Riwaya: M Z I G O

Willy Gamba 1

JF-Expert Member
Jan 5, 2015
352
376
RIWAYA; MZIGO
MTUNZI; AHMAD MNIACHI

SEHEMU YA KWANZA

Niliwasili Dar es salaam saa tisa na nusu alasiri,
ilikuwa ni mapema zaidi kuliko nilivyotarajia. Mvua
ambayo ilinyesha masaa kadhaa yaliyopita ilisaidia
kupunguza vumbi ingawa ilisababisha fukuto la
joto kuzidi.
Watu walikuwa wametawanyika ovyo pale kituo
kikuu cha mabasi Ubungo kana kwamba ni siafu
walioangukiwa na kaa la moto. Miongoni mwao
walikuwa ni abiria ambao wanasafiri huku wengine
wakiwasili. Pia walikuwepo wapiga debe ambao
walileta kero kubwa kwa abiria.
Bonge alinionya kuwa nisipitie sehemu nyingine
kabla ya kumfikishia mzigo wake. Pia alinitisha
kuwa iwapo sitatekeleza maagizo yake, basi
asingenipa malipo yangu kwa kazi ya kusafirisha
mzigo ule. Vile vile alinikumbusha kuhusu ile picha
ambayo ilikuwa inaniweka katika wakati mgumu.
Ni picha ambayo leo inanifanya niwe mtumwa
inanifanya pia nishindwe kuamua iwapo nitekeleze
au nisitekeleze kile nitakachotumwa. Ndiyo ni hii
picha ambayo imenifanya nijikute nakuwa mtumwa
wa Bonge, huku nikitekeleza maagizo yake kana
kwamba yeye ni rimoti na mimi ni runinga.
Kwa sababu ambazo mpaka leo sijazielewa
nikaamua kuvunja maagizo yake kwa kupitia
nyumbani kwangu Yombo buza. Sifahamu kama
kuna nguvu ya ziada kutoka nje ya nafsi yangu
ilinituma kufanya uamuzi huo wa aina yake;
Kuvunja maagizo ya mtu kama Bonge halikuwa
jambo la kawaida. Pengine chuki yangu juu ya
Bonge ilinipa ujasiri wa kufanya hayo yote, lakini
pia inawezekana ni ujasiri wa nafsi yangu ambao
nimetunukiwa na Muumba.
Ilikuwa siku ya tatu toka nikabidhiwe begi lile.
Sikujua kilichokuwamo ndani yake ingawa hisia
zilinituma kuwa huenda ni almasi au dhahabu.
Nilijikuta nikianza kuingiwa na mashaka kwani
nilitishwa kuwa iwapo nitathubutu kufungua tu
basi adhabu yangu itakuwa kifo!
“Hivi kweli nikiufikisha huu mzigo nitaweza
kuepukana na hicho kifo?” Lilikuwa ni swali gumu
ambalo nilijiuliza bila kupata jibu.
Lazima nifungue kwani Martin na Bonge watajuaje
kuwa mzigo umefunguliwa?
Nilipofika chumbani nikalitua begi lile kitandani,
moyo wangu ulikuwa unaenda mbio kama mtoto
aliyemuona daktari akiwa na sindano mkononi.
Martin alikuwa miongoni mwa watu ambao
niliwafikiria sana kila liliponijia wazo la kufungua
begi, huyu ndiye aliyenitisha zaidi, jinsi alivyo!
Ana umbo kubwa lenye misuli iliyojengeka kama
mnyanyua vitu vizito, macho yake ni makubwa
kama kurunzi huku uso wake ukipambwa na kovu
kubwa lililopita katikati ya uso wake likionyesha
kila dalili kuwa kilikuwa kidonda kikubwa ambacho
kilishonwa kwa nyuzi kadhaa kabla ya kuwa kovu
la kutisha. Kwa jinsi alivyo alitosha kabisa
kumnyamazisha mtoto anaelia kwa neno moja,
huyo Martin anakuja, labda awe hajawahi
kumuona.
Pale alipokuwa ananitazama nilikuwa sijamkosea
chochote lakini alikuwa anatisha kama yule nyoka
anayeshambulia kwa kurusha mate ya sumu.
Macho yake yalionesha wazi dalili zote za mtu
muovu kama si muuaji kamili, ni bora kusimuliwa
kuliko kukutana na mtu kama huyo usiku. swali
kubwa nililo jiuliza lilikuwa atanifanya nini
akigundua kuwa nimefungua ule mzigo? Iwapo
alikuwa ananitazama kwa sura ambayo kwake
ilikuwa ya upole lakini kijasho chembamba
kilinitoka, vipi nikutane naye siku ambayo
amekasirika? Halafu ajue kuwa maagizo
waliyonipa nimeyavunja, nini kitatokea?
Bila shaka atanifanya kama alivyofanyiwa yule
mwanamke kule guest. Nilikuwa sijawahi kuona
mtu aliyeuwawa kikatili namna ile. Taswira yake
ilinijia kichwani mara kwa mara, mwili ulisisimka
na kufanya vipele vidogovidogo kama mtu
anayehisi baridi kali.
Maskini Merina, Mungu amlaze mahali pema
peponi.
Shauku yangu ya kutaka kujua kuhusu mzigo ule
ilisababishwa na vitisho vya Martin na Bonge.
Adhabu ya kifo kwa kufungua mzigo tu? Woga
niliokuwa nao ulimezwa kabisa na hamu ya kujua
kilichomo ndani yake, na sasa nilikuwa nimeamua
kuchagua kufuata maelekezo ya nafsi yangu na si
yale ya Bonge.
Laiti wasingenionya kiasi kile nisingekuwa na wazo
lolote juu ya mzigo wao. Ningeufikisha kama
walivyotarajia bila hata kuwa na chembe ya wazo
juu ya kutaka kujua kilichomo ndani.
Kwa mara nyingine nikalikazia macho begi lile
jeusi, lilikuwa kama refarii katika maisha yangu.
Nifungue niishi kwa mashaka au niache niishi kwa
amani. Kwangu lilikuwa jambo zito sana kwani
sijawahi kubeba kitu ambacho sikifahamu.
Jambo moja ambalo lilinikosesha raha ni kuwa
iwapo sitafungua basi nitakuwa na fumbo moyoni,
fumbo ambalo sitaweza kulifumbua maisha yangu
yote. Nakumbuka sana nilipokuwa mwanafunzi
jinsi nilivyoumiza kichwa kwenye mafumbo.
Nilikuwa sikubali kushindwa. Lakini kwa mara ya
kwanza leo nakabiliana na fumbo ambalo gharama
ya kufumbua kwake ni kifo.
Nikubali kushindwa?
Kweli nilikuwa naelekea kushindwa. Lakini kwa nini
nishindwe?
Nikiwa mtaalamu wa mafumbo nilikuwa na kazi
mbili, kwanza mzigo halafu uhai wangu. Lengo
lilikuwa ni kujua kuhusu ule mzigo bila kupata
matatizo, yaani nilitaka kuuwa ndege wawili kwa
jiwe moja.
Nikatabasamu huku nikiwa nalitazama vizuri begi
lile ambalo niliahidiwa pesa nyingi kwa kulifikisha
kwa muhusika bila kuvunja masharti. Fedha
nilizoahidiwa sijawahi kufikiria hata siku moja
kuwa ipo siku nitakuja kuzihesabu achilia mbali
kuzimiliki.
Kwanini kusafirisha lile begi kutoka Mwanza
nilipwe pesa zote hizo? Kutatua fumbo lile kwangu
lilikuwa jambo kubwa kuliko zawadi ambayo
ningepewa na bonge huku fumbo likiendelea kubaki
kama maisha ya kaburini ambayo maiti tu ndiye
anayejua yalivyo.
Haiwezekani! Lazima begi lifunguliwe.
Kabla sijafungua nikapata wazo muruwa kabisa.
Nikatabasamu, Lilikuwa wazo kabambe sana.
Nilitaka niue ndege wawili kwa jiwe moja.
Nilidhamiria kulifumbua fumbo lile bila kupata
matatizo yoyote. Nilianza kujihisi kuwa mshindi
ingawa bado niliendelea kujionya juu ya hatari
ninayokabiliana nayo. Bonge hajawahi kuliona lile
begi likoje kwani lilionekana wazi kuwa ni jipya, hii
ilinifanya niamini kuwa wazo langu litakuwa
muruwa.
Kabla sijafanya lolote nikakaa kitandani kwanza
kisha nikaegemea ukuta nikavuta pumzi kwa nguvu
na kuzishusha, taratibu zikaanza kunijia fikra juu
ya mambo ya ajabu ambayo yanatokea katika
maisha yangu.
Muda huu mfupi ambao nilikaa hapo uliweza
kunifanya niyatazame maisha yangu kama mtu
anayetazama filamu ndefu ya kusisimua. Nilikuwa
kama mtu ninayejitazama mwenyewe kwenye kioo.
Ilikuwa kana kwamba ninajisimulia kitu fulani.
Kabla sijaendelea naomba nikusimulie mwanzo wa
yote mpaka kufikia hapa, kwanza ingekuwa vema
unifahamu mimi ni nani?……
***
Naitwa Kajuna Daudi Kazakamba, ni mtoto wa
kwanza katika familia yenye watoto watatu, mimi
na wadogo zangu wawili wote wa kike Koku na
Waridi………
***
Baadhi ya watu wanaoishi Dar es salaam wana
akili za ajabu sana. Hawapendi kuishi maeneo
yenye nafasi na hewa nzuri. Hupenda sehemu
zenye misongamano ya watu na hususani zile
zilizoko kando ya barabara. Mfano mzuri maeneo
kama Kinondoni na Manzese. Hilo ndilo jambo
lililomfanya baba yangu kununua kiwanja eneo
ambalo liko karibu na barabara. Madhara yake
yalikuwa makubwa kwa baba na familia kwa
ujumla.
Ikiwa ni miaka kumi na mitano toka ajenge
nyumba hiyo akapokea barua kutoka serikalini
ikimtaka kuhama eneo hilo. Katika barua hiyo
serikali ilidai kuwa baba amejenga katika eneo
ambalo linatambuliwa kisheria kuwa ni hifadhi ya
barabara. Kwa masikitiko makubwa kabisa
nikashuhudia nyumba yetu ikibomolewa. Hakuna
fidia iliyotolewa ingawa vyombo vya habari
vikiwanukuu viongozi husika vilitoa taarifa kuwa
waathirika wote wamelipwa fidia zao.
Ukawa mwanzo mpya wa maisha ya kupanga na
kuhamahama, mpaka pale baba alipojenga nyumba
nyingine Mwananyamala baada ya kupata fedha
zake za mafao kutoka shirika la reli Tanzania
ambako alifanyia kazi. Fedha hizi zilipatikana kwa
mbinde, iliwalazimu wazee kuandamana na kulala
barabarani wakati wa kudai mafao hayo. Wakati
mwingine polisi walilazimika kutumia nguvu za
ziada kuwadhibiti wazee hao.
Fedha zote za kiinua mgongo ziliishia kwenye
ujenzi wa nyumba hiyo. Mwaka huo nilikuwa
kidato cha sita shule ya sekondari Tambaza.
Mapema mwaka uliofuata nikahitimu masomo
yangu.
Kama zilivyo hadithi za watoto wengine wanaotoka
kwenye familia kama zetu hapo ndio ikawa tamati
sikuweza kuendelea.
Nikaanza kutangatanga kutafuta maisha.
Nikahama Mwananyamala kwa wazazi wangu
nikahamia Yombo buza. Huko nilihama nyumba
kadhaa hatimaye nikapata sehemu ambayo nilikaa
muda mrefu kuliko nyumba nyingine.
Chumba kimoja, kitanda, ndoo na vyombo vidogo
vidogo vilikuwa vinaonesha taswira halisi ya
maisha yangu. Ulikuwa mkusanyiko usiovutia ndani
ya chumba hicho cha kupanga, hakukuwa na
tofauti kubwa na sehemu inayouziwa pombe za
kienyeji. Niliridhika kuishi maisha hayo kuliko
kumuongezea baba mzigo, kwani biashara yake
kubwa kipindi hicho ilikuwa ni samaki ambao
alikuwa anawauza katika mitaa ya Mwananyamala
na Kinondoni, pale inapotokea hali ya hewa si nzuri
alikuwa anachoma mahindi na kuyauza. Baba
yangu hakuwa mtu anayependa kukaa bila kazi
mwenyewe alijisifu kwa kusema yeye ni zao la
Tanu Youth league.
***
Ilikuwa saa 12.37 jioni. Nilivua sare zangu za kazi
nikazitia kwenye boksi. Nikachagua nguo safi
kutoka kwenye kamba ya nguo. Kamba hiyo
niliifunga kwenye misumari ambayo niliigongea
ukutani. Baadhi ya wenye nyumba hawapendi
mtindo huu wa kutoboa ovyo nyumba zao kwa
misumari. Nyumba niliyoishi haikuwa na masharti
kama hayo, vyumba vyote vilikuwa vimetobolewa
kwa misumari. Kimsingi ulikuwa ni uharibifu ambao
wakati mwingine uliweza hata kusababisha nyufa
ndio maana baadhi ya wenye nyumba walikuwa
hawaridhishwi na hilo. Sisi tulikuwa na bahati
kwani mwenye nyumba alikuwa mlevi hivyo wewe
fanya lolote lakini siku ikifika mpe chake akalewe.
Hakuwa na uchungu sana na nyumba yake labda
kwa kuwa ni nyumba ya urithi. Nilikuwa naamini
kuwa kitu ambacho mtu hukipata bila kukitolea
jasho mara nyingi hakionei uchungu na wala
hakithamini kama kile ambacho amekifanyia kazi.
Niliitazama kalenda ya kampuni ambayo nilikuwa
nafanyia kazi, nikagundua kuwa ilikuwa ni ya
miaka miwili iliyopita. Niliziangalia kwa hasira
picha za watu ambao walikuwa wanacheka kwenye
kalenda ile. Walikuwa na matumbo makubwa
ambayo bila shaka yalikuwa yanawapa shida
wakati wa kupumua na kulala. Hivi hawa
wanakumbuka kweli kuwa kuna watu wanapata
shida duniani au wanajali matumbo yao tu?
Kwenye picha ile kulikuwa na Watanzania wenye
asili ya kiasia na wale weusi kama sisi.
Nikaitazama tena kwa uchungu kalenda ile.
Kalenda mpya zilikuwa zinatoka kila mwaka, ili
uweze kupata kalenda hizo ulitakiwa
kuwabembeleza waajiri waweze kukupatia. Wengi
wao walikuwa ni watu wenye majivuno. Sikuwa na
muda wa kumbembeleza mtu, kazi yenyewe
sikuipenda, tatizo kubwa sikuwa na kazi nyingine
ya kufanya. Kilichonikera zaidi kazi zenyewe
hazikuwa za kila siku huku siku nenda rudi
tukiendelea kuwa vibarua.
Tulikuwa tunarushiwa vikaratasi ambavyo
vimekunjwa, ukifungua unakuta idadi ya siku
utakazofanya kazi kwa mwezi pamoja na malipo
utakayolipwa. Ilikuwa ni kampuni inayojishughuli
sha na utengenezaji wa juisi za aina mbalimbali,
biskuti na mikate. Ilikuwa ni miongoni mwa
makampuni yanayosifika sana kwa kusamehewa
kodi. Nilipata kusikia tetesi kuwa ni ya shemeji
yake kigogo mkubwa wa wizara ya viwanda na
biashara. Roho iliniuma sana, Mungu
ametuzawadia sote hii nchi, lakini kuna watu
wanaoifanya kuwa mali yao.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA PILI
Tulikuwa tunarushiwa vikaratasi ambavyo
vimekunjwa, ukifungua unakuta idadi ya siku
utakazofanya kazi kwa mwezi pamoja na malipo
utakayolipwa. Ilikuwa ni kampuni inayojishughuli
sha na utengenezaji wa juisi za aina mbalimbali,
biskuti na mikate. Ilikuwa ni miongoni mwa
makampuni yanayosifika sana kwa kusamehewa
kodi. Nilipata kusikia tetesi kuwa ni ya shemeji
yake kigogo mkubwa wa wizara ya viwanda na
biashara. Roho iliniuma sana, Mungu
ametuzawadia sote hii nchi, lakini kuna watu
wanaoifanya kuwa mali yao. Hawa ni wale ambao
hata sheria haifanyi kazi upande wao.
Nilizikagua tena zile nguo nikaridhika kuwa ni safi.
Nikavaa shati jeupe, suruali nyeusi na viatu vyeusi.
Sikusahau kufunga tai siku hiyo. Nikaonekana
kama mmoja wa wafanyakazi wa benki kwa nguo
nilizozinunua kwa mmachinga. Nikazikagua nywele
zangu, hazikuhitaji kitana kuzichana. Nikachukua
brashi, nikaanza kupitisha kichwani huku
nikijiangalia kwenye kioo kidogo.
***
Sikuwa mpenzi wa kumbi za starehe lakini siku
hiyo niliamua kusafisha macho. Nguo zile zilikuwa
zinanipendeza sana ilibidi mtu afanye kazi ya ziada
kugundua kuwa zote nilikuwa nimenunua kwa
wamachinga mitaani.
Jioni ile nilikuwa nazunguka maeneo mbalimbali ya
mji bila mpangilio maalum. Hakuna nilichokuwa
natafuta, labda ilikuwa ni furaha ya malipo yangu
kibaruani. Siku hiyo mifuko yangu ilikuwa imenona
kwa noti za kitanzania . Mwisho nikafika sehemu
ambayo nilihitaji kupumzika. Nilikuwa nimechagua
baa moja iliyoko maeneo ya Tabata Mawenzi. Ni
sehemu ambayo inasifiwa kwa utulivu. Nililijuwa
hilo kupitia kwa baadhi ya vibarua wenzangu
wanaoishi maeneo hayo.
Nikakaa kwenye kona ya kushoto ya baa. Vitu
vingi mle ndani vilikuwa vigeni kwangu. Mazingira
ya mle ndani yalikuwa ni ya aina yake. Kuna vitu
ilikuwa ndio kwanza naviona humu ndani. Kubwa
ilikuwa ni staili ya mavazi, hasa yale ya wanawake.
Wengi walikuwa wamevaa mavazi ambayo
yaliruhusu mapaja yao kuwa nje, nilimeza mate.
Kwa upande wa wanaume walikuwa na mavazi yao
ya siku zote, ya kawaida. Sijui kwanini nilipokuwa
kwenye kundi la watu nililaumu sana mavazi haya
ya kina dada, leo niko peke yangu najikuta
nikivutiwa na mavazi haya, tena nilitamani ufupi
wa sketi zao ungezidishwa ingawa kimsingi
zilikuwa zimefika mwisho.
Labda ni unafiki.
Hii ndio baa bwana, starehe nyingi zinapatikana
huku. Mapaja ya hawa watoto wa kike yalinifanya
nipagawe kabisa. Siku nyingi nilikuwa sijaona
mambo ya namna hii kwani toka nianze hivyo
vibarua mara nyingi nilikuwa nashinda nyumbani.
Moyo ulikuwa unaenda mbio kila nilipokuwa
ninatizama vitu adimu namna hii, nilihisi kubanwa
na pumzi kutokana na kuwatazama viumbe hawa.
Kona ya kulia ya baa ile kulikuwa na meza kubwa
ambayo ilikuwa imefunikwa kwa zulia la kijani.
Meza hii ilikuwa imewekwa vishimo sita, vitatu kila
upande. Katikati kulikuwa na mipira midogo yenye
rangi tofauti tofauti. Wazee kwa vijana niliwaona
wakishindana kuipiga ile mipira kwa kuiingiza
kwenye vile vitundu. Walifurahi na kushangilia
lakini nilikuwa sijui kabisa nini maana ya mchezo
ule ambao baadaye nilikuja kugundua kuwa
unaitwa ‘pool’. Kwani siku zile ulikuwa ndio
kwanza unaanza kupata umaarufu nchini.
“Kaka nikusaidie nini?” Nilishtushwa na sauti ya
kike, nikageuka. Duh, huwezi kuamini! Nilishindwa
kutofautisha muhudumu wa baa na mfanyakazi wa
benki. Mwanamke mrembo alikuwa amesimama
mbele yangu. Alikuwa na uso wa duara ambao
ulisanifiwa vizuri na mola muweza kwa ngozi laini
nyeusi ambayo haikuhitaji vipodozi vikali. Macho
yake yalikuwa makubwa kiasi cha kuyafanya
mapigo ya moyo wangu kuongezeka pale
alipokuwa ananitazama. Umbo lake lilikuwa ni lile
ambalo linajulikana kama namba nane.
Nilimshangaa mrembo huyu ambaye hakuwa na
nyongeza zaidi ya urembo wa asili.
“Inakuwaje mwanamke mrembo kama huyu
anafanya kazi baa!” Niliwaza.
“Naomba pepsi baridi tafadhali!” Yule dada
alinitazama kwa mshangao kidogo. Bila shaka ni
kutokana na kujisahau na kumshangaa wazi wazi.
Sio siri alikuwa anavutia. Akatabasamu kidogo
kisha kwa sauti ileile ya kuvutia akaongea.
“ Naomba ulipe kwanza tafadhali ” alisema huku
akinyoosha mkono wake wa kulia. Nikampatia noti
ambayo tayari nilishaiweka kwenye mfuko wa
shati.
Aliporudi alikuwa amebeba sinia likiwa na pepsi na
karatasi laini ikiwa ndani ya glasi. Akanikabidhi
chenji yangu
Niliwaona watu wengi wakinywa vinywaji vyao
taratibu, kwa kuwa nilikuwa na kiu sikuupenda
utaratibu ule. Nikajimiminia pepsi yangu kwenye
glasi, nikanywa ile soda funda tatu za nguvu.
Ndani ya dakika moja na nusu glasi ikawa tupu.
Nikamalizia soda kidogo ambayo ilibaki kwenye
chupa. Ile soda ilikuwa tamu mno! labda kwa kuwa
nilikuwa nakunywa mara moja moja. Sikuwa na
uwezo wa kununua soda kila siku, kwa mshahara
gani!? Hata pale nilipokuwa nyumbani kwa wazazi
wangu bado soda kilikuwa kitu adimu. Soda
ilikuwa haipatikani mpaka ushikwe na homa tena
baada ya kudeka sana na kukataa vyakula
mbalimbali ndipo utaletewa, pia soda ilipatikana
siku za sikukukuu; Hapo familia nzima itakunywa
soda.
Nilimalizia funda la mwisho huku nikiusikilizia ule
ubaridi ulivyokuwa unashuka kooni na kunipa raha
na faraja. Angalau uliweza kunisahaulisha ugumu
wa kazi za vibarua vya viwandani. Nilitamani hali
ile ingekuwa kila siku, lakini zilikuwa ni ndoto na
mawazo ya masikini ambaye kutwa haachi kuwaza
kupata fedha za ghafla na ndoto zilizojaa bahati
nasibu ya kuokota kiroba cha noti au dhahabu.
Ghafla, akaingia mwanamke ambaye alivuta hisia
za wanaume wengi. Kila mwanaume aliyegeuka
kumwangalia aligandisha jicho lake kwa sekunde
kadhaa kisha akarudisha jicho mahala pake. Wengi
walikuwa na wapenzi wao mle ndani hivyo
walijifanya kama hawajaona chochote kumbe
walikuwa wanazuga tu. Niliona mmoja akipigwa
kibao na mtu niliyehisi kuwa ni mkewe baada ya
kugandisha jicho lake kwa muda mrefu zaidi.
Nikacheka! Kwani yule mtu alikuwa na umri ambao
ungemfanya awe anakaribia kustaafu serikalini au
ameshastaafu karibuni.
Sikujishugulisha sana na yule mwanamke, nilijua
wazi hakuwa katika daraja langu. Sikupenda
macho yauumize moyo wangu. Nikamgeukia tena
yule muhudumu, alikuwa anahudumia wateja
wengine. Nikaendelea kumkazia macho ili akigeuka
nimwite kwa ishara ya mkono. Baada ya dakika
chache akageuka nikamwashiria kwa mkono kuwa
nahitaji huduma. Nilimpenda sana muhudumu
huyu. Sura yake ilikuwa na kila dalili ya upole na
busara. Ndio maana sikutaka kumwita muhudumu
mwingine.
“Samahani kaka naweza kukaa hapa” Sauti ya kike
ilinishtua na kunifanya niache kumtazama yule
muhudumu.
“Kaa tu dada, hakuna mtu hapo” Nilimjibu huku
kwa mbali nikihisi mapigo ya moyo yakiongeza
kasi yake. Nilijitahidi kupambana ili nisiruhusu hali
hiyo.
Alikuwa ni yule mwanamke ambaye kwa dakika
kadhaa nahisi alibadilisha mapigo ya mioyo ya
baadhi ya wanaume mle ndani. Sikubabaika, wala
sikuruhusu moyo wangu ushtuke zaidi. Nahisi
wengi mle baa walitamani bahati ile ingekuwa
upande wao, kukaa meza moja na yule mrembo
kwao lilikuwa jambo kubwa sana. Wengine
walilaani kwa nini walikuja na wapenzi wao mle
ndani. Wakati natafakari kuhusu yule Msichana
nikamuona muhudumu akiisogelea meza yangu.
“Naomba Pepsi nyingine tafadhali” Nilitamka baada
ya kumuona amesimama mbele yangu kwa
heshima, Sijui kama ilikuwa ni heshima kweli au
ndio zile heshima za baa za kijana kuitwa mzee.
“Naomba unipatie Redbull!” Aliongea yule dada
kwa sauti ambayo ilikuwa na mikwaruzo kiasi.
Yule muhudumu akaondoa chupa na glasi ya
kwanza bila kusema lolote. Dakika mbili baadaye
akarudi na vitu tulivyoagiza. Yule mwanamke
alianza kunywa kinywaji chake taratibu. Alionekana
mwenye mawazo mengi. Hata kile kinywaji
alionekana kujilazimisha. Kisha akanigeukia kwa
aibu kwani alikuwa hajanisalimia.
“Habari yako kaka!” alinisalimia kwa sauti ya upole
na uungwana.
“Salama dada!”. Nilijibu huku nikiwa sina uhakika
kama sauti yangu ilikuwa
imetoka vizuri, kwani mapigo ya moyo wangu
yalikuwa yanaenda kasi sana. Sijui kwanini huyu
dada alikuja kwenye meza hii, alinivurugia kabisa
amani niliyokuwa nayo kwani nilianza kupotelewa
na ule ujasiri niliojisifu kuwa nao. Alivuruga hata
mfumo wangu wa kawaida wa mawazo. Sikupenda
aendelee kukaa pale lakini nilikuwa sina jinsi.
Kitu kimoja kilikuwa wazi katika macho ya yule
dada, hakuwa na furaha. Hili lilinipa udadisi sana.
Nilitaka kumuuliza lakini moyo ukasita.
Nikaamua kuachana nae. Nikaendelea kutembeza
macho yangu ndani ya ukumbi ule wa kisasa.
Watu walikuwa wametulia kwenye viti vyao
wakinywa vinywaji tofauti tofauti.
“Siwezi! Nasema siwezi……!” Nilishtushwa na sauti
ya yule dada. Tukakutanisha macho. Hapo ndipo
nilipogundua kuwa yule dada alikuwa na tatizo.
Hata hivyo bahati ilikuwa upande wake, wengi mle
ndani hawakuweza kumsikia. Sauti yake ilimezwa
na sauti nzito ya muziki mnene uliokuwa unapigwa
mle ndani.
Kitendo kile cha kuongea kwa sauti kali mbele
yangu kikamfanya ajisikie aibu.
Hakuchelewa akainuka kwenye kiti na kuondoka.
Akawa anasindikizwa na macho ya wanaume
wenye uchu wa fisi.
***
Muda ulikuwa umeenda sana. Ilikuwa ni saa sita
na nusu usiku muda uliotangazwa na serikali wa
kufunga baa ulikuwa umefika. Watu walianza
kupungua taratibu. Nilikunywa pepsi tatu tu lakini
nilikaa pale karibu masaa matano. Wakati nataka
kuinuka ndipo nikagundua kuwa yule dada alikuwa
amesahau kipochi chake pale mezani. Sikujiuliza
nilikichukua nikakiweka mfukoni.
Nilikaa muda mrefu mle baa kwani walionekana
kutozingatia onyo la serikali la kufunga baa saa
sita kamili, nikaamua kuondoka. Kabla sijaondoka
nilitamani sana kuonana na yule dada ambaye
mara zote alikuwa ananihudumia. Nikatembeza
macho yangu huku na huko bila mafanikio.
Sikutaka kuongea nae chochote. Nilitamani
kuingalia tena miguu yake illiyojaa vizuri,
sikumuona.
Nilipofika getini ndipo nikamuona yule dada.
Alikuwa amevaa mavazi mengine. Alikuwa amevaa
sketi ndefu nyeusi, blauzi nyeupe ya mikono mirefu
pia alikuwa amezifunika nywele zake zilizosukwa
mtindo wa rasta ya majongoo kwa kilemba cha
kijani. Nilijiuliza amebadilisha nguo zile muda gani.
Nikamsogelea.
“Habari yako dada!.” Nilimsalimia huku nikipanga
namna ya kuanzisha maongezi.
“poa!” Alinijibu kwa mkato huku akiniremburia
macho. Alionekana kama anasubiri kupewa taarifa
fulani. Nilitishika, lakini nikapiga moyo konde.
Nilikuwa sijiamini kabisa kwani hata pale
nilipokuwa nataka kuongea nilihisi kubanwa na
pumzi.
“Samahani sister, nina maongezi kidogo na wewe.”
Niliongea huku nikijitahidi kuficha woga niliokuwa
nao.Hata hivyo sikujua kama niliyoongea
yamesikika au yametoka kwa ufasaha. Nilijihisi
kama niliyekosea, hata lugha niliyotumia niliona
kuwa si sahihi. Nilihisi kuwa ili kuweza kuwanasa
kiurahisi viumbe hawa basi kulikuwa na umuhimu
wa kuchanganya na lugha za kigeni hususani
kiingereza, sikuamini kama kiswahili peke yake
kinaweza kutosha kumnasa mrembo yule. Hata
hivyo nilikuwa nimetawaliwa na hofu ya kuongea
kiingereza kwa kuchelea kuvurunda kwa kuongea
kiingereza kibovu. Hapa nilimkumbuka sana
mwalimu wangu wa kiingereza Chambuso ambaye
alikuwa anapenda kutukejeli kwa kutuambia kuwa
kiingereza chetu ni kibovu, eti “You know…..” ni
nyingi. Kweli huyu mwalimu alichangia kunifanya
nikose kujiamini .
“Oh! Pole kakaangu, muda umeenda sana halafu
nimechoka tafuta muda kesho tuongee” hapo
nilishusha pumzi kwani angalau aliniweka kwenye
nafasi nzuri ya kujiandaa. Nilianza kuhisi ushindi
ndani ya nafsi yangu. Mambo mengine haya yana
wataalamu wake, mimi si mtaalamu kiasi hicho,
hata hivyo nilianza kuhisi ushujaa kwenye nafsi
yangu, ule woga ambao ulinivaa hapo mwanzo
uliyeyuka nikajihisi furaha kana kwamba
nimezaliwa upya.
“Kama utakuja naomba ufike upande ule kule wa
kaunta, kisha uliza sister Betty!” Alinitazama
akatabasamu. Tabasamu lake lilikuwa kama mkuki
wenye ncha kali kwenye moyo wangu. Nikahisi
kama moyo wangu unataka kusimama. Nikaingiwa
na kitu ambacho nilishindwa kutafsiri ni kana kwamba moyo ulimwaga sumu fulani kwenye mwiliwangu.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA TATU
. Mambo mengine haya yana wataalamu wake,
mimi si mtaalamu kiasi hicho, hata hivyo nilianza
kuhisi ushujaa kwenye nafsi yangu, ule woga
ambao ulinivaa hapo mwanzo uliyeyuka nikajihisi
furaha kana kwamba nimezaliwa upya.
“Kama utakuja naomba ufike upande ule kule wa
kaunta, kisha uliza sister Betty!” Alinitazama
akatabasamu. Tabasamu lake lilikuwa kama mkuki
wenye ncha kali kwenye moyo wangu. Nikahisi
kama moyo wangu unataka kusimama. Nikaingiwa
na kitu ambacho nilishindwa kutafsiri ni kana
kwamba moyo ulimwaga sumu fulani kwenye mwili
wangu.
Tukatazamana. Kuna kitu kilikuwa kinapita kwenye
macho yetu au sijui kwenye macho yangu tu.
Mpaka kufikia hapa napenda ufahamu kuwa
Sikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke
yeyote Yule lakini kwa mara ya kwanza moyo
wangu unaangukia kwa muuza baa ‘Bar maid’ .
Nilimpenda si utani.
***
Nilifika nyumbani saa 7.30 usiku. Eneo lote lilikuwa
kimya kabisa. Sikutaka watu wajue muda niliorudi,
kwani haijatokea hata siku moja ambayo
nimechelewa kiasi kile.
Kwa kuhofia kugundulika, nikautumbukiza ufunguo
kwenye kitasa kwa namna ya kunyenyekea sana.
Hata pale nilipokuwa natekenya kitasa ili kifunguke
bado nilihofia kubainika. Mlango ukafunguka bila
makelele, nikaingia ndani huku nikiwa na furaha
baada ya kufanikiwa kuingia bila ya kubainika kwa
yeyote.
Nilijilaza kitandani. Sikuhitaji hata kuoga kutokana
na kibaridi kilichokuwa kinapiga siku ile. Hata hivyo
umbali wa kutoka chumbani hadi bafuni nao
ulinifanya nisite kwenda kuoga. Wakati nafsi yangu
ikikataa kwenda kuoga, mawazo mengine yalikuwa
yanapita kichwani kwangu. Nilikumbuka jinsi siku
ile nilivyotumia fedha bila utaratibu. Kwa kipato
changu kukodi taksi kutoka Tabata hadi Buza ni
ubadhirifu mkubwa.
“Aa mara moja moja sio mbaya” Niliwaza na
kujifariji mwenyewe.
Mawazo yangu yakarudi kwa Betty. Bado
nilishangaa kwanini aliamua kufanya kazi ya
uhudumu wa baa. Alikuwa msichana aliyeumbika
kwelikweli. Macho makubwa yasiyohitaji
kungumanga ili aweze kurembua. Uso wake
ulikuwa wa duara, mashavu yenye vishimo vidogo
ambavyo unaweza kuviona kwa urahisi pindi
anapotabasamu au kucheka. Kilichonimaliza zaidi
katika sura yake ni mwanya. Ee bwana eeh!
nilikuwa sijaona mwanya mzuri kama ule. Ulikuwa
ni mwanya wa kuvutia. Haukuwa mwanya wa
kuchongwa, ulikuwa wenyewe wa kutunukiwa na
Muumba. Nilikuwa dhaifu kwenye aina hii ya
maumbile. Mwanya na vile vishimo vidogo
vinavyoonekana mashavuni pindi mtu
anapotabasamu. Sijui vinaitwaje vile… Nilitumia
muda mrefu kumfikiria yule mwanamke hadi pale
usingizi uliponichukua.

2

Miale ya jua ilinipiga usoni, nikashtuka kutoka
usingizini. Moja kwa moja nikaelekeza macho
yangu ukutani. Saa yangu kuukuu ilinionesha kuwa
ni saa 2.37. Nikainua macho nikitafuta wapi
nilikovulia suruali yangu usiku. Nilikuwa nimeiweka
juu ya kiti. Nilitaka kuchukua fedha ambazo
zilibakia mfukoni. Nikatembea huku nikipiga
mwayo mrefu wa mtu aliyetoka usingizini.
Nilipoishika ile suruali nikashtushwa na mtetemeko
mdogo uliofanywa na ile suruali.
“Ni nyoka kwenye suruali yangu?” Nilijiuliza huku
nikianza kutawaliwa na hofu.
Bado suruali iliendelea kutikisika huku ikitoa kitu
kama mngurumo mdogo na kunifanya nitamani
kukimbia . Nikapiga moyo konde na kuinyanyua ile
suruari, ikaacha! Sikujua ni nini kiliifanya ile suruali
itikisike yenyewe kwani baada ya kuiinua iliacha
kabisa. Nikiwa nimetawaliwa na woga, niliendelea
kuikagua ile suruali. Nilikuwa nafanya hayo yote
huku nikiwa nimeiweka sawa miguu yangu ili
iwapo kitatokea kitu cha hatari niweze kutimua
mbio.
Nikaanza kuingiza mikono katika mfuko mmoja
baada ya mwingine. Hapo ndipo nilipobaini kitu
ambacho kilinishangaza. Nilishasahau kabisa kuwa
niliokota kipochi ambacho yule dada alikisahau
pale baa. Ndani ya kipochi kulikuwa na simu
ambayo haikuwa na mlio. Ilikuwa imewekwa muito
wa mtikisiko ‘Vibration’ . Nikatabasamu baada ya
ugunduzi huo mdogo kisha nikashusha pumzi na
kupotelewa na hofu ambayo ilinitawala muda
mfupi uliopita.
Nikaitoa ile simu kwenye kile kipochi. Ilikuwa simu
kubwa kwa umbo. Jina lake lilikuwa geni katika
macho yangu. LG maandishi hayo mafupi ndiyo
yaliyoinadi simu hiyo katika ulimwengu wa
watumiaji wa simu. Moja kwa moja nikabonyeza
kwenye menyu ya simu. Sehemu ya kwanza
iliyonivutia kufungua ni ile ya meseji. Watu wengi
wana udhaifu wa kupenda kufungua maeneo hayo
hata kama hawajaruhusiwa. Ni eneo hatari sana
kwani wakati mwingine hutunza siri za mmiliki wa
simu.
Nikabofya kitufe ambacho kilinionesha maeneo
mengi ya kufungua. Nikavutiwa na inbox yaani
sehemu ya ujumbe ambao mwenye simu
ametumiwa, nikafungua.
Ujumbe niliokutana nao ulinitisha kidogo, pia jina la
mtumaji lilinishangaza, Kimeo. Nilikuwa sijawahi
kusikia mtu anaitwa Kimeo labda baadhi ya watu
ambao huhifadhi majina ya mafundi simu kwa
kuwaita vimeo, lakini si jina rasmi la mtu.
“Bila Shaka ni jina la kizushi.” Nilijisemea ndani ya
nafsi yangu.
Mwanamke tekeleza maagizo yetu la
sivyo………………….
Ujumbe ulikuwa hivyo na mtumaji alikuwa Kimeo.
Nikafungua meseji ya pili. Hii ilikuwa na ujumbe
mrefu kidogo kuliko ile ya kwanza. Please, usikose
kufika. Zingatia kuwa zawadi nono ya fedha,
nyumba pamoja na gari inakusubiri. Ukifanikiwa
kumuua Pili. Nikajikuta napatwa na mshtuko
baada ya kusoma ujumbe huo.
Meseji zilizoko kwenye in box zilikuwa zimeisha.
Nikafungua sent items yaani ile sehemu
inayoonesha ujumbe uliokwishatumwa, ‘sent items
empy’ lilikuja neno hilo pale nilipojaribu kufungua,
nikafungua sehemu imeandikwa outbox, Kulikuwa
na meseji ambayo kama ile ya kwanza nayo
ilinitisha kidogo. Kilichonisisimua zaidi ni tarehe ya
ile meseji. Ilikuwa ni tarehe ya siku ile ambayo
tulikutana na yule mwanamke mwenye kipochi kule
baa.
“Yaani ni meseji ya jana?!” Nilijiuliza kwa
mshangao, kisha nikarudia kuisoma ile meseji.
Samahani sana mpenzi wangu, sina imani ndani ya
moyo wangu. Namuogopa sana yule Bonge. Bonge
ataniua tu. Kesho njoo Tabata Kisukuru. ZAWADI
GUEST HOUSE chumba no. 7 saa 12 jioni. Lazima
nitoroke haraka iwezekanavyo na hali jinsi ilivyo
siwezi kulala nyumbani.usikose mpenzi wangu .Ni
mimi nikupendaye Merina Dismas.
Kwa mfumo wa ile simu ni kwamba ile meseji
ilikuwa imehifadhiwa kwenye simu haikutumwa
kokote.
Alitaka kumtumia nani? Nilijiuliza.
Nilitanabahi kuwa najiuliza maswali ya kijinga
kwani ni wazi kuwa alikuwa anahitaji kuonana na
mpenzi wake ambaye kwa muda huo nisingeweza
kumfahamu.
Moyo wangu ulikuwa na hamu ya kujua ni nini
kilikuwa kinamfanya yule dada ambaye kupitia
meseji nilifahamu jina lake kuwa ni Merina, atake
kutoroka mji. Ilikuwa ni siku nzuri kwangu, siku ya
Jumapili. Siku hiyo na Jumamosi zilikuwa ni siku
za mapumziko kwangu hivyo niliamua kufuatilia
suala lile. Sikujua, nasema sikujua, Laiti ningejua
mapema kuwa umbeya ule wa aina yake
ungezusha matatizo makubwa sidhani kama
ningethubutu kufanya nilichofanya.
Kuna kitu kimoja ambacho mpaka hii leo
kinanishangaza. Kwa tabia yangu ya asili huwa
sipendi kufuatilia mambo ya watu. Kilichonishanga
za ni nini kilinisukuma kutaka kujua mengi kuhusu
yule dada. Kimsingi ni mambo ambayo yalikuwa
hayanihusu. Lakini kitendo kile cha siku moja tu,
kimejenga mambo ambayo hayataweza
kusahaulika. Yatabaki kwenye historia kama
kumbukumbu ya aina yake, naamini kuwa hata
kama nitakufa ni vigumu kufutika.
*********

Saa 7.30 niliwasili maeneo ya Nyumba ya kulala
wageni iitwayo ZAWADI pale Tabata Kisukuru.
Sikupata shida sana kuuliza wapi iliko nyumba
hiyo, sidhani kama ni sahihi kuita nyumba ya
kulala wageni. Najiuliza usahihi wa nyumba hizi
zinazoitwa za kulala wageni kwa sababu kila
nilipochunguza daftari ambazo husajili wageni basi
wengi utakuta wanatoka Dar es salaam
wanakwenda Dar es salaam.
Niliposhuka kwenye daladala pale Tabata Kisukuru
maarufu kwa Swai, nikaona kibao ambacho
kilikuwa na maandishi yaliyonielekeza kule
nilikotaka kwenda. Nilifuata maelekezo ya kile
kibao. Nyumba hiyo haikuwa mbali sana na kituo
cha magari kisukuru. Nilifika kwa Swai nikaenda
mbele kidogo, nikaliona kanisa dogo ambalo
limejengwa juu ya muinuko upande wa kulia.
Nikafuata kijia kidogo ambacho kilikuwa kinaelekea
upande wa kushoto. Nilipotembea kama hatua
kumi nikaiona ile nyumba.
Kabla hujafika kwenye ile nyumba yaani hatua
kama kumi kutoka pale ilipo nyumba ile kuna
banda la mkaanga chips, niliamua kwanza kwenda
ili nipate mlo kabla sijaenda kuchukua chumba.
“Habari yako!” Nilimsalimia muuza chips
“Poa kaka mkubwa, karibu sana.”
“Ahsante, naomba uniwekee chips moja.”
“Chips mayai au kavu?”
“Naomba na mayai kama inawezekana niwekee
matatu”
“Usijali mkubwa.” Alinijibu huku akifanya haraka
kuvunja mayai.
Nilikaa pale kwa dakika kadhaa huku nikijaribu
kujiuliza kama nilikuwa sahihi kwa uamuzi wangu
wa kuja huku. Upande mwingine nilianza kujikosoa
huku upande mwingine udadisi wa ule ujumbe wa
simu ukinihimiza kutorudi nyuma. Baada ya dakika
chache mlo wangu ulikuwa tayari.
“Naweza kupata soda?”
“Nipe hela nikuchukulie hapo kwenye kioski.”
“Nichukulie Mirinda nyeusi.” Niliongea huku
nikimpatia noti ya shilingi elfu moja.
Baada ya dakika chache akarudi akiwa na ile soda
niliyomuagiza. Nikala chips huku nikinywa soda
yangu taratibu. Baada ya kumaliza mlo nikanawa
na kufuta mikono yangu kwa leso yangu kisha
nikaelekea kule nilikokusudia baada ya kuhakikisha
kuwa nimelipa kiasi anachodai muuza chips.
Ilikuwa ni nyumba yenye vyumba takribani ishirini.
Ilikuwa imejificha kidogo, Kama si kile kibao
nisingeweza kufika. Mfukoni nilikuwa nimebakiwa
na elfu thelathini tu baada ya kula zile chips.
Sikuwa na akiba nyingine zaidi ya hiyo. Nilihisi
kuwa gharama za kulala pale huenda zikalingana
na hela niliyokuwa nayo.
Potelea mbali.
Nilifika mapokezi, kulikuwa na kidirisha kidogo
ambacho kilikuwa na kiubao kidogo ambacho
kilitokea kwa mbele kidogo kama kikofia. Pembeni
ya kile kidirisha kulikuwa na sofa zuri lililovikwa
kitambaa ambacho kinafanana na ngozi ya chui
kwa jinsi kilivyonakshiwa maua yake. Nikakaa pale
kwenye sofa karibu kabisa na kile kidirisha
ambacho kiliandikwa RECEPTION Msichana
mweusi mwenye nywele ndefu ambazo alizibana
kwa kibanio kwa nyuma akanipokea.
“Karibu kaka.”
“Ahsante habari za kazi.”
“Nzuri, karibu sana.” Alinijibu huku akitabasamu.
“ Nahitaji chumba aunt”. Nilimwambia baada ya
kusalimiana.
“Vyumba vipo. Sijui unataka vya uani au vya
ndani?”
“ Kama inawezekana naomba chumba namba 7”
“Kwanini umechagua namba hiyo?”
“Ndivyo nilivyoelekezwa na mnajimu, kuwa hiyo
ndiyo namba yangu ya bahati”
Yule dada akacheka kabla ya kunijibu.
“Hicho kimeshachukuliwa, tena kimelipiwa toka
jana asubuhi lakini mwenyewe amefika leo.”
“Haya nipe angalau kinachokaribiana na hicho”
“ Labda namba 18 maana vinatazamana”
Nilifurahi sana, ingawa sikutaka kumuonesha yule
muhudumu furaha yangu.
“Shilingi ngapi?”
“Elfu tano kulala, Mapumziko mafupi elfu tatu”
Alinijibu huku nikiwa nimeingiza mkono mfukoni.
Nililipa huku nikiwa nafurahia gharama ile ndogo.
Aliandika kwenye daftari lake la kusajili wageni.
Wakati wa kuweka sahihi yangu ndipo nikapata
mwanya wa kuchungulia jina la yule mwanamke.
Kumbe alikuwa anaitwa Merina. Nikakumbuka jina
lile lililoko kwenye simu Merina Dismas. Nikajiona
mshindi kwa kukamilisha hatua ile.
***
Ilikuwa yapata saa 3.18 usiku. Nilizima taa
ambayo niliona inaleta joto nikawasha ya rangi,
iliyokuwa na mwanga hafifu kwani ile swichi
ambayo ilikuwa inaning’inia pale kitandani ilikuwa
na uwezo wa kuchagua aina ya taa unayotaka
kutumia kama ni ile ya mwanga wa kawaida au ile
nyingine ambayo mwanga wake ulikuwa hafifu wa
rangi ya kijani. Halafu nikachomeka vizuri
chandarua, nikajitupa kitandani. Huku nikilitazama
pangaboi lilivyokuwa linazunguka na kuleta upepo
ambao ulinifariji.
Nilikaa kimya kwa muda usiojulikana nikitafakari
juu ya yule mwanamke. Nilianza kujutia hamu
yangu ya kutaka kujua mambo yasiyonihusu.
Lakini kama mtu anataka kuuwawa kwanini
isinihusu? mimi ni raia mwema nina wajibu wa
kutoa msaada. Nikaanza kuwakumbuka watu wa
kubuni ambao walikuwa wahusika wakuu kwenye
riwaya mbalimbali jinsi walivyofanya mambo
makubwa kwa ajili ya kuokoa wengine.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA NNE
Nilikaa kimya kwa muda usiojulikana nikitafakari
juu ya yule mwanamke. Nilianza kujutia hamu
yangu ya kutaka kujua mambo yasiyonihusu.
Lakini kama mtu anataka kuuwawa kwanini
isinihusu? mimi ni raia mwema nina wajibu wa
kutoa msaada. Nikaanza kuwakumbuka watu wa
kubuni ambao walikuwa wahusika wakuu kwenye
riwaya mbalimbali jinsi walivyofanya mambo
makubwa kwa ajili ya kuokoa wengine. Walinivutia
sana ingawa kimsingi ilikuwa ni tafsiri tu ya
mawazo ya mwandishi. Ndani yake nilikutana na
mashujaa wa kufikirika ambao walilitetea taifa kwa
nguvu zao zote, walikuwa ni wazalendo wa kweli.
Ilisisimua sana hata ikasababisha msomaji ajione
kuwa ndiye yeye huyo shujaa wa kufikirika. Lakini
ukweli unabaki wazi kuwa mashujaa hao wa
kufikirika ni tafsiri ya mashujaa halisi kama
Mkwawa, Kinjekitile na wegineo.
Lengo langu lilikuwa ni kumsubiri mpenzi wake yule
mwanamke. Nilipanga kuwa atakapoingia nitavizia
mlangoni ili nisikie wanazungumza nini. Mpaka
wakati huo nilikuwa nafanya mambo hayo bila
kujua hasara au faida yake.Nashindwa kujua kwa
nini nilijiingiza kwenye umbea kama ule. Labda
nilikuwa nasukumwa na nguvu fulani ambayo
sikuifahamu. Kwa kifupi nilikuwa kama mtu
ambaye nina dalili za matatizo ya kiakili. Wakati
nikiendelea kuwaza usingizi nao haukufanya ajizi,
ukaniondoa kwenye dunia halisi na kunipeleka
kwenye dunia ya ndoto. Nikawa nje kabisa ya
chumba kile nikimiliki magunia ya fedha.Ah! ndoto
bwana…….
***

Ghafla, nikashtuka kutoka usingizini. Kuna kitu
kilinishtua,.“Lazima kuna kitu” Niliwaza. Kwanza
nilihisi kuwa mlango wangu umegongwa. Mwanzo
nilifikiri ni ndoto. Lakini baadaye nikasikia sauti za
viatu vya watu waliokuwa wanatembea kwenye
korido. Kilichonishtua ni muundo wa gesti ile kwani
kila chumba kilikuwa na choo na bafu. Saa nane
za usiku hao watu wanatafuta nini? Balaa
likaanzia hapo.
Nilitembea kwa kunyata hadi mlangoni. Nikauvuta
ufunguo kwa tahadhari kubwa ili usiweze kuleta
makelele. Kumbe nililala bila kufunga mlango.
Kujisahau namna hii ni hatari sana. Lakini muda
huo sikuwa na fursa ya kuufunga tena mlango ule
kwani ningejaribu ningewashtua wale jamaa.
Nilikuwa natetemeka kiasi cha kuhisi kubanwa na
haja ndogo. Niliganda pale mlangoni kwa dakika
kadhaa.
Kwa kutumia Tundu la funguo niliweza kuona
viwiliwili vya watu waliokuwa wanatembea kwenye
korido. Walikuwa wamevaa makoti makubwa kama
yale yanayovaliwa na polisi. Walikuwa wanatoka
upande mmoja na kurudi upande mwingine.
Utembeaji ule ulikuwa unanitia hofu kwani nilihisi
kuwa wanataka kufanya jambo baya. Baada ya
sekunde chache nikagundua kilichokuwa
kinaendelea. Nilimuona mmoja akiwa anachungulia
kwenye tundu la ufunguo chumba alicholala yule
mwanamke.
Wanataka nini na wamejuaje kama yupo huku?
Wale watu waliokuwa wanatembea kwenye korido
waliendelea na utaratibu wao ule ambao ulinitisha,
kuna wakati niliona kama wanataka kufungua
mlango wa chumba changu.Mapigo ya moyo
wangu yalikuwa yanaenda mbio sana kutokana na
hofu niliyokuwa nayo. Nilijihisi kubanwa na haja
ndogo lakini nikmaingiwa na hofu kwani niliona
kuwa iwapo nitafungua mlango wa kule chooni
watanisikia.
Hatimaye walifanikiwa kufungua mlango. Hapo
mapigo ya moyo wangu yaliongezeka maradufu.
Niliona kundi lote likiingia mle chumbani. Sina
uhakika kama kuna mtu alikuwa amesalia. Kwa
makadirio ya chini walikuwa watano. Moyo wangu
ulikuwa unaenda kasi zaidi nilipomuona yule mtu
wa mwisho akiwa na bisu kubwa lenye mpini
mweusi. Nilihamanika kijasho chembamba
kikaanza kunitoka.
Baada ya muda usiozidi robo saa wale watu
wakatoka mle chumbani. Nikaamua kwenda ili
nijue kama yule Mwanamke yuko salama. Huku
mapigo ya moyo wangu yakienda kasi nilitoka
chumbani kwangu na kuuendea mlango wa
Chumba namba 7. Huku mikono yangu ikitetemeka
nilishika kishikio cha kitasa nikakifungua taratibu.
Mlango ukafunguka. Chumba kilikuwa na giza,
nikapapasa ukutani nikaipata swichi. Nikawasha.
Nilichokiona ilikuwa ni moja ya kumbukumbu
mbaya katika maisha yangu. Nilijihisi kuishiwa na
nguvu kwa hofu niliyokuwa nayo. Kijasho
chembamba kiliendelea kunitoka, maungio ya
miguu yalikuwa kama yameingiwa na ganzi hali
iliyonifanya nipige magoti karibu na kile kitanda.
Mwili wa Merina ulikuwa kama alivyozaliwa.
Sikuwa na shaka kuwa alianza kubakwa kabla kisu
kikali hakijafanya kazi yake. Alikuwa amechomwa
kisu tumboni na kusababisha utumbo utoke nje, pia
bisu kubwa jeusi lilikuwa limezama kwenye titi la
kulia. Mdomoni alikuwa amejazwa matambara, bila
shaka ilikuwa ni kumzuia asipige kelele. Pamoja na
kisu hicho kuzama hadi pale ulipoishia mpini, bado
kulikuwa na dalili za uhai. Nikamsogelea Merina ili
nimfungue na kumpa msaada zaidi.
Kitu cha kwanza ilikuwa ni kumuondoa matambara
ambayo alijazwa mdomoni. Baada ya kuondoa yale
matambara akakohoa kwa nguvu na kuanza
kuhema. Damu zilianza kumtoka mdomoni na
puani.
“On…n…ndoka..wa..takuuu..wataku..ua…”. Kwa
sauti ndogo yenye kila dalili ya mauti Merina
alisisitiza. Nilimtazama bila kumjibu huku machozi
yakinilengalenga.
“ Kwani umewafanya nini?” Nilimuuliza swali hilo
nikionesha kuipuuza kauli yake ya kuondoka”.
“Sii ..siri..ii….go..oh, mh nakufa ondoka
…..wata….yukk kaaa…ssspill” Hakumaliza kauli
yake, alikuwa anaongea vitu ambavyo vilikuwa
havieleweki tena. Hatimaye akakata kauli.
Mwili wangu ulikuwa umelowa kwa jasho.
Niliutazama ukuta wa chumba kile jinsi
ulivyochafuka kwa damu ambazo bila shaka
ziliruka baada ya kuchomwa kisu. Harufu ya damu
ilikuwa inanuka. Nikaishika maiti ya Merina bila
kutarajia. Huyu binti alikuwa jasiri kweli hata
mwisho wa uhai wake bado alikuwa na moyo wa
kumtahadharisha kiumbe mwenzake. Alikuwa
anataka kusema neno lakini hatima yake ilikuwa
imefika. Tayari alikuwa ameuacha ulimwengu huu
ulimwengu wenye kila aina ya vituko. Ulimwengu
wa dhulma, dhambi na ufisadi. Nikajikuta nikiwa
nimeshikilia kisu ambacho kilikuwa kimezama
katika kifua cha Merina, nilijisikia uchungu kana
kwamba nilikuwa nafahamiana na Merina miaka
mingi iliyopita.
Ghafla, nikashtushwa na mwanga mkali ambao
ulikuwa kama tochi iliyowashwa ghafla na
kuzimwa. Nilipogeuka nikawaona watu wawili.
Mmoja alikuwa ameshika kamera na yule
mwingine alikuwa na bastola mkononi. Nilikosa la
kufanya. Nilikuwa nimepatikana, jamaa alikuwa
amenipiga picha. Picha mbaya kabisa. Mkono
mmoja nilikuwa nimeshika bega la kushoto la
Merina huku ule mwingine nikiwa nimeshika kisu
ambacho kilikuwa kimezama kwenye titi la kulia.
Ee bwanaee! ilikuwa si mchezo yaani ile picha
kama itafika mbele ya jaji ambaye si makini au
amekula rushwa ni kitanzi tu. Swali la haraka
lilipita kichwani kwangu huu ni mtego?
Balaa.
Wale jamaa walinitazama bila kusema lolote
wakaondoka.Huku nikiwa nimetawaliwa na hofu
nikatoka ndani ya kile chumba na kurudi chumbani
kwangu nikiwa nimechanganyikiwa kabisa. Ghafla
kengele ya tahadhari ikalia kichwani kwangu. Sasa
nilianza kuiona wazi jela ikinukia. Kwanza jamaa
walinipiga picha, halafu kuna alama za vidole
ambazo nimeziacha kwenye kisu. Sikuwa na wazo
zaidi ya kutoroka. Nikae nifanye nini wakati
kuisaidia polisi ni adhabu kamili ambayo
inamtosha mhalifu yeyote. Sijui kwanini
sikukumbuka taratibu za polisi za kuchunguza
alama za vidole. Nikatoka mbio kuelekea
Mapokezi. Nilishangaa kwani msichana wa
mapokezi alikuwa anakoroma tena mkoromo
ambao ulisikika nje ya chumba kile.
Nikaona bora niingie kule mapokezi ili aweze
kunifungulia mlango niondoke. Nilifahamu wazi
kuwa angetaka kujua kilichotokea mpaka niondoke
muda huo lakini sikujali kwani nilijiandaa kumjibu
kutokana na aina yoyote ya swali
atakalouliza. ......Nikagonga mlango kama mara
tatu hivi lakini mlango haukufunguliwa. Nikajaribu
kukinyonga kile kitasa, kumbe mlango ulikuwa
haujafungwa kwa funguo. Nilipoingia mle chumbani
ndipo nilipokutana na tukio lingine la aina yake,
msichana wa mapokezi alikuwa anakoroma huku
povu likimtoka mdomoni, haukuwa mkoromo wa
kawaida ulikuwa MKOROMO WA MAUTI.
Sikutaka kupoteza muda tena kama mara ya
kwanza, nikapiga hatua za haraka haraka
kuuendea mlango wa kutokea nje. Bahati ilikuwa
upande wangu, bila shaka wale jamaa
hawakufunga na funguo ule mlango. ‘Nitatoka?’
Swali hilo ndilo nililojiuliza kwa wakati huo

***
Saa 9.37 usiku, nilivuka bonde la mto msimbazi.
Bonde hili liko maeneo ya Barakuda tabata
chang’ombe. Nilijikuta nikiyaingia maji ambayo
yalifika nusu muundi. Sikujali hali ile ambayo
ilisababisha suruali yangu ilowe. Jambo la muhimu
kwangu lilikuwa kujinusuru na mikono ya dola na
wale jamaa ambao sikufahamu ni kina nani.
Saa 9.54 nilikuwa maeneo ya viwandani. Nikavuka
barabara na kutokea kituo cha Jet. Hapo hofu
ikapungua kwani nilijua nikifika Lumo nitakuwa
kwenye amani zaidi.
Nikiwa eneo la Jet nikawaona watu wanne
wakinifuata kwa kasi, moyo ulitoa mlipuko wa
hofu. Nikaanza kutimua mbio kama mtu
anayeshiriki mbio za mita fupi. Kila nilipofikiria
adhabu ya kunyongwa nilijikuta nikiongeza mbio.
Jamaa waliendelea kunifukuza, jambo la ajabu ni
jinsi walivyokuwa wananifukuza kimya kimya.
Nikaamua kuongeza mbio bila kugeuka. Nilipofika
maeneo ya Kigilagila nikapunuza mwendo na
kugeuka nyuma. Nikagundua jamaa nilikuwa
nimewaacha mbali sana. Lakini baada ya
kuwatazama vizuri nikagundua kuwa walikuwa ni
vibaka. Nikasonya kabla ya kuanza kutembea
taratibu kwani jamaa walionekana kuchoka kabisa
na kusimama, bila shaka walikuwa
wameshangazwa na kasi yangu ambayo haikuwa
ya kawaida kwao.
Saa 10.22 nilikuwa mbele ya mlango wa chumba
changu. Angalau niliweza kushusha pumzi.
Haikuwa mara yangu ya kwanza kuona maiti.
Lakini ajabu ni taswira ya maiti ile kujirudia
kichwani mara nyingi na kunikosesha usingizi. Pia
niliwaza sana juu ya yule dada wa mapokezi, kwa
vyovyote vile nilijua wazi kuwa yule dada hatofika
asubuhi, nilijiuliza ni vipi wateja watahamanika
baada ya kukutana na tukio lile la aina yake, pia
nilivuta hisia jinsi watakavyopata msukosuko
katika adhabu isiyo rasmi iliyopewa jina la
kuisaidia polisi. Huku nikiendelea kuwaza hatimaye
nikaamua kujifunika shuka, baada ya dakika
kadhaa, hatimaye nikapata usingizi.
Haukuwa usingizi mzuri, ulikuwa ni usingizi wa
mang’amung’amu. Mara kadhaa niliota nikiwa
mbele ya jaji kujibu tuhuma za mauaji. Wakati
mwingine niliota babu akinipokea ndani ya kaburi.
IIi mradi niliandamwa na ndoto za ajabu ajabu.
Ndoto ya mwisho ninayoikumbuka sana ni ile ya
watu wenye makoti makubwa wakinikimbiza huku
kila mmoja akiwa na kisu chenye mpini mweusi
mkononi……….

***
Niliamka saa 5.30. Nikabaini kuwa nilikuwa
nimelala bila kuvua suruali yangu ambayo ilikuwa
imelowa kwani nilipovuka pale mto msimbazi
nyuma ya Barakuda sikukumbuka hata kukunja
nguo. Afadhali hilo la kulala na nguo iliyolowa
balaa zaidi ni kulala na viatu! Kimsingi matatizo
yote nilikuwa nimejitakia. Sikuwa na sababu yoyote
ya kufuatilia mambo kama Polisi. Lakini najua
sana kilichoniponza, kupenda kusoma riwaya za
upelelezi. Riwaya hizi mara nyingi zilinisisimua na
kunifanya nijihisi kama mimi ndio muhusika mkuu.
Mara nyingi nilitamani kufanya kazi idara ya
Usalama wa Taifa, pia nilitamani kuwa kachero.
Nakusudia wale askari polisi ambao hawavai sare
kama wengine. Nilihisi kuwa ninaweza. Lakini
ilikuwa ngumu kupata nafasi hizo, kama huna
ndugu huko uwe na pesa na kama huna pesa……
we ulie tu.
 
SEHEMU YA TANO

Niliamka saa 5.30. Nikabaini kuwa nilikuwa
nimelala bila kuvua suruali yangu ambayo
ilikuwa imelowa kwani nilipovuka pale mto
msimbazi nyuma ya Barakuda sikukumbuka
hata kukunja nguo. Afadhali hilo la kulala na
nguo iliyolowa balaa zaidi ni kulala na viatu!
Kimsingi matatizo yote nilikuwa nimejitakia.
Sikuwa na sababu yoyote ya kufuatilia mambo
kama Polisi. Lakini najua sana kilichoniponza,
kupenda kusoma riwaya za upelelezi. Riwaya
hizi mara nyingi zilinisisimua na kunifanya
nijihisi kama mimi ndio muhusika mkuu. Mara
nyingi nilitamani kufanya kazi idara ya Usalama
wa Taifa, pia nilitamani kuwa kachero.
Nakusudia wale askari polisi ambao hawavai
sare kama wengine. Nilihisi kuwa ninaweza.
Lakini ilikuwa ngumu kupata nafasi hizo, kama
huna ndugu huko uwe na pesa na kama huna
pesa…… we ulie tu.
Nilitazama juu kana kwamba kuna kitu nilikuwa
natafuta huko. Ukweli ni kwamba dali ile ilikuwa
dhaifu sana mbele ya Fikra zangu. Fikra zangu
ziliweza kupenya dali ile kama mwanga
unavyopenya kwenye dirisha la kioo.Hamu ya
kwenda kazini iliniishia.
“Niende wapi?”, ni swali ambalo nilijiuliza
nikakosa jibu. Na ile picha niliyopigwa? Duh!
Nilihisi tumbo likinguruma baada ya
kuikumbuka ile picha. Sijui kwanini wale jamaa
walinipiga picha bila kuongea lolote. Bila shaka
walikuwa na ajenda ya siri, ni ajenda gani? hilo
ndilo swali lililoutesa moyo wangu.
Nikaamua kuyapuuza mawazo ya ile picha.
Nikamkumbuka Betty, yule muhudumu wa Baa
ambaye nilitokea kumpenda sana. Pamoja na
purukushani nyingi katika maisha, kwenye
uwanja wa mapenzi sikuwa mzoefu. Hivyo kila
nilipokumbuka kukutana na Betty, kidogo
niliingiwa na hofu. Niliwashangaa wale watu
majasiri sijui niwaiteje yaani anaweza kukutana
na binti kwenye siti ya gari na ndani ya nusu
***
Siku hii niliamua kuwatembelea baadhi ya rafiki
zangu waishio Mwananyamala. Nikiwa kwenye
daladala ndipo nilipokutana na kile ambacho
sikukitarajia kwa muda huo.
“Vipi tena?” Niliuliza baada ya kuona askari
wengi barabarani. Yaani gari lilikuwa haliwezi
kupita eneo la Tazara bila kukaguliwa.
“Kuna jamaa, kaua watu huko Tabata, leo kila
kwenye makutano ya barabara kuna askari.
“Aah, kwa hiyo mpaka wamalize kukagua
magari yote hayo?” Niliuliza huku nikianza
kuingiwa na woga.
“Ina maana wakimuona huyo muuaji
watamjua?” Aliuliza abiria mwingine ambaye
alikuwa amekaa siti ya jirani yangu.
“Itakuwa hivyo mbona siku zingine
hawasimamishi?” Abiria mwingine akajibu.
“Sasa kama walimuona si wangemkamata
muda huohuo?”
“Labda aliahidi kufanya hivyo kabla?”
Majibizano ya abiria yaliendelea na sasa
nilikuwa siwasikii tena kwani akili yangu ilikuwa
inawaza ni jinsi gani nitajinasua katika zoezi
lile.
“Aah, wanataka kutuchelewesha hawa,
nifungulie nianze mdogomdogo.” Nilimwambia
konda ambaye alinielewa na kunifungulia
mlango kisha nikashuka.
Nikatembea taratibu lakini kwa tahadhari
kubwa huku nikiwapita askari ambao
hawakujishugulisha kunitazama. Ingawa
niliwapita salama lakini nilikuwa na hisia kuwa
kuna askari anakuja au wanakuja nyuma yangu,
hali hiyo ikanifanya nijione kama ninayerudi
nyuma badala ya kwenda mbele. Nilihisi kama
mwili unataka kuishiwa nguvu. Kila kitu kilikuwa
kimebadilika katika maisha yangu, furaha yangu
ilipotea na nafasi yake ikachukuliwa na hofu na
mashaka. Ni wakati kama huu ambao watu
tuliomsahau Mungu huwa tunamkumbuka sana
tena kwa imani hasa. Nilijilazimisha kila
nilipowaona askari kutowakwepa na kuelekea
upande waliopo ili kuwaondolea hofu juu yangu,
kwa hilo nilifanikiwa sana kwani askari
walikuwa wamejishugulisha na watu wa kwenye
magari. Nilitembea hadi Buguruni sheli hapo
nikakona na kufuata kichochoro ambacho
kinaenda kwa Mnyamani. Safari yangu ya
kurudi nilikotoka ilinifikisha Vingunguti eneo la
kiembe mbuzi ambako niliamua kufuata reli
ambayo ilinifikisha nyuma ya viwanda vilivyoko
Kipawa. Nikafuata kichochoro kinachotokea
barabarani, nikavuka barabara na kutokea eneo
la Jet club ambapo nilipanda gari kurejea
nyumbani.

3

Ilikuwa ni jioni ya Jumatatu tulivu. Haikuwa
siku ambayo tulikubaliana kukutana na Betty
lakini sikuwa na jinsi kwani nilimuhitaji kwa udi
na uvumba. Siku ile ya kwanza kumuona nilivaa
kama afisa fulani serikalini au sehemu ambazo
pesa si tatizo. Jumatatu hii nilikuwa nimevaa
Fulana Nyeusi na suruari ya jeans ya bluu.
Niliingia ndani ya ile baa nikaanza kumtafuta
Betty kwa macho, sikumuona. Wateja walikuwa
wachache kwa sababu ilikuwa ni siku ya kazi
lakini sikuweza kumuona.
Nikaamua kuhamishia macho yangu kwa
wacheza pool. Nilifurahi jinsi walivyokuwa
wanaigonga mipira ile na kuiingiza kwenye
vishimo vidogo. Kitu kimoja tu walikuwa
wananikera, walipenda sana kutumia lugha ya
matusi. Pamoja na kutumia lugha hiyo mbaya
lakini hakuna aliyekasirika, wenyewe waliona
kuwa jambo la kawaida kwani hata mtu
aliyesifia kitu aliisindikiza sifa hiyo kwa tusi kali
mengine yakiwa ya nguoni.
Nikaachana na wacheza pool nikaanza
kuzungusha macho yangu huku na kule. Muda
mfupi baadae mmoja wa wahudumu wa baa
alikuwa amesimama mbele yangu. “Nikusaidie
nini kaka” alisema huku akiwa ameibana sauti
kama anayeongelea puani. Nikamtazama kidogo
kwa jicho la kutathmini. Bado alikuwa
hajamfikia Betty kwa uzuri wake.
“Naomba pepsi baridi tafadhali.” Nilimjibu huku
nikiwa nimemkazia macho angalau ajisikie
kuwa nimemjali. Nilikuwa na uwezo wa kuvunja
mawe makubwa na kubeba mzigo mzito wa
mawe lakini kukabiliana na hawa viumbe
ilikuwa ni zaidi ya huo mzigo wa mawe.
Muda mfupi baada ya kuhudumiwa nikamuona
Betty akiingia. Alikuwa ameshika gazeti
mkononi. Tulikutanisha macho yetu. Kidogo
nilimuona akibabaika, bila shaka alikuwa
anajaribu kuvuta kumbukumbu ya sura yangu,
wapi aliniona. Hilo lilikuwa swali ambalo nahisi
lilipita kichwani mwake. Siku hiyo hakuwa
amevaa sare. Nikamwita kwa ishara ya mkono.
Akaja akakaa, sikuwa na hofu tena kama
ilivyokuwa siku ya kwanza.
“Habari yako Betty.” Nilimsalimia kwa ujasiri
huku nikitabasamu.
“nzuri!” alijibu kwa mkato huku akionesha wazi
mshangao jinsi nilivyoweza kufahamu jina lake.
“Utakunywa nini?” Nilimuuliza huku nikiendelea
kushangaa jinsi alivyoumbika. “Ahsante sijisikii
kunywa kitu cha baridi.” Alinijibu huku
akitabasamu. Niliinamisha kichwa changu
mezani nikitafakari namna ya kuanzisha
maongezi.
”Nikununulie bia ya moto?”
“Hapana, nahitaji kitu cha moto kama chai au
maziwa.” Alinijibu, nikatumia nafasi hiyo
kumuuliza swali.
“Unanikumbuka?” lilikuwa swali langu la
kwanza.
“ Sura yako si ngeni sana, naona kama
nilishawahi kukuona mahali” Jibu lake kidogo
lilinifariji.
“Nilikuja hapa juzi, tukapanga kukutana jana
lakini…………” Sikumaliza nilichotaka kuongea.
“ Aah, sawa. Sasa nimekumbuka. Samahani
sana jana nilikuwa off hata hivyo nilikuwa
nimesahau kabisa!” Hiyo nikaiona fursa nzuri
kwangu.
“Jana nimekaa sana hapa mpaka wakati wa
kufunga baa ndipo nikaondoka!” Nilikuwa
namuongopea yule mwanamke.
“Enhe, lete story.” Aliongea kwa upole na
uchangamfu kitu ambacho sikukitarajia.
Nikakohoa ili kuiweka sawa sauti yangu.
Nikapatwa na mshtuko baada ya kukiona
kichwa cha habari ambacho kilikuwa kwenye
gazeti ambalo alikuwa amelishika Betty
mkononi. MAUAJI YATIKISA TABATA.
Sikuthubutu kuomba lile gazeti kwani kichwa
cha habari tu nilijisikia kubanwa na haja ndogo
vipi niisome habari mzima halafu nikute picha
yangu……. Sikutaka kudhihirisha mshtuko wangu
kwa Betty. Lile gazeti kwa kiasi fulani lilikuwa
limenipunguzia nguvu na ujasiri wa kuongea na
Betty.
“Betty, sina maneno mengi ya kuongea
isipokuwa ni neno moja tu; Hilo ndilo
limenifanya nifunge safari kutoka nilikotoka hadi
hapa. Kwa kifupi nakupenda.” Nilishusha pumzi
na kumkazia macho Betty.
“Sijakuelewa bro, kwanza hata jina
sijakufahamu, kwa kifupi hatufahamiani vizuri!”
Nikajisikia aibu baada ya kutanabahi kuwa
nilikuwa nimeanza mazungumzo yale bila
umakini. Kidogo nikajisikia Vibaya ingawa
nilipiga moyo konde na kutaka kuendeleza
mazungumzo yale. Kisha akaendelea
kuongea“usijali sana, mimi naitwa Betina
Samson Masawe, nimezaliwa wilaya ya Moshi
mkoa wa Kilimanjaro. Elimu yangu ni kidato cha
nne. Sina mtoto, sina mume wala sina
mchumba na sihitaji mume wala mchumba.”
Alimaliza kwa kauli ambayo ilikuwa kama mkuki
kwenye moyo wangu. Nilimtazama tena Betty,
nikainamisha uso wangu chini kwani alianza
kunipa wakati mgumu kutokana na kauli yake
hiyo.
“Kwa nini hutaki mume ina maana hutaolewa”
Nilimuuliza.
“Utapeli wao ndio unao nifanya nitamani zaidi
kuwa peke yangu!” Alinijibu kwa upole lakini
akionesha kutokuwa na mzaha na kauli yake.
“Utapeli upi?” Nilimuuliza kwa sauti iliyokata
tamaa.
“Kama huu ambao unauleta wewe sasa, eti
unanipenda, mimi baamedi?”
“Una uhakika kuwa naongopa?”
“Kwa asilimia mia moja” Alinijibu kwa msisitizo.
Nikamtazama Betty kwa hasira kidogo kwani
sikupenda kuitwa tapeli.
“Narudia, sitaki mwanaume hivyo hata wewe
sikutaki labda kama unataka kuwa kaka yangu
wa hiyari, leo unanitaka kesho unitangaze
vijiweni kuwa malaya eti kisa kuuza baa.”
Nilishindwa kuvumilia maneno makali ya Betty,
nikainuka na kutaka kuondoka. Nilikuwa
nimeshapiga hatua mbili nikamsikia Betty
akiniita.
“Bro…Mbona unaondoka?” Aliniuliza Betty kwa
sauti ileile ya upole.
“Nimekata tamaa.” Nilimjibu kwa hasira.
“ Kwa hiyo hata kuagana hatuagani!”
“Kwa heri.” Nilimjibu huku nikiwa nimemkazia
jicho la hasira.
“Kwaherii, yaani leo niandike kwenye diary
yangu nilikutana na mtu hakunitambulisha jina
wala nini….. kaniita na kuniambia eti
ananipenda kisha kwa heri!” Naye aliongea
huku akionesha hasira na dharau kwa jinsi
nilivyokosa ustaarabu.
Nikaamua kuituliza hasira yangu la sivyo
tusingeelewana. “Betty..” Nilianza huku nikiwa
nimesimama nyuma ya kiti ambacho nilikalia.
“Kwanza naomba samahani kwa
kutokukufahamisha jina langu. Naitwa Kajuna
Kazakamba. Elimu yangu ni kidato cha sita.
Sina kazi. Sijaoa wala sina mchumba. Nahitaji
mke, nakuhitaji wewe.” Nilimaliza na
kumtazama Betty huku hasira zangu zikiwa
zimepungua.
“Mimi ni baamedi, inakuwaje unihitaji mimi
hujawaona wengine ambao ni tofauti na mimi
huko unakotoka?” Lilikuwa swali gumu kidogo.
“Hakuna tatizo kwangu kama unaweza
kujiheshimu katika kazi yako hiyo, kwa jinsi
nilivyokuona naamini unajiheshimu.” Betty
alikuwa kama anayepingana na akili yake
akubali au akatae.
“ Ah, hapana Kajuna siwezi na sitaki
mwanaume anivurugie maisha yangu, Kwa
heri.” Aliinuka kwenye kiti na kuanza kuondoka.
Hakuweza kukatisha pale niliposimama
nikaudaka mkono wake wa kushoto. Alikuwa
anahangaika kutaka kujinasua kwenye mikono
yangu. Sikumpa nafasi, kwa kutumia mkono
wangu wenye nguvu nikambana. “Kaju…
niachiee” alikuwa analalamika kwa sauti ndogo
lakini yenye hasira. Nikazungusha mikono
yangu mgongoni kwake. Nikamvutia kifuani
kwangu kwa nguvu nikamkumbatia.
Bahati ilikuwa upande wangu kwani wakati huo
spika zilikuwa zinatoa sauti kubwa ya muziki
laini ulioimbwa na Shania Twain Your still the
one. Yeyote aliyetuona alijua kuwa tunacheza
muziki huo. Nikawa nalazimisha kukutanisha
ndimi zetu. Ndimi zikakutana. Nikaitoa mikono
yangu, alikuwa anahema kweli kweli. Ajabu,
alikuwa amekilaza kichwa chake kwenye bega
langu la kulia. Nikaanza kumpapasa mgongoni
kwa namna ambayo ilimfanya asisimke na
kuniganda safari hii ikiwa kwa hiyari yake.
“Kajuna, Ilove you”.Kwa sauti iliyojaa
kitetemeshi alitamka Betty na kunifanya nihisi
kuwa niko ndotoni. Alikuwa hana ujanja tena,
kijana nilikuwa nimeshinda ‘gemu’.
“Twende nyumbani!” niliongea kwa sauti ndogo
ya kubembeleza.
“Twende kwetu”
“Wapi?”
“Si mbali” alinijibu. Nikamfuata kama kondoo
anayeenda kuchinjwa……..
***
Miezi mitatu ya mapenzi yangu na Betty ilikuwa
imepita salama bila misukosuko, hata zile
habari za mauaji ya kule Kisukuru zilipotea
kama upepo . Betty alikuwa anaendelea na kazi
yake ya baa. Alikuwa mwanamke mwenye
msimamo thabiti. Hakuyumbishwa na yeyote.
Pamoja na usumbufu mkubwa alioupata kutoka
kwa wanaume wenye fedha, bado alinithamini
na kunijali.

ITAENDELEA
 
Utamu kolea ndio umeanza ntamaholo na wengineo njooni pande hii

mkuu
Willy Gamba kwanza kama hujapokea likes na pongez zangu ktk riwaya ya risasi nne, pokea kwanza.

pili kwa uhondo nilioupata kwa kusoma riwaya weekend ile, nasisitiza msimamo wangu. nitakuwa nachungulia tu hadi nione neno MWISHO ndo nianze.

kidi kudi ameninyima raha na imani kk
 
Last edited by a moderator:
Gamba tena hapa! mimi hiyo kasi yako kama ya bwana usein nati (bolt)hunisisimua sana pamoja sana.
 
SEHEMU YA SITA
***
Miezi mitatu ya mapenzi yangu na Betty ilikuwa
imepita salama bila misukosuko, hata zile habari
za mauaji ya kule Kisukuru zilipotea kama upepo .
Betty alikuwa anaendelea na kazi yake ya baa.
Alikuwa mwanamke mwenye msimamo thabiti.
Hakuyumbishwa na yeyote. Pamoja na usumbufu
mkubwa alioupata kutoka kwa wanaume wenye
fedha, bado alinithamini na kunijali.
Ikatokea siku miongoni mwa siku ambazo ni
ngumu kuzisahau katika maisha yangu. Siku hiyo
ndio ilikuwa mwanzo wa kubadilika mfumo wa
maisha yangu. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa
kipindi kigumu kabisa katika historia yangu
ambachi sifikirii kama kitakuja kutokea tena.
Ilikuwa ni Jumamosi kama zilivyo jumamosi
nyingine. Tofauti ni kwamba siku hiyo niliamua
kupumzika nyumbani. Siku hiyo sikuwa na ahadi
ya kukutana na mpenzi wangu Betty. Hivyo
niliamua kuitumia siku hiyo kwa kazi ndogo ndogo
za nyumbani. Kutokana na uchovu wa kazi ngumu
za vibarua vya juma zima niliamua kurudi tena
kitandani baada ya kumaliza kazi zangu.
Wakati usingizi ukianza kunichukua nikasikia
mlango unagongwa. Nikainuka kitandani na
kwenda kufungua. Nilipofungua mlango, nikashtuka
kidogo kwani mtu niliyemuona alikuwa mgeni
kabisa machoni mwangu. Licha ya ugeni wa mtu
yule bado sikuona kama nina hadhi ya
kutembelewa naye. Alikuwa pandikizi la mtu
ambaye kama hufahamu jina lake unaweza
kumwita Bonge. Alikuwa ananukia manukato
yaliyomtofautisha na mtu mwenye kipato cha
kawaida kwenye jamii. Alikuwa na uso wa duara
huku akiwa amenyoa ndevu zake kwa mtindo wa
‘O’ ukijulikana zaidi kwa jina la ‘Timberland’ .
Alikuwa amevaa suti ya kijivu ambayo bila shaka
ilikuwa ni ya gharama kubwa. Miguuni alivaa viatu
vyeusi ambavyo viling’arishwa vema kwa dawa.
Alikuwa anapendeza.
Amefuata nini?
“Habari yako bwana Kajuna.” Alinisalimia na
kunizidishia mshangao. Kwani alikuwa kama mtu
anayenifahamu siku nyingi.
“nzuri, karibu ngoja nikuchukulie stuli.” Niliwahi
kumzuia ili asije kuingia ndani, niliogopa mtu
mzima nitaadhirika.
“Hapana siwezi kukaa kwa sasa isipokuwa nina
mazungumzo machache, kama hutajali naomba
unifuate tukaongelee kule kwenye gari langu.”
Aliongea huku akinyoosha kidole kule liliko gari
lake. Lilikuwa Toyota Landcruiser nyeupe.
“Hakuna tatizo” Nilimjibu huku tukielekea kule liliko
gari lake. Majirani walikuwa wananitazama kwa
jicho la husuda wakati naondoka na Bonge
kuelekea kule kwenye gari. Walikuwa
wananong’ona, sikujua ni kitu gani kiliwafanya
wanong’one.
Jambo usilolijua!
“Ndugu Kajuna nafikiri hii ni mara yetu ya kwanza
kukutana mimi na wewe.” Alitulia kidogo na
kunikazia macho. Kisha akaendelea. “Mimi ni
mgeni kwako lakini wewe si mgeni kwangu,
nakufahamu sana Kajuna.” Sikutaka kujiuliza sana
kwani moyo ulikuwa unaenda mbio sana pia
sikuona sababu ya kuumiza kichwa kwa kujiuliza
mwenyewe wakati nina uhakika wa kupata majibu
kutoka kwa mtu huyo ambaye alikuwa mbele
yangu yaani nilikuwa sioni haja ya kuandikia mate
wakati wino upo.
Nilianza kuhisi kuwa huenda huyu mtu ni polisi.
Nilikuwa nimesahau kabisa tukio la kule Zawadi
guest house lakini sasa nilianza kuileta picha ya
tukio lile katika nafsi yangu. Nilichanganyikiwa ile
mbaya. Yule jamaa alikuwa hatari sana kwani
muda wote alikuwa kama anayesoma mawazo
yangu.
“Usiwe na wasiwasi Kajuna, nimekuja na habari
njema kwako. Habari hizi zitabadilisha kabisa
maisha yako wewe na Betty. Lililo muhimu kwako
ni kunisikiliza kwa makinini kile nitakachokueleza”
Akatulia tena na kunikazia macho. Alizidi
kunichanganya kwani badala ya kupunguza
aliongeza maswali ambayo ilikuwa ni vigumu
kuyajibu. “Kamfahamu vipi Betty?” Nilijiuliza huku
nikihisi tumbo langu likichafuka na kunguruma.
Nilimkazia macho kwa hamu ya kutaka kujua nini
alitaka kuongea. Naye kama aliyekusudia kunitia
umakini akatulia kwa dakika mbili.
“Utakuwa tajiri tena tajiri mkubwa kama
utatekeleza kazi nitakayokupa”. Akatulia tena kama
mwanzo.
“Mimi niwe tajiri!”Niliwaza huku upande mwingine
nikiona kama ninayefanyiwa dhihaka.
“Safari hii hutakiwi kuua mtu kama ulivyofanya
kule guest, itakuwa kazi nyepesi sana.” Niligwaya
baada ya kusikia kauli ile. Nilitamani arudie tena
maana nilikuwa kama sijamuelewa vizuri.
“ Au unabisha kuwa hujaua mtu wewe!” akaingiza
mkono mfukoni akatoa kitu ambacho kwa wakati
huo nilikitarajia sana, PICHA! Ilikuwa ni picha ya
lile tukio la yule mwanamke. Mandhari ya ile picha
ilinitisha sana. Nilikuwa muuaji kamili kwa mujibu
wa picha ile.
“Samahani sana kwa kukukumbusha kitu cha
kuogofya kama hiki, lakini hii nakuonesha kuwa
sina nia mbaya na wewe maana mimi ni ofisa wa
polisi hivyo ningetaka kukuweka ndani
ningekuweka siku nyingi!” Akatulia tena. Huwezi
kuamini jamaa aliniteka kabisa kwani nilikuwa
tayari kwa lolote ili mradi ile picha asiipeleke
kunakohusika. Kisha akaendelea.
“ Lengo la kukufuata tunataka kukutuma, si kazi ya
bure. Malipo makubwa yatafuata baada ya
kukamilisha kazi yetu!”
Wanataka kunituma, wao kina nani wanataka
kunituma nini na wapi? yalikuwa maswali yaliopita
haraka sana kichwani mwangu. Safari hii Jamaa
hakuruhusu niwe na muda mwingi wa kujiuliza.
“unatakiwa kwenda Mwanza, huko kuna mzigo
ambao jukumu lako ni kuufikisha salama Dar.
Malipo yako ni dola elfu hamsini. Jambo la
muhimu ni kutekeleza masharti utakayo pewa,
ukivunja masharti utasababisha matatizo makubwa
kwani zile picha bado tunazo, pia unatakiwa
ufahamu kuwa mimi ndiye niliyekabidhiwa jukumu
la upelelezi wa mauaji ya Muhudumu wa gesti na
yule binti ambaye ulimuua kwa kumchoma kisu.”
Akaingiza mkono mfukoni akatoa kitita cha noti.
Zilikuwa noti za shilingi elfu kumikumi. Sikujua
zilikuwa shilingi ngapi kwani baada ya kunikabidhi
niliziweka mfukoni.
“ Jiandae kwa safari, safari yako itakuwa
keshokutwa Jumatatu.” Yule jamaa alikuwa
amemaliza maongezi, akaingia ndani ya gari na
kuliondoa kwa kasi.
Nilibaki nimeduwaa nikilitizama gari lile lilivyokuwa
linatokomea kwenye barabara ya vumbi.
Nilisimama pale kwa dakika kadhaa huku nikiwa
nimechanganyikiwa nisijue la kufanya.
Nikarudi nyumbani na kukuta kina mama wakiwa
makundi makundi. Kumbe muda wote wakati
naongea na yule jamaa wao walikuwa hawajatoka
pale wakinikazia macho, umbea tu ndio
uliowashugulisha hata wakaacha kazi zao.
Walinisindikiza kwa macho hata pale nilipokuwa
naingia chumbani kwangu. Hali hii ilinikera sana
kwani kuna ajabu gani mimi kutembelewa na mtu
kama yule.
***
Tamaa ya fedha ilinifanya nisifikirie sana kuhusu
kukataa au kukubali kwenda kuchukua huo mzigo.
Nilikata shauri kukubali kwani siku niliyokutana na
Bonge alinipa shilingi milioni moja ambazo
hazikuwa na masharti wala makubaliano. Sijawahi
kuzishika pesa hizo hivyo ilikuwa ni furaha kubwa
kwangu. Mwanza tu! Kufuata mzigo ambao
sikutakiwa hata kujua ndani yake ulikuwa na nini.
Bora niuage umaskini mapema.
Siku iliyofuata Bonge alikuja nyumbani saa saba
usiku. Nilishangazwa sana na ujio huu. Lakini
tamaa ya fedha ilikuwa imenishika kiasi cha
kuweza kusahau ile picha. Nakumbuka siku hii
Bonge alikuja akiwa ‘sirias’ sana. Niliingiwa na
hofu kubwa kwani alinitisha.
“ Kajuna kesho ndio siku ya safari zingatia
maagizo yangu. Jambo la kwanza utakaporudi
kutoka Mwanza hutakiwi kupitia sehemu yoyote
mpaka uufikishe mzigo mikononi mwangu. Sharti
la pili hutakiwi kufungua huo mzigo, narudia
hutakiwi kufungua huo mzigo. Naomba uelewe
wazi kuwa picha zako za mauaji tunazo. Pia
napenda ufahamu kuwa kama utavunja sharti la
Kwanza basi adhabu yako itakuwa ni kukosa
malipo na kama utavunja sharti la pili basi si
kingine zaidi ya Kifo.”
Aliongea bila kuonesha chembe ya mzaha hata
kidogo. Niliogopa sana, nikaanza kuhisi chuki juu
ya huyu jamaa. Sijui kwanini huyu jamaa hata pale
alipokuwa anaongea taratibu nilimuogopa sana.
Nilishindwa kumuangalia machoni kwani nilihisi
moyo ukienda mbio sana.
Nitoroke? Nilijiuliza. Wazo lolote nililokuwa nalo
lilivurugwa na tamaa ya fedha. Kiasi alichoniahidi
Bonge kilikuwa kikubwa mno. Nilikubali, nilikubali
masharti yote ya Bonge, pesa bwana… kila kitu
pesa!
***

Napenda sana kusafiri. Lakini safari hii ya Mwanza
sikuifurahia. Ninaposafiri huwa napenda kushangaa
hili na lile hasa misitu wanyama na kadhalika.
Safari hii ilikuwa ni ndefu kwangu kuliko urefu
wake wa kawaida. Ingawa nilikuwa dirishani bado
nilikuwa sielewi nini kilikuwa kinaendelea huko nje.
Dola elfu hamsini si mchezo, zilinitoa jasho kweli
kweli. Mpaka kufikia hapo sikuwa na mawazo
mengi juu ya huo mzigo. Nilichohitaji ni pesa, pesa
tu na si kingine. Nilijikuta nikijenga na kubomoa
kwenye kichwa changu. Nilijenga nyumba nzuri ya
vigae Kinondoni nikaibomoa, nikajenga,
nikajenga…… ili mradi nikajenga nyumba nyingi tu
za kufikirika.
Safari ya Basi kwenda Mwanza ni ndefu sana.
Lakini urefu huo ulizidishwa mara mbili na fikra
zangu. Niliwatazama abiria wenzangu, wengi
walikuwa wamelala. Nikatoa karatasi ambayo
ilikuwa na maelezo jinsi nitakavyokutana na Martin
ambaye atakuwa mwenyeji wangu huko Mwanza.
Yaweza kuwa wanataka kumdhulumu huyo Martin
hivyo ili kupoteza ushahidi ndo wameamua
kunituma mimi.
Masaa kadhaa baadae nami nikasalimu amri kwa
kuungana na abiria wenzangu, nikalala. Sijui
usingizi wangu ulichukua Muda gani lakini
niliposhtuka tayari tulikuwa tumeingia Mwanza.
Niliteremka kwenye gari lile ambalo hata sikuwa na
muda wa kujua ni nani mmiliki wake.
4
Saa 7.30 mchana niliwasili Mwanza. Nilipokelewa
na baridi kali. Abiria wengi walitoa nguo mbali
mbali ambazo zingewakinga na baridi yakiwemo
makoti na majaketi. Sikuwa na ufahamu na hali ya
kijiografia ya jiji la Mwanza. Lakini niliipenda sana
hali hii ya hewa. Wakati nikiendelea kuwaza ghafla
nikaguswa begani. Nilipogeuka nikamuona kijana
mrefu ambaye alikuwa amesimama nyuma yangu,
tukasalimiana. Kisha akanielekeza kwenye gari
ndogo aina ya Toyota carina.
“Bila shaka wewe ndiye mgeni wa Mr. Martin.”
“Ndiyo mimi.” Nilimjibu kisha tukaingia kwenye
gari alilokuja nalo.
“Karibu sana Mwanza, nimetumwa kuja
kukuchukua na kukupeleka nyumbani kwake”
“Ahsante.”
“Hii ni mara yako ya kwanza kuja Mwanza?”
“Ndiyo” Nilimjibu kwa mkato huku akiwa anakata
kona kuingia katika mtaa ambao sikuufahamu.
“Mimi naitwa Masanja nimetumwa na Mr.Martin
kuja kukuchukua!” Aliongea kwa lafudhi ya
kisukuma.
Tuliendelea kukona hapa na pale nashindwa
kuelezea mitaa hii kwani Siifahamu mitaa ya
Mwanza ingawa nilikuja kuambiwa baadae kuwa
maeneo hayo yanaitwa Nyakato.
“Umefahamu vipi kuwa mimi ndie mgeni
mwenyewe?”Nilimuuliza ili kuvunja ukimya
ulioanza kutawala kwenye gari.
“picha yako!” Alinijibu na kunifanya nisikie tumbo
likinguruma. Sijui ni picha ya aina gani huyu jamaa
alikuwa anaizungumzia. Kama ni ile niliyopigwa
kule gesti basi ni balaa kubwa. Jibu lake lilinifanya
nikose hamu ya mazungumzo kwa kuhofia
kukumbushwa mkasa ule wa aina yake.
Gari ilifunga breki mbele ya Nyumba moja kubwa
ambayo ilikuwa imezungushiwa ukuta wa tofali za
kuchoma. Lango likafunguliwa baada ya kupiga
honi mara tatu. Gari ikapaki mbele ya bustani
ndogo ya maua.
“Tumefika.” Alisikika Masanja huku akifungua
mlango wa upande wake, nami nikafungua upande
wangu nikashuka.
“Huyu ndiye mgeni wa Martin ambaye nilimfuata.”
Alimuelekeza yule mtu aliyetufungulia geti.
“Kwaheri ndugu, jukumu langu lilikuwa ni
kukufikisha hapa.” Masanja aliongea huku akiingia
kwenye gari lake.
Nikasalimiana na yule mtu aliyetufungulia lango.
Akanielekeza kwa ishara niingie ndani.
“ Mr. Martin amefuata mzigo Shinyanga hivyo
utamsubiri hapa mpaka kesho atakaporudi”.
Niliitikia kwa kichwa huku nikijitupa pale kwenye
sofa. Nilikuwa nimechoka sana. Yule mtu ambaye
bila shaka alikuwa ni mlinzi alikuja na kunielekeza
chumba cha kwenda kupumzika. Nikaingia ndani
ya chumba hicho. Kabla sijapumzika akaja
“Ebwana kama utahitaji chakula naomba
unifahamishe.”
“Sawa.” Nilimjibu kwa mkato kwani sikujisikia kula
kwa muda huo.
Niliikagua mandhari ya Chumba kile. Kilikuwa ni
chumba kikubwa kizuri,kikiwa na bafu na choo.
Zaidi ya zulia zuri la hariri na kitanda cha futi sita
kwa sita hakukuwa na kitu kingine mle ndani.
Nikaingia kule bafuni, baada ya kuoga nikarudi
chumbani.Nikajilaza kitandani, usingizi
ukanichukua.
***
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA SABA
Nikaingia kule bafuni, baada ya kuoga nikarudi
chumbani.Nikajilaza kitandani, usingizi
ukanichukua.
***

Kutokana na uchovu wa safari nililala kwa masaa
kadhaa pale chumbani. Ghafla! Nikashtuka kutoka
usingizini. Kuna watu walikuwa wanaongea.
Niliwasikia vizuri, Bila shaka walikuwa
wamesimama kwenye korido karibu na chumba
changu.
“Vipi mzigo wa mheshimiwa tayari?” Aliuliza
mmoja.
“Uko tayari, nimeupata kutoka Shinyanga maeneo
ya Mwadui tena mzigo safi kabisa” Ilijibu sauti
nyingine.
“Kwa hiyo kesho utamkabidhi jamaa ausafirishe”
“No, jamaa tutamkabidhi kesho lakini atasafiri nao
kesho kutwa!”
“Huoni hatari kama atalala hapa kesho?”
“Nishamchukulia chumba gesti hata hivyo sikuwa
na uhakika wa kupata mapema mzigo ndio maana
nikakata tiketi ya kesho kutwa” .
Kwa akili ya haraka nikajua kuwa pengine huo
mzigo ni almasi kwa sababu nilisikia kuwa
umetoka Mwadui. Nikatabasamu kwa furaha.
Kumbe ndio maana bonge alinionya kuwa
nisifungue mzigo! Alijua iwapo nitafungua
nitaingiwa na tamaa” Niliwaza. Wakati nikiwaza
hivyo nilisikia milango ya vyumba viwili tofauti
ikifunguliwa. Nikajuwa wale jamaa watakuwa
wameenda kulala.
Usiku ule sikupata usingizi mawazo yangu
yalikuwa juu ya mzigo. Ni mzigo gani? Kwanini
uwe na masharti magumu kwa kuusafirisha tu,
kama thamani yake ni kubwa kwanini
wasiusafirishe wenyewe? Kama hauna thamani
kwanini wakubali kutumia gharama zote hizo.
Maswali yalikuwa magumu pia yaliniumiza sana
kichwa. Nilikuwa nashindwa hata kuhisi undani wa
jambo lile.
Wakati nikiendelea kuwaza juu ya mzigo nikapata
wazo. Wazo hilo nililiona kuwa zuri. Bonge
alinionya kuwa nisipitie sehemu yoyote kabla
sijampelekea mzigo wake. “Huu mzigo itakuwa
wameupata kwa njia zisizo halali, kwa hiyo si
mbaya hata mimi nikiuchukuwa”. Niliwaza. Almasi
kutoka Mwadui niziache nichekwe? Haiwezekani.
Dawa ya moto ni moto kama wao wamefanya
dhulma kuupata huo mzigo basi si vibaya hata
mimi nikiwadhulumu.
***

Saa 1.05 nilikuwa mbele ya Martin. Tofauti na
nilivyotarajia, Martin alikuwa pandikizi la mtu
mwenye sura ya kutisha. Macho yake yalikuwa
mekundu. Bila shaka alikuwa mvutaji mzuri wa
bangi. Alikuwa amevaa fulana ya mikono mifupi
ambayo iliruhusu misuli yake iliyojengeka
kimazoezi kuonekana. Katika mikono yake alikuwa
na michoro ya nge, nyoka na mingine ambayo
nilishindwa kuilewa. Kama ungemtazama machoni
lazima ungekubaliana na mimi kuwa ni muuaji.
Hakuhitajika mtaalamu wa saikolojia kulitambua
hilo. Hata pale alipokuwa anaongea hakuonesha
mzaha hata kidogo. Nakuambia huyu jamaa
alikuwa anatisha si mchezo hata kama ungekuwa
na mtoto analia ukamtisha kumpeleka kwake huyo
mtoto angenyamaza.
“Bwana Kajuna karibu sana! ” alianza baada ya
kusalimiana.
“Ahsante!” Nilijibu huku nikishangazwa na karibu
hiyo ambayo ni wazi haikutoka moyoni.
Unafiki tu.
Hapo alijitahidi kuonesha upole na uungwana lakini
hakufanikiwa alitisha tu, tena sana. Alikuwa kama
chui anayemchekea mbuzi ili kumzubaisha, hakuna
mbuzi atakayetambua kicheko cha chui. Akicheka
anachekea nyama akikasirika anajiandaa kuvamia,
tafsiri itabaki kuwa hivyo daima katika maisha ya
mbuzi.
“Mimindio Martin kama ulivyoelezwa na bosi.
Mzigo ulioambiwa uko tayari nitakukabidhi dakika
kumi zijazo. Tafadhali usisahau maelekezo yetu.
Aliongea kwa sauti ndogo yenye amri kali. “Kama
utathubutu kuvunja maelekezo……., tena ole wako
ufungue mzigo lazima nikuue kwa mkono wangu,
tena si kukuua tu! Bali nitakuua kifo kibaya sana.
Narudia, kitakuwa kifo kibaya sana.” Aliongea kwa
msisitizo mpaka nikaingiwa na hofu. Eeh, angalau
sasa alianza kujionesha dhahiri jinsi alivyo.
Sikujibu lolote lakini mpaka kufikia hapo hamu
yangu yangu ya kufungua ule mzigo ilikuwa
imeisha. Hata awe nani kwa vitisho ya Martin
lazima angetii tu. Nilihisi joto kali kutokana na
hofu. Dakika chache za vitisho kutoka kwa Martin
zilitosha kabisa kuifanya dakika moja ionekane
kuwa saa nzima.
***

Mzigo ukaletwa. Lilikuwa begi jeusi la kawaida.
Halikuwa tofauti na yale mabegi yanayouzwa pale
Karume Dar es salaam kwa wauza mitumba.
Nikatabasam kimoyomoyo. Nilianza kuhisi ushindi
fulani ndani ya nafsi yangu.Nikakabidhiwa begi na
Martin Kisha tukaingia kwenye gari lilelile
lililonileta. Wazo likanijia, wakati naingia ndani ya
lile gari nikasoma namba zake nikazikariri
kichwani. Nilipoingia kwenye gari nikaziandika
kwenye note book yangu. Tukaondoka kuelekea
‘guest’. Saa tatu na robo tulikuwa mbele ya jengo
lile la kifahari ambalo lilikuwa katika mtaa ambao
nilifahamishwa kuwa unaitwa Kirumba.
Martin alikuwa amemaliza kazi yake, akaniacha
peke yangu pale ‘guest’. Akaondoka baada ya
kuhakikisha kuwa amenikabidhi tikiti ya gari
ambalo lilikuwa linaondoka kesho. Akili yangu
ilikuwa inafanya kazi haraka kuliko uwezo wake wa
kawaida. Kwa kiasi fulani hili lilinishangaza.
Nikachukua begi langu na kuondoka pale ‘guest’.
“Anko vipi mbona unaondoka?” Aliniuliza dada wa
mapokezi
“Nimepata simu ya msiba hivyo siwezi kulala
hapa!” Nilimjibu huku nikiwa nimeshapiga hatua
kadhaa kuuendea mlango wa kutokea nje.Bado
aliendelea kuongea lakini sikumuelewa, akili yangu
yote ilikuwa juu ya mzigo na safari yangu.
Teksi chache zilikuwa zimeegeshwa nje ya ‘guest’
hii. Nikaisogelea moja ya teksi zile. “ Sema bosi
unaenda?” aliniuliza mmoja wa madereva wa
teksi. Nikaitikia kwa kichwa. “Naomba uniwahishe
kokote ninakoweza kupata magari yanayokwenda
Dar”nilisema huku nikiwa tayari nimeshakaa siti ya
nyuma.
“Duh! Saa hizi utapata lakini siti za nyuma”
“Hakuna shida ninachotaka ni kusafiri leo hata
kama itakuwa ni lori la samaki niko tayari!”
“ Nahisi Saibaba halijaondoka!” alisema huku
akikoleza mwendo wa gari yake. Baada ya dakika
kumi na tano tulikuwa Kituo kidogo cha magari
yanayoelekea Dar.
“ Shilingi ngapi?”
“Elfu tano Mkubwa”. Nikachomoa noti ya shilingi
elfu tano nikampa.
Mungu alisikia maombi yangu. Nilipofika tu, dada
mmoja akanifuata. “Kaka samahani kama unasafiri
nina tiketi yangu naiuza tena ni D 5 yaani dirishani,
mimi nimeahirisha safari mpaka kesho” Alisema
yule dada kabla hata ya kusalimiana. “ Unaonje
tukibadilishana tiketi, mimi nikupe ya kesho!”
“Nitashukuru sana kaka yangu maana kuna mizigo
muhimu nimesahau.”
Mchezo ulikuwa umekwisha, lengo lilikuwa
limetimia. Ni kama Mungu aliamua kunisaidia.
Moyo wangu ulitawaliwa na furaha nikajihisi amani
zaidi.
Tikiti aliyonipa ilikuwa ni ya basi la Mwanza
Coach. Safari yetu ikaanza saa sita kamili. Kama
ni mawazo basi safari hii nilikuwa na mawazo
zaidi kuliko ile ya kwanza. Ule mzigo
ulinishughulisha sana. Kuna nini ndani ya ule
mzigo.
”Ngoja nifike Dar nitaamua nini cha kufanya”
Niliwaza. Lakini upande mwingine nilikuwa nasikia
sauti ambayo ilikuwa inanionya, watu wenye
vitisho namna ile kweli wataniacha hai
nikishafikisha huo mzigo wao, kwanini walimuua
yule mwanamke? Maswali hayo yalizidi kunitisha
lakini yakiniongezea ujasiri wa kuvunja masharti.
***

Niliwasili Dar es salaam saa tisa na nusu alasiri.
Hii ilikuwa ni mapema zaidi kuliko nilivyotarajia.
Safari yetu ilichukua siku tatu. Watu walikuwa
wametawanyika hovyo pale kituo kikuu cha mabasi
cha Ubungo. Walikuwa kama siafu walioangukiwa
na kaa la moto. Miongoni mwao walikuwa nia
abiria ambao wanasafiri huku wengine wakiwasili.
Pia walikuwepo wapiga debe ambao walileta kero
kubwa kwa abiria.
Bonge alinionya kuwa nisipitie sehemu nyingine
kabla ya kumfikishia mzigo wake. Pia alinionya
kuwa iwapo sitatekeleza maagizo yake, basi
asingenipa malipo yangu kwa kazi ya kusafirisha
mzigo ule. Vile vile alinikumbusha kuhusu ile picha
ya hatari. Ni picha yangu ambayo ilikuwa
inaniweka katika wakati mgumu. Ni picha ambayo
leo inanifanya niwe mtumwa.
Kwa sababu ambazo mpaka leo sijazielewa
nikaamua kuvunja maagizo yake kwa kupitia
nyumbani kwangu Yombo Buza. Sifahamu kama
kuna nguvu ya ziada kutoka nje ya nafsi yangu
ilinituma kufanya uamuzi huo wa aina yake.
Kuvunja maagizo ya mtu kama Bonge halikuwa
jambo la kwaida.
Ilikuwa ni siku ya tatu toka nikabidhiwe begi lile.
Sikujua kilichomo ndani yake ingawa hisia
zilinituma kuwa huenda ni almasi. Kidogo nikaanza
kuingiwa na mashaka kwani nilionywa kuwa iwapo
nitathubutu kufungua tu, basi adhabu yangu
itakuwa ni kifo! “Hivi kweli nikiufikisha huu mzigo
nitaweza kuepukana na hicho kifo?” Lilikuwa ni
swali gumu ambalo nilijiuliza bila kupata majibu.
Lazima nifungue kwani Martin na Bonge watajuaje
kuwa mzigo umefunguliwa?
Nilipofika chumbani nikalitua begi lile kitandani.
Moyo ulikuwa unaenda mbio kama mtoto
aliyemuona daktari akiwa na sindano mkononi.
Nilimfikiria sana Martin. Huyu ndiye aliyenitisha
zaidi, jinsi alivyo! Ana umbo kubwa lenye misuli
iliyojengeka kama mnyanyua vitu vizito, macho
yake ni makubwa kama kurunzi huku uso wake
ukipambwa na kovu kubwa lililopita katikati ya uso
wake. Kwa jinsi alivyo alitosha kabisa
kumnyamazisha mtoto anaelia kwa neno moja,
huyo Martin anakuja!
Pale alipokuwa ananitizama nilikuwa sijamkosea
chochote lakini alikuwa anatisha kama nyoka
anayetaka kumrukia mtu. Macho yake yalionesha
wazi dalili zote za mtu mwovu kama si muuaji
kamili. Atanifanya nini akigundua kuwa nimefungua
ule mzigo? Iwapo alikuwa ananitazama kwa sura
ambayo kwake ilikuwa ya upole lakini nilibanwa na
haja ndogo, vipi nikutane naye siku ambayo
amekasirika? Ndo ajue sasa maagizo waliyonipa
nimeyavunja, atanifanya nini?
Bila shaka atanifanya kama alivyofanyiwa yule
mwanamke kule guest. Sijawahi kuona mtu
aliyeuwawa. Maiti ambazo nimewahi kuziona kwa
macho yangu ni za ajali ya gari. Taswira yake
ilinijia kichwani mara kwa mara. Mwili ulisisimka
na kufanya vipele vidogovidogo kama mtu
anayehisi baridi kali.
Maskini Merina, Mungu amlaze mahali pema
peponi. Amin.
Shauku yangu ya kutaka kujua kuhusu mzigo ule
ilisababishwa na vitisho vya Martin na Bonge.
Adhabu ya kifo kwa kufungua mzigo tu! Balaa
Laiti wasingenionya kiasi kile basi nisingekuwa na
wazo lolote juu ya mzigo ule. Ningeufikisha kama
walivyotarajia bila hata kuwa na chembe ya wazo
juu ya mzigo wao.
Nikalikazia macho begi lile jeusi. Lilikuwa kama
refarii katika maisha yangu. Nifungue niishi kwa
mashaka au niache niishi kwa amani.
****Hebu fungua huko bwana, vipi???
 
SEHEMU YA NANE
Laiti wasingenionya kiasi kile nisingekuwa na wazo
lolote juu ya mzigo wao. Ningeufikisha kama
walivyotarajia bila hata kuwa na chembe ya wazo
juu ya kutaka kujua kilichomo ndani.
Kwa mara nyingine nikalikazia macho begi lile
jeusi, lilikuwa kama refarii katika maisha yangu.
Nifungue niishi kwa mashaka au niache niishi kwa
amani. Kwangu lilikuwa jambo zito sana kwani
sijawahi kubeba kitu ambacho sikifahamu.
Jambo moja ambalo lilinikosesha raha ni kuwa
iwapo sitafungua basi nitakuwa na fumbo moyoni,
fumbo ambalo sitaweza kulifumbua maisha yangu
yote. Nakumbuka sana nilipokuwa mwanafunzi
jinsi nilivyoumiza kichwa kwenye mafumbo.
Nilikuwa sikubali kushindwa. Lakini kwa mara ya
kwanza leo nakabiliana na fumbo ambalo gharama
ya kufumbua kwake ni kifo.
Nikubali kushindwa?
Kweli nilikuwa naelekea kushindwa. Lakini kwa nini
nishindwe?
Nikiwa mtaalamu wa mafumbo nilikuwa na kazi
mbili, kwanza mzigo halafu uhai wangu. Lengo
lilikuwa ni kujua kuhusu ule mzigo bila kupata
matatizo, yaani nilitaka kuuwa ndege wawili kwa
jiwe moja.
Nikatabasamu huku nikiwa nalitazama vizuri begi
lile ambalo niliahidiwa pesa nyingi kwa kulifikisha
kwa muhusika bila kuvunja masharti. Fedha
nilizoahidiwa sijawahi kufikiria hata siku moja
kuwa ipo siku nitakuja kuzihesabu achilia mbali
kuzimiliki.
Kwanini kusafirisha lile begi kutoka Mwanza
nilipwe pesa zote hizo? Kutatua fumbo lile kwangu
lilikuwa jambo kubwa kuliko zawadi ambayo
ningepewa na bonge huku fumbo likiendelea kubaki
kama maisha ya kaburini ambayo maiti tu ndiye
anayejua yalivyo.
Haiwezekani! Lazima begi lifunguliwe.
Kabla sijafungua nikapata wazo muruwa kabisa.
Nikatabasamu, Lilikuwa wazo kabambe sana.
Nilitaka niue ndege wawili kwa jiwe moja.
Nilidhamiria kulifumbua fumbo lile bila kupata
matatizo yoyote. Nilianza kujihisi kuwa mshindi
ingawa bado niliendelea kujionya juu ya hatari
ninayokabiliana nayo. Bonge hajawahi kuliona lile
begi likoje kwani lilionekana wazi kuwa ni jipya, hii
ilinifanya niamini kuwa wazo langu litakuwa
muruwa.
Kabla sijafanya lolote nikakaa kitandani kwanza
kisha nikaegemea ukuta nikavuta pumzi kwa nguvu
na kuzishusha, taratibu zikaanza kunijia fikra juu
ya mambo ya ajabu ambayo yanatokea katika
maisha yangu.
Muda huu mfupi ambao nilikaa hapo uliweza
kunifanya niyatazame maisha yangu kama mtu
anayetazama filamu ndefu ya kusisimua. Nilikuwa
kama mtu ninayejitazama mwenyewe kwenye kioo.
Ilikuwa kana kwamba ninajisimulia kitu fulani.
Kabla sijaendelea naomba nikusimulie mwanzo wa
yote mpaka kufikia hapa, kwanza ingekuwa vema
unifahamu mimi ni nani?……
***

Naitwa Kajuna Daudi Kazakamba, ni mtoto wa
kwanza katika familia yenye watoto watatu, mimi
na wadogo zangu wawili wote wa kike Koku na
Waridi………
***
Baadhi ya watu wanaoishi Dar es salaam wana
akili za ajabu sana. Hawapendi kuishi maeneo
yenye nafasi na hewa nzuri. Hupenda sehemu
zenye misongamano ya watu na hususani zile
zilizoko kando ya barabara. Mfano mzuri maeneo
kama Kinondoni na Manzese. Hilo ndilo jambo
lililomfanya baba yangu kununua kiwanja eneo
ambalo liko karibu na barabara. Madhara yake
yalikuwa makubwa kwa baba na familia kwa
ujumla.
Ikiwa ni miaka kumi na mitano toka ajenge
nyumba hiyo akapokea barua kutoka serikalini
ikimtaka kuhama eneo hilo. Katika barua hiyo
serikali ilidai kuwa baba amejenga katika eneo
ambalo linatambuliwa kisheria kuwa ni hifadhi ya
barabara. Kwa masikitiko makubwa kabisa
nikashuhudia nyumba yetu ikibomolewa. Hakuna
fidia iliyotolewa ingawa vyombo vya habari
vikiwanukuu viongozi husika vilitoa taarifa kuwa
waathirika wote wamelipwa fidia zao.
Ukawa mwanzo mpya wa maisha ya kupanga na
kuhamahama, mpaka pale baba alipojenga nyumba
nyingine Mwananyamala baada ya kupata fedha
zake za mafao kutoka shirika la reli Tanzania
ambako alifanyia kazi. Fedha hizi zilipatikana kwa
mbinde, iliwalazimu wazee kuandamana na kulala
barabarani wakati wa kudai mafao hayo. Wakati
mwingine polisi walilazimika kutumia nguvu za
ziada kuwadhibiti wazee hao.
Fedha zote za kiinua mgongo ziliishia kwenye
ujenzi wa nyumba hiyo. Mwaka huo nilikuwa
kidato cha sita shule ya sekondari Tambaza.
Mapema mwaka uliofuata nikahitimu masomo
yangu.
Kama zilivyo hadithi za watoto wengine wanaotoka
kwenye familia kama zetu hapo ndio ikawa tamati
sikuweza kuendelea.
Nikaanza kutangatanga kutafuta maisha.
Nikahama Mwananyamala kwa wazazi wangu
nikahamia Yombo buza. Huko nilihama nyumba
kadhaa hatimaye nikapata sehemu ambayo nilikaa
muda mrefu kuliko nyumba nyingine.
Chumba kimoja, kitanda, ndoo na vyombo vidogo
vidogo vilikuwa vinaonesha taswira halisi ya
maisha yangu. Ulikuwa mkusanyiko usiovutia ndani
ya chumba hicho cha kupanga, hakukuwa na
tofauti kubwa na sehemu inayouziwa pombe za
kienyeji. Niliridhika kuishi maisha hayo kuliko
kumuongezea baba mzigo, kwani biashara yake
kubwa kipindi hicho ilikuwa ni samaki ambao
alikuwa anawauza katika mitaa ya Mwananyamala
na Kinondoni, pale inapotokea hali ya hewa si nzuri
alikuwa anachoma mahindi na kuyauza. Baba
yangu hakuwa mtu anayependa kukaa bila kazi
mwenyewe alijisifu kwa kusema yeye ni zao la
Tanu Youth league.
***
Ilikuwa saa 12.37 jioni. Nilivua sare zangu za kazi
nikazitia kwenye boksi. Nikachagua nguo safi
kutoka kwenye kamba ya nguo. Kamba hiyo
niliifunga kwenye misumari ambayo niliigongea
ukutani. Baadhi ya wenye nyumba hawapendi
mtindo huu wa kutoboa ovyo nyumba zao kwa
misumari. Nyumba niliyoishi haikuwa na masharti
kama hayo, vyumba vyote vilikuwa vimetobolewa
kwa misumari. Kimsingi ulikuwa ni uharibifu ambao
wakati mwingine uliweza hata kusababisha nyufa
ndio maana baadhi ya wenye nyumba walikuwa
hawaridhishwi na hilo. Sisi tulikuwa na bahati
kwani mwenye nyumba alikuwa mlevi hivyo wewe
fanya lolote lakini siku ikifika mpe chake akalewe.
Hakuwa na uchungu sana na nyumba yake labda
kwa kuwa ni nyumba ya urithi. Nilikuwa naamini
kuwa kitu ambacho mtu hukipata bila kukitolea
jasho mara nyingi hakionei uchungu na wala
hakithamini kama kile ambacho amekifanyia kazi.
Niliitazama kalenda ya kampuni ambayo nilikuwa
nafanyia kazi, nikagundua kuwa ilikuwa ni ya
miaka miwili iliyopita. Niliziangalia kwa hasira
picha za watu ambao walikuwa wanacheka kwenye
kalenda ile. Walikuwa na matumbo makubwa
ambayo bila shaka yalikuwa yanawapa shida
wakati wa kupumua na kulala. Hivi hawa
wanakumbuka kweli kuwa kuna watu wanapata
shida duniani au wanajali matumbo yao tu?
Kwenye picha ile kulikuwa na Watanzania wenye
asili ya kiasia na wale weusi kama sisi.
Nikaitazama tena kwa uchungu kalenda ile.
Kalenda mpya zilikuwa zinatoka kila mwaka, ili
uweze kupata kalenda hizo ulitakiwa
kuwabembeleza waajiri waweze kukupatia. Wengi
wao walikuwa ni watu wenye majivuno. Sikuwa na
muda wa kumbembeleza mtu, kazi yenyewe
sikuipenda, tatizo kubwa sikuwa na kazi nyingine
ya kufanya. Kilichonikera zaidi kazi zenyewe
hazikuwa za kila siku huku siku nenda rudi
tukiendelea kuwa vibarua.
Tulikuwa tunarushiwa vikaratasi ambavyo
vimekunjwa, ukifungua unakuta idadi ya siku
utakazofanya kazi kwa mwezi pamoja na malipo
utakayolipwa. Ilikuwa ni kampuni inayojishughuli
sha na utengenezaji wa juisi za aina mbalimbali,
biskuti na mikate. Ilikuwa ni miongoni mwa
makampuni yanayosifika sana kwa kusamehewa
kodi. Nilipata kusikia tetesi kuwa ni ya shemeji
yake kigogo mkubwa wa wizara ya viwanda na
biashara. Roho iliniuma sana, Mungu
ametuzawadia sote hii nchi, lakini kuna watu
wanaoifanya kuwa mali yao. Hawa ni wale ambao
hata sheria haifanyi kazi upande wao.
Nilizikagua tena zile nguo nikaridhika kuwa ni safi.
Nikavaa shati jeupe, suruali nyeusi na viatu vyeusi.
Sikusahau kufunga tai siku hiyo. Nikaonekana
kama mmoja wa wafanyakazi wa benki kwa nguo
nilizozinunua kwa mmachinga. Nikazikagua nywele
zangu, hazikuhitaji kitana kuzichana. Nikachukua
brashi, nikaanza kupitisha kichwani huku
nikijiangalia kwenye kioo kidogo.
***

Sikuwa mpenzi wa kumbi za starehe lakini siku
hiyo niliamua kusafisha macho. Nguo zile zilikuwa
zinanipendeza sana ilibidi mtu afanye kazi ya ziada
kugundua kuwa zote nilikuwa nimenunua kwa
wamachinga mitaani.
Jioni ile nilikuwa nazunguka maeneo mbalimbali ya
mji bila mpangilio maalum. Hakuna nilichokuwa
natafuta, labda ilikuwa ni furaha ya malipo yangu
kibaruani. Siku hiyo mifuko yangu ilikuwa imenona
kwa noti za kitanzania . Mwisho nikafika sehemu
ambayo nilihitaji kupumzika. Nilikuwa nimechagua
baa moja iliyoko maeneo ya Tabata Mawenzi. Ni
sehemu ambayo inasifiwa kwa utulivu. Nililijuwa
hilo kupitia kwa baadhi ya vibarua wenzangu
wanaoishi maeneo hayo.
Nikakaa kwenye kona ya kushoto ya baa. Vitu
vingi mle ndani vilikuwa vigeni kwangu. Mazingira
ya mle ndani yalikuwa ni ya aina yake. Kuna vitu
ilikuwa ndio kwanza naviona humu ndani. Kubwa
ilikuwa ni staili ya mavazi, hasa yale ya wanawake.
Wengi walikuwa wamevaa mavazi ambayo
yaliruhusu mapaja yao kuwa nje, nilimeza mate.
Kwa upande wa wanaume walikuwa na mavazi yao
ya siku zote, ya kawaida. Sijui kwanini nilipokuwa
kwenye kundi la watu nililaumu sana mavazi haya
ya kina dada, leo niko peke yangu najikuta
nikivutiwa na mavazi haya, tena nilitamani ufupi
wa sketi zao ungezidishwa ingawa kimsingi
zilikuwa zimefika mwisho.
Labda ni unafiki.
Hii ndio baa bwana, starehe nyingi zinapatikana
huku. Mapaja ya hawa watoto wa kike yalinifanya
nipagawe kabisa. Siku nyingi nilikuwa sijaona
mambo ya namna hii kwani toka nianze hivyo
vibarua mara nyingi nilikuwa nashinda nyumbani.
Moyo ulikuwa unaenda mbio kila nilipokuwa
ninatizama vitu adimu namna hii, nilihisi kubanwa
na pumzi kutokana na kuwatazama viumbe hawa.
Kona ya kulia ya baa ile kulikuwa na meza kubwa
ambayo ilikuwa imefunikwa kwa zulia la kijani.
Meza hii ilikuwa imewekwa vishimo sita, vitatu kila
upande. Katikati kulikuwa na mipira midogo yenye
rangi tofauti tofauti. Wazee kwa vijana niliwaona
wakishindana kuipiga ile mipira kwa kuiingiza
kwenye vile vitundu. Walifurahi na kushangilia
lakini nilikuwa sijui kabisa nini maana ya mchezo
ule ambao baadaye nilikuja kugundua kuwa
unaitwa ‘pool’. Kwani siku zile ulikuwa ndio
kwanza unaanza kupata umaarufu nchini.
“Kaka nikusaidie nini?” Nilishtushwa na sauti ya
kike, nikageuka. Duh, huwezi kuamini! Nilishindwa
kutofautisha muhudumu wa baa na mfanyakazi wa
benki. Mwanamke mrembo alikuwa amesimama
mbele yangu. Alikuwa na uso wa duara ambao
ulisanifiwa vizuri na mola muweza kwa ngozi laini
nyeusi ambayo haikuhitaji vipodozi vikali. Macho
yake yalikuwa makubwa kiasi cha kuyafanya
mapigo ya moyo wangu kuongezeka pale
alipokuwa ananitazama. Umbo lake lilikuwa ni lile
ambalo linajulikana kama namba nane.
Nilimshangaa mrembo huyu ambaye hakuwa na
nyongeza zaidi ya urembo wa asili.
“Inakuwaje mwanamke mrembo kama huyu
anafanya kazi baa!” Niliwaza.
“Naomba pepsi baridi tafadhali!” Yule dada
alinitazama kwa mshangao kidogo. Bila shaka ni
kutokana na kujisahau na kumshangaa wazi wazi.
Sio siri alikuwa anavutia. Akatabasamu kidogo
kisha kwa sauti ileile ya kuvutia akaongea.
“ Naomba ulipe kwanza tafadhali ” alisema huku
akinyoosha mkono wake wa kulia. Nikampatia noti
ambayo tayari nilishaiweka kwenye mfuko wa
shati.
Aliporudi alikuwa amebeba sinia likiwa na pepsi na
karatasi laini ikiwa ndani ya glasi. Akanikabidhi
chenji yangu
Niliwaona watu wengi wakinywa vinywaji vyao
taratibu, kwa kuwa nilikuwa na kiu sikuupenda
utaratibu ule. Nikajimiminia pepsi yangu kwenye
glasi, nikanywa ile soda funda tatu za nguvu.
Ndani ya dakika moja na nusu glasi ikawa tupu.
Nikamalizia soda kidogo ambayo ilibaki kwenye
chupa. Ile soda ilikuwa tamu mno! labda kwa kuwa
nilikuwa nakunywa mara moja moja. Sikuwa na
uwezo wa kununua soda kila siku, kwa mshahara
gani!? Hata pale nilipokuwa nyumbani kwa wazazi
wangu bado soda kilikuwa kitu adimu. Soda
ilikuwa haipatikani mpaka ushikwe na homa tena
baada ya kudeka sana na kukataa vyakula
mbalimbali ndipo utaletewa, pia soda ilipatikana
siku za sikukukuu; Hapo familia nzima itakunywa
soda.
Nilimalizia funda la mwisho huku nikiusikilizia ule
ubaridi ulivyokuwa unashuka kooni na kunipa raha
na faraja. Angalau uliweza kunisahaulisha ugumu
wa kazi za vibarua vya viwandani. Nilitamani hali
ile ingekuwa kila siku, lakini zilikuwa ni ndoto na
mawazo ya masikini ambaye kutwa haachi kuwaza
kupata fedha za ghafla na ndoto zilizojaa bahati
nasibu ya kuokota kiroba cha noti au dhahabu.
Ghafla, akaingia mwanamke ambaye alivuta hisia
za wanaume wengi. Kila mwanaume aliyegeuka
kumwangalia aligandisha jicho lake kwa sekunde
kadhaa kisha akarudisha jicho mahala pake. Wengi
walikuwa na wapenzi wao mle ndani hivyo
walijifanya kama hawajaona chochote kumbe
walikuwa wanazuga tu. Niliona mmoja akipigwa
kibao na mtu niliyehisi kuwa ni mkewe baada ya
kugandisha jicho lake kwa muda mrefu zaidi.
Nikacheka! Kwani yule mtu alikuwa na umri ambao
ungemfanya awe anakaribia kustaafu serikalini au
ameshastaafu karibuni.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA NANE
Shauku yangu ya kutaka kujua kuhusu mzigo ule
ilisababishwa na vitisho vya Martin na Bonge.
Adhabu ya kifo kwa kufungua mzigo tu! Balaa
Laiti wasingenionya kiasi kile basi nisingekuwa na
wazo lolote juu ya mzigo ule. Ningeufikisha kama
walivyotarajia bila hata kuwa na chembe ya wazo
juu ya mzigo wao.
Nikalikazia macho begi lile jeusi. Lilikuwa kama
refarii katika maisha yangu. Nifungue niishi kwa
mashaka au niache niishi kwa amani.
Kitu kimoja ambacho kilinikosesha raha ni kuwa
iwapo sitafungua basi nitakuwa na fumbo moyoni,
fumbo ambalo sitaweza kulifumbua maisha yangu
yote. Nakumbuka hata nilipokuwa mwanafunzi
niliumiza sana kichwa kwenye mafumbo. Nilikuwa
sikubali kushindwa. Kwa mara ya kwanza leo
nakabiliana na fumbo, fumbo ambalo kufumbua
kwake ni kifo. Nikubali kushindwa? Kweli nilikuwa
naelekea kushindwa. Lakini kwa nini nishindwe!?
Nikiwa mtaalamu wa mafumbo nilikuwa na kazi
mbili, kwanza mzigo halafu uhai wangu. Lengo
lilikuwa ni kujua kuhusu ule mzigo bila kupata
matatizo.
Nikatabasamu huku nikiwa nalitazama vizuri begi
lile ambalo niliahidiwa pesa nyingi kwa kulifikisha
kwa muhusika bila kuvunja masharti. Fedha nilizo
ahidiwa sijawahi kufikiria hata siku moja kuwa
nitakuja nizitie mikononi.
Kwanini kulisafirisha lile begi kutoka Mwanza
nilipwe pesa zote hizo? Kutatua fumbo lile kwangu
lilikuwa jambo kubwa kuliko zawadi ambayo
ningepewa na bonge huku fumbo likiendelea kubaki
kama maisha ya kaburini ambayo maiti tu ndiye
anayejua yalivyo. Haiwezekani! Lazima begi
lifunguliwe.
Kabla sijafungua nikapata wazo. Nikatabasamu.
Lilikuwa wazo kabambe. Nilitaka niue ndege wawili
kwa jiwe moja. Nilidhamiria kulifumbua fumbo lile
bila kuniletea matatizo. Nilianza kujihisi kuwa
mshindi ingawa bado niliendelea kujionya.
***

Kama nilivyoeleza lile begi halikuwa na tofauti na
yale Mabegi yanayouzwa pale Karume. Kwa akili
ya Bonge ningewasili Dar Jioni ya siku iliyofuata.
Hivyo nilikuwa huru kutekeleza malengo yangu
mapema zaidi.
Nyumba niliyokuwa naishi haikuwa mbali sana na
Kituo cha magari Buza Kanisani. Ilinichukua dakika
takribani kumi kutoka nyumbani hadi kituoni.
Nilipofika nikapanda bajaji ambalo lilikuwa linaenda
kituo maarufu ambacho kinajulikana kama mwisho
wa lami. Siku za nyuma hapo ndio ulikuwa mwisho
wa lami kama unatokea Lumo, lakini sasa lami
ilikuwa imevuka hapo. Jina halijabadilika.
Nikiwa ndani ya bajaji nilikuwa nafikiria jinsi
nitakavyotumia fedha za mauzo ya almasi ambazo
zipo kwenye begi.
”Ni matanuzi tu si kingine!” niliwaza.
Ukweli ni kwamba sikuwa na uhakika ni mzigo gani
ambao ulikuwa kwenye lile begi lakini sikuwa na
shaka kuwa thamani yake ilikuwa kubwa sana.
Dola elfu hamsini kwa kufuata mzigo tu, unafikiri
mzigo kama huo utakuwa na thamani gani? Tena
mtu anakupa milioni moja zisizo na maelezo wala
masharti.
Bajaji lilikuwa limefika eneo maarufu la mwisho wa
lami. Nikamlipa dereva wa bajaji hela yake.
Nikapanda daladala kutoka Mwisho wa lami hadi
Lumo. Mpaka hapo naomba uelewe wazi kuwa
nilikuwa na fedha za kutosha ambazo sijawahi
kuzishika maishani mwangu. Fedha hizo ni zile
nilizopewa na Bonge . Kwani nilipozihesabu
zilikuwa shilingi milioni moja. Nilikuwa sijawahi
kushika kiasi kikubwa cha fedha kama hicho katika
maisha yangu. Lakini thamani ya zile fedha niliiona
kuwa ndogo sana kila nilipoufikiria ule mzigo.
Nilijua kuwa miezi mitatu ijayo nitakuwa tajiri
mkubwa sana. Ajabu! Nilikuwa nawaza mtaa
ambao utanifaa baada ya kupata fedha zangu.
Nilikuwa nimeshaamua akilini mwangu kuutorosha
ule mzigo, tatizo lilikuwa ni mbinu gani salama ya
kuutorosha mzigo ule. Nilitaka kutafuta mbinu
ambayo haitamshtua Bonge mapema. Labda
agundue wakati nitakapofika sokoni Nairobi,
maana nasikia huko ndiko waliko wanunuzi
wakubwa wa madini.
Nilifika kituo cha teksi Lumo. Moyo ulikuwa
unaenda mbio sana, nilikuwa nimeshavunja sharti
la kwanza. Nilikuwa nakaribia kuvunja sharti la pili
tena kwa staili mbaya zaidi kuliko alivyotarajia
muonyaji.
Potelea mbali!
“Vipi boss! tunaenda wapi?” Dereva teksi aliniuliza
baada ya kuona nimeingia kimyakimya kwenye gari
lake bila kumueleza lolote. Hapa nilianza kuona
hali ya hatari niliyokuwa nakabiliana nayo, akili
yangu haikuwa katika hali ya kawaida kwani
nilikuwa nimeingia kwenye gari bila kujijua.
Nilikuwa nimezidiwa na mawazo kiasi ambacho
mwili ulikosa mawasiliano mazuri na akili.
“ Nipeleke Karume tafadhali”
“Vipi boss unapenda muziki?” aliniuliza huku
akikata kona kona kutoka kituo cha teksi na
kuingia barabara inayoelekea kariakoo.
“Poa tu!” Nilimjibu kwa mkatao lakini kimsingi
sikuhitaji aina yoyote ya burudani kwa wakati huo.
Muziki mzuri uliokuwa unatoka kwenye gari lile
haukuweza kuniliwaza hata kidogo. Ulikuwa muziki
wa siku nyingi ambao uliimbwa na Washirika
Tanzania stars watunjatanjata.
Tulipofika maeneo ya Tazara tukaiacha Bara bara
ya Pugu ambayo sasa inajulikana kama barabara
ya Mwalimu Nyerere tukaingia barabara ya
Mandela. Sikuipenda sana tabia hii ya kupachika
karibu kila kitu jina la Mwalimu Nyerere. Ingekuwa
bora kama mambo mengi yangefanywa kwa kuiga
tabia zake na aina ya uongozi wake. Mimi sio
mwanasiasa lakini kitu kimoja kinanifanya
nimheshimu na kumthamini Mwalimu, Mwalimu
alithamini rasilimali zetu. Mwalimu hakupenda
tabia ya kujilimbikizia mali hovyo, Wakati wa
mwalimu hakukuwa na misamiati ya ajabu kama;
Mafisadi papa, mafisadi nyangumi na mafisadi nini
sijui…….
Wakati bado naendelea kuwaza dereva
akasimamisha gari kwenye kituo cha mafuta cha
Buguruni. Akajaza mafuta, kisha akaiondoa teksi
kwa kasi. Akafuata barabara ya uhuru.
Tulifika Karume Saa 11.47. Nikachagua saizi ya
begi nililolitaka. Dereva wa teksi nilishamwambia
anisubiri, hivyo nilipolipata lile begi nikaingia
kwenye teksi tukarudi Lumo. Tulipofika Lumo
nikamwamrisha dereva anipeleke Buza kanisani.
“Shilingi ngapi?” nilimuuliza baada ya kufika.
“Elfu ishirini bosi!” Alijibu huku akitikisatikisa
funguo za gari lake kama mtu anayesubiri upinzani
kutoka kwangu tuanze mabishano.
“Poa nisubiri!” Nilimjibu huku nikilipeleka begi lile
ndani.
Nilipofika ndani nikaliacha lile begi ambalo
nimetoka nalo Karume kisha nikachukua lile
ambalo nilitakiwa kumfikishia Bonge. Hapo
nilishaamua kufanya ujanja wa kubadilisha mzigo.
Nilipotoka nilikuwa na begi lingine kama lile
tulilotoka nalo Karume. Tofauti na madereva teksi
walio wengi huyu hakuwa mwongeaji. Muda
mwingi alikuwa kimya na alionesha kuwa mtu
makini. Tabia yake hii ilinivutia na kunifanya niwe
na hamu ya kuongozana nae kila nilikokwenda.
Lakini kitu kimoja hakikufichika kwenye sura yake,
alikuwa mtu mwenye dalili za huzuni hakuwa na
furaha. Hata ule uchangamfu mdogo aliouonesha
kwangu ulikuwa wa kulazimisha.
“Tuna safari nyingine bosi?” Aliniuliza baada ya
kuona nikiingia na begi kwenye gari. Niliitikia kwa
kichwa.
“wapi?” aliuliza tena kwa mkato.
“Mbagala charambe!” nilimjibu kwa mkato.
Nilichomoa noti mbili za shilingi elfu kumi
nikampa. Hayo yalikuwa ni malipo ya mizunguko
ambayo tulikwishaifanya.
***

Kama ilivyo ada, baadhi ya watanzania wenye
kipato hupenda kuibatiza majina mabaya au ya
dharau mitaa ya watu wenye kipato duni. Hili
lilikuwa miongoni mwa maeneo ambayo huitwa
Uswahilini. Sijui kwanini watu wenye kipato
wanapenda kuyapachika maeneo haya kwa majina
dharau kama hayo. Uswahilini sio jina baya tatizo
ni kusudio la hao waitaji, kimsingi huwa
wanakusudia kuwa ni maeneo ya chini ambayo
watu waliostaarabika hawastahili kuishi. Ni wazi
kuwa watu hawa wamerithi kasumba ya wakoloni
ya kudharau watu weusi, kitu kimoja watu hawa
hawajagundua. Laiti wangejua kuwa wao ni
watumwa na nafsi zao zimehiyari utumwa kuliko
uungwana wasingethubutu! Kwanini wasiwe
watumwa wakati hawa ndio wale waliohiyari kuwa
mbwa ulaya kuliko binadamu Afrika? Heri babu
zetu waliingia mikataba ya ulaghai bila kujua kuliko
wao waliohiyari kuutumikia uhayawani huko ulaya
na kupoteza utu wao ambao thamani yake ni
kubwa.
Nyumba za maeneo haya zilikuwa zimejengwa bila
kufuata utaratibu. Zilikuwa zinaonesha taswira
halisi ya Mtanzania wa hali ya chini. Mtanzania
ambaye ni vigumu kukamilisha milo mitatu kwa
siku. Hata watoto ambao ungekutana nao mitaa hii
wangekuwa ni tafsiri tosha kwa yeyote yule kujua
kuwa maeneo haya ni ya watu wa hali ya chini.
Niliteremka kwenye teksi nikamuashiria dereva
anisubiri. Alionekana kuniamini. Akanisubiri wakati
naingia kwenye vichochoro vya Mtaa wa Charambe
magengeni. Ghafla! Nikamuona mzee wa makamo
ambaye alikuwa ananifuata kwa hatua za haraka.
“Aah, mjomba huyo, Karibu sana!” Alikuwa ni
mjomba’angu Mzee Francis Kipupwe. Ni kaka wa
mama yangu mzazi. Akanishika mkono na
kuutikisa kwa furaha huku akinitembeza kwa kasi
kuelekea kule iliko nyumba yake.
“ Haya mjomba habari za siku tele!” alinisalimia
kwa furaha huku akionesha wazi kufurahishwa na
ujio wangu.
“Salama mjomba shikamoo.”
“Marhaba!”
Akaingia ndani na kunitolea stuli chakavu.
“Haya mjomba kwanini umetupa jongoo na mti
wake!?”. Nilijichekesha chekesha kabla ya kumjibu.
“Si unajua mjomba, maisha yamekuwa magumu
sana.”
“Sawa lakini siku hizi kuna mitandao kwanini hata
simu hutaki kutupigia? “
“Nisamehe mjomba nitajirekebisha!” Nilimeza mate
kisha nikaendelea
“Kwa leo naomba unisamehe mjomba sina muda
wa kupoteza nina kazi muhimu ambayo inabidi
niifanye, naomba tu hili begi langu niliache hapa
kwako nitalifuata Kesho kutwa Mungu akipenda.”
“Hakuna shida mjomba!”. Kitendo cha kuacha begi
langu kilionekana kumfurahisha sana mjomba.
Nikaingiza mkono mfukoni nikatoa noti za shilingi
elfu kumikumi, nikahesabu noti tano. Wakati
nahesabu nilimuona mjomba akiwa amezikodolea
macho yenye uchu. Nikampatia shilingi elfu
Hamsini. Ni kawaida ya mjomba kupenda kucheka
lakini siku hiyo alicheka akapitiliza. Niliweza
kuyaona hata meno yake ya mwisho.
Nikarudi kwa dereva wa teksi.
“ Vipi shwari?” aliniuliza.
“Shwari twen’zetu!”. Tuliingia kwenye gari
tukaondoka. Dereva teksi alinifurahisha sana kwani
hirimu yetu ilikuwa moja halafu alikuwa mtu makini
sio mropokaji. “Samahani muda mwingi wa safari
yetu tumekuwa tunatembea bila kufahamiana hata
majina” nilisema kisha nikamtambulisha jina langu.
“Naitwa Omari Kisilani, Pale kijiweni najulikana
zaidi kama Ommy Kiss au Mjeda” “Kwanini
unaitwa Mjeda!”
“Nimewahi kufanya kazi jeshini miaka miwili
nikaamua kuacha” sikutaka kuhoji kwanini aliacha
kazi hiyo kwani kila mtu ana namna yake
anavyopenda kuishi.
“Ok, nahitaji kwenda Mwananyamala!”
“Poa.” Alinijibu
***

Saa 3.30 Tuliondoka maeneo ya Mwananyamala
ambako nilienda kuwasalimia wazazi na wadogo
zangu. Wote niliwakuta wakiwa wazima.
Niliondoka nyumbani nikiwa na huzuni sana.
Sikuwa na uhakika kama nitaweza kuwaona tena
ndugu zangu. Nilikuwa katika mikono ya mauti
muda huo. Sikujua hatma yangu. Niliitazama tena
tena nyumba ya baba yangu nikajikuta nikitiririkwa
na machozi.
Gari lilifika kwenye kona tukaiacha nyumba ile
sikuweza kuiona tena nyumba yetu. Nilikuwa
nasikia uchungu kwelikweli. Kimsingi safari yangu
ilikuwa ni kwenda kuaga. Niliwakumbuka rafiki
zangu mbalimbali ambao nilikuwa nikicheza nao
maeneo yale.
“Rafiki yangu mkubwa Bundu Mayala yeye alikuwa
amebahatika kuajiriwa katika benki ya CRDB tawi
la Lumumba akiwa dirishani sijui ndio keshia au
nani vile … Lakini bahati iko upande wake maana
tumemaliza wote kidato cha sita na yeye
hajasomea kozi yoyote kama mimi.” Hayo yalikuwa
ni mawazo tu ambayo yalikuwa yanapita kichwani
mwangu. Niliwaza mambo mengi mengine yakiwa
ni ya utotoni, nilimkumbuka sana shangazi yangu
mama Douglas, alikuwa ameiacha dunia wakati
nampenda huenda kifo ikawa sababu ya kukutana
naye. Sijui kama watu waliokufa wanakutana au
ndio wale wanaogeuka mizimu na kusumbua watu,
sijui kama kweli kuna mizimu maana huwa naiona
kwenye filamu tu! Lakini kwanini niwaze zaidi kifo?
Ah! Siko tayari kufa, sijajiandaa nimejiandaa kuishi.
***

Tulifika Tabata Kisukuru saa 4.19. Betty Alikuwa
amepanga mbele kidogo ya kituo cha Kimanga
mwisho. Alikuwa karibu kabisa na Mazda bar.
“Twende mpaka mtaa wa nyuma pale Mazda bar”
Nilimuelekeza Ommy ambaye pamoja na kupata
mteja wa kutwa bado hakuonekana mwenye
furaha. Tulipofika nyumbani kwa Betty
nikamuashiria Ommy anisubiri nje. Akalaza kichwa
chake kwenye usukani, ni wazi alikuwa ameniamini
alijua siwezi kutoroka.
Nikaingia chumbani kwa Betty baada ya kubisha
hodi dakika kadhaa, pamoja na upole uliokuwa
katika sura ya Betty lakini hakuweza kunificha
hasira aliyokuwa nayo. Kwa makusudi mazima
niliamua Betty awe mtu wa mwisho kutokana na
uzito na umuhimu wake. Mwanamke mpole
mwenye mapenzi ya kweli, ua la moyo wangu.
Nikatabasamu licha ya hasira alizokuwa nazo.
“Ulikuwa wapi siku nne mfululizo hatujaonana?”.
Alianza kuuliza kabla hata ya salamu.
“Usiwe na haraka mpenzi nina mambo mazito ya
kukueleza.”
“Haya lete huo uongo wako maana nilishasema
mapenzi siku hizi yamejaa utapeli!” alisema Betty
kwa hasira huku akinisogezea kiti cha plastiki.
Tukakutanisha macho yetu. Sikuweza kuvumilia
machozi yalianza kunitoka. Betty ndiye mpenzi
wangu wa pekee. Sijawahi kuwa na mpenzi kabla
ya Betty. Kama walikuwepo basi ni michezo ya
mimi Baba wewe Mama. Kwa kifupi nilikuwa
nimetulia. Nilimtazama kwa jicho la huzuni kwa
sababu sikuwa na uhakika kama nitaweza
kumuona tena Betty. Aliniona nikiwa na majonzi
akanisogelea nakuanza kunifuta machozi kwa
kanga yake.
“Betty sina uhakika kama baada ya kesho
tutaweza kuonana tena na wewe……..”Nilimkazia
macho Bety ambaye alionekana kushtushwa sana
na kauli yangu, hasira zake zote zikaisha. Akawa
na shauku kubwa ya kutaka kujua nini kimetokea.
Nikamueleza kila kitu mpaka safari ya Mwanza
lakini sikumweleza wapi nimeuficha ule mzigo.
Alinitazama kwa jicho lililojaa udadisi huku akikosa
la kuongea. Niliona machozi yakitiririka kwenye
mashavu yake kama maji ya chem chem kwenye
miamba. Alikuwa na majonzi makubwa mpaka
nikajuta kwa nini nilimueleza ukweli. Nikasimama
kisha nikamsogelea nikampiga mabusu mfululizo.
“ Kwanini siku zote hukunieleza mambo mazito
kama hayo?”
“Ni tukio la juzi tu ningekueleza lini?”
“Huyo Mwanamke aliyeuwawa gesti kauwawa
juzi?”
“Ni tukio ambalo lilitokea kabla hatujawa wapenzi!”
“Lakini kulikuwa na umuhimu wa kunieleza”
aliongea huku akiendelea kutokwa na machozi! “
“Samahani kwa hilo mpenzi, yaliyopita si ndwele”
niliendelea kujitetea
“Sawa sasa kwanini usiwape huo mzigo wao?”
“Sina uhakika kama nikiwapa wataniacha hai”
“Na usipowapa?”
“Nina uhakika wataniua wakinitia mikononi mwao”
“Basi bora uwape uepukane nao!”
“Sikiliza mpenzi huu ni mchezo wa kifo, hainiingii
akilini kwa wauaji wakubwa kama wale kukubali
kunilipa dola elfu hamsini eti kwa kusafirisha mzigo
tu!”
“Kwa hiyo unaamua vipi?”
“Nitawapelekea mzigo feki ili hata wakiniua tukose
wote” Nikamuona Betty akiitikia kwa kichwa
kukubaliana na mimi.
“Iwapo watakulipa hali ya kuwa umewapa mzigo
feki utafanyaje?”
“Nina uhakika hawatanilipa kwani muonekano wao
umejaa unafiki mkubwa!”
“Betty, mi nafikiri hatuna muda zaidi wa kupoteza
tutaonana Mungu akipenda.” Niliamua kumuaga
baada ya kuona muda mrefu tukitazamana kwa
hisia za majonzi na si mapenzi kama ilivyo
kawaida yetu.
“Kajuna mpenzi, unaonaje tukiwa wote katika kila
hatua yako!”
“Betty, sipendi nikusababishie matatizo huu ni
mchezp hatari kuhusika kwako kunaweza kuzalisha
mambo mengine mabaya zaidi, bora uniache peke
yangu niicheze hii ngoma na si vinginevyo.”
Nilipojibu hivyo nikainuka na kuuendea mlango.
Kabla sijaondoka Betty akaniita kwa sauti ndogo.
“Kajuna mpenzi.” Nikageuka akanivuta kwake kisha
akanikumbatia. Akanikumbatia kwa nguvu sana.
“Kajuna, naamini kuwa una mapenzi ya kweli
kwangu, naamini kuwa uko nami kwa kila hali,
kitendo cha kuniamini na kuniambia siri hii nzito ni
imani kubwa uliyo nayo kwangu sina cha
kukushauri fanya unaloona kuwa bora niko nyuma
yako kwa moyo wangu wot…….” Alimaliza kwa
kilio.
“Betty naomba nikuahidi kuwa iwapo huu mchezo
nitaumaliza salama basi nitaanzisha safari mpya
katika maisha yangu, nakusudia kufunga pingu za
maisha wewe ndio chaguo langu, wewe ndio………”
sikuweza kuongea chochote nilichokusudia
machozi yalikuwa yanadondoka kama matone ya
mvua, Donge lilikuwa limenishika kooni nikajikuta
nikiendelea kumkumbatia Betty kwa hisia kali.
Ommy alikuwa ametulia kwenye usukani huku
akiwa hana wasiwasi kabisa. Alikuwa mpole lakini
mwenye huzuni. Nilishindwa kujua huzuni ya
Ommy inatokana na nini. Nilikuwa nashindwa
kumuuliza kwani kuna mambo mengi ambayo hata
yeye angeweza kuniuliza lakini hakufanya hivyo.
Tabia yake hii ndio ilionitisha na kunifanya hata
mimi nisithubutu kuuliza.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA TISA
Ommy alikuwa ametulia kwenye usukani huku
akiwa hana wasiwasi kabisa. Alikuwa mpole lakini
mwenye huzuni. Nilishindwa kujua huzuni ya
Ommy inatokana na nini. Nilikuwa nashindwa
kumuuliza kwani kuna mambo mengi ambayo hata
yeye angeweza kuniuliza lakini hakufanya hivyo.
Tabia yake hii ndio ilionitisha na kunifanya hata
mimi nisithubutu kuuliza.
***

Saa 6.39 nilifika nyumbani kwangu Yombo buza.
Nilikuwa nimechoka sana. Sikuweza kufanya jambo
lolote zaidi ya kulala Ikiwa ni baada ya kula Chips
kwenye baa iliyokuwa karibu kabisa na nyumbani
kwangu.
Niliamka saa 11 Alfajiri. Ilikuwa ni siku ya ahadi.
Siku ngumu kuliko zote zilizowahi kutokea katika
maisha yangu. “ Lakini kwa nini nipeleke mzigo, si
nitoroke nao tu?” Niliwaza. Wazo la kutoroka
liliondoka haraka akilini kwangu, kwasababu
sikuwa na uhakika kama ule mzigo ulikuwa na kitu
chenye manufaa kwangu. Hivyo ilikuwa lazima
kwanza nizipate dola elfu hamsini nilizoahidiwa na
Bonge ndipo nitoroke. Siwezi kutoroka na mzigo
ambao sijajua una nini ndani yake. Isije kuwa ni
madawa ya kulevya. Itakuwa ni balaa zito maana
sitajua wapi kwa kuuza. Pia sikutamani kabisa
kujihusisha na biashara hiyo ambayo inapigwa vita
dunia nzima.

5

Muda wa siku moja ulinitosha kumtambua Ommy
kuwa ni mtu anayenifaa sana. Nilipofika Lumo
madereva teksi wakaanza kunigombea. Sikuwajali,
nikaanza kutembeza macho yangu huku na kule
hadi nilipomuona, kumbe alikuwa amesimama
karibu na gari lake huku akinyoosha mkono ili
nimuone.
“Ah! Ommy mteja wako huyo sijui mwenzetu una
kizizi maana sisi wengine toka asubuhi lakini
mwenzetu hicho kichwa cha tatu!” Alilalamika
mmoja wa madereva tax. Ommy hakumjibu badala
yake akacheka na kuingia kwenye gari.
“vipi bosi wangu!”
“Shwari Ommy, leo naomba unipeleke Ubungo.”
“Pia nitakuomba ufanye kazi nyingine ya ziada
lakini usijali nitakulipa tu.”
“wewe tena bosi wangu…… usiwe na wasiwasi tuko
pamoja.” Alinijibu huku akitekenya swichi ya gari
lake.
“Enhee.” Akanishtua baada ya kuona bado
sijamueleza hiyo kazi ya ziada niliyomuomba
kuifanya.
“Tukifika Ubungo nitaomba ufuatilie nyendo zangu
bila mtu yeyote kufahamu!” “Hapo sijaelewa bosi!”
“Ni hivi, kuna mtu atakuja kunisubiri ubungo.
Anajua kuwa naingia kutokea Mwanza leo nikiwa
na huu mzigo wake” nilimwonesha lile begi jeusi.
“Kutokana na makubaliano yetu jamaa inabidi
anilipe kiasi fulani cha pesa kwa sababu huu mzigo
nilioubeba ni almasi, hivyo naomba ufuatilie nyendo
zetu ili kama ana nia ya kunidhulumu utoe taarifa
polisi.”
“Hapo nimekupata mkubwa, hii ngoma nzito inabidi
tuicheze kikomando!” Alitamka Ommy na kunifanya
nitabasamu.
“Lakini kwanini usitafute sehemu salama kwa ajili
ya biashara yenu hiyo”
“Hakuna sehemu salama kwenye mambo ya fedha
kwa sasa, hata huyo polisi anaweza kukugeuka
akiona noti.” Alitikisa kichwa kukubaliana na kauli
yangu
Tuliiacha barabara ya Pugu tukaingia Lumumba,
hofu ikaanza kunitawala upya kwani nilijua wazi
kuwa tulikuwa tunaitafuta Ubungo.
“Sikiliza bosi saa hizi ni mapema sana unaonaje
badala ya kusubiri hapa Ubungo tukajivuta hadi
vijiji vya jirani huko utapanda gari ambalo huyo
muheshimiwa atajua kuwa unatoka Mwanza”
“Duh, Ommy una akili sana hiyo plani yako ni
sahihi halafu wewe utanisubiri pale Ubungo”
“sawa!”
***

Kitu kimoja nieleze wazi, maelezo yangu kwa
Ommy yalianza kunitia hofu, Kiasi fulani nilijutia
kitendo changu cha kumsimulia kuhusu almasi
kwani niliogopa asije kunigeuka kwa tamaa ya
pesa. Hii ilitokana na tetesi kuwa kuna baadhi ya
madereva wa teksi hushirikiana na majambazi.
Tulifika safari yetu salama. Hatukwenda mbali
sana, tulikuwa mwanzo tu wa jiji la Dar-es-
salaam. Saa 1.07 gari la Shabib liliingia ndani ya
jijila Dar es salaam. Mapigo ya moyo wangu
yaliongeza kasi yake. Nilisimama kando ya
Barabara nikajaribu kusimamisha lakini Dereva
alionekana kunipuuza na kuongeza mwendo.
Nikahisi kuwa alikuwa na wasiwasi kuwa
anasimamishwa na majambazi. Kosa tulilolifanya
ni gari la Ommy ambalo lilipaki kando ya barabara.
Lakini lilipofika mbele kidogo likasimama.
Nikalikimbilia.
“Samahani muheshimiwa naomba unifikishe hapo
Ubungo Terminal Gari yetu imetuharibikia!”
“Panda haraka basi usitucheleweshe!” alilalamika
konda huku akionekana wazi kukerwa na kitendo
changu.
Tulipofika makao makuu ya Tanesco nikaliona gari
la Ommy likikatisha kwa kasi. Nikashusha pumzi
kwa faraja, kwani mpaka wakati huo mtu wangu
wa karibu alikuwa Ommy. Ingawa sikumueleza siri
ile lakini Ommy alitoa ushirikiano kwa moyo
mmoja.
Mapigo ya moyo wangu yaliongeza kasi yake kama
ndege inayotaka kupaa. Kukutana na Bonge
halikuwa jambo la mchezo. Ni wazi kuwa nilikuwa
nacheza na kifo. Nilipokumbuka ile picha hofu
yangu ikaongezeka. Hapa nataka nikueleze siri
ambayo ilinifanya niamue kuwasaliti na kuvunja
maagizo yao. Ni kweli sikuwa na uhakika kama
kwenye lile begi kuna almasi au kitu kingine
ingawa nilikuwa ingawa hisia zangu kwa asilimia
kubwa nilihisi kuwa zile ni almasi au kitu kingine
chenye thamani kubwa. Kumbuka kuwa picha
yangu walikuwa nayo, hivyo walikuwa wanayaweka
maisha yangu katika himaya yao. Kwani sikujua
baada ya huu mzigo nini kingefuata, Kwa ufupi
niliogopa sana kugeuzwa mtumwa wao. Pamoja na
hayo yote nilianza kuingiwa na wasi wasi wa
kulipwa dola elfu hamsini walizoniahidi. Ilikuwa
haiingii akilini kwa watu ambao wananitishia kifo
waje kunipa kiasi kikubwa cha fedha kama kile.
Ndio maana nilimuomba Ommy afuatilie nyendo
zangu. Kama wasingekuwa na ile picha ya tukio la
kule Tabata ningewatoroka. Lakini ile picha ilikuwa
kama mbu aliyeingia ndani ya chandarua hana kwa
kutokea.
Kuna wakati niliwaza kutoroka ili liwalo na liwe
lakini wazo hilo lilipotea haraka sana. Nilikuwa
kwenye mtafaruku mkubwa na nafsi yangu kwani
nilikuwa nawaza mambo huku nikikubaliana nayo
kwa upande mmoja lakini kwa upande mwingine
nikiyakataa. Mkanganyiko huu mkubwa wa
mawazo uliniumiza kichwa.
Sikutamani kabisa kukutana na Bonge lakini
nilikuwa sina ujanja. Ni mtu ambaye alikuwa
ananitisha sana kila nilipomkumbuka. Zaidi
nilimuogopa Martin kwani kwa upande wangu
alikuwa anatisha kuliko kifo chenyewe. Kuna watu
kule kukutana nao tayari inakuwa ni adhabu.
***

Gari liliingia kituo kikuu cha Mabasi ubungo saa
1.28, Nikateremka kwenye basi lile na kuongoza
kule abiria wengine walikokuwa wanaelekea.
Nilikuwa naangaza macho huku na huko kama
nitaweza kumuona Bonge lakini sikumuona.
Nikatembea kwenye milango ya kutokea. Moyo
ulikuwa unaenda kasi ajabu. Nilikuwa nahisi joto
kali sana, lakini hali ya hewa ilikuwa ya kawaida
kabisa. Tumbo liliunguruma hali niliyoitafsiri kuwa
ilitokana na woga.
Ilikuwa kama niliyegusa waya wa umeme, mshtuko
nilioupata ulikuwa mkubwa sana baada ya
kumuona Bonge akiwa amesimama karibu kabisa
na milango ya kutokea. Akanipokea lile begi jeusi
huku akiwa amekunja uso. Hakuonesha dalili
yoyote ya furaha baada ya kumkabidhi mzigo.
Tukaenda moja kwa moja kule alikoegesha gari
lake. Tukaingia kwenye gari yake Toyota Rav4.
Safari ikaanza huku nikiwa sijui wapi tunaelekea.
Safari yetu ilitawaliwa na ukimya.
Ukimya wake ukaanza kunitia hofu.
Hivi kweli huyu mtu atanilipa fedha zangu katika
hali kama hii? Niliwaza huku nikijaribu kupoteza
mawazo kwa kuangalia hili na lile nje. Vile vile
nilikuwa najiuliza kama kweli ile picha yangu
nitarudishiwa mwenyewe baada ya kuwakabidhi
mzigo wao. Lakini kwa kiasi kikubwa nilikuwa
nawazia zawadi mbaya kabisa ambayo hawa
jamaa wangenipa, sidhani kama kuna kitu
ningezawadiwa zaidi ya kifo. Kitu kimoja kilinifariji,
nitakapokufa sote tutakuwa tumekosa. Wataukosa
mzigo nitaukosa uhai lakini safari ni moja mimi
nitatangulia wao watafuata nyuma. Tumeumbwa
kwa mavumbi tutarudi mavumbini.
Tulfika maeneo ya Mtoni mtongani huku bado
sijaelewa hatima ya safari yetu kwani mpaka
kufikia hapo nilikuwa sijaongea lolote na Bonge.
Alikuwa amekunja uso kama mtu aliyelazimishwa
kula ndimu. Bado safari ilikuwa inaendelea.
Tulipofika maeneo ya Rangi tatu tukanyoosha
kufuata barabara iliyokuwa inaelekea Kongowe.
Hapo hofu yangu ikaongezeka maana tulikuwa
tunaanza kuelekea nje ya jiji. Bado niliendelea
kujuta. Hivi kwanini sikumueleza baba yangu juu
ya mkasa huu? Hilo ndilo swali lililoanza kukitesa
kichwa changu. Kitu kimoja kilinifanya nishindwe
kumwambia baba, angeshangaa sana kusikia
mkasa wenyewe ulikoanzia, pia angenigombeza
kama ningemwambia jinsi nilivyomfuatilia yule
mwanamke kule ‘guest’, “Ah! Bora niicheze
mwenyewe hii ngoma nione mwisho wake”
niliwaza.
Tukafika maeneo ya mpakani. Hapo kulikuwa na
kibao ambacho kiliandikwa Karibu wilaya ya
Mkuranga nikajua kuwa sasa tumeingia mkoa wa
pwani. Hapa hatukwenda mbali tukakata kushoto
na kuiacha kulia shule ya sekondari ya St.
Matthews. Tukafuata kichochoro ambacho
kilitufikisha eneo ambalo nyumba zake nyingi
zilikuwa mpya huku nyingine zikiwa bado
Hazijamalizika ujenzi wake. Gari likasimama mbele
ya nyumba moja kubwa. Kitu kimoja
kilinishangaza, nyumba hii ilifanana sana na ile
niliyoiona Mwanza. Nilikuwa najiuliza kama
zilikuwa zinamilikiwa na mtu mmoja au vinginevyo.
Mawazo yangu yakakatishwa na Msukumo wa
Lango lile. Lango lilifunguliwa kwa kusukuma
upande wa kulia, Lilikuwa limewekewa
magurudumu maalum ya chuma. Gari likaingia
ndani na kusimama kwenye sehemu maalum ya
kuegesha magari. Hapa naomba uelewe kuwa ni
katika sehemu ambayo nilikuwa nakaribia kupoteza
fahamu kwa hofu niliyokuwa nayo. Jasho lilinitoka
pia nilihisi joto kali sana. Tumbo liliunguruma na
kufanya mvurugiko usiokuwa wa kawaida. Huu
mzigo ulinitia mashaka sana. Mzigo feki! Itakuwaje
akifungua mbele yangu. Nilishaonywa kutopitia
sehemu yoyote kabla ya kukabidhi mzigo,
nilishaonywa kutofungua mzigo. Ajabu! Nilikuwa
nimefanya zaidi ya vile nilivyo onywa. Mzigo
nimebadilisha na malipo nayataka. Kweli nilikuwa
kwenye mdomo wa mauti.
“ Karibu mkuu!” Sauti ya mmoja wa vijana
aliyetokea ndani ya jengo lile ilisikika. Akatikisa
kichwa bila kuongea lolote. Nami nikamfuata
Bonge bila kusita. Swali moja nilikuwa najiuliza nini
kitatokea iwapo atafungua mzigo mbele yangu.
Bila shaka kwa mshtuko atakao upata ataniua
papo hapo. Hapa lazima nijipongeze kwani
nilijitahidi kuficha hofu niliyokuwa nayo mbele ya
Bonge. Nilijifanya niko kawaida lakini ukweli ni
kwamba nafsi ya mtu ni kichaka kwani haja ndogo
zilikuwa zinakaribia kuniadhiri kwa hofu niliyokuwa
nayo. Nikarudisha mawazo yangu kwa Betty.
“Sawa sasa kwanini usiwape huo mzigo
wao?”sauti yake ilijirudia kichwani kwangu wakati
ule ananionya kuhusu mzigo. Nilikuwa kwenye
mkanganyiko mkubwa sana.
Nilikaribishwa katika sebule kubwa ambayo ilikuwa
na samani ambazo bila shaka hazikununuliwa kwa
fedha za kitanzania. Ilikuwa ni sebule iliyotimia,
samani za gharama ziliipamba sebule hii na
kuifanya mandhari yake isitofautiane sana na ikulu.
Kutokana na hofu niliyokuwa nayo nilishindwa
kuisanifu vema sebule ile. Kila nilichokuwa
naangalia sikuweza kukimaliza kwani kilikatishwa
na mkanganyiko wa mawazo niliokuwa nao. Dakika
tano nilizokaa pale niliziona kama saa kumi.
Kulikuwa na kiyoyozi kina fanya kazi lakini
kilishindwa kabisa kupoza joto la mwili wangu
ambalo lilipanda kweli kweli.
Baada ya dakika chache nikamuona Bonge akiingia
na begi jeusi sebuleni. Hapo nashindwa hata
kuelezea hofu niliyokuwa nayo kwani nilijua saa
yoyote atafungua mzigo. Sikuweza kukadiria
ukubwa wa balaa litakalojitokeza hapo. Akaanza
kufungua zipu za lile begi. Muda huo nilikuwa
natamani sana ardhi inimeze.
Mungu mkubwa! Kumbe halikuwa lile begi
nililokuja nalo. Ndani ya begi hili kulikuwa na vitu
tofauti kabisa. Kulikuwa na ‘Briefcase’ mbili ndogo
moja nyekundu nyingine nyeusi, akachukua
‘Briefcase’ nyeusi akanikabidhi. Kama alivyoupokea
mzigo wangu nami nikapokea mzigo wake bila
kuufungua. Akaingiza mkono mfukoni na kutoa
simu na kuanza kuongea.
“Hallow, mzigo umewasili salama lakini bado
magugu hayajang’olewa!” Baada ya mtu wa
upande wa pili kuongea Bonge akajibu.
“Magugu tumeyawekea sumu nafikiri yataisha
baada ya muda si mrefu, tutalima vizuri shamba
letu.” Akacheka na kukata simu.
Namshukuru Mungu hapa ndipo nilipouona
umuhimu wa kusoma masomo ya fasihi nikiwa
shuleni. Mimi ndio nilikuwa magugu yenyewe na ni
wazi kuwa lengo lao lilikuwa ni kuniua. Kutokana
na hali yangu duni Bonge hakuweza kubaini kuwa
nilikuwa tajiri wa kupambanua mambo. Nilielewa
wazi kuwa lengo lao lilikuwa ni kuniua. Angeniua
vipi? Nikahisi kuwa sumu anayoisema pengine
kaniwekea watu waje kunivamia. Nikatoka nikiwa
na Lile ‘briefcase’ mkononi. Hofu ilikuwa
imeshanitoka kwani sasa nilijua wazi kuwa
napambana na kifo hivyo sikutakiwa kuwa mwoga
tena. Bonge hakuwa na ujanja wa kuongea
mafumbo mbele yangu. Nilikuwa na kazi moja tu!
Nilitakiwa kuwa makini na safari yangu kwani kifo
kilikuwa kinanifuata. Hofu yangu ilipungua kidogo
nilipomkumbuka Ommy. Nilijua atakuwa
ananisubiri huko nje kwani Bonge hajui kama nina
usafiri huko.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI

Nikatoka nikiwa na Lile ‘briefcase’ mkononi. Hofu
ilikuwa imeshanitoka kwani sasa nilijua wazi kuwa
napambana na kifo hivyo sikutakiwa kuwa mwoga
tena. Bonge hakuwa na ujanja wa kuongea
mafumbo mbele yangu. Nilikuwa na kazi moja tu!
Nilitakiwa kuwa makini na safari yangu kwani kifo
kilikuwa kinanifuata. Hofu yangu ilipungua kidogo
nilipomkumbuka Ommy. Nilijua atakuwa
ananisubiri huko nje kwani Bonge hajui kama nina
usafiri huko.
Nikatembea taratibu kuelekea barabarani.
Nilipotokea barabarani nikakuta kuna foleni. Magari
yalikuwa yanaenda taratibu. Sikumuona Ommy. Hili
nalo likanitisha kidogo. Nikaanza kutembea kwa
miguu kuelekea kituo cha daladala cha Kongowe.
Moyo wangu ulikuwa tayari kwa lolote. Nikatembea
kwa umakini wa hali ya juu nikijaribu kuangalia
balaa litatokea upande upi. Kwa mbali nililiona gari
la Ommy likinifuata taratibu. Umakini huu wa
Ommy ulinifurahisha sana. Dakika chache baadae
nikaiona foleni ikiyeyuka nafikiri, nikagundua kuwa
kunagari lilikuwa limezimika katikati ya barabara
na sasa lilikuwa limewaka.
Ghafla, gari ndogo iliipita kwa kasi gari ya Ommy.
Ikafunga Breki za ghafla mbele yangu. Watu wawili
ambao wote walikuwa na Bastola wakanifuata kwa
kasi huku wakiwa wameninyooshea bastola.
“Lete hilo ‘Briefcase’” Alisema mmoja wa wale
watu kwa sauti yenye amri, mbele ya bastola,
mbele ya watu wasio na mzaha sikufanya ubishi
nikawapa walichotaka. “Wametumwa?” Hilo
lilikuwa swali la kwanza lililopita kichwani kwangu.
Ommy akaongeza kasi ya baada ya kuliona tukio
lile. Giza lilikuwa limeshaingia lakini aliweza kuona
vizuri kila kilichokuwa kinaendelea kutokana na
mwanga ulioletwa na taa za magari mbalimbali.
Akafunga breki mbele yangu na kunifungulia
mlango kwa haraka nami nikajitoma ndani.
“Mwanangu tusikubali hawawezi kutunyang’anya
fedha kikondoo namna hii!” Alifoka Ommy huku
akishindwa kudhibiti hasira zake. Aliliondoa gari
kwa kasi, akaanza kulitafuta lile Nissan patrol .
Nilikuwa nimechukia vibaya sana. Dakika chache
nilikuwa naota utajiri dakika chache ndoto
ikafutika. Nilikuwa na hasira sana. Bahati ilikuwa
upande wetu, wale jamaa hawakuweza kugundua
kuwa walikuwa wanafuatwa.
Walipofika maeneo ya Mtongani wakaingia bara
bara iliyokuwa inaelekea Kijichi kupitia kwa Buruda.
Tukaendelea kuwafuata kimyakimya. Wakasimama
maeneo ya Mbagala kuu karibu na kituo maarufu
kwa fundi redio. Bila shaka hapa walikuwa
wanataka kuangalia kilichokuwemo kwenye
‘briefcase’.
“Tulia Kajuna wana bastola hao watakuua”.
Aliniambia Ommy huku akinizuia kwa mkono wake
nisiteremke kwenye Gari, alionekana kurudiwa na
umakini wake kwa kutambua hatari iliyoko mbele
yetu. Tulikuwa tumesimamisha gari letu kama
hatua Thelathini kutoka pale waliposimama.
Ingawa nilikuwa mbali kwa kutumia taa yao ya
ndani niliweza kuwaona vizuri wale jamaa
wakihangaika kufungua lile ‘briefcase’ mmoja
alionekana wazi akicheka kwa furaha. Roho
iliniuma sana. Nikaanza kuhisi kuwa huenda ni
njama za Bonge kutaka kunidhulumu. Nikazidi
kumchukia!
Ghafla! nikashuhudia tukio ambalo sikulitarajia.
Lilikuwa ni tukio la kutisha na kushangaza mno
kwani halikuwa jambo nililolitarajia. Moyo ulienda
kasi lakini nilijikaza kiume na kuendelea kukazia
macho eneo la tukio. Watu walikimbia hovyo na
kujikuta wakigongana kila mmoja akijaribu kuokoa
maisha yake.
“Kudadekii….Walikutegeshea bomu mshikaji sio
mapene wala nini!” Alitamka Ommy kwa kihoro.
Ulikuwa ni mlipuko mkubwa ambao bila shaka
ulikuja baada ya wale jamaa kufungua ‘Briefcase’.
Nililishuhudia lile gari likirushwa juu na
kutawanywa vipande vipande, pia niliweza kuona
kichwa cha mtu kikiwa kimerushwa juu na kutua
chini. Duh, kifo kibaya kama hiki nilikiona kwenye
filamu za hollywood tu na niliamini kuwa ni jambo
ambalo haliwezi kutokea. Vioo vilitawanyika ardhini
huku vingine vikiwa na athari ya damu na kuleta
taswira ya kutisha. Mkono na vidole ni miongoni
mwa vitu nilivyoviona vikiwa vimejitenga na mwili
na kuangukia senti meta chache kutoka pale lilipo
gari.
Baada ya hapo ukafuata moto ambao ulikuwa
unawaka kuteketeza kabisa masalia ya gari
lile.Hapo ndipo nilipoelewa maana ya fumbo la
Bonge kuwa angeng’oa magugu baada ya muda
mfupi kwani alikuwa ameyawekea sumu yale
magugu.Likanitoka tusi zito la nguoni bila
kutarajia.
“Unafikiri huu ndio mwisho?” Aliniuliza Ommy
“Hapana Ommy huu ndio mwanzo!”
“Mwanzo wa nini sasa!” Aliuliza Ommy kwa
mshangao.
“Mwanzo wa vita!”
“Na nani?” Sikumjibu baada ya kuona maswali
yake yanakuja mfululizo. Kwa upande mwingine
nilijipongeza kuwapa mzigo tofauti na ule
walioutarajia. Sasa ngoma droo kama walivyoimba
waswahili wa bongo! Niliwaza huku nikikuna
kichwa. Kumbe ndio maana akili ilikuwa inakataa
kabisa kuuacha ule mzigo bila kufungua!
Nilistaajabia mwenyewe maamuzi yangu ingawa
upande mwingine nilianza kujilaumu kwani kama si
msaada wa wale vibaka sijui majambazi hata mimi
nisingefikiria zaidi ya kuufungua ule mzigo bila
tahadhari. Lakini hata hivyo ni tahadhari gani
ningeichukua hali ya kuwa sina ujuzi wowote wa
mambo ya milipuko. Ningekufa tu tena kama
----- Fulani vile.
“Twenzetu mshikaji kimeo hicho, tusipoangalia
tutaisaidia polisi muda mfupi ujao” Akanishtua
Ommy baada yakuona watu wakianza kurudi na
kulizunguka eneo la tukio kama ilivyo kawaida yao.
Tukageuza gari kurudi tulikotoka. Nikageuka
nakuutazama moto ulivyokuwa unaivisha viungo
vya majambazi wale!
“Mtego wa panya, ameingia asiyekuwemo!”
Nilisema huku nikimshuhudia Ommy akiongeza
kasi ya gari.
“Afadhali wale wajinga wameramba garasa katika
mchezo usiowahusu!” Aliendelea kuropoka Ommy.
Toka nimfahamu hakuna siku niliyomuona Ommy
kuwa na maneno mengi tena mengine ya kihuni
kama hii. Kiasi fulani nilimuona akiwa kasahau
kabisa huzuni ambayo ilikuwa kwenye sura yake
toka siku ya kwanza niliyokutana naye. Alionekana
kuvutiwa na kuchangamshwa na mlipuko ule kana
kwamba ni burudani fulani ingawa alificha udadisi
mkubwa kwenye nafsi yake. Nilijua lazima
ataniuliza tu!
Tulipofika Maeneo ya kituo cha Buruda
tukapishana na gari tatu za polisi ambazo bila
shaka zilikuwa zinaelekea eneo la tukio. Hatua
chache mbele yetu kulikuwa na gari kubwa la jeshi
nalo lilikuwa linaelekea eneo la tukio. Eneo hili la
tukio ndio lilelile ambalo lilitokea milipuko ya
mabomu ambayo yalitikisa jiji la Dar es salaam.
Hivyo wanajeshi walikuwa wanaelekea eneo la
tukio kwa kuhisi kuwa huenda ni yale mabomu
yao. Mlipuko haukuwa mkubwa sana kiasi cha
kuleta askari wengi namna ile, tatizo labda ni
maelezo ya watu waliotoa taarifa. Kuna
uwezekano mkubwa wa kutoa maelezo kuwa yale
mabomu yameanza kulipuka tena. Taarifa kama
hiyo isingeweza kupuuziwa na vyombo vya
usalama kwani ni kama mtu aliyeng’atwa na nyoka
angeshtushwa hata na uzi mwembamba wa
kushonea nguo.
***

Tulifika Lumo sasa 6.15. Nikashusha pumzi baada
ya kubaini kuwa niko eneo ambalo kwa kiasi fulani
ni salama kwangu.
“Hivi kwanini hawa jamaa wakufanyie hivi?”
Aliuliza Ommy huku akipunguza mwendo wa gari.
Nikamtazama Ommy kabla ya kumjibu. Mpaka
kufikia hapo Ommy alikuwa ni msaada mkubwa
kwangu.
“Sikiliza Ommy, Ukweli nimekuwa nikikuongopea
juu ya tukio zima.” Nikaanza kumuelezea tukio lote
bila kumficha.
Jambo la kustaajabisha ni kuwa baada ya simulizi
yangu hiyo nilimuona Ommy akitokwa na machozi.
Nikashangaa sana kwani sikujua nini kilikuwa
kimemgusa katika tukio hilo ingawa kimsingi
lilikuwa ni tukio la kusikitisha.
“Vipi Ommy nini kinakuliza?” Nilimuuliza kwa
huruma.
“Umenikumbusha majonzi Kajuna, huyo mwanamke
aliyeuwawa gesti alikuwa mpenzi wangu.
Tulipendana mapenzi ya dhati kabisa sasa sijui
nini kilimpeleka huko gesti, nahisi alikuwa
ananisaliti ndo wahuni wakamuua hukohuko.”
“La!……Hapana Ommy, tatizo lilisababishwa na
ujumbe ambao aliutuma kwenye simu, nahisi
haukukufikia!”
“Simu ipi?” aliuliza Ommy huku akionesha
kutoelewa nini nilichokusudia..
“Ommy nafikiri haya mambo tunatakiwa kuongea
usiku huu huu kwani niko kwenye wakati mgumu
sina uhakika kama siku ya kesho nitaimaliza
nikiwa hai” Nilimtazama Ommy ambaye niliona
mshtuko na umakini kwenye uso wake baada ya
kumdokeza mambo yale ya kutisha. Alikuwa na
majonzi mara mbili, kwanza alihisi kusalitiwa na
mpenzi wake pili kifo cha mpenzi wake. Nilielewa
wazi kuwa Ommy alikuwa hanielewi hivyo
nilimuomba twende nyumbani kwangu nikampe kitu
ambacho kingemfanya anielewe.
Tukaanza safari ya kutoka Lumo hadi Buza.
tulipofika nikaingia ndani, nikachukua simu ya
marehemu Merina. Kisha nikampa Ommy akawa
anasoma meseji akaanza kutokwa machozi zaidi.
Ghafla kama aliyezinduka kutoka usingizini
akanishika bega.
“Kajuna, hapa kwako si sehemu salama tena,
Chukua kila kilicho chako tuondoke. Hawa watu
wakigundua kuwa mzigo uliowapa ni feki lazima
watarudi kuja kuutafuta huku kwako” Ndipo
nikabaini uwezo mkubwa wa kufikiri aliokuwa nao
Ommyn kwani sikufikiria kitu kama hicho kabla
kwa namna Fulani nikajikuta nikizidi kuwa na imani
na Ommy katika wakati ule mgumu. Nikarudi ndani
haraka sana nikachukua begi langu maana ndilo
nililoliona muhimu kwa wakati huo. Nikakimbia
kuelekea kule aliko Ommy. “Sikiliza Ommy, litoe
gari maeneo haya kisha ‘upaki’ sehemu ambayo ni
salama halafu tujaribu kuangalia kama kuna yeyote
atakayekuja” nilimshauri naye hakupinga
akakubaliana nami.
Tukalificha gari umbali wa kilomita moja kutoka
nyumbani kwangu kisha tukarudi nyuma
kushuhudia kama kuna lolote litakaloendelea.
Mpaka saa 10.12 alfajiri hakuna lililotokea
tukaamua kuondoka kwenye maficho yetu na
kuliendea gari kule tulikoegesha.
Tukaondoka kuelekea nyumbani kwa Ommy.
Wakati tunaenda ndipo Ommy akaanza kunisimulia
kisa cha mpenzi wake. Haikuwa hadithi ndefu
ilikuwa ni hadithi fupi ya kushangaza,
kustaajabisha na kusikitisha.
“Merina alikuwa ni Katibu muhtasi katika Kampuni
ya kusindika ngozi, Kulikuwa na mfanyakazi
mwenzie wa kike ambaye alikuwa anaitwa
Pili.Huyu Pili alikuwa ni rafiki mkubwa wa Merina.
Siku moja Pili alikuja na habari za kutisha kwa
Merina. Alimsimulia kuwa kuna Watu
wanajishugulisha na biashara ya ngozi za
binadamu pale kiwandani. Alipotaka kumsimulia
akatokea mmoja wa wahusika ‘story’ ikakatishwa.
Baada ya hapo Mpenzi wangu akawa anafuatwa na
watu mbalimbali akiwemo huyo Bonge ambaye
aliniambia hakuwa mfanyakazi kiwandani hapo.
Walimwahidi pesa nyingi kwa kazi ya kumuua Pili.
Alipewa vidonge ambavyo vilikuwa ni sumu kali
sana lakini alikataa katakata. Huyo Bonge ndiye
aliyekuwa anamfuatilia zaidi. Zikapita siku tatu
sijamuona wala kupata mawasiliano yake, Siku ya
nne nikapata taarifa za kuuwawa kwa Merina.”
Alikuwa amemaliza hadithi yake.
“Huyo Pili yuko wapi sasa!” “Pili alikufa Siku moja
kabla ya kifo cha Merina, Inasemekana alikufa
ghafla bila hata kuugua”
“Ooh my God, walimuua bila shaka!”
“Na ndio maana mpenzi wangu aliamua kuukimbia
mji lakini bahati haikuwa yake!” Alipofika hapo
nikamuona akianza kutoa tena machozi.
“Hicho kiwanda cha ngozi kinaitwaje?”
“Kinaitwa NAI COMPANY l.t.d yaani NEW ASIAN
INVESTORS” Nilitikisa kichwa kuonesha
kukifahamu kiwanda hicho lakini nilikuwa sifahamu
walikuwa wakijishughulisha na usindikaji wa ngozi.
“Unaonaje tukienda kutoa taarifa Polisi?” Aliniuliza.
“We! Usithubutu kwa sasa. Kumbuka kuwa wale
watu wana picha yangu nafikiri ni bora tuwafuatilie
kimya kimya kwa sababu kwa akili zao nitakuwa
nimekufa kwa lile bomu au nimetoroka” Ommy
akaonekana kukubaliana nami.
Ommy Alikuwa anaishi maeneo ya Makangarawe
karibu na kituo kidogo cha Polisi. Alikuwa
amejenga nyumba ndogo ya vyumba vitatu. Ni
eneo ambalo kiasi fulani lilikuwa tulivu kuliko kule
kwetu. Alikuwa anaishi peke yake. Akanionesha
sehemu ya kulala. Baada ya kuoga nikaingia
chumbani.
Ajabu sikupata usingizi, nilikuwa najiuliza maswali
mengi ambayo hayakuwa na majibu. Kwanini kazi
ya kumuua atumwe Merina wakati wenyewe
waliiweza. “Huenda walitaka likishatokea watafute
namna ya kumuweka kwenye himaya yao kama
walivyonifanyia mimi kule Tabata”.
Hayo yalikuwa ni mawazo yangu, kimsingi nilikuwa
sina jibu sahihi. Hata hivyo niligundua kitu, hawa
jamaa wakikuahidi zawadi basi kinachofuata ni kifo
na si vinginevyo. Ndiyo lazima kifo kinaniwinda
sasa na Mzigo wao tu ndio utakaochelewesha kifo
change.
Nilikuwa najiuliza kwa nini hawa watu waliamua
kutumia ubabe kunituma mzigo wao. Kama ule
mzigo ulikuwa na thamani kubwa kwanini
wasiuchukue wenyewe? Au walishajua kuwa sina
ujanja kwa kuwa wana picha yangu ambayo
inaonesha kuwa mimi ndiye muuaji wa Merina?
Bado nilikuwa sina jibu la maswali yote hayo.
Likaja swali ambalo lilikuwa gumu kuliko yote. Hivi
hawa watu ni kina nani na wanataka nini? Ni
magaidi? Swali hilo lilinikosesha raha, shauku ya
kuufungua ule mzigo ikaongezeka. Kama ule mzigo
hauna thamani kwanini Bonge alinipa milioni moja
ambayo haikuwa sehemu ya malipo yangu na
kwanini wametumia gharama kubwa kunitegea
bomu baada ya kuwafikishia mzigo wao. Bado
swali lilikuwa pale pale ule mzigo ni mzigo gani?
Mawazo yangu yakahamia kwa Betty. “Kama
nitamaliza salama matatizo haya lazima nifunge
ndoa na Betty. Yeye ndiye liwazo na ua langu la
moyo”niliwaza. Ukweli ni kwamba muda huo
nilikuwa nahitaji sana faraja kutoka kwa Betty.
Wakati nikiendelea kuwaza taratibu usingizi
ukanichukua. Haukuwa usingizi nzuri, ndoto za
milipuko ya mabomu na mauaji makubwa zilikuwa
zimetawala.
Mara kadhaa niliota nikifukuzwa na watu wenye
silaha huku wakinikosakosa risasi kdhaaa. Pia
kuna wakati nilijikuta nikiwa katika mikono ya
polisi tayari kujibu maswali kwa kosa la mauaji.
***

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Mawazo yangu yakahamia kwa Betty. “Kama
nitamaliza salama matatizo haya lazima nifunge
ndoa na Betty. Yeye ndiye liwazo na ua langu la
moyo”niliwaza. Ukweli ni kwamba muda huo
nilikuwa nahitaji sana faraja kutoka kwa Betty.
Wakati nikiendelea kuwaza taratibu usingizi
ukanichukua. Haukuwa usingizi nzuri, ndoto za
milipuko ya mabomu na mauaji makubwa zilikuwa
zimetawala.
Mara kadhaa niliota nikifukuzwa na watu wenye
silaha huku wakinikosakosa risasi kdhaaa. Pia
kuna wakati nilijikuta nikiwa katika mikono ya
polisi tayari kujibu maswali kwa kosa la mauaji.
*******

Niliamka saa 4.15. Nilikuwa na uchovu mwingi,
nikaenda sebuleni nikamkuta Ommy akiwa amekaa
kwenye kiti. Alionekana mwenye mawazo mengi
sana. Hali hiyo ilimfanya asitambue ujio wangu
pale sebuleni. Ukutani alikuwa amepachika picha
yake kubwa akiwa amekumbatiana na Merina.
Merina alikuwa amerudi mavumbini kule tulikotoka,
njia ambayo kila mmoja ataiendea.
“Unafikiri ni muda muafaka sasa kwenda kufungua
mzigo?” Nilimshtua kutoka kwenye lindi la
mawazo. Aliinua macho yake na kunitazama,
Macho yake yalikuwa yanalengwa lengwa na
machozi.
“Kajuna…..” aliniita kisha akatulia kidogo kabla ya
kuendelea.
“….. Inabidi nifanye kila niwezalo kumlipia kisasi
mpenzi wangu!” Alitamka Ommy kwa uchungu.
“Sawa lakini mpaka uwafahamu waliohusika vipi
kuhusu mzigo, tuufungue?”. “Tusiwe na haraka na
huo mzigo, kwanza tuangalie usalama wako lazima
ujue kuwa maisha yako yapo hatarini.” Niliukubali
ushauri wake nikawa nafikiria nini cha kufanya.
“Hivi huyo Pili alikuwa na mume?” Nilianza
kumsaili.
“Pili yupi?”
“Yule uliyenieleza kuwa alikuwa rafiki wa Mpenzi
wako!”
“Hapana.”Alijibu kwa mkato.
“Alikuwa anaishi wapi?”
“Ilala Shariff shamba alikuwa anakaa na mdogo
wake wa kike ambaye anaitwa Debora”
“wewe unaifahamu nyumba aliyokuwa anaishi?”
“Hata majirani zake wananifahamu!”
“Mimi nafikiri tuanzie huko nyumbani kwa Pili”
Nilimweleza akanitazama kwa mshangao.
“Huko tutaenda kufanya nini!?” Aliniuza Ommy kwa
mshangao.
“ Lazima tuanze kumtafuta adui yetu kuanzia
huko!” Ommy akanitazama kwa mshangao wa
wazi kisha akakubaliana nami kwa shingo upande.
“ Kuna ‘stationery’ hapa jirani” Nilimuuliza.
“Ndiyo!”
“Nahitaji passport size yako!” Jamaa alikuwa
ananishangaa kwelikweli. Nikafungua kwenye begi
langu nikatoa picha yangu ya mkato ‘Passport
size’ Nikachukua na ile ya Ommy nikaenda nazo
Kule ‘stationey’. Ommy alikuwa ameshaelewa
nilichokuwa nafanya.
“Sasa nipeleke kwa mchonga mihuri!” Ommy
alikuwa hoi jinsi akili yagu ilivyokuwa inafanya kazi
haraka.
“Lakini kitambulisho cha usalama wa Taifa kina
maandishi ya chuma kwenye gamba lake wewe
utapata wapi hilo gamba!”
“Mtu professional kama wewe unaweza kufahamu
hilo lakini kule ninakokusudia najua hawafahamu
lolote lile!”
Akacheka bila kuongeza neno lolote zaidi ya
kutikisa kichwa.
******

Saa 10.30 tulikuwa maeneo ya Ilala Sharif
shamba. Ommy alinielekeza nyumba aliyokuwa
anaishi Pili. Nikavuka bara bara na kuifuata
nyumba ile ambayo ilikuwa ndani kidogo. Ilikuwa ni
nyumba yenye rangi ya bluu ambayo ilipauka sana.
Ni wazi kuwa nyumba hii ilijengwa wakati
Tanzania haijapata uhuru au miaka ya mwanzo ya
uhuru. Ilikuwa imezungushiwa uzio wa bati
ambazo zilibadilika rangi na kuwa rangi isiyo rasmi
ambayo ilifanana na udongo kutokana na kutu.
Nikauendea mlango ambao ulitengenezwa kwa bati
la debe la mafuta ya KORIE. Baada ya Kubisha
hodi mara tatu mama mtu mzima akaja
kunifungulia. Alikuwa ni mama ambaye umri
ulianza kumpungia mkono.
“Bibi shikamoo”nilimsalimia kwa heshima za
kibantu.
“Marahaba mwanangu hujambo!”
“Sijambo bibi, samahani hapa ndio nyumbani kwa
marehemu Pili” Nilimuuliza.
“Ndio hapa mwanangu tena mdogo wake amefika
sasa hivi alikuwa huko kazini kwake, chumba
chake hicho hapo!”. Alinijibu yule mama huku
akinionesha kwa kidole chake cha shahada kile
chumba, moja kwa moja nikaelekea Kule
alikonielekeza. Kilikuwa chumba cha nje. Nikabisha
hodi. Mlango ukafunguliwa, msichana mwenye sura
ya kuvutia akafungua mlango. Akasimama
mlangoni akitaka lililonileta nimweleze palepale
bila kuingia ndani. Alikuwa amesimama mlangoni
huku akiwa amefungua nusu ule mlango mkono wa
kulia alikuwa ammeshika kitabu maarufu cha
riwaya kinachoitwa MJELEDI. Niligeuka na
kumtazama yule bibi alikuwa ameingia ndani. Yule
msichana alionekana kunitazama kwa hasira kitu
ambacho kilinishangaza kidogo.
“Habari yako!”
“Nzuri nikusaidie nini?” aliniuliza kwa jazba.
“Nina maongezi na wewe kama inawezekana
tafadhali naomba unikaribishe ndani!”
“Sikiliza wewe, mimi kuuza baa haina maana kuwa
nauza mwili. Please naomba mambo yote yaishie
kulekule baa hapa ni nyumbani nahitaji kupumzika
nahitaji kuheshimiwa. Narudia tena mimi nauza
baa siuzi mwili.”
“Umemaliza?” nilimuuliza kwa sauti yenye utulivu
mkubwa.
“Ondoka, nasema ondoka unanipotezea muda wa
kusoma kitabu changu!”
Sikusema neno lolote nikafanya kitu ambacho
hakukitarajia. Nikamsukumia ndani kwa ghafla!
Akayumba na kuangukia kwenye zulia ambalo
lilikuwa mle ndani. Nikafunga mlango kwa haraka
sana. Akataka kupiga kelele kwani nahisi alidhani
kuwa lengo langu ni kumbaka. Kwa haraka sana
nikatoa kitambulisho changu cha kugushi ‘feki’
nikamrushia pale alipolala. Nilikuwa mtulivu huku
nikionesha kujiamini sana. Kitambulisho kile
kilionesha kuwa ni Afisa mwandamizi wa idara ya
Usalama wa Taifa.Nikamuona akinitazama kwa
macho yaliyojaa mshangao.
“Uko tayari kutoa ushirikiano kwangu?” nilimuuliza
kwa sauti ya upole. Akaitikia kwa kichwa huku
akiona aibu kwa mambo aliyonifanyia. Nilijipongeza
moyoni kwa kutengeneza kitambulisho hiki.
Nilikuwa nimetengeneza vitambulisho viwili kimoja
kilikuwa cha Ommy. Nilifanya hivyo baada ya
kugushi mihuri ya ofisi ya Rais.
“Naomba tuanze na jina lako!”
“Naitwa Deborah Boimanda” alinijibu huku
akitetemeke.
“Marehemu pili alikuwa nani kwako?” Nilimuuliza
kwa sauti iliyojaa utulivu mkubwa.
“Alikuwa dada yangu wa mama mmoja”
“Mlikuwa mnalala wote chumba kimoja!”
“Ndio tena chumba chenyewe ndio hiki!”
“Marehemu alikuwa na mume au mpenzi?”
“Hapana…ah, alikuwa naye lakini ni hizi siku za
mwisho za uhai wake”
“Unaweza kujua nini kilimuua Dada yako!”
“Hapana ninachokumbuka alikuwa analalamika
kizunguzungu akaanza kutoa povu mdomoni
hatimaye akafa nikiwa nimempakata.” Akaanza
kutokwa na machozi. Nikamuacha mpaka
nilipomuona akiwa amerejewa na utulivu.
“Hiyo hali ya kizunguzungu ilimuanzia hapa
nyumbani?”
“Hapana ilianza muda mfupi baada ya kurudi
kutoka kwa mpenzi wake”
“Unamfahamu vizuri huyo mpenzi wake?”
“Ndiyo anaitwa Masudi alikuwa anafanyakazi
kampuni moja na dada!”
“Kwa nini unasema alikuwa anafanya kazi ina
maana ameacha?”
“Hapana na yeye ni marehemu kwa sasa!”
Nilishtuka lakini sikutaka Debora agundue.
“Alikuwa mgonjwa?”
“Hapana, nasikia alijiua baada ya kifo cha dada.”
Nikashusha pumzi na bila kutegemea nikajikuta
nakaa pale kitandani. Siku nyingi nilikuwa
natamani kusoma kitabu kile cha MJELEDI kwani
kilikuwa gumzo mitaani na watu walikuwa
wanakitafuta kila kona bila mafanikio kutokana na
nakala zilizotolewa kuisha mapema. Ni kitabu cha
kusisimua ambacho kiliteka hisia za wapenzi
mbalimbali wa riwaya Afrika mashariki. Hata hivyo
kutokana na mawazo na mkanganyiko wa mambo
niliokuwa nao sikutamani hata kidogo kusoma
kitabu hicho kwa wakati huo ingawa niliweka azma
ya kuja kuazima kitabu hicho pale mambo
yatakapoisha salama.
“Ahsante kwa maelezo yako, tafadhali naomba
usimueleze yeyote kuwa umekutana na mtu kama
mimi” akaitikia kwa kichwa. Nikakiacha kile kitabu
kitandani kisha nikaondoka mle ndani.
********

Nilirudi kwa Ommy nikamkuta akiwa ameshikilia
usukani. Akawasha gari tukaondoka.
“Enhe lete story” alianza Ommy tukiwa
tumeshaingia barabara ya kawawa.
“Duh, hii ishu nzito rafiki yangu inaonekana
mzunguko wake ni mrefu”
“Kwanini?”
“Nahisi Pili kauwawa na mtu ambaye alijifanya
mpenzi wake, tena na yeye alikuwa anafanya kazi
kiwanda kilekile cha ngozi!”
“Sasa Ugumu uko wapi hapo?”
“Huyu mpenzi wake yuko nyuma ya wauaji!”
“Una maana gani?”
“Nilichogundua ni kuwa wauaji hawapendi kufanya
kazi yao wenyewe wanapenda kupitia kwa watu
fulani kwa hiyo hata huyo aliyejifanya mpenzi wake
hana analoelewa zaidi ya kurubuniwa pesa kwa
kazi hiyo tena cha kushangaza hata yeye
kauwawa.”
“Unafikiri ni kwanini wamemuua?”
“Wanataka kuwachanganya Polisi na yeyote
atakayejaribu kuchunguza mauaji hayo.”
“Kivipi?”
“Pale yeyote atakapogundua kuwa fulani ni muuaji
bado atakutana na changamoto ya muuaji
kauwawa kwa hiyo hatajua kwanini muuaji kaua!”
Kisha nikamsimulia mahojiano yangu na Debora.
“Niambie ukweli Kajuna hivi hujawahi kuwa askari
wewe!?” Aliniuliza kwa mshangao.
“Siwezi kukuficha rafiki yangu!”
“kama ni hivyo una akili ya ajabu maana mbinu
zote ulizotumia ni za kiaskari sijui kwanini serikali
haijawaona watu kama wewe.” Nikatabasamu bila
kuongea lolote.
Baada ya nusu saa tukafika nyumbani kwa Ommy,
Njaa ilikuwa imeanza kunishika. Nikachukua kiasi
cha fedha nikampa Ommy ili ajaze mafuta kwenye
gari na nyingine anunulie chakula. Ilikuwa ni saa
12.33 nikajilaza kitandani nikapitiwa na usingizi.
Saa mbili na nusu Ommy akaniamsha. Alikuwa
amenunua Chips mayai na soda. Njaa ilinifanya
niuvamie mlo huo kwa pupa. Baada ya kushiba
nikajinyoosha kiuvivu.
“Unafikiri kuna haja ya kuyafikisha Polisi haya
mambo?” Nilimuuliza Ommy. “Hapana! Sasa
nakubaliana na ushauri wako wa mwanzo, unajua
tatizo la hawa polisi wetu ukipeleka ishu kama hii
wataanza na wewe halafu utafuata mlolongo wa
watu ambao hawana hatia mpaka waje kuachiwa
watakuwa wamesota sana halafu mtuhumiwa
atakuwa hajapatikana na watautangazia umma
kuwa wanaendelea na upelelezi mkali na
kuwathibitishia kuwa watamtia hatiani
mtuhumiwa.” Nikafurahi baada ya kugundua kuwa
Ommy ameanza kuelewa mpango wangu.
“Nafikiri huu ni wakati muafaka wa kumtembelea
Betty” Nilisema huku nikimuangalia Ommy ambaye
alionekana kukubaliana na mawazo yangu.
Nikaingia chumbani. Nikachagua nguo ambazo
niliona zitanifaa kwa usiku huo. Niliamua kuvaa
suruali nyeusi ya jeans na fulana rangi ya udongo
huku nikimalizia kwa raba za rangi ya udongo
miguuni . Akafunga mlango tukaingia ndani ya gari
lake na kuondoka.
“unajua kesho ni lazima tuufungue ule mzigo?”
Nilisema huku nikimkazia macho Ommy .
“Hata mimi nina shauku kubwa ya kutaka kujua lile
begi lina nini ndani yake.”
“Bila shaka itakuwa ni almasi ”. Nilitamka kwa
kujiamini.
6
Saa nne kasorobo (3.45) tuliwasili Tabata
Kimanga, tukavuka daraja dogo lililokuwa mbele ya
Mazda bar kisha tukasimamisha gari hatua kumi
kutoka pale ilipo nyumba ya mpenzi wangu Betty.
Nilitembea taratibu kuelekea pale kilipo chumba
chake. Kwa mbali niliweza kusikia sauti ya muziki
kutoka Redioni. Taa ilikuwa inawaka jambo
lililonipa matumaini kuwa mwenyewe yupo. “Hodi!
…”Kimya. Nikabisha hodi kama mara tatu lakini
nililakiwa na ukimya uleule.
Betty alikuwa anakaa vyumba vya uwani lakini
hata nyumba kubwa ilikuwa kimya kabisa.
Haikuwa kawaida kwa nyumba hiyo kukosa watu.
“Leo kuna nini?” niliwaza. Nikagonga kwa nguvu
kidogo. Mambo yalikuwa yale yale. Nikaamua
kujaribu kufungua kitasa cha mlango ule,
ukafunguka.
Kwanza nilipokelewa na harufu nzito ambayo
haikuwa ya kawaida pili nikashtushwa na
mtawanyiko wa vitu mle chumbani, viti vingine
vilikuwa vimepinduliwa. Nguo zilikuwa
zimetawanywa huku na huko. Ni wazi kwamba
kulikuwa na vurugu hapo ndani. Nilianza kuingiwa
na hofu ya kuwa kuna jambo si la kawaida
limetokea, nilihisi kuwa huenda Betty ametekwa.
Nilikosea sana kwani sekunde chache baadae
nilifumbuka macho na kufahamu nini kimetokea
humo ndani. Mshtuko nilioupata haukuwa wa
kawaida. Kama nilifikiri kuwa Merina ndiye mtu
aliyeuwawa kikatili basi nilikuwa nimekosea.
Nilichokiona nilitamani iwe ndoto. Hayakuwa
mauaji ya kawaida. Mauaji ambayo hayakufanywa
na binadamu mwenye akili timamu.
Mwendawazimu tena zaidi ya mwendawazimu.
Nilikosa nguvu nikaegemea ukuta huku nikiendelea
kuangalia kitu ambacho nilitamani iwe ni ndoto tu.
Haikuwa ndoto lilikuwa tukio la kweli ambalo kama
utasimuliwa unaweza kusema ni simulizi
zinazotoka kwenye filamu za kusisimua hususani
za Wanaijeria.
Kichwa cha Betty kilikuwa kimekatwa kikawekwa
Mezani, mikono na miguu nayo ilikuwa imekatwa
na kupangwa mezani kama wanavyofanya wauzaji
wa nyama za kuku. Utumbo ulikuwa umetolewa na
kuwekwa kitandani. Kitanda chote kilikuwa
kimelowa damu. Yeyote aliyefanya hivyo alikuwa
amedhamiria kuleta maudhi makubwa kabisa.
Nilitetemeka kwa hasira.
“Ole wao hawa mbwa!” niliwaza. Nilizunguka kwa
hasira huku nikipiga ngumi ukuta. Naweza kusema
katika kumbukumbu zangu hakuna siku mbaya
katika maisha yangu kama siku hiyo na sidhani
kama itakuja kutokea siku kama hiyo.
Amewakosea nini? Kwanini makosa yangu yawe
mateso kwa mtu mwingine? Niliikumbuka sana
siku niliyokutana na Betty pale baa. Alikataa,
akakataa…Nikambembeleza, nikambembeleza kwa
maneno ya uungwana. Maskini sikujua kuwa
uhusiano wangu ungemponza kiasi hiki. Bora
ningekutana naye baada ya mkasa huu. Nilijiuliza
swali moja ambalo lilinitisha na kuniongezea hofu.

NANI ATAFUATA?
ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom