RIWAYA: Kikosi cha Pili

RIWAYA: Kikosi cha Pili

Sehemu ya 23*


Meja Salim komba aliwasha gari yake na kuingia barabarani,alitaka kukutana na Zedi chalinze bar kama kawaida yao ili amshirikishe katika jambo alilodokezwa na makomando walioko nchini Kongo kinyume cha taratibu.

Akakanyaga mafuta na kuzidi kuiacha Msata,lakini kitu ambacho hakujua ni kuwa wakati anaondoka nyumbani kwake kuna mtu alikuwa akimtizama,na kuondoka kwake machoni mwa mtu yule nae akapiga simu anakokujua kutoa taarifa ya kuonekana kwa meja kuifunga safari kusiko julikana.
****
Ibra mbaya ndie aliepokea simu yenye taarifa za nyendo za Meja Salim komba,akatabasamu kidogo na kujipa tafakari kidogo

"Baada ya miaka mingi hatimae leo naenda kukutana na mbaya wangu,atashangaa kuniona mbwa yule,na kama alidhani nimekufa au kuzeeka basi leo nitamwonesha mimi huwa sifi kizembe na..."

Ibra hakumalizia kauli yake akasikia tusi zito likimtoka dereva wa gari lao aliekuwa akijaribu kuliweka sawa gari baada ya kupitwa na gari flani kwa kasi ya ajabu.

Ibra mbaya alipojua kisa cha dereva wao kutukana akaamuru dereva alifukuze gari lile na alipite au amsimashe wazungumze kwanini anaendesha usiku kwa mwendo ule,dereva nae akatii ukawa mfukuzano wa magari mawili ya mahisimu ambao hawakujuana wakati huo.

Meja Salim komba ndie alikuwa wa kwanza kufika pale bar,akapaki gari lake na kushuka kisha akaangaza kushoto na kulia hakuona mtu akachepuka kidogo na kulisogelea gari lingine na kufungua mlango kisha kukaa ndani ya gari lile huku mawazo yakipita kichwani pake.
***
Zedi alipolipita gari lile hakuwa na Shaka nalo,lakini kadri muda ulivyokuwa unazidi kusogea ndivyo alivyohisi tofauti hasa pale gari lile lilipoanza kumfuata nyuma kwa kasi mara kwa mara dereva wa gari lile akimulika taa kumpa ishara zedi asimame.

Ili kujiridhisha na hisia zake akapunguza mwendo wa gari lake na kuwa kama anaetaka kusimama,na kabla hajatimiza azma yake akavaa mawani zilizomsaidia kuona kizani hata nyuma ya kioo kisha akasimama.

Wakati gari lile lilipokuwa likimpita kwa mbele ili lisimame alipata kuona watu watatu wakiwa wamekaa viti vya nyuma huku mmoja Kati yao akiwa na bastola mkononi na hapo akajiwa na hisia mbaya zaidi.

Baada ya gari lile kusimama,tofauti na matarajio yao Zedi yeye akiingia barabarani na kukanya mafuta hadi mwisho na kufanya kina Ibra wasipate tena kumuona japo walijitahidi kumfukuzia lengo wamtie adabu mtu yule,ila ni kwa kuwa hawakujua adui yao ndie walie mwacha awatangulie kufika kwa Meja Salim komba.

Meja Salim komba alimwona zedi wakati akipaki,akampa ishara ya kijasusi,nae akapaki pembeni na kuchepuka kuingia ndani ya gari lile alilokuwako Meja.

***
Walitazamana kisha Meja akasema
"wako wapi wageni wangu uliosema upo nao?"
Zedi hakujibu kitu akageuka na kutizama nyuma,jambo lile likamfanya Meja nae ageuke na hapo akashuhudia wanaume wanne wakiteremka haraka haraka ndani ya gari lao na kuliendea gari la Zedi na kuanza kulilagua.

Meja Salim hakuwa anawajua watu wale ila alijua ni watu wa kazi,pia hakujua kwanini wanajiamini vile lakini majibu aliyapata baada ya mmoja wa watu wale kuvua kofia kwa minajili ya kujikuna kichwa.
Alimanusura Meja salimu komba augue kifafa baada ya kumtambua mtu yule kwa msaada wa taa za nje ya bar ile na akajikuta akitamka taratibu kwa mzubao
"Ibra Mbaya"
Baada ya kutajwa jina hilo tu Zedi nae akageuka kutazama nae mwili ukamfa ganzi kwa sekunde kadhaa..
***


Nb:karibu kwenye kundi la riwaya la whatsapp kwa malipo ya Tsh 2500/=
Karibu usome riwaya ya KISA CHA WAFU riwaya ya kipelelezi na mambo ya dunia ya pili,karibu usome elimu ya Tafakari(meditation)ndani ya riwaya hii.
Karibu usome riwaya ya UTATA na nyinginezo namba kwa ajili ya whatsapp
0658564341

Kwa malipo ni 0758573660

Asalaam Kudo
 
SEHEMU YA 24*


REJEA NCHINI KONGO

Baada ya koplo Makame na Koplo Ziga kutoka nyumbani kwa papaa Deo Mukamba,safari yao ilikuwa ni kuifuata gari iliokuwa imetegeshwa kifaa cha kusoma eneo au GPS katika lugha ya watalamu.

Safari yao iliwafikisha hadi Shelaton Hotel, wakatafuta maegesho ya gari yao hotelin pale,kisha akaanza kushuka Koplo Makame na kutangulia kuingia ndani.

Alikuta ndani kumefurika watu wa aina mbalimbali,wazungu wachache na waafrika wengi wakiwa wamekaa kwenye viti huku kila mmoja akiburudika na akipendacho.

Koplo Makame akachagua eneo zuri la kukaa huku akitizama eneo la mlango wa kuingilia ndani ya hotel ile.

Mhudumu alimfikia na kumuuliza atakacho,yeye Kwa makusudi akaagiza supu ya pweza huku akijua nchini Kongo ni nadra sana kukutana na chakula kile.

Mhudumu aliaga baada ya kushindwa kukidhi matakwa mteja wake.

Akiwa palepale kakaa akamwona msaidizi wa mtu waliemfuata akiwa anatoka ndani ya Hotel ile kisha alipofika nje kidogo ya mlango akatokea mtu mwingine na akawaona wakiteta jambo kwa muda mfupi kisha msaidizi yule akarudi ndani.

Koplo Ziga na yeye akatokea,ila yeye hakwenda kukaa akapitiliza Mika kwa moja hadi ulipo mlango wa kuingilia ndani ya Hotel akiwa kama mteja anaetafuta chumba cha kulala.

Alipofika ndani na yeye akapata kushuhudia msaidizi yule akiishilizia kuzipanda ngazi kwelekea vyumba vya juu.

Alimfuata binti aliekuwa mapokezi kisha yeye akajitambulisha kwa jina la Msuke Paul ni mjumbe kutoka Afrika ya kusini na anahitaji kuonana na Waziri wa Michezo kutoka Tanzania.

Mhudumu yule akawa mgumu kutoa ushirikiano ila kwa hila za komando yule mbobezi akadanganywa kwa cheki bandia kama hongo na mhudumu akakubali kuonesha kilipo chumba cha Waziri wa michezo Tanzania bwana Muruga Wesa.

Koplo Ziga akazipanda ngazi na kutokea juu kulipokuwa na korido pana huku kukiwa na vyumba kadhaa kushoto na kulia kwake.

Akazidi kujongea huku macho yake yakiwa makini kutazama kushoto na kulia kutafuta chumba namba 15C.

Haikumchukua muda akakiona,kwa tahadhari kabisa akakisogelea chumba kile na kutega sikio ili kusikia chochote mle ndani na hakusikia akitakacho.

Akasukuma mlango kuujaribu kama upo wazi nao ukasukumika ishara ya kuwa upo wazi.

Kwa hila kabisa akausukuma ukabaki wazi huku yeye akiwa hajaingia bado.

Akasikilizia kwa sekunde kadhaa kisha bila kujishauri akadunda na kudondondokea ndani bila kutoa kishindo huku bastola yake ikiwa mkononi kwa lolote.

Ajabu chumba kilikuwa kitupu na kwa mbali alisikia maji yakimwagika upande kulipokuwa na chumba cha maliwato,hapo akajua mlengwa wao yupo huko.

Akatazama kushoto na kulia ndani ya chumba kile hakuona cha maana akataka kumfuata mheshimiwa hukohuko maliwato ila akasita baada ya kuona kumpyuta mpakato ikiwa kitandani na ipo wazi ikimaanisha ilikuwa ikitumiwa muda mfupi uliopita.

Kwa haraka akaipekuwa na kukutana na mafaili kadhaa ila faili moja ndani ya kompyuta ile lilimsutua lilikuwa limeandikwa "TIKISA".

akalitazama kisha akataka kulifungua akakutana na neno lilohitaji aweke nywila au neno la siri katika lugha rahisi.

Kichwa kikamgonga kwa wahka,akafikiri kidogo kisha akabinya sikio lake yakatoka maneno machache kumfikia Koplo Makame aliekuwa nje nae akaelekeza machache yakamrudia koplo Ziga.

Koplo Ziga akajaribu alichoambiwa na kweli kikazaa matunda na alichokikuta ndicho kilichomshawishi awasiliane nchini Tanzania kwa njia ya email na Meja Salim Komba alie amini anaweza kumpa utatuzi japo kwa hapo walipofikia walikuwa hawamwini mtu na alituma kucheza pata potea.

Akiwa anatafakari cha kufanya mlango wa kuingilia ukagongwa kwa nguvu roho yake ikaruka sarakasi za vandame,.

Maliwatoni kuna mtu na mlangoni kuna mtu hadi hapo papara isingemsaidia.....

****

Unangoja nini kujiunga kwenye group la whatsapp fanya hivyo sasa

Lakini pia bado napoke mchango wa kiasi chochote na kwa yeyote na achangiae ataingia kwenye group hilo bila garama nyingine
Karibuni
0758573660
0658564341


Asalaaam Kudo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom