwa nimwanamke ambaye hakuwa na umbo la kuliridhisha wanaume wengi. Umbo alilonalo liliendelea kumtosha katika kuhimili mwendo wake wa madaha. Mkoba wake mdogo wa kamba ndefu ulining’inia bega la kushoto na kumwachia uwazi wa kuzikumbata daftari zake vizuri kifuani. Hakuwa na haraka ya kwenda sehemu yoyote ile. Alitembea tu kutoka darasa ya Room B na kuelekeza barabara inayopita jengo la TPC kuvuka vikalio (Vimbweta) vya Peasant.

JUMA REHMA AYOUB Ndio jina lililomfikisha chuoni hapo.. jina hilo lilirembwa vyema katika kifua chake likipeperusha kitambulisho cha chuo kutoka kushoto hadi kulia. Kulia hadi kushoto. Labda upepo huo ulisababishwa na kamba ya kitambulisho; kilichoandikwa ufupi wa maneno ya chuo kikuu cha Dar es Salaam; “UDSM-Student”. Bado alining’inia na kitambulisho chake hadi karibu na barabara ya kutokea Hostel za Hall III. Akaganda kidogo, akiangaza sauti inayomuita.

“Rey!,.. hapaa!!!.. Rey!!!...” aligeuka na kukutana na shangwe la mkono likimpungia kwa kasi ya kimbunga. Akacheka kidogo na kujibu wito huo kwa mkono wa kulia huku mwingine ukiendelea kubana vikorokoro vyake kifuani. Alikuwa mcheshi wa kutumia lugha ya ishara.

“SIMBA!..” akaita kwa mbwembwe akitazama kundi la wanawake sita limezunguka kimbweta.

“SOPHIA R!... niambia AYUBU!” aliyepayuka kumwita mwanzo, alijibu kama ilivyopaswa. Walitambuana kwa majina.

“Kichaa wangu Sophy, mbona unapayuka hivyo.. mtu yupo kibaha unamwita kwa mdomo Mbezi?” alijibu Rey na kugawa salamu kwa wengine aliowakuta pale.

“Mbezi ipi hiyo unayozungumzia wewe?” alijibu kwa mshangao huku akisimamia ufupi wake awe mrefu kuliko wote kwenye kimbweta. Lakini ilishindikana, kwani kuna warefu zaidi yake licha ya hao warefu walikuwa wamekaa.

“Ajenda gani imewakusanya hapa mapema yote hii?” aliuliza Rey akiweka sawa vitu vyake kwenye mkoba na kubaki na Simu tu mkononi.

“Unaijua mapema wewe?, umbea tu shoga!, tumejisikia kupashana habari za weekend!..” alijibu mwingine mkono ukishika shavu na kutumbua macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.

“Mwana.. wa Idd!..” aliita kwa kumjua zaidi.

“Ndio haswa jina langu.. deshdesh mchumba angu.. Upo hapo!!” alimshushua Rey.

“Na wewe!. Mchumba hiyo kwio!” Sophia alijitutumua naye kumuumbua mwana. Wote wakacheka sana hata wale walijiita watulivu wa kundi.

“Jamani.. naomba niulize kitu hapo!.. ivi..” aliishia njiani Rey na kisha kuangaza kila mtu sehemu hile. Aliacha kuongea na kushuhudia utulivu katika kundi. Roho ilimsuta kwa jambo alilotaka kuuliza. Aliona atavamiwa kwa michambo na wenzake. Akawa kimya Rey.

“Ulizaaa na wewe khaa!” Mwanaid alionesha uharaka wa kutaka kujua Rey anataka kuuliza nini. Wote wakamuunga mkono Mwana na kumshinikiza Rey aseme kile alichotaka kusema.

“Ah!, nimeghairiiiii nimegundua nyie wote watoto hapa na hamna vifua vya kutunza jambo hilo!” aliwakebehi.

“Nyook*!, hatuna vifua kwahiyo haya maindi et!” mwingine alijibu akijitunisha kifua chake ambacho hakina hata dalili za kuchomoza chochote.

“Sio hivyo Mariamuu!. Ni jambo nyeti sana.. na!… kwani nishawai kuwaficha kitu jamani? Ee, mda ukifika nitawauliza”.

“Huyu nae!. Eboo… sema uko” Sophia nae alikazia palepale alipoachia MAriamu.

“Ok Fine.. ah! Kuna mkaka hivi anasoma Literature bila shaka. Sijawai kumwona kabla hapa chuoni mwaka wangu wa pili huu. Ah sijui hata anaitwa nani yani da!” aliongea kana kwamba anajiongelesha mwenyewe. Wote pale wakaduwaa wasijue mwenzao ameuliza au alikuwa anatoa taarifa.

“I, mean.. kuna kaka mmoja hivi bhana, nyie hamjui aaahg!, mrefu hivi. Maji ya kunde. Anaswaga akitembea hivi… yaaani aaaagh!..” alieleza kwa hisia na mwendo wa harakaharaka.

“Nani sasa?, Peter!?” mwingine ambaye hakuongea mwanzo aliropoka.

“Yupi!”

“Lt CR (Class Representative)”

“No!, kwani huyo simjui?”

“Sa nani?, Dauce!”

“Hapana!... agh!” alighazibika na kushika mashavu yake kwa mikono yake yote miwili. Huyu dada kwa kweli hakuna alichokosa. Dompozi nyepesi zinaonekana mashavuni bila kutumia nguvu. Kuna muda huwezi jua kuwa amekasilika au anacheka.

“Au Willy?....” Mwingine naye akaotea.

“Kwani kafanyaje.. usije tunapata shida kumtafuta hapa watu sita afu mwishowe useme ulimwazima kalamu yako. Tutakupiga kufa!” Sophia alikuwa na hulka ya aina yake. Kwa jinsi mwili wake ulivyo uwezi kuzania kabisa kama analandana na maneno ambayo yanamtoka.

“Ok. Ok Ok!, Subirini nitampata tu hapa…” aliwasubirisha wenzake na kuzungusha kichwa chake moja kwa moja hadi vimbeta vyote vya peasant. Kulikuwa kuna watu wengi sana, alishindwa kutuliza akili.. akabaki kujigongagonga tu mashavuni mwake kwa kushindwa kueleweka.

“By the way!.. nimemuelewa sana yule kaka.. for Sure!” alimaliza Rey na kuwaacha wenzake katika butwaa na kuwafanya kucheka. Kundi nzima walicheka sana.

“Mapenziiiiii…. Mpenziiii oooh Mapenziiiii, Mapenzi ooooh yananitesa mie!.. Tuondoke bhana!” Mariamu aliimba kwa furaha na kuona mwenzake hana maana kabisa.

Aliwakusanya wengine watano na kunyanyuka pale wakiwa bado wanacheka. Wakatoweka zao na kuwaacha Sophia na Rey palepale.

“It’s real dear!. Naomba nisaidie hilo please!. Unajua nimekumbana nae wakati natoka lecture hadi mwili umesisimka!. Mashetani yalinipanda palepale na sio kawaida kabisa kutokewa na hali hii.. nifanyie mpango Sophie!” alimbembeleza rafiki yake kwa kumshika mikono amfanyie dili la kumuunganisha nae.

“Utanilipa nini?” Aliuliza Sophia huku akiwa na uso wa tabasamu. Kidogo alianza kumuelewa.

“Si wanijua mimi mpenzi!. Dili likitiki tu.. we mwenyewe utafurahi..” aliongea kwa haraka huku kichwa chake kikiendelea kukagua watu wanaopita kwenye njia ya karibu walipo.

“Sophie!, unaweza kupenda mtu Zaidi mmoja wewe….” Aliuliza na kuishia njiani na kauli yake. Chini kabisa ya vimbweta vya kontena alimwona yule mkaka anayemzungumzia.

“Yes!, Yes!!” alipiga kunga kidogo na kuelekeza mkono upande wa chini.

“Yulee!” alionesha Rey. Alishakuwa nusu kichaa.

“Nani?”

“Si huyo mkaka bhana!..”

“Yupi wa blue yule?”

“Bhanaa… huyu.. angalia karibu na Lecture Hall… na Kontena!. Pele wapo watano.. sasa wa kulia yule ameinama.” Alijitahidi kuelekeza na sasa Sophia alinyanyuka kuendana na urefu wa sehemu ambayo anaonyeshwa.

“Pale…. Kuna!, Mtitu Kelvin, kuna Willy, Kuna Nickson Ernest, Huyu nani!!... Yule RoySon Johnson… aagh! Au unamsemea Roy huyu wa kushoto huku ameshika kitabu!” aling’amua kwa udadisi Sophia bila kukosea.

Macho ya Sophia yalirudi kwa Rey na kumtazama kwa jinsi alivyo na furaha. Sophia alikaa kitako tena na kumtazama mwenzake. Alitikisa kichwa kuonesha huruma ya wazi kabisa. Alimuurumia mwenzake.

“Hiyo ni mada ndefu sana!. Ebo! Nyanyuka haraka twende mbele nitakuelezea njiani!” Sophia alimtaka mwenzake kunyanyuka. Wakanyanyuka kwa pomoja huku bado macho ya Rey yakiganda kwa Roy!

Mapenzi Ukichaa, ukipenda umeugua!

Rey hakuonyesha kabisa kama anadalili ya kumfumbia macho Roy, mwili wake ulionesha wazi kuhitaji joto la mwanaume. Alihisi anaugua kidonda ambacho kinamuhitaji Roy kama upepo wa kufukizia nzi wanaoendelea kumwozesha kidonda chake. Alihisi anadoa kwa kukosa mtu wa muhimu kama Roy! Sasa alimtambua kwa jina. Barabara nzima aliita Roy! Usije akasahau tena Jina ilo.

INAENDELEA…..
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 03

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email: xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



“Hiyo ni mada ndefu sana!. Ebo!. Nyanyuka haraka twende mbele nitakuelezea njiani!” Sophia alimtaka mwenzake kunyanyuka. Wakanyanyuka kwa pomoja huku bado macho ya Rey yakiganda kwa Roy!.



Mapenzi Ukichaa, ukipenda umeugua!.

Rey hakuonyesha kabisa kama anadalili ya kumfumbia macho Roy, mwili wake ulionesha wazi kuhitaji joto la mwanaume. Alihisi anaugua kidonda ambacho kinamuhitaji Roy kama upepo wa kufukuzia nzi wanaoendelea kumwozesha kidonda chake. Alihisi anadoa kwa kukosa mtu wa muhimu kama Roy!. Sasa alimtambua kwa jina. Barabara nzima aliita Roy!!. Usije akasahau tena Jina ilo….



KIPANDE CHA 3;

REHMA AYOUB, Mzaliwa halisi wa mji wa Tanga!, aliyatumikia maisha yake katika mkoa huo kwa asilimia zaidi ya 70 huku asilimia 20 akiishi mkoa wa Pwani katika kutumikia elimu yake ya A-Level na asilimia 10 zikibaki zinambakisha Dar es Salaam, hapa alipelekwa na Chuo. Alikuwa na miaka miwili sasa tokea afike Ubongo.



Alikuwa mzuri aliyependa uzuri wake. Hakupenda kuona kasoro yoyote ile inachafua uso wake. Kila muda hujidibika rangi tofauti kwenye kope za macho yake pamoja na lipsi za midomo yake. Katika uzuri wake zidisha kila kitu ila usiweke kitu kinachoitwa ‘kujichubua!” hapo utakuwa umemkosea mtoto wa watu!. Wanasema ‘Mwenye Miti mingi; ndio mjenzi huyo’ Alijua kujiweka katika muonekano mzuri zaidi kila siku.



Achana na wanaume ambao wanagonga hodi kila siku mwilini mwake; hakika alikuwa mwanamke mgumu sana na mvivu kufungua mlango kwa kila mwaume. Aliwatesa kwa majibu ya kuwakubalia na kutowapa chochote!. Alikuwa mtu sugu katika kuvua au kuvuliwa nguo zake za ndani. Lililopendeza zaidi alizishika vyema nguzo za kiislamu; hakutaka zilegee wala kuanguka.



Bado waliendelea kuzikata mbuga Sophia akiwa na Rey wake. Roho ya Sophia ilikuwa inajiongelesha yenyewe bila kutokwa na sauti. Miguu yake ndio alikariri njia ya kupita na sio akili. Akili ilikuwa kwenye mapenzi mapya ya rafiki yake Rey na Roy.

Alichanganyikiwa nini aseme na nini asiseme kwa rafiki yake huyo. Alipofika katika kona moja kuchepukia ALMAGATHA Sophia alimvuta Rey karibu na sehemu ya kivuli.



“Upo serious My!, kwamba kweli unampenda Roy?!” Aliuliza majibu Sophy na kuangalia jibu la ishara kutoka kwa Rey.



Alitikisa tu kichwa kisha kumkokota tena na kwa mwendo wa haraka wakachepukia katika Hostel ya kibinafsi ambayo wameweka mizigo yao hapo kwa muda.



Ndani ya Chumba chao kulikuwa na wasichana wengine wawili. Achana na huyu anaemwita ‘Twin’ kwa kigezo cha kuishi naye maisha mengi kuliko rafiki mwingine. Pia kulikuwa na Glory ambaye alikuwa mreufu wa kimo. Mweusi. Mwembamba kidogo, huyu alikuwa yu uchi karibia mwili mzima. Sio mbaya kwa joto la Dar Es Salaam.. hakuridhishwa na upepo wa feni. Glory alikuwa amevua nguo kabisa na kijiegesha kitandani.



“Dear sipo upande wako kabisa juu ya huyo mwanaume… nakupenda sana Rey ndio maana nakuambia hivyo!..” aliongea Sophy bila kumwangalia yoyote mle ndani. Aliweka mkoba wake kitanda cha juu, kisha kupanda na yeye mwenyewe.



Alipokaa vyema sasa alitumia macho yake kuongea na Rey ambaye alikuwa haelewi kitu zaidi ya kuweka mkono wake tu kwenye kingo moja ya kitanda. Macho yakiwa juu kwa Sophia.



“Najua unielewi… ila…! (alisita na kuendelea) Eti Glory unamjua RJ?” alipayuka sauti ya maulizo kwa mwenzake.



“RJ?, sii niii… Rey and Johari?” Swaumu (Twin) alidakia swali juujuu kama mpira wa kichwa. Aliutulizia mgongoni na kuutelemshia mguuni. aliropoka.



“Ummuh!!... Rey and Johari tena? (akikodoa macho yote kwa Glory), kwani we Sophy unamzungumzia mtu au kampuni?” Glory nae Aliuliza kuonesha hakuelewa.



“Unamjua Roy wa DUCE!” Aliuliza tena Sophia; sasa alieleweka vyema zaidi.



“Mh!, kumbe huyo!” Swaumu alisonya kwa mbali na kuendelea kuchana nywele zake.



“Ehe, uyo kaka jamani!. Namjua.. vizuri tu!. Tena…” Hakumaliza Glory akachunga mdomo wake.



“Ah rafiki yangu!, Ebu njo juu tuongea kwa kina” Sophia alimpandisha Rey na wote wakawa juu sasa. Maongezi yakaanza.



“Rey! huyo RoySon sio my mzuri kabisa!. Hakika nakuambia!!.. nina ushahidi mimi” aliongea Sophia.



“Mhh!, kwema huko au kuna mwingine kanasa Sophy?” Glory nae alilopokwa na maneno machafu. Swaumu aliyekuwa anachana nywele zake akawa sasa bize kusikiliza.



“Tafuta nwingine dear!, Yule sio mtu mzuri kabisa.. atakupa homa yule!” aliongea Sophy na Rey.



“Makubwa!!” Glory alishaelewa kuwa mwenzao, Rey; ameshamezwa na jinamizi la mahaba la Roy, na sasa lilikuwa linapelekesha mputa.



“Sitakuja kumsahau Royson Johnson… hakika yule sio binadamu!” Glory akadakia tena na kumwacha Rey katika sitofahamu.



“Umesikia? Hata Glory nae ndio huyo amebaki na kumbukumbu chafu juu ya huyo mtu unaesema unampenda!. Roy ni mchafuzi sana!… sijui kwani anajivunia nini!. Akili?, uzuri au? Ukimwona kwa mbali kama malaika hivi; jamani jamani… usithubutu kumsogelea… ni shetani yule kaka. Labda kwa leasure!!” alijibu Sophy.



“Ni kweli kama unampenda kwa hamu tu ya mapenzi ah.. unaenda tu. Amekuwa msaada mkubwa sana kwa wanawake wengi wenye hamu ya muda mfupi.. ila kama unamalengo yako ya mbali na yeye…. Ohooo mfute kabisa yule kaka. Namba chafu ile. Na yeye hana wasiwasi wala shida ya mwanamke… kuna kitu anajivuna yule!!. Mara kila siku ananamba mpya. Daah!” Glory akamwagika. Rey akabaki kimya.



“Rey nisikufiche mpenzi. Mimi ndio nilikuwa kati ya wanawake wa kwanzakwanza kutoka na Roy. I swear nilimpenda kuliko baba yangu kwa kipindi kile.. na sikujua ni kwanini!... Loh! alinigalagaza kwa siku mbili mfurulizo!. Roy alinifanyisha mapenzi yote lakini baada ya kuachana nae siku ya pili na mawasiliano yalikata!. No calls!, no Sms!. Nilimtafuta ila alichonijibu!..” Sophy aliachia hapo na kuanza kuangusha chozi bila kilio. Rey alisisimka mno.



“Hmmm, hadi wewe Sophy” kumbe tupo wengi! Haaahshi!” Glory nae akaweka chuku yake.



“Roy ni moja kati ya wanaume ambao wanatafutwa sana na Mungu… lazima afe mapema yule ili akajibu dhambi hii anayoendelea kuitenda… sijui kama kuna mwanamke hapa DUCE amemuacha kweli yule mkaka… in shot yupo vizuri.. anaswaga!. Anaweza kukutongoza ukakubali…. Akakufanyiaaa weee siku kucha then akakumwaga; afu akaja tena akakupiga soundi na ukakubali… yani yule sijui anatumia dawa za kuwapumbaza wanawake??.. (Glory, aliiacha simu yake chaji na kunyanyuka na nguo yake ya ndani tu.., akakaa sawa na kuendelea).



Nina miezi mi nne sasa toka niachane nae yule mwanaume, hakika aliniteka… labda kwa sababu nilimpenda mimi, ila yeye hakunipenda..



Nilikutana nae discussion jioni.. Niliipenda style yake kwa kweli, ni mtu wa point sana.. sana yani kwa kweli alinivutia sana… usiku uleule nikapiga nae hatua tukapanga kukutana siku iliyofuata kwa kweliiiii… ooohps hakika sijawai kupata mapenzi kama yale toka nizaliwe!. Jamani kaka anajua yule.. anajua kuzitafuta shanga hata kama hujawai kuvaa.. anajua kiuno kinaanzia wapi na kinaishia wapi. Mi sidanganyi!! alinitosheleza kabisa yani.. nikasahau chuo kwa siku 3 mfurulizo.



Akaniweka logde kule kurasini!. Alilipa kila kitu… yaani kwa siku hizo tatu.. alibonyeza kila sehemu ya mwili wangu.. nikajiona nimefika vilele vyote duniani.. siku ya tatu alikaa na mimi na kuniambia misemo yote ya mababu… sikumwelewa ila nakumbuka tu aliniambia kuwa ‘haupo vizuri sana.. jitahidi kuendana na kasi ya mwanaume!. Unachoka mapema sana kabla hamu haijakata!..’ Jamani.. nililia siku hiyo kwani alipotoka hapo Logde hakufika tena...



Zaidi alinitumia tu Sms kuwa nahitajika chuo. Tena kuna Test!. Akiii tena nilipata sifuriii ule mtihani na hadi sasa nina koziweki ya saba!, yani naiona CarryOver hii hapa!. Sitamsahau yule mwanaume mimi..” alimaliza Glory na kuvuta pumzi ndefu. Ndani kukabaki kimya mno. Kila mtu akitafakari simulizi ile.



INAENDELEA….
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 04

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email: xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



Akaniweka logde kule kurasini!. Alilipa kila kitu… yaani kwa siku hizo tatu.. alibonyeza kila sehemu ya mwili wangu.. nikajiona nimefika vilele vyote duniani.. siku ya tatu alikaa na mimi na kuniambia misemo yote ya mababu… sikumwelewa ila nakumbuka tu aliniambia kuwa ‘haupo vizuri sana.. jitahidi kuendana na kasi ya mwanaume!. Unachoka mapema sana kabla hamu haijakata!’ Jamani.. nililia siku hiyo kwani alipotoka hapo hakufika tena. Zaidi alinitumia tu Sms kuwa nahitajika chuo kuna Test!. Akii nilipata sifuriii ule mtihani na hadi sasa nina koziweki ya saba!, yani naiona CarryOver hii hapa!. Sitamsahau yule mwanaume mimi..” alimaliza Glory na kuvuta pumzi ndefu. Ndani kukabaki kimya mno. Kila mtu akitafakari simulizi ile.



KIPANDE CHA 4!..

“Yaani rafiki yangu!, sikatai kwamba umependa!; Hapana. Ila umempenda kwa wakati ambao sio. Roy si mwanaume wa kuvumilika yule. Na ananyota sana yani. Ukimwangalia kwa mara moja hivi huwezi kuacha kumpenda.. anaushawishi sana. Sasa amekuwa kama tiba hivi kwa wanaweka wanaopenda mapenzi ovyo. Sijui kama anaangalia umri wala uzuri yule.. ilihali tu umemkuta yupo katika siku zake anakubutua… rafiki yangu pia Happie!. Walifanya kazi pamoja ya kundi na kazi ikabaki kwa Roy!. Ya Mungu mengi akamwita geto akachukue kazi… yaani nasikia alimpumulia tu masikioni na rafiki yangu akalegea hapohapo.. yeye mwenyewe Happie akavua nguo. Akaja kujua baada ya kumaliza matendo yote ya ndoa. Akawa chakula cha jioni kwa siku hiyo.. so No!, No Kumbwa my dear.. sikushauri” aliyasema Sophy akionesha kutetemeka kwa usiri huu aliokuwa anauficha moyoni.



“Daaah!, Sophy hivi kweli ndio yule niliokuonesha anafanya haya au umekosea kuangalia?” aliuliza Rey kwa kushindwa kuamini masikio yake maneno ya wenzake.



“Si huyu apa! (akichomoa simu kwenye chaji Glory) huyu mkaka wa watu… jambazi la mapenzi. Uwezi kumdhania yani” akapekua na kukutana na picha moja ya Roy.. ni yeye alikuwa RoySon JohnSon.



“Shhhhiiit!!!, its tru!, ni yeye!.” Alijisemea moyoni huku akifumba macho yake kumkana mbele ya toba hii ya muda mfupi. Alimuomba Mungu amuepushie mbali na ujinga ambao mwanzo ulimuingia..



Nani anasema mapenzi ujinga?!.

Rehma aliyasikiliza maneno yote kutoka kwa marafiki zake na mwishowe kujitupa kando na kitinda chake!. Akashusha kwanza pumzi kumbwa uliyombana toka apokee taarifa zilizomchanganya. Mawazo yakamburuta na kumfikisha hadi katika njozi. Alijikuta yupo katika njozi Roy!.



“Nakuhadi nakupenda hadi kufa Roy!. Wewe ni mwanaume wa maisha yangu!.. nakuamini sana.” Rey alikuwa katika maongezi na Roy. Yote yalitendeka katika njozi hiyo.



“Upo tofauti na wanawake wote niliowapitia Rey!. Nashukuru Mungu kwa kunionesha mwanamke sahihi wa maisha yangu!. Nakuhidi makubwa sana Rey!. Sipaswi kuwa mwongofu kwako..” Roy naye alitiririka na maneno ya mahaba.



Wote walionekana katika giza nzito lililosababishwa na kuzimwa na taa.. jasho liliwachuruzika mara dufu baada ya kazi nzito waliofanya punde. Rey akishikilia kanga iliyoegeshwa karibu na matiti yake, miguu yake ikigongagonga kitanda polepole kupokea mikono ya Roy ambaye naye alitiririkwa na jasho tu. Alikuwa kando ya Roy akimshika kwa mkono wake wa kuume huku kichwa cha Rey kikiwa kifuani mwa Roy.



“Mpenzi.. hakika nilikutunzia hii kwa muda mrefu sana!, mwanzo nilikuwa sikuamini Roy!. Ila sasa naona kweli unanipenda!. Niwekee ahadi yako jamani.. penzi la leo lisiwe mwisho.. liwe mwanzoo, nataka tena Mpenzi!..” Rey nae aliendelea kutiririka maneno. Hakuna wa kuwakataza. Waliamua wenyewe kuwe huru. Waliendelea kutupiana maneno pasi kukinai.



Mara ‘Paaap’ Taa ikawaka!.

“Kulikoni..” wote walikuwa macho. Kwa muda huu taa ilipowaka walizunguka kitandani kwa Rey. Wote wakitumbua macho alipolala mwanzao.



“Nyie vipi!. Mnanitisha!” alikurupuka Rey.. msobemsobe na nguo yake akajikusanya hadi kuketi kitandani.



“We Rey kumbe chizi e?” Yusra ambaye si mgeni wa tabia za wenzake alimdadisi.



“Tena sio chizi wa nchi hii!!, et oh ‘Mpenzi.. hakika nilikutunzia hii kwa muda mrefu sana!, mwanzo nilikuwa sikuamini Roy!. Ila sasa naona kweli unanipenda!.” Sophy aliiga maneno ambayo aliyasikia kutoka kwa Rey si mda mrefu.



“Ama!, Mapenzi? We mtoto unamjua vizuri Roy wewe?” Yusra aliwaka kwelikweli. Aliweza kutumia ufupi wake kutamba kwa muda ule.



Rey akawa kimya; nae alianza kugutuka kuwa alikuwa anaota ndoto!. Tena ndoto ya sauti ya ukweli. Alikuwa anaota ametoka kufanya mapenzi na Roy na sasa walipumzika kwa kuambiana mawili mitatu. Alimaanika Rey.



“We mtoto huyo Roy unaemwota amechafua kila sehemu!. Adi mimi mama yako kanipitia.. hahahahaha!” alimaliza kwa kucheka Yusra..



“Tumemwambia sisi jioni tu hapa tumetoka kuongea nae!. Lakini haya makubwa hahahha” Glory nae alicheka na wote kurudi vitandani mwao. Tayari walishashuhudia kupotea kwa rafiki yao kipenzi. Wote waliendelea kucheka chumba kizima. Yusra aliongeza maongezi na wengine kumsapoti. Baada ya kulala wakaanza kusimuliana soga.



“Hapo zamani za kale alitokea YU na Ro..” alianza kusimulia Yusra.



“Enhee!!” wengine waliitika kwa hamu ya kicheko. Maana walimjua mwanzao kwa kuyavurumisha maneno. Rey bado alikuwa anaikana ile ndoto yake aliyoiota kuhusu Roy. Aliikana kwa muda mrefu sana.



“Mara Paaaaap! YU na Ro hawa hapa Gest! Hahahahaha mara Ro anaanza kumshika shika Yu.. Yu anasogea karibu na malango anaufunga kwa fungua afu anaumeza tumboni ile funguo…”



“Hahahaha!, Enhee”



“… Basi pale Ro si hajui kama Yu amemeza funguo!. Anaamua kusapraizi kwa kumrukia!..”



“Enhee!”



“Kumbe Yu kibonge ila mwepesi bhana.. anarukiwa kwa nguvu anaanguka chini anakufa! Hahahahaha”



“Hha ha ha hahahahaha!... Enhee!”



“Na hadithi yangu imeiishia hapo!.. inatufundisha hiviiii…. Kumeza funguo ni muhimu!!!”



“Hahahahahahaha hahahahaha ahahahaha ahahhaha aaaaahgh, kwa kweli!” walicheka sana ndani mule. Hadi Rey ambaye alikuwa bize kuwaza amewazaje kuota ndoto kama ile alianza kucheka. Mwenzao Yusra alikuwa kituko kabisa. Walikaribisha kiza na kiza kiliwakaribisha wao.. usiku ukawa usiku wa manane.. hatimaye palikucha.



--- UPANDE WA I---

Majira ya jioni wakati kijua kikiendelea kubisha bisha kuondoka. Roy alikuwa kando na simu yake.. alionesha kuwa na mawazo sana hadi waliomzoea walimgundua.



Alikuwa bize kufuta kioo cha simu yake iPhone kwa kutumia dore gumba. Kichwani alikuwa anawaza anampata vipi mwanamke ambaye amemchanganya kwa siku ile.



“Ey Boi.. unamatatizo gani leo!. Alikuwa Bahame Edwadi.





“Enhe, Kaka wa Taifa!, ebu nishauri kwanza.. (akapunguza sauti). Kuna mtoto nimemwelewa.. sasa simjui jina wala namba zake sina.. ila kwa sura namjua… da naomba nishauri napataje mawasiliano nae leo hiihii.”



“Mkubwa mboni zoezi gumu ilo!. Vipi rafiki zake!” alijibu Bahame.



“Oh, No. sijapata connection hata ya rafiki zake. Ndio kwanza nimeuona leo kwenye macho yangu!.”



“Ah ingekuwa poa hapo ungewajua wenzake.. au kama ata ku wa, ah.. eh kama atakuwa Whatsap ameweka Dp yake.. ebu mcheki kwenye makundi ya chuo!.” Alitoa wazo.



“Yes Man Good Idea.. daa” Bahame akatoweka zake baada ya kutoa msaada.



“DUCE 2nd Year!” akalivamia kundi hilo na kutafuta mmoja baada ya mwingine; Hora!. Hakupata chochote. Akalivamia lingine la Literature.. akapekua hadi kufikia namba yenye Dp inayoifahamu.



Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio tayari. Alipoigusa ile picha ikatokea kama alivyohitaji.. Mtoto alikuja kama yule aliyemkuta chuo asubuhi. Kichwa kiligota kidogo ukutani nusura aumie.. lakini Hakujali.. alianza kuangaza picha na kung’ata lipsi zake za chini kwa meno ya juu. ….



INAENDELEA…
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 05

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email: xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



ILIPOISHIA…

“Yes Man Good Idea.. daa” Bahame akatoweka zake baada ya kutoa msaada.



“DUCE 2nd Year!” akalivamia kundi hilo na kutafuta mmoja baada ya mwingine; Hora!. Hakupata chochote. Akalivamia lingine la Literature.. akapekua hadi kufikia namba yenye Dp ya sura anayoikumbuka.



Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio tayari. Alipoigusa ile picha ikatokea kama alivyohitaji.. Mtoto alikuja kama yule aliyemkuta chuo asubuhi. Kichwa kiligota kidogo ukutani nusura aumie.. lakini Hakujali.. alianza kuangaza picha na kung’ata lipsi zake za chini kwa meno ya juu. ….



KIPANDE CHA 5.



“Beby!, What’ happen!. Unafurahi mwenyewe eh!” Irene, mmoja kati ya wanafunzi ambao anaishi nao hapo hostel.



Alipomwona Irene anajongea sehemu ambayo yeye yupo aliipoteza picha ile kwa kufunika simu.



“Unajua sifa ya kwanza ya binadamu ni kukubali ukweli kwa kutumia uongo!. Sijajua kama sifa hiyo ni ya kwanza au la. Nadhani umekuja muda muhafaka mno wa kunipa solution ya swali ambalo nilikuhoji jana!. Please kaa chini.” Aliomba Roy, na Irene akakaa. Akazungusha mkoba wake na kuuweka mbele kuziba tundu ndogo lililoachwa na sketi yake.



“Swali gani dear!” alipokea maongezi.



“japo nilichelewa kuingia hostel jana.. ila wewe ulichelewa zaidi yangu.! Harufu yako niliisikia sa saba za usiku? Hmmm!. Jitetee!”



“My!, nilikuwa kwa dada. Nilikupa taarifa!. Then nimetoka mapema tu sa kumi na limoja! (akitabasamu kuziba wivu wa Roy). Na.. daladala ndio tatizo lingine.. foleni pia.. aaagh!. Mbagala mbali bhaaana..” akamaliza na Tabasamu Irene. Akanyanyuka bila kusubiri maneno ya Roy; akamsogea na kumpiga busu sehemu yake ya paji la uso na kisha akaongoza ndani.



“Just for fanny..” alijiongelea mwenyewe kichwani Roy, akimaanisha bado anaendelea kumuinjoy tu mwenzake.



Taratibu za kuendelea kufungua moyo wake zikaendelea. Akainua simu na kuangaza tena picha ile ya mwanamke aliyempenda. Hakuikuta!. Akahamaki kwa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango!.



“Jesus!” alijisemea na kuharakisha tena katika kundi lilelile kuangaza tena kwa maana Picha ilikuwa imepotea.



Aliipata na kuangalia #Bio ya namba ile akakuta imeandikwa @~Rehma_Ayoub alitabasamu sana. Hakutaka kujisumbua kulitafuta tena jina lake. Tayari alijihakikishia mwanamke huyo anaitwa Rehema Ayoub. Akapambana kuangalia na muda wa mwisho mtu huyo kuwa ndani ya mtandao. Simu yake ilimuonesha kuwa ni jana yake ndio siku ya mwisho Rehma kuingia mtandaoni.



Mapenzi ni asili!

RoySon JohnSon kama ajiitavyo katika mihura yake yote ya masomo; ni mtoto wa kwanza na wa mwisho wa Mama Royson mwenyewe. Katu hakuwai kuonja uhondo wala utamu wa Baba toka asaidie kuletwa duniani. Mapenzi yake yote ni baina ya Mama tu!.



Hakutokea katika familia yenye pesa sana wala wenye shida sana. Mama yake alikuwa mtafutaji!. Alimfundisha jinsi ya kuwapenda wanawake hadi mwisho. Alimtupia pesa nyingi kila anapohitaji; ukichanganya na boom kutoka serikalini unapata utajiri mkubwa sana kwa kijana wa rika chini ya miaka ishirini na tano. Huyu ndie Roy. Mcheshi wa tabasamu na mtu mwenye swager!.



ROY aliendelea kuusubiri usingizi kitandani akiangalia ni muda gani malaika wake atatokea Online. Hadi kufikia sa tano hakuna mrejesho mwema alioupata kuwa Rehma atakuwa mtandaoni. Alijisonya mara kadhaa kwa kujiuliza vipi aanze kumtumia text au asubiri kwanza awe online ndio aanze kazi. Alijiuliza bila kuwepo na majibu. Akatumia nafasi ya kuwa peke yake chumbani humo kujiwekea ndoto nyingi juu ya mwanamke huyo.



“..Ah, Rey upo wapi Mama, siamini kama umeiba kabisa taswira ya mama yangu mzazi. Na kama hutakuwa na mahusiano na mimi ninakuhaidi nitapata taabu sana kukubali hali hii.. nimesadiki kuacha takataka zote kwa ajili yako. Ebu njoo nirekebisha na kuniambia wapi nilikuwa nakosea… au pia ukuje tu!, ukujeee japo hata kunijibu. Ulikuwa wapi mama?. Hivi ni kweli hujawai kunitia machoni kweli au… Doh! We mtoto. Hakika wewe ni paji la roho mtakatifu. Umechukua akili na utashi kwa sekunde tu!. Dadeki!” Roy alikuwa kuwaza kwa kujiuliza maswali mwenyewe na mengi kukosa majibu. Alijikuta anaamka saa tisa za usiku na kukuta ujumbe katika simu yake.



“Rey!, hatujaonana leo!” aliisoma text hiyo na kutikisa kichwa kidogo kuangalia aliyetuma!. “Reeny” alikuta ni Irene; akaisoma tena ile sms.



“Roy!, hatujaonana leo!” kwa sasa Alisoma vyema kabisa. Alianza kuchanganyikiwa kwa maana mara ya kwanza aliona ujumbe umeandikwa Rey. Na aliposoma tena alikuwa jina lake la Roy. Alianza kuchanganya matango poli na kujilisha yeye mwenyewe. Akaamua kumpigia simu Irene mda uleule na simu ilipokelewa sekunde tu.



“Dogo unasoma au?” kwa sauti ya usingizi, Roy akamuuliza Irene.



“Kusoma wapi?!, umenizoesha my!. I can’t sleep!. Sijakuona!!” alijibu kwa kubinya pua yake kama mtu anayeigiza.



“Ohp!, nimekuzoesha vibaya we mtoto!. Ebu njo mara moja!” alimwita Reeny usiku ule. Hiyo ndio nafasi ambayo Reeny alikuwa anaisubiri kwa muda sana. Hakukata simu, tayari alifika mlangoni mwa Roy.



“Kama jini!” Roy aliongea kwa sauti huku akiruka kitandani na kufungua mlango. Chumba cha Roy na Irene ni kama pua na mdomo. Ni upande wa pili tu!.



“Jana ulinikalipia sana ndio maana sijapaswa kuja kukufungulisha leo. Niliogopa my!” aliongea Irene na kuingia ndani. Alionesha kuwa mwenyeji katika chumba hicho. Akawasha taa na kuketi kando ya kitanda. Bega moja likilegea kufanya nguo ya kulalalia aliyoivaa kukosa pa kumshikilia. Ikabaki kama inaanguka hivi.



“Reeeeny my dear!” aliite Roy



“Yes! Darling!. Nambie!” alijibu.



“I know unanipenda sana mrembo!. (Roy alisogea hadi kumkalibia Reeny karibu na kitanda. Akamshika-shika mashavu yake na kisha kuendelea kuongea).



“Nimeota ndoto mbaya sana leo..! hakika nisingekuwa macho mda hu!”



“Jamani, ndoto gani tena!!. Mizuka?” Reeny alianza kujikumbata kuhakikisha woga wake haumtoi nishai.



“No!, No!, nimeota nakusaliti Reeny!”



“Kunisaliti? kiaje?!, umeniua au?”



“No!, nimeota umenifumania na mwanamke wa maisha yangu!”



“Hah hahaha!” alicheka kidogo Reeny na kumshika kifua Roy.



“Mpenzi umenisaliti mara ngapi na sijafanya chochote?, almost all of your bitch!. Wengi sana my!, but akuuu!!!. Najua utafanya sana mapenzi na wanawake wengine ila kwangu utarudi tu!. Na sijawai kukukataza. So what’s wrong?” alijiamini Reeny.



“Ok!. Najua Reeny unaamini hivyo ila kila siku siachi kukuambia ukweli kuwa.. we just enjoy!. Tunainjoiana tu hakuna kutu mbele!. Nashukuru unanielewa ila unakuwa mbishi!. Why!” Aliuliza.



“Toka siku ya kwanza navua nguo yangu ya ndani humuhumu ndani tena… kuna kitu nilikuambia Roy!. Huna akili ya kusahau mapema hivyo!. Nilikuambia ‘ukitaka uachane na mimi basi uniue!’” aliongea na kutabasamu Reeny. Roy alishusha pumzi.



“Ok!, Ok!. Pole kama nakuumiza lakini.. na kama unanipenda basi naomba nifanyie kitu kimoja.. I will pay you!. Chochote utakacho nitafanya. Ila baada ya kunifanikishia jambo hilo!” aliongea Roy macho akitazama sakafu!.



“Nimefanya mengi sana mchumba!. Mi sina cha kuomba kingine zaidi ya kutoniacha tu! Hata kama ukioa Roy!. Usinisahau!. Wewe ndio faraja yangu!” Reeny alianza kutia huzuni. Zilikuwa ni dalili kabisa za kilio. Roy aligundua hilo. Akamkumbatia kifuani kwake.



“Naitaji connection!” aliomba Roy.



“Ya mwanamke!” alijibu Reeny na kujichomoa kifuani mwa Roy.



“Ndio Reeny. Kuna mtu ananiumiza sana kichwa!. Namuhitaji kumpata kwa kila aina ya gharama!.” Alisema japo kwa upole.



“..And!, baada ya kumpata?!”



“Just yeye na wewe tu!. Naacha kabisa kurukaruka. I swear!”



“Kha!, lakini Roy mboni we huna kipingamizi kabisa katika kupendwa. Kila neno lako ni zawadi kwa watoto wa kike. wengi wamekuja wenyewe!. So what? Unataka nini labda!.”



“Nataka tucheze Game!. Mimi na wewe tu!.” Alisita kidogo. Akaendelea.



“In shot nampenda. Na nataka awe wa mwisho katika mapenzi yangu hapa duniani. Najua hadi sasa atakuwa amenisikia vibaya sana kupitia maneno ya watu!. Hilo najua. Hata kama nikimtongoza mwenyewe hawezi kukataa, ila atakubali kwa One night tu! (usiku mmoja). Mimi sitaki hivyo. Nahitaji adumu maishani mwangu. Nimwite mama watoto wangu!.”



“Mhhhh, but Please!, ukimpata usinisahau Roy!. Nakuamini tafadhali!.. Enhe!, aina gani ya gemu wataka!”.



ITAENDELEA…….
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 06

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email: xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



ILIPOISHIA…

“Kha!, lakini Roy mboni we huna kipingamizi kabisa katika kupendwa. Kila neno lako ni zawadi kwa watoto wa kike. wengi wamekuja wenyewe!. So what? Unataka nini labda!.”



“Nataka tucheze Game!. Mimi na wewe tu!.” Alisita kidogo. Akaendelea.



“In shot nampenda. Na nataka awe wa mwisho katika mapenzi yangu hapa duniani. Najua hadi sasa atakuwa amenisikia vibaya sana kupitia maneno ya watu!. Hilo najua. Hata kama nikimtongoza mwenyewe hawezi kata ila atakubali kwa One night tu! (usiku mmoja).mimi sitaki hivyo. Nahitaji adumu maishani mwangu. Nimwite mama watoto wangu!.”



“Please!, ukipata usinisahau Roy!. Nakuamini tafadhali!.. Enhe!, aina gani ya gemu wataka!”.



KIPANDE CHA 6.

ROY alisogeza mdomo kando ya sikio la Reeny na kumtakia maneno kadhaa kisha kuinuka. Reeny baada ya kusikia maneno hayo alivuta pumzi ndefu sana kabla ya kukubali.



“Sawa!” aliitika Reeny na kunyanyuka kama mtu ambaye alikubali kwa shingo upande.



Alishikwa tena mkono alipokuwa mlangoni na kugeuzwa hadi kutazama na Roy!. Wakaoneana aibu na mwanga ule ulikuwa unawatazama kwa kuwafumania. Reeny akajichomoa kwa Roy na kuelekea katika chumba chake. Alimwacha Roy akitafakari mpango ambao ameuandaa juu ya kumteka kabisa Rey!. Alijua atamuumiza Irene (Reeny) lakini hakuwa na jinsi. Alimfahamu Reeny kuwa ni mwanamke mwenye mipango sana. Kazi hiyo ilimfaa vyema sana.

---



“.. As you!.. so on how Bloom’s Taxonomy occupied in our system of education… it helps curriculum planners and implementers to arrange teaching and learning according to the required level.. therefore, you as student teacher….” Dr. Erick alikuwa mbali sana katika kuelezea soma lake asubuhi hii iliyokumbwa na baridi kali. Ilikimbiza kabisa joto la Dar na kufanya somo kueleweka kwa urahisi. Juu ya bao la kusomea paliandikwa CT 200.



“Rehma!, nimekosa peni mwenzako!” Alikuwa Reeny kando ya Rehma. Tayari alimshampata Rey hadi sehemu ambayo anapendelea kukaa.



Reeny alikuwa mwanamke wa kunyumbuka sana. Kuna baadhi ya mambo kama haya ya kutafutiana ‘koneksheni’ au kufanya upelelezi alikuwa amezaliwa nayo. Alikuwa na uelewa mkubwa sana wa kumwingia mtu. Haikuwa ngumu kwake kumpata Rey. Ni asubuhi tu hiyohiyo tayari Rey alikuwa mikononi mwa Reeny.



“Shostii, umetambika weeh! hadi kati ya kipindi!, husemi kama huna peni. Unakodoa tu macho..” jibu la Rey, lilimfanya Reeny kutabasamu. Rey akaingiza mkono kwenye mkoba wake mdogo na kutoka na peni mbili.



“Rangi gani?” Aliuliza Rey huku akimcheka mwenzake huyo ambaye ameamua kuandika katikati ya kipindi angali mwanzo wa kipindi hakuanza hata kuandika. Hakusubiri jibu tayari alishampa peni nyeusi na yeye akaendelea kusikiliza kipindi.



“Hahaa..” akacheka kidogo Reeny huku macho yake yakiwa kwenye simu yake. Rey alimwangalia mwenzake na kughuna tu ndani ya moyo. Akampotezea.



Reeny aliandika baadhi ya sentensi kwenye kurasa za daftari zake. Akafunika daftari na mwisho kuwa bize na simu yake.



“Hahaaha..” akacheka tena akionesha anafuraha sana Reeny. Hali ambayo ilimvutia Rey kuuliza kulikoni.



“Shosti nimekupa peni mpya hiyo. Mboni unaitumia kuchekea?” Aliuliza kwa uchokozi kabisa kutaka kujua nini kinamfurahisha mwenzake.



“Ah, Rey!, kuna mtu ananichekesha hapa!. Haha, Achana naye taila huyu!. We andika mwaya!.” Alijibu kwa mkato na kuendelea kuwa bize na simu yake. Rey alianza kumshangaa Reeny.



“Shostii!, unajua sio rahisi kama unavyodhani?, me hata Sikufahamu eti.. lakini we umenitaja hadi jina?, usikute unamfahamu hadi mchumba angu!” Rey sasa aliacha kuandika na kuwa bize na mahojiano yasiyo rasmi. Hiki ndicho kilimleta Reeny karibu naye. Reeny Alifanikiwa tayari.



“Eh, nakujua shosti!. Hahaa, mwaka wa kwanza tulikuwa kundi moja!.. la KI!... ila ni muda sana. Kundi namba moja!. Tunafikaa tu chuo…”



“Oohps!. Sina kumbukumbu kabisa yako, namkumbuka tu yule Eunice, kuna Grace.. Ila sawa. Jina nani?”



“Reeny!”



“Reeny?!.. Reeny… Reeeny!..” Rey aliendelea kuita jina hilo kichwani mwake. Akatoa peni yake mdomoni na kuendelea kuandika alichosikia kutoka kwa mwalimu.



“Ireeneee bhana!.. hahaa” alimfafanulia na kisha naye kuendelea na simu yake.



“Hahahaa… daah, huyu kaka taila kweli yani.. hahahaha” alicheka sana Reeny. Alikuwa kero mtaa mzima. Kuna baadhi ya watu waliacha kabisa kuandika kwa kumshangaa yeye. Hakujali. Aliendelea kufanya kazi yake tu. Rey aliona sio mbaya akiuliza.



“Jamani!, huwezi kutulia we Ereni?” alimwita kwa jina jingine kabisa la utani. Alijua atakuwa amemkera Reeny kwa kumwita Ereni, lakini wapi. Aliendelea kucheka tu hadi Rey nae alitabasamu kwa mshangao. Aliyekaa naye alikuwa kituko siku hiyo.



“Hahaaha, yani nacho kicheka huku ndio hichohicho!.. hahahaa, mwenzako huku nae anakazana kuniita Ereni. Hahaha yaaani wewe unaniita Ereni na Roy nae ananiita Ereni”



“Roy?” Aliuliza kwa mshangao Rey nusura angushe kichwa chake chini kwa mshangao.



“Eh, RoySon we humjui jamani.. anautani sana yule kaka. Nampenda hadi basi!” alimaliza Reeny. Hii inaitwa ua kushoto.. fufua kulia..



“Ah, namjua huyo kaka.. ila so saana!. Tuseme tu nimechelewa kumjua!..” Rey akajawa na hamu ya kutaka kujua zaidi Roy ni nani.



Sasa alianza upelelezi yeye mwenyewe binafsi wa kujua Je? Waliyoyasema wenzake wakina Sophia yana ukweli wowote? Akaamua kutumia fursa ya uwepo wa Reeny hapo kumjua Roy vizuri zaidi. Kumbe alianzia sehemu sipo kabisa. Aliyekuwa anamuulizia naye alikuwa anamfukuzia.. kama ni mpira wa miguu hapa ni pale unamuhonga Mesi aifunge Barcelona.



Kwisha Kazi!.

“Khe! Huyo kaka anapendwa sana na watu wengi basi!. Mana sio mara ya kwanza kumsikia!. Itakuwa ni mtu mkubwa sana eti?”.



“Ah, wapi kapuku mmoja wa mbeya hapo!, shosti! ni kakijana tu bhana kapo simpo sana ila daa wengi wanakapa sifa za ajabuajabu ambazo hata mie sijawai kumwona nazo..”



“Eh, kweli jamani ila mie nimesikia baadhi tu.. zote za kumsifia. Eti wanasema ni mtaratibu sana” Rey alikuwa anaongea kwa kumtega Reeny na Reeny yeye anajua kila kitu. Naye alikuwa anamjibu kwa maunganisho sahihi. Hakutaka kukosea.



“Ah, hapana bhana.. unajua hakuna binadamu mkamilifu!. Hilo ndio nalijua mimi.. na Roy ni mmoja kati yao. Roy anatatizo moja tu!, basi.. hajawai kupata mwanamke wa maisha yake. Sasa kila mwanamke anapoenda anakuwa kama anamjaribu hivi afu akitoka kwake anaanza kumsema maneno ya ajabuajabu jamani. Mimi nipo nae mwaka wa pili huu. Lakini sijawai kuprove wrong kwake. Namuaona yupo sahihi. Sio kama watu wanavyomsema. Da!” Reeny alitiririka vilivyo kabisa kwa kuongeza na chumvi mboga ipate radha.



“Oh!, kweli!, huyo kaka ila hata mi.. mi… sijui kwanini yani nashindwa hata kujua kwanini..” aliongea kwa mkato Rey bila kumaliza neno. Reeny alishangaa sana kwa ukweli, kwani hakutarajia kabisa kila anachotaka kuongea Rey. Akaganda machoni pake kumsisitizia amalizie. Hata y.eye nini?



“Ah, yani nashindwa kabisa kujikonto!, ebu nisaidie rafiki yangu!..” Rey alishazama mazima kwa Roy. Hakuyajali mapungufu ambayo wenzake wamemuhorozoshea. Ndoto anazoziota za Roy zinamdadisha kufanya kitu.



Reeny alitikisha kichwa kimoyomoyo kuashilia kazi yake imekuwa nyepesi sana. Alikuwa ni winga machachari aliyepewa penati ya bila kipa. Alitumia kisigino tu kusukumiza mpira kwa nyavu.



“Oh!, Rey!!!, unampenda Roy!” aliacha kuchezea simu sasa Reeny na kuongeza umakini kwa mazungumzo.



“Ah. No hapana!. Na sio kama simpendi… aaaagh! Mungu wewe!” alikuwa aelewiki kabisa Rey kama anataka kama anakataa.. Reeny alitabasamu machoni.



“Ah, kwani wewe sio mpenzi wake?” alimtupia swali Reeny.



“Hapana bhana na haiwezi kuwa. Nampenda na kumweshimu kama kaka yangu. Labda tungekuwa wapenzi toka mwaka wa kwanza. Lakini mimi nishachumbiwa na mchumba wangu yupo hapahapa Dar!. So nipo nae tu karibu sana. Ananisaidia sana kwa kweli.. ni charming, SmileMan, yani hacomplicate mambo ya ajabuajabu.. sio mtu wa viwanjaa.. mimi nashindwa kumwelezea. Lakini ni moja kati ya watu waomjua yeye kwa undani kabisa kuliko wengine. Lakini ukimgusa mwingine basi watakuambia yule Kaka Malaya sana!. Sijui kwa nini wanamfanyia hivi mpenzi wangu!”



“Mpenzi wako?” Aliuliza Rey akiyatoa macho kwa nguvu!. Reeny alikosea makusudi yote ni kuona tu hisia ambazo Rey amekuwa nazo..



INAENDELEA…

PATA SIMULIZI HII YOTE KWA TSH. 1000 TU. WASAP NAMBA 0672493994. AU NITUMIE INBOX SMS.
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 07

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email: xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



ILIPOISHIA…

“Hapana bhana na haiwezi kuwa. Nampenda na kumweshimu kama kaka yangu. Labda tungekuwa wapenzi toka mwaka wa kwanza. Lakini mimi nishachumbiwa na mchumba wangu yupo hapahapa Dar!. So nipo nae tu karibu sana. Ananisaidia sana kwa kweli.. ni charming, SmileMan, yani hacomplicate mambo ya ajbu ajabu.. sio mtu wa viwanjaa.. mimi nashindwa kumwelezea. Lakini ni moja kati ya watu waomjua yeye kwa undani kabisa kuliko wengine. Lakini ukimgusa mwingine basi watakuambia yule Kaka Malaya sana!. Sijui kwa nini wanamfanyia hivi mpenzi wangu!”



“Mpenzi wako?” Aliuliza Rey akiyatoa macho kwa nguvu!. Reeny alikosea makusudi yote ni kuona tu hisia ambazo Rey amekuwa nazo..



KIPANDE CHA SABA!.

“NDIO kaka!, kaka tu yani!..” alijibu Reeny



“Ah, me nina.. siku moja tu toka nimuone uyo Roy!. Hmmm.. hatari. Ok! Naomba namba yake!” alijibamiza kwenye ubao wa moto Rey.



“Hmm inaonaje nimuulize mwenyewe kwanza!.. mana hapendi namba yake niitoe toe!” aliongea kwa kujishaua Reeny.Alipata 100 kwenye mtihani wake.



“Ah, hapana bhana mimi nataka nimsaprise!. Usimwambie bhana!” Nae Rey mapozi yakawa mengi.



Rey na Reenywakazama katika maongezi, lakini Reeny aligoma kutoa namba ya Roy. Alisisitiza hadi akaongea nae kwanza ndio atampa namba yake. Alikuwa anajua kuwa Rey anaweza kuipata namba ya Roy sehemu yyoyote ile akiitaji. Ila yeye alimnyima kusudi kumwamisha kuwa Roy ni mtu wa muhimu na si mhuni kama watu wanavyosema. Rey akaweka tiki kubwa kwenye moyo wake.



“Sitojali wanasemaje!, ‘samaki harudi rivasii’” alijiongelea mwenyewe Rey hadi mwisho wa kipindi. Hakuna kingine alichongamua katika kipindi hicho kama hii mada ya Roy. Hakika Reeny alimfundisha kwa umahili kabisa. Hakuacha doa moyoni. Alisafisha moyo wote wa Rehma.

-----



UPANDE WA I.

“KELVIN. Bila shaka mrejesho ambao nilikuwa nausubiri umeshafika tayari..” Roy na Kelv walisimama njiani kuangalia simu ya Roy. Roy alikuwa anamwonesha Kelv ujumbe mfupi kutoka kwa Reeny.



“Nimemaliza mimi!. Kazi kwako dear!” ujumbe huo ulikuwa unasomeka hivyo. Kelv alishindwa kuzungumza chochote kile alibaki kushangaa tu ule ujumbe asiouelewa.



“Reeny nilimtuma anifanyie ‘koneksheni’ kwa Rey!” maelezo ya mdomo yalifuata kutoka kwa Roy.



“Rey ndo nani?” Aliuliza Kelv.



“Mtoto wa kitanga!. My heart controller!.. hahaa ushaachwa mjini wewe!” alijibu Roy na kuongoza njia kuelekea sehemu wanayoishi.



“Kuna mwanafalsafa alisema hivi.. if you feel good!, Do it!. Just Do it!..”alisema Kelv.



“Nakuelewaga sana mwanangu!. Unanipa vitu adimu sana. Wewe nakuweka nafasi ya tatu! Sawa!?. Anaanza Rehma, then Vitabu, then wewe! Hahahaha” Roy alipanga vitu vyake anavyovikubali na mwishowe kuachia ucheko wa nguvu.



Kelv alishangaa nafasi ya kwanza anawekwa mwanamke. Tena mwanamke wa siku mbili tu. Tena mwanamke ambaye anafahamu kuwa hata dumu nae hata wiku tu kwa mujibu wa mapenzi ya Roy.



“Uliponiacha hoi ni apo ulipomweka huyo mwanamke wa kwanza. Ungeanza na Mama ungepungukiwa nini… ok!, ila mzee umeniangusha kitu kimoja tu!.. unamtumiaje Reeny!. Kwani unamwonaje yule?”



“Reeny ni mwanamke mrembo, jasiri-shupavu, yani ana.. kila-kitu ambacho mwanamke mzuri anatakiwa kuwanavyo. Ila amekosa kimoja tu basi!”



“Kipi?”



“Nafasi..”



“Ya wapi?”



“Kwangu.. yaani vyumba vimejaa!. Licha ya kila kitu ambacho anaendelea kunifanyia lakini bado kabisa yani. Moyo wangu haujampokea kabisa, amekuwa mwanamke wa kukata hamu yangu tu pale napojisikia kiu.” Alijitapa Roy.



“So unajua kama anakupenda, na anawivu juu yako. Then still unamtumia akuunganishie mwanamke mwingine? Na amefanya?!. Masikini!!!!!..” Alishika kichwa Kelv kusikitika. Maneno ambayo yalimwingia kisawasawa Roy.



“Lakini naye anajua kuwa hana nafasi.. nilimwambia ilaa… ye anaforce tu. Sa mimi nifanyaje.?”



“Hata kama! ila hupaswi kumfanyia hivi. Fanya mambo yako yote ila usidharau mbachao kwa msala... ohoo!. Kuna siku utajikuta Rey hayupo, Irene hayupo sijui utakuaje...”



“Hahaha, hapo nitakuwa kwa Mama bro!, hahaha!” alicheka Roy. Japo Kelv alikuwa muelewa sana na tabia ya Roy, haikumsumbua hata kidogo kumwambia ukweli. Alimshauri kila anapokosea. Japo ushauri wake hua unapitaga tu kama gari moshi, unakuwa na kelele nyingi na haufiki mbali…



Royson na Kelvin ni marafiki wa kushibana sana ambao walikutana mwanzoni tu mwa semista ya kwanza ya mwaka wa kwanza. Walipenda aina yao ya maisha na hatimaye kuishi pamoja kwa kumsaidia mambo yote yanayohusu taaluma. Urafiki wao unampaka mmoja tu!. Wanawake!. Mpaka huo hakuna aliyeuvunja. Kila mmoja aliheshimu mapenzi ya mwenzie.



Roy na Kelv waliongozana hadi kufika hostel ambayo wanaishi wote kwa pamoja. Utofauti ni vyumba tu. Kila mmoja alikata kona yakekwenda kupumzika. Ratiba ya chuo haikuwabana kabisa wawili hao. Waliipanga vizuri mno ili kupata muda mzuri wa kupumzika na kufanya mambo mengine.



Roy alifika chumbani mwake na kukaa kitandani. Hamu yake ya kutaka kusikia jibu la mdomo kutoka kwa Reeny ikamfika. Alihitaji kujua je kazi aliyoiagiza Imekwenda kama alivyopanga. Akainyanyua simu yake na kutafuta namna ya kuwasiliana na Reeny, lakini kabla hajafanikiwa kubonya sehemu ya kupigia kuna simu nyingine iliingia.Roy aliishangaa namba ngeni kwa sekunde kisha kupokea.



“Darling!..” aliyepiga alianza kuongea na kusubiri jibu kutoka kwa Roy. Kimya!.



“Hallow!..” aliita.



“Yes!.” Roy sasa alijibu na alikuwa anasubiri aliyepiga kujitambulisha.



“Ah, Roy bhana hujaacha tu mambo yako. Mi Rehema hapa!” alijitambulisha.



“Nani?” alijibu kwa mshangao mno. Hakusubiri jibu tayari iliichomoa simu kutoka sikioni na kurudia kuisoma namba ile iliyopiga. Bado ilionekana haina jina.



“Oh!, My Gosh!.. Rey?” Aliuliza.



“Eh, wa mbeya!” alikomea hapo.



“Oh!, Shit!!…. ‘Rey wa Mbeya!..’” alitafakari jina hilo na mwishowe kupata majibu. Alikuwa ni msichana kutoka kwao, walikutana siku moja tu!, tena katika pilikapilika za Kabwe.Walizungushana kutwa nzima na safari yao ikakomea saa kumi na mbili asubuhi. Baada ya kumaliza mambo yao usiku mzima, Roy akasahaupenzi hilo na Rey huyu wa Mbeya bado akaweka katika kumbukumbu.Na sasa alimkumbuka kwa simu.



“Ndio!, Roy.. yaani navyo kuambia hivi nipo Dar!. Roy wikiemdi hii tuonane basi.!” Alimaliza.



“Oh!, ok sawa!” alijibu kwa mkato Roy na kukata simu.



Hii ndio tabia ya Royson Johnso. Kama hajakupenda basi sahau kitu kinahusu kukumbukana. Anapenda sana wakati ujao kuliko wakati uliopita. Wanawake alikuwa anawatumia kama sabuni tu awapo maliwatoni. Nimuhimu ili ajitakatishe na jasho la saa, lakini akishatumia huacha sabuni hizo na povu lake chooni naye kutafuta manukato mengine. Wanawake aliwafaninisha na sabuni tu awapo chooni. Na sasa amependa kabisa. Amechanganyikiwa kabisa, Rey alimwingia kichwani, moyoni na rohoni. Sasa Rey alikuwa mwimbo wa taifa kwa Roy. Wimbo rahisi, mzuri wenye beti moja tu na maneno yasiyozidi mawili. “Rey”. Aliuimba kutwa nzima.

-----



“Reeny!, ahsante kwa kumaliza kile ambacho ulinihaidi. Lakini bado ninaombi la mwisho mpenzi…” Roy sasa alikuwa mapajani mwa Irene, waliposoma kitabu mwishowe Roy akaingizia tena jambo lake.



“Lipi Baba!..” alijibu Reeny.



“Naomba mchezo uendelee.., nimeona matunda kuwa Rey anaanza kuwa karibu yangu!.Jana nilikuwa naye!, tumezunguka sana chuo pamoja. Ila sijaweka wazi dhumuni langu kutokana na sumu aliyonayo. Bila shaka amefahamu kuwa mimi sio mtu mzuri. Na kweli mimi sio mzuri kabisa.. nakubali.. (aliinuka kutoka pale alipolala kwenye miguu ya Reeny. Akainuka.) ...lakini nakuapia mpenzi. Rey nampenda. Na nitabadilika Reeny. Naomba ufanye kitu”.



“Mhh!, unamajaribu wewe jamani Roy!..” Reeny sasa alichukia. Alifunika kitabu na kuifunga mikono yake huku wa kulia ukienda kushoto na kushoto kwenda kulia.



“No!, no Reeny, this will be the last!. Trust me!” Roy alim’bana Rey kifuani kwake na kumpapasa kidogo maeneo yake ya shingo. Alijua udhaifu wa Reeny. Roy alikuwa mnyanyasaji wa fikra na saikolojia. Alijua jinsi ya kumwingia kila mtu ila kwa Rey alihitaji msaada.



“Niambie.”



“Oh, Ahsante mpenzi. Nakupenda!. Pumzi zangu zimesimama sasa!, naona jinsi gani unanithamini Reeny!. Wewe ndio msaada wangu. Wewe ndio daraja langu la mafanikio. Nivushe mpenzi!... “Aliendelea kumpapasa kila maeneo ambayo anajua mwenza wake anakuwa dhaifu. Akampata vilivyo.



“Roy bhaaana, sema bhaaaasi baba!”aliwaka Irene. Sasa alikuwa anachanua mawimbi, nusura amalizie ibada kwenye nyumba za wageni.



“Naomba nikulipie kila kitu!, naomba nikutoe hapa!, naomba nikuhamishe na ukaishi kwa muda na Rey!. Nakuomba nakuomba!” aliongea Roy.



“Sijakuelewa..”Reeny alichomoka mikononi mwa Roy na kuuliza.



“Nataka nikupeleke kule anaishi Rey!. Naomba ukamjenge kwa fikra na kumwaminisha kuwa, mume wake nipo na ninamsubiri kwa hamu tu!. Vingine vyote nitamaliza mwenyewe, nisaidie kwa hilo tu…”



“Doh..” alishusha pumzi nzito Reeny. Machozi yalianza kumlengelenga. Kwa kweli alikuwa ananyanyaswa. Tena mnyanyaso wa sekta zote za maisha, kimapenzi, kimwili, akili na karoho. Alihisi kuishiwa pumzi. Leo aliamua kudondosha chozi hadharani. Alilimwaga mbele ya Roy.





INAENDELEA…

PATA SIMULIZI HII YOTE KWA TSH. 1000 TU. WASAP NAMBA 0672493994. AU NITUMIE INBOX SMS.
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 08

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email; xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



ILIPOISHIA…

“Sijakuelewa..”Reeny alichomoka mikononi mwa Roy na kuuliza.



“Nataka nikupeleke kule anaishi Rey!. Naomba ukamjenge kwa fikra na kumwaminisha kuwa, mume wake nipo na ninamsubiri kwa hamu tu!. Vingine vyote nitamaliza mwenyewe, nisaidie kwa hilo tu…”



“Doh..” alishusha pumzi nzito Reeny. Machozi yalianza kumlengelenga.Kwa kweli alikuwa ananyanyaswa. Tena mnyanyaso wa sekta zote za maisha, kimapenzi, kimwili, akili na karoho. Alihisi kuishiwa pumzi.Leo aliamua kudondosha chozi hadharani.Alilimwaga mbele ya Roy.





KIPANDE CHA NANE!.

“REENY please, you promise me!, uliniahidi!, nakuomba timiza ahadi yako nami nitafanya chochote kile.Hakuna kitakacho aribika. Niamini!” aliyashika mashavu ya Reeny kwa mikono yake yoye miwili.Aliyabinya binya kama mchaguzi wa nyanya za kachumbari.



Walikuwa wanatazamana kama watu walioshikana ugoni. Reeny alikuwa anasita kumkazia macho Roy kwasababu ya chozi ambalo ametoka kilimwaga mda huohuo.Roy alisogeza mdomo wake karibu na Reeny, wakapokezana vimimika kwa sekunde..kabla purukushani za hisia hazijaibuka. Roy alikurupuka na kumwacha Reeny!.



“No!, Reeny hatuwezi fanya.. hatuwezi kuendelea.. namuhitaji Rey kwanza!” aliongeaRoy pasi kuangalia mazingira. Neno hilo lilimtoa nduki Reeny hadi chumbani kwake. Spidi zake zilikuwa kamamwanamke ambaye anaelekea kutapika nje kuficha wazazi wasijue kama ameukwaa ujauzito. Aliumia sana Reeny. Nafasi yake ilinyanganywa mara kadhaa na baadhi ya wanawake lakini hawakuwa na madhara kabisa katika penzi lake. Lakini picha hili mpya ambalo ndo kwanza alaiona treila lake linamnyanyasa haswa. Wapi lipo jembe akachimbe shimo ajifukie?. Leo hii hana uhuru na Roy??.



UPANDE WA II.

Kilikuwa ni kikao cha watu sita sasa. Wote walikuwa na sura tofauti kwa mwenzao. Lengo la kikao ni kutoa amri moja tu!.“ACHANANA ROY”. Ilikuwa ni ajenda rasmi ya kumsema mwanzao “Rey” katika kujihusisha na mapenzi na Roy licha maonyo kadhaa aliyoyapata kutoka kwa marafiki wake. Alikuwa Mis. Mogella, Salma, Yusra. Glory, Saudath naRehma mwenyewe.



“Mpenzi wangu, nilishakuonya mimi kuhusu huyo Roy!, ataharibu maisha yako mpenzi!,tumesema, tumesema lakini hata huelewi asee!. (akaachana na Rey na kuwageukia wengine). ..jamani, jana!, jana tu.. nimewaona wanadhurula chuo kizima. Na sijui kama jana hiyohiyo hawajamalizana..na kama sio jana sijui… Uwiiii!..” Sophy alionekana kabisa kutabiri mahusiano ya mwenzake. Aliwaona Rey na Roy wakiandamana huku na huko. Wakiwa hawana cha peni wala karatasi.



“Nimewaona sana hata mimi. Tena walianzia vimbweta vya bichi, wakaneda vya laibrari, haooo uwanjani, mara makaburini.Mwanangu unahamu gani hiyo ya mapenzi ambayo hata sisi ndugu zako hatuwezi kukusaidia? Au lazima awe Roy?” Yusra nae akatoa lake.



“Jamani!, nami pia nilikuwa siamini kabisa mambo ambayo mlikuwa mnaongea kuhusu Roy, Ile juzi... Msema ukweli ni mpenzi wa mungu jamani mimi siku hile ambayo mlikuwa mnamwonyaRey kuhusu Roy Nilijua ni story tu za kutungwa. Si mnakumbuka nilikuwa nachana nywele,..najiandaa hivi?...” Swaumu aliuliza lakini hakusubiri jibu, akaendelea.



“Muandao wote ule, ulikuwa wa Roy. Mtoto wa watu na juba langu mwili mzima, nikabu usoni. Hadi karibu naRaha Leo Pub.Pale upande wa pili tu kuna mchochoro wa nyumba za wageni. Tuliahidiana nitakuwa na Roy huko..basi nikachukua chumba kama tulivyokubaliana. Nikalipa kwa pesa yangu, nikamsubiri huyo mwanaume…” alipoanza kusimuliza Sally,watu hawakuwa maanani kumsikiliza.Lakini wote sasa walitumbua macho kusikiliza.Walionesha kutoamini kile anachosema Salma. Yani na uislamu wake wa swala tano alienda na Roy chumba cha wageni. Hadi wasiowahi kushangaza walishangaa siku hiyo. Wote wakaweka kituo kwaSally.



“Eeh!,nilikaa mwenyewe lisaa lazima. Nakumbuka nilitoka hapa sakumi na moja, kumi na mbilihivi. Wote mlikuwa mmelala humu.Nilimsubiri huko hadi sa moja unusu masikini….Alichelewa kuja lakini nashukuru alifika yule mkaka. Hahahaha, ila yupo vizuri kwa kweli. Kwanza Alipofika alinirudishia pesa zangu nilizolipia chumba.Nilipaga kwa siku nzima hadi kesho yake asubuhi, kwa maana tutalala humo… lakini yeye alinirudishia pesa yangu yote na aligoma kulala humo. Nilimwambiabaada ya kumaliza tendo, basi tutaondoka sote.



Basi pale, tukaanza kazi, mwanamke nikavua nikabu yangu nikarushia hukoo, nikavua juba langu nikaweka kulee, nikavua navingine vilivyobaki... Akanishika, akanishika, akanishika..nilikuwa hoi!, hoi!, hoi. Nilikuwa nimelowa mwili mzima, hapo kushikwa tu jamani!.Basi akaanza na yeye kuvua nguo zote. Jamni anamwili yule kaka!. Lo!, sijui kama kuna mwanamke hapendi mwili kama ule.Kwa mwonekano tu, ukimwona lazima umwage. Hahahaha” Salma hadithi ya kusikitisha aliendelea kuisimulia kwakuchekesha, wenzake wote walimshangaa. Sally akaendelea.



“Masikini yule kaka alitumia dakika nne tu, yaani kuingiza na kutoa, kuingiza na kutoa.Mwishowe akakomea kwenye kutoa. Alijikusanya pembeni yangu na kuning’oneza sikioni. ‘Eti oh,I’m sorry mrembo, nashindwa kuendelea ku-sex sipo vizuri leo. Sina hamu kabisa, eti hamu imekata, nitakutafuta siku nyingine’ jamini, jamani jamani jamaniii, sikuwa na uhakikika na kitu alichoniambia. Yani mda huo nilikuwa bado sana kufika nako enda lakini aliniacha njiani na kiu, hakuna maji wala mtu wa kunisindikiza… just Imagine jamani, amenichezea tu mwili mzima kwa kunishikashika, sijui alijua ninahamu ya kutofanya mapenzi kwa muka mzima?. Huwezi amini!!!Akakomea hapohapo.Nawaambia, alivaa nguo zake na kuondoka. HUYUHUYU ROY.Sasa ndio nimeamini, hakuna wa kunisumulia” Alimaliza Sally.



“yehlewiiii!, we Sally?! Khaaa, ko ulienda kuhakikisha kuwa tuliyokuwa tunasema kweli au la!” Sophia Aliuliza.



“Ndio!, kuhakikisha, hiyo moja.Pili, ni kuona je hizo raha ambazo kila mtu anazungumzia ni kweliiii..ndo nikajionea mwenyewe. Pia nilikuwa nina apointimenti nayeee! Tena mda mrefu tu nilikuwa natafuta hiyo nafasi..” alijibu Sally.



“Malaya mkubwa wewe!, yaniii… hahahaha” Glory alimpaka mwenzake matope.



“Kama ni Malaya basi wote hapa tumeonja huo umalaya!, sijui kama mtu ameachwa salama hapa, hahaha!”



“Mimi!, sijawai fanya mapenzi na mwanaume yoyote hapa Dar!.” Rey alijibu.Wote wakamwangalia.Waliocheka walicheka, waliosikitika walisikitika.



“We hujafanywa jana kweli wewe?”, Yusra Aliuliza na kufuatiwa na vicheko.



“Kweli sijafanya!,na hata kama nikitaka nae kufanya si ni mimi bhana, kwani shi ngapi?. Mboni nyie mmefanyaaa!. Mimi nani nipimge?” alijibu Rey kwa ujasiri.Macho ya kikao kizima yaliamia upande wake bila kusema chochote.



“Umesema?” Mogella Aliuliza kana kwamba hakusikia vizuri”



“Jamani rafiki yangu!,umeharibikia wapi jamani?” Sophiaalisikitika.



“Jamani Rey unajua we bado katoto afu kazuri.Usikubali kirahisi hivyo, kuna magonjwa mama. Bora hata utupe sisi hilo penzi... pengine tunaweza kukusaidia. Sisi si wanawake wenzake?. (akiwauliza wenzake) Rey Kama upo na hamu sema tutasaidiana tu kuliko kumpa tu ambaye hana hata chembe huruma” Yusra alikazia.



“Ah, marafiki hamna dogo!, yani wote hapa mmefanya nae si ndio?... nimebaki mimi tu! Afu mnaniwekea kauzibe?. Roy hayupo hivyo kama mnavyosema. Nimeanza kumjua kwa undani kabisa yani. Hakuna la kunidaganya msimzingizie mkaka wa watu jamani, muwe na huruma..”aliongea Rey.



“Ivi wewe nif*la eti??” Sophie alikasilika.



“Ofcourse yaweza kuwa fala, chizi!, ila ndo nawaambia hivyo. Sasa kama mnataka kuona tabia halisi za Roy, nawaombeni muwe watulivu. Roy nitakuwa naye kwa mapenzi kwa muda mrefu tu kuliko mwanamke yoyote yule. Nitawafundisha nyie nini maana ya mapenzi!” aliongea mfurulizo Rey na kuwaacha wenzake wote wameduwaa.Wote walijua fika kabisa tabia ya Roy. Sasa leo Rey analeta mpya. Wote walilowa kamamapanzia ya mama ntilie nyakati za jioni. Wakamsindikiza tu Rey akitoka chumbani humo na kutokomea nje ya chumba.



“Nyie, hivi huyu ameleogwa et!?” Sophie aliwauliza wenzake waliobaki.



“Huyu hana la kuwasikia saizi. Mwacheni kwanza apige mbija, atatapika tu!.Mboni dalili za mgonjwa hujulikana!” Saudath aliyekuwa kimyakwa mudaakamtuliza Sophie.“Yaani, kila siku naawambia kuwa hakuna mwalimu mzuri katika mapenzi..kwa sababu wote ni wanafunzi. Kila mtu anajifunza kitu kipya kuhusu mapenzi.Rey bado hajajifunza chochote kile.Kwani ashawai kuwa na mwanaume mwingine hapa chuo?”Saudath Aliuliza.



“Hapana!” jibu likapatikana.



“Sasa kama ni hivyo, tumwache tu wapenzi..ajue kwanza hasara na faida za mapenzi. Mbichi na mbivu za Roy afu akiharibika atakuja kuomba ushauri..binadamuanarekebishika pale tu anapohisi jambo alilohisi atalifanya kwa ustadi amelikosea. Hapo ukimwambia atakusikia lakini kumvalisha nguo Mbuzi ni sawa na kumwonea tu. Haoni umuhimu!”Saudath akamaliza.



Kikao kiliishia na makubakubaliano ya kumwacha Rey afanya vile anavyoona yeye inafaa. Sophie alipinga katakata mwanzoni lakini hakuwa na la zaidi. Hakuwa na njia nyingine ya kumshika mkono rafiki yake huyo kumweleza kuhusu maisha. Moyoni aliapa kuwa hawezi kuruhusu jambo hilo linatokea kwa rafiki yake. Waliamua tu kukubaliana tu kumwacha kwanza kama mambo hayataenda sawa basi lazima aje kuomba ushauri tu. Hawezi kuhimili pekeyake mikiki hii.



INAENDELEA…

PATA SIMULIZI HII YOTE KWA TSH. 1000 TU. WASAP NAMBA 0672493994. AU NITUMIE INBOX SMS.
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 09

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email; xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



ILIPOISHIA…

“Sasa kama ni hivyo, tumwache tu wapenzi.. ajue kwanza hasara na faida za mapenzi. Mbichi na mbivu za Roy afu akiharibika atakuja kuomba ushauri.. binadamu anarekebishika pale tu anapohisi jambo alilohisi atalifanya kwa ustadi amelikosea. Hapo ukimwambia atakusikia lakini kumvalisha nguo Mbuzi ni sawa na kumwonea tu. Haoni umuhimu!” Saudath akamaliza.



Kikao kiliishia na makubakubaliano ya kumwacha Rey afanya vile anavyoona yeye inafaa. Sophie alipinga katakata mwanzoni lakini hakuwa na la zaidi. Hakuwa na njia nyingine ya kumshika mkono rafiki yake huyo kumweleza kuhusu maisha. Moyoni aliapa kuwa hawezi kuruhusu jambo hilo linatokea kwa rafiki yake. Waliamua tu kukubaliana tu kumwacha kwanza kama mambo hayataenda sawa basi lazima aje kuomba ushauri tu. Hawezi kuhimili pekeyake mikiki hii.



KIPANDE CHA TISA!.

Siku ya kwanza kumwona.., moyo ukaesema inshallah. ….. nafsi ikasema ewalaa… karibu nyumbani madale, karibu chumbani my darling.. we ndio malkia.

=Msanii; Dause Mason – Wimbo; Nitamfwata”


Mapenzi pia ni kama taranta pevu ambayo wachache wametunikiwa kuyatawala. Nimesema wachache kwa sababu maalumu!. Sababu ambazo zinajitosheleza katika riwaya hii ya “Love Spaer”

------



Roy alikuwa ameketi kando na Kelvini nashemejiye Mwanaidi (Mwana), hawakuwa na mada kuu iliyowaweka pamoja siku hiyo. Yalikuwa maongezi machache sana kuhusu maisha.



“Roy!, kaa vizuri basi tupige picha, Shemu!” Mwana aliomba kupigwa picha ya pamoja wakiwa wamekaa kwa pamoja wote watatu.



“Kwachaa!” Mbaya!. Likatolewa tena wazo la kupigwa nyingine. Nayo ikawa mbaya kuliko iliyopigwa mwanzo. Mpigaji picha akabadilika na nyingine ikapigwa. ‘Nzuri’ wakakubaliana.Picha ikapigwa na kusambazwa kwa wote watatu!.



“Shemmmm, tupige na sisi wawili tu!” kazi alipewa Roy kupiga picha kwa wawili hao wapendanao. Aliishika simu kwa muda mrefu Roy bila kupiga chochote.



“Hakika namuona Rey anakuja kuwa nuru ya maisha yangu. Nasi tutapiga picha tukiwa wawili tu na kuweka kumbukumbu ya maisha. Rey! Uje basi tupige na sisi picha..” Roy alikuwa anawaza bila kufanya kile ambacho ameombwa na shemeji yake.



“Shemu?” aliita Mwana. Kimya. Akamwangalia Kelvi na kurudisha macho kwa Roy. Roy hakuwa pale. Alikuwa mbali sana kimawazo. Alishapanda treni ya Rehma Ayoub na kutowekea peponi. Aliganda tu akiwa na simu mkoni.



“Shemu!!” aliita tena Mwana na sasa Roy alisikika. Akakodoa macho kuitika wito. Alikuwa na mshangao kama mfanyakazi aliyehaidiwa kulipwa mshahara wake wa miezi mitatu iliyopita.



“Vipi tayari?!” alimuuliza kama alishapiga picha.



“Tayari nini!” alijibu Roy. Alishasahau kabisa.



“Whoooy!. Picha shemu!” aling’aka Mwana. Kelv alikuwa anacheka tu.



“Ohp!.. bado nilipiga mbili.. zikiwa mbaya.. aya weka pozi sasa.. weka!.. weka!”.



“Kwacha!!” ikapigwa, akapeleka simu kwa Shemejiye.



“Jamani shemu unaniniiii… tupige wote na kelv. Hahaha mboni Kelv umemkata.. hahahaha uwiii!” Roy alipiga picha ya Mwana tu!. Hakumuhusisha Kelv hata kidogo kwenye picha aliyopiga japo naye Kelvin alikuwa katika pozi. Sio kama hakumwona la asha, alisahau kabisa kama anatakiwa awapige wote kwa pamoja. Kelv alijua kinachomzumbua rafiki yake. Hakumshangaa.. aliendelea kucheka tu.



“Brother!, hivi upo serious au!” Kelv Aliuliza swali baada ya Mwana kuondoka.



“Yaap!, kuhusu nini kwanza?” akakaa vizuri Roy.



“Rehma!” alijibu



“Agh, bro acha tu! Sina hata raha yani. Sijui nimerogwa?”



“Hapna bro!, ila da!... unanitia shaka sana!. Sanaa, sanaa yani kwa hali hii. Kweli umependa asee!”



“Ndio hivyo bro. sio kwamba siwezi kumpata muda hu!, shida ni namuhitaji kama mke wangu. Sijui kama atakuwa anamawazo kama hayo. Bila shaka ashasikia kila kitu nilichofanya kwa wenzake. Ila si unakumbuka nilikuhaidi kubadilika kaka!... yah!. Hakika nikimtia mikononi na akikubali kuwa nami kwa kila hali basi nahakika atakuwa ameniokoa sana... jana jioni nilikuwa naye chuo anaonesha mtu wa wasiwasi sana…”



“Unahakika mwanamke huyo yupo kwa ajili yako?” Aliuliza Kelvin



“Naamini sana katika hisia. Moyo wangu haujawai kunidanganya hata kidogo. Ivi unajua kweli kuna muda moyo unasimama na kupisha kwanza Rehma apite ndio uendelee kudunda. Sio drama hii.. ni real!” aliongea akiwa makini sana Roy.



“Ok!, ushampeleleza ni aje, huyo Rehma kama anamtu au la?”



“Mtuu!, no siangalii hilo. Nitacheza pati yangu hadi awe wa pekeyangu!..”



“Rakini ulishawai kuniambia kuwa hakuna mwanamke wa mtu mmoja?”



“Aaagh ni kweli, ila kama nilisema mimi basi leo natengua hiyo kauli. ‘Massamba’ tu na ‘wenzake’walianzisha tanzu za fasihi za kitambo sana miaka ya tisini na ushehe huko.. miaka ilivyozidi kumfundisha vya kutosha akajua amekosea; Akatendua kauli na kuhainisha tanzu nyingine. Yeye ni mwalimu, mwanafalfasa, alikuwa dokta na sasa ni Profesa na PhD yake. Mimi nani nisibadili.. agh!, nitahakikisha tu anakuwa wangu pekeyangu!. Dunia inapaswa kubadilika Kelv. Mwanamke ni wa mwanaume mmoja tu! Kwisha!!” alijibu Roy. Kelvin alitabasamu tu.



“Vyovyote sawa tu!, Lakini nimekuona na wanawake wengi sana, wazuri sana sana sana sana yani.. huyo Rey haingii hata robo!. Kwanini yeye!”



“Brother, kuna aina nyingi za uzuri, ila inategemea na kigezo unachotumia cha kuanisha uzuri. Kwa mfano kwa kutumia kigezo cha mapenzi; kuna aina mbili za uzuri, uzuri wa nje na uzuri wa ndani. Sina shaka kwa nje amekizi kila kigezo. Mwembamba sio sana, mnene sio kabisa. Mrefu sio sana, mfupi sio. Mweupe sio saana, mweusi sio. Bila shaka ujamuona akinyata akienda kuoga kaka!, vuta picha amevua nguo sana, kwanza ushawai kumwona akiwa anatembea? (Kelvin akiendelea kucheka)



“Eeh!, kila kitu amebeba kama mwanamke, chuchu za kawaida.. kama hajawai kushikwa kabisa na mtu. Mzigo bado mzito ule, bila shaka anaupapasa mwenyewe anapolala.. hana dalili ya kushikwa.. nakuambia.. aya sasa huo ni uzuri wa nje. Njo wa ndani… njoo sasa. Japo sijakaanaye sana ila moyo wangu unaniambia ni mtu ambaye haitaji skendo, anafanya mambo yake kwa muda, anazingatia maadili ya dini… ooohps!, kwa ujumla ukitumia kuangalia vitu hivyo basi nina asilimia zangu zaidi ya tisini kuwa anatabia nzuri?. Swali ni je? Mwanaume gani hapenzi nilivyovianisha hapo?” Roy alimaliza kwa kumtupia swali Kelv ambaye alishacheka hadi machozi kumtoka. Roy alikuwa siliazi et!.



“Hahaaaaa!, mzee umeshinda asee!. Da!.. enhe na kwanini yeye!. Jibu kifupi!”



“Nimekujibu mkubwa.. aya!. Ah! Toka nije hapa chuo for real sijawai kupenda kama nilivyompenda huyu dada. Nakuambia nimetumia sekunde mbili tu kumjua na kumpenda. Ile natoka tu darasani tupo nje tukatazamana.. yeye huyu, mimi huyu. Alikuwa na aibu mwenyewe, akaangalia chini, akanitupia salamu ambayo sikumbuki kama niliijibu kutokana na mawazo juu yake. Moyo wangu ulidunda kwa nguvu sana, nilihisi nimepatwa mshituko wa moyo. Na tokea hapo mwili na moyo wangu unasema na yeye. Yani nikilala, namwota. Nikimwona mwanamke yeyote basi labda nimkosee jina na kuwita Rey!. Huoni ni nina uhitaji nae mapema?”



“Hhahahaha, umejitahisi sana.. hapo ndo umejibu kifupi bila shaka. Ok bro!.. mie namfahamu vizuri sana Rey.. nilikuwa ane kwenye kundi moja mwaka jana. Ila si mtu wa kujiweka sana mbele mbele, hivyo wengi hawamjui. But katika uchunguzi wangu wa muda mfupi toka uniambie unampenda, nilimfanyia uchunguzi… nilipata kuwa anamtu wake kwao!. Yani amemlipia kila kitu hadi wazazi wanamjua.. huoni ni hatari hiyo?”



“Ah!, bro ivi ushajaribu kula mboga za majani zikiwa katika mapishi tofauti. Yaani chaina ya kukaanga na chaina ya kuunga na chaina ya kukausha kwa pamoja yani na ugali?. Hizo stori tu. Tena akiwa na mtu ni safi tu.. si ananisaidia kulea na kuhudimia vitu ambavyo vipo juu ya uwezo wangu?”



“Dooooh!,… sijawai kuona chizi kama wewe dunia hii.. wewe ni namba moja mzee...”



“Shemu wangu wa faida!, mambo?” alifuka Reeny kando ya mazungumzo ya Kelv na Roy. Wote walikuwa wanaishi hostel moja. Walijuana vyema kabisa. Neno Shem halikuwatenganisha.



INAENDELEA….

PATA SIMULIZI HII YOTE KWA TSH. 1000 TU. WASAP NAMBA 0672493994. AU NITUMIE INBOX SMS.
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 10

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email; xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



ILIPOISHIA…



“Ah!, bro ivi ushajaribu kula mboga za majani zikiwa katika mapishi tofauti. Yaani chaina ya kukaanga na chaina ya kuunga na chaina ya kukausha kwa pamoja yani na ugali?. Hizo stori tu. Tena akiwa na mtu ni safi tu.. si ananisaidia kulea na kuhudimia vitu ambavyo vipo juu ya uwezo wangu?”



“Dooooh!,… sijawai kuona chizi kama wewe dunia hii.. wewe ni namba moja mzee...”



“Shemu wangu wa faida!, mambo?” alifuka Reeny kando ya mazungumzo ya Kelv na Roy. Wote walikuwa wanaishi hostel moja. Walijuana vyema kabisa. Neno Shem halikuwatenganisha.



KIPANDE CHA 10!..

“Naamu karibu Shem.. mimi poa tu! Nipe habari!” Alijibu Kelv jicho kwa Roy.



“Dear One!, njoo kaa karibu yangu basi” Roy alimvuta Reeny na wote kukaa karibu, wanavipimo wanasema Ziro distansi.



“Shemu naomba nilindie huyu mtu.. tafadhali asitoke hapa. Nakuja” Kelv aliaga kisailensa kwa Reeny. Lengo ni kuwapisha waongee. Alijua fika kuwa wanamengi ya kuchembezana pale. Uelewevu wake ukamkimbiza mbele ya wawili hao.



“Dear one!, vipi hali..” Aliuliza Roy huku jicho likiviringwa hadi machoni mwa Reeny.



“Mimi ni dear one!? Na Rehma?” aliulizwa swali lisilo na ukakasi.



“My!!!, ooh!, mboni mtihani” alishindwa kujibu Roy.



“Umenipa kazi ambayo unajua kabisa siwezi kuifanya. Na kama nitaifanya basi si kama itakavyopaswa. Naumia sana Roy!”(alimpiga kijembe Roy na kuangalia pembeni). “Ok, nimefanya!.. ah.. da Roy hivi utanikumbuka kweli mimi?” sasa alimwangalia usoni Roy.



“Ondoa shaka, nilikuhaidi jamani.. niamini basi..” alijibu Royjapo kwa mashaka.



“Ok, ni Maamuzi yako. Sijawai na sipaswi kupinga. Mipaka yangu ni kukupenda wewe basi!. Haijalishi utaoa au nitaolewa...”



“Kwanini Unaongea hivyo?” Roy alimkatisha Reeny kabla hajamalizia.



“Unaenda kutengana na mimi Roy!, ulinizoesha Roy!. Unadhani mimi nitahishi vipi?”



“Dah!” Roy alihisi kuumia kwa maneno ya Reeny, lakini hadi kufikia hapo alishindwa namna ya kumsaidia. Tayari ilimpasa kusogea kupenda sehemu nyingine. Kwaufupi Reeny hakuwa na nafasi kabisa kwa Roy.



“Dah au Dar, Hapa Dar ni jua tu Baba, kivuri kaotee kwenu!” Reeny leo alikuwa mtu wa tofauti kabisa. Aliongea vitu ambavyo hata yeye hajui vinatokea wapi. Alimshushua Roy na mwishowe akawa muwazi.



“Sawa, Dear One!.. kazi yako inaenda vizuri.. nimemshawishi Rey tukapange chumba kimoja na amekubali lakini kwa sherti la semista inayofuata. Hadi amalize kwanza pango yake anapoishi..” alifunguka Reeny.



“Yes Good!, fanya kama tulivyokubaliana. Nashukuru sana Rey... no! Reeny.. ahyi!” Roy alikuwa amechanganyikiwa sana. Reeny alitikisa tu kichwa kwa masikitikiko, yani hadi yani Roy anasahau hadi jina lake?. Hana chake kabisa. Amelima kwenye Maliasili ya serikali.



“Sawa!, aya wewe muweke karibu sasa.. ili niwe na urahisi kumjenga kama mke. Kazi yangu imeisha hapa kwa muda huu. Tukimaliza semista nahama hostel. Naenda kuishi nae chumba kimoja!... (akigeuka na kumkazia macho Roy).. Ukizungua tu kwa kutonikumbuka. Namnyonga humohumo chumbani.Namuua!” Reeny alikua mboga pasina kuweka chumvi ya aina yoyote. Alipomaliza kauli hiyo alinyanyuka na kuondoka bila kuaga.



“Ah!, ama Reeny kiboko. Siku tatu tu tayari amemaliza kila kitu!. Amewezaje kumwingia kirahisi hivi? Au ndio kila shetani na mbuyu wake?.. ahsante Reeny kazi kwangu sasa”.



Roy kwa kweli alikuwa ni mtu ambaye amekufa kabisa. Hakuonyesha kupumua kabisa katika dunia hii ambayo wengi tunaishi. Sasa alikuwa anawaza kujenga dunia yake ambaye hakuna mtu zaidi ya yeye na Rehma bin Juma. Mioyo yao iliungana kweli kweli. Roy alikubali kuacha kila aina ya ‘Ufuska’’ ili tu awe mtulivu kwa Rey.Aliweka ahadi kwa Mungu ya kubadilika na kuwa baba bora baadae.



UPANDE WA II.

“UMEONA TANGAZO?” Sophia aliuliza akiwa kifua mbele usoni mwa Rey.



“Laa!!, Boom au?” alijibu Rey akiendelea kuandika.



“La kasheti na vimbama!, nyoo!” alijibu Sophia. Macho mazito yakishindwa kuinuka vizuri.



“Shoga angu! naona kama una ka usingizi hivi.. hahahaha!”



“Si unataka nikubembeleze twende nyumbani?, Rey kama umetumwa na kijiji?” Sophia aliongea huku akifunika daftari la Rey.



“Namalizia bhana!” alideka kidogo Rey na kufungua daftari lake kisha kuanza tena kuandika.



“Ko vipi na kuhusu hilo tangazo!. tutahudhuria au?”



“Wapi?? Hapo New Lecture C!” Aliuliza macho yakitazamana na Sophia, Sophia alitikisa kichwa tu. Anatarajia jibu akiuliza swali lakini anapokea tena swali baada ya kupata jibu.



“Jibu ndio au hapana!” Sophia aling’aka.



“Hapana!”



“Ko hutaingia huko!. Utaenda wapi?”



“Nop!, sijawahi hudhuria Festival kama hizo, we tamasha liankuwa fujo tu, utaenda tu mwaya!”



“Lakini ni muhimu, Barnaba Boy atakuwepo!”



“Haha, hata angekuwepo Baba wa Taifa, nisingenda!”



“Khaa!, na Roy?”



“Kafanyaje?”



“Angekuwepo yeye?”



“Ningeendaa!”



“Nyooo!”



“Hahahaha” wote walicheka, utani ulikuwa sehehemu yao kama kiburudiko.



Iliwachukua nusu saa kuongea na kutaniana, hatimaye Rey akanyanyuka na Sophia, na safari ya kuelekea kwao ikaanza. Kila mmoja akieleza kwa jinsi ambavyo njaa na usingizi vinavyowasumbua. Mdogomdogo wakiwa njiani mambo yakapamba moto.



“Sophie nina mambo mengi kichwani… na sijui nikueleze vipi, nahisi kusita kukuambia yote!” Rey aliweka begi lake chini na kuongoza mazungumzo.



“Na useme yote!,ole wako unipe nusunusu!” alijibu Sophia.



“Moja ni… ah!, kwanza ngoja nikuulize kitu!.. (Akaondoa mtandio wake kichwani na kuacha kitambaa kingine ambacho anapenda kuvalia kabla ya mtandio. Rangi yake nyuepe pee ikaangaza kila kona ya chumba na kuacha kimya kikitawala, akauliza).“Vipi kuhusu semista ya pili Sophy?, unapanga?” mwisho akauliza.



“Ah!, dear!, ni changamoto sana. Naenda kuishi na mtu ambaye sijamzoea kabisa!. Kabisa. Ungewai wewe mapema basi ningeka na wewe!. Mariamu sijamzoea kiviile!” alijibu kwa kutoa maelezo, shingo ikilegea kusikitika.



“Kwahiyo unapanga si ndivyo?” Aliuliza tena Rey.



“Ndio! vipi wewe?”



“Nami pia!”



“Enhe! unakaa na nani mwaya?”



“Irene”



“Ndo yupi?”



“Huwezi mjua, ila dada mmoja smart sana. Pia kuna faida nikikaa na yeye!. Nataka nimtumie katika jambo langu.”



“Jambo lako!, enhe jambo lipi?” Aliuliza kwa mashaka Sophia. Hakuonekana kupepesa macho.



“Mdogo mdogo tu Sophy wangu, utajua kila kitu!” alijibu kwa makato.



“Enhe jambo lingine unalotaka kusema ni lipi?” akambana Rey azungumze jambo la pili.



“Ah!, Mchumba!. Nashindwa jizuia na mapenzi. Kuna kitu nataka kufanya ila nahisi nitachanganya kwa sasa!”



“Kipi?”



“Ah!. Roy tena!. Roy, RoySon. RJ…”aliongea na kuinama chini. Sophia alimtazama tu.



“Kuna Jeffrey afu kuna Roy… aah!. Shit!” Rey alianza kuwa kama mtu aliyepagawa. Alishika kichwa chake na kuendelea kuinama chini kama anatunga sheria. Alionekana kuchanganywa sana na watu hao wawili.



“Jeffrey ndo nani?” Aliuliza Sophia kwa kushanganzwa na jina mpya.



“Ah!, Mtu wangu!. Naye hayupo hapa. Don’t mind hana madhara, shida ni huyu Roy!”



“Bado sijakuelewa mama!. Who is Jeffrey??..” swali la nguvu likafuata tena.



“Is my Lo…. My previously lover!. My Ex!” alijibu pia kwa mkato.



“Mh!. Mwe!!, sasa kama Exboi, wa nini mahari hapa na unamchanganyaje na Roy?”



“Dear hadi nahisi kupagawa, ndio maana mie nashindwa kung’amua... ah. Naomba nipate mda tafadhali.



“Yupo wapi huyo Jeffrey au bado anahadhina kwako ambayo anaitaji kuirudisha mikononi mwake?” Aliuliza tena Sophy.



“Sophy!, Sophy Eh!. Niache basi mpenzi!” Rey aliongea kwa kuzuka. Alipaza sauti ndani kote. Hata wale wadudu ambao hawaonekani kwa macho walitulia kumsikiliza. Ndani kukawa kimya. Sophy akabaki na mshangao wake!, asijue wapi pa kuanzia. Mwisho akatoka kitandani kwa Rey na kimya kikafuata.



“Rey!, ukiyasindikiza mapenzi jua kabisa utachelewa kurudi… yatakutongoza uyafikishe hadi kwao!, ukikubali tu kuyasindikiza mapenzi. Umekweisha. Kwisha kazi kabisa. Sijui hata umeangukiaje huko!...” Sophia alibaki kujiongelea mwenyewe tu kitandani kwake, alishindwa jinsi ya kumtibu rafiki yake huyo hadi alipofikia hapo. Kitanda kilikuwa hakitoshi kwake aligeuka na maneno yake hadi kukaribiamasaa ya jioni.

-----



INAENDELEA…

PATA SIMULIZI HII YOTE KWA TSH. 1000 TU. WASAP NAMBA 0672493994. AU NITUMIE INBOX SMS.
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 11

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email; xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------



ILIPOISHIA…



“Rey!, ukiyasindikiza mapenzi jua kabisa utachelewa kurudi… yatakutongoza uyafikishe hadi kwao!, ukikubali tu kuyasindikiza mapenzi. Umekweisha. Kwisha kazi kabisa. Sijui hata umeangukiaje huko!...” Sophia alibaki kujiongelea mwenyewe tu kitandani kwake, alishindwa jinsi ya kumtibu rafiki yake huyo hadi alipofikia hapo. Kitanda kilikuwa hakitoshi kwake aligeuka na maneno yake hadi kukaribia masaa ya jioni.

-----

KIPANDE CHA 11.



PENZI UCHANUA AHSUBUHI;

Mapenzi baiana ya Roy na Rey yalianza kuchanua kwa kasi sana, kila pande ikijihidi kuonekana na upekee wa kumpenda mwenzake. Hisia zao hazikuachana mbali sana kiasi kwamba washindwe kuelewana mapema. Kila mmoja alijawa na penzi la dhati la mwingine.. ilikuwa ni siku mpya ambayo Roy alimweka mbavuni Rey kwa mazungumzo ya kina zaidi. Mazungumzo hayo yalifanyika yakiwa rasmi kabisa uwanja wa mpira wa miguu ya Duce majira ya saa moja ya jioni.



“Rey Mama!, mbona kama waniogopa hivi… nakutisha au?”



“No!, No Roy.. unajua.. ah! Haha!. Hamana Babaa, nipo vizuri!” alijibu akilibinua jicho kumchungulia Roy kiwiziwizi.



“Au.. wanionea aibu nini mamaa..!” Nae Roy hakuacha kujimwambafai kwa Rey. Macho yao yalipokutana walioneana aibu. Rey akingata kucha za kidole cha shahada mkono wa kushoto na Roy akikandamiza lipsi zake kwa meno juu na chini.



“Roy!, unaweza kuniambia kitu na nikakuamini?” aliuliza Rey.



“Bila shaka!. Nina memgi ya kuwasilisha kwako!. Naomba samahani kwa kuwa sitaweza kuwasilisha hayo yote kwa kutumia maneno. Naomba nipe mda kukuaminisha kuwa nakupenda Rey!..” alijimwaga Roy.



“I See!. Naona kwa vipi unaniwaza katika moyo wako!. And kama ungepata nafasi yaw ewe kuwa mimi basi ungejionea upendo huohuo ulionao kwangu, name nanao. Roy!. Mda ukifika nikikuambia nakupenda!. Basi amini hivyo nakupenda!” Rey hakuwa mbali na Roy. Aliendelea kujisherehesha mwenyewe na moyo wake.



“Rey!, sema chochote name nitafanya!...”



“Mhhhh!, kweli?”



“Ndio… hata mda huu!”



“Ni kiss!!!..” alisema Rey huku macho yakiona aibu kutazama uso wa Roy. Roy alibaki kinywa wazi asisikie vizuri jambo hilo kutoka kwa Rey.



“Real?” aliuliza.



“No!, bado hujanipokea kumbe!. Let me wish yu…” aliongea kwa sauti ya chini akikusanya mkoba wake tayari kuinuka.



“Mamaa!...” aliita Roy akisimama pamoja na Rey. Wote wakasimama na kupimana vimo vyao. Urefu u karibia kufanana japo Roy alipanda zaidi. Wote wembamba wa kunufaika, sio wembembe ule wa fagio za chooni.



“Abee!”, aliitika Rey akiikunja mikono yake yote miwili mbele ya macho yake. Roy alimsogea hadi pale alipo, alichukua mda kidogo kumtazama Rey anavyojinyonganyonga kama msichana ambaye amemkoea baba yake mzazi kwa kushika mimba angali anasoma. Alitabasamu Roy.



“Sasa naona amani katika moyo wangu!. Mbingu zimefunguka kunionesha upendo huu ambao nilikuwa nausuburi kwa muda mrefu!. Karibu kwenye moyo wangu Rey!” aliongea Roy kimoyomoyo kisha kumvuta kidogo Rey. Rey alikuwa kama amemwagiwa maji.



“Can I Kiss You!” aliuliza Roy macho yakiwa mdomoni mwa Rey ambaye anatamani kuongea kitu lakini anakosa nafasi ya kutoa sauti. Anabaki kumeza mate tu Rey.



“Mamaa!” aliita Roy



“Abee!!” Rey alijibu. Roy hakuongea chochote kile zaidi ya kuchanua tabasamu lake kama yale makreti ya mayai ya kuku wa kienyeji.



Alichukua mkono wake wa kulia na kumpapasa Rey kwenye paji la uso kama anamfuta jasho hivi. Mkono huohuo wa kuume ulishuka hadi shingoni mwa Rey. Ukaibana vyema shingo Rey kama anamkaba ili kumpotezea uhai. Mwishowe alimsogeza taratibu hadi karibu na mdomo wake. Akakutanisha ndimi zao taratibu huku mapigo ya moyo kila mtu yakisikika kila pande.



Walichukua takribani sekunde ishirini kusimama hivyohivyo kabla Rey kushituka na kumsogeza Roy. Akafuta matemate yaliobakia kwenye lipsi zake kwa kutumia kiganja chake uku mengine akionesha kuyameza kabisa. Akalegeza jicho hadi Roy ambaye aliduwaa palepale bila kuganduka. Rey akawasha miguu yake kwa hatua za haraka na kumwacha Roy palepale. Roy alizikata dadika akiwa palepale!. Alitikisa macho tu na mdomo wake ambae aliendelea kurambaramba masalia ya tamu aliyotoka kuramba mda mchache.



Rey alitoweka kabisa nje ya chuo na kwenda zake hosteli anapoishi, Roy alibaki hapohapo uwanjani hadi saa mbili kamili za usiku asijue nini anafanya. Alikuwa mtu ambaye amelegea kabisa kwa penzi la Rey. Hakuna alichopoteza kwa siku hiyo. Akaweka alama ya umaisha kwa mrembo wake Rehma.



SIKU YA TAMASHA…

“Wote sema D.U.C.E..!,” ni MC. Makubi akishika nafasi ya kusherehesha umati.



“DUCEE!!..” umati ukaitika.



“Sey DUCEE!”



“DUCEE!..”



“Alright!!, Alright Alright!!!, Dj… Shikilia hapoo!...!, tunafanya kama Vible ndo linaamka au niadje!!...”



“Ndiooo!..” umati ukishangilia kwa kelele za aina yake.



“Ora, Ora Oraaaaa!... oya wanangu wa hukuu, bado sijaona!.... piga keleeee!!!... naaaam!. Itifaki kuzingatiwa!. Ratiba kwa mukono na anayefuata kwa burudani ni… kriiiiiiiiiiiii…. Ni… ni… Mr. Promise! (Mc Makubi akifunika karatasi la Ratiba kuishika MIC kwa mikono miwili.. jasho likimmiminika mwili mzima.) Mwuiiiiiiite!, Dauce Mason!....!!! (Watu Oyooo!).



“Eviction order, kazi sina.. bosi kachachamaa…

Kudate uoga, mi ni mtu mzima, nilinde na tamaa…

Nitaleta posaaa.. sina lengo la kukuchezea we..

We kisima mi oda, we ndo changu kigoda.. (ni bora).

Nipoteze vyote nibaki na wewe my lover..

Na usijezuga, konakona: ukanivuruga’ ka maradona..

Ni Promise… I want to marry you!.”



Wakati Dauce anaendelea kudondosha hoja zake kwa mwandani wake.. akimpa ahadi ya upendo wa dhati na ahadi ya kuwa wote maishani, pembeni kabisa mwa ukumbi alikuwako Roy na Rey wake!. Wote wawili wakiendelea kupata ujumbe ambao unawahusu kabisa. Kila mmoja akimhaidi mwenzake kwa kutomuangusha hadi mwisho wa maisha yao.



“Umesikia mashairi hayo Mama!...”



“Yeah!. Lakini hayo ya Dauce.. nataka yako!” alijibu Rey huku akiendelea kujimwemwelesha na mdundo maradidi uliosambaa kila kona ya ukumbi hadi hadi watu kushindwa kusikilizana vizuri.



“We subiri tu!, baada ya kutoka Barnaba basi nitaingia mimi… nitaimba sana na hutaamini!.”



“Ohoo, hayupo Barnaba!”



“Si walisema yupo lakini!..”



“Nop bado hajaja hadi muda huu!!..”



“Uhh. Umejuaje?”



“Ah!, si watu wakubwa Roy!. Hayupo Barnaba hapa!”.



“Ok, achana na Barnaba hapa. Kuna jambo nataka kuongea na wewe!. Ukishakinai kusikiliza musiki basi niambie nikueleze.”



“Mhhh, me kwenye muziki hunitoi!, and also neon lako ni muziki tosha kwangu!. Unaweza niambia tu Babaa” Rey aliringa na macho yake mazuri ambayo yalimpa shida Roy kuyatazama vizuri kutokana na mwanga hafifu wa ukumbi. Walizima taa zote za nyuma na kubaki taa za mbele ya jukwaa tu.



“Rey!, saa sita hii na dakika nne!. Naomba uongozane name!”



“Yahp.. nimekaa hadi mda huu huku chuo. Najua nipo na mtu ananilinda. Tutaongozana tu dear..”



“No.. bado hujanielewa..” Roy aliongea na kuvuta pumzi ya kumuelewesha vizuri kipenzi chake.



“Ah!, Rey I mean… tunaongozana hadi napoishi mimi, ukapajue tu japo!”



“Kupajua?, Now!” aliuliza kwa mshangao. Kupajua sa sita za usiku. Alichoka Rey.



“No!, usiwaze vibaya Mama… kwenu kule hakupo salama saana.. utalala hostel kwetu, na mapema tu ntakurudhisha!...” aliongea Roy huku uso wake ukiona aibu ya kutamka maneno ya ajabu.



“Unataka tukafanye mapenzi?” aliongea Rey bila kupepesa macho. Sura yake ikiwa makini mno na kupeteza furaha yote ya mwanzo.



“Hapana, hapana Mama, ni mapema mno kufanya. Bado nahitaji muda wa kujiaminisha kwako kama sina lengo baya na wewe…, just sleeping tu!, basi. Hakuna kingine.”



“We unaweza kulala na mwanamke chumba kimoja bila kumsumbua?”



“Eh, Ah. Ndio. Kwa upande wangu naweza nina selfcontrol..” alijibu Roy akiwa hana imani na Rey. Alijua Rey amechukia kwa kauli yake hiyo.



“So, unataka tukalale pamoja leo?”



“Ndio, Rey!!. Nina jambo zuri naitaji share na wewe!. Tukiwa pamoja leo itakuwa vizuri sana sana. Utanipa nafasi ya kuwasilisha kile ambacho ninacho moyoni. Nakupenda Rey niamini…”



“Da, unanipa mtihani dear… kwa kweli siwezi!” alijibu…



“ohp!” hakuwana cha kuongea Roy alibaki kimya tu!.



“Ok, fine. Tunaenda kulala. But ole wako unishike!!!. Narudia tena Roy.. OLE WAKO UNISHIKE!”



INAENDELEA…

PATA SIMULIZI HII YOTE KWA TSH. 1000 TU. WASAP NAMBA 0672493994. AU NITUMIE INBOX SMS.
 
RIWAYA: LOVE SPEAR 12

MTUNZI; AUTHOR XAV

NAMBA; 0672493994

Email; xavemmanuel12@gmail.com

----------------------------

ILIPOISHIA…

“Da, unanipa mtihani dear… kwa kweli siwezi!” alijibu…



“ohp!” hakuwana cha kuongea Roy alibaki kimya tu!.



“Ok, fine. Tunaenda kulala. But ole wako unishike!!!. Narudia tena Roy.. OLE WAKO UNISHIKE!”



KIPANDE CHA 12;



“Usijali mama, nashukuru Rey unaonyesha kwa jinsi gani unanipenda!. Hakika Mungu hajakosea kabisa kunionesha wewe. Nakuhaidi sitakushika hadi Asubui!.”



“Ah Rehma!!. Mpumbavu wewe!. We si umenikatalia mimi hutafika wewe!. Masikini!” Sophia alitokea upande wa nyuma na kumvaa kipenzi chake Rey.



“Usinifokee..!” alijibu Rey huku akicheka.



“Jamini wewe dada utakuwa muuaji…” Sophia alikazia.



“Ni.. Emergencey kipenzi..” alijibu kwa ustaharabu Rey.



“Mh, haya!. Kaka Mambo!” alijisalimisha kwa Roy.



“Poa mambo?” alijibu Roy.



“Roy!,” aliita Rey baada ya kusikia sauti ya Roy. Roy hakujulikana mwanzo kutoka na kofia aliyoivaa hadi machoni.



“Makubwaa!...” Sophia alitoweka mahari hapo haraka mno. Mbio mbio hadi kwa wenzake ambao nao walikaa upande mwingine mwishoni kabisa. Walikuwa si chini ya wanawake sita!.



“Wapenzi, kumbe hatujakosea mwe!. Ni yeye!. Ni Roy!” alimwaga mchele ule mbele ya kabineti lake. Wote walishangaa na kupiga mayowe chumba kizima huku sauti zao zikishindana na sauti ya mziki.



“Me si nilikuambia?... Ni yeye!.!” Suzy Mogella. Akiwa wa kwanza kuitika ujumbe ule..



“Ko Rey ameshawishika na mjumbe wake!. Yururuu… ama bucha halikosi nyama.” Yusra nae kama kawaida yake.



“Sasa Sophia nawe mbona hata hujafanya ka tukio sasa… au Yu twende palepale tukamchokoze mjumbe!...” Farida naye akaweka lake.



“Weeeee.. mwache Roy wangu. Kwanza bado nampenda mimi nisiwafiche!...”



“Haha, ko kumbe unamziba Rey afu na wewe unataka…? Hehehee!. Kizuri kula na wenzakooo!...” Mariamu akachangia.



“Ila mwenzetu amepiga hatua nzito kweli yani.. hadi wanakaa hadharani vile?. Mhhh wakati sisi tulipewa kapenzi katamu kidogo tena kwa siri…” Yusra akaongeza.



“Ila kapenzi kake kazuri kwa kweli... sema basi tu…” Farida tena, hakusita kuongeza.



“utakuta tumekosa wapenzi… Kelvin na Mwana wapo kulee… Willy na Leah wapo kuleeee…. Nickson na wake nao walee…. Nashangaa sisi hapa tupo sita afu wote wanawake.. hahaha!.” Saudath naye hakubaki nyuma. Akawapayukia wenzake.



“Ila kweli… tukitembea sitasita, tutalemaa… sasa naanza kuwakatakata!... shwaaapu!, nyie wawili mtakua bibi na bwana… Shwaaaapu!, nyie wawili mtakua bibi na bwana… na sisi wawili tutakuwa hivyoo mimi bwana na Farida bibi sawa!! hahahaha!” Yusra akanogesha maongezi na kufanya kusahau kabisa kuangalia stegi na kujikuta wanahangaika na mambo yao…

--



“Hiii… Roy! Mwone Eunice alivyopendeza!”. Rey alisimama kumwangalia vizuri mwanamitindo aliyepita mbele kuonesha ulimbwende wa mavazi.



“Wooow!, Eunice.. yupo vizuri!” aliwehuka Roy.



“You know her before?” aliuliza Rey akiganda kuangalia muenendo wa mwanamke huyo…



“Unamaana gani?”



“Ulimjua toka mwanzo?” aliuliza tena Rey na sasa alikaa kwenye kiti.



“Yeahp.. she is my friend!. Just friend tu!” alijibu Roy japo kwa kubabaika.



“No more?” aliuliza Rey akimtazama Roy kwa macho ya wivu.



“No!.. hakuna lolote!. Hata urafiki wenyewe ni wa kufifia!” alijibu tena Roy.



“Real?” aliuliza tena Rey kana kwamba alishafahamu kitu kuhusu Roy na Eunice…



“Darling… Yunny ni rafiki angu tu… and No more!. Kama kuna kingine basi ilikua mwanzo na sio mda huu…” alijitetea Roy.



“Ok!. Tuachane na Eunice, nataka nikuulize swali!”



“Unaweza Mama” Roy alimruhusu Rey kuuliza swali wakati huo moyo wake umeanza kucheza tayari. Alihofu Rey amejua uhusiano wake wa mwanzo na Eunice.



“Katika maisha yako ushawai kumpa mwanamke ujauzito?” aliuliza Rey akionyesha umakini mkubwa kwa Roy. Roy nusu ajikojolee.



“Nani Eunice!!.. No!... sikumbuki…” alijibu kwa kubabaika Roy.



“Yunny kaingiaje tena hapo wakati tumesema tumwache?. Au jibu la swali langu lipo kwake?”



“Yahp. Tumwache.. and kuhusu ujauzito bila shaka kweli kuna mwanamke alishawai niambia ameshika ujauzito wangu!. Kwa kuwa sikuwa na hakiki… ah!. Sikujua hiyo kesi imeishia wapi… naa… kwanini umeniuliza hivyo dear?” Alihamaki Roy.



“Hapana ila Eunice ni rafiki yangu!” alijibu Rey akiendelea kumtega Roy.



“Oh!, Shit!. Nakumbuka umeniambia kuwa tusimwongelee Yunny. Ok ok ok, sawa.. rafiki yako kwani mlishawai kuongea labda?



“Kuhusu nini dear one!?..” alijibu Rey huku mkono wake ukiivua kofia ya Roy na kuchezea nywele zake. Moy wa Roy ulianza kuruka viunzi vya mashindano ya dunia.. ulikuwa unakimbia riadha ya kuepuka mkenge.



“Alishawai kukuambia labda… yaani I meaaaan.. I, (akimeza mate kidogo na kuangalia pembeni), yani Eunice alishawai kukugusia lile suala lake la kupata…. Oh No!. umesema tusimgusie e?” alibabaika Roy.



“Unajua nini RJ, mie ni mtu mzima.. and nishaexpress kila kitu kuhusu mimi kwako.. usiwe mficha maradhi dear!.. kama kuna jambo lolote usisite kuniambia kuliko uje unitese mbeleni au unisumbue mimi nitafute ukweli!. I want to know all your relationship before. Sorry for that.. and we should start afresh… tuanze upya My, au we unasemaje!?” alimpoza kidogo Roy.



“Yea. Ya. Ni kweli RJ. Dear One.. mimi sipendi sana kuchimbua makaburi yaliokwisha zikwa tayari... let’s start afresh!. Na… nitakuambia kila hatua ambayo Mungu alinijalia kupita. Na kuhusu Eunice..” hakumaliza Roy akazibwa mdomo na kidole.



“Tusimwongelee!.. or unataka niwe bored?” Rey aliongea akipunguzia sauti sikioni mwa Roy.



“Ok, Ok!”. Ikawa nafuu kwa Roy. Akashusha pumzi na kuipachika tena kofia yake.



“So, tunaweza enda mda hu?” aliuliza Rey.



“Wapi?” alijibu Roy



“Mhhh”, aliguna tu Rey na kisha kumnyanyua Roy hadi nje ya ukumbi. Wakaja kutokea kwenye ngazi za jingo la vioo.



“Roy. Mwanzo umenitongoza. Umesema nipajue kwenu usiku huu.. muda umefika, na nimekumbia twende, unauliza tena wapi. Unataka kunighairi My!” Roy alijizungusha kila kona ya ngazi. Kama angekuwa mlemavu wa miguu basi mwili wake ungeanguka kwenye chumba kimoja wapo kati ya Room A, au Room B.



“Tukalale?” Roy aliuliza tena, alikuwa kama bwege.



“Oh!, masikini weee!” hakujibu Rey. Alimshika tena Roy na kushuka naye ngazi hadi chini kabisa. Wakashika korido ya kuelekea ofisi za Daruso, mwishowe kukata kona hadi korido ya kuelekea Vimbweta vya Hall Three, hatua kadhaa wakaangukia nje ya geti. Rey bado alimsika bayana Roy kama mwizi aliyesakata wizi kwa takribani milongo minne. Na sasa alikuwa ametiwa nguvuni na jemedari, kamanda, komandoo wa kikosi cha siri. Hakuponyoka Roy. Alibaki kucheka tu na hoyo yake kwa kutimia hazima ambayo iliitafuta kwa muda mrefu.



“Dear one!. Sipajui Baba.. niongoze..” Rey alideka kwamba hafahamu hata njia ya kuelekea anapoishi Roy. Roy akachukua nafasi ya kumuegesha Rey ubavuni mwake na tayari kuvuka barabara kuelekea machinjioni. Siku ya Eid ya kuchinja iliwadia. Walikongojana kuianza Keko Machungwa.



“Your so pretty girl!. I wonder; why don’t you reach Dilazi?” Roy aliendelea kumshangaa mwenzie kwa kutopajua Dilazi. Mtaa maharufu kuliko yote Keko.



“So ukiwa mzuri, lazima ujue kila sehemu?” Rey naye hakuwa mchovu, alimtwanga swali Roy bila kusita. Akabaki kumungunyuka tu na midomo yake.



“it’s one among of the famous place all over the Keko!”



“We wapajua Tanga?” aliuliza kumkomoa Roy.



“No!..”



“It’s most beautful, shine and famous region than Dar Es Salaam!, so stop complaining!!” alimkomoa kabisa Roy. Kuwa mzuri sio sababu ya kufahamu au kupajua kila sehemu. Hapa Roy alijiisi anahitaji kuanza upya elimu ya msingi. Kidevu chake chenye ndevu chache kikainama kwa aibu na mguu kuingia hostel anayoishi…



“Welcome!...” alikaribisha Roy laikini aliyemkaribisha bado aliganda mlangoni.



“Kwetu, kumkaribisha mtu unaanza na mguu wa kulia na si wakushoto!” aliongea Rey.



“Unamaana gani?”



“Tumia lugha Mama kumkaribisha mtu!. Nadhani neon Karibu linamaana sana kuliko ilo Welcome?”



“Rey!!.. I’m Sorry!”



“Ee, na huo ndio mguu wa kulia. Mkaribishe mtu kwa tahadhari ya anapoenda. Mfano ungekuwa kwetu ningekukaribisha kwa kilugha…” Rey alionekana kumzidi Roy baadhi ya jumbe za maisha.



“Karibu….” Alijitahidi Roy kumkaribisha Roy. Hostel nzima ilikuwa kimya mno. Pasi na shaka wote waliitwa na Barnaba huko Duce. Ukawa mpenyo wa wawili hao kupita bila aibu usoni.



“Karibu tena Rey!... na Asante kwa kuniamini!, take a seat!”



“Seat!... Dear One.. nimechoka kwisha… naomba tulale!” alideka Rey na tayari bila kupoteza wakati alianza kuangusha baadhi ya vitu chini ya sakafu. Akapunguza uzito kama mtu anayejiandaa kupigana masumbwi ya uzito wa kati. Begi na mtandio tayari vilisharushwa chini ya sakafu.



INAENDELEA…

PATA SIMULIZI HII YOTE KWA TSH. 1000 TU. WASAP NAMBA 0672493994. AU NITUMIE INBOX SMS.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom