Riwaya: M Z I G O

Riwaya: M Z I G O

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Ole wao hawa mbwa!” niliwaza. Nilizunguka kwa
hasira huku nikipiga ngumi ukuta. Naweza kusema
katika kumbukumbu zangu hakuna siku mbaya
katika maisha yangu kama siku hiyo na sidhani
kama itakuja kutokea siku kama hiyo.
Amewakosea nini? Kwanini makosa yangu yawe
mateso kwa mtu mwingine? Niliikumbuka sana
siku niliyokutana na Betty pale baa. Alikataa,
akakataa…Nikambembeleza, nikambembeleza kwa
maneno ya uungwana. Maskini sikujua kuwa
uhusiano wangu ungemponza kiasi hiki. Bora
ningekutana naye baada ya mkasa huu. Nilijiuliza
swali moja ambalo lilinitisha na kuniongezea hofu.
NANI ATAFUATA?

Bila kujitambua nilikuwa nazunguka zunguka mle
ndani kwa muda wa dakika tano. Nilikuwa nahisi
kichefuchefu, mwili wote ulikuwa wa baridi. Hofu
ilikuwa imenitawala. Nilikuwa nimechanganyikiwa
vibaya, nikasikia sauti ya Ommy.
“Vipi mshikaji mbona unapoteza muda?”
“Ingia!” Nilimwambia kwa sauti iliyojaa utulivu.
Akaingia.
“Haa! My God, they killed her”(Mungu wangu
wamemuua).
Akashtuka huku akiwa ameziba mdomo. Ommy
aligwaya vibaya sana. Kwa dakika kadhaa alikuwa
ametumbua macho kwa mshangao.
“Twenzetu Kajuna hii ni kesi nzito!”. Wakati nataka
kuondoka nikauona ujumbe wa karatasi ambao
nilihisi umeachwa na wauaji. Sikutaka kupoteza
muda, nikaichukua ile karatasi na kuiweka mfukoni.
Kabla sijatoka mle ndani nikaanza kuhisi
kichefuchefu kikizidi. Nikaanza kusikia maumivu ya
kichwa ghafla. Ommy hakutaka kuruhusu hali hiyo
akanishika mkono kwa nguvu na kuanza kukimbia.
Nikajikuta nikikimbia bila kutaka.
“Kimbia kijana Polisi watakuja hapa muda si
mrefu!”. Tukaingia ndani ya gari kisha akaliondoa
kwa kasi. Baada ya dakika kama tano tukakutana
na gari aina ya 110 defender likiwa na askari
wapatao watano. Wote walikuwa na silaha. Ommy
aliongeza kasi ya gari kitendo kilichonifanya niwe
na hofu zaidi. “Ulijuaje kama askari watafika?
Nilimuuliza kwa mshangao.
“Mazingira ya ile nyumba yanaonesha kuwa
wanaishi watu wa familia tofauti haiwezekani wote
wawe wameondoka ni hofu tu ndo imewakimbiza
pale na ni lazima watoe taarifa Polisi”. Alijibu huku
akiendelea kuongeza mwendo wa gari lile. Spidi
ilikuwa inatisha mpaka wakati fulani nilihisi kuwa
tutaingia kwenye mtaro. Kutokana na kasi ile
niliogopa kuendelea kumsemesha kwani angekosea
kitu kidogo tu sidhani kama tungesalimika. Ule
mwendo ungeweza hata kuwashawishi askari wa
usalama barabarani kulitilia mashaka gari letu.
***

Jua lilipochomoza tu, Kitu cha kwanza ilikuwa ni
kukusanya magazeti ya siku ile. Magazeti mengi
yalikuwa na vichwa ambavyo viliyafanya yauzike
kwa siku ile. DAR YATIKISWA KWA MAUAJI
MENGINE YA KUTISHA. Baadhi ya magazeti
yalijinadi. Nilikuwa najua wazi kuwa hakuna jipya
nikachukua gazeti na kuanza kusoma. Kama
nilivyotarajia zilikuwa ni habari za Mauaji ya Betty.
Mwisho habari ilimalizia kwa kusema Polisi
wanaendelea na uchunguzi mkali.
Nikatulia kidogo nikitafakari tukio la jana. Kwa
namna fulani nilianza kujishangaa mwenyewe,
nilishaanza kuzoea matukio ya kutisha kwani
katika hali ya kawaida tukio la Betty lingeniumiza
sana kichwa lakini nikajikuta likinizidishia hasira na
kutamani kukutana tena na Bonge. Sikuwa na
woga tena mbele ya Bonge, nilitamani aingie
kwenye anga zangu nimuonyeshe kazi. Nilikuwa na
hasira kiasi ambacho mtu angekuwa karibu yangu
angeweza kusikia jinsi nilivyokuwa nasaga meno.
“Ole wake, ipo siku tu!….” Niliwaza.
Wakati nikiwa kwenye mawazo hayo mazito ndipo
nikakumbuka kile kikaratasi ambacho nilikichukua
eneo la tukio. Huku nikianza kurudiwa na woga
ambao ulishapotea nikaanza kukisoma kile
kikaratasi.
…..Tunajua uko hai makosa yalifanyika, uliandaliwa
kifo kitamu tena cha heshima. Ni raha ilioje
kutangazwa kuwa umekufa kwa bomu, je! Huoni
kuwa huo ni ujasiri? Umekataa kifo kile…… safari
hii tunataka kukusamehe lililo muhimu kwako ili
kupata msamaha tunaomba mzigo wetu…. La sivyo
tutakuuwa kinyama kuliko alivyouwawa huyo
malaya wako.Pia lazima ukumbuke kuwa picha
yako tunayo tunaweza kukuweka matatizoni.
Mtemi.
Niliusoma tena ule ujumbe, nikatikisa kichwa.
“Eti watanisamehe!” Nilijikuta nikisema kwa sauti
na kumshangaza Ommy ambaye alikuwa anaingia
kutoka bafuni.
“Watakusamehe kina nani!?” Sikumjibu nikampa
kile kikaratasi asome mwenyewe. Akakisoma,
alipomaliza nikamuona akitikisa kichwa.
“Wendawazimu kamili, uwape mzigo wakuache
hai!?” Alisema Ommy huku akiwa amekunja sura.
“Kifo cha heshima, kifo ambacho kingetawanya
viungo vyangu huku wao wakicheka na kula kuku!”
Nilitamka kwa sauti iliyojaa utulivu.
Walinishangaza sana hawa viumbe ambao
niliwatoa katika kundi la binadamu. Vyovyote
ambavyo ungeweza kuwaita kinyume cha
binadamu na malaika kwangu ilikuwa sahihi.
Ukiwaita mbwa sawa, ukiwaita nguruwe sawa
ukiwaita…….. jina lolote lile ambalo litawatoa katika
kundi la binadamu wastaarabu wao liliwastahili.
“Leo wapi?” Aliuliza Ommy.
“Leo ilikuwa siku ya kufungua mzigo” Nilimjibu
nikamuaona ananitazama kwa mshangao.
“Unasema ilikuwa siku ya kufungua Mzigo ina
maana hatufungui tena?”
“Mzigo utafunguliwa lakini sioni sababu ya
kufungua leo wakati bado tuko kwenye majonzi ya
kifo cha Betty. Sitaki nisherehekee wakati mbele
yangu kuna tatizo kubwa kiasi hiki.”
“Sawa wazo lako ni zuri, kwahiyo leo tutafanya
nini?”
“Leo tuna mambo mawili Ommy, kwanza nahitaji
kuonana na Debora pili nataka kufika eneo la
msiba ili niweze kujua nini kinaendelea.”
“Ina maana unataka kuhudhuria mazishi!”
“Hapana Ommy, Ingawa majirani walikuwa
wananifahamu lakini ndugu wa marehemu
hawanifahamu.”
“Sasa utaenda kufanya nini huko?”
“Nataka kujua kilichotokea kama itawezekana.”
“Unataka kuhoji watu msibani?”
“La, nataka kujaribu kama naweza kupata fununu
kutoka kwa waombolezaji.”
“Na huko kwa Debora?”
“Huko lazima niende kwani kuna mengi nataka
kujua kutoka kwa yule binti!”
“Ok, twenzetu.”
***
Watu walikuwa wengi pale msibani. Ndugu jamaa
na marafiki walikusanyika kwa wingi, kingine
ambacho kilisababisha kuvuta zaidi watu bila
shaka ni aina ya tukio lililosababisha kifo. Mauaji
yalikuwa ya aina yake, mtu kukatwa kiungo
kimojakimoja halikuwa jambo la kawaida.
Dakika tano zilipita tukiwa ndani ya gari.
Sikuthubutu kuteremka kwani niliona kuwa ni
hatari kwangu kama wangeniona watu ambao
walikuwa wanafahamu uhusiano wangu na Betty.
Sijui ni kwanini ujasiri wa kwenda pale msibani
uliniishia ghafla.
“Kajuna!”
“Sema Ommy!”
“Tutaganda hapa mpaka saa ngapi?”
“Mi nafikiri kuna umuhimu wewe uende kule ukajue
ukweli wa mambo, kwani kila ninavyowaza nahisi
kama kuna hatari inaniandama!”
Ommy akashuka garini na kuelekea kule msibani,
pale nilipokaa nilijitahidi kuinama ili macho ya
watu yasinifikie.
Nilikaa pale kwa muda wa nusu saa nikimsubiri
Ommy ambaye alishapotea katika macho yangu
baada ya kujichanganya kwenye umati ule wa
watu. Mara moja moja niliinua kichwa na
kuchungulia kule msibani lakini sikumuona Ommy.
Nilishangaa baada ya kuona nusu saa inamalizika
bila ya kumuona Ommy.
Niliamua kujilaza kwenye siti, sikutaka kusumbua
tena kichwa changu kujiuliza mambo yanayokuja.
“Oyaa vipi tena unalala!”
“Sijalala nimeamua kuificha sura yangu si unajua
anaweza kutokea mtu anayenifahamu nikaibua
mambo mengine?”
“Vipi una ripoti?”
“Ripoti si mzuri.”
“Kivipi?” Niliuliza huku kwa mara nyingine kijasho
chembamba kikianza kunitoka.
“Unatakiwa kuendelea kujificha zaidi kuliko
mwanzo.”
“Mhhhh!” Nilishusha pumzi nikamuangalia Ommy
ambaye alikuwa anaonesha kutaka kuendelea
kuongea. Kisha akaendelea.
“Eti wewe ndio mtuhumiwa namba moja wa mauaji
yale!” Tumbo lilishika joto ghafla baada ya kusikia
kauli hiyo. Nikaganda bila kuongea lolote huku
nikihisi kama midomo yangu imekauka.”
“Inawezekana vipi?” Kwa sauti iliyokauka yenye
mikwaruzo nilijikuta nikijikakamua na kuuliza swali
hilo.
“Inasemekana mara ya mwisho ulipoondoka kuna
uwezekano mkubwa kuwa mligombana na ndio
maana baada ya wewe kuondoka Betty hakuwa na
furaha mpaka kifo kilipomkuta!”
“Duh, bila shaka ni baada ya kumsimulia mkasa
wangu!”
“Sawa lakini kwa majirani hilo hawakulitambua na
ndio maana wameripoti kuwa huenda yale mauaji
yalikuwa ni ya wivu wa kimapenzi!”
“Duh huu msala sasa na kwa jinsi
ninavyowafahamu polisi hawana dogo hizo taarifa
watazishikia bango utafikiri wamethibitisha!”
“Lakini ni vizuri tumefahamu hatari iliyoko mbele
yako.”
“Na ndio maana nilihitaji kuja huku.”
***

Jua lilikuwa linawapungia mkono wakazi wa jiji la
Dar es salaam, giza nalo lilikuwa linapiga hodi na
kuwafanya baadhi ya wakazi wa jiji hili kuwa
katika hekaheka tofauti. Wako ambao huo ndio
ulikuwa muda wao wa kuanza shughuli huku
wengine wakiwa wanarejea mapumzikoni baada ya
kumaliza harakati zao za kimaisha.
Palepale ambapo tulisimama siku iliyopita ndipo
tuliposimama siku hii pia. Kama ilivyokuwa na siku
hii pia nilimuacha Ommy kwenye gari nikaelekea
nyumbani kwa Debora. Nilitembea haraka na kwa
kujiamini sana kwani jua lilikuwa limepotea na
hivyo nilifanikiwa kusitirika kwa kigiza chepesi
ambacho kilianza kutawala. Sikugonga kama
nilivyofanya siku ya kwanza kwani nilikuta ule
mlango wa bati la KORIE ukiwa wazi.
Kutoka nyumba kubwa nilikuwa nasikia muziki wa
taarabu ulioimbwa na marehemu Issa Matona.
Sauti ya kiutu uzima ilisikika kwa mbali ikifuatisha
wimbo huo. Taa ilikuwa inawaka chumbani kwa
Debora. Kwa kuwa kazi zake ni za usiku nilihisi
kuwa saa hizo atakuwa anajiandaa kuondoka.
Niliposogea mlangoni nikashtuka baada ya kusikia
mtu akifoka.
“Usitake kuongopa chochote wewe mbwa sema,
Kajuna alifuata nini hapa kwako?”
“Mimi simfahamu huyo Kajuna.” Niliisikia sauti ya
Debora ikiwa yenye kwikwi kwa kilio
“Uhai wako uko mikononi mwangu, ili uweze
kunusurika unatakiwa kuwa mkweli, yule mtu
aliyeingia hapa kwako jana alifuata nini?”
Kikapita kimya kirefu bila kujibiwa chochote.
Nikaangaza macho pale uani nikayaona matofali
ambayo yalikuwa yamepangwa sehemu moja.
Yalikuwa mengi kiasi bila shaka. Nikajitwisha moja
nakusogea pale mlangoni.
“Sasa kwa kuwa hutaki kusema nitakupa kile
unachohitaji.”
“Nis..s..sameh…. mimi simjui yul…….”
Hakuwahi kumaliza kauli yake niliuusukuma
mlango kwa nguvu na kuingia ndani. Yule mtu
akiwa ameduwazwa na uvamizi huo wa ghafla
alishindwa kufanya lolote licha ya kuwa na bastola
mkononi. Niliitumia Fursa hiyo kwa kumpiga kwa
tofali lile zito kichwani. Nilitumia nguvu zangu zote
nikamshushia kwa nguvu katikati ya paji lake la
uso.
“Mungu wangu… umeua kaka nitafanya nini mimi?”
Alianza kulia yule binti.
“Shhhiiiiiiiiiii!” Nilimtuliza kwa kuweka kidole cha
shahada katikati ya mdomo wangu.
Niliufunga mlango haraka kisha nikamkazia macho
makali.
“Tuna maiti humu ndani na muda si mrefu
unaweza kuwa kwenye mikono yas polisi, lazima
ujue kuwa wewe utakuwa mtuhumiwa namba moja
uko tayari?”
Alionesha mshtuko zaidi nilipotoa kauli hiyo lakini
hakujibu kitu.
“Nimekusaidia nimemuua mtu aliyetaka kukuua au
ulipenda ufe wewe?” Alikataa kwa kutingisha
kichwa.
“Sikia we mwanamke, Chukua kilicho muhimu
kwako haraka sana kwani kuendelea kukaa hapa ni
hatari kwako.”
“Niende wapi?”
“Nifuate!”
Akili yake ilionekana kutulia kidogo, akakusanya
vitu ambavyo aliona kuwa muhimu kwake
akaviweka kwenye begi kubwa. Tukaondoka
kuelekea kule aliko Ommy huku tukisaidiana
kushika begi lile kubwa.
“Aaah, Shemeji!” Alishtuka Debora baada ya
kumuona Ommy ndani ya gari.
“Vipi na huyu?” Aliuliza Ommy huku akionesha
mshangao wa wazi baada ya kuona nimeongozana
na Deborah tena akiwa na begi lake.
“Mkuu tuondoke haraka kwani nimeua mtu huko
ndani.”
“Umeua?” Aliuliza Ommy huku akichochea moto
kwenye gari.
“Ilibidi!” Nilimjibu kwa mkato.
Nikamsimulia Ommy kilichotokea kisha nikampa
maelekezo tuelekee Ubungo.
“Kuna nini Ubungo?”
“Ni huyu binti hatakiwi tena ndani ya Dar kwani
usalama wake bado uko hatarini!”
“Sasa utampeleka wapi?”
“Yeye mwenyewe atasema.”
“Shemeji… unatakiwa kusafiri utaenda wapi kwani
ni lazima uondoke ndani ya jiji!”
“Musoma kwa mama.” Alijibu Deborah huku
machozi yakitiririka kwenye macho yake.
“Yule mtu aliyetaka kukuua unamfahamu?”
“Nilikuwa namuonaona tu huko nje.”
“Umeanza kumuona lini!”
“kama sikosei nimeanza kumuona maeneo ya jirani
na nyumbani akiuza kahawa baada ya kifo cha
dada!”
“Mh, hawa jamaa wana mpango gani?” Aliuliza
Ommy.
“Inashangaza maana kila kona wameweka mtu,
bila shaka ni watu hatari sana.” Niliongea huku
nikihesabu fedha kwa ajili ya nauli ya Debora.
Tulifika Ubumgo saa 3.02, bahati ilikuwa upande
wetu kwani tulipata nafasi kwenye gari ambalo
lilikuwa linaondoka siku ya pili.
***

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU
“Yule mtu aliyetaka kukuua unamfahamu?”
“Nilikuwa namuonaona tu huko nje.”
“Umeanza kumuona lini!”
“kama sikosei nimeanza kumuona maeneo ya jirani
na nyumbani akiuza kahawa baada ya kifo cha
dada!”
“Mh, hawa jamaa wana mpango gani?” Aliuliza
Ommy.
“Inashangaza maana kila kona wameweka mtu,
bila shaka ni watu hatari sana.” Niliongea huku
nikihesabu fedha kwa ajili ya nauli ya Debora.
Tulifika Ubumgo saa 3.02, bahati ilikuwa upande
wetu kwani tulipata nafasi kwenye gari ambalo
lilikuwa linaondoka siku ya pili.
********

Nilijisikia tofauti kidogo kila nilipowaza kufungua
mzigo. Niliwaza iwapo nitakuta almasi ambazo
nilikuwa nazifikiria basi lazima niitafute familia ya
Betty kokote iliko ili niwape sehemu ya malipo
ambayo ingemstahiki Betty au sehemu ya
rambirambi yangu.
Oh, maskini Betty umeniacha.
Saa 2.15 tulifika maeneo ya Charambe magengeni.
Nilimwacha Ommy pale nilipomwacha siku ya
kwanza wakati napeleka ule mzigo kwa mjomba.
Kama kawaida nikaanza kutembea taratibu kufuata
vichochoro vinavyotokea kwa mjomba Kipupwe.
“Ooh! karibu mjomba, karibu sana!” Ingawa
alinichangamkia niliuona wazi mshangao ambao
ulikuwa kwenye macho yake.
“Vipi mjomba ulikuwa unaumwa!?” aliniuliza kwa
mshangao.
“Kwani vipi mjomba, mbona niko kawaida?”
“hapana, mjomba ingawa nimekuona siku chache
zilizopita lakini leo nakuona umebadilika, Kuna
tatizo?”
“Hapana ni kazi ngumu tu mjomba!” nilimjibu huku
nikikaa kwenye kigoda.
“Haya, habari za siku mbili tatu”
“salama mjomba shikamoo!”
“Marhaba mama yako hajambo?”Ainiuliza huku
akifunga vizuri msuli wake kiunoni. “Toka
nimemuona ile siku niliyokuja hapa sijamuona
tena!”Nilimjibu huku nikitamani amalize mapema
maswali yake nichukue begi langu.
“Mjomba nimefuata lile begi!”
“Ah! hapa ni kwako mjomba ingia tu uchukue!”
“Nikaingia ndani , nikawasha kibatari nikaingia
chumba ambacho nilihisi kuwa begi limewekwa
huko. Wakati natoka nikakutana na mke wa
mjomba mlangoni. “ooh! Kajuna Mwanangu
unataka kuondoka bila hata kunisalimia!” Alisikika
mke wa mjomba akiongea kwa sauti ya kulalamika
kana kwamba nilikuwa namdharau. “Samahani
shangazi si unajua maisha yanatupeleka puta,
hatuna hata muda wa kukaa mahali nusu saa”.
Nilimjibu huku nikiwa na hofu ya kukalishwa na
kuendelea kucheleweshwa. Nashukuru shangazi
hakuwa na maongezi mengi.
Nikabeba begi langu na kuondoka kuelekea kule
aliko Ommy. Kwa mbali tuliweza kusikia kama
harufu fulani ya kitu kilichooza kikitoka kwenye lile
begi. Haikuwa harufu kali sana lakini
haikutofautiana sana na nyama iliyokaa siku mbili
tatau kwenye friji.
“Labda ni dawa za kuhifadhia Almasi!” Niliwaza.
Mpaka kufikia hapo naomba niweke wazi kuwa
mapigo yangu ya moyo yaliongezeka maradufu.
Kijasho chembamba kilikuwa kinanitoka nilikuwa
kama mtu anayesubiri kupewa taarifa za mgonjwa
anayepumulia mashine.
“Huu mzigo umenisababishia matatizo mengi sana
una nini ndani yake?” Hicho ndicho kilichonipa hofu
zaidi.
“Kajuna, unajua nauogopa sana huo mzigo hasa
kutokana na mambo mengi yanayojitokeza!”.
Nilitabasamu baada ya kugundua kuwa kumbe
Ommy naye alikuwa na hisia kama zangu.
“Yaani jinsi moyo unavyopiga kwa nguvu nahisi
kama unataka kuchomoka!” alisema Ommy na
kunifanya nicheke. Aliwasha gari akaliondoa kwa
mwendo wa kawaida.
********

Tulikuwa tumepanga kufungua ule mzigo baada ya
kumaliza kula. Kwani kama ule mzigo ungekuwa
na almasi ambazo tulisadiki kuwa zimo basi
tusingeweza kula kwa furaha ambayo tungekuwa
nayo. Tulitazamana na Ommy kana kwamba
tulikuwa tunaambiana fungua wewe. Nililitazama
tena lile begi nikapiga moyo konde.
“ Naomba kisu!” nilisema kwa sauti ambayo hata
Ommy alibaini kuwa ilikuwa na kitetemeshi.
Akanipa kisha akasimama kando.
“Fungua!” Nilisema huku nikimpa kile kisu.
“Hapana Kajuna moyo wangu una hofu kweli
siwezi!” Niliona wazi Ommy akipotelewa na ujasiri.
Kweli alikuwa hataki kabisa kufungua lile begi.
Tukabaki tukitazamana kwa dakika kadhaa. Mzigo
huu una nini? Hilo pia lilisababisha hofu. Hakuna
aliyekuwa tayari kuchukua jukumu la kufungua
mzigo huo. Kingine kilichonifanya nihofu ni
kumbukumbu ya lile Briefcase hawa watu ni vichaa
kamili wanaweza kuweka hata bomu kwenye mzigo
huu.
Nikaamua liwalo na liwe tu wakati wa kufungua
begi ulikuwa umefika. Begi lilikuwa limefungwa kwa
kufuli ndogo la shaba. Kwa kutumia kisu nikatanua
sehemu ambayo ilishikilia vishikio vya zipu. Kikawa
kimebaki kishikio cha upande mmoja huku kile
kingine kikining’inia kwenye kufuli. Mzigo
ukafunguliwa! Chochote kilichohifadhiwa kilikuwa
kimefunikwa kwa kitambaa cheusi ambacho
kilikuwa juu yake. Nikakitazama kile kitambaa
halafu kwa mikono inayotetemeka nikafunua.
Huwezi kuamini! Nasema huwezi kuamini….. Hata
kama ungesimuliwa bado ungekipa shida kichwa
chako kutafakari ni kwa namna gani jambo hilo
linaweza kuwa na ukweli. Akili ya kawaida
ingekataa. Oh, huu ndio MZIGO ambao umenitesa
na kuniweka njia panda, huu ndio mzigo ambao
umesababisha uhai wa mpenzi wangu kukatishwa,
MZIGO umenipa majonzi…………. Ah! MZIGO.
Si mimi wala Ommy, sote tulikuwa tumeacha
midomo yetu wazi. Ni vigumu kuamini lakini zilipita
dakika kumi tukiwa tumeukodolea macho mzigo
ule. Baada ya hapo zilifuata dakika tano nyingine
ambazo tulikuwa tunatazamana bila kusema neno
lolote.
“Si mchezo babaake!” Ommy alivunja ukimya.
Sikusema neno lolote badala yake nilikaa kwenye
kiti nikashika tama. Ilikuwa haiingii akilini kabisa
kuwa siku zote nilikuwa natembea na mzigo wa
ajabu namna ile. Mzigo ambao umenitesa na
kuniingiza kwenye misukosuko mizito. Mzigo
ambao kama ningekutwa nao nilikuwa sina ujanja
wa kukwepa hukumu ya kifo kwani aliyekutwa na
ngozi ndiye mwizi wa mbuzi. Kama ningenusurika
basi ingechukua muda mrefu kubainika kuwa
sijahusika. Mpaka hapo ningekuwa nimepoteza
muda mwingi gerezani.
Kwa moyo wenye ujasiri niliinuka kwenye kiti
nikauendea ule mzigo. Nikawa naukagua vizuri.
Hapa niliweza kubaini kuwa binadamu amefikia
kiwango cha ushenzi zaidi ya mnyama. Mnyama
mara nyingi hufanya mambo kwa mipaka lakini
kwa hili binadamu alikuwa amevuka mpaka. Ndani
ya lile begi kulikuwa na miguu miwili na mikono
miwili ya Albino, yote ikiwa ni ya kulia,
nilihamanika vibaya sana. Kwa makadirio ya
haraka viungo hivyo vilikuwa ni vya watoto wenye
umri wa kati ya miaka tisa na kumi na nne.
“This is too much…” Aliropoka tena Ommy huku
akiwa ameshika kiuno kwa mikono yote miwili.
“Unafikiri kuna haja ya kuripoti Polisi!?” Niliuliza
huku bado nikiwa nastaajabia mzigo ule.
“Uko tayari kuwa mshukiwa namba moja?”Aliniuliz
a huku akiwa amenikazia macho kwa mshangao.
Niligwaya.
“Unafikiri hili tukio linamaanisha nini?” Nilimuuliza
tena.
“Mwisho wa dunia!”
“Kwa vipi?”
“Huyu au hawa watu wangekuwa wanataka pesa si
bora wangefanya uporaji Benki kuliko haya
waliyoyafanya, na hii si tabia yetu Watanzania”
“Nafikiri kuimarishwa kwa ulinzi kwenye Mabenki
ndio maana wameshindwa!” “Hapana usiniambie
hawa watu wana matatizo ya fedha nafikiri kuna
kitu kimejificha hapa!”
“Kwanini?”
“Unajua haya mauaji ya Albino yanapofanyika
hawa watu wanatumia gharama kubwa hili
linanifanya nijiulize wanataka nini zaidi?”
“Ukiuliza hivyo utakuwa unarudi kwenye jibu lako,
hii ni dalili ya mwisho wa dunia!” “Pamoja na
kuwa ni dalili ya mwisho wa dunia sikutegemea
kitu hicho kifanywe na Mtanzania!” Alijibu Ommy
huku akiwa bado ameshika kiuno.
“Unafikiri tufanye nini sasa?” aliniuliza Ommy.
“Mimi nafikiri tufuatilie mkasa huu kwa tahadhali
kubwa pale tutakaposhindwa tutaomba msaada
Polisi!”
“Yaah! Kwa hilo nafikiri uko sahihi kwani si ajabu
kukuta baadhi ya polisi wanahusika.”
**********

Saa 1.09 tulikuwa maeneo ya Yombo Buza.
Tuliegesha gari Buza kwa Lulenge halafu tukaanza
kutembea kwa miguu kuelekea Buza Kanisani.
Kulikuwa na Umbali wa Kilomita Moja na nusu.
Jinsi tulivyokuwa tunatembea hakuna aliyeweza
kugundua kuwa safari yetu ilikuwa moja.
Tulipokariba Ommy akasimama kwenye Mkorosho
akanipa ishara iliyonifahamisha kuwa yeye
atanisubiri hapo.
Nikatembea taratibu kuelekea nyumbani. Nilipofika
wapangaji wenzangu walikuwa vyumbani mwao
wakiangalia kipindi cha vichekesho ambacho
hurushwa na moja ya runinga za hapa nchini.
Niliishukuru Mungu maana kama ningewakuta nje
wangeanza kuuliza hili na lile kitu ambacho
sikutaka kabisa kitokee.
Nikafungua mlango nikaingia ndani kisha
nikawasha taa. Nilichokiona nilikuwa nimekitarajia.
Chumba changu kilikuwa kimepekuliwa. Kila kitu
kilikuwa kimetawanywa mle ndani. Nikamshukuru
mungu ambaye aliniongoza kukutana na Ommy
kwani kwa kumbukumbu zangu Ommy ndiye
aliyenishawishi nisilale nyumbani kwangu.
Nikaangalia mle ndani sikuona kitu cha umuhimu
zaidi ya uhakika kuwa wale jamaa walifika.
Nilikiangalia chumba changu kwa uchungu,
machozi yalianza kunitoka na kujihisi unyonge kila
nilipokitazama kile chumba kwani kilinirejeshea
kumbukumbu ya mpenzi wangu Betty yaani
amekufa hata hajui naishi wapi! Nilijua siku moja
Betty atakuja kuwa mama watoto wangu.
Tungekaa hapa siku chache kabla ya kutafuta
makazi mengine. Bado kidonda cha uchungu wa
kifo cha kikatili cha Betty ulikuwa kwenye nafsi
yangu.
Nikafunga mlango kimyakimya ili majirani
wasigundue ujio wangu. Nikaangalia huku na huko
sikuona mtu nikanza kuondoka kumfuata Ommy
pale nilipomwacha, sikumkuta! Kidogo nikaanza
kuingiwa na hofu. Si kawaida ya Ommy kuvuruga
utaratibu. Sikutaka kujiuliza zaidi nikaendelea
kupiga hatua kuelekea kwa Lulenge. Ingawa
ilikuwa ni usiku kichochro nilichokuwa napita
kilikuwa na giza zaidi kwa sababu ya miti
iliyokuwa imelizunguka eneo hilo. Sikutembea
hatua zaidi ya kumi nikashtushwa na sauti kali
iliyojaa amri.
“Tafadhali simama na usithubutu kugeuka, sipendi
nikulipue kabla muda wako haujafika!” Ilikuwa ni
sauti ambayo haina hata chembe ya mzaha.
Nikaanza kuongozwa kikondoo huku nikiwa na
uhakika kuwa kama Ommy hajauwawa basi
atakuwa ametekwa. Kiasi fulani nikaanza kujilaumu
kwanini tukio lile nilikuwa sijaripoti polisi mapema.
Tukatembea hadi sehemu ambayo wale jamaa
walikuwa wamepaki gari. Lilikuwa ni gari la
kizamani aina ya Toyota Corrola, tulipolifikia
nikamkuta mtu ambaye alinifungulia mlango wa
mbele kwenye siti ya abiria kisha watu wawili
wakakaa siti ya nyuma huku wakipiga mikwala
mizito.
Dereva alikuwa ni mtu mfupi mwenye mapele
mapele usoni. Macho yake yalikuwa mekundu na
alionesha kuwa hakutoka kuvuta bangi muda
mrefu kwani alikuwa ananuka harufu ya bangi.
Nikamtazama mara mbili, sura yake haikuwa
ngeni. Nilijaribu kuvuta kumbukumbu hatimaye
nikamkumbuka. Ni huyu ndiye aliyetufungulia lango
siku niliyopeleka mzigo feki kwa Bonge.
“Hivi hawa wamemfanya nini Omari!” Niliwaza
nikiwa na ghadhabu iliyochanganyika na hofu. Gari
liliondolewa kwa kasi sana. Tukapitia bara bara ya
vumbi inayoelekea Abiola. Hata kama ungekuwa na
wazo la kuruka kwenye gari kwa kasi hiyo
usingethubutu. Ilikuwa ni ‘spidi’ kubwa ambayo
ilimshangaza yeyote aliyeliona gari hilo. Wengi
walilitilia mashaka. Lakini hakuna hata aliyejaribu
kutoa taarifa polisi.
Tulipofika katika mteremko mkali ambao uko
karibu na reli ya Tandika likatokea tukio la ghafla.
Nikasikia kishindo kikubwa kama mlipuko.
“Mshenzi…anatuuaaaa….”nilimsikia dereva
akilalamika huku akimalizia kwa matusi ya nguoni,
bila kuelewa kilichotokea nikaliona gari likiacha
barabara na kuserereka kuelekea bondeni.
‘Buuuuu….’ Kilikuwa ni kishindo kikubwa ambacho
kilinifanya nifumbe macho. Nikajiona nazama
kwenye kiza kizito sana.
“Sijui ndio kufa kwenyewe….” Niliwaza hatimaye
nikapotelea kwenye hicho kiza halafu sikukumbuka
kitu tena baada ya hapo.
7
Nilifumbua macho nikakutana na mwanga mkali
ambao uliumiza macho yangu. Nikafumba tena.
Chumba kilikuwa na harufu kali ya Dawa.
Nikafumbua tena macho yangu, nilishindwa kujua
kama niko ndotoni au niko katika mazingira gani.
Nilipoangalia vizuri mle ndani nikagundua kuwa
niko hospitali.
“Mbona sina tatizo lolote la Afya” nilijiuliza huku
bado nikiendelea kushangaa mandhari ile. Kuna
wakati mtu unaweza kuota na ukajuwa kuwa uko
ndotoni, basi nilifikiri kuwa ndio wakati huu.
“Hii sio ndoto ni kweli kabisa!” Niliwaza.
“Kama ni hospitali nimefikaje, au nina kifafa,
mbona sina kumbukumbu ya kitu kama hicho au
kimeanza ukubwani!?” Nilijiuliza maswali mengi
ambayo hayakuwa na majibu. Nikajaribu
kuzungusha macho yangu mle ndani, hapo
nikaanza kusikia maumivu makali ya kichwa.
Nikajaribu kunyanyuka hapo ndipo nilipopatwa na
mshangao zaidi. Mkono wangu wa kulia ulikuwa
umefungwa Pingu.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

“Mbona sina tatizo lolote la Afya” nilijiuliza huku
bado nikiendelea kushangaa mandhari ile. Kuna
wakati mtu unaweza kuota na ukajuwa kuwa uko
ndotoni, basi nilifikiri kuwa ndio wakati huu.
“Hii sio ndoto ni kweli kabisa!” Niliwaza.
“Kama ni hospitali nimefikaje, au nina kifafa,
mbona sina kumbukumbu ya kitu kama hicho au
kimeanza ukubwani!?” Nilijiuliza maswali mengi
ambayo hayakuwa na majibu. Nikajaribu
kuzungusha macho yangu mle ndani, hapo
nikaanza kusikia maumivu makali ya kichwa.
Nikajaribu kunyanyuka hapo ndipo nilipopatwa na
mshangao zaidi. Mkono wangu wa kulia ulikuwa
umefungwa Pingu.
“Hii ajabu kweli! Hivi hapa ni Polisi magereza au
hospitali?” Bado mlolongo wa maswali uliendelea
kuongezeka. Nilipoangalia vizuri kumbe nilikuwa
nimetundikiwa chupa ya damu. Nikawa najitahidi
kuvuta kumbukumbu kwanini niko pale. Nikaanza
kukumbuka safari yangu ya Mwanza.
“Hivi nilisharudi Mwanza au bado niko Mwanza?”
Nikatulia nikikumbuka kipande hicho cha Mwanza.
“Kwani jamaa alishakata tikiti ya kurudia?”Nikaku
mbuka jinsi nilivyoagana na Martin. Kipande cha
Mwanza kikapita. Ikaja kumbukumbu ya kuuwawa
kwa mpenzi wangu Betty nikashtuka nikataka
kuamka, nikakutana na Maumivu makali ya kichwa
yakanifanya niendelee kutulia kitandani. Hatimaye
ikanijia kumbukumbu ya lile tukio la kuanguka na
gari pale karibu na reli ya Tandika. Nikawa
nimeipata kumbukumbu ya kile kilichotokea. Sasa
ilikuwaje nikaletwa Hospitali tena nikiwa
nimefungwa pingu hicho kilikuwa ni kitendawili
ambacho kiko nje ya uwezo wangu.
Hivi kweli nilipona mbona kama nilishakufa?
Wakati bado niko kwenye lindi la mawazo
nikauona mlango wa chumba kile ukifunguliwa.
Mpaka kufikia hapo nilikuwa sina uhakika kama ile
ni wodi au chumba cha kawaida ambacho kina
mkusanyiko wa vifaa vya hospitali. Akaingia
muuguzi ambaye alikuwa amevaa sare nyeupe.
“Ooh! umeamka ashukuriwe Mungu wa mbinguni”
aliongea yule mama ambaye umri wake katika kazi
ulikuwa unaelekea ukingoni.
“ Mwanangu pole sana kwa matatizo. Najua ni
shetani tu ndo’ alikuteka mpaka ukaingia kwenye
ujambazi, lakini bado nafasi unayo kwani Bwana
anakuita…… Bwana asema……” Chochote
alichoongea sikuweza kusikia kwani alinishtua mno
eti shetani ndo alikuteka ukaingia kwenye
ujambazi! Ina maana mimi ni jambazi? Nilitishika
kidogo kwani ni wazi kuwa niko kwenye mikono ya
Polisi. Angalau nilikuwa sehemu ambayo ina
usalama kidogo kuliko ningeangukia kwenye
mikono ya Bonge na kundi lake. Lazima
wangeniadhibu. Lakini hata huku niliko kama
nitakuwa nimefikishwa kwa kutumia ushahidi wa
ile picha bado niko hatarini.
Sijui kama yule mama aliongea mpaka mwisho au
alikatisha maongezi yake kwani fikra zangu
zilikuwa mbali sana. Ninachokumbuka ni kusikia tu
baadhi ya maneno kama Matayo…Wakorintho na
wengine sijui nani vile…. Eee! Nimekumbuka
Waefeso lakini sijui alizungumzia nini zaidi. Bila
shaka alikuwa ananihubiria kitu fulani akijua kuwa
mimi ni jambazi. Sikumsikia, sikumsikiliza. Hata
jinsi alivyoondoka mle ndani sijui.
Baada ya muda kidogo nikasikia mlango
ukifunguliwa tena. Pamoja na maumivu niliyokuwa
nayo nikageuza kichwa ili kujua ni nani alikuwa
anaingia. Moyo ukanipiga “Paaaa…” alikuwa ni
mzee Kazakamba yaani baba yangu mzazi, alikuwa
ameongozana na mama yangu mzazi. Walikuwa
wamesindikizwa na askari wa jeshi la polisi
ambaye bila shaka alikuwa amekaa nje akinilinda
nisitoroke. Duh! Kwangu lilikuwa jambo la
kustaajabisha yaani mimi nimekuwa mtuhumiwa
kwa lipi? Mbona sina kumbukumbu ya tukio baya
ambalo lilistahili hata kukaa gerezani kwa siku
kadhaa. Nikakumbuka kitu PICHA, moyo ukalipuka
tena “Paaaaa!” Kweli nilikuwa kitanzini. Na sasa
baba yangu mzazi kaja kuniona kama nani
mtuhumiwa mgonjwa au………….. vyovyote vile
hakuna zuri kwangu kwanza kajuaje?
“Mwanao ni mtu hatari sana mzee, anahusika na
mauaji ya watu wengi yanayoendelea hapa mjini!”
Alisema yule askari huku akiwa amesimama
kiubabe ubabe. Nilimwangalia baba usoni, machozi
yalikuwa yanamlengalenga. Kwa upande wa mama
yeye alikuwa analia kabisa.
“Baba…” nikafanikiwa kutoa sauti. Kwa kuwa
nilikuwa naongea kwa sauti ndogo akanisogelea.
“Niamini baba...mimi ni mwanao niombeeni kwa
Mungu kwani sina hatia na hii kesi naamini
nitashinda tu.
” Niliongea huku nikiwa nimefumba macho kwani
mwanga ulikuwa unaniumiza kichwa. Baba
akanitazama kwa huruma kisha akajikakamua na
kuuliza.
“Hivi ilikuwaje Kajuna Mwanangu?” Baba aliniuliza
kwa sauti yenye majonzi
“Ni habari ndefu sana inahitaji muda
kuelezea!”Kabla sijaendelea na maongezi yule
askari akaingilia kati.
“Mzee mimi nimekufanyia uungwana tu, kimsingi
huyu haruhusiwi kuongea na mtu mwingine zaidi
ya Polisi na daktari!” Alisema yule askari huku
akifungua mlango na kuwataka wale wazee wawili
waondoke. Nilimuona mama akifuta machozi kwa
kitenge chake. Nilihisi kitu fulani kikiwa kimenishika
kooni, lilikuwa ni donge la uchungu, mama analia
baba analia naonewa mimi.
***

Ilikuwa ni siku ya tatu nikiwa katika hospitali ile
ambayo hata jina sikuifahamu. Kila aliyeingia
alikuwa hana muda wa kusikiliza shida yangu.
Nilikuwa nachukiwa na askari na wauguzi. Wakati
mwingine wauguzi walikuwa wakilalamika kwa nini
kazi ya kuhudumia majambazi wapewe wao. Wapo
waliotamka wazi kuwa eti bora askari
wangenimaliza moja kwa moja kuliko kuwaletea
usumbufu. Niliumia sana moyoni. Hivi hawa
hawajui kabisa kuwa kesi nyingine huwa
zinajitokeza kwa makosa tu! Mbona kuna watu
wamechomwa moto kwa kudhaniwa kuwa ni wezi.
Hujafa hujaumbika bwana, hawakuwa na haki ya
kuninyanyasa kiasi kile. Kwa upande mwingine
hawa wauguzi walipendeza zaidi kuwa askari
kuliko hivi walivyo. Nakumbuka siku zile nikiwa
mdogo muuguzi akinichoma sindano atanipa pole,
atanibebembeleza, ata…. Ili mradi atanifanyia kila
lenye kuleta faraja. Hawa wauguzi gani ambao
huwasimanga hata kina mama wajawazito wakati
wa kujifungua! Sina kwa kutolea malalamiko yangu
ningewaambia wauguzi jirekebisheni muwe kama
wale wa zamani au sijui hawa tulio nao ndio wale
wanaoingia kazini kwa migongo ya ndugu zao?
Wakati nikiendelea kuwaza akaingia askari
mwingine. Nilikuwa nimeshapata nafuu. Yule askari
akanijia pale kitandani akaongea kwa sauti ya
kunong’ona.
“Kijana usalama wako uko katika mambo mawili
tu. Moja ni kufunga mdomo na la pili ni kurudisha
mzigo! La sivyo utafute majibu ya kumridhisha Jaji
kuwa hujaua mwanamke kule gesti picha yako
tunayo na nakala nyingine iko polisi!" Lilikuwa
kama pigo kali la radi.
“Huyu nae yumo!?”. Nilichanganyikiwa vibaya
sana. Nilikuwa najua nipo kwenye mikono salama
kumbe ni wafuasi wa bonge. Yaani bora angetaja
kitu kingine chochote kuliko habari ya picha.
Ghafla, mlango ukafunguliwa. Akaingia askari
mwingine ambaye aliduwaa kwa dakika kadhaa
baada ya kumuona askari mwenzake ambaye
hakuwa kwenye ratiba na pengine alikuwa
hamfahamu kabisa. Ajabu! Yule askari alionekana
kushtushwa na ujio wa askari mwenzake. Nikauona
mkono wa kulia wa yule afande wa kwanza
ukitafuta kitu kwenye mfuko wake.
Mungu wangu! Bastola. Jamaa alichomoa bastola
bila kushtukiwa na askari wa pili. “Nooo!”
Niliropoka kwa kihoro baada ya kukiona kidole cha
shahada cha yule askari wa kwanza kikiwa
kimeelekea kwenye kitasa cha kufyatulia risasi!”
“Paaaa! paaa….” Mlio wa risasi mbili mfululizo
uliwashtua watu pale hospitali. Jamaa alikuwa
ameelekeza bastola kwangu. Nilikuwa nakiona kifo
wazi wazi. Nikataka kuruka kitandani, lakini pingu
ikanishika barabara kwani ilikuwa imefungiwa
kwenye moja ya pembe za kitanda kile cha chuma.
Badala yake nikapiga mwereka mkubwa kitanda
kikaniangukia na kunifunika. Nikasikia risasi
nyingine tatu ambazo zilikilenga kitanda kile.
Sikuwa na uhakika kama risasi zilikuwa zimenipata
au la! Kwani maumivu yalikuwa makali kutokana
na kuangukiwa na kitanda halafu kutonesha
majeraha ambayo yalikuwa yameanza kupona.
Nje kulikuwa na balaa kubwa. Kwa kelele
nilizokuwa nasikia nahisi hata wagonjwa waliacha
vitanda vyao na kuanza kukimbia. Wakati nikiwa
bado nimefunikwa na kile kitanda nikasikia
milipuko mingine ya risasi. Maumivu yalikuwa
makali lakini nikajikaza kiume na kujiinua pale
chini. Duh! Ilikuwa inatisha. Nilimuona yule askari
akitapatapa kwenye dimbwi la damu. Alikuwa
anarusha miguu huku na huko kwa uchungu wa
kifo. Baada ya dakika chache nikamshuhudia yule
askari akikodoa macho ukodoaji ambao si wa
kawaida. Alikuwa amekufa!
“Duh!Huu sasa msala mpya, Askari ameuwawa
kwa bastola mbele yangu nitaeleweka
kwele?”Niliwaza huku nikiwa na wasiwasi wa
kuongezewa idadi ya mashtaka yanayo nikabili.
***

Ukimya ulikuwa umetawala katika korido hii.
Nilikuwa nimefungwa kitambaa usoni. Nilijua
kabisa eneo hilo ni korido lakini sikujua ni sehemu
gani. Nilikuwa na uhakika kuwa niko ghorofani
nikipelekwa chumba hiki na kile bila kuambiwa
lolote. Nikaingizwa katika chumba ambacho nafikiri
walikusudia kunifikisha, wakanifungua kitambaa.
Kulikuwa na watu watano ambao nyuso zao
zililikuwa na mikunjo ya hasira kama mtu
anayekula kitu kichungu.
Kwa mtazamo wa haraka niliwatambua kuwa ni
askari, lakini nahisi walikuwa ni askari maalum.
Chumba hiki kilinitisha sana kilikuwa na vitu vingi
vya ajabu ajabu. Vitu nilivyovitambua ndivyo
vilivyonifanya niingiwe na hofu. Kulikuwa na visu,
mikasi, nyundo na kiti ambacho nilikitambua mara
moja kuwa kimetegeshwa nguvu za umeme,
maalum kwa kuadhibu wahalifu. Nilikifahamu kiti
hiki kupitia filamu za kizungu, nilikuwa naona jinsi
watu walivyokuwa wanateswa kwa kiti hicho
kwenye filamu hizo. Askari wote walikuwa
wananitazama kwa macho makali bila kuongea
neno lolote. Moyo ulikuwa unaenda mbio ajabu!
Askari mmoja akanielekeza kwa kidole niende
kukaa kwenye kile kiti cha umeme.
“Vipi bado?” aliuliza askari mmoja.
“Tunamsubiri afande Edwin, si unajua yeye ndo’
mtaalamu wa mambo kama haya hata akiwa bubu
ataongea tu!” Duh! Niligwaya baada ya kusikia
kauli hiyo lakini nikapiga moyo konde.
Nikarejesha mawazo yangu nyuma. Nikakumbuka
tukio la kuuwawa askari pale Muhimbili. Nilikuja
kugundua kuwa ni hospitali ya Muhimbili ile siku
ambayo madaktari walithibitisha kuwa Afya yangu
ni nzuri hivyo kuwaruhusu askari kunichukua.
Kilichonishangaza ni msafara wa magari mawili
yaliyokuwa na askari lukuki tena wenye silaha!
Kana kwamba haitoshi nilikuwa nimefungwa pingu
mikononi na miguuni. Tena nikapigwa na butwaa
baada ya kuliona kundi kubwa la watu likiwa nje
huku wakifanya purukushani za kutaka kuniona.
Wapiga picha nao hawakuwa nyuma, sijui kama
walikuwa ni wapiga picha wa magazeti au wale wa
kawaida. Lakini kitu kimoja niliweza kukibaini
kutoka kwenye kundi hili la watu. Bila shaka
nilikuwa ni mtu ambaye nimefanya tukio ambalo
limetikisa jiji la Dar es salaam. Mle wodini sikupata
fursa ya kusoma habari wala kusikiliza taarifa ya
habari hivyo nilikuwa sijui nini kinaendelea huko
nje. Nikachukuliwa hadi kituo cha polisi Temeke
pale Chang’ombe. Nikafungiwa bila kuambiwa wala
kuhojiwa chochote kwa muda wa siku tatu. Halafu
ndio ikafika siku hii ya leo ambayo nimefungwa
kitambaa na kuondolewa pale Temeke kwa gari
hadi huku ambako sikufahamu.
“Hivi nimeletwa huku kwa kosa gani?” niliuliza
baada ya kuona hakuna ninachoelewa. Askari
wakanitazama bila kunijibu kisha wakaendelea na
maongezi yao. Kutokana na mawazo sikuweza
kujua walichokuwa wanaongea. Kitendo cha
kunidharau na kuendelea na maongezi yao
kilinifanya niwe na hasira. Wakati nikiwa kwenye
bahari hiyo ya mchanganyiko wa mawazo
nikauona mlango wa chumba kile ukifunguliwa.
Watu wawili waliovaa suti na tai ambao bila shaka
nao walikuwa ni askari wakaingia. Wakakaa
kwenye viti. “Vipi mbona hamjaanza kazi?” aliuliza
mmoja wa wale walioingia. “Ah, mtu mwenyewe
kama ni huyu hatuoni sababu ya kufanywa na
watu mia kazi ndogo kama hii!”
Dharau?
“Tulijua hii kazi anaweza kuimaliza afande Edwin
hata akiwa peke yake”
Ukimya ukatawala ndani ya chumba kile hakuna
aliyeongea baada ya kauli ile ambayo kwa upande
wangu niliiona kuwa ni ya dharau kubwa
“ Vipi afande mko tayari?” aliuliza mmoja wa
askari wale. Akaitikia kwa kichwa. Wale askari
wengine wakaondoka mle ndani wakabaki wale
wenye suti. Wakanifunga kwa mikanda maalumu
pale kwenye kiti cha umeme. Nikamuona mmoja
wa askari wale akivua koti. Akafungua tai, akavua
shati lake jeupe. Akawa amebaki na fulana ya
ndani tu.
“Kijana tunataka majibu mazuri kwa maswali yote
tutakayokuuliza sawa?” alianza yule ambaye bado
alikuwa kwenye vazi lake la suti.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO

Ukimya ukatawala ndani ya chumba kile hakuna
aliyeongea baada ya kauli ile ambayo kwa upande
wangu niliiona kuwa ni ya dharau kubwa
“ Vipi afande mko tayari?” aliuliza mmoja wa
askari wale. Akaitikia kwa kichwa. Wale askari
wengine wakaondoka mle ndani wakabaki wale
wenye suti. Wakanifunga kwa mikanda maalumu
pale kwenye kiti cha umeme. Nikamuona mmoja
wa askari wale akivua koti. Akafungua tai, akavua
shati lake jeupe. Akawa amebaki na fulana ya
ndani tu.
“Kijana tunataka majibu mazuri kwa maswali yote
tutakayokuuliza sawa?” alianza yule ambaye bado
alikuwa kwenye vazi lake la suti.
“Jina lako ni nani?”. Alianza kuuliza huku
akizunguka zunguka kiti nilichokalia. “Kajuna Daudi
Kazakamba”
“Kajuna Daudi Kazakamba!” akayakariri yale
maneno huku akiandika kwenye kidaftari chake
kidogo.
“Kabila lako?”
“Mhaya!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo!”
“Mimi naitwa Rutashobya nataka tuongee kihaya
ili nithibitishe kauli yako uko tayari?”
“Hapana!”
“Kwanini?”
“Nimezaliwa na kukulia hapa hapa Dar es salaam.”
“Unataka kuniambia hata bibi yako hujawahi
kumuona?”
“Nimewahi kumuona kwani nilikuwa naenda na
kukaa wiki moja tu!”
“Hapa Dar es salaam unafanya kazi gani?”
“Sina kazi maalum!”
“ndio maana umeamua kuwa muuaji?”
“katika maisha yangu sijawahi kuua hata mbuzi!”
‘Paaaa….’ Jamaa akanizaba kibao kikali ambacho
kilinifanya nione vimulimuli fulani kama nyota vile.
Kilikuwa kibao cha haja cha mtu aliyeshiba.
“Tulianza vizuri lakini sasa unaanza kuharibu!”
Sikumjibu nikamtazama bila kuongea chochote.
“Ninachotaka kujua si kama uliua au hukuua.Kwa
nini unaua watu na kuleta hofu hapa mjini?”
lilikuwa swali lililoniingia kama ncha ya kisu
katikati ya moyo wangu. Sikujibu hadi
niliposhtushwa na kofi lingine safari hii likiwa la
upande wa kulia. Shavu lilikuwa kama
lililomwagiwa mafuta ya moto kwa ukali wake.
“Narudia kwanini unaua hovyo na kusababisha
hofu hapa mjini?”
“Afande nikuambie mara ngapi kuwa si mtu tu!
Sijawahi kuuwa hata mbuzi.” Afande akashikwa na
jazba akanishika sehemu za siri, akanibinya kwa
nguvu kule sehemu …sehemu. Maumivu yalikuwa
makali nikajikuta nikitokwa na matusi ya nguoni.
“Nataka uniambie kwa nini unaua?”. Nikamtazama
yule afande kwa hasira.
“Hivi uliniona wakati naua?” Nilimuuliza kwa jazba.
“Afande Edwin naomba hiyo picha!”. Sikushtuka ni
kama niliyetarajia. Ilikuwa ile ile picha ya Merina.
Niliitazama ile picha kwa umakini mkubwa kisha
nikatikisa kichwa.
“Hii picha ni ya nani?” aliniuliza huku akiendelea
kukizunguka kiti changu.
“Ni yangu!”
“Unafanya nini hapo?”
“Nimeshika kisu huku nikiwa na uchungu kwa kifo
kile!”
“Kwa nini uue halafu usikie uchungu!”
“Nasema sijaua!”
“Umesema picha ni yako halafu unasema hujaua
tukuelewe vipi?”
“Hapo nimeshika kisu afande na kama unaitazama
vizuri hiyo picha huo mkono hauonyeshi dalili
yoyote ya kuchomoa au kukandamiza hicho kisu
uwe unatumia akili mambo mengine!” Nilifoka
“pumbavu! umeua hujaua!” Ilikuwa ni sauti kali ya
yule askari aliyeitwa Edwin.
“We huna akili nimeshaongea mara nyingi kuwa
sijaua kwanini uendelee kuniuliza?” Nilimjibu huku
nikiwa na hofu kwani nilimuona akiiendea ile swichi
ambayo inaleta umeme kwenye kile kiti.
Akaiwasha. Siwezi kusimulia kwani sina kitu cha
kufananisha na maumivu niliyoyasikia. Sekunde
ishirini zilikuwa kama siku saba.
“Haya sema umeua hujaua?” alirudia swali.
“Niseme mara ngapi sijaua, ukitaka fanya lolote
lakini ukweli ni huo!” Niliongea kwa kujiamini huku
nikiwa tayari kuendelea na adhabu ile.
“Narudia, umeua hujaua?”
“Kamuulize mama yako!” Niliamua kuongeza jeuri.
“Lete koleo!” Aliagiza Edwin ambaye alikuwa katili
kuliko yule wa kwanza.
Akaubana mdomo wangu kwa mkono wake wa
kulia kisha akaingiza ile koleo mdomoni. Akalibana
jino moja kwa nguvu sana. “naomba uwe mkweli
vinginevyo leo nahamisha meno yote mdomoni
ubaki kama pakacha!”
“Naomba ukubali umeua hujaua!”
Nikakaa kimya nikifikiria ukubwa wa adhabu ya
kung’olewa jino. Usifanye mchezo na polisi, bora
uwasikie redioni tu! Hapo nikawa na mawazo
mengi ajabu. Nilimfikiria sana Ommy. Yuko wapi?
Huko aliko anafanya nini? Hivi alipotea vipi siku ile
ambayo nilitekwa?”
Nikashtuka baada ya kumuona yule askari katili
akichukua bendeji tayari kwa kung’oa jino.
“ Jiandae kuingia kwenye ulimwengu mpya wa
vibogoyo!” Lilikuwa ni tangazo lenye kuleta hasira.
Nikamtazama bila kuongea lolote. Mapigo ya moyo
yalikuwa yameongeza kasi yake, kung’olewa jino
bila ganzi si jambo la mchezo.
Chochote alichotaka kufanya Hakuwahi. Mlango
ukagongwa akasitisha zoezi lake. Akaenda
kufungua mlango.
“Mkuu anamuhitaji mtuhumiwa!” alikuwa ni askari
wa kike ambaye kama wale wengine hakuwa na
sare.
“Bahati yako!” aliongea yule askari katili huku
akionesha wazi kukerwa na wito ule ambao ni wazi
ulikuwa umevuruga burudani yake. Yaani watu
wengine sijui wameumbwaje! Huyu jamaa
nilivyomtazama tu nilijua kuwa matendo yake haya
alikuwa anasikia raha. Bila shaka alikuwa
anavimba kichwa zaidi pale anaposifiwa.
Nilimchukia!
Mpenda sifa!
Nikafunguliwa pale kwenye kiti. Kisha nikafungwa
tena kitambaa usoni. Sijui hata maana ya kitendo
kile, nilikuwa naogopwa tofauti na vile nilivyo.
Lakini sijui kama nilikuwa naogopwa au hawa
jamaa walikuwa wanaigiza. Nilikuwa nashindwa
kuelewa inakuwaje polisi ambaye kasomea kazi
yake ameshindwa kugundua kuwa ile picha
hainihusishi moja kwa moja na mauaji. Kwanini
asiulizwe aliyepiga ilikuwaje akanipiga picha katika
mazingira kama yale halafu asitoe taarifa mapema.
Swali hilo lilinifanya niutilie mashaka uwezo wa
askari wale. Kama uwezo wanao kweli basi
watakuwa wanahusika na wanajua siri yote. Ni
hapa ndipo nilipowaza jinsi ajira ya jeshi la polisi
inavyotolewa. Kwa nini wasichague watu ambao
wana uwezo wa kufikiri? Badala yake kumekuwa
na utaratibu mbovu wa kuwaingiza watoto wa
maafande. Pia upande mwingine nilikuwa
nauchukia huu utaratibu wa kutaka watu warefu
tu! wako watu wengine ni warefu kwa maumbo
lakini akili zao ni fupi. Pia wapo ambao ni kinyume
chake hawa ni wafupi wenye akili ndefu. Si kila kitu
kinahitaji nguvu au mbio! Mambo mengine
yanahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri. Jeshi letu
linakosa watu makini wa kuwahoji wahalifu
kutokana na utaratibu huu mbovu.
“Mwanangu amemaliza…….hana kazi!”
“Mlete kuna nafasi zinatolewa na jeshi la polisi
zitatangazwa wiki ijayo!” Hivi ndivyo walivyopeana.
Tukaingia kwenye chumba kingine kile kitambaa
kikafunguliwa tena. Nilikuwa kwenye chumba
kingine kipana, kizuri. Kwa mandhari ya chumba
kile nafikiri ni ukumbi mdogo wa mikutano. Mbele
yangu kulikuwa na watu wawili ambao
walionekana kunawiri kwa madaraka waliyokuwa
nayo. Mmoja alikuwa mnene huku akiwa na
kitambi kikubwa ambacho kilikuwa kimegusa meza
iliyokuwa mbele yake, alikuwa amevaa sare ya
kipolisi ambayo ilikuwa na nyota tatu begani Yule
mwingine alikuwa na umbo gumu kuelezea kama
ni mnene au mwembamba lakini ilikuwa ni rahisi
kuelezea kimo chake, alikuwa mrefu. Alikuwa
amevaa shati la bluu, suruali nyeusi na viatu
vyeusi. Alikuwa anapendeza sana. Sikuona dalili ya
ukatili kwa mtu huyu ambaye nilihisi kuwa ni
askari. Sikuwa na uhakika lakini kwa kuwa alikuwa
mazingira haya nilihisi ni mmoja wao.
“Samahani bwana Manyika nahitaji kuongea na
huyu mtu Faragha!”
“Usiwe na wasiwasi Mr.Mtuvu Viko vyumba
maalum kwa kazi kama hiyo!” Tukaondoka bila
kufungwa tena kitambaa. Tukaingia kwenye
chumba ambacho kilikuwa na maandishi
MAHOJIANO MAALUM. Tukaingia kwenye chumba
hicho ambacho kilikuwa na viti vinne, meza moja
na mtungi mkubwa wa maua. Ukutani kulikuwa na
picha mbalimbali za wakuu wa jeshi la polisi wa
mikoa mbalimbali na ile ya Rais wa kwanza wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania.
“Naitwa Jerrome Mtuvu, natokea idara ya Usalama
wa Taifa makao makuu, ni mkuu wa kitengo cha
operesheni maalum!" huyu alikuwa anaongea kwa
utulivu mno hali ambayo ilinifanya niwe makini
zaidi.
“Unavuta sigara!” aliniuliza huku akiingiza mkono
mfukoni
“hapana!” Nikamwona anachomoa sigara ambayo
mpaka leo sijaifahamu kwani ilikuwa pana kuliko
zile nilizozoea. Akawasha na kuanza kuvuta.
“Samahani kijana, sina njia nyingine kwani siwezi
kuanza lolote kabla ya kuvuta kidogo.” Akawa
anavuta huku anautazama moshi unavyopotelea
hewani. Huyu alionesha ustaarabu wa hali ya juu
tofauti na matarajio yangu ingawa kitendo chake
cha kuvuta sigara mbele yangu kilinifanya nimtilie
mashaka kidogo.
Mawazo yangu yakarudi kwa Edwin, sijawahi
kuona mtu katili kama yule yaani aning’oe meno
kwa koleo. Duh! angening’oa sijui ningekuwa
mgeni wa nani? Watu wengine wanapenda sifa za
ajabu!” Mawazo yangu yakarudi kwa Betty, ua la
moyo wangu lilikuwa limechanua na kunyauka
ghafla. Ilinitia uchungu sana eti kwa sababu yangu
Betty amekufa. “Usijali mpenzi nitakulipia kisasi
nikishindwa nitakufuata !” Niliwaza.
“Kama sikosei unaitwa Kajuna Kazakamba!”
“Ndiyo”
“tafadhali naomba uwe mkweli naomba unileze
chanzo cha mauaji yote haya!” “Akatulia kidogo na
kunikazia macho. Nikaanza kumsimulia kuanzia
mwanzo hadi mwisho huku nikificha habari za
Ommy!”
“Sawa nimekuelewa kijana, nahitaji kukusaidia,
kwa kuanzia leo nitakutoa hapa polisi lakini
naomba unithibitishie haya ndiyo utakayoeleza
mahakamani?”
“Ndiyo na yako mengi zaidi ambayo nikitoa
ushahidi lazima hawa watu wachukuliwe hatua
kali!”
“Umesema huo mzigo uko wapi?”
” kuna mahali nimeuficha ili uwe ushahidi baadae!”
“Unafikiri utakusaidia vipi huo ushahidi?”
“Utasaidia kufuatilia chanzo cha mauaji kwa kujua
aliyeuwawa alikuwa anaishi wapi nani kanikabidhi
huo mzigo na je kuna alama ya vidole aliacha?”
Akatulia na kuangalia simu yake nikamuona
akibofya bofya. Mara, mlango ukafunguliwa.
Akanishtua yule aliyeingia. Alikuwa ni waziri wa
bunge na usimamizi wa vikao vya serikali.
Alikaa kwenye kiti kivivuvivu baada ya kuhakikisha
mlango umefungwa.
“Vipi mmefikia wapi maana naona mambo yanazidi
kuharibika!”
“Usijali mzee mtaro utafunikwa tu!”
“Umejaa takataka au unataka kuufunika tu!”
“Tena unatakataka za sumu!”
“Duh!” aliguna Mheshimiwa waziri. Kama si kuwa
waziri yale maneno yao yangenitia hofu sana.
“Hivi unafikiri ni ushahidi gani utautoa kuweza
kukuokoa kwenye tuhuma hizi mzito?”
“Ninazo picha za wahusika kwani matukio mengine
nilikuwa napiga picha bila wenyewe kufahamu!”
Niliongopa
“Hizo picha ziko wapi?” Ziko sehemu salama kwani
hakuna anayeweza kuzifikia huko ziliko.”
Nilimuona muheshimiwa waziri akiniangalia kwa
macho yaliyojaa hofu. Nikaanza kumtilia mashaka
mheshimiwa huyu nikaamua kuongezea msumari
wa moto.
“Pia kuna picha nimemuachia mtu fulani ili
aujulishe umma wa Watanzania nini kilitokea
iwapo nitakufa kabla sijapata fursa ya kuweka
mambo bayana.”
Ulikuwa ni msumari wa moto kweli kwani nilianza
kuona kijasho chembamba kikimtoka waziri.
“Unaweza kuwataja baadhi ya hao watu?” Waziri
ambaye alionekanakuchanganyikiwa akalazimika
kuniuliza.
“Wengi wao ni watu maarufu na wazito katika nchi
hii kwa hiyo bora tusubiri mahakamani!”. Sasa
nilipata uhakika waziri hakuwa mtu mzuri kwani
hofu yake ilikuwa bayana. Hata yule aliyejitambulis
ha kuwa ni afisa usalama nilimuona akiwa na hofu
iliyofichika.
Baada ya muda nikaondolewa mle chumbani
nikapelekwa chumba kingine. Nikafungiwa huko.
Ubaya wa jengo hili ilikuwa ni vigumu sana kujua
kama ni usiku au mchana. Ni taa tu ndizo
zilizoniwezesha kuona. Toka niingie kwenye jengo
hili sijawahi kuuona mwanga wa jua. Kwani kila
chumba nilichoingia hakikuwa na madirisha, ni
viyoyozi tu ndivyo vilivyosaidia kuifanya hali ya
hewa iwe mzuri. Mpaka leo ninapoandika huu
mkasa bado sijagundua nilikuwa ndani ya jengo
lipi.
Baada ya kukaa masaa kadhaa mara mlango
ukafunguliwa. Askari wawili wakaingia wakanifunga
tena kitambaa kilekile kisha nikatolewa ndani. Jinsi
tulivyokuwa tunatembea nilijua wazi kuwa tulikuwa
tunashuka kutoka ghorofani. Kama ni msaada
kwanini nifungwe kitambaa usoni, huu usiri ni
wanini? Maswali hayo na mengineyo yaliendelea
kunitesa.
Nikaongozwa kuingia ndani ya gari bila
kufunguliwa kitambaa. Baada ya mwendo wa
masaa kadhaa nikasikia sauti “mfungue!” Ee
bwana eeh! Almanusura nipoteze fahamu kwa
kihoro, huwezi kuamini, nilipofunguliwa kitambaa
nikajikuta nikiwa mbele ya nyumba ile ambayo
nilileta mzigo. Nilichanganyikiwa vibaya! Nilihisi
miguu ikigongana gongana. Mbele yangu
nilimwona yule aliyejitambulisha kwangu kwa jina
la Jerrome Mtuvu akiwa ametangulia. Nyuma
yangu kulikuwa na watu watatu wenye bastola.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA
Nikaongozwa kuingia ndani ya gari bila
kufunguliwa kitambaa. Baada ya mwendo wa
masaa kadhaa nikasikia sauti “mfungue!” Ee
bwana eeh! Almanusura nipoteze fahamu kwa
kihoro, huwezi kuamini, nilipofunguliwa kitambaa
nikajikuta nikiwa mbele ya nyumba ile ambayo
nilileta mzigo. Nilichanganyikiwa vibaya! Nilihisi
miguu ikigongana gongana. Mbele yangu
nilimwona yule aliyejitambulisha kwangu kwa jina
la Jerrome Mtuvu akiwa ametangulia. Nyuma
yangu kulikuwa na watu watatu wenye bastola.
Nikageuka! Duh, kama kuna siku nilitamani sana
ardhi inimeze nididimie basi ni siku hii. Nyuma
yangu kulikuwa na watu wa mwisho kabisa ambao
nilitamani kukutana nao katika Maisha yangu.
Nilimwona yule mtu mwenye kila dalili ya muuaji
mzoefu yaani Martin, hakuwa Martin mwingine ni
bali yuleyule aliyenikabidhi mzigo kule Mwanza,
katikati alikuwa ni yule askari alieuwa askari
wengine kule Muhimbili ‘askari feki’ na mwisho
kabisa alikuwa yule jamaa aliyenipiga picha kule
Tabata. Sikuona dalili yoyote ya kunusurika safari
hii. Nilikuwa katika mikono ya kifo. Ommy hayupo,
nashukuru sikumtaja mbele ya yule mnafiki
aliyekuwa ananihoji. Eti Jerrome Mtuvu afisa wa
idara ya usalama wa Taifa kitengo cha Operesheni
maalum, mpumbavu mkubwa. Waombe Mungu
nisiwatie mikononi. Sina bunduki lakini hata
upanga au kisu nitashindwa kutumia? Lakini sijui
kama nitatoka hai hapa
8
Niliingizwa kwenye chumba kizuri ambacho
kilikuwa na kila kitu muhimu kwa matumizi ya
binadamu ndani. Kuta zake zilikuwa zimepakwa
rangi ya maziwa huku kwa chini kukiwa na ufito
wa rangi ya udongo. Kulikuwa na kabati kubwa
lililotengenezwa kwa alminium kabati hili liliwekwa
karibu kabisa na mlango. Kwenye kona nyingine ya
chumba hiki kulikuwa na Jokofu zuri refu la rangi
ya fedha.
Nilifungua friji nikakuta matunda, juisi, mikate na
vitu tofauti. Sikutaka kujiuliza nikaanza
kuishambulia milo mbalimbali ambayo ilikuwa
ndani ya lile friji. Nilipohakikisha kuwa nimeshiba
nikaanza kukagua chumba kile kama kuna
uwezekano wa kutoka. Nikagundua kuwa
uwezekano ulikuwa mdogo. Mbaya zaidi kama
ningekutana na walinzi ningepambana nao vipi?
Ukubwa wa hatari iliyopo mbele yangu nilikuja
kuuona baada ya kugundua kuwa kuna kiongozi
mkubwa anahusika. Waziri! Waziri na viungo vya
albino wapi na wapi! Hili la waziri kuhusiana na
hawa watu lilinichanganya sana. Mwanzo wakati
anaongea na yule mnafiki Jerrome alikuwa
anaongea mafumbo ambayo nilishindwa kuyatafsiri
kwa sababu ilikuwa ni vigumu kuamini kama waziri
ambaye yuko mstari wa mbele kutetea maslahi ya
wananchi anaweza kufanya mambo ya ajabu
namna ile. Sasa huyu naona anafaa kuitwa
mnafiki. Ndiyo huyu ni mnafiki kamili, halafu yule
Jerry.. Yule…yule ah! Atabaki kuwa Jerry afisa
usalama wa kughushi. Hivi yule anapoomba kura
huwa anatumia maneno gani kuwashawishi wapiga
kura? Ni yeye huyu ambaye hutoa hutuba za
kusisimua akiwasisitizia wabunge jinsi serikali
itakavyopambana na majanga mbalimbali likiwemo
la mauaji ya Albino, Mnafiki mkubwa kabisa.
“Lakini kwa nini hawa watu wamekuwa wakarimu
kwangu? Au ndiyo maisha ya binadamu na mbuzi?
Atamtafutia majani kokote yaliko lakini mwisho wa
siku ni kitoweo, lazima atamchinja tu.
Nikapata wazo! Ilikuwa ni lazima nifanye kitu la
sivyo siwezi kuokoka. Nikatabasamu, lilikuwa wazo
zuri ajabu! Unajua mawazo mengine yanakuja
katika wakati ambao ni muhimu mno. Hapa lazima
nikiri kuwa mambo mengine huwa ni msaada wa
Mungu. “Ahimidiwe Bwana, Bwana wa mbingu na
ardhi. Unastahili sifa ee Mola wetu….” Nilikuwa
namtukuza Mungu wangu kwa nguvu zote lakini
moyoni nikiwa na lengo la kumbembeleza Mola
wangu anipe mbinu zaidi. Kipindi hiki cha matatizo
nilijikuta nikimuweka karibu sana Mungu lakini
kabla ya hapo nyumba za ibada kwangu zilikuwa
kama kituo cha polisi.
Nilifungua friji nikatoa chupa ambayo ilikuwa na
kinywaji ambacho sikukifahamu. Sikuwa na muda
wa kusoma maandishi ya chupa ile. Nikakipiga
chini kikapasuka. Nikashika kile kipande cha chupa
ambacho kilibaki mkononi. Moyo ulikuwa unaenda
mbio sikuwa na uhakika kama mbinu nilizokuwa
nazifikiria kwa wakati huo ni sahihi. Nikapanda
dirishani, mikono yangu ilikuwa imefikia kwenye
ubao wa dari ‘ceilingboard’ nikaanza kujaribu
kupapatua. Kazi ilikuwa ngumu kwa sababu
nilikuwa na kazi mbili mkono mmoja ulikuwa
umeshika dari huku mwingine nikijaribu kuharibu
ubao ule.
Nilishindwa kabisa kufanikisha zoezi langu.
Nilianza kufikiria mbinu za ziada za kufanikisha
nafasi ile ya mwisho kwangu kuweza kujiokoa.
“Nimekwisha!” Niliwaza. Wakati nikiendelea
kuwaza nitaifikia vipi ile dari nikasikia mlio wa
viatu. Kuna mtu alikuwa anakuja. Kama alikuwa
anakuja kwangu basi nilikuwa sina la kufanya.
Nilisikia uchungu sana, nilijua wazi kuwa iwapo
hawa jamaa wataniua basi maiti yangu
isingeonekana tena. Nilihuzunika sana, nilimfikiria
zaidi mama yangu. Angejisikiaje kuishi bila kujua
kama mwanae niko hai au nimekufa. “Eeee, Mungu
nisaidie na uniokoe mja wako mkosefu!” Niliwaza.
Kumbe yule mtu alikuwa anapita, bila shaka
alikuwa anakagua usalama mle ndani. Nikashusha
pumzi. Ilimradi nilikuwa natapatapa kutafuta
namna ya kujiokoa.
Nikapata wazo jingine, nikazima swichi inayopeleka
umeme kwenye friji. Nikalisogeza friji karibu na
dirisha. Nikapanda juu ya friji. Nikaigusa vizuri ile
‘ceilingboard’ nikaisukuma kwa nguvu. Nikahisi
misumari inaanza kuachia mbao ndogondogo
zilizoshikia ubao ule. ‘Ta! ta! ta……’ Nilikuwa
nasikia raha misumari ilipokuwa inatoa sauti ya
kujiachia.
Ghafla! Nikasikia hatua za mtu aliyevaa buti zikija
kule nilikokuwa nimefungiwa. Nikaruka haraka juu
ya friji, kwa kuwa sikuvaa viatu sikutoa kishindo
ambacho kingemshtua yeyote aliyeko nje.
Mlango ukafunguliwa. Alikuwa ni Martin, Martin
muuaji, Martin ambaye kanipa mzigo unaonitesa
mpaka leo. Viungo vya albino! Tena huku
akisisitiza safari hii nimepata mzigo safi kutoka
Mwadui, huyu ni zaidi ya mnyama. “Mungu wangu!
Sijui itakuwaje akiona sehemu ya dari ambayo
imepapatuliwa.” Niliwaza huku nikiwa na hofu
kubwa sana. Sikupenda kabisa yule ibilisi agundue
kilichofanyika.
“Na hii friji imefuata nini huku?” aliongea Martin
kwa hasira.
“Angalia bwana mdogo ujanja wowote utakaojaribu
ujue unaharakisha kifo chako.” Akasogeza lile friji
mahali pake. Mungu mkubwa, hakuinua macho
kutazama juu. Akafunga mlango kwa funguo.
Nikashusha pumzi kwa nguvu zaidi kuliko mwanzo.
Sauti ya viatu vyake ikapotea masikioni mwangu,
nikajua ameshafika mbali. Nikaanza tena harakati
zangu za kujinusuru
Sikuwa na muda wa kupoteza, nikapanda kwenye
ukingo wa dirisha kisha nikasukuma kwa juu ile
sehemu ya ubao ambayo bado ilikuwa
imeng’ang’ania pale kwenye dari. Nikashuka chini
nikachukua kipande cha chupa ambayo niliipasua
nikakiweka mfuko wa nyuma wa suruali yangu ya
‘jeans’. Nikavua fulana yangu nyeusi ambayo
ilikuwa inanuka kutokana na kutofanyiwa usafi siku
nyingi. Kwa ujumla nguo zangu zote zilikuwa
zinanuka. Sikumbuki ni lini nilioga au kufua nguo
zangu. Hata kama kile chumba kilikuwa na bafu
lakini sikujisikia kabisa kuoga.
Nikapanda kule darini, Oh! nashukuru Mungu
ingawa kulikuwa na ukuta lakini ukuta ule
ulitenganisha vyumba vya upande wa kulia na
kushoto tu. Hivyo niliweza kutembea upande huu
wa kulia kadri ya uwezo wangu.
Kule juu nilikuwa kama kipofu kutokana na giza,
nilikuwa nimeshaamua kujaribu bahati yangu kwani
kuendelea kukaa pale na kusubiri kitu ambacho
sikijui ni wehu kamili.
Baada ya hatua kadhaa kule juu nikafika sehemu
ambayo niliweza kusikia kilio cha mtu kwa chini,
nahisi nilikuwa kwenye usawa wa chumba kingine.
“Mhh! mmh! mmh!.....” kilikuwa kilio cha mtu
ambaye ni wazi alikuwa anaugulia maumivu.
Nikakanyaga kwa nguvu sehemu ile ya dari.
Pakabomoka bila utaratibu. Nikaangukia chumbani
huku nikifanya kishindo ambacho kingemshtua
yeyote aliyeko nje ya chumba hicho. Chumba
kilikuwa na giza ingawa niliweza kukiona kitanda
kikiwa na mtu ambaye sikuweza kumtambua.
“kuna nini tena!” nilisikia sauti kutoka nje ya
chumba. Nikasikia funguo zikiingizwa kwenye
tundu la kitasa. Sikuwa na muda wa kujiuliza nini
cha kufanya nilikuwa nimeshayakoroga ilikuwa
lazima niyanywe. Nikajibanza kando ya ule mlango,
nikachomoa kile kipande cha chupa. Moyo wa
ujasiri ulikuwa umeniingia. Naomba nieleze wazi
kuwa muda huu nilimkumbuka sana Betty, hivyo
hasira zilizidi. Ilikuwa ni fursa yangu ya kumlipizia
kisasi. Nilishaamua kuingia kwenye mchezo wa
kifo. Ilikuwa ama zangu ama zao.
Alipofungua mlango akawa anaenda upande
ambao ulikuwa na swichi, sijui ujasiri ulitoka wapi
nilijikuta nikimrukia na kuanza kudidimiza kile
chupa kooni kwake.Haikuwa rahisi kama
nilivyofikiri, Jamaa alikuwa na nguvu kwelikweli
hakukubali kufa kikondoo. Ingawa kulikuwa na giza
lakini niligundua alichotaka kufanya. Alikuwa
anaingiza mkono mfukoni ili atoe bastola. Ajabu!
Nikamuona analegea na kuanguka chini kabla ya
kutoa bastola yake.
Nikawasha taa. Duh! Ile chupa hatari kweli, yaani
damu zilizomwagika pale sakafuni huwezi kuamini.
Alikuwa maiti!. Nikatabasamu kabla ya kukigeukia
kitanda. Kama ungeniona wakati huo lazima
ungekimbia nilikuwa nanuka damu, hofu ilikuwa
imenikimbia kabisa sikuwa kajuna wa kawaida.
Sura na moyo wangu vilivaa kwa muda vazi la
ukatili na hasira.
Nilipigwa na butwaa pale nilipoangalia kitandani.
Mwanamke alikuwa amelazwa kitandani huku
akiwa amefungwa mikono na miguu. Kikubwa
kilichonishtua nilifikiri ni Mchina lakini
nilipomwangalia vizuri zaidi ndipo nilipogundua
kuwa ni mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi
yaani albino. Duh huu sasa unyama yaani binti
nzuri kama huyu amehifadhiwa kama bidhaa ya
dukani. Roho iliniuma sana.
“Hawa watu sijui wana roho za aina gani?”
nilijiuliza huku nikimwangalia kwa makini
mwanamke yule ambaye kama angekuwa anasoma
basi angekuwa mwaka wa kwanza au wapili chuo
kikuu yaani bado alikuwa mbichi. Alikuwa
amefungwa plasta mdomoni, bila shaka
hawakutaka apige kelele. Sikutaka kuanza na huyu
mwanamke, nikarudi kule kwa yule jamaa
aliyeanguka. Kiunoni alikuwa na kisu kikubwa
chenye mpini mweusi, nikakichukua kile kisu na
bastola ambayo ilikuwa kwenye mfuko wa kushoto
wa suruali yake. Nilikitazama mara mbili kile kisu
ama kwa hakika kilifanana sana na kile kisu
kilichotumika kufanyia mauaji ya Merina kule
Tabata. Kisu kilinirudishia tena kumbukumbu ya lile
tukio, kwa dakika kadhaa nilikuwa nimeduwaa
nikikikodolea macho kile kisu.
Nikamgeukia yule binti albino aliyelala kitandani.
Nikamfungua kamba alizokuwa amefungwa kisha
nikatoa ile plasta aliyofungwa mdomoni.
“Niacheee!” alianza kufoka kwa sauti kali na ya
hofu.
“Shiiiiiiiii!” nikaweka kidole cha shahada katikati ya
mdomo kumuashiria anyamaze. Akanirushia ngumi
nikawahi kuudaka mkono wake.
“Una kichaa wee mwanamke!” Nilimfokea. Kidogo
nikamuona ametulia alianza kunielewa.
“Vipi Dula mbona unachelewa!” sauti kutoka nje
ilinizindua na kunifanya nijiweke tayari.
Nikamuashiria mwanamke akae kitandani.
Nikaruka kidimbwi cha damu nikaenda kusimama
palepale niliposimama mwanzo. Akafungua
mlango, akaingia. “Aah! We mwanamke,
umemfanya nini Dula!” alifoka bila kufikiria huku
akichomoa bastola yake kijingajinga. Hakuwahi!
nilimrukia nikapitisha kisu katikati ya shingo yake,
nikakata kwa nguvu zangu zote koo lake,
akatapatapa hadi alipokata roho. Chumba kilikuwa
kinanuka damu.
“Wewe nani?!’’ aliniuliza yule mwanamke kwa
mshangao uliochanganyika na woga. Kwanza
sikumjibu nikachomoa kile kisu kutoka katika mwili
wa yule jamaa. Nikafuta damu kwa kutumia suruali
yake kisha nikamgeukia yule mwanamke.
“Naitwa Kajuna sijui wewe unaitwa nani?”
“Johari, na umefikaje huku?”
“Sikiliza Johari hatuna muda wa kuendelea
kuulizana hili na lile la msingi ni kutafuta namna
ya kutoka humu ndani!”
“Mimi sitaki kutoka humu ndani!”
“Kwa nini!”
“Maisha yangu yamekosa thamani halisi nimekuwa
kama bidhaa kila ninakoenda naitwa dili bora nife
kuliko kuishi kwa mashaka!”
“hapana Johari yatupasa kuondoka, bado kuna
watu wana roho nyeupe tena nyeupe kama theluji
wanakuhitaji”
“Hapana Kajuna nashukuru kwa kunijali lakini
naomba uniache, waje wanichinje wanifanyie kafara
sijui madudu gani niache……..” alianza kulia huku
akiwa hataki kabisa kujaribu bahati ile ya kujiokoa.
“Lakini kwa nini unakuwa mbishi we mwanamke!”
“Kama baba yangu mzazi amethubutu kuniuza kwa
hawa jamaa unafikiri nani atanithamini!”
“Mwanamke twende utakufa hayo maneno
tutayachambua baadae!”
Bado alikuwa na msimamo wa kutaka kufa,
alinishangaza na kuniacha kinywa wazi.
Ghafla! Nikasikia honi ya gari kutoka nje.

ITAENDELEA
 
bw Willy Gamba 1 huyu mtunzi wa riwaya hii uliyemtaja sio mtunzi halisi. bora usimtaje kabisa kuliko kutaja mtu asitye mwandishi. namfahamu mwandishi na nawasiliana nae kuona kama kazi yake imeibwa na huyu aitwae Ahmad Mniachi
 
Last edited by a moderator:
bw Willy Gamba 1 huyu mtunzi wa riwaya hii uliyemtaja sio mtunzi halisi. bora usimtaje kabisa kuliko kutaja mtu asitye mwandishi. namfahamu mwandishi na nawasiliana nae kuona kama kazi yake imeibwa na huyu aitwae Ahmad Mniachi

mkuu mimi nimeleta kadri ilivyo na utakuwa unanionea kunilaumu mimi sababu hata mimi nimekuta imeandikwa hivyo
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA KUMI NA SABA

“Hapana Kajuna nashukuru kwa kunijali lakini
naomba uniache, waje wanichinje wanifanyie kafara
sijui madudu gani niache……..” alianza kulia huku
akiwa hataki kabisa kujaribu bahati ile ya kujiokoa.
“Lakini kwa nini unakuwa mbishi we mwanamke!”
“Kama baba yangu mzazi amethubutu kuniuza kwa
hawa jamaa unafikiri nani atanithamini!”
“Mwanamke twende utakufa hayo maneno
tutayachambua baadae!”
Bado alikuwa na msimamo wa kutaka kufa,
alinishangaza na kuniacha kinywa wazi.
Ghafla! Nikasikia honi ya gari kutoka nje.
“Twende!” akakataa. Sikuwa na muda wa kupoteza
nikampiga kofi kali la shavu, akayumba
nakuangukia kitandani.
“Pumbavu twende!” Nilifoka huku nikimuongezea
ngumi ambayo ilimuangushia tena kitandani pale
alipojaribu kuinuka. Nikamwonesha kile kisu
ambacho dakika chache zilizopita nilikitumia kwa
mauaji, akashtuka hakutegemea kama nitachukua
hatua kali namna ile. Nilikuwa nimebadilika
nilikuwa Kajuna Mwingine kabisa.
“Nimesema twende!” Alikuwa hana hiyari zaidi ya
kunifuata. Nilimshika mkono nikaanza kukimbia
kuelekea mlangoni.
Nasema hakuwa na hiyari, naye alikuwa anakimbia
kunifuata kwani nilimshika kwa nguvu ili asije
akaleta tena upuuzi wake. Nikamuona mlinzi
anahangaika kufungua komeo ambalo lilikuwa
limeshikia lango, bado honi zilikuwa zinapigwa.
Sikutaka kupoteza muda niliuacha mkono wa
Johari nikakimbia kwa kasi. Laiti ungebahatika
kuniona jinsi nilivyokuwa nakimbia usingeweza
kunitofautisha na mtu anayeshiriki mashindano ya
mbio za mita mia moja. Kwa kuwa nilikuwa sijavaa
viatu na ule mngurumo wa gari vikamfanya mlinzi
ashindwe kugundua kuwa kuna mtu alikuwa
anamfuata. Nilipomkaribia alikuwa anataka
kufungua komeo la mwisho. Hakuwahi!
Nikamrukia, tukapiga mwereka mzito akataka
kupiga yowe, alichelewa! Nilididimiza kisu kile
kikubwa katikati ya mdomo wake kikatokea nyuma
ya shingo yake. Nilikuwa nimekata mawasiliano
yake ya sauti. Nikamwacha akigaagaa kupigania
roho yake. Nikakiingiza kisu mfuko wa nyuma wa
suruali yangu. Nikarudi kwa Johari nikamshika
mkono tukawa tunakimbia kuelekea nyuma ya
nyumba ile. Hakukuwa na mlango.
Ukuta haukuwa mrefu lakini nilijua wazi kuwa
Johari hawezi kupanda ule ukuta. Kwa ujasiri wa
ajabu nikamweka Johari mgongoni.
“Nishike vizuri!” nilimwamrisha. Kwa jinsi
nilivyokuwa mkali na alivyo nishuhudia nikiuwa
watu alijua sitaki mchezo hivyo hakuleta ubishi.
Alijishikia vizuri mgongoni kwangu nikaruka na
kudaka juu kwenye matofali. Kwa kutumia nguvu
zangu zote nikajivuta hadi juu ya ukuta. Kisha
nikaangukia upande wa pili. Nyuma ya ule ukuta
kulikuwa na nyumba nyingi ambazo ujenzi wake
ulikuwa haujakamilika. Eneo hili lilikuwa na
nyumba chache ambazo zilikuwa zinaishi watu.
Kwa kuwa giza lilikuwa limeingia sikupata hofu ya
kukamatwa. Johari hakuwa na nguvu ya kukimbia
nikambeba kwa mikono miwili. Alikuwa kimya
akisubiri hatma yake.
Huku ni kiwa na kile kisu chenye damu nikaingia
kwenye jengo moja ambalo lilikuwa halijamalizika
ujenzi wake.
“Mwanamke! Tulia hapa.”Niliongea kwa ukali.
Nikamwacha Johari mle ndani. Nikarudi kule
nilikotoka. Nikaenda mbele ambako kulikuwa na lile
lango lakuingilia. Nikajificha kwenye kichaka. Bado
lile gari lilikuwa linapiga honi kwa fujo. Angefungua
nani? mlinzi alikuwa amekufa. Nikasikia sauti ya
hatua za miguu ya mtu aliyekuwa anakimbia
kuelekea getini.
“Mungu wangu, nani kafanya huu ushenzi?”
Nilimsikia huyo mtu akiropoka kwa kihoro bila
shaka baada ya kuiona maiti ya yule mlinzi. Bado
yule mtu hakutosheka na mshtuko huo akaendelea
kumimina matusi mazito ya kulaani kitendo kile.
Nikashuhudia lango likifunguliwa. Gari likataka
kuingia halafu nikaona dereva anasita na kurudi
nyuma. Wanaume wanne wakashuka kutoka
kwenye ile Rav4, wote walionekana watu ambao
wamenawiri kwa fedha. Sikumtambua hata mmoja
zaidi ya Bonge. Walikuwa wamebaki vinywa wazi.
“Nini kinaendelea hapa!” aliuliza Bonge kwa
mshtuko.
“Yule mshenzi amemuua Dula na Suma huko ndani
halafu amemalizia na huyu Peter!” “yuko wapi
alifoka Bonge akiwa ameanza kuingia ndani!”
“Ametoroka! Tena ametoroka na ile mali yetu
mpya!”
Jinsi jamaa walivyoshtuka huwezi kuamini. Kama
wangenikamata muda ule nafikiri kulikuwa hakuna
mjadala tena.
“Dawa ya muheshimiwa waziri ishatengenezwa?”
alihoji mmoja.
“Hapana mkuu ilikuwa yule binti achinjwe leo usiku
lakini keshatoroshwa sijui itakuwaje!”
“hii damu ni mbichi sana inaonesha tukio si la
muda mrefu msake mpaka umpate!” Ilikuwa ni
amri kali. Wakaingia ndani huku wakiongea
maneno ambayo sikuweza kuyasikia vizuri. Mungu
mkubwa, jinsi jamaa walivyo kuwa
wamechanganyikiwa inafurahisha. Waliingia ndani
wakasahau kufunga milango ya lile gari.
Nikazunguka nyuma haraka. Nikambeba tena
Johari , sikuwa na uhakika kama ninaweza kuwahi
kabla hawajafika. Nikiwa nimembeba Johari
mikononi nikamwingiza ndani ya lile gari. Sikuwa
na leseni ya udereva lakini nilikuwa naweza
kuendesha kwani mara mojamoja rafiki yangu
Salumu Kapirimba rafiki yangu niliyesoma naye
sekondari alinifundisha.
Nikawa nahangaika kutaka kuwasha. Huku
nikitetemeka nikawasikia jamaa wakitembea kwa
kasi kuja liliko gari. Hofu ilianza kunitawala upya.
Upande fulani nilianza kujilaumu kwanini nilikuja
huku kwenye gari wakati sina taaluma ya udereva.
“Mtafuteni haraka!” Nilisikia sauti ya Bonge
akiendelea kufoka. Gari lilikuwa linakataa kuwaka.
Mungu wangu! Johari ambaye alikuwa upande wa
kulia aliinuka na kunipa ishara ya kutaka nimpishe.
Sikufanya ubishi nikampisha. Nikaishika vizuri
bastola yangu. Nilikuwa sijawahi kutumia bastola,
lakini kwa uzoefu wa kuangalia filamu mbalimbali
sikuwa na wasiwasi wa nini cha kufanya.
Nikafyatua kitunza usalama cha bastola ile. Johari
alikuwa ameiwasha gari. Kwa kuwa lango lilikuwa
halijafungwa nikawaona wale jamaa wakija kwa
kasi kulifuata lile gari. Sikutaka kuchelewa
nikaishika vizuri bastola. Kutokana na giza
hawakuweza kuniona vizuri. Nikalenga shabaha
katika kifua cha bonge nikaifyatua. Mlipuko
mkubwa ukawashtua majirani.
Wale watu wakapatwa na kihoro baada ya
kumuona Bonge akirushwa juu na kuanguka chini
baada ya kumpata risasi ile. Alikuwa ameanguka
kama mzigo. Sikuwa na uhakika kama alikufa au
alikuwa mzima. Nikatabasamu baada ya kumuona
Johari akiirudisha ‘rivasi’ gari ile. Kisha akaiondoa
kwa kasi. Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika
kwani tulishambuliwa kwa risasi mfululizo. Hata
hivyo Mungu alikuwa upande wetu. Tukatoka
salama na kuingia barabarani. Gari lilikuwa
linaendeshwa kwa kasi ambayo sikuitarajia.
“Kumbe unaweza gari!” Nilimsemesha Johari
ambaye muda wote alikuwa kimya.Akatabasamu,
kisha akacheka na kuruhusu mwanya wake
kuonekana. Alipokuwa anacheka mashavu yaliweka
vishimo vidogo vilivyovutia sana. Hapo nikagundua
kuwa Johari alikuwa mwanamke mrembo. Sura
yake kidogo ilinifanya nisahau kama nipo kwenye
wakati mgumu. Nilisahau kabisa kuwa nina kisu
chenye damu huku nikiwa nimeshika bastola
mkononi.
“Please hide your pistol!” Johari alinishtua.
Nikaweka bastola mfukoni.
Kitendo cha Johari kutabasamu na kuanza kuongea
kilinipa nguvu na faraja kubwa sana. Angalau nusu
ya upweke niliokuwa nao ilianza kupotea. Nilikuwa
na shauku kubwa ya kujua aliyomsibu Johari lakini
haukuwa muda muafaka. Niliendelea kumkazia
macho huku nikistaajabia uzuri wake.
***

Tukaitelekeza gari kituo cha magari cha Temeke
mwisho, kwani inavyoonesha hawa jamaa
walikuwa na mtandao mpana hivyo nilihofu kama
tutaendelea kuitumia tungekutana na askari wa
usalama barabarani ambao wangetukamata na
kuturudisha katika mikono yao. Sikupenda hilo
litokee!
Kama niliyeota dakika chache baadaye nilianza
kusikia ving’ora vya gari la polisi vikija maeneo
yale.
“Giza lishaingia gari nishaitelekeza kwa leo
hawanipati abadani!” Niliwaza baada ya kuhisi
kuwa huenda hao polisi wamepewa taarifa zangu
hivyo wananitafuta.
Tulitembea kwa miguu huku nikiwa sina shati wala
viatu miguuni. Watu walikuwa wanatushangaa
sana. Tulijitahidi kupita vichochoro ambavyo
havikuwa na watu wengi hadi tulipotokea maeneo
ya Abiola. Ili kuogopa usumbufu nikaamua kupita
nyuma ya kituo cha Polisi. Hatimaye nikatokea
nyumbani kwa Ommy. Nilikuwa natamani sana
kuonana na Ommy ili anijulishe kile kilichojiri siku
ya mwisho ambayo nilijikuta hospitali. Licha ya
kutaka kujua Ommy ndiye pekee niliyemuona kuwa
mshirika wangu wa karibu kwenye matatizo yale.
Angekuwa mtu mwingine siku niliyomueleza kuhusu
mzigo wa almasi pengine angeweza hata kuniua
kwa tamaa ya utajiri wa haraka. Ommy alikuwa
mtu na pia utu alikuwa nao.
***

Hali ya nyumbani kwa Ommy kidogo ilinitia
mashaka. Nyumba ilionekana kupooza. Ilikuwa
kama gofu, hakukuwa na dalili zozote za uhai
kwenye nyumba ile. Hali ile ilinishangaza sana,
haikuwa dalili nzuri kwangu kwani ilimaanisha
kuwa Ommy ana siku nyingi hajalala pale ndani.
Kwa kuwa pale tulipokuwa tunauficha ufunguo
nilipafahamu vizuri sikupata shida. Niliinua lile
tofali, nilishangaa kuuona ufunguo ukiwa na kutu.
Hii ilimaanisha kuwa Ommy alikuwa na siku nyingi
zaidi ya vile nilivyofikiri hajakanyaga pale
nyumbani. Nikafungua mlango na kuingia ndani.
Ndani hakukuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya
vumbi na buibui ambao walishageuza kuta za
nyumba ile kuwa makazi yao ya kudumu.
“kimetokea nini?!?” nilijiuliza kwa mshangao.
Nilianza kurudiwa na huzuni ambayo ilishapotea.
Yuko hai kweli?
Nikaingia kwenye chumba changu. Nikafungua
mfuko mdogo wa begi langu, “uhuuuu!”
Nikashusha pumzi baada ya kuziona zile fedha
nilizokuwa nimezihifadhi zikiwa salama. Sikuwa na
haja ya kuzihesabu kwani hata kama zingepungua
ningemuuliza nani? Niliacha laki sita na elfu
hamsini. Niliporudi sebuleni nikamkuta Johari
akiwa amekaa kwenye sofa. Alikuwa amechoka
sana.
“Utahitaji kuoga?” aliitikia kwa kichwa. Nikaangalia
kwenye ndoo zote zilikuwa na maji kama
tulivyoacha mara ya mwisho.
“Mh! Hii hatari sana ina maana Ommy akurudi
tena nyumbani.” Nikakagua vitu vingi mle ndani
vilikuwa kama tulivyoacha mara ya mwisho. Katika
vitu ambavyo sikutamani kusikia muda ule ni kifo
cha Ommy. Moyo ulikuwa unaenda kasi ajabu!
Nikamwekea Johari maji bafuni akaenda kuoga.
Wakati yuko bafuni ndipo nikakumbuka kuwa
mfukoni kuna kisu chenye damu. Nikakitoa mfukoni
na kukiweka pale mezani. Nikaiangalia vizuri ile
bastola. Sikuwa mtaalamu wa mambo ya silaha
hivyo sikuweza kujua ni bastola ya aina gani na
inatoka nchi gani, labda angekuwepo Ommy.
Nikakumbuka kitu, nikaenda kwenye chumba cha
Ommy. Kama nilivyotegemea, nikalikuta begi
ambalo lilikuwa na viungo vya albino likiwa juu ya
Meza ndogo. Juu ya lile begi kulikuwa na barua.
Bila shaka ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Ommy.
Nikatabasamu, angalau nilianza kufarijika kidogo
baada ya kuuona ujumbe ule. Nilikuwa na
matumaini angalau ya kupata taarifa kuwa Ommy
katoroka au vinginevyo na si kifo chake.

9
Nilikagua tena lile begi, nikashangaa kuona vile
viungo vya albino havijaharibika. Nilipoangalia
vizuri nikagundua kuwa kuna dawa maalum ilikuwa
imewekwa. Kumbe ndio maana nilisafiri na mzigo
huu bila kusikia harufu. Nikachukua ile barua
iliyoachwa na Ommy nikaiweka mfukoni. Sikutaka
Johari alione lile begi nilihofu angeweza kujisikia
vibaya kisha akarudia ule msimamo wake wa
awali. Nikalifunga vizuri nikaliweka uvunguni mwa
kitanda.
Nikarudi sebuleni nikamkuta Johari akiwa amekaa
pale kwenye sofa. Alikuwa amevaa nguo zake
zilezile. Alikuwa amevaa blauzi ya rangi ya kijani
na sketi ndefu ya kijivu. Nywele zake zilikuwa
zimetunzwa vizuri kiasi cha kunishangaza kwani
mazingira tuliyokutana nilitegemea nywele zake
zingekuwa hovyo hovyo. Kabla sijaanza kumuhoji
lolote nikaamua kuanza kusoma barua ya Ommy.
Rafiki yangu mpendwa;
Naandika barua hii nikiwa sina uhakika kama
tutakuja kuonana tena, kama tutaonana basi
itakuwa ni heri kubwa na iwapo hatutaonana basi
naomba Mungu atukutanishe katika kivuli cha
wapenda haki huko mbinguni. Siku zote nimekuwa
nikikuthamini kwa kuwa nimekuona ni rafiki
mwema na mpenda haki, Mungu akubariki kwa
hilo. Ninaandika nikiwa sina uhakika kama
utaisoma barua hii! Sina uhakika kama bado uko
hai au umekufa. Kama umekufa naamini Mungu
ataufikisha ujumbe huu huko uliko kwenye
mapumziko ya milele. Kajuna ulikuja kwangu kama
mzaha nami nikakupokea lakini kupitia kwako
yamekuja bainika mambo mazito sana.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA NANE

. Ninaandika nikiwa sina uhakika kama utaisoma
barua hii! Sina uhakika kama bado uko hai au
umekufa. Kama umekufa naamini Mungu
ataufikisha ujumbe huu huko uliko kwenye
mapumziko ya milele. Kajuna ulikuja kwangu kama
mzaha nami nikakupokea lakini kupitia kwako
yamekuja bainika mambo mazito sana. Lengo la
ujumbe wangu huu ni kukusimulia kwanza jinsi
tulivyoachana siku ile. Nilikuwa nawasiwasi huenda
ukafikiri kuwa nilikusaliti, haikuwa hivyo kajuna.
Wakati wewe unaingia ndani nikawaona watu
wenye bastola wakikufuatilia. Nikaamua kutoka
kwenye yale maficho yangu kisha nikawafuata
taratibu hadi ulipotekwa ukaingizwa kwenye lile
gari. Gari ilipokuwa inaelekea Tandika ndipo
nikaigonga na kusababisha ile ajali iliyotokea.
Kumbe wale washenzi walisoma namba za gari
langu wakawa wananifuatilia nyendo zangu. Nami
nikawa nafuatilia nyendo zao. Nimegundua mambo
mengi sana mojawapo ni kuhusika kwa baadhi ya
vigogo kwenye ushirikina mkubwa wa viungo vya
albino. Tafadhali naomba uwe makini na sehemu
hii: Wanaohusika ni baadhi ya wabunge kwa
sababu za kisiasa, wavuvi na wafanyabiashara
wakubwa. Kiongozi wao ni mheshimiwa Stefano
Kenge waziri wa bunge na usimamizi wa vikao vya
serikali, pia naomba ufahamu kuwa yule Bonge
ndiye Samson Kipusa mfanyabiashara mkubwa wa
madini ambaye pia ana tuhuma mbalimbali za
ujambazi. Uwezo wangu wa kuchunguza umeishia
hapo lakini sina uhakika na uhai wangu na wako
lakini napenda kukuahidi kuwa sitarudi nyuma.
Kama watakuuwa nitalipa kisasi, na kama
wataniua naomba upambane hadi tone la mwisho.
Najua unaweza kufikiri kuwa ni kazi kubwa lakini
nakuhakikishia kuwa Mungu yuko pamoja nasi.
Kama mungu atatukutanisha tutaongea mengi
sana.Mwisho naomba uchukue namba hii 0756
465 265, hii ni namba ya mtu ambaye nahisi
atakusaidia sana anaitwa Jerrome Mtuvu. ALUTA
KONTINUA.
Hayo ndiyo maneno ya mwisho kwenye barua hiyo.
Maneno hayo yalinitia simanzi . Nikainamisha
kichwa chini huku nikifikiria upya kuhusu Ommy,
mtu ambaye ameamua kuutoa moyo wake
kupigania maslahi ya wengine. Nilimfananisha na
wanamapinduzi mbalimbali wa Afrika kama Kwame
Nkurumah wa Ghana na Samora Machel wa
msumbiji. Tuna watu wachache sana wa aina hii
katika kizazi chetu cha sasa. Hakuna wazalendo
wa kweli na hawatatokea tena. Nani atakuwa
tayari kuipigania nchi iliyojaa dhuluma na ufisadi?
Nani yuko tayari kwenda kutoa taarifa ya uhalifu
wakati baadhi ya polisi wana urafiki mkubwa na
majambazi. Nani yuko tayari kutoa hata taarifa ya
mtu aliyechomwa kisu mtaani, lazima ataogopa
kwani bila shaka atakuwa mtuhumiwa namba moja
huku akisota gerezani kusubiri upelelezi wa muda
mrefu wa Polisi ukamilike. Moyo huo alikuwa nao
Ommy na wachache ambao ni vigumu
kuwafahamu. Nilitamani zirudi zama za wazalendo
wa ukweli kama kina Nelson Mandela na wengineo
kama yeye.
Niliinua Macho nikatazama saa iliyokuwa ukutani,
Ilikuwa ni saa 6.01 usiku nikagundua kuwa Johari
alikuwa na njaa ingawa hakutaka kuongea.
Nikaenda kuoga haraka haraka, nikabadili nguo
kisha nikaenda kutafuta chochote kwenye baa
ambazo zilikuwa hazijafungwa ili tuweze kula mimi
na Johari.
***

Aluta kontinua! maneno ya Ommy yalijirudia
kichwani kwangu huku nikimtazama Johari ambaye
alikuwa anamalizia zile ndizi za kuchomwa. Kitu
kimoja kilikuwa kinaichanganya akili yangu, Ommy
alikuwa amenipa namba ya Jerrome Mtuvu eti
nikaombe msaada kwake wakati nafahamu fika
kuwa ndiye yule mnafiki aliyekuwa ananihoji polisi
kisha akanirudisha katika mikono ya Bonge
ambaye sasa nilimfahamu kwa jina la Samson
Kipusa.
“Au na yeye alilaghaiwa na Jerrome kuwa ni mtu
mzuri akamuamini?” Niliwaza.
Johari alikuwa amemaliza kula, muda wote alikuwa
kimya akinitazama ili ajue nini kitafuata.
“Johari!” nilimwita, kabla hajaitika nikaendelea
“Tuna mengi ya kuongea, tena mengi sana lakini
kwa leo inabidi tupumzike!” nikainuka pale
nilipokaa nikatumia ishara ya mkono kumtaka
anifuate.
“Utalala hapa!” Nilimwonesha kile kitanda
nilichokuwa nalalia wakati Ommy akiwepo.
“Peke yangu!?”
“sasa ulitaka ulale na nani?” Nilimuuliza kwa
mshangao kidogo.
“Siwezi kulala peke yangu kajuna, watanikuta……”
“Kina nani?” nilimkatisha.
“tafadhali usiniache Kajuna naogopa kulala peke
yangu!” alikuwa na hofu ya kweli, sikuwa na jinsi.
Tukalala kitanda kimoja. Tukalala mzungu wa nne.
Kwa jinsi nilivyochoka sikuchelewa kushikwa na
usingizi, nikalala. Ilitakiwa mtu mwenye moyo wa
jiwe.
Ndiyo lakini mzungu wa nne yataka moyo.
Usiku haukuwa mzuri kwa Johari , alikuwa
anashtuka na kuweweseka sana. Akashindwa
kulala upande wake akageukia upande wangu.
Akawa amelala huku amenikumbatia. Ilikuwa
hatari.
Wee thubutuu! Nani kakwambia bila kupima siwezi.
Nikaomba Mungu usiku uishe salama. Niliweza,
inawezekana mambo mengine tunayaendekeza tu.
***

Niliamka mapema zaidi. Nikakaa sebuleni,
sikuweza tena kuendelea kukumbatiwa na Johari
pale kitandani. Sina roho ya chuma. Ingawa
alikuwa anafanya hivyo kutokana na woga wake
kwangu ilikuwa adhabu tosha, kuna wakati
niliweza kujisahau nikahisi kuwa nimekumbatiwa
na Betty, pia niliweza hata kumpapasa pale
nilipojisahau. Ah…. Yamepita.
Jambo kubwa lililokuwa linaumiza kichwa ni jinsi
nitakavyotoka mle ndani kwenda kupata mahitaji
bila kujulikana. Nilihisi pengine sura yangu
ilishakuwa maarufu kwenye magazeti. Sina
uhakika kama magazeti yalishaautaarifu umma juu
ya kitendo changu cha kutoroka na kufanya mauaji
makubwa.
Nikavaa mawani ya jua ambayo alikuwa anatumia
Ommy siku za jua kali. Hakuwa akiitumia mara
kwa mara hivyo bado ilikuwa kama mpya ingawa
ilikuwa ni ya muda mrefu. Sehemu ya kwanza
ilikuwa ni kituo cha magazeti. Nikakusanya
magazeti mengi, sikujali ni ya lini kwani muda
mrefu nilikuwa kwenye dunia ya nusu wafu.
Nikaenda dukani, nikanunua vitu mbalimbali bila
kusahau chupa ya chai. Kama kawaida ya mitaa
kama hii, kulikuwa na vibanda vingi vya kina
mama wauza chakula. Vibanda hivi vilikuwa
vimepambwa kwa sanaa ambayo ilitafsiri hali halisi
ya maisha ya Mtanzania, Karibu vibanda vyote
vilikuwa vimezungushiwa kanga au vitenge
vilivyochoka. Watu wengi hususani makapera
walikuwa wakipata huduma zao humo. “Niwekee
vikombe sita tafadhali”
“Sita haviingii humu, vitano na nusu tu!”
“haya weka vitano, unifungie na chapati tano” yule
mama mnene akanifungia chapati zangu
nikaondoka kurudi nyumbani.
Wakati narudi ndipo nilipopatwa na mshtuko baada
ya kuwaona watu wawili wakinifuata kwa hatua za
haraka. Nilipowatazama vizuri nikamkumbuka yule
mmoja. Alikuwa yule dereva wa gari lilonichukua
na kisha kupata ajali kabla sijajikuta niko hospitali.
Ina maana hakufa? Nilijiuliza. Kitu ambacho
kilinifanya nimtambue kuwa ni yeye ni unene wake
na ile nundu iliyoota kwenye paji la uso. Tofauti na
siku ya kwana kuna kitu cha ziada kilikuwa
kimeongezeka kwenye sura yake. Jicho, alikuwa
hana jicho moja nahisi lilipotea siku ya ajali.
Kwa kuwa nilishafika karibu na nyumbani sikutaka
wafahamu pale nilipo. Hata hivyo nahisi walikuwa
hawajagundua kuwa nimewaona maana ingawa
walikuwa wanakuja kasi bado walikuwa kama ni
watu wanaonivizia. Nikaamua kutumia vizuri fursa
hiyo kwa kufuata barabara inayoelekea makaburini.
Nikaongeza kasi nami nikiendelea kujifanya
sijawaona, mara kwa mara niliinua mkono wangu
nikijifanya kuangalia saa. Nilikosea, nilikosea sana
kwani mbele yangu niliwaona watu wengine
wakinifuata. Sasa ni wazi nyuma kulikuwa na watu
mbele pia. Hapo nikaamua kukona na kufuata
kichochoro ambacho kinaelekea kituo cha polisi
Makangarawe. Nilipofika mbele nikaingia kwenye
nyumba mbovu ambayo ilikuwa inatumika kama
dampo la kutupia takataka.
“Amepotea?” Nilisikia watu wakiulizana.
“Inavyoonesha anaishi kule bondeni tatizo ni ninyi
mliokuwa mbele yake inaonesha kuna mmoja
amemtambua, sisi tulikuwa tunamfuatilia vizuri na
hakujua kama anafuatwa!’
“Sasa?”
“Ni vizuri tukiweka doria maeneo haya kuanzia
leo.”
“Hilo ni wazo la kipuuzi, bosi amesema yule jamaa
ana akili sana. Sidhani kwa mtu mwenye akili
kuweza kuendelea kukaa hapa baada ya kugundua
kuwa anatafutwa.”
“Dah, sure mwana hapa tumempoteza tuondoke
zetu si unaona hata nyumbani kwake haonekani
kabisa?”
Nikasikia sauti za nyayo za watu, bila shaka
walikuwa wanaondoka. Nikaondoka pale mafichoni
na kuelekea nyumbani.
Johari alikuwa ameamka. Alionekana kuwa na
mawazo mengi na hasira. Nikamsogelea
nikambusu shavu la kulia, akaniangalia kwa
kustaajabu.
“Wewe! huogopi?”
“niogope nini?” Nilimuuliza
“Si wanasema ni nuksi kumbusu albino?”
“Kwani kila linalosemwa lina ukweli?”
“Mh, we hujui kama lisemwalo lipo?”
“Wapo waliosema dunia imefika mwisho na
hatukuuona!” Nikacheka kisha nikampiga mabusu
mfululizo ili kumuondoa hofu.
Kabla ya kunywa chai nikaanza kusoma magazeti.
Vichwa vya habari vilinitisha, vilikuwa na habari
ambazo kwa wasomaji wa kawaida ni za
kusisimua. Zilinitisha. Gazeti moja liliripoti kuwa
MTUHUMIWA ATOROKA NA KUFANYA MAUAJI
MENGINE. Habari hii ilikuwa inaeleza juu ya mauaji
ya walinzi wa Samson Kipusa huku ikielezea pia
kupigwa risasi kwa Samson mwenyewe. Taarifa
iliendelea kueleza kuwa kwa sasa Samson
amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututri pale
Muhimbili baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi.
Habari ikamalizia kuhusu uporaji wa gari ambalo
lilitelekezwa Temeke.
Nikamimina chai kwenye kikombe nikampa Johari .
“kunywa rafiki yangu!” Johari akatabasamu huku
akinitazama kwa macho yaliyojaa aibu. Akaanza
kunywa chai huku akinitazama jinsi nilivyokuwa
nasoma magazeti. Baada ya kumaliza kusoma
magazeti hayo ambayo yalinitisha nikamimina chai
kwenye kikombe. Sikutaka kuumiza kichwa kwa
habari hizo ambazo zilikuwa zinaonesha kuwa
mimi ni jambazi sugu.
“Johari.”
“Abee.” Akaitika.
“Nadhani muda umefika sasa wa kuweza
kuelezana kile kilichosababisha tukutane mimi na
wewe.”
“Nitaanza kukusimulia mimi kilichotokea hadi
tukakutana kisha nitasikia kutoka kwako”
kisha nikamsimulia kila kitu. Alikuwa ananisikiliza
kwa makini na kutokwa na machozi hasa pale
nilipomsimulia kuhusu mpenzi wangu Betty na
habari za ule mzigo wa Mwanza.
***

“Naitwa Johari Iyina Mayala, ni mzaliwa wa
Shinyanga katika wilaya ya Mwadui. Mimi ni mtoto
wa pili katika familia ya mzee Mayala ambaye
aliwahi kuwa diwani katika kata tofauti za
Shinyanga mjini. Mama yangu mzazi alifariki dunia
nikiwa kidato cha nne shule ya sekondari ya
Biashara ya Shinyanga .
Wakati wa uhai wa mama yangu niliishi kwa
furaha sana kwani alinijali na kunithamini.
Matatizo yalianza kujitokeza baada ya kifo cha
mama yangu. Kuna wakati baba yangu alikuwa
ananiambia maneno ambayo yalikuwa yananitia
uchungu sana. Alikuwa ananiambia wazi wazi
kuwa mimi ndiye ninatia nuksi katika familia.
Maduka yake hayaendi vizuri, magari yanaharibika
mara kwa mara eti chanzo ni mimi. Ikafikia wakati
akaamua kuoa mwanamke mwingine.
Akatulia kidogo na kunywa maji, kisha akaendelea.
Huyo mama alipokuja ikawa mwanzo wa mashaka
na mateso, nilikuwa nimefundishwa kuendesha gari
wakati wa uhai wa mama yangu. Mara moja moja
nilikuwa nachukua gari na kwenda nalo mjini.
Wengi walinisifia kuwa nilikuwa dereva nzuri, lakini
baada ya kuja mama mwingine nikawa nimezuiwa
kabisa kutumia magari hayo kwa madai kuwa eti
nitayatia mkosi. Nilianza kuumwa kichwa mara
kwa mara kutokana na mawazo!” akatulia na
kuanza kutokwa na machozi.
“Enhee, endelea!” nikamuhimiza baada ya
kumuona amesita kusimulia.
“Ikatokea siku ambayo siwezi kuisahau katika
maisha yangu. Siku hiyo alikuja mtu ambaye
nilihisi kuwa ni mganga wa kienyeji. Akawa
anaongea na baba. Toka nianze kunyanyaswa
nilikuwa nimejenga tabia ya kujificha na
kuwasikiliza baba na mama walikuwa wanaongea
nini kuhusu mimi. Nikiwa karibu na dirisha niliweza
kusikiliza vizuri sana maongezi yao. Nikamsikia
yule mganga akiongea.
“Kama ni ubunge utaupata lakini masharti yake
kidogo ni magumu!”
“Masharti gani?” aliuliza baba
“Mizimu inataka kafara ya mkono wa kulia na
mguu wa kushoto wa albino” nilimuona baba
akishtushwa na kauli hiyo.
“hivi imewahi kweli kutokea kafara ya aina hiyo!?”
Aliuliza tena baba.
“Toka siku za nyuma kafara za aina hii tumekuwa
tukizifanya, ili kukwepa mikono ya sheria tuliamua
kupandikiza imani kuwa albino huwa hafi bali
hupotea, lakini siku hizi mambo yameanza kuwa
wazi kutokana na uwingi wa vyombo vya habari!”
Baba alikuwa ametulia huku akimsikiliza kwa
makini yule mzee hali iliyonitia hofu. “Unataka
kuniambia nikifanya hiyo kafara nitafanikiwa?”

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TISA

“Mizimu inataka kafara ya mkono wa kulia na
mguu wa kushoto wa albino” nilimuona baba
akishtushwa na kauli hiyo.
“hivi imewahi kweli kutokea kafara ya aina hiyo!?”
Aliuliza tena baba.
“Toka siku za nyuma kafara za aina hii tumekuwa
tukizifanya, ili kukwepa mikono ya sheria tuliamua
kupandikiza imani kuwa albino huwa hafi bali
hupotea, lakini siku hizi mambo yameanza kuwa
wazi kutokana na uwingi wa vyombo vya habari!”
Baba alikuwa ametulia huku akimsikiliza kwa
makini yule mzee hali iliyonitia hofu. “Unataka
kuniambia nikifanya hiyo kafara nitafanikiwa?”
“siwezi kukudanganya mzee katika orodha yangu
nina wavuvi wa samaki na wafanyabiashara wa
madini, hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuja
kulalamika kuwa hajafanikiwa. Tena nilitaka
kusahau katika orodha ya wateja wangu yupo
waziri mmoja anaitwa……” sijui alitaja jina gani
sina kumbukumbu kama alisema ni muheshimiwa
Kenge au kingi.” Akatulia tena na kunifanya niwe
na hamu kubwa ya kuendelea kumsikiliza.
“Baada ya kuongea vile baba akamweleza yule
mganga kuwa ana mtoto wa kike ambaye ni albino,
yule mganga akacheka sana, kisha nikamsikia
akisema “Kama una mtoto wako mwenyewe hata
ukiutaka uraisi utaupata.”
“Ah! Hapana kwa sasa nahitaji ubunge kwanza
labda uchaguzi unaokuja.” Nikashtuka baada ya
kauli hiyo. “Ina maana baba yuko tayari
kuniangamiza?” nilijiuliza huku nikisikia uchungu
sana. “Ili umtumie vizuri inabidi achukuliwe mzima
kwani itanisaidia kufanya kafara ya watu wengi
kwa pamoja. “niko tayari kumtoa mwanangu ili
mradi niupate huo ubunge!” aliongea baba kitu
ambacho kilinifanya nipatwe na msthuko mkubwa.
Sikutaka kupoteza muda nikaamua kutoroka,
nikaenda kujificha kwenye jengo moja ambalo bado
lilikuwa halijakamilika liko mtaa wa kaunda.
Nikakaa humo hadi usiku. Maisha yangu yakawa
ya kutangatanga kwani mara kadhaa nilipita
majalalani kutafuta chakula na ilipofika usiku
nilitafuta gofu nikalala hapo. Maisha yangu
yalikuwa hivyo kwa siku kadhaa, nilikonda
nikadhoofika. Matangazo yakatolewa kuwa
natafutwa nimepotea! Ni kipindi kigumu ambacho
siwezi kukisahau kwani niliishi kama kichaa.
Ulifika muda ikawa hatima ya maficho yangu
kwani nilipatwa na homa, nikaenda kwenye
zahanati ya daktari ambaye ni rafiki mkubwa wa
baba kwani naye ni kada mwenzake wa chama.
Nahisi yeye ndiye aliyetoa taarifa kwa baba kuwa
niko pale. Baada ya dakika arobaini wakati
nasubiri huduma ghafla nikamuona baba anaingia
pale zahanati akiwa ameongozana na watu wanne
wote wakiwa wanaume. Nilipatwa na mshtuko
nikapoteza fahamu.
Nilipozinduka nikajikuta nimefungiwa kwenye
chumba cha wageni. Baada ya siku saba ndio
nikasafirishwa kuja Dar, nikawekwa kwenye
chumba kile kama ulivyonikuta! ” akamaliza
kusimulia na kunifanya nitafakari zaidi. Inakuwaje
mtu anaamua kuitoa damu yake sadaka, huku ni
kupoteza mwelekeo.
“Ulisafirishwa vipi kutoka Shinyanga?” Nilimuuliza.
“Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Ijumaa asubuhi.
Kule chumbani nilikofungiwa walikuja watu wanne.
Yule mganga, baba na wengine wawili ambao
sikuwafahamu, ingawa yule mmoja nilisikia akiitwa
Martin mwingine sikubahatika kusikia jina lake.
Yule mganga akachukua kitu kama mkia wa
ng’ombe akawa ananipiga nao kichwani huku
akiongea maneno ambayo sikuyaelewa”
“Wakati anafanya hivyo haukupiga kelele!”
“Hapana nilishakata tamaa tena ajabu nilitamani
zaidi kifo kuliko kitu kingine thamani yangu ilikuwa
mbele ya Mungu duniani sikuiona tena, ndio
maana ulipotaka kuniokoa nilikukatalia Nashukuru
kwani umeonesha ubinadamu mkubwa kwangu!”
“Usijali, enhe ikawaje?”
“Kisha yule mtu mbaya ambaye wanamwita Martin
akanichoma sindano, baada ya dakika chache
nikalala. Nilipoamka ndo nikajikuta nipo kule
ulikonitoa.”
***

Katika habari za magazeti yale ilinivutia makala ya
gazeti moja ambalo nililihifadhi ili nilisome baadae.
Nililitunza kwasababu makala yake ilinivutia kidogo
nilipanga kuisoma baada ya kumaliza mahojiano
na Johari . Ilikuwa na kichwa cha habari
kilichosomeka UKWELI KUHUSU MAUAJI
YANAYOENDELEA habari yenyewe iliandikwa kwa
mtindo wa makala hivyo nililazimika kuisoma kwa
vipande vipande. Kipande kimoja kiikuwa na
maandishi ambayo mwandishi alililalamika kuwa
vyombo vya usalama havikuwa makini kwani
haiwezekani matukio yote yale ya kutisha
niyafanye mimi tena bila sababu za msingi,
mwisho akamaliza kwa ahadi ya kueleza kiini cha
yote yale toleo lijalo. Kwa kuwa lile gazeti lilikuwa
linatoka kila siku nikaamua kusubiri siku
itakayofuata nione mwandishi ataeleza nini
anachokijua. Yule mwandishi alikuwa anafahamika
kwa jina la Stela Mangungu.
“Hivi huyu Stella mada nyingine anazoanzisha
haogopi?” niliwaza.
Nilianza kuhisi hatari inayomwandama mwandishi
huyu kwa makala aliyoandika. Najua wazi nia yake
ya kuandika kiini cha yote katika toleo linalokuja
inatokana na mawazo yake binafsi. “Lazima
nimsaidie la sivyo atakufa huyu!” Niliwaza.
Namshukuru Mungu kuwa mpaka kufikia muda huo
akili yangu ilikuwa inafanya kazi kwa wepesi wa
ajabu sana. Nikaikumbuka simu iliyoachwa na
marehemu Merina. Nilikuwa nimeshamkabidhi
Ommy, nikaenda kuitafuta kwenye mabegi yake,
nikaiona. Alikuwa ameihifadhi kwenye mfuko wa
pembeni wa begi. Haikuwa na chaji. Nikaenda
katika kibanda kinachotoa huduma za simu.
Nilitaka niichaji simu ile lakini yule jamaa alikuwa
na chaja za aina mbalimbali hivyo nikaamua
kununua kununua chaja ambayo nitaimiliki
mwenyewe.
Nikarudi nyumbani kwenda kuchaji ile simu.
Saa 7.15 simu ilikuwa imejaa chaji. Nikampigia
Stella yule mwandishi wa gazeti la UKOMBOZI.
Nashukuru huu utaratibu wao wa kuandika namba
za simu baada ya makala ndio ulionisaidia sana.
Stella alikuwa hewani.
“Unaongea na na Sebastian Mumba hapa!”
niliongopa.
“Nikusaidie nini?” sauti ya kike iliuliza.
“Nahitaji kuonana na wewe nitakupata vipi?”
“Unajua unaongea na nani?”
“Bila shaka ni Stella Mangungu!”
“Ok! Njoo nyumbani saa kumi na mbili, naishi
kinondoni nyuma ya shule ya sekondari ya
Ridhwaa seminary shuka kituo cha mkwajuni.
Ukifika maeneo hayo uliza kwa mzee
Mwakasungura! ” Nikakata simu kisha nikaanza
kuitafuta namba ya Ommy.
Nilipoipata nikapiga, hakupatikana!. Kidogo
nikaingiwa na hofu, yuko wapi Ommy? Wakati
nikiwaza hilo mara simu ikaanza kuita. Alikuwa ni
Stella.
“Enhe, sema!”
“Samahani nilikuwa nataka kujua wewe ni nani na
una shida gani?”
“Nafikiri nimeshakueleza kuwa naitwa Sebastian
Mumba, nimevutiwa na ile makala yako juu ya
mauaji ya kutatanisha yanayoendelea hapa nchini
kidogo nimeona unaelekea kwenye ukweli hivyo
nataka kukusaidia ili uandike kitu sahihi na siyo
makala kama Insha za sekondari!”Nikasikia
akishusha pumzi kwenye simu.
“Sawa!” alijibu baada ya kuwa hewani kwa
sekunde kadhaa bila kuongea.
***

Niliwaza sana jinsi gani nitafika mitaa ya
Kinondoni nikiwa mtu ninayetafutwa kila kona.
Nikacheka baada ya kupata wazo. Johari akawa
ananitazama kwa mshangao bila kuuliza wala
kuongea chochote. Alikuwa na mawazo mengi
sana. Bila shaka alikuwa anataka kujua hatima ya
yote haya itakuwa nini. Nikatoka kwenda kununua
mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na vifaa vya kazi
ambayo nilitarajia kuifanya usiku huo. Nikanunua
redio ndogo aina ya Rising, redio hii ilikuwa
inarekodi. Nikanunua mikanda mitatu ya ‘tape’
ambayo ilikuwa haijarekodiwa chochote. Pia
nikanunua vazi aina ya kanzu na baraghashia.

10
Daladala nililopanda liliwasili Kinondoni mkwajuni
saa 11.00, ilikuwa ni saa moja kabla ya muda
tuliokubaliana kukutana. Nilitembea taratibu
kuelekea upande nilioelekezwa na Stella. Simu
nilikuwa nimeiacha hivyo sikuweza kumfahamisha
Stella kuwa nimefika na sikutaka afahamu ujio
wangu. Sikuwa na shida ya kuonana na stela muda
huo nilikuwa na mawazo yangu binafsi. Nilijua wazi
kuwa Stella atakufa kama sitatoa msaada kwake.
Tatizo kubwa ambalo lingemgharimu Stela ni
kitendo changu cha kuwatoroka wale Mashetani.
Pengine Stella angeweza kuhisiwa kupata habari
kutoka kwangu. Jukumu lao kubwa lilikuwa ni
kumfunga mdomo. Lazima wangemtafuta Stella.
Kwa kuwa nilishaingia kwenye mapambano haya
ya aina yake nilikuwa na jukumu la kuhakikisha
Stela anakuwa salama.
Nikiwa ndani ya vazi la kanzu na baraghashia
nikaanza kutembea taratibu kuelekea mbele kidogo
kutoka pale kituoni.
“haloo kijana, unaweza kunielekeza nyumbani kwa
Mwakasungura” nilimuuliza kijana mdogo ambaye
alikuwa anacheza mpira na wenzake
“nyumba ileee!” alinionesha kwa kidole nyumba
ambayo haikuwa mbali kutoka pale niliposimama,
huku akionesha wazi kukerwa na kitendo changu
cha kukatisha burudani yake. Nikatembea taratibu
kuifuata nyumba ile. Sikuwa na wasiwasi kwa
sababu vazi la kanzu na kibaraghashia vilinifanya
nipewe Salam aleikum nyingi sana. Hii ina maana
kuwa sikutambulika licha ya baadhi ya magazeti
kuchapisha picha yangu.
Ingawa jua lilikuwa linaelekea kuliaga jiji la Dar es
salaam sikuthubutu kabisa kuvua miwani ile ya
jua, niliogopa kutambulika kwa urahisi zaidi.
Nilipofika usawa wa ile nyumba sikusimama hadi
kwenye banda la chips ambalo lilikuwa jirani.
“Naomba chips mayai!”
“poa ustadhi wangu!” Alinijibu muuzaji baada ya
kuagiza mlo huo ambao unapendwa sana jijini Dar.
“Zikauke sana ustadhi wangu?” Aliuliza tena.
“Eee kausha!” Nilimjibu huku nikimeza mate kwa
hamu ya mlo huo.
Chips zilikuwa tayari kwenye sahani. Nilianza kula
taratibu huku nikitembeza macho yangu hapa na
pale kwa namna ambayo mtu yeyote asingeweza
kugundua kuwa nilikuwa kwenye kazi fulani.
“Inaelekea biashara ni ngumu mbona sioni
wateja?” nilimuuliza muuzaji “wateja wa hapa
wengi ni wa usiku” alinijibu. Nikawa nimeanzisha
maongezi ya kuongelea hili na lile kuhusu biashara
ili mradi nicheleweshe muda.
Baada ya kuona chips ambazo nilikuwa nakula
taratibu mno zinaisha nikaagiza soda, yote ikiwa ni
moja ya mbinu za kupoteza muda.
Nilikuwa nakaribia kukata tamaa ndipo nilipoliona
gari la kampuni ya magazeti ya Ukombozi likiingia.
Likasimama mbele ya nyumba ya Mwakasungura.
Nililijua kwa sababu nyuma lilikuwa na nembo
kubwa ya kampuni ile. Kama nilivyotarajia
aliyeteremka alikuwa ni Stella. Ukweli sikuwa na
shida ya Stella, nilikuwa nawahitaji wale wauaji.
Kwa jinsi nilivyowafahamu nilijua wazi ni lazima
watamfuatilia Stella kutokana na makala
aliyoandika. Nikatulia pale kwenye banda la chips
kwa muda mrefu kidogo hatimaye nikaamua
kuondoka na kutafuta eneo lingine ambalo
lisingekuwa mbali na pale kwa Stella.
Bado hali ilikuwa shwari kitu ambacho kilinipa
moyo kuwa huenda wauaji walikuwa hawana
mpango na huyu dada. Nikaamua kuondoka na
kurudi kituo cha daladala. Nikasimama hapo
nikisubiri gari za buguruni. Nuru ya jua ilikuwa
imetoweka kabisa. Taa zilizokuwa zinawaka
kwenye majengo mbalimbali zikaanza kuchukua
utawala wake.
“Lakini kwanini nisionane naye? Watamuua huyu!”
Nilijiuliza. Nilikata shauri kurudi kwa Stella.
Nilipofika nikabisha hodi, mzee wa makamo
akanifungulia mlango.
“Shikamoo mzee!”
“Marhaba mwanangu, karibu!”
“Ahsante, samahani naomba kuuliza, nimemkuta
Stella yule…..” akanikatisha
“Ni nani wako!” aliuliza yule mzee.
“Huwa ananiita mara nyingi kumsomea dua!”
“Ahaa, nenda huko nyuma utakuta milango mitatu
huo wenye pazia la njano ndio mlango wake”
Nikaelekea uani moja kwa moja. Nikakiona chumba
alichonielekeza. Nikakiendea huku mapigo ya moyo
yakienda kasi. Sijui ni kwa nini lakini kadri
nilivyokisogelea kile chumba nilihisi mapigo ya
moyo yakiongezeka. Nilipofika mlangoni nikasita
kubisha hodi. Nilipoangalia vizuri kumbe kilikuwa
chumba na sebule.
Nikaendelea kuganda pale mlangoni huku nikisikia
muziki wa taarabu ukirindima mle ndani. Kwa
mbali niliweza kusikia sauti za watu wanaongea
mle ndani. Nikashika kitasa cha ule mlango
nikafungua taratibu. Nilikuwa natetemeka
sana ,kwani nilijiuliza iwapo nitaingia kwa mfumo
huu na kukutana na stella bila shaka nitapigiwa
kelele za mwizi.
Nikaupeleka mkono wangu kwenye mfuko suruali
ambayo nilikuwa nimevaa, huku ikifichwa vema na
kanzu. Ilikuwepo! Ile bastola yangu ambayo
niliipata Mbagala.
Nikafungua mlango, nikawa natembea kwa kunyata
kuelekea kule chumbani.
”Hivi nikimkuta Stella na mumewe nitamueleza
nini?” Niliwaza. Nikaufikia mlango wa chumbani,
kijasho chembamba kilianza kunitoka.
“Tafadhali kuwa mtulivu kama ulivyokuja!” Sauti
nene ilinishtua na kukatiza zoezi langu. Nikahisi
kitu kigumu chenye ubaridi kikiwa kimegusa
kisogoni kwangu. “Ujanja wowote utakaojaribu
kuufanya nitakulipua!” mapigo yangu ya moyo
yalikuwa yanakaribia kuzimika kwa woga niliokuwa
nao.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA ISHIRINI.

“Tafadhali kuwa mtulivu kama ulivyokuja!” Sauti
nene ilinishtua na kukatiza zoezi langu. Nikahisi
kitu kigumu chenye ubaridi kikiwa kimegusa
kisogoni kwangu. “Ujanja wowote utakaojaribu
kuufanya nitakulipua!” mapigo yangu ya moyo
yalikuwa yanakaribia kuzimika kwa woga niliokuwa
nao.
Muda ule ule nikapata wazo, iwapo nitaendelea
kuwa mwoga basi kifo kilikuwa kinakaribia. Hata
hivyo kifo kilikuwa kimekaribia tu! Kama ni kurudi
katika mikono ya wale jamaa basi hakukuwa na
hukumu nyingine zaidi ya kifo. Nilifikiria kumpiga
teke kwa nyuma lakini nikaogopa ile kanzu, ilikuwa
haiwezi kutanuka na kutoa teke la haja. Akili
ilikuwa inafanya kazi kutafuta namna ya kujiokoa
lakini sikuiona. Nikaamua kutulia ili liwalo na liwe.
“Hivyo hivyo naomba ujibu maswali yangu!”
Akatulia kabla ya kuanza kuuliza.
“Wewe ni nani na unatoka wapi?”
“Naitwa Athumani Kipande natokea idara ya
usalama wa taifa operesheni maalum!” Nilijibu kwa
kujiamini
“Hapa umefuata nini?”
“Nimekuja kumsalimia mpenzi wangu Stella!”
“Kwa hiyo unapokuja kumsalimia mpenzi wako
huwa unakuja kwa utaratibu wa kunyata tena bila
kubisha hodi?!”
“Hapana nimesikia sauti ya kiume hivyo nilikuwa
nakusudia kufumania!” “Unataka kuniambia
humuamini mpenzi wako?” Sikujibu nikakaa kimya
“Narudia ina maana hutaki kumuamini mpenzi
wako!”
“Achakuniuliza maswali yakipuuzi unanipotezea
muda!” Nilifoka.
“Pumbavu, yaani unaona mimi napoteza muda?”
“Ndiyo kwa sababu najua wazi kuwa huwezi
kunifanya lolote!”
“We nyang’au maneno gani unaongea!”
“Nina uhakika huwezi kunifanya lolote kwani hata
jinsi ulivyoingia tumekuona, na hivi
ninavyokuambia yule kiongozi wenu
ashakamatwa!” Nilikuwa najaribu bahati yangu
kwa kumzubaisha yule jamaa.
Kweli nilikuwa nimempatia kwani niliweza kusikia
pumzi zake zikipanda na kushuka kwa hofu. Pia
nilihisi kuwa amelegeza mkono ambao ameshika
ile bastola. Ilikuwa ni fursa ambayo sikutakiwa
kuipoteza. Ghafla, niligeuka kwa kasi nikatumia
mkono wangu wa kulia kuupiga ngumi mkono
uliokamata ile bastola. Akiwa ameduwazwa na
kitendo kile cha ghafla nilimsukuma kwa mikono
yote miwili akaangukia juu ya meza ndogo
iliyokuwa pale sebuleni. Ilikuwa ni meza ya duara
yenye mguu mmoja. Nikaishuhudia ile meza
ikianguka na kumfanya yule jamaa apige mwereka
mkubwa huku akifuatiwa na ile meza kwa juu.
Sikuwa na muda zaidi nikaiokota ile bastola yake.
Nikafyatua huku nikiwa nimemlenga usoni.
Nilishuhudia damu iliyochanganyika na ubongo
ikitawanyika sakafuni huku ile bastola ikiwa
haijatoa sauti kubwa ya mlipuko. Ilileta kinyaa!
Nilishangaa bastola ile kwa nini haikutoa mlio
kama nilivyotarajia. Badala yake ikatoka sauti
ndogo sana kama kikohozi cha mtoto mchanga.
Nikakumbuka kuwa kuna bastola ambazo zina
kiwambo cha kuzuia sauti. Kama kulikuwa na mtu
kule chumbani basi alishtushwa na kishindo cha
mtu kuanguka.
“Vipi Steve kuna tatizo?” sauti iliuliza kutoka
chumbani. Hakuwahi kupata jibu nilifungua mlango
wa chumbani. Alikuwa amenipa mgongo hivyo kazi
ilikuwa rahisi nilimtandika risasi mbili za kichwa
haraka haraka. Akaruka juu na kutua chini kama
gunia la pumba. Alikuwa amekufa!
Nilimwona mwanamke ambaye nilihisi kuwa ndiye
Stella akiwa mdomo wazi. Alikuwa haamini mambo
yaliyokuwa yanatokea.
“Usiogope naitwa Kajuna Kazakamba !” Nikatoa
baraghashia ambayo nilikuwa nimevaa, akapatwa
na mshangao kwani hakutarajia kabisa ugeni huu
wa aina yake.
Hakuweza kuongea lolote.
“Shusha mikono tafadhali kwani uko kwenye
mikono salama!” Niliongea kwa sauti ya upole ili
kumuondolea hofu.
“kuna maiti mbili humu ndani naomba tuondoke
haraka kabla mambo hayajaendelea kuharibika!”
Simu yake ilikuwa mezani sikuomba nikapiga polisi,
112 ni namba ngumu kupatikana lakini siku hiyo
haikuwa na usumbufu. Nikatoa taarifa polisi kisha
nikamgeukia Stella.
“Tafadhali chukua kitu chochote ambacho ni
muhimu kwako ujiandae tuondoke!” “Twende
wapi?”
“Sikiliza we mwanamke itabidi ukae mafichoni kwa
muda wa wiki moja la sivyo utakufa. Ni hiari yako
ukitaka utaondoka na mimi vinginevyo kwaheri!”
Sauti yangu haikuwa na mzaha. Aliniogopa kwani
nilikuwa nimebadilika na kuvaa sura ya ukatili.
Akachukua begi kubwa la nguo. Sikutaka kumzuia
ingawa kwa maficho ya wiki moja hakukuwa na
ulazima wa kuchukua begi kubwa kama lile. Katika
mawazo yangu nilishapanga ile kazi niimalize
ndani ya wiki moja, yaani kama kufa nife kama
kupona nipone. “Hapana tukodi tax!” alisema
baada ya kuniona nikielekea kituo cha daladala.
Alikuwa anatetemeka sana.
Ilikuwa ni saa 3.34, wakati tunaelekea kituo cha
teksi tukapishana na gari ambalo lilikuwa na askari
wenye silaha. Mwanamke alinifuata kwa woga.
Hakuwa na imani kuwa yuko kwenye mikono
salama au la! Kitendo cha kumuokoa kutoka
kwenye mikono ya wale washenzi kidogo kilimpa
moyo.
“Tandika!” Nilimwambia kwa mkato dereva tax.
“Elfu kumi!” Alijibu kwa mkato huku akiwasha gari.
Tulikuwa kimya kwenye lile gari huku kila mmoja
akijaribu kuchambua hili na lile katika kichwa
chake. Hakuna aliyeongea mpaka tulipofika
Tandika.
Tukatembea hadi kituo cha magari cha Buza
kanisani. Huko tukachukua teksi nyingine kwa
shilingi elfu tatu hadi Yombo abiola. Kwa kutumia
njia zile zile tukafika pale nyumbani kwa Ommy.
Nikagonga, Kimya! Mlango haukufunguliwa.
Nikagonga mara tatu bado kulikuwa na ukimya
ulionitia mashaka.
“Mimi Kajuna naomba unifungulie tafadhali!”
Nikasikia mlio wa hatua za mtu ambaye alikuwa
anakuja mlangoni. Mlango ukafunguliwa. Johari
alikuwa amesimama mlangoni huku akionesha
wazi hofu kubwa.
Kuna kitu nilikisoma kwenye macho ya Johari .
Wivu! Sikutegemea kukiona kitu hicho kwenye
wakati mgumu kama huo.
“Hivi inawezekana kuwa huyu mwanamke
ananipenda?” Nilijiuliza huku nikivua ile kanzu.
“Johari kutana na Stella yule mwandishi ambaye
nilimpigia simu asubuhi!” wakapeana mikono.
Niligundua wazi ujio ule ulimkosesha raha Johari .
Nikaamua kufanya kitu cha ajabu kidogo ili kutatua
tatizo. Nikamshika Johari nikamvutia kwangu kisha
nikamkumbatia. Nikampiga busu shavuni kisha
nikamtakia usiku mwema.
“Unakuja kulala?” Aliniuliza.
“Leo utalala na huyu rafiki yako lakini tukimaliza
maongezi kwanza!” Nilimjibu baada ya kumuona
akiwa na wasi wasi wa kuachwa kwenye mataa.
Nilimkazia macho Stella ambaye bila shaka
asingeweza kulala bila kuelewa chanzo cha yote
yale. Sikumficha kitu nikamsimulia kuanzia
mwanzo hadi kufikia pale. Muda wote niliokuwa
namsimulia nilimuona akiwa makini, alikuwa
ameshangazwa na habari zile za kutisha. Hadi
mwisho nilipomsimulia kuhusu nilivyopatwa na
wasiwasi kuhusu ile makala yake. Akaniangalia
kwa kustaajabu sana!
“Ulishawahi kupitia mafunzo ya polisi!” Aliniuliza
kwa mshangao
“Hata mgambo sijawahi kupitia nafikiri
nishakueleza nimemaliza kidato cha sita na
sikuweza kujiendeleza kwa lolote zaidi ya kuomba
vibarua vidogovidogo kwenye viwanda!” Alizidi
kushangaa.
“Uliwezaje kutumia silaha?” Aliniuliza. Nikacheka
sikuwa na jibu kwa swali hilo kwa sababu
sijasomea chuo chochote mafunzo ya kutumia
silaha. Pengine ilitokana na uzoefu wa kutumia
bastola za watoto.
“Unaweza kunieleza ni nini ulitaka kuandika kuhusu
mauaji yale?”
Nilimuhoji.
“Unajua, nilikuwa sifahamu chochote isipokuwa
nilikuwa naandika kama mawazo yangu tu, lakini
cha ajabu toka asubuhi nimekuwa nikipokea meseji
za vitisho!” alitulia kisha akaendelea .
“Haya mambo niliyoyasikia ni mazito hivyo sina
budi kukushukuru sana kwa msaada wako”
Aliongea Stella kwa sauti tulivu.

11
Niliamka saa 12.10. Nikaelekeza macho yangu juu.
Nilikuwa katika hatua za mwisho. Hatua ambazo
zilikuwa ni karata katika maisha yangu. Ilikuwa
lazima nipambane. Nikaamua kuchukua simu ya
marehemu Merina. Nikapiga namba ambazo Ommy
aliandika kwenye ujumbe wake kuwa ni za
Jeromme Mtuvu. Huku nikiwa na wasiwasi
nikapiga.
“Unaongea na Jerrome Mtuvu, nani mwenzangu!”
“Naitwa Kajuna Kazakamba!”
“Ni utani?” Aliuliza kwa mshtuko
“Ina maana sauti yangu umeisahau?” Nilimtega.
“Sauti yako?”
“Ndiyo umesahau mara ya mwisho kabla
hamjaniteka tena kule polisi si ulinihoji!”
Nilisikia upande wa pili mtu akishusha pumzi.
Nikasikia simu ikiniashiria kuisha salio, hatimaye
ikakata. Baada ya sekunde chache simu ikaanza
kuita. “Halloo mbona sikuelewi? Kwanza namba
yangu umeipata wapi?”
“Hiyo namba nimeipata kwenye barua ambayo
nimeachiwa na rafiki yangu Ommy!”
”Mh, naomba kama inawezekana tuonane!”
Kwa jinsi alivyokuwa na mshangao nikahisi
anaweza kuwa mwingine na si yule mnafiki.
Nilishaamua kuonana naye. Nilishaamua liwalo na
liwe.
“Wapi?”
“Njoo sasa hivi maeneo ya mnazi mmoja utanikuta
kwenye ofisi za CRDB tawi la Lumumba pale
wanapouzia magazeti.” Sikutaka kuchelewa
nikaiweka sawa ile bastola yangu niliyoipata
Kinondoni. Nikawaita Stella na Johari , nikawaaga.
Nikawaambia wazi kuwa huenda ule ukawa
mwisho wa maisha yangu. Johari na stella
walikuwa wanalia. Johari alionekana kusikia
uchungu zaidi, alikuwa ananipenda haikuwa siri.
***

Nilitembea taratibu nikikatiza mitaa mbalimbali ya
Kariakoo. Nilipofika mtaa wa Kipata nikaongeza
kasi kwani hakukuwa na watu wengi kama mitaa
ya Lindi na Gerezani. Nikatokea nyuma ya jengo la
CRDB Lumumba. Nikafuata kichochoro ambacho
kilikuwa kinatokea mbele ya benki ile. Nilipofika
nikawaona watu wengi wakiwa wamezunguka
meza ya magazeti iliyopambwa na maandishi
makubwa THE CITIZEN AVAILABLE HERE.
Ingawa nilikuwa nacheza karata hatari sana
kwenye maisha yangu bado sikuwa na hofu.
Nilijihisi utulivu kwani nilikuwa tayari kwa lolote.
Nilikuwa simjui mtu niliyekubaliana kukutana naye.
Nilianza kuingiwa na mashaka kuwa kuna mtego.
Nikazungusha macho huku na kule. Hatimaye
macho yangu yakatua kwa mtu mmoja ambaye
alikuwa amevaa suti ya kijani. Alikuwa anaangaza
macho huku na kule huku akijaribu kupiga simu
ambayo bila shaka ilikuwa haipatikani kwani
nilimuona akikunja uso kwa hasira.
“Bila shaka ni yeye!” Niliwaza baada ya kumuona
uso wake ukibadilika na kuwa na mikunjo baada ya
kushindwa kuipata namba ambayo aliikusudia.
Huku mapigo ya moyo yakiongeza kasi yake
nilimsogelea. Nikamgusa bega!
“Jerry!”
“Yaah! Kajuna?” Nikakubali kwa kichwa.
Tukapeana mikono, mkono wake ulikuwa mgumu
kidogo kiasi kwamba nilisikia maumivu wakati
tunasalimiana. “karibu kijana uko very smart!”
“Aaah, ahsante!”Nilimjibu huku nikijitazama mavazi
yangu na kuushangaa usmart anaouzungumzia.
“Simaanishi mavazi kijana, nakusudia utaratibu
ulioutumia mpaka tunaonana ni makini na
unaokubalika!” Akanipa tena mkono na kuutikisa
kwa furaha kisha nikamfuata. Tukaliacha jengo lile
la ushirika tukafuata ghorofa moja chakavu ambalo
lilikuwa linapakana na jengo lile.
Tukaanza kupanda ngazi kuelekea juu. Nilianza
kuingiwa na hofu kuwa huenda niko katika mikono
ya Bonge kwa mara nyingine. Tulipofika juu
tukaelekea upande wa kulia wa korido ile. Upande
wa kushoto kulikuwa na madarasa ya wanafunzi
waliokuwa wanasoma masomo ya kidato cha nne
kwa miaka miwili yaani QT. Upande ule ulikuwa na
milango mingi huku kila mlango ukiwa na
maandishi yalioutambulisha. Chumba tulichoingia
kilikuwa na maandishi MSHAURI NASAHA. Kilikuwa
ni chumba kipana ambacho kilikuwa na vitu vingi
sana. Nilishindwa kuelewa chumba cha mshauri
nasaha kinakuwaje na vitu vya ajabu namna ile.
Upande wa kushoto kulikuwa na kabati kubwa
ambalo lilikuwa na vitabu vingi. Upande wa kulia
kulikuwa na mlango mdogo ambao ulikuwa
unaingia kwenye chumba kingine kidogo. Mezani
kulikuwa na vitabu vingi huku nikivutiwa na kile
ambacho kilikuwa na jalada jekundu huku
kikipambwa na picha ya bastola.
Nikaanza kufunua kitabu kile ambacho kiliandikwa
kwa lugha ya kiingereza. Nilivutiwa sana na kitabu
kile. Lever action pistols ndivyo maandishi ya
ukurasa wa kumi wa kitabu kile yalivyoanza.
Kulikuwa na picha ya bastola ambayo chini ilikuwa
na maandishi yaliyokolezwa kwa wino mweusi
Volcanic Pistol .41 cal. Nikatabasamu kwani
lilikuwa somo zuri kwangu. Nilisoma kuwa aina hii
ya bastola ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja na
Horace Smith na Daniel B Wesson, hii ilikuwa ni
mwaka 1854. Aina hii ya bastola ilitengenezwa
Norwich. Baada ya kuanguka wamiliki hawa wawili
kiuchumi ikawa chini ya Oliver F Winchester.
Alianza kumiliki kampuni inayomiliki silaha hiyo
July 1855. Baada ya hapo jina la bastola hiyo
likabadilishwa….. Sikuweza kumaliza maelezo
kuhusu bastola hiyo kwani Jerry alikuwa amefika
kutoka kwenye chumba kile kidogo.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

Lever action pistols ndivyo maandishi ya ukurasa
wa kumi wa kitabu kile yalivyoanza. Kulikuwa na
picha ya bastola ambayo chini ilikuwa na
maandishi yaliyokolezwa kwa wino mweusi
Volcanic Pistol .41 cal. Nikatabasamu kwani
lilikuwa somo zuri kwangu. Nilisoma kuwa aina hii
ya bastola ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja na
Horace Smith na Daniel B Wesson, hii ilikuwa ni
mwaka 1854. Aina hii ya bastola ilitengenezwa
Norwich. Baada ya kuanguka wamiliki hawa wawili
kiuchumi ikawa chini ya Oliver F Winchester.
Alianza kumiliki kampuni inayomiliki silaha hiyo
July 1855. Baada ya hapo jina la bastola hiyo
likabadilishwa….. Sikuweza kumaliza maelezo
kuhusu bastola hiyo kwani Jerry alikuwa amefika
kutoka kwenye chumba kile kidogo.
“Naitwa Jerrome Mtuvu ukipenda niite Jerry ni
afisa usalama wa Taifa kitengo maalum!” Alianza
kujitambulisha huku akipanga panga mafaili
mbalimbali pale mezani, nikakumbuka hata yule
Jerry mnafiki alianza kujitambulisha kama huyu.
“Nashukuru sana bwana Jerry kukutana na wewe
saa hizi!” Nikatulia kidogo na kumwangalia Jerry
ambaye alikuwa ametulia sana pale nilipoanza
kuongea. Nikaanza kumsimulia kuanzia mwanzo
wa tukio mpaka mwisho. Alikuwa ametulia huku
maelezo yale yakiingia moja kwa moja kwenye
kifaa maalum ambacho alikuwa anatumia kurekodi
mazungumzo yangu.
“Umesema muheshimiwa Stefano Kenge pia
anahusika! Unaweza kunifafanulia anahusika vipi?”
Aliniuliza huku akizidisha utulivu ambao badala ya
kunifariji ulionifanya nimuogope.
“Ndiyo anahusika kwa asilimia tisini!”
“Kama ningekuwa Jaji ungenithibitishia vipi ili
niweze kumtia hatiani?” “Ungekuwa Jaji ingekuwa
vigumu kidogo lakini kwa kuwa ni wewe
nitakueleza vitu vitatu ambavyo vinanifanya niwe
na uhakika wa asilimia tisini kuwa anahusika.
Moja ni maelezo niliyoyapata kutokana na barua
ya Ommy, pili ni ushahidi niliopewa na Johari kuwa
muheshimiwa huyo alitakiwa kufanyiwa kafara
ambayo ingehusisha kuchinjwa kwake na mwisho
ni mimi mwenyewe ambaye nilimshuhudia pale
kituoni akiongea na yule Jerrome wa uongo
aliyekuja kunihoji hatimaye kunitorosha!” Nikatulia
na kumkazia macho Jerry.
“Nini kilikutuma kumfuata stella kule Kinondoni?”
“Kama nilivyokueleza bwana Jerry watu hawa ni
hatari sana kiasi kwamba yeyote anayeonekana
kunusa au kutaka kunusa mambo yao basi hukumu
yake ni kifo! Hivyo kitendo cha Stella kuandika
makala ambayo inakaribia ukweli kilinifanya
nitambue wazi kuwa uhai wa Stella uko
mashakani”
“Uliwezaje kukaa na siri nzito namna hiyo badala
ya kuitoa katika vyombo husika?”
“Njia zangu zote zilikuwa zimefungwa nilikuwa
kama mtumwa niliogopa sana kuhusu ile picha na
kubwa zaidi lililonichanaganya ni kuhusika kwa
baadhi ya askari kwenye mkasa huu!” Baada ya
mahojiano ya hapa na pale nikamuona akibadili
mwelekeo wa mazungumzo yetu nilishindwa
kuelewa anakusudia nini.
“Umeshapata mpenzi baada ya kifo cha Betty!”
Swali hilo kidogo lilinishangaza, “sijapata!”
Nilimjibu kwa mkato
“Ningefurahi sana kama angekuwa Johari !”
Nikatabasamu kisha nikashindwa kujizuia
nikacheka.
“Kwanini awe yeye?”
“Kutokana na masimulizi yako inaonesha kuwa
umemthamini sana kiasi cha kutumia nguvu
kumuokoa basi hata yeye atakuthamini maisha
yako yote!” Kwa mara nyingine nikatabasamu
lakini sikusema lolote. Nikainamisha kichwa chini
huku nikitafakari juu ya kauli ile, alikuwa
amenigusa.
“Bwana Kajuna nashukuru sana kwa ujio wako na
natumai tutashirikiana vema!” Aliongea huku
akinitazama kwa upole, kisha akaendelea.
“Kwa sasa naomba nikuruhusu uende, kesho
naomba tukutane hapa saa 4.00” Alimaliza kisha
tukaagana. Kidogo hili lilinishangaza. Niliona swala
lile amelifanya kuwa rahisi mno. Afisa wa idara ya
usalama tena wakutoka kitengo cha operesheni
maalum kwanini asiniwekee utaratibu mzuri wa
ulinzi badala yake kirahisi rahisi tu eti ananiambia
nenda!
Niliondoka pale ofisini nikiwa mnyonge sana,
sikutegemea kama swala zito kama lile
lingemfanya mtu mwenye wadhifa mzito serikalini
aniruhusu hivihivi baada ya kuniuliza maswali
ambayo hata polisi wa kawaida wangeuliza.
Ghafla, nikiwa nimeliacha kabisa eneo lile
nikakiona kitu ambacho kilinishtua sana. Ilikuwa ni
maeneo ya gerezani. Sikuamini! Alikuwa ni mmoja
kati ya watu niliowaona kule Mbagala.
Nilimtazama vizuri nikamkumbuka. Alikuwa yule
askari Bandia ambaye alikuja Hospitali akazusha
tafrani kubwa baada ya kuua. Nikasimama eneo la
wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama
wamachinga. Nilitaka kujua yule mtu ataelekea
wapi.
Muda mfupi baadae akaja mtu mwingine mnene
mfupi ambaye alivaa suti nyeusi. Wakapeana
mikono kisha wakaondoka eneo lile kuelekea
maeneo ya mtaa wa Lindi. Nikaendelea kuwafuata
kwa tahadhari kubwa. Baadae wakaingia mtaa wa
Kongo. Bado sikusita kuwafuata. Wakaingia
kwenye duka moja la madawa na vifaa vya
Hospitali. Nikasimama nje takribani dakika ishirini.
Walipotoka walikuwa na boksi kubwa ambalo bila
shaka lilikuwa na dawa mbalimbali. Wakaondoka
na kuelekea maeneo ya Msimbazi. Wakasimama
pale klabu ya simba. Nikasogea karibu kiasi cha
kuweza kusikia maongezi yao.
“Vipi lakini kuna matumaini ya kupona!” Aliuliza
yule askari feki kwa sauti ya chini sana. Matumaini
ni makubwa mno kwani tumefanikiwa kuondoa ile
risasi……….” Sikuweza kusikia maneno ya mwisho
kwani gari lilikatisha na kuleta kelele ambazo
zilinifanya nishindwe kusikia maneno ya mwisho.
Bado magari yaliendelea kukatisha kwa uwingi na
kusababisha nikose kusikia maneno yote
yaliyoendelea.
Dakika chache baadae ikaja gari ambayo
niliitambua sana. Ni ile Rav 4 nyekundu ambayo
mara nyingi ilikuwa inatumiwa na Bonge. Wale
watu wawili wakaingia kwenye ile gari. Sikupata
tabu kuifuata ile gari kwani msongamano wa
magari ulikuwa mkubwa. Wakaingia barabara ya
uhuru. Kutokana na msongamano mkubwa wa
magari niliendelea kutembea kwa miguu hadi
maeneo ya shule ya uhuru huku lile gari likiwa
halijapotea machoni mwangu.
Nikafika kwenye kituo cha teksi cha shule ya
uhuru. Mmoja wa madereva teksi akanifuata kwa
kasi.
“Twende bosi wangu!” Alinidaka haraka na
kunihimiza niingie kwenye gari lake. Teksi lake
halikuwa na ufito wa rangi ya yoyote kama yale
mengine ambayo yalikuwa na ufito wa njano.
Kutokana na haraka niliyokuwa nayo sikuweza
kujiuliza sana.
“Wapi bosi!”
“Naomba tuifuatilie ile Rav4 nyekundu!” Nilisema
huku nikimuonesha kwa kidole ile gari ambayo
ilikuwa kwenye foleni.
“Poa!” alijibu kwa mkato.
Safari yetu ilitufikisha barabara ya Mandela, huku
foleni ilikuwa imepungua ingawa hapa na pale
tulilazimika kusimama.
“Hizi foleni zinakera sana!” Niliongea kwa sauti
iliyojaa hasira.
“Mbona hata wewe unakera!” Alinijibu dereva kauli
ambayo ilinishangaza.
“Aaah, acha utani bwana mimi sijawahi kumkera
mtu!” Nilimjibu huku nikijifanya kuichukulia
kawaida kauli yake.
“Si kweli, kero yako ni kubwa kama usingekuwa
kero usingefuatilia watu kama hivi unavyofanya
kufuatilia mambo yasiyokuhusu!” Safari hii kauli
yake ilinitisha zaidi. Kisha akatoa kauli nyingine
ambayo ilinitisha zaidi.
“Mbona maovu yako hakuna anayefuatilia?” Hapa
sikuweza kuficha hasira zangu. “Naomba
unishushe hapa!” Nilitamka kwa hasira.
“Utashuka tu lakini usisahau hii picha yako!”
Akatoa ile picha yangu ya Tabata. Lilikuwa pigo
jingine kubwa katika moyo wangu.
“Naomba nishuke tafadhali!” Sasa niliongea kwa
ukali zaidi.
“Hutaki kwenda kumuona majeruhi wako !” Sauti
nzito ilitoka nyuma yangu. Sijui nilikosa vipi
umakini kiasi cha kushindwa kuwagundua watu
wawili ambao walijificha siti za nyuma. Ilikuwa ni
uso kwa uso na Martin.
Hasira zake hazikuweza kufichika. Nadhani alikuwa
anatamani aniue pale pale lakini mazigira yalikuwa
hayaruhusu.
“Mtoto mdogo umevuruga mambo mengi sana!”
Aliongea yule mwingine ambaye alikuwa mgeni
machoni kwangu.
“Leo utapata malipo kwa kufungua mzigo!”
Ailiongea Martin kwa sauti kavu iliyojaa hasira.
Bastola mbili zilikuwa zimelenga kichwa changu.
Sikuwa na la kufanya zaidi ya kukaa kimya.
Nilikuwa nimenasa. Hakuna muujiza ambao
ungeniokoa kwenye tukio hilo. Nilikuwa nategemea
zaidi muujiza, sikuwa mjuzi wa kupigana kiasi cha
kupambana na majitu mawili yaliyoshiba namna
ile. Gari ilionyoosha kuelekea Ubungo kupitia
barabara ya Mandela.
Nilikuwa sielewi tena tunaelekea wapi kwani akili
yangu ilikuwa haina nguvu yake ya kawaida.
Nilikuwa nusu Mfu. MZIGO umeniponza. Katika
nafsi yangu nilimlaumu sana Jerry kwa
kutolichukulia ‘sirias’ suala langu.
Ghafla, nikahisi kitu kizito kikinigonga kichwani.
Nikaanza kujiona kama ninayefunikwa blanketi zito
lisilo hata na nafasi ya kutoa hewa. Nikapotea,
nikapotea……….Sikumbuki kitu tena baada ya hapo
ingawa neno la mwisho nililosikia ni sauti ya
Martin aliposema” lazima achinjwe leo
akicheleweshwa atazusha balaa lingine kubwa!”
Kisha kikafuata kicheko kikubwa ambacho kilikuwa
kama radi. Baada ya hapo sikuwa tena katika
dunia ya kawaida. Nilikuwa nusu mfu.
***

Nilifumbua macho yangu, nikahisi maumivu makali
ya kichwa. Taa yenye mwanga mkali ikanipiga
usoni. Bado akili yangu ilikuwa na uwezo wake wa
kawaida. Ingawa ilinichukua dakika mbili kuweza
kujitambua. Nilikuwa nimelazwa kwenye kitanda
kikubwa huku nikiwa nimetundikiwa dripu ya maji.
Hakukuwa na mtu kule chumbani. Mandhari ya
chumba ilinishangaza. Kilikuwa ni chumba kipana
chenye madirisha makubwa. Nilishindwa kubaini
hawa watu wana lengo gani. “Kwanini wameniacha
hai mpaka saa hizi wakati mimi ni adui yao namba
moja!
Niliendelea kuisanifu mandhari ya chumba kile,
haikuwa na kitu cha ajabu zaidi ya vitu vya
kawaida ambavyo unaweza kuvikuta kwenye
chumba cha kijana yeyote ambaye kayapatia
maisha karibuni.
Wakati nikiendelea kukisanifu chumba kile mlango
ukafunguliwa. Maajabu! Msichana mrembo
akaingia.
“Waooo, Umeamka mpenzi!” Aliongea kwa sauti
nyororo yenye kuvutia. Lilikuwa ni jambo lingine la
ajabu. Akanisogelea na kunibusu shavuni.
“Vipi unajisikiaje?” Alinisaili.
“Najisikia vema!” Nilijikakamua kumjibu huku
nikificha mshangao wangu. Akanihudumia kama
mgonjwa yeyote anavyostahiki kuhudumiwa.
Akanionesha upendo wa hali ya juu sana.
Maigizo mengine?
“Samahani sister, hivi hapa ni wapi nimefikaje na
wewe ni nani?” Uvumilivu ulinisahinda nikalazimika
kuuliza. Akacheka kabla ya kujibu. Usihofu Kajuna,
mimi nina uwezo wa kujibu swali moja tu, mengine
utajibiwa na wahusika!”
“Kina nani hao wahusika?”
“Usihofu utawajua tu muda ukifika!”
“Haya nijibu sasa hilo unaloweza kunijibu!”
“Naitwa Beatrice Kamugisha ni muuguzi katika
hospitali ya Hindu Mandali”
“Kwa hiyo hapa ni Hindumandal!”
“hapana!”
“Ni wapi sasa?” Akatabasamu kabla ya kunijibu.
“Usiwe na haraka mimi sijaruhusiwa kujibu swali
kama hilo!” Alinijibu huku tabasamu lake likiwa
halijafutika usoni. Nilishindwa kuelewa kilichokuwa
kinaendelea.
Muda mfupi baadae nikaanza kuhisi usingizi nzito
ukininyemelea . Nikajitahidi kupambana na hali ile
lakini haikusaidia kitu. Nikalala.
***

Nilipoamka kwa mara nyingine macho yangu
yakakutana na sura ya Beatrice ambaye alikaa
kando ya kitanda changu. “Amka ule mpenzi!”
Aliongea kwa sauti ya kubembeleza.
Hivi huyu anatania au kuna ukweli….. mpenzi
mimi?
Nilijiuliza huku nikitofautisha kabisa hadhi yangu
na yake.
Ni utani tu! Nilijibu mwenyewe.
“Kajuna!” Aliita Beatrice kisha akaanza kuongea.
“Kuna wageni wanahitaji kuonana nawe,
wameniambia kama unajisikia vizuri niwaruhusu
lakini kama bado hali yako si mzuri basi
watakutana nawe siku nyingine” Kwa jinsi
nilivyokuwa na udadisi moyoni hata kama hali
yangu ingekuwa mbaya vipi bado nilihitaji kuonana
na huyo mgeni hata kama atakuwa Bonge na kundi
lake.
“Waruhusu niko tayari!” Nilijibu haraka kwa shauku
ya kutaka kuwaona hao wageni.
Kama ni mshangao basi kwangu ilikuwa zaidi ya
mshangao. Nashindwa kueleza kitu kinachozidi
mshangao kinaitwaje! Huyu hapa Ommy alikuwa
mbele ya macho yangu! Sikutegemea kama
nitakuja kumuona tena. Pamoja naye alikuwa Jerry
na mzee wa makamo ambaye sura yake ilikuwa
ngeni machoni mwangu. “Ommy!” Niliongea kwa
mshtuko mkubwa
“Kajuna!”Naye alionekana kuwa na mshangao
kama wangu.
“Siamini kama ni wewe kweli!”
“Ndiyo mimi Kajuna rafiki yangu!”

ITAENDELEA
 
MWISHO SEHEMU YA KWANZA.

Kama ni mshangao basi kwangu ilikuwa zaidi ya
mshangao. Nashindwa kueleza kitu kinachozidi
mshangao kinaitwaje! Huyu hapa Ommy alikuwa
mbele ya macho yangu! Sikutegemea kama
nitakuja kumuona tena. Pamoja naye alikuwa Jerry
na mzee wa makamo ambaye sura yake ilikuwa
ngeni machoni mwangu. “Ommy!” Niliongea kwa
mshtuko mkubwa
“Kajuna!”Naye alionekana kuwa na mshangao
kama wangu.
“Siamini kama ni wewe kweli!”
“Ndiyo mimi Kajuna rafiki yangu!” Tulitazamamana
dakika kadhaa bila kuongea chochote. Katika nafsi
zetu ilipita furaha na faraja ya hali ya juu.
Tukapeana mikono ya furaha huku tukiitingisha na
kuzikumbuka siku chache zenye matukio mazito
tulizokaa kwenye urafiki wetu.
Jerrome Mtuvu ambaye muda wote alituacha
tumalize furaha yetu akasogea pale kitandani. Yule
mzee wa makamo alikuwa amekaa kwenye kiti
huku akituangalia jinsi tulivyokuwa na furaha.
“Samahani kwa kukukatishieni furaha yenu ya
kukutana!” Aliongea Jerry kwa sauti tulivu kisha
akaendelea.
“Bwana Kajuna naomba utambue uwepo wa
mkurugenzi mkuu wa idara usalama wa taifa hapa
nchini Dokta Zakaria Mkude, siku tatu mfululizo
alikuwa anakuja hapa ili aongee nawe lakini kwa
bahati mbaya ulikuwa haujarudiwa na fahamu!” Ina
maana niko hapa kwa siku tatu au zaidi!
Nilistaajabu.
“hivyo basi sioni sababu ya kuongea kwa niaba
yake wakati mwenyewe akiwa hapa” Bwana
Zakaria Mkude akasogezewa kiti karibu na kitanda
changu.
“habari Ndugu Kajuna!” Alinisalimia baada ya
kuketi kwenye kiti alichowekewa. “Nzuri
shikamoo!”
“Marhaba,awali ya yote naomba nitoe shukrani
kubwa na dhati kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambaye alitaka kuonana
nawe lakini majukumu ya kitaifa yamesababisha
akose fursa hiyo adhimu. Pili naomba nikupongeze
kwani jina lako limeingia kwenye orodha maalum
ya Mashujaa wa nchi hii, hivyo hata kama utakufa
leo au kesho basi unastahiki kuzikwa kwa heshima
zote za kijeshi, Kimsingi kazi uliyoifanya ni kubwa
na unastahili sifa, Umejitoa kwa moyo wako wote
kupambana na watu ambao wamekuwa
wakiendesha mauaji ambayo yamelitia Doa kubwa
Taifa letu. Taifa letu si kisiwa cha amani tena
kama kilivyokuwa kikijulikana kutokana ya wenzetu
wenye ulemavu wa ngozi. Tena ajabu! Tanzania
imekuwa soko zuri kwa watu wa Burundi na
Rwanda kuja kufanya biashara hiyo. Tumekuwa na
sifa mbaya kiasi cha kuwaambukiza jirani zetu
tabia hii ya kishetani. Kwa msaada wako
tumeweza kugundua mtandao mkubwa wa
wahusika wa biashara hii ambayo ni ya
udhalilishaji. Hivi ninavyokueleza yule waziri anaye
husika ameshakamatwa baada ya kupata kibali
maalum kutoka kwa Rais. Sina mengi ya kuongea
nimelazimika kuacha shughuli zangu kutokana na
uzito wa kazi ulioifanya hivyo utamaliza shughuli
yako kwa kushirikiana nasi bega kwa bega ingawa
kimsingi hii kazi ilibidi tuifanye sisi lakini itakuwa
ngumu bila msaada wako kwani wewe unafahamu
mengi zaidi.” Akatulia na kuniangalia kwa macho
yaliyojaa upole. Ingawa alikuwa mzee lakini
alikuwa na mwili mkakamavu. Akasimama, akanipa
mkono ikiwa ni ishara yakuagana na kutakiana
heri.
***

Baada ya kuondoka yule mzee nikamgeukia
Jerrome Mtuvu!
“Hivi hapa ni wapi pia nataka kujua nimefikaje?”
Hilo lilikuwa swali ambalo nililirusha moja kwa
moja kwa Jerry. Ni kama aliyelitarajia swali hilo.
Akakaa pale kwenye kiti ambapo alikuwa amekaa
mkuu wake wa kazi.
“ Ningekuwa mjinga na mtu nisiyeijua kazi yangu
kama nisingefuatilia nyendo zako baada ya kutoka
pale ofisini. Baada ya kupata simu yako tu, eneo la
mnazi mmoja tayari lilikuwa na vijana kumi
maalum ambao walikuwa wanafuatilia kuanzia
ujaji wako hadi uondokaji wako. Ulipoondokapale
ofisini nilikuwa makini kuwasiliana na vijana wangu
kwa nyendo zako zote. Nilifanya hivi kwa sababu
mbili tofauti moja kanuni hazikutaka nikuamini
mapema kiasi kile hivyo niliamua kukufuatilia ili
nijue mengi kuhusu wewe kama ni mkweli au ni
muhusika halisi wa mauaji. Pili nilifanya hivyo ili
kama ulichozungumza ni sahihi basi uwe chini ya
uangalizi maalum kwani inaonesha ulikuwa
unawindwa kila kona! Ndiyo maana ulipofika mitaa
ya Gerezani hukujua kama ulikuwa umeshaingia
kwenye mtego wa wale jamaa. Wale waliokuwa
mbele yako walijua wazi kuwa uko nyuma yao
wakakuchelewesha makusudi huku wakiwasiliana
na wenzao wengine kwa meseji bila wewe
kutambua. Nikaelezwa yote hayo na vijana wangu.
Baada ya kuona hatari imekuwa kubwa kiasi hicho
ndipo nikaamua kuingia rasmi. Ulipofika Karume
ukatekwa hiyo ikawa fursa nzuri kwetu ya kuweza
kukufuatilia. Nikiwa na vijana wangu wenye
mafunzo maalum tukakufuatilia hadi ulipoingizwa
kwenye nyumba moja kubwa kule kunduchi, Baada
ya muda mfupi tukawaona wale watekaji
wakiondoka! Tukaiweka chini ya uangalizi mkali ile
nyumba ili kuhakikisha hautolewi mle ndani. Baada
ya hapo nikapiga simu polisi nyumba ikawekwa
chini ya ulinzi wa polisi, wote waliokuwa humo
ndani wakakamatwa. Nikakuchukua wewe na
kukuleta huku kwa ajili ya matibabu kwa sababu
tulikukuta ukiwa umepotelewa na fahamu!”
Nikashusha pumzi baada ya kusikia kisa hicho cha
kusisimua.
Kama hao watekaji wa mwanzo waliwahi kuondoka
basi Martin atakuwa hajakamatwa! Niliwaza huku
nikiwa na wasi wasi. Beatrice akaja pale kitandani
akaondoa ile dripu niliyotundikiwa kwani maji
yalikuwa yameisha. Kisha akaondoka tena na
kutuacha watatu mle chumbani. Nikamgeukia
Ommy.
” Vipi Ommy nini kimekusibu baada ya kuachana
siku ile?”
“Nafikiri mengi nilikueleza kwenye barua yangu
kwa kuchelea wale watu kunigundua nikaamua
kuitelekeza nyumba yangu kwa muda kwani kama
wale watu wangediriki kunifuatilia vizuri basi
wangegundua wapi ninaishi, Nami nikaanza
kuwawinda, nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka
kujua vile viungo vya albino vinatumika kwa kazi
ipi! Nikaenda hadi kule Kongowe. Nikapindukia
ndani ya lile jengo ambalo ulipeleka ule mzigo.
Nilipofika pale watu wote walikuwa ndani. Kwa
kuwa ilikuwa ni usiku niliweza kujificha nje karibu
na dirisha la chumba ambacho ndani alikuwepo
Samson Kipusa au Bonge kwa jina ulilozoea pia
nikashtushwa na uwepo wa Mheshimiwa waziri wa
Bunge na vikao vya serikali Bwana Stefano Kenge.
Kwa kuwa taa ilikuwa inawaka ndani ya chumba
kile niliweza kuwachungulia vizuri bila ya wao
kuniona kwani taa ya nje ilikuwa haijawashwa.
Mjadala wao ulikuwa ni wa kutisha sana kwani
kulikuwa na raia wanne wawili kutoka Burundi na
wawili wengine walikuwa wanatoka Rwanda. Hawa
walikuwa wameleta Viungo kutoka katika nchi zao.
Baada ya kujadiliana wakakubaliana walipe shilingi
milioni Mia moja kwani walileta viungo vya albino
sita. Nilishtuka sana kwani sikutegemea kabisa
kama jambo hili linaweza kufanywa na mtu mzito
kama yule!”
“Enhee ikawaje?” Niliuliza huku nikiwa na shauku
kubwa ya kusikiliza habari ile ambayo ilikuwa
inasisimua sana.
“Baada ya kukubaliana bei wakawaomba wale
wageni watoke kidogo mle chumbani ili waweze
kujadili, Mjadala huu ndio ulionifunulia sura halisi
ya Mheshimiwa. Ni chui ndani ya ngozi ya kondoo
kwani waziri alitoa amri kuwa wale wageni
wauwawe na wazikwe mle ndani! Hapo
nikakumbuka jinsi ulivyotegewa bomu kwenye lile
brifkesi lakini Mungu alikuwa upande wako! Baada
ya dakika kama kumi nikaanza kusikia vilio mle
ndani kisha kukawa kimya bila shaka wale jamaa
walikuwa wameuwawa! Duh, wale jamaa watu
hatari sana kuua kwao ni jambo dogo sana. Baada
ya hapo nikarudi nyumbani haraka nikaandika ile
barua kisha nikapanga kuwa sitarudi nyumbani
mpaka nisikie mheshimiwa Stefano Kenge
amekamatwa. Kutokana na kuchanganyikiwa na
tukio lile nikaamua kwenda ikulu ili niweze
kuonana na Raisi nimueleze tatizo hili.
Kabla sijaonana na rais nikakamatwa na walinzi
wa ikulu. Ishu ile ikapewa uzito mkubwa kuliko hali
halisi nikapelekwa Idara ya usalama wa Taifa
kwenda kuhojiwa huko nikakutana na Jerrome
Mtuvu ambaye nilikuwa namfahamu kupitia kwa
mdogo wake ambaye niliwahi kufanya naye kazi
kambi moja wakati nikiwa mwanajeshi. Yeye ndiye
aliyenipa namba ya kaka yake wakati niko jeshini.
Ndiyo ile namba niliyokuandikia kwenye barua!”
Baada ya kuhojiwa nikapata msaada mkubwa
kutoka kwa Jerrome kwani nilifichwa sehemu
maalum wakaanza upelelezi wao wa chinichini!”
Akatulia na kunikazia macho. Nikashusha pumzi
kwa mara nyingine.
“Kitu kimoja nilitaka kusahau, Mheshimiwa Stefano
Kenge anataka kutangaza nia ya kugombea uraisi
hivyo anatumia kafara na mazindiko ili aweze
kuingia ikulu!” “Unafikiri nini kitatokea iwapo
viongozi washirikina wataingia madarakani?”
nilimuuliza.
“Siwezi kujua nini kitatokea, iwapo hata hao
ambao tunaamini sio washirikina hatuoni
wanachokifanya sijui wakiingia washirikina
itakuwaje!”
“Lakini nasikia waganga wa jadi hupata wateja
wengi kipindi ambacho uchaguzi unakuwa
umekaribia!”
“Unamaanisha nini?” Aliniuliza Jerrome ambaye
muda mrefu alikuwa kimya. “Inawezekana kuwa
viongozi wetu wengi ni washirikina!” Nilimjibu.
“Usirudie tena hiyo kauli wakikusikia watakujadili
bungeni kuwa umewadhalilisha!” Aliongea Ommy
na kutufanya mimi na jerry tuangue vicheko.
“Nafikiri Hali yako ni mzuri Kajuna tutakuacha
hapa kwa siku nne ukipumzika na kupata matibabu
madogo madogo!” Aliongea Jerry.
“Lakini bado sijafahamu hapa nilipo ni wapi?”
“Hapa ni kunduchi na hii ni nyumba maalum ya
serikali ambayo hutumika kwa shughuli maalum
tu!”
“Kama shughuli ipi kinyume na hii?”
“Nitakujibu kwa kifupi na baada ya hapo sitapenda
udadisi zaidi kuhusu hii nyumba. Wakati mwingine
kuna maraisi ambao hufanya safari za siri ambazo
hazijulikani nchini kwao na haziwi wazi hapa
nchini huwa wanafikia hapa!” Kweli sikutaka
kuuliza tena. Nilielewa kwanini aliniambia
nisiendelee kuuliza kuhusu ile nyumba.
Hatimaye muda wa kuagana nao ukafika,
wakaondoka na kuniacha peke yangu. Muda huo
niliwaza mambo mengi sana ndipo nikawakumbuka
stella na Johari . Sijui kwanini nilisahau
kuwazungumzia kwa Jerry. Hata hivyo inaonesha
hata Jerry alisahau kuuliza kuhusu yule
mwanamke. Kutokana na uwepo wa Stela niliamini
wazi kuwa atatoa msada kwa Johari ambaye
kisaikolojia alihitaji msaada mkubwa na ukaribu.
Hakutakiwa kupata nafasi ya kutosha kukumbuka
matukio yale ya kusikitisha. Kama angepata muda
wa kutosha kukumbuka tukio lile basi ingeweza
kusababisha arudiwe na msimamo wake wa kutaka
aachwe kwenye mikono ya wahalifu.
Wakati nikiogelea kwenye bahari ile ya mawazo
mara, yule nesi akaingia tena. “Karibu mpenzi!”
Nilimkaribisha tena kwa namna ya utani ambayo
mwenyewe ndiye aliyeianzisha.
“Hivi ilikuwaje ukapata fursa ya kufanya kazi
huku?”
“Mimi nimfanyakazi wa Hindumandal lakini pia ni
mwajiriwa wa Idara ya usalama wa Taifa kitengo
cha tiba, pia mimi si nesi kama unavyoniona kwa
ishara ya mavazi ni daktari bingwa wa mifupa”
Nilitosheka sikuwa na swali lingine.

12
Ilikuwa ni siku miongoni mwa siku ambazo
sitazisahau katika maisha yangu. Ni kumbukumbu
nyingine mbaya kabisa kuwahi kutokea. Haiwezi
kufutika kwenye kumbukumbu zangu abadani.
Ilikuwa ni Jumanne tulivu. Jerry alinifuata, ilikuwa
ni siku ambayo Jerry aliniambia natakiwa kukutana
na tume maalum iliyoundwa na kamati maalum
iliyoundwa na Mheshimiwa Rais kutafuta chanzo
na tiba ya mauaji ya albino. Nakumbuka siku hiyo
Jerry hakuwa na furaha kabisa. Alikuwa mtu
mwenye huzuni na mawazo mengi.
Kuna nini? Nilijiuliza!
Nilimuona akiwa mwenye hasira kali na kukunja
ngumi kwa hasira, vitu vingi alikuwa akiniashiria
kwa mkono tu. Jinsi alivyokuwa niliogopa hata
kumuuliza. Macho yake yalikuwa yameiva na
kufanya wekundu.
Huyu alikuwa na jambo tu, tena jambo zito!
Nilishindwa kabisa kumuuliza.
“Twende!” Alisema kwa kauli fupi huku maelekezo
mengine yote yakifuata kwa ishara. Nilipotoka nje
ndipo nilipobaini kuwa jengo lile lilikuwa ni la
ghorofa nne. Lilikuwa karibu na shule ya sekondari
ya Wasichana ya Kunduchi. Halikuwa mbali na
kitengo maalum cha Sayansi ya bahari cha chuo
kikuu cha Dar es salaam.
“Vipi kuna nini leo Jerry!” Nikauliza baada ya
uvumilivu kunishinda.

ITAENDELEA
 
MWISHO SEHEMU YA PILI

Nilimuona akiwa mwenye hasira kali na kukunja
ngumi kwa hasira, vitu vingi alikuwa akiniashiria
kwa mkono tu. Jinsi alivyokuwa niliogopa hata
kumuuliza. Macho yake yalikuwa yameiva na
kufanya wekundu.
Huyu alikuwa na jambo tu, tena jambo zito!
Nilishindwa kabisa kumuuliza.
“Twende!” Alisema kwa kauli fupi huku maelekezo
mengine yote yakifuata kwa ishara. Nilipotoka nje
ndipo nilipobaini kuwa jengo lile lilikuwa ni la
ghorofa nne. Lilikuwa karibu na shule ya sekondari
ya Wasichana ya Kunduchi. Halikuwa mbali na
kitengo maalum cha Sayansi ya bahari cha chuo
kikuu cha Dar es salaam.
“Vipi kuna nini leo Jerry!” Nikauliza baada ya
uvumilivu kunishinda.
“Mambo si mazuri Kajuna tutaongea vizuri tukifika
ofisini. Tukaingia ndani ya gari Toyota land
cruiser. Haikutuchukua muda mrefu kufika mnazi
mmoja. Tukapanda ngazi za jengo lile taratibu
huku nikiwa na hofu kubwa ya kwenda kusikia nini
kilichotokea. Kidogo hali ya Jerry ilikuwa imerudi
kawaida ingawa hakuweza kuongea chochote .
Ghafla, nikamuona akibadilika kutoka kwenye
furaha na sura yake kurudi kama mwanzo.
“Bwana kajuna umekutana na mengi sana umeishi
katika kipindi cha mpito, kipindi kigumu ajabu!
lakini kubwa ninaloweza kusema ni kuwa Mungu
amekuchagua kulikomboa taifa kutoka kwenye aibu
kubwa inayolikabili. Mara nyingi yamekuwa
yakitokea mauaji ya albino lakini vyombo vya
usalama havijapata ufumbuzi wa kadhia hiyo,
hivyo ninachokiona hapa ni kuwa Mungu
amekuchagua, kwa kuwa Mungu amekuchagua
basi unatakiwa uwe mfano wa manabii…..”
Akatulia kidogo na kunikazia macho huku akiniacha
kwenye mshangao mkubwa zaidi.
” Umepoteza mpenzi, nasikitika kukufahamisha
kuwa umepoteza rafiki pia lakini naomba haya yote
yasikurudishe nyuma Taifa linakutegemea kwani
mambo uliyofanya ni mazito na yanastaajabisha”
Akatulia kidogo na kuonesha huzuni na wasiwasi
wa kile anachotaka kukizungumza.
“Naomba ieleweke kuwa wote hawa wanaingia
kwenye historia kama wapigania haki za binadamu
tuwaombee Mungu huko waliko” Akatulia huku
akiwa ameshika tama.
Niliogopa sikutaka aniambie kuwa Ommy naye
kauwawa, sikutaka kabisa kusikia habari hiyo
moyo ulienda mbio. Ingawa alishatanguliza pole
kwa kueleza juu ya mpenzi wangu lakini pia
aligusia rafiki jambo lililonitia hofu. Nilikuwa
natetemeka. Nafikiri umeona vitu vya kutisha vingi,
kidogo utakuwa mzoefu. Bado sikumuelewa.
“Nifuate!” Aliniamrisha nami nikamfuata kuelekea
kile chumba kidogo. Kulikuwa na jokofu moja
kubwa, niliogopa kutokana na fikra nilizoanza
kuwa nazo kuhusu Ommy. Akafungua lile jokofu
nikamtazama kwa hofu kubwa zaidi. Nilikuwa
natamani kumzuia lakini nilikuwa nimeyavulia nguo
maji. Nilikuwa nimeushika mkono wake kwa nguvu
ili asifungue lakini nilishachelewa Akafungua!
***

Tulifika maeneo ya Posta saa 12.30 jioni. Nilikuwa
sina raha. Kitendo cha Ommy kuuwawa na
kuachwa bila kiwiliwili kilinifanya nitamani sana
kukutana na Samsoni kipusa ‘Bonge’. Nilikuwa
nimemchukia kuliko mtu yeyote duniani. Sikuwa na
uhakika kama risasi niliyompiga siku ile kule
Mbagala ilimuua au ilimjeruhi. Mtu wa pili
niliyemchukia zaidi ni Martin kisha nilihisi chuki
kwa wote wanaohusika na mauaji ya albino.
Angalau sasa nikiwa na Jerry nilikuwa najihisi
kuwa na amani. Picha ya kichwa cha Ommy
ambacho nilikiona kwenye jokofu ilinitia simanzi
kila iliponijia kichwani. Wakati tukipanda ghorofa la
jengo lile la wizara ya mambo ya ndani
nikakumbuka kitu,nilikuwa sijamuuliza jerry Ommy
kauwawa vipi?
“Hivi ilikuwaje Ommy akauwawa?”
“Ni hadithi fupi sana, tulipoondoka hapa na
kukuacha Ommy aliniomba afike nyumbani kwake
mara moja maana ni siku nyingi hajafika huko.
Sikumzuia kwa sababu nilijua wewe ndio
unayetafutwa zaidi kuliko Ommy. Sikuweza
kufikiria kuwa anaweza kuandamwa kiasi kile.
Nikashangaa kuona siku ile hakurudi tena. Jambo
hilo likanitia mashaka tukajaribu kuwasiliana na
vituo vyote vya polisi, ndipo siku ya pili tukapata
taarifa kuwa Polisi wameokota kichwa cha mtu
huko Kigamboni. Nikafuatilia ndipo nikabaini kuwa
Ommy ameuwawa.
Uchungu niliousikia siku hiyo ulinikumbusha kifo
cha Betty. Huzuni yangu ikakusanya majonzi ya
misiba miwili. Kwanini mimi, Rafiki sina, mchumba
nae…..
***

Saa 12.45 Tuliingia katika moja miongoni mwa
ofisi nyeti katika jengo lile. Moyo wangu ulianza
kwenda kasi tena. KATIBU MKUU, maandishi hayo
makubwa yalikuwa kwenye kibao chembama
ambacho kilikuwa mbele ya meza moja ndefu
kikimtambulisha mtu mnene ambaye alikaa mbele
ya meza ile. Licha ya yule mnene kulikuwa na watu
wengine mle ndani, niliogopa sana. Wengi wao
sura zao hazikuwa ngeni machoni mwangu.
Niliweza kumwona Kamanda wa polisi wa Tanzani
IGP akiwa miongoni mwa watu waliohudhuria
mkutano huo ambao sikuutarajia. Kulikuwa na
watu wapatao watano.
“Karibu Jerry vipi umetuletea mgeni?” Sauti nene
ya yule mzee ilisikika. Jerry akanionesha kiti
nikaketi. Wageni au watu waliokuwepo mle ndani
walionekana kushangazwa na ujio wangu. Ni wazi
kuwa hawakupewa taarifa hapo kabla.
“Tulikuwa tunakusubiri bwana Jerry, umechelewa
sana!” Sauti nyingine ya mtu ambaye nilikuja
kutambua baadae kuwa ni naibu waziri wa mambo
ya ndani ilisikika.
Jerry hakusema kitu akaenda moja kwa moja
mpaka kule mbele ambako kulikuwa na kiti karibu
kabisa na kile cha katibu mkuu. Nilishindwa
kuelewa Jerry ana cheo gani mpaka aonekane
kuwa muhimu kiasi hiki. Akakaa.
“Kwanza niwaombe radhi kutokana na kuchelewa
kwangu!” Alianza Jerry huku akipangusa uso wake
kwa kitambaa. Kisha akaendelea
“Kuchelewa kwangu kumekuwa na faida kwetu na
kwa kikao chetu cha leo, lakini kabla sijafika huko
naomba niwatambulshe kwenu huyu kijana ambaye
anaitwa Kajuna!” Baada ya kutaja jina hilo wote
wakanigeukia na kunikazia macho.
“Nafikiri jina lake sio geni kwenu huyu ndio yule
kijana tuliyekuwa tunamtafuta sana tukimuhusisha
na mauaji hapo kabla. Pia napenda kukupa haki
yako Bwana kajuna kwa kukutambulisha hawa
waliopo hapa mbele ni tume maalum iliyoundwa na
muheshimiwa Rais kuchunguza mauaji ya albino
yanayoendelea hapa nchini, kutokana na uzito na
ugumu wa jambo lenyewe tume hii imekuwa
ikifanya kazi yake kwa usiri mno. Kutoka kulia ni
naibu Waziri wa Ulinzi na usalama wa raia
Muheshimiwa Hashim Bakari, anayefuata ni mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini Bi Anna Ngonyani wa tatu
ni Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani Enerst
Shadi, huyo mwingine ni mkurugenzi wa usalama
wa Taifa Bwana Zakaria Mkude na mwisho ni
kamishina maalum wa jeshi la polisi bwana
Stefano Nyimbo!” Akatulia na kunikodolea macho
“Pia yupo Jaji Sebastian Pinda ambaye nafikiri
hayuko mbali na eneo hili kwani niliambiwa nae
atakuwepo hapa!” Kabla hajamaliza kuongea
mlango ukafunguliwa akaingia mtu ambaye nilihisi
kuwa ndiye Jaji aliyetajwa. Sikukukosea kwani
Jerry alinitambulisha kwa huyo Jaji. Baada ya
hapo Jerry akaanza kutoa habari zangu kuanzia
mwanzo hadi nilivyokutana nae.”
Ukafika muda ambao nilitakiwa kuthibitisha kama
yale yaliyosemwa na Jerry ni ya kweli.
Nikathibitisha huku nikikumbusha baadhi ya
vipengere ambavyo vilisahaulika. Ilikuwa ni
mshangao wa wazi katika macho yao. Bila sahaka
ni kutokana na vile nilivyotafsirika mwanzo kuwa ni
muuaji na miongoni mwa wahusika wa biashara
hiyo ambayo haikubaliki kabisa.
Ikafika zamu ya maswali, nikaulizwa maswali
mengi lakini nikayajibu kwa ufasaha. Katika
maisha yangu sikutegemea kama itatokea siku
ambayo nitapeana mkono na waziri, Kwa mara ya
kwanza nilijikuta nikipewa mikono na watu hawa
nyeti serikalini tena kwa heshima kubwa. Kwa
mara ya kwanza toka nianze kukabiliana na tukio
hili nilianza kuhisi furaha kwenye nafsi yangu.
Angalau wazee hawa ambao walikuwa kwenye
kikao maalum cha kutafuta ufumbuzi walinipa
moyo.
Nikamkumbuka sana afande Edwin ambaye
alikuwa anataka kuning’oa meno bila ganzi,
nilitamani sana angekuwepo akaona jinsi wakubwa
wake walivyoniheshimu na kunithamini. Kama si
kifo cha Ommy basi hii ilikuwa ni siku ambayo
ningefanya sherehe, kupeana mkono na Jaji, waziri,
katibu mkuu na mkurugenzi wa nini sijui huko juu,
lilikuwa jambo la faraja kwangu.
Ukafika muda ambao maazimio yalitakiwa
kupitishwa, jambo la kwanza lilikuwa ni kusaidiwa
mzigo, ikaamuliwa kuwa kuanzia muda huo kamati
ile nyeti ndiyo itakayokuwa na jukumu la
kuwatunza Stela na Johari pia liliwekwa azimio la
kufanyika upelelezi wa siri ili kuwabaini wote
waliokuwa wanashirikiana na muheshimiwa Waziri
kufanya vitendo vile vya kishetani. Sambamba na
hilo nilipewa heshima kwa kupewa nakala ya
upelelezi wao wa mwanzo pale walipoishia. Katika
nakala hiyo iliwagusa zaidi wavuvi wa samaki
ambao walikuwa wakitumia viungo hivyo vya
binadamu wenzao kwa dhana kuwa vinasaidia
kupata samaki wengi. Haikuwa nakala ambayo
ilionesha uozo wa viongozi, labda kwa sababu
mbele ya jamii kiongozi alionekana mtu safi asiye
na tatizo lolote. Kwaya, nyimbo, mashairi na
ngonjera vilimfanya aonekane mtu safi mbele ya
jamii.
***

Saa 3.11 tulifika maeneo ya Yombo Abiola,
tukaenda moja kwa moja nyumbani kwa Ommy
ambako Stela na Johari niliwaacha huko. Huku
nikiwa na furaha niligonga mlango kwa nguvu
kidogo. Nililakiwa na ukimya. Nikagonga mara ya
pili lakini bado kulikuwa kimya. Tukatazamana na
Jerry. Nikaanza kushikwa na hofu. Nikashika
kitasa na kufungua. Ndani kulikuwa na giza. Moyo
ulikuwa unapiga kwa nguvu sana. Ujasiri na furaha
niliyokuwa nayo vikatoweka. Nikapapasa ukutani
nikaipata swichi. Nilipowasha taa ndipo nilipozidi
kuingiwa na woga. Damu ilikuwa imetapakaa pale
sakafuni. Hakukuwa na yeyote mle ndani.
Jerry akatembea kwa kutumia vidole vya mbele
vya miguu yake huku akiwa na bastola mkononi.
Aina hii ya bastola nilikuwa sijawahi kuiona hata
katika filamu. Baadae alinifahamisha kuwa ilikuwa
inaitwa Luger au P00 Parabellum ilianza kutumiwa
na majeshi ya kiswisi mwaka 1900 hadi 1949.
Akaufikia mlango wa chumba ambacho walikuwa
wanalala Stela na Johari , mlango ulikuwa
umefungwa.
“Johari ni mimi Kajuna, fungua tafadhali!” Nikasikia
nyayo za mtu ambaye alikuwa anakuja kufungua
mlango. Nilijiuliza maswali mengi ndani ya muda
mfupi sana. Ina maana stella amekufa? Au ni
Johari …… Swali lolote nililotaka kujiuliza
lilikatishwa na mtu aliyefungua mlango ule. Jerry
alikuwa mwepesi ajabu. Kitendo cha kitasa cha ule
mlango kuguswa tu Jerry alikuwa ameruka na
kujibanza upande wa kushoto wa ukuta ulioshikilia
mlango ule. Nilishusha pumzi baada ya kumuona
aliyefungua mlango ni Johari .
“Stella yuko wapi?” Lilikuwa ni swali lililokuja
ghafla kabla hata ya salamu.
“Yupo huku chumbani.
“Na hizi damu…”
“mbona hutulii kwanza tukusimulie?” Nikamuona
stella akitoka mle chumbani. “Tulivamiwa aliongea
stella huku akionesha wazi kuwa na hofu.
“Watasimulia kwenye gari kwa sasa hili eneo
lishaonekana halina usalama!” aliongea Jerry
baada ya kugundua kuwa wote wako salama.
Tukiwa kwenye gari stella akaanza kusimulia jinsi
walivyovamiwa na mtu mwenye kisu. Walijitahidi
kupambana naye. Stela aliweza kumpiga huyo
jamaa kwa stuli usoni. Inasemekana jamaa alivuja
damu vibaya lakini aliwahi kukimbia. Kutokana na
maelezo yao nikabaini huyo mvamizi hakuwa na
uhusiano na kundi la Bonge, alikuwa ni mwizi wa
kawaida ambaye alibeba kisu ili aweze kujihami
ikitokea dharura.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA MWISHO.
Tukiwa kwenye gari stella akaanza kusimulia jinsi
walivyovamiwa na mtu mwenye kisu. Walijitahidi
kupambana naye. Stela aliweza kumpiga huyo
jamaa kwa stuli usoni. Inasemekana jamaa alivuja
damu vibaya lakini aliwahi kukimbia. Kutokana na
maelezo yao nikabaini huyo mvamizi hakuwa na
uhusiano na kundi la Bonge, alikuwa ni mwizi wa
kawaida ambaye alibeba kisu ili aweze kujihami
ikitokea dharura.
Jerry aliendesha kwa kasi kutokana na bara bara
kutokuwa na msongamano muda huo. Ni Jerry
pekee ndiye aliyekuwa anajua wapi tunaelekea.
Tukaiacha barabara ya Pugu tukafuata ile ya
Mandela. Saa 4.02 tulikuwa maeneo ya Mbezi
Luis. Tukafika mbele ya jumba moja kubwa.
Tulipofika karibu na lango akapiga honi mara tatu.
Mlango ukafunguliwa na mtu ambaye nilihisi kuwa
ni mlinzi. Tukashuka kwenye gari tukasalimiana na
yule mlinzi, kisha tuka tambulishwa kwa mlinzi
ambaye alikuwa anaitwa Ibrahim Kondo.
Tukaachwa ndani ya Jumba lile ambalo halikuwa
na watu wengine mle ndani, lakini ajabu! Lilikuwa
na kila kitu.
13
Tulikaa ndani ya jumba lile kwa siku tatu huku
tukiwa chini ya uangalizi maalum wa Jerry. Jambo
ambalo lilinifurahisha ni kutembelewa na tume ile
iliyoundwa na Rais. Pamoja na furaha niliyokuwa
nayo bado nilitamani sana kukutana na Bonge.
Ommy na Betty walinifanya nitamani sana
kukutana naye. Kama ile bastola niliyompiga siku
ile ilimpata basi ni heri kubwa na kama ilimjeruhi
LAZIMA NIMUUE.
“Hivi humu ndani tutakaa hadi lini?” Aliuliza Stella
na kunikatisha mawazo yangu. “Nafikiri saa ya
ushindi ikifika!” Nilimjibu huku nikimiminia maji
kwenye glasi. “Unafikiri tutashinda?” Aliuliza tena
“Tutashinda lakini vita itakuwa ndefu!”
“Kivipi?” Safari hii Johari naye alinirushia swali.
“Hata wakikamatwa hawa wanaotusumbua bado
kuna mlolongo wa watu wenye roho za kishetani
ambao wana mawazo kama yao!”
“Hao utapambana nao vipi?”
“Haliwezi kuwa jukumu langu peke yangu ni jamii
mzima hususani viongozi wa dini ndio hasa
wanatakiwa kubadilisha nyoyo za watu.”
Huku nikiwa kwenye lindi la mawazo nikasikia
lango linafunguliwa, nikachungulia dirishani.
Alikuwa ni Jerry. Nikamuona akiliingiza gari lake
sehemu ya kuegeshea. Baada ya kushuka
akatembea taratibu kuja kule tuliko. Muda huo
Stella na Johari wao walikuwa chumbani kwao
wakitazama runinga. Urafiki wao ulinifariji sana
kwani angalau Johari alianza kurudi kwenye hali ya
kawaida. Mara mlango ukafunguliwa, Jerry akiwa
mwenye furaha alikuja pale nilipokaa akanisalimia
huku akinishika mkono kwa nguvu na kuutikisa
kwa furaha.
“Leo Rais katoa kibali cha kukamatwa
muheshimiwa mwingine!” Aliongea Jerry huku
akionesha furaha ya wazi kabisa
“Ni nani huyo muheshimiwa?”
“Naibu waziri wa Bunge!”
“Naye pia anahusika?”
“Yeye na mkuu wake wote wanahusika!”
“Saa ngapi atakamatwa?”
“Hivi ninavyozungumza vijana kutoka makao
makuu ya polisi wameelekea nyumbani kwake
wengine ofisini kwake ili kokote ambako atakuwepo
muda huu aweze kukamatwa!”
“Na wale wengine?”
“Tunaandaa kikosi maalum unatakiwa kujiandaa
kwani leo usiku utatupeleka huko iliko nyumba ya
Samson Kipusa”
“Ina maana tajiri mkubwa kama yule mulikuwa
hamfahamu wapi anaishi?” “Hapana, yule ana
nyumba yake Mbezi inaonesha hiyo nyumba
ambayo wewe umeitaja ni maalum kwa shughuli
zao!”
Habari ile ilikuwa ya kufurahisha kwangu. Niliona
masaa yakienda taratibu mno.
***

Hali ilikuwa tulivu mno, usingeweza kuamini kuwa
hii ndio ile barabara ya Mbagala ambayo inakuwa
na msongamano mkubwa wa magari.
Magari yalikuwa machache mno hivyo kuifanya
safari yetu mimi na Jerry kuwa rahisi.
“Umechukua bastola yako?” Aliuliza Jerry.
“Ndiyo” “Naomba niione!” Nikampa.
“Hii sio mzuri, chukua hii ya kwangu!” Akanipa
bastola nyingine ambayo haikuwa nzito kama ile
ya kwangu.
“We, utatumia nini?”
“Kisu na mikono!” Nilimwangalia kwa mshangao.
Tukafika maeneo ya Kongowe. Tukaicha gari kwa
mlinzi wa shule ya sekondari ya St.Matthews.
Tukatembea taratibu kana kwamba tunaenda
harusini.
“Tangulia!” Jerry alinihimiza. Nikawa mbele
akaniacha takribani hatua kumi. Ule upande ambao
tulitoroka nikiwa na Johari ndio tulioutumia
kuingilia ndani.
Ndani kulikuwa na nyasi na maua ambayo
hayakutuzwa vizuri. Tukasikia nyayo za mtu
ambaye alikuwa anakuja kule nyuma. Jerry
akakimbia kwa kasi bila kufanya vishindo akaenda
kuegemea ukuta wa jengo lile. Nikataka kumfuata .
Akaniashiria kwa mkono kuwa nisimame pale pale.
Huyu jamaa ananiuza nini? Niliwaza baada ya
kuona sehemu ambayo aliniambia nisimame ni ya
wazi mno.
Nikasimama palepale. Dakika chache baadae
akatokea mlinzi.
“We nani?” aliuliza mlinzi huku akijiweka tayari
kwa kwa shambulizi. Hakuwahi kufanya lolote,
nilishuhudia aina ya mateke ambayo nayaona
kwenye filamu za kichina likitua katikati ya koo la
yule mlinzi.
“Kumbe Jerry ni mtu hatari namna hii?” Niliwaza
baada ya kumuona yule mlinzi akianguka kama
gunia. Akaniashiria kwa mkono niende kule aliko.
Nikamfuata bila kusita. Akaniamrisha nilale chini.
Tukaanza kutambaa kama nyoka, nilikuwa nasikia
maumivu ya tumbo lakini nilivumilia na kufuatisha
vile alivyokuwa anafanya.
“We Pembe uko wapi?” Ilisikika sauti nyingine.
“Njoo huku!”Alisema Jerry jambo lililinifanya
niingiwe na hofu kwani lazima yule mtu
angeshangazwa na sauti ile.Huyu alikuja na tochi.
Alishaanza kuingiwa na mashaka. Sijui ni staili
gani ilitumiwa na Jerry kuinuka pale chini kwani
hata kwenye sinema nilikuwa sijawahi kuiona.
Nilimshuhudia akimrukia yule jamaa na kumpiga
kabali ya nguvu. Baada ya dakika moja yule jamaa
alikuwa hajitambui. Akamlaza pale chini
tukaondoka.
“Inaonesha kulikuwa na walinzi wawili tu huku
nje!” Sikumjibu nikaendelea kumfuata . Tukaingia.
Ndani kulikuwa kimya bila shaka hakukuwa na
watu mle ndani. Tulitembea kwa kujiamini ndani ya
nyumba ile kubwa. Wakati tunasonga mbele
tukasikia sauti ya watu waliokuwa wanaongea.
Jerry akachungulia kwenye tundu la ufunguo la
chumba kilichokuwa kinasikika sauti za watu”
“Tuondoke hatari!” Alininong’oneza.
Kama tulivyoingia ndivyo tulivyoondoka.
“Tuna bahati sana Kajuna, kazi itaisha mapema
kuliko nilivyofikiria!” Aliongea tukiwa mbali kidogo
na eneo lile.
“Kwa nini?” Nilimuuliza.
“Karibu wahusika wote muhimu wako humu ndani
bila shaka wana kikao muhimu!” Tulikuwa tumefika
pale tulipoliacha gari. Tukangia kwenye gari .Gari
iliendeshwa kwa kasi kubwa mpaka nikahisi kuwa
ajali iko karibu. Sikujua kwanini Jerry aliamua
kuondoka badala ya kuwa shambulia wale jamaa.
Tulitumia dakika kumi na mbili tu kutoka Mbagala
hadi makao makuu ya jeshi la Polisi.
“Nisubiri hapo kwenye gari!” alisema huku
akikimbia kuelekea ndani ya jengo lile la makao
makuu ya Polisi. Baadhi ya polisi waliokuwa pale
nje walimsimamisha kwani aliwatia hofu kwa
kitendo kile cha kukimbia. Alipotoa kitambulisho
chake kila mmoja alisimama pembeni baada ya
kumpa heshima yake ya kiaskari.
Dakika chache baadae alikuwa anashuka kutoka
kwenye jengo lile la makao makuu ya jeshi la polisi
nchini. Nyuma yake alikuwa anafuatwa na askari
polisi mwenye nyota moja begani.
“Samahani Kajuna, wewe utakuja na askari ambao
watahitaji msaada wako kwa kuwaelekeza eneo la
tukio.”
Akaniacha kwa Polisi yule mwenye nyota moja.
Akaondoka kwa kasi kurudi Mbagala.
***

Hali ilikuwa shwari hivyo kuruhusu msafara wetu
wa magari matatu kuwa huru barabarani. Bastola
ambayo nilikuwa naitumia ilishachukuliwa na Jerry.
Mimi nilikuwa sina silaha ya aina yoyote kitendo
ambacho kilinikosesha raha sana.
Tulikuwa tunakaribia kufika eneo la tukio jukumu
langu lilikuwa ni kuwaelekeza tu ndio maana
sikupewa silaha.
Dakika chache baadae tukawasili eneo la tukio.
Nikaambiwa nibaki pale kwenye gari. Kwa unyonge
nikakaa pale nikiwaangalia askari jinsi
walivyokuwa wanagawana pande za nyumba ile.
Nilishangaa sikumuona Jerry kwenye kundi lile.
Wakati nikimfikiria Jerry nikashtushwa na Mlipuko
wa silaha. Askari walikuwa wamepindukia ndani.
Nikawa nasikia mfululizo wa milipuko hiyo. Ingawa
nilikuwa na hamu ya kwenda moja kwa moja eneo
la tukio nilijikuta nikitetemeka pale nilipokaa.
Upande wa kushoto wa nyumba ile nilimuona mtu
akiruka ukuta na kuanza kukimbia, Mungu wangu!
Alikuwa Martin. Nilijilaumu kwanini
sikung’ang’ania kupewa silaha kwani
ningeuburudisha moyo wangu kwa kumlipua muuaji
huyu.
Nikaanza kusikia vilio vya watu ambao bila shaka
walikuwa wamepigwa risasi huko ndani. Nilimuona
wazi Martin akiingia kwenye jengo moja bovu.
Kabla sijaamua lolote kuhusu Martin nikaona lango
la nyumba ile likifunguliwa. Nikawaona askari
wawili wakiwa wamebeba kitu kama machela.
Waliposogea karibu ndipo nilipogundua kuwa
walikuwa wamembeba Samson Kipusa. Alikuwa
hajiwezi. Bila shaka alikuwa anatibiwa mle ndani
kutokana na risasi niliyompiga siku niliyotoroka.
Nilijisikia furaha sana kumkomesha mshenzi huyu.
Akaletwa mle kwenye gari.
“Kijana muangalie huyu” aliongea askari mmoja
huku wakirudi tena ndani. Hakuwekwa kwenye gari
alilazwa pale nje, leo utajiri wake haukuwa na
thamani tena. Duh! Kweli mshahara wa dhambi ni
mauti. Askari walifanya kazi yao inavyotakiwa.
Nilimwangalia Bonge alikuwa anapumua kwa shida
sana. Nikamfuata pale chini alipolazwa
Nikamkandamiza kwa nguvu kisha nkamziba pua
na mdomo. Jamaa alitapatapa hatimaye akakata
roho. Nikarudi pale niliposimama huku nikijihisi
utulivu moyoni.Nilifanya hivyo kwa kuchelea
maamuzi ya mahakama kwani kama angesimama
mahakamani akatumia pesa zake vibaya ungesikia
kaachiwa huru au kafutiwa makosa ya mauaji na
sasa anashtakiwa kwa kosa la kutumia utajiri wake
vibaya au kosa la kutotoa taarifa mapema. Kosa
hilo lingemfanya aumikie kifungo cha miezi sita au
mwaka mmoja.
***

Saa 8. 54 kazi ilikuwa imekwisha kwani Martin
aliuwawa baada ya kuwaelekeza Polisi kule
alikojificha. Huku tukiwa na furaha tulikuwa
tunarudi uwanja wa vita. Katika msafara wa kurudi
tuliongezewa magari manne kwani tulikuwa na
maiti nne za majambazi na mateka saba. Upande
wetu alijeruhiwa askari mmoja tu! Wananchi wengi
wa maeneo ya Kongowe na Mbagala rangi tatu
walishangazwa na milipuko ya risasi. Wengi
walikuwa nje ya majumba yao baada ya kusikia
ving’ora vya polisi. Walisimama kando ya
majumba, nahisi walikuwa wanajiuliza maswali
yasiyo na majibu kwani hawajawahi kuona
msururu wa magari ya polisi kama ambao
niliongozana nao siku hiyo. Wengine walikuwa
wamevaa misuli, wengine mabukta tu, kwa upande
wa kina mama wengi wao walitoka na kanga moja
huku wengine wakiwa na magauni ya kulalia tu.
Ama kwa hakika lilikuwa tukio la aina yake.
Nilikuwa na furaha mno kurudi tena kwenye
ulimwengu wa kawaida. Angalau sasa nilijua kuwa
jina langu litakuwa safi mbele ya jamii.
Saa 9.36 nilifika mafichoni kwetu kule Mbezi.
Stella na Johari walikuwa sebuleni eti walisema
kuwa hawakulala walikuwa wananisubiri kwa hamu
ili wajue nini kimetokea. Niliwasimulia kila kitu
kilichotokea.
***

Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya tatu baada ya tukio
lile la kuvamia Mbagala. Afrika mashariki ilitikiswa
kwa habari nzito za kukamatwa kwa waziri na
naibu wake, Mbunge na wafanyabiashara kadhaa
kwa tuhuma za biashara ya ngozi za binadamu na
ushirikina wa kutumia viungo vya Albino. Watu
wengi walionekana kwenye vituo vya kuuzia
magazeti. Ni siku ambayo magazeti yaliisha
mapema sana. Habari hizo zilinisafisha na kunitaja
kuwa shujaa. Nilijihisi kama mtu niliyezaliwa upya.
Wakati nikiwa kwenye furaha ile mara akaingia
Jerry.
“Kajuna nina habari za kufurahisha sana kwako,
serikali imekuzawadia nyumba kubwa ya kifahari,
gari pia una nafasi ya kwenda kusoma huko Cuba
kwani kuanzia sasa wewe ni muajiriwa katika idara
yetu!” Nilikuwa kama naota sikuamini.
“Hivi ninavyokuambia nimeitwa ofisi ya Rais
kufuatilia barua yako pia Rais anataka kuonana na
wewe!”
Hilo la Rais kuonana na mimi lilinitisha sikuona
kama ninauwezo wa kukabiliana na Rais katika
maongezi. Jerry akaondoka akatuacha mimi Stella
na Johari .
“Leo nataka nikawasalimie wazazi wangu!”
Niliwaambia Johari na Stella. “Kajuna!” Stella
aliniita kwa sauti ndogo wakati naelekea chumbani
kwangu. Nilipogeuka akanitazama kwa aibu kisha
akatamka neno ambalo hata Johari alilisikia.
“Nakupenda!” Neno hilo lilikuwa kama kisu kwenye
moyo wangu. Pale niliposimama nilikuwa nawaona
vizuri wote wawili, Johari akatembea kwa haraka
kunifuata kule niliko. Akanishika mkono na
kunivutia kwake kisha akaninong’oneza sikioni.
“Kajuna umeniokoa, sasa unataka kuniua?” Kabla
sijamjibu nikashikwa mkono mwingine na Stella.
Johari akaja mbele yangu akakilaza kichwa chake
kifuani pangu. Kila mmoja alikuwa anaonesha
mapenzi kwangu. Nikawa navutwa huku na huku
hali iliyoniweka njia panda. Ghafla, Stela akaniacha
na kumfuata Johari, kidogo niliingiwa na wasiwasi.
“Johari!” Alisikika Stela kwa sauti iliyotulia.
“Nakutakia maisha mema na kajuna. Nampenda
hilo liko wazi lakini nahisi wewe una haki zaidi
kwake…………” Hakumaliza machozi yalikuwa
yanadondoka na kufanya michirizi kama ya
chemchem inayokaribia kukauka.
Nikamtazama tena Johari kwa macho yaliyojaa
mapenzi, nikamvuta upande wangu.
Nikamkumbatia kwa nguvu.
“Nataka kufunga ndoa na wewe Johari uko tayari?”
Akacheka na kuruhusu mwanya wake wa kuvutia
kujidhihirisha katika macho yangu.
“Uamuzi wa busara!” Alisikika Stela ambaye
alikuwa nyuma yangu. Nilipogeuka nikamuona
anatabasamu. Machozi yalikuwa yamekauka.
MWISHO
 
Wlly Gamba nakuamini mwisho ufikapo ndo mwanzo wa nyingine tunakungoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom