Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

Alihitaji sana kufika kigamboni kwa wakati ule. Alihitaji kwenda kuipumzisha akili yake japo kwa dakika kumi, lakini haikuwa Rahisi. Haikuwa Rahisi kwa kuwa bado hakujua Rais wa nchi alipo. Bado hakujua kwa nini mke Wa rais aliuawa ndani ya Ikulu. Hapo akakumbuka kuwa alikuwa ameichukua simu ya Neema. Simu ambayo aliamini inaweza kuwa na mambo mengi ya kumsaidia katika hili. Akaitoa mfukoni na kuanza kuitizama kabla ya kuingia kwenye sehemu ya Ujumbe Mfupi. Akaanza kufungua kusoma meseji moja baada ya nyingine. Kila meseji aliokutana nayo ilikuwa imeandikwa katika Lugha tata. Lugha ya kijasusi. Lugha ambayo haiwezi kuwa ngumu kwa mtu kama Mohamed. Meseji ya kwanza kukutana nayo ilionekana kutumwa muda mfupi uliopita. Hii ilitoka kwa mtu anayeitwa Carl Jack. Mtu huyu alionekana kuwa mgeni hapa nchini kwani mawasiliano yake na Neema Mtobwa Yaliianza siku mbili zilizopita. Alifuatilia sms zile moja baada ya nyingine. Kila Sms alioisoma iliusisimua Mwili wake. Hakutaka kuamini kama kweli Kile kilichokuwa kikiandikwa na Neema kilikuwa Cha kweli. Carl Jack Alikuwa ni Jasus wa CIA aliyeingia nchini baada ya mawasiliano kati yake na Neema. Akaliacha hilo na kuufuata Ujumbe Mwingine, Huu Ulikuwa ukitoka kwa mtu anayejiita Abdulmarick Janeed. Huyu alikuwa Raia Wa pakistan, huyu naye alikuwa kama Carl Jack lakini tofauti yao ilikuwa sehemu wanayotokea na mashirika ya kijasusi watokako. Huyu naye alianza mawasiliano na Neema Mtobwa Siku mbili Zilizopita. Na kila mmoja alionekana kuingia Nchini Tanzania Siku iliopita. Ilikuwa hivyo katika wote aliobahatika kusoma jumbe zao. Hapo akaiona kazi ikirudi kwenye Ubichi. Akaiondoa ile hamu ya kwenda kupumzika. Sasa akaamua kuingia katika kazi ya kuwamaliza hawa watu ambao kila mmoja alikuwa amefikia katika hoteli tofauti.

Muda mfupi alikuwa akiinuka na kukiendea kitu cha tax maeneo ya Shekilango. Akaichagua tax moja ambayo aliiona ingemfaa kwa shughuli kwa usiku ule. AkAeleza sehemu ambayo anataka kwenda. Haikuwa safari ndefu kwa usiku kutokana na barabara kuwa Nyeupe. Kutoka Shekilango mpaka Landmark Hotel si chini ya Dakika sita ama saba, Hivyo haikuwachukua Muda Kufika. Baada ya kufika Mohamed akashuka kisha kulipa harafu akaongoza kuingia ndani ya Hoteli kama Mteja. Hakuwa pale kwa Sababu ya kujipumzisha bali alikuwa pale kwa sababu ya kazi, kazi ya kumpoteza Carl Jack jasusi kutoka katika Shirika la kijasusi la Marekani CIA. Akatokea mapokezi ambapo alikutana na mwanadada mrembo ambaye hakuchosha kutizama hata siku nzima.

''Habari yako Bibie? Alisabahi Mohamed. Binti yule ambaye alikuwa akisinzia akanyanyua kichwa kuruhusu macho yake kumuona mteja aliyembele yake. Hata pale macho yake yalipokutana na tabasamu kutoka kwa Mohamed, Binti hakuweza kutoa Jibu katika salamu bali Macho yake yakatulia Machoni kwa Mohamed. Wakaangaliana kwa Muda bila kuongea kitu, walikuwa wakitizama katika aina fulani ya kujuana. Mohamedi akakiona kitu kingine Cha Ziada kwa binti huyu. Aliiona Hofu, akaiona Hasira na kisha kuliona tabasamu la Dhihaka. Naam! Alikuwa akiangaliana na mtu mwenye taaluma kama yake. Taalum katika kile alichonacho Mohamed. Wakatabasamu kwa pamoja tabasamu ambalo lilimezwa na mlipuko Mdogo kutoka ndani ya Hoteli. Mohamedi Hakugeuka kutizama, hakugeuka Kuangalia huko. Bado Macho yake yalibaki Usoni kwa mwanadada Yule.

Kwa macho yake yaliozoea kuona kisichoonwa, yakashuhudia mikono ya mwanamke yule ikishuka chini. Hakumpa Hiyo nafasi, hakumpa hata sekendu ya kusogeza mkono. Mlipuko mdogo kwa mara nyingine ukasikika. Huu haukuwa mlipuko kutoka ndani bali ulikuwa mlipuko kutoka kwenye bastola ya Mohamed. Risasi ikapenya kwenye Paji la Uso la mwanadada yule. Akatulia bila hata kutupa miguu. Hakusubiri tena akaondoka pale kuelekea ndani. Hatua mbili mbele alikutana na mwili wa Askari ukiwa umelala kifudi fudi katikati ya dimbwi la Damu. Hakuujali wa kuangalia mwili wa Askari Yule. Akaendelea kupiga hatua akiangalia huku na kule. Hatua tano mbele akutana na miili miwili ya wahudumu wa hoteli ile wakiwa wamelala kama alivyolala yule askari aliyempita. Kengele ya Tahadhali ikaendelea kugonga kichwani. Akaendelea kusonga huku bastola imetangulia mbele. Akaupita ukumbi wa chakula na sasa alikuwa akielekea Vyumbani. Macho yake yalikuwa yakizunguka mfano wa Bundi. Alitizama huku na kule, Akatizama nyuma na mbele, bado harufu Ya damu ilitamalaki. Bado Harufu Ya Damu ilinukia puani kwa Mohamedi. Wakati anataka kuinua mguu kuingia ndani zaidi akahisi hakuwa mwenye, akahisi Uwepo wa Mtu nyuma Yake. Kwa silika ya aina yake akageuka huku bastola Ikiwa tayari Mikononi. Alikuwa amechelewa, alikuwa amebugi.. Sekunde Moja alijikuta Akianguka Chini mfano wa Furushi huku bastola akianguka pembeni Zaidi. Hakuchelewa, Akachupa na Kusimama akiwa tayari kwa mapambano.. Hakuipata Hiyo Nafasi, alijikuta akitizamana na Midomo Minne ya bastola kutoka kwa watu wawili wanaoonyesha Hawana Utani. MUDY AKATULIA
 
Back
Top Bottom