Riwaya - Gereza la Kifo

Riwaya - Gereza la Kifo

as
Gereza la Kifo - 58

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

Happy aliondoa vyombo mezani huku Masunju akimpiga jicho la uchu kwa jinsi alivyokuwa anatamanisha usiku huo akiwa amevaa sketi yake fupi na blauzi fupi iliiyokuwa imeacha kitovu chake nje.

Msichana huyo mrembo alimkaribisha chumbani na kisha akamwambia anatoa vyombo nje kwa ajili ya kuvisafisha baadaye.

Masunju alibaki chaumbani na ndipo Happy akachepuka haraka haraka hadi kwenye dirisha la chumba walimokuwa akina Walari na dada yake Ramla kuwaambia kwamba waje kuvamia baada ya dakika zisizozidi kumi.

Wakati yule kijana aliyejifanya mchumba wa Happy hakuwa na wasiwasi wowote kuanza safari ya kwenda kumvamia Masunju, yule mpiga picha alianza kuogopa.

Endelea...

"Huyu mtu kweli hana bastola? Mimi naogopa bwana," akasema yule mpiga picha.

Wakati dakika kumi alizokuwa amewapa Happy zinaisha bado Ramla, Walari na Marare walikuwa wakimbembeleza yule mpiga picha asiogope lakini ilishindikana licha ya kumwongezea pesa kutoka sh. 40,000 walizokuwa wamemuahidi awali hadi sh. 60,000.

Ingawa Walari na Marare walipanga wawe wakishuhudia kwa mbali, lakini ilibidi sasa Marare aamue kuchukua kamera ya yule mpiga picha wa mtaani kwenda.

Yule kijana aliyepanga kujifanya mchumba wa Happy, akiwa hana wasiwasi alitangulia na alipofika akasukuma mlango wa kuingilia sebuleni na moja kwa moja akasukuma ule wa chumba walimokuwa Masunju na Happy. Happy alikuwa ameacha kuufunga kwa makusudi.

Masunju ambaye alikuwa uchi wa mnyama, huku akiwa amemkumbatia Happy ambaye alikuwa akijifanya yuko katika harakati za kuvua nguo, alishituka sana.

Happy alikurupuka na kwenda kupiga magoti akimwomba samahani yule 'mchumba' wake.

Masunju akiwa amechanganyikiwa alitaka kuchukua nguo zake alizokuwa amezitunduka ukutani haraka haraka, lakini yule 'mchumba' akaziwahi na kuzirusha nje ya chumba huku akimzuia kwa nguvu asitoke.

‘Mchumba’ huyo, akaanza kumhoji inakuwaje anafanya mapenzi na mchumba wake, wakati yeye yuko katika harakati za kufunga ndoa na msichana huyo na sasa walikuwa wanahesabu miezi tu.

Masunju, akiwa bado uchi alimuomba msamaha yule kijana huku akinyanyuka na kumuomba amuache achukue nguo zake na kwamba hilo suala wangelimaliza.

Yule kijana akiwa amekasirika 'sana' alitaka ampe maelezo ya kuridhisha kwa kitendo cha kumrubuni mchumba wake wakati yeye Masunju ana mke.

"Utakuwa mtu mshenzi sana wewe. Bila shaka wewe ni mpenzi wa shemeji Ramla na mimi nilishakuona unakuja hapa hapa mara kwa mara kwa dada yake huyu mchumba wangu. Huwa tunapishana tu. Sasa inakuwaje tena unamchukua mdogo wake ambaye ni mchumba wangu mimi?" Akawa anafoka kijana huyo aitwaye Bwire kwa hasira.

"Kijana samahani sana. Punguza hasira. Tutayamaliza tu kijana. Naomba sana unirudishie nguo zangu nivae," aliomba Masunju.

"Sikubali. Nimeshamhangaikia sana huyu binti. Unajua hasa aliyekuwa akimlipia karo ya shule ni nani? Si unajua hawa mabinti ni yatima?" Akazidi kufoka Bwire huku akina Walari waliokuwa nyuma ya dirisha wakisikia.

"Kijana tutayamaliza tu," akaomba Masunju huku sasa Happy akiwa amemgeukia kwa kumlaumu kwamba amemponza kuhusu mchumba wake na dada yake akipata habari hizo atamfukuza.

Masunju akazidi kumsihi Bwire ampe nguo zake, halafu wamalizane na sasa akamtaka atamke pesa anazotaka. Bwire huku akifunga mlango wa chumba kwa komeo alitoka kama vile anamleta nguo zake alizokuwa amezirusha sebuleni.

Alienda kumchukua Marare ili aje kumpiga picha Masunju. Marare alilazimika kuvaa kofia walioiazima haraka haraka ili kujaribu kuficha sura yake Masunju asimtambue.

Walipoingia mule chumbani ambako Masunju alikuwa bado ameketi kitandani akiwa uchi wa mnyama Marare ambaye alikuwa ameandaa tayari kamera akampiga haraka haraka picha.

Masunju aliposhituka kwamba anapigwa picha alisimama haraka haraka na kujaribu kuficha sura yake huku pia akifunika sehemu zake za siri kwa viganja. Baadaye akafanikiwa kuvuta shuka iliyokuwa kitandani lakini alikuwa ameshachelewa. Marare alikuwa keshampiga picha kadhaa na kutoka nje haraka, akimwacha Bwire akiendelea kuzozana na Masunju ambaye sasa alikua amechanganyikiwa.

Sasa Masunju alianza kugomba kuhusu suala la kupigwa picha, lakini Bwire akamjibu kwa jeuri kwamba ni lazima ampige ili kuweka ushahidi atakapokuwa anadai pesa zake nyingi ambazo ameshamgharimia Happy.

Masunju alizidi kumsihi kijana yule amsamehe, kisha ampe mkanda wa picha alizopigwa huku akiahidi kumpa gari dogo aina ya Toyota Carina pamoja pesa taslimu shilingi milioni moja.

"Mzee, mimi sasa ninakuruhusu uende zako, mambo ya pesa na gari tutaongea siku nyingine kadri tutakavyoafikiana na mchumba wangu kuhusu kadhia hii," akasema Bwire huku akitoka nje ya chumba ambako alichukua nguo za Masunju na kumrushia pale kitandani.

Mwanamume yule menene, Masunju alivaa haraka haraka, tena akiwa amesahau nguo ya ndani ambayo, Happy toka mapema, alikuwa amesukuma uvunguni mwa kitanda bila Masunju kufahamu.

Bwire, huku mawazoni akiingiwa na uchu wa gari, alizidi kumwambia Masunju kwa kiburi kwamba suala la kupeana pesa au gari wangelizungumzia siku nyingine ndipo ampe mkanda wa picha zake.

Masunju alizidi kubembeleza lakini Bwire alikataa na kutoka nje ambako kulikuwa na giza. Happy alikuwa amezima taa ya nje makusudi.

Masunju naye alitoka akizidi kumbembeleza Bwire ambaye alikuwa amesimama nje karibu na mlango. Akamsihi sana ampe mkanda wa picha aliyopigwa.

"Mzee, nimeshakwambia mkanda huupati leo. Kwanza mpiga picha mwenye ameshaondoka zake," akajibu Bwire.

"Kwenda wapi?"

"Kwenda kwake mzee. Wewe huoni huu ni usiku?"

Ghafla Masunju alichomoa bastola ambayo ilikuwa kwenye nguo zake na kumgusisha nayo Bwire kwenye paji la uso. Hicho ni kitu ambacho Bwire alikuwa hakukifikiria.

"Sasa kijana ninakuua ukileta masihara. Nimekupa kila ahadi hutaki kusikia. Mimi siondoki hapa bila kupata mkanda wa picha mlizopiga. Kwanza ninajiuliza huyu mpiga picha katokea wapi?" akafoka Masunju.

Bwire alivaa ujasiri na kumjibu kwamba yeye haogopi kifo wakati anapokuwa anafuatilia haki zake.

"Niue tu kama unataka. Lakini hili si suluhisho na utakuwa unajiweka katika matata zaidi. Niue kama unataka."

"Nyamaza. Mbwa wewe. Weka mikono juu la sivyo nitafumua ubongo wako sasa hivi," alifoka zaidi Masunju.

Bwire sasa alianza kuingiwa na wasi wasi huku akijilaumu ni kwa hakukagua bastola kwenye mifuko ya Masunju. Aliona yule mtu amekasirika kuzidi upeo wa kawaida na angeweza kumuua kweli.

"Sasa tuseme ndiyo unataka nikupe mkanda kwa nguvu halafu ahadi uliokuwa unainiambia ya pesa na gari ndiyo umefuta? Si ninakwambia kwamba hilo tutaliongelea siku nyingine?"

"Siwezi kuondoka hapa bila huo mkanda. Nikishaupata huo mkanda au kufuta hizo picha zote sasa tutazungumza," akasema Masunju akizidi kugandamiza mtutu wa bastola kwenye uso wake.

Bwire alizidi kuogopa.

"Naomba tuwasiliane kesho kwa sababu yule mpiga picha nilimbahatisha tu wakati nimetoka nje, lakini anakwenda kupiga picha katika ukumbi mmoja ambao kuna dansi usiku huu. Kwa hiyo ameshakwenda huko, si rahisi kumpata," akajibu Bwire.

"Bwana mdogo, usinifanye mimi mjinga. Hii inaonekana ni kitu cha kupanga. Inaonekana ulimuandaa huyo mpiga picha wako. Nipeleke kwa huyo mtu kabla sijachukua hatua mbaya kwako."

Muda wote wakiwa wanajibishana pale mlangoni, Happy alikuwa ameshakimbia baada ya kuona Masunju ametoa bastola. Akina Walari, Marare na Ramla walikua wamezunguka nyuma ya nyuma na kuchuchuma nyuma ya banda la kufugia kuku lililokuwa umbali mfupi kutoka mahala walikokuwa wamesimama Masunju na Bwire kiasi cha kusikia kila walichokuwa wakiongea.

Itaendelea...
eseeh!🙂🙂🙂🙂huu utamu umekolea sana cjui uongezee uzii kidogo bishop maan naona keshoo mbalii
 
Hii riwaya imenikumbusha wakati flani nlivyolala selo pale central Morogoro,daaah tulikuwa wengi selo ndogo chumba kichafu yani ukilala ubavu mmoja ndo usijigeuze utashangaa nafasi yako imekua occupied, selo/jela sio kuzuri kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
R.I.P Zuhura.

Pole sana Walari, piga moyo konde....maisha lazima yaendelee.
Gereza la Kifo - 24

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

"Ninapenda sana kutoa damu hata dakika hii, lakini si unajua tena siku hizi damu zetu haziaminiki? Na kusema kweli naogopa sana kupima. Majibu yakionyesha kwamba ninao (Ukimwi), si nitakufa kihoro?"
"Kwanza ninakusahihisha. Kwa vile ninakuona una afya njema, ukipima, kinachoweza kuonekana ni virusi na sio Ukimwi. Ukimwi ni ugonjwa ambao humpata mtu aliyeambukizwa virusi baada ya kupita muda. Lakini ninachojua mimi ukitoa damu, kama itakuwa chafu, ni siri ya hao waliokupima, nawe au mtu mwingine hatojua chochote, labda kama wewe mwenyewe utataka uambiwe. Na hata kukwambia, kama utapenda kujua, kama mambo si mazuri, hawakurupuki tu, mpaka wakuandae kisaikolojia kupokea majibu hayo. Hilo litafuatiwa na kukupa ushauri nasaha. Nurdin kupima afya yako ni jambo jema sana rafiki yangu."

Endelea...

"Wewe ulishapima? Mbona wayajua haya!"
"Ninapima kila mara. Hata hivi mimi na mke wangu kwa sababu ya ujauzito tulishajipanga tena kupima. Inshallah, akipona janga hili tutapima, ingawa itakuwa kama ushahidi tu kwani wote tunajiamini tuko fiti. Ninamwamini mke wangu kwa kuheshimu ndoa na mimi ninajiamini pia."
Walari aliondoka akimwacha Nurdin akienda kutoa damu.
Ilikuwa asubuhi hiyo atume habari ya gereza EBC lakini badala yake alipofika kwenye ofisi yake mpya, mwandishi mwenziye ambaye ilikuwa ahamie makao makuu ya nchi muda wowote, alilazimika kumhoji na kutuma habari kuhusu kuvamiwa na majambazi. Hata hivyo, Walari katika mahojiano na mwandishi huyo wa EBC aliepuka kumtaja Masunju kama mtuhumiwa namba moja kwa sababu bado hakuwa na ushahidi wowote, na isitoshe alikuwa bado anafuatilia vipengele fulani katika habari yake kuhusu gereza.

******************************

Saa tisa na nusu mchana, madaktari waliokuwa wakimfanyia upasuaji Zuhura walitoka chumba cha upasuaji, huku Walari, Nurdin na waandishi wenziye watatu pamoja na mpangaji mwenzake wakiwa pale nje ya chumba hicho.
Madaktari hao wakiwa na nyuso za huzuni hawakusema chochote, isipokuwa dakika ileile Walari akaona wauguzi wakipita haraka wakimsukuma mkewe kwenye kitanda cha matairi kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi.
Hali ile ilimshtua sana Walari na wenzake aliokuwa nao. Alimfuata daktari mmoja na kutaka kujua maendeleo ya mkewe.
"Bado tunamtibu lakini tumeshamfanyia operesheni na tayari mtoto, kwa vile hajatimiza miezi yake, keshapelekwa kwenye chumba maalumu. Lakini mkeo hali yake ni mbaya sana na ndio hivi unaona tuko katika kujaribu kuokoa maisha yake. Mapigo yake ya moyo hayaendi vizuri."
"Kajifungua mtoto gani?"
"Ni mtoto wa kike. Mtoto anaonekana hana matatizo yoyote," alijibu daktari yule.
Baadaye Walari alielekea kwenye chumba cha mapokezi kuulizia kama kuna mtu alikuwa kalazwa katika hospitali hiyo baada ya kutobolewa na kitu chenye ncha kali kama vile mkuki.
Huko aliambiwa kwamba kulikuwa hakuna mtu kama huyo, na kisha akaonyeshwa kitabu cha orodha ya watu waliolazwa katika siku hizo.
Yule mtu wa mapokezi pia alimwambia kwamba kulikuwa na askari wawili ambao pia walikuja kuulizia mtu wa aina hiyo lakini hawakumpata.
"Nimesikia wanasema kuwa wanaelekea kwenye hospitali za watu binafsi labda akawa kalazwa huko," akajibu mtu yule wa mapokezi.

****************************

Saa 12:15 Asubuhi, Walari akiwa amembeba mwanaye, Ashraf, alikuwa anawasili katika hospitali ya Bulibuli.
Kwa siku tatu mfululizo hali ya mkewe ilikuwa bado mbaya. Licha ya jeraha la risasi na jeraha la mshono, matatizo ya moyo yalikuwa yakimsumbua sana na mara kadhaa alikuwa akipoteza fahamu.
Kutokana na hali hiyo, Walari alikuwa ameshindwa kufanya kazi na karibu muda wote alikuwa anashinda hospitali au polisi.
Baada ya kuomba ulinzi polisi akidai kwamba anahofia maisha yake, polisi walikuwa wamempuuza na hivyo Nurdin akawa amemshauri ahamie kwake kwa njia ya kificho, isijulikane analala wapi, kwani walihisi kwamba kama shambulio lile lilikuwa la 'kigaidi' na si ujambazi, basi wahusika wangeweza kuwa wanatafakari kumvamia tena Walari kwa lengo la kumuua. Hata safari zake za kwenda hospitali alikuwa akizifanya kwa uangalifu mkubwa. Alikuwa akivaa miwani ya jua na kofia pana.
Katika siku hizo tatu, Walari alianza kugundua kitu kingine. Polisi walionekana hawafuatilii chochote na wala walikuwa hawataki kumhoji Masunju ambaye Walari alimtaja kama mtuhumiwa namba moja.
Polisi sasa walibadili msimamo. Wakawa wanadai kwamba tukio lile wanaliona kama la ujambazi tu, na hivyo kulikuwa hakuna maelezo yoyote ya maana ya kuwafanya polisi wafikie hatua ya kumhoji ofisa wa juu wa serikali, kama Mkuu wa Gereza kwa tuhuma za eti kumfanyia ujambazi mwandishi huyo wa habari.
Polisi walimwambia kwamba kama angekuwa ana uthibitisho wowote, kama vile Masunju kudondosha kitambulisho chake cha kazi katika eneo la tukio, pengine wangefikiria kumhoji lakini hakuwa na ushahidi wa aina hiyo.
Wakamweleza kuwa hawawezi kufanya kazi kwa hisia ama kuridhisha tu matakwa yake.
Alipowaambia kuwa ana ushahidi wa maneno aliyomrekodi ofisa huyo wa magereza, polisi wale wakacheka wakasema huo hautoshi kuthibitisha kwamba yeye Masunju atakuwa kamkodia majambazi na kwamba anaweza kuiga sauti yake na kuirekodi.
Pia walimjibu kwamba hawajasikia mtu yeyote aliyelazwa hospitalini kwa kupigwa mkuki. Lakini Walari aligundua kuwa polisi walikuwa hawajazungukia mahospitali ya binafsi kama walivyoahidi siku walipokwenda hospital ya mkoa.
Wauguzi wawili walimkaribisha mwandishi huyo ambaye asubuhi hiyo hakuwa ameandamana na rafiki yake Nurdin isipokuwa shemejiye, yaani mke wa Nurdin, ambaye alikuwa kabeba kifungua kinywa kwa ajili ya mgonjwa wao.
"Leo mgonjwa wako kalala na hali mbaya zaidi," akasema muuguzi mmoja baada ya Walari kuwasili pale wodini.
"Usiku wa leo kwa kweli hakulala na pengine asubuhi hii tutamrudisha kule kwenye wodi ya wagonjwa mahututi ambako ataungwa kwenye vifaa vya kumsaidia kupumua."
Taarifa hizo za muuguzi alizisikia kama zinachoma maini yake kama upanga. Jana yake alikuwa ameona matumaini ya mkewe kupona yanarejea baada ya kuonekana ana hali njema na akiongea kidogo, tofauti na siku za nyuma, hali iliyosababisha atolewe kwenye wodi ya wagonjwa mahututi na kuletwa ile ya kawaida.
Walari alikwenda kwenye kitanda cha mkewe na kumkuta akigugumia kwa maumivu. "Nakufa. Nakufa... Nakufa bila kumbeba mwanangu mchanga," akawa analalamika mwanamke huyo Walari akiwa kainama pale kitandani.
Mwandishi huyo wa habari, akiwa na mwanae Ashraf pembeni, alimshika mkewe kifuani kisha akamwita kwa sauti ya chini.
Mkewe ambaye alikuwa akionekana mwenye maumivu makali alifumbua macho na kumtazama mumewe.
"Mume wangu, sidhani kama nitapona... Nasikia vibaya sana. Ninakuomba uwaangalie watoto. Naomba sana uchague mwanamke mwingine wa kuoa ambaye atajali watoto wetu. Usikurupuke kuoa mwanamke atakayetesa watoto. Usiache ibada. Usiache kuniombea kila unaposwali," akasema mwanamke yule kwa taabu.
"Usiseme hivyo, Zuhura, Inshallah Mwenyezi Mungu atakunusuru na kifo," alisema Walari akiwa bado kamwinamia mkewe na kuomba dua pamoja na kumsomea mkewe Qur’an ili Mwenyezi Mungu Mlezi amfanyie wepesi. Pembeni mwake akiwa kasimama mke wa Nurdin, maarufu kama mama Hadija, sasa akiwa ametua chini ule mzigo wake wa kifungua kinywa aliokuja nao kwa ajili ya mgonjwa huyo.
Zuhura alitaka kuongea kitu lakini akashindwa. Jasho likawa linamtoka kwa wingi kwenye paji la uso.
Alinyoosha mkono kwa taabu na hatimaye akafanikiwa kusema, "mwanangu Ashraf, sogea nikuage...."
Alimshika kichwani mtoto huyo ambaye alikuwa amesogea karibu na kitanda cha mama yake. Akataka kuongea maneno mengine lakini akashindwa. Akafanikiwa kusema maneno ya Kiarabu Laa ila ha-illallah (hakuna apaswaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja) Akashtuka kidogo na mara mkono wake ukalegea ukiwa bado juu ya kichwa cha mwanae.
Walari alimshika kifuani. Moyo ulikuwa umesimama kusukuma damu kuashiria kwamba uhai ulikuwa umemtoka mwanamke huyo mswalihina. Tena kifo hicho kilikuwa kimempata siku chache kabla hajaanza kufunga mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Walari hakutaka aamini kwamba Zuhura alikuwa ameshindwa kupambana na kifo. Aliamini kwamba muda wowote Mwenyezi Mungu anaweza kufanya maajabu yake mkewe akarudishiwa uhai wake.
Mwandishi huyo alibaki ameduwaa akitazama mwili wa mkewe pale juu ya kitanda huku mkono wake ukiwa bado umenyooka juu ya kichwa cha mtoto wao Ashraf.
Alijaribu kumwita. Mwanamke yule hakuitika. Akamwita huku akimtikisa lakini mwanamke yule hakuitika.
"Mpenzi Zuhura, usife tafadhali... Zuhura usife," akawa anasema Walari akiutingisha mwili wa mkewe pale kitandani. Lakini Zuhura, akiwa kama aliyelala usingizi hakuitika wala kutikisika.
Walari akaanza kulia kwa sauti. Yule mke wa Nurdin (Mama Hadija) alishajua kwamba Zuhura amekata roho. Alijua pia kwamba shemeji yake keshachanganyikiwa na haamini tukio lile lililotokea mbele yake.

Itaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gereza la Kifo - 58

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

Happy aliondoa vyombo mezani huku Masunju akimpiga jicho la uchu kwa jinsi alivyokuwa anatamanisha usiku huo akiwa amevaa sketi yake fupi na blauzi fupi iliiyokuwa imeacha kitovu chake nje.

Msichana huyo mrembo alimkaribisha chumbani na kisha akamwambia anatoa vyombo nje kwa ajili ya kuvisafisha baadaye.

Masunju alibaki chaumbani na ndipo Happy akachepuka haraka haraka hadi kwenye dirisha la chumba walimokuwa akina Walari na dada yake Ramla kuwaambia kwamba waje kuvamia baada ya dakika zisizozidi kumi.

Wakati yule kijana aliyejifanya mchumba wa Happy hakuwa na wasiwasi wowote kuanza safari ya kwenda kumvamia Masunju, yule mpiga picha alianza kuogopa.

Endelea...

"Huyu mtu kweli hana bastola? Mimi naogopa bwana," akasema yule mpiga picha.

Wakati dakika kumi alizokuwa amewapa Happy zinaisha bado Ramla, Walari na Marare walikuwa wakimbembeleza yule mpiga picha asiogope lakini ilishindikana licha ya kumwongezea pesa kutoka sh. 40,000 walizokuwa wamemuahidi awali hadi sh. 60,000.

Ingawa Walari na Marare walipanga wawe wakishuhudia kwa mbali, lakini ilibidi sasa Marare aamue kuchukua kamera ya yule mpiga picha wa mtaani kwenda.

Yule kijana aliyepanga kujifanya mchumba wa Happy, akiwa hana wasiwasi alitangulia na alipofika akasukuma mlango wa kuingilia sebuleni na moja kwa moja akasukuma ule wa chumba walimokuwa Masunju na Happy. Happy alikuwa ameacha kuufunga kwa makusudi.

Masunju ambaye alikuwa uchi wa mnyama, huku akiwa amemkumbatia Happy ambaye alikuwa akijifanya yuko katika harakati za kuvua nguo, alishituka sana.

Happy alikurupuka na kwenda kupiga magoti akimwomba samahani yule 'mchumba' wake.

Masunju akiwa amechanganyikiwa alitaka kuchukua nguo zake alizokuwa amezitunduka ukutani haraka haraka, lakini yule 'mchumba' akaziwahi na kuzirusha nje ya chumba huku akimzuia kwa nguvu asitoke.

‘Mchumba’ huyo, akaanza kumhoji inakuwaje anafanya mapenzi na mchumba wake, wakati yeye yuko katika harakati za kufunga ndoa na msichana huyo na sasa walikuwa wanahesabu miezi tu.

Masunju, akiwa bado uchi alimuomba msamaha yule kijana huku akinyanyuka na kumuomba amuache achukue nguo zake na kwamba hilo suala wangelimaliza.

Yule kijana akiwa amekasirika 'sana' alitaka ampe maelezo ya kuridhisha kwa kitendo cha kumrubuni mchumba wake wakati yeye Masunju ana mke.

"Utakuwa mtu mshenzi sana wewe. Bila shaka wewe ni mpenzi wa shemeji Ramla na mimi nilishakuona unakuja hapa hapa mara kwa mara kwa dada yake huyu mchumba wangu. Huwa tunapishana tu. Sasa inakuwaje tena unamchukua mdogo wake ambaye ni mchumba wangu mimi?" Akawa anafoka kijana huyo aitwaye Bwire kwa hasira.

"Kijana samahani sana. Punguza hasira. Tutayamaliza tu kijana. Naomba sana unirudishie nguo zangu nivae," aliomba Masunju.

"Sikubali. Nimeshamhangaikia sana huyu binti. Unajua hasa aliyekuwa akimlipia karo ya shule ni nani? Si unajua hawa mabinti ni yatima?" Akazidi kufoka Bwire huku akina Walari waliokuwa nyuma ya dirisha wakisikia.

"Kijana tutayamaliza tu," akaomba Masunju huku sasa Happy akiwa amemgeukia kwa kumlaumu kwamba amemponza kuhusu mchumba wake na dada yake akipata habari hizo atamfukuza.

Masunju akazidi kumsihi Bwire ampe nguo zake, halafu wamalizane na sasa akamtaka atamke pesa anazotaka. Bwire huku akifunga mlango wa chumba kwa komeo alitoka kama vile anamleta nguo zake alizokuwa amezirusha sebuleni.

Alienda kumchukua Marare ili aje kumpiga picha Masunju. Marare alilazimika kuvaa kofia walioiazima haraka haraka ili kujaribu kuficha sura yake Masunju asimtambue.

Walipoingia mule chumbani ambako Masunju alikuwa bado ameketi kitandani akiwa uchi wa mnyama Marare ambaye alikuwa ameandaa tayari kamera akampiga haraka haraka picha.

Masunju aliposhituka kwamba anapigwa picha alisimama haraka haraka na kujaribu kuficha sura yake huku pia akifunika sehemu zake za siri kwa viganja. Baadaye akafanikiwa kuvuta shuka iliyokuwa kitandani lakini alikuwa ameshachelewa. Marare alikuwa keshampiga picha kadhaa na kutoka nje haraka, akimwacha Bwire akiendelea kuzozana na Masunju ambaye sasa alikua amechanganyikiwa.

Sasa Masunju alianza kugomba kuhusu suala la kupigwa picha, lakini Bwire akamjibu kwa jeuri kwamba ni lazima ampige ili kuweka ushahidi atakapokuwa anadai pesa zake nyingi ambazo ameshamgharimia Happy.

Masunju alizidi kumsihi kijana yule amsamehe, kisha ampe mkanda wa picha alizopigwa huku akiahidi kumpa gari dogo aina ya Toyota Carina pamoja pesa taslimu shilingi milioni moja.

"Mzee, mimi sasa ninakuruhusu uende zako, mambo ya pesa na gari tutaongea siku nyingine kadri tutakavyoafikiana na mchumba wangu kuhusu kadhia hii," akasema Bwire huku akitoka nje ya chumba ambako alichukua nguo za Masunju na kumrushia pale kitandani.

Mwanamume yule menene, Masunju alivaa haraka haraka, tena akiwa amesahau nguo ya ndani ambayo, Happy toka mapema, alikuwa amesukuma uvunguni mwa kitanda bila Masunju kufahamu.

Bwire, huku mawazoni akiingiwa na uchu wa gari, alizidi kumwambia Masunju kwa kiburi kwamba suala la kupeana pesa au gari wangelizungumzia siku nyingine ndipo ampe mkanda wa picha zake.

Masunju alizidi kubembeleza lakini Bwire alikataa na kutoka nje ambako kulikuwa na giza. Happy alikuwa amezima taa ya nje makusudi.

Masunju naye alitoka akizidi kumbembeleza Bwire ambaye alikuwa amesimama nje karibu na mlango. Akamsihi sana ampe mkanda wa picha aliyopigwa.

"Mzee, nimeshakwambia mkanda huupati leo. Kwanza mpiga picha mwenye ameshaondoka zake," akajibu Bwire.

"Kwenda wapi?"

"Kwenda kwake mzee. Wewe huoni huu ni usiku?"

Ghafla Masunju alichomoa bastola ambayo ilikuwa kwenye nguo zake na kumgusisha nayo Bwire kwenye paji la uso. Hicho ni kitu ambacho Bwire alikuwa hakukifikiria.

"Sasa kijana ninakuua ukileta masihara. Nimekupa kila ahadi hutaki kusikia. Mimi siondoki hapa bila kupata mkanda wa picha mlizopiga. Kwanza ninajiuliza huyu mpiga picha katokea wapi?" akafoka Masunju.

Bwire alivaa ujasiri na kumjibu kwamba yeye haogopi kifo wakati anapokuwa anafuatilia haki zake.

"Niue tu kama unataka. Lakini hili si suluhisho na utakuwa unajiweka katika matata zaidi. Niue kama unataka."

"Nyamaza. Mbwa wewe. Weka mikono juu la sivyo nitafumua ubongo wako sasa hivi," alifoka zaidi Masunju.

Bwire sasa alianza kuingiwa na wasi wasi huku akijilaumu ni kwa hakukagua bastola kwenye mifuko ya Masunju. Aliona yule mtu amekasirika kuzidi upeo wa kawaida na angeweza kumuua kweli.

"Sasa tuseme ndiyo unataka nikupe mkanda kwa nguvu halafu ahadi uliokuwa unainiambia ya pesa na gari ndiyo umefuta? Si ninakwambia kwamba hilo tutaliongelea siku nyingine?"

"Siwezi kuondoka hapa bila huo mkanda. Nikishaupata huo mkanda au kufuta hizo picha zote sasa tutazungumza," akasema Masunju akizidi kugandamiza mtutu wa bastola kwenye uso wake.

Bwire alizidi kuogopa.

"Naomba tuwasiliane kesho kwa sababu yule mpiga picha nilimbahatisha tu wakati nimetoka nje, lakini anakwenda kupiga picha katika ukumbi mmoja ambao kuna dansi usiku huu. Kwa hiyo ameshakwenda huko, si rahisi kumpata," akajibu Bwire.

"Bwana mdogo, usinifanye mimi mjinga. Hii inaonekana ni kitu cha kupanga. Inaonekana ulimuandaa huyo mpiga picha wako. Nipeleke kwa huyo mtu kabla sijachukua hatua mbaya kwako."

Muda wote wakiwa wanajibishana pale mlangoni, Happy alikuwa ameshakimbia baada ya kuona Masunju ametoa bastola. Akina Walari, Marare na Ramla walikua wamezunguka nyuma ya nyuma na kuchuchuma nyuma ya banda la kufugia kuku lililokuwa umbali mfupi kutoka mahala walikokuwa wamesimama Masunju na Bwire kiasi cha kusikia kila walichokuwa wakiongea.

Itaendelea...
Shukrani Bishop.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom