Riwaya: Joka la Mdimu

Riwaya: Joka la Mdimu

Quinton Canosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2012
Posts
1,228
Reaction score
1,264
Habari Wanajamii Forum

Mwandishi, Abdallah J. Safari.

Leo ngoja niwaletee riwaya moja ambayo kwa hapa kwetu Tanzania inaweza ikatuangazia sana maisha yetu.Riwaya inaitwa Joka la Mdimu.
JOKA LA MDIMU ni nyoka anayeishi katika miti ya kijani. Nyoka huyu hupendelea kuishi katika miti ya Minyaa na Midimu inayofanana na rangi yake. Nyoka huyu awapo kwenye miti hiyo si rahisi kumtambua kutokana na rangi yake kufanana sana na miti hiyo. Hivyo ni nyoka hatari sana kwa binadamu.

Mwandishi anatumia taswira ya Joka la Mdimu kufananisha na viongozi ambao ni wananchi wenzetu, wanafanana na sisi, ni ndugu zetu damu yetu. Lakini ni hatari mno kwani hutugeuka na kuwa mafisadi, wala rushwa, hawatimizi majukumu yao, ni walaghai nk. Badala ya kusaidia wananchi wao hujali maslahi yao kwanza na hivyo kusababisha mifumo ya kiuchumi kuendelea kuwa migumu kwa wananchi na kupelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha watu walio maskini au hohehahe. Hivyo jina la kitabu linasawiri yaliyomo ndani ya kitabu na katika jamii.
Hivyo basi nawasihi hawa wote wanaodai wanatupenda hasa viongozi wetu wa kisiasa wengi ni majoka ya mdimu tuwe makini nao sana na tusitegemee jipya sana kutoka kwao kwani wengi wao kwa ulimwengu huu ni watafuta mali na waroho wa madaraka

Muwe na siku njema
 
Back
Top Bottom