Willy Gamba 1
JF-Expert Member
- Jan 5, 2015
- 352
- 377
HOFU
SEHEMU YA KWANZA
PORT ELIZABETH
Ilikuwa tarehe 24 Machi, baada ya mauaji ya
kikatili ya waafrika 19, katika kitongoji cha
Langa, karibu na Vitenhage; mji ulio karibu na
ule mji wa viwanda wa Port Elizabeth, katika
Jimbo la Cape Mashariki. Mauaji hayo yalikuwa
yamefanyika tarehe 21 Machi, siku ya
kukumbuka mauaji ya kikatili kwenye mji wa
Sherpville mnamo mwaka 1960. Wakati
wazalendo 69 walipouawa kikatili. Mnamo
tarehe hiyo ya 24 Machi, huko mjini Port
Elizabeth kulifanyika mkutano katika ofisi ya
Mkuu wa Polisi mnamo saa sita usiku.
Ndani ya chumba cha mkutano huo walijumuika
watu ambao wamekuwa chanzo cha vilio na
malalamiko mengi kutoka kwa wazalendo wa
Afrika Kusini dhidi ya makaburu. Katika mkutano
huo alikuwemo waziri wa sheria na usalama wa
makaburu, Kamishna wa Polisi, Mkurugenzi wa
shirika la Ujasusi la makaburu na Kamanda wa
kikosi cha Jeshi kiitwacho 'KULFUT'yaani
'Gongo la Chuma' wote hao walikuwa ni
makaburu. Lakini vile vile mkutano huo
ulihudhuliwa na watu weusi ambao walikuwa
wameitwa haraka haraka.
Hawa walikuwa wamefanyiwa mipango maalumu
ya usafiri ili mladi wafike kwenye mkutano huo
muhimu. Walikuwa wamesafiri kwa kutumia
ndege ya Jeshi la Anga la makaburu. Weusi
hawa walikuwa ni Mkuu wa Magaidi wa UNITA,
wenye kupinga Serikali ya Angola, Mkuu wa
Magaidi wa MNR wenye kupinga Serikali ya
Msumbiji na Mkuu wa Magaidi wa LLA wenye
kupinga Serikali ya Lesotho, kwa kifupi tu ni
kwamba, Magaidi wote hawa ni vibaraka wa
Serikali ya Makaburu na ilikuwa ni serikali ya
makaburu iliyowagharamia kufanya ujahili dhidi
ya nchi zilizo mstari wa mbele katika Ukombozi
wa Afrika Kusini, ili kuzizorotesha kisiasa na
kiuchumi kwa nia ya kuziangusha hatimaye.
Waziri wa sheria, ambaye alikuwa Mwenyekiti
wa mkutano huo, alianza kwa kusema;
"Kwanza lazima nitoe shukrani zangu kwa nyinyi
wote kuweza kufika hapa kwa muda uliopangwa,
shukrani zangu za dhati ziwaendee nyinyi
wageni wetu ambao mmetoka nje ya nchi hii.
Pili tumeitana hapa usiku wa manane
kuzungumzia suala muhimu sana. Ningependa
tufanye na kumaliza mazungumzo yetu usiku
huu ili muweze kuondoka kabla
hapajapambazuka, kwani shughuli hii ni ya siri
sana. Mimi nikiwa mwana siasa nitazungumza
tu kwa ujumla kuhusu nia ya mkutano. Halafu
nitawaachia wataalamu wa utekelezaji walio
hapa kuchambua vipengele vinavyohusika kwa
undani zaidi".
"Nafikiri nyote mnaelewa kwamba kumekuwa na
wimbi la maasi la waafrika katika nchi nzima ya
Afrika Kusini. Wimbo hili, kwa kiasi fulani
limetutia wasiwasi. Migomo imeongezeka katika
sehemu za kazi kiasi cha kutishia uchumi wa
nchi yetu. Maandamano yameongezeka kiasi cha
kutishia utulivu na amani ya wananchi. Vitendo
vya hujuma vinavyofanywa na magaidi
wanaojiita wapigania uhuru'wa Afrika Kusini
vimeongezeka kiasi cha kutishia mashirika ya
nje yenye raslimali zao humu nchini.
"Sasa Serikali imeamua kukomesha vitendo
vyote hivi. Serikali ilikuwa na nia ya kulegeza
vipengele fulani fulani katika sheria zetu kwa
manuafaa ya weusi. Lakini imegundulika kuwa
kufanya hivyo kutawafanya watu hawa kuwa
kichwa ngumu zaidi. Na kama alivyosema Rais
wetu, hakuna mtu yeyote Ulimwenguni
atakaetuzuia kulinda usalama wa nchi yetu na
watu wake wapendao amani!'. Na hapa
nasisitiza tena hatutaki mchezo.
"Ghasia hizi ambazo zimekuwa zinaendelea
zimefanya mashirika na makampuni kutoka nje
kuwa na mtazamo mpya. Yanaanza kuwa
wasiwasi juu ya uwezo wetu na pia kuelekea
kuwa na imani katika vyama vinavyodai
vinapigania uhuru. Hali hiyo siyo nzuri na ni
tishio kubwa kwetu".
"Uchumi wetu umeanza kuanguka. gharama za
maisha zimepanda kwa kadri asilimia kumi na
saba!, ukame umeathiri uzalishaji wa chakula.
Bei ya dhahabu imeanguka saba mwaka huu na
kufanya bei za vitu muhimu, kama vile Petroli,
kuongezeka kufuatana na kushuka kwa thamani
ya fedha yetu, ukilinganisha na thamani ya dola
ya kimarekani. Jumuia ya Kimataifa inapiga
kelele na kuyataka makampuni yasiweke
raslimali na vitegauchumi vyao nchini mwetu".
"Mambo yote haya yanatokana na mwamko wa
Ulimwengu dhidi ya siasa yetu ya ubaguzi. suala
la kuzungumzia ni nini kufanyike ili kulekebisha
hali hii ndio sababu leo mko hapa kutafuta
ufumbuzi. kuanzia sasa tunataka kufanya
macho ya Jumuia ya Kimataifa kuelekea
sehemu nyingine ili sisi tupate nafasi ya
kurekebisha mambo humu nchini. Macho yao
yanataka yaelekee kwenye nchi zilizo mstari wa
mbele na vile vile Namibia. Tutafanya vitendo
katika nchi hizo vitaifanya Jumuia ya Kimataifa
kushughulikia sana; ikitafuta njia za kuwasaidia
wananchi wa hizo. Wakati Jumuia ya Kimataifa
inashughulika kiasi hicho, sisi tutaanza kuwapa
fundisho hawa watu weusi wanaoleta ghasia
hapa nchini. Jumuia ya Kimataifa ikija kugeuza
macho yake kuyaelekeza kwetu. tutakuwa
tumeisha wakomesha hawa watu weusi ambao
ni wakorofi watakuwa wamenyooka kama
mpini".
"Hivyo tumeamua kuanzisha 'UTAWALA WA
HOFU' dhidi ya weusi walio humu nchini na pia
walio katika nchi zilizo mstari wa mbele kwa
ujeuri. Ni imani yangu kuwa mmenielewa na
ninawashukru tena kwa kunisikiliza. Wakuu wote
wa usalama wako hapa. watawaeleza jinsi
utekelezaji wa jukumu hili utakavyokuwa.
Ahsanteni sana".
Alipomaliza kusema hayo, Waziri wa sheria na
usalama alifunika jalada lake, kisha akasimama
na wengine wakasimama pia. Huku akiwapungia
mkono wa kwaheri, Waziri alisindikizwa na
Kamishina wa Polisi mpaka kwenye mlango.
Alifunguliwa mlango huo na kutokomea gizani.
Baada ya Kamishina wa Polisi kurudi kwenye
nafasi yake, Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la
Makaburu alichukua uwanja kueleza namna ya
utekelezaji wa mpango huo.
"Nafikiri nyinyi wote mmemsikiliza waziri kwa
makini. Mambo ni kama hayo na hatuna budi
kutekeleza, nyinyi wenzetu wa UNITA, MNR na
LLA tunahitaji msaadawenu kikamilifu.
Tumesaidiana mambo mengi sana. Bila sisi
kusingekuwepo na UNITA, MNR au LLA", alisema
huku akiwakazia macho viongozi wa vyama
hivyo vya magaidi.
Wote walimwemwesa huku wakionyesha kwa
vichwa vyao ishala ya kukubaliana nae.
"Kuanzia sasa misaada kwenu inaongezwa
mara dufu". Wote walishangilia kwa kupiga
makofi.
"Lakini", aliendelea Mkurugenzi wa Shirika la
Ujasusi la Makaburu, "Misaada hii haikuongezwa
bure. Kutakuwa na kazi kubwa ya kufanya.
Alinyamaza huku akiwaangalia viongozi wa
magaidi kujua kama walikuwa wanampata.
"Mmesikia kuwa tunaanzisha utawala wa hofu'
dhidi ya watu weusi waliomo humu nchini na pia
nchi zilizoko mstari wa mbele pamoja na
Namibia. Utekelezaji wa mpango huo utakuwa
kama ifuatavyo.
"Kwanza sisi tutajitangazia uhuru nchini
Namibia. Baada ya kufanya hivyo tutapambana
na SWAPO. Kama ikibidi tutauwa watu Namibia
kwani nchi ile ni lazima kuitawala. Tumeanzisha
Jeshi linaloitwa KULFUT, yaani Gongo la
Chuma'. Hili ndilo Jeshi litakalosababisha Hofu
huko Namibia na nchi fulani fulani zinazojidai
kuwa mstari wa mbele. Jeshi hili limeundwa na
Makomandoo watupu na lenye uwezo mkubwa.
Limefundishwa kwa kipindi cha miaka kumi
sehemu mbali mbali Ulimwenguni na sasa liko
tayari kabisa kutia hofu popote litakapotumwa.
Upande wetu umejiweka tayari. Baadhi ya vikosi
vya Jeshi hili vitaletwa kwenu".
Wajumbe walipiga makofi.
"UNITA", aliendelea "Kazi yenu itakuwa kutia
hofu huko Angola. Hakuna mazunguzo na
Serikali ya Angola tena. Mtapewa kila msaada
wa hali na mali. Lazima kuhakikisha kuwa
uchumi wa nchi hiyo unaanguka kabisa.
Kamanda wa KULFUT yupo hapa atapewa kikosi
cha Jeshi hilo kusaidia katika dhima hiyo,
wapiganaji wenu wasiwe na huruma, bali
kuchinja na kuua kiumbe chochote kilicho mbele
yenu. Hakikisha mnawaangamiza wale wote
wanaojiita wapigania uhuru wa Namibia. Sisi
tuko nyuma yenu kwa lolote lile litakalotokea.
Nguvu zetu mnazijuwa. Kwa hoyo hakuna
atakayechezea".
"Nyinyi MNR", alimgeukia kiongozi wa MNR,
"Kazi yenu mnaijuwa. Kama watakavyofanya
hawa watu wa UNITA. Fanyeni vurugu ndani ya
Msumbiji. Watu wapate hofu kuliko wale
walioishi wakati wa NAAzI iliyosababishwa na
Wajerumani".
Mara alimuona Kamanda wa MNR amenyoosha
kidole akitaka kuzungumza.
"Eh, unasemaje?, aliuliza kwa shauku kubwa.
"Sisi tuko tayari kabisa", alisema Kamanda wa
MNR, "Lakini lazima niseme kwamba mkataba
wenu wa Nkomati unatutatanisha. Ni mkataba
wa amani kati ya Msumbiji na Afrika Kusini.
Sasa kwetu sisi kuendeleza mapambano
inakuwa vigumu ingawa mnatusaidia. Mkataba
huo unatuathiri sana".
Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Makaburu
alijibu. "Achana na siasa. Mkataba wa Nkomati
ni siasa tu. Sahau kabisa. Tangu uwekwe saini
hakuna mtu ambaye ameutekeleza. Ndio sababu
misaada kwenu imeendelea. Kazi yenu ni kama
nilivyosema: fanya hali ya Msumbiji iwe ya hofu
tupu. Lengo la mkataba wa Nkomati ilikuwa
kuwachota akili viongozi wa serikali ya
Msumbiji. Tumegundua kwamba wanawaogopa
sana nyinyi watu wa MNR. Nyinyi ndio mlikuwa
chanzo cha mkataba huo. Walitaka amani. Sasa
kinachohitajika ni kuwatia hofu zaidi kwa vita na
si ajabu mkachukuwa madaraka. La sivyo,
angalau waje kusujudu kwetu na kutulamba
miguu. Kwa hivyo sahau kitu kama mkataba wa
nkomati".
"Nakuapia", alisema Kamanda wa MNR,
"Watakiona cha mtemakuni".
Ndipo Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la
Makaburu alipoendelea, "Kazi ya LLA haina
tofauti na wengine askari kutoka jeshi la KULFUT
watawasaidia kuleta vurugu na hofu kubwa huko
Lesotho na Botswana. Sisi tuachieni Zimbabwe,
Zambia na Tanzania. Vikosi vyetu maalumu vya
uhujumu katika Jeshi la KULFUT vitazionyesha
cha mtemakuni nchi hizo. Ili kuonyesha nguvu
zetu, sisi tutaanzia Tanzania. Tunataka tutie
vurugu na kuleta rindi la hofu katika nchi hiyo
dunia itashangaa. Tanzania haijawahi kupewa
fundisho kwa sababu hiyo nchi ina kiburi na ndio
shina la hawa wanaojiita wapigania uhuru".
"Bila Tanzania, hawa watu wasingetupa taabu
kiasi hiki. Nchi hiyo inawapa hifadhi watu hao
na kuwapatia mafunzo ya kijeshi. Baadae
inawapenyeza kwetu na kutupa shida,
shambulizi tutakalofanya huko Tanzania.
litawatia hofu hao wanaojiita wapigania uhuru
na kuwafanya wasambae bila mpango,
itawachukua karne nzima kuweza kujikusanya
tena. Litakuwa pigo takatifu ambalo litaiacha
dunia nzima inagwaya. Mipango ya awali juu ya
kipigo hicho iko tayari na hatuna wasiwasi".
Mkuu wa UNITA aliamusha mkono ikiwa ni
ishara yake ya kuomba kusema.
"Eh, unasemaje?". Mkurugenzi wa Shirika la
Ujasusi la Makaburu alimuuliza Mkuu wa UNITA.
"Mimi nasikia moyo wangu unakwenda mbio
kwa shauku", alisema Mkuu wa UNITA. "Kama
kweli mtaipa kipigo Tanzania mpaka ikakoma
kutamba, basi sisi kazi yetu itakuwa rahisi kama
kunywa maji. Nchi hiyo ina kiburi na ndio
inayowapa kichwa ngumu wale wanaodai
kupigania uhuru, na nchi nyingine za mstari wa
mbele. Iwapo Tanzania itashika adabu, basi
vyama vyetu vitapata ushindi wa kutawala.
Lakini napenda kukutahadhalisha kuwa nchi
hiyo ni imara sana. Mimi nimewahi kuishi huko
na ninajua kazi yenu haitakuwa rahisi".
Mara alikatizwa na Mkurugenzi.
"Usiwe na wasiwasi", Mkurugenzi alianza
kujitapa. "Hakuna nchi itakayonusurika. Na
Tanzania itakuwa ya kwanza. Nyinyi mtasikia.
Kusema kweli baada ya kipigo hicho, hao
wapigania uhuru; na pia nchi nyingine zilizo
mstari wa mbele watabaki wanagwaya".
"Ili yakutoke mashaka", alidakiza Kamanda wa
KULFUT, "Matayarisho ya kipigo hicho yalianza
siku nyingi. Jeshi la KULFUT likishikiana na
Shirika la Ujasusi hakuna wasiwasi kuhusu
kipigo hicho, nakuhakikishia kuwa Tanzania na
wenzake watakipata cha mtemakuni. Tumetumia
miaka kumi kujitayarisha na muda huo siyo
mchezo".
"Saa zimekwenda sana. Tumetumia muda
mwingi sana kuzungumzia suala hili wakati
ambapo nyie mnapaswa kuondoka kwa siri sana
kabla ya mapambazuko". Hapa Mkurugenzi
alinyamaza kidogo kisha akaendelea kusema.
"Kamanda wa KULFUT' atawapatia msaada
mnaohitaji katika kutekeleza mpango huo.
Hatuwezi kukubali kushindwa kwani hiyo ina
maana kuwa huo utakuwa ndio mwisho wetu -
kitu ambacho hakiwezekani. Lazima nipate ripoti
ya maendeleo ya mpango huu kila siku ili niweze
kuipa taarifa serikali. Kamishina wa Polisi
anasema hana wasiwasi juu ya weusi wa hapa
kwani atawatia vurumai mpaka wajute
kuzaliwa".
:Nafikiri mmesikia kuwa mwezi Februali
tuliwakamata vingozi wa vyama vya upinzani.
Hao tumewaweka kiporo na baada ya kuipa
kipigo Tanzania. Nyinyi mtasikia vurumai
tutakavyoifanya, au uongo Kamishina?".
Akionyesha majivuno, Kamishina wa Polisi
alijibu, "Watajuta kuzaliwa kwani walikuwa
wanaleta mchezo. walikuwa wamediliki
kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe
hapa nchini. Kitu kama hicho hakiwezi kutokea
wakati bado niko hai".
Mkurugenzi alifunga mkutano huo kwa dharura
kwa kusema, "Ahsanteni sana. Ni mategemeo
yangu kuwa mmeelewa hali halisi na hivyo
mtatekeleza itasavyo. Naamini tutakapokutana
tena kwenye mkutano kama huu hali haitakuwa
hivi, bali kusherekea ushindi dhidi ya adui. Sura
ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
itabadilika kwa kupata tawala mpya".
Mkutano ulifungwa saa kumi na moja alfajiri.
ITAENDELEA