SEHEMU YA 26*
CHALINZE USIKU
wakiwa wametulia ndani ya gari,walizidi kuwatizama wale watu wanne walivyokuwa wakihaha kumtafuta mmliki wa gari ile iliowapa usumbufu njiani.
"Unaonaje tuwasombe au!" aliuliza Meja Salimu Komba
"Ngoja tuone nia yao ni nini,ni kulifuata gari na mmliki wake au walikuwa wanajua wanaemfuata"akajibu Zedi.
***
Ibra Mbaya hakuona umuhimu wa kuendelea kuizunguka gari ile,japo kumkosa mhusika lilikuwa ni kosa walilolifanya na hawakuwa na namna ya kuliacha lipite.
Akawaamuru vijana wake waendelee na safari ili wawahi kuikamilisha hatua yao wanayoitarajia kuipiga kwa kumwondoa Meja Salimu Komba.
Ibra na vijana wake wakati wakiondoka waliacha mjadala nyuma yao,mjadala wa Meja na Zedi.
"Hii ni hatari sana kuonekana kwa mwanaharamu yule" aliongea Meja
"Nashangaa hata Mimi amewezaje kuwepo wakati niliona kabisa mwisho wake kule Uganda,na aliendelea vipi kuwasiliana na watu wa hapa?" aliongea Zedi kwa kuuliza
"Hata Mimi sina jibu kama wewe ila ni hatari sana na naona nchi inaenda kuingia kwenye machafuko muda wa usoni" alisema Meja
"Sasa na huko wanaenda kufanya nini ?" aliuliza Zedi kana kwamba anaemuuliza anajibu
"Sijui Zedi lakini nadhani..." Meja Salim Komba hakumalizia kauli yake Zedi akadakia
"Watakuwa wamegundua uhusika wako na mimi na wanaenda kukupa salamu za mauti"
Kauli ile ikamtetemesha kwa hasira Meja Salim komba na bila kujiuliza akapiga ngumi hewani kwa kukabwa koo la uchungu na kisha akasema
"Hawajui kuteleza kwa nyoka ni ishara ya kulipa windo uzubaifu,wasidhani mimi ni nge asimamishae mkia huku akijua hana mfupa wa kuzuia kuvunjika kwa mgongo wake,washa gari tuwafuate sijazeeka bado"
Zedi akamtazama mzee yule aliepata kuelekea miaka hamsini na mitatu hivi kisha pasipo kutia neno akawasha ile gari na ukawa ni mtafutano kwenye barabara usiku ule.
***
Ibra alikuwa na taarifa za Meja Salim komba kuwepo njiani lakini hadi muda huo hakuona dalili za kukutana nae ama kuliona gari lake.
Akawaamuru wapunguze mwendo huku akijaribu kutafakari afanye nini usiku huo maana kulikuwa na mawili yawezekana alipotoka alielekea morogoro ama alikuwa akielekea chalinze.
Akapiga chapuo la kinywa akawatazama vijana wake anaowafahamu kiundani kisha akamtazama mgeni katika wao Niyankuru aliekuwa kimya muda wote wa safari.
Ibra Mbaya akamtazama tena kijana yule wa Kikongo,akatabasamu maana mara nyingi alipenda vijana watulivu na wanaofanya mambo yao kwa weledi japo alikuwa hajamshudia katika hilo.
"Kuna gari nyuma yetu,tangu muda sasa haitaki kutupita" Alisema dereva wa gari la Ibra.
Ibra nae akageuka nyuma na kweli akaliona gari nyuma yao japo hakuwa na hakika ni dogo au kubwa kulingana na usiku kuwa wa kiza na alienyuma aliwasha taa kali.
Akaamuru dereva aendeshe kwa kasi, alichokifikiria ndicho kilitokea gari nyuma yao nayo ikaongeza mwendo,Ibra akatabasamu kisha akawaamuru vijana wakae tayari na hapo zikavutwa mashine za vita kutoka chini ya viti vya gari kisha zikakokiwa na kukaa tayari.
Dereva akapunguza mwendo makusudi na kwa kasi ya ajabu vijana wakafungua milango na kujitupa nje katika mtindo wa kuvutia kisha wakachukua nafasi kungojea kifuatacho.
Ibra alisalia katika gari lakini hakudumu nae akachumpa na kukita mguu kwenye rami kisha akahepa katika majani mafupi yaliokuwa pembezoni mwa barabara na kuicha gari ikienda kusimama hatua kadhaa mbele yao.
***
Matukio yote yalifanyika mbele ya macho ya Zedi na Meja Salim Komba.
Meja akiwa ndani ya bukta fupi akachukua bastola yake ya 45H&K USP yenye bulge kubwa na uwezo wa kumdondosha adui dakika sifuri,.
Zedi yeye alichukua M42 double colt kisha kwa usanii mkubwa akaipunguza mwendo na kuruka nje huku Meja tayari akiwa nje na yeye.
Jambo ambalo Ibrahim Mbaya hakujua ni kuwa gari liliachwa makusudi na wababe wale wa Vita.
Wakati likienda bila dereva lilikuwa likiyumba kushoto kulia na kwa kuwa lilikuwa linawaka taa basi liliwamulika vizuri maadui walipochutama na walionekana kirahisi kwa kuwa hakukua na majani marefu ya kujificha likawa kosa upande wa Ibra na kuwagarimu vijana wake wawili katika muda mfupi.
***
Pale alipodondokea Meja Salim alipata kuwaona vizuri kabisa adui wawili wakiwa wanajaribu kuotea kujificha nae pasipo ajizi akaachia risasi mbili zilizowapata wale vijana na kuanguka papo hapo.
Akatumia nafasi hiyo kusonga mbele huku akijitahidi kuchutama ili akingwe na majani.Na katika jitihada zake akawafikia wale vijana akawakagua mifukoni mwao hakukuta chochote na wakati huo akasikia ukimya wa ajabu katika eneo lile.
Akatambaa kama mamba kuufuata mti mmoja uliokuwa kando ya barabara ile ili apate kusimama na kutizama eneo lile kwa uzuri kabisa.
Kitu ambacho hakujua Meja Salim Komba ni kuwa kwenye mti ule alikuwepo Niyankuru na alikuwa akimtizama kila hatua yake,.
Niyankuru kule juu ya mti alipojaribu kupiga kwa kutumia bunduki,hakuona kama ni busara huwa anaamini zaidi mikono kuliko silaha.
Kulekule juu ya mti ajigeuza kama nyoka na akaanza kushuka kwa kasi bila kutoa sauti huku pigo lake likiwa limemlenga vizuri Meja Salim Komba aliekuwa akifanya jitihada za kujinyanyua ili aegemee ule mti.
Meja Salim Komba kwa mbali alihisi mjongeo wa kitu kichwani pake ni kama aliotea hivi akahepa kidogo na akalikwepa pigo la kifo la Niyankuru.
Japo alikwepa lakini hadi muda huo hakujua bastola yake ilikuwa wapi na tayari ilikuwa mbali na mikono yake,na bila kutegemea alijikuta akiwa chini na maumivu makali katikati ya kifua huku adui yake akiwa kasimama kimya bila kusema.
Meja alijiinua kivivu,kisha akasimama akamtazama adui na akafanya pata potea akarusha ngumi ikapita bila kitu,akatulia kidogo lakini kwa uwezo wa ajabu akashangaa akitandikwa makonde mazito na sehemu nyeti kabisa akaona akizubaa atakufa kwa nguvu zake zote akajirusha nyuma ili awe mbali na kijana yule alionekana fiti katika medani za mapigano ya ana kwa ana.
Akatua pembeni lakini hakuwa na nguvu hata kidogo,alikuwa ameotewa kupigwa maeneo ya kunyongonyesha, na akawa hajiwezi kwa lolote hadi wakati huo.
Niyankuru hakuona sababu ya kumchelewesha adui akanyanyua bunduki yake iliokuwa ikining'inia mgongoni na kwa hasira akamimina risasi kuelekea alipodondokea Meja.
Niyankuru hakutaka kuhakikisha shabaha yake akaweka silaha yake na kupepea.
***
Zedi aliendelea kutambaa kuelekea kule alikoona kadondokea Ibra Mbaya.
Katika harakati hizo za kutambaa kama Mamba akajikuta akitazamana na domo la bastola alikuwa ni Ibra Mbaya aliekuwa na yeye akitambaa akajikuta akikutana na Zedi.
Wote bastola mbele huku wakiwa wamelala chini ni vichwa tu vikitazamana kizani.
"Karibu tena kwenye mpango Tikisa"alisema Ibra Mbaya.
"Naona umeubadili kutoka ule wa Agano hadi Tikisa" alijibu Zedi
"Sikuwa na hakika kama ni wewe Zedi Wimba umenijibu nimekwel..."
Ibra hakumaliza kauli yake akajikuta akimshudia Zedi akiwa kasimama kwa mtindo wa Japan Kicks na miguu yake kaitanua hewani kwa shambulizi.
Ibra hakuwa mjinda na yeye pale alipo akaanza kwa kunyanyua miguu na kama ungelimtizama kwa mbali basi ungeamini ni wale aina ya nge wanyanyuao mikia(tandu),kisha akaifanya itangulie chini na kifua kikafuata lakini akaambulia teke maridhawa kutoka kwa Zedi ambae alikuwa amempa mgongo.
Katika dakika tatu Zedi aliutawala mchezo alimpiga atakavyo Ibra Mbaya lakini hazikufika dakika nne Ibra Mbaya Mwanaharamu akarudi katika ubora wake akaanza kumpelekea za nguvu Zedi sasa ikawa ni patashika nguo kuchanika.
Wahenga walisema ivumayo haidumu licha ya Ibra kufurukuta lakini uwezo wa Zedi ukawa bado upo imara na ilihitaji mbinu mbadala kumdhibiti.
Ibra Mbaya akiwa anapiga hesabu za kuijinasua mara ukatokea usadizi alikuwa ni Niyankuru aliengia kusaidia pambano na kwa kutaka sifa akaanza mbwembwe za kurusha ngumi mfululizo ila zote zikatua kwa mikono imara ya Zedi.
Zedi alijiweka kimkakati maana alikuwa anapambana na watu wawili hatari hivyo kosa moja lingempa tiketi ya kifo.
Akaanza kupambana na wale wababe,lakini hakufua dafu akajikuta akipokea kipigo kila dakika inavyosogea.
Akajipanga upya lakini hakufanikiwa hila zake,ukatokea mvumo wa risasi na akajitupa pembeni kisha kujivuruta kuelekea pahali salama.
Mvumo ulipokoma akaisimama akaishudia gari ya akina Ibra ikiyoyoma kwenda Morogoro na yeye alipotizama kule risasi zilipotokea alimwona Meja akiwa kasimama.
Kwa haraka akamfikia Meja na hakukawia kujua Meja alikuwa na jeraha mkono wa kushoto na alihitaji Msaada akaliendea gari lao lililokuwa limeacha barabara kidogo akamweka ndani na wakageuza kurudi Dar huku akipiga simu kwa Sajini Mina na Afsa kuomba msaada wa dharura.
*****
Asalaam Kudo
Tukutane whatsapp 0658564341 na 0758573660 kwa garama ya Tsh 2500/=