RIWAYA: Kikosi cha Pili

RIWAYA: Kikosi cha Pili

Hizi riwaya ya JF ni pasua kichwa tu, mtunzi kama umeshatoa kitabu nipe bei ninunue nakala yangu. Nimechoka kusubiria hapa
 
Hizi riwaya ya JF ni pasua kichwa tu, mtunzi kama umeshatoa kitabu nipe bei ninunue nakala yangu. Nimechoka kusubiria hapa
Samahani mkuu kwani nimekaa siku ngapi bila kupost?je umetaka kujua kwanini sijafanya hivyo?

Kumbuka hata Mimi ni kama wewe nina majukumu mengine pia lakini pia ninahudumu hapa na group la kulipia ambalo hujasapot chochote,na hujawahi fanya hivyo,na hata nikkupa bei yake hutanunua coz kujitolea tu nilipohitaji msaada umeshindwa utaweza kununua kwa elfu 12000/= na garama za kukufikia?

Acheni kuwa na tabia za Kasamadambwi ndugu nilijitolea kuweka hapa na nitaendelea kuweka bila kushurutishwa na mtu tafadhali usije ukafanya watu wengine wakose kusoma kwa ajili yako.

Kuna watu wameanza kupost hii stor kwenye group za whatsapp bila Mimi kuwaruhusu na wengine kwenye blogs na kwenye page za facebook,.

Na imekuwa tatizo pia hata baadhi ya riwaya zangu tulizoshirikiana kuandika na baadhi ya waandishi kila mtu akikufuata anakwambia ashasoma hizo kimsingi ukimuuliza kanunua atakujibu hapana so vyote hivyo ni changamoto za ambazo Mimi na mwenzangu tunajaribu kushugulikia lakini bado mnalalamika bila kuona uzito wa mambo haya

Niliahidi mwenyewe nitaimaliza hii Riwaya hapa so usitake kunitoa kwenye mood ingali mapema kabisa hata Wiki haijaisha tangu nipost mara ya mwisho

Asalaam Kudo.
 
Samahani mkuu kwani nimekaa siku ngapi bila kupost?je umetaka kujua kwanini sijafanya hivyo?

Kumbuka hata Mimi ni kama wewe nina majukumu mengine pia lakini pia ninahudumu hapa na group la kulipia ambalo hujasapot chochote,na hujawahi fanya hivyo,na hata nikkupa bei yake hutanunua coz kujitolea tu nilipohitaji msaada umeshindwa utaweza kununua kwa elfu 12000/= na garama za kukufikia?

Acheni kuwa na tabia za Kasamadambwi ndugu nilijitolea kuweka hapa na nitaendelea kuweka bila kushurutishwa na mtu tafadhali usije ukafanya watu wengine wakose kusoma kwa ajili yako.

Kuna watu wameanza kupost hii stor kwenye group za whatsapp bila Mimi kuwaruhusu na wengine kwenye blogs na kwenye page za facebook,.

Na imekuwa tatizo pia hata baadhi ya riwaya zangu tulizoshirikiana kuandika na baadhi ya waandishi kila mtu akikufuata anakwambia ashasoma hizo kimsingi ukimuuliza kanunua atakujibu hapana so vyote hivyo ni changamoto za ambazo Mimi na mwenzangu tunajaribu kushugulikia lakini bado mnalalamika bila kuona uzito wa mambo haya

Niliahidi mwenyewe nitaimaliza hii Riwaya hapa so usitake kunitoa kwenye mood ingali mapema kabisa hata Wiki haijaisha tangu nipost mara ya mwisho

Asalaam Kudo.
Samahani sana kiongozi na pole kwa changamoto unazokumbana nazo.

Niko tayari kununua kitabu. Kikiwa tayari tuwasiliane.
 
SEHEMU YA 25*


koplo Ziga alikaa mkao wa mwizi wa maziwa kwenye susu,huku mawazo yake yakifanya kazi kama mpiga hesabu za Mada ngumu kabisa ya kidato cha pili,ya tafuta thamani ya X huku x unaiyona haina thamani imekaa tu.

Mlango ukagongwa tena kwa nguvu zaidi ya mwanzo na hapo koplo Ziga,akasikia michakacho ya mtu kule maliwato ikipanda na kushuka chini hii ilimpa ishara kuwa mtu yule alikuwa anavaa.

Upepo uliopiga kutokea nyuma ya mwili wa Ziga ndio uliomkurupua katika hesabu za pata potea alizokuwa akizipiga komando Ziga.

Akageuka kama mwehu na kutizama nyuma hapo ubongo wake ukajenga tabasamu kama mtu aliebeti na kushinda pesa.

Bila kujiuliza akalivamia dirisha liliokuwa nyuma yake tena likiwa wazi,akatoa kidogo pazia akapata upenyo wa kuchomoka mle ndani na dakika hiyo hiyo akasikia kishindo cha mtu aliusukuma mlango kwa nguvu na kuingia ndani,ila yeye hakujali na alikuwa tayari akifanya jitihada za kulifikia bomba la maji machafu lililokuwa limeanzia juu kushuka chini na yeye akalitumia kama usafiri wa kuondoka katika vyumba vile vya juu hotelini pale.

Alipofika chini akabinya tena sikio na kusema maneno machache ya kijasusi kisha akafanya jitihada za kuuruka ukuta wa hoteli ile ili atoke nje maana alikuwa kadondokea nyuma kabisa.

Dakika moja mbele alikuwa ndani ya gari ya kizamani pamoja na koplo Makame wakijaribu kuiacha Goma iliokuwa imejaa taharuki visivyokifani.

***
Papaa Deo Mukamba,baada ya kutoka kumsindikiza mshirika wake kutoka Tanzania waziri wa Michezo bwana Muruga wesa,alikuwa akiingia ndani kwake huku walinzi kama sita wakiwa nyuma yake.

Mlinzi wa mmoja wakati akizungusha macho yake alipata kuona mlinzi waliemwacha akiwa kadondoka chini na kwa haraka akatoa ishara kwa wenzie ambao bila kufikiri wakamzunguka mkubwa wao ili kumkinga na hatari yoyote.

Papaa Deo Mukamba akiwa na uoga ndani yake,akaamuru mlinzi mmoja aende kushuhudia ni nini kilichomkuta mwenzao.

Kwa hatua za tahadhari mlinzi yule alikuwa akimsogelea mlinzi yule,ni wakati akikaribia akaona hakuwa peke yake,walikuwa walinzi wote wa mbele walikuwa chini tayari ni maiti akarudisha taarifa kwa mkubwa Papaa.

Mlinzi mwingine akatumwa ndani,nae hakukaa sana akarudi na taarifa kuwa ndani nako kuna maiti za walinzi.

Katika siku za uchungu na woga ilikuwa siku hiyo.Papaa Deo Mukamba alijiuliza bila majibu ni nani wa kuingia katika ngome yake na kufanya mauaji kiasi kile kisha akatoka salama?

Moyoni mwake alikiri watu au mtu huyo alikuwa fundi katika medani ya kivita.

Alijaribu kufika katika kila maeneo yake muhimu,akakuta kuko salama lakini baadhi ya bahasha za muhimu pia hakuzikuta hapo akachanganyikiwa, haraka akakimbia chumba cha ulinzi huko akakuta askari aliemwacha akiwa maiti na alipotizama kamera zilirekodi nini akaambulia kuona mgongo wa kidume Ukitoka na nyaraka mkononi.

Hakuwa na namna akaamua kuwapigia wafadhili wake huko ufaransa kisha akapiga simu Tanzania kutoa taarifa ya nyaraka kadhaa kutua mikononi mwa asie hitajika.

***

Kimbu kiongozi wa LPFaliwapokea makomando wale wakitanzania katika kambi yao ilioko mafichoni katikati ya misitu ya Goba.

Baada ya maelekezo machache ya usalama wa kambi yao ulikuwa ni muda wa kupumzika baada ya hekaheka za siku nzima.

Ni kawaida kwa komando yeyote kutokupata usingizi mzuri ndani ya masaa mawili hasa wanapoukuwa katika hekaheka zozote,na ndivyo ilikuwa usiku alfajiri ile.

Koplo Ziga alikuwa akiwaza stakabali ya maisha yao ndani ya mji ule wa Goba katika nchi ya kidemokrasia ya Kongo.

Aliwaza usaliti aliofanyiwa na viongozi wake yeye na wenzie,lakini kubwa alikuwa na hofu ya jambo flani linalotaka kutokea katika nchi yake.

Si yeye tu hata koplo Makame alikuwa katika mawazo hayohayo.

Koplo Ziga hakuona umuhimu wa kulala akanyanyuka kisha kukaa punde Koplo Makame nae akanyanyuka na kukaa huku kila mmoja akiwa kimya akitafakari yake.

Wakiwa vilevile wakasikia hatua za mtu zikijongea kikakamavu kulifuata hema lao.

Alikuwa ni Kimbu.Alipofika akakohoa kama ishara ya kuweka amani katika vichwa vya makomando wale ambao aliamini walikuwa tayari kwa lolote muda huo,kisha akasukuma kimlango cha miti kilichokuwa kimeegeshwa pale mlangoni mwa hema lile.

Alipoingia akakutana na makomando wakiwa katika mkao wa lolote,nae bila salamu akaweka yaliompeleka mule ahsubuh ile.

"Kama mjuavyo mwenzenu yupo bado kwa waasi,basi nami nimekuwa nikifanya jitihada za kujua anaendeleaje huko.Lakini kwa taarifa nilizozipata muda mfupi uliopita 01 leo jioni anasafirihswa kwenda Goma na kuna Makubaliano flani kati ya Papaa Deo Mukamba na Kiongozi wa waasi,hivyo basi nasubiri mawazo yenu nini kifanyike"

Walitazamana Makomando wale,kisha Makame akasema

"Hatutaweza kuruhusu hili litokee na kuanzia sasa inabidi atumwe kijana hodari aanze kufuatilia nyendo za waasi wale,na..."

Hakumaliza kauli yake kikasikika kipenga cha hatari pale kambini na kwa haraka wakatoka nje na kukutana na vijana wengi wakiwa wamekamata silaha kumwelekezea mtu mmoja aliekuwa kaloa damu kuashiria kapigika muda mfupi uliopita.

Wakasogea hadi kwa mtu yule na hapo wakapokea taarifa kutoka kwa kiongozi wa vijana wale shupavu.

"Amekuwa hapa usiku kucha akipiga picha na kuchora,nasi tumekuwa nae kila hatua bila yeye kujua na wakati akijiandaa kutoka tukamweka kati alijaribu kujitetea lakini tumefanikiwa kumdhibiti"

Kimbu akatabasamu na hakuwa na shaka yule alikuwa ni mpelelezi kutoka mahali fulani,akaagiza vijana wamfunge asubiri hukumu yake na hilo likatekelezwa mbele ya macho ya Koplo Makame na koplo Ziga.

*****

Asalaam Kudo.
 
Ziga zedi umemix mkuu au ni mm usingizi unaninyemeles??

Asante kwa kunitag
 
Naona umekunywa Reds za kutosha la basi utakuwa na usingizi umeshindwa kuikumbuka Riwaya

Zedi yupo bongo na Ziga yupo Kongo kumbuka vipande vya nyuma
Namanisha umetumia jina moja kwa kila mtu ndio jimeona hivo mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom