Riwaya - Gereza la Kifo

Riwaya - Gereza la Kifo

Safi sana stori ilikuwa nzuri
Gereza la Kifo - 59

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

"Bwana mdogo, usinifanye mimi mjinga. Hii inaonekana ni kitu cha kupanga. Inaonekana ulimuandaa huyo mpiga picha wako. Nipeleke kwa huyo mtu kabla sijachukua hatua mbaya kwako."

Muda wote wakiwa wanajibishana pale mlangoni, Happy alikuwa ameshakimbia baada ya kuona Masunju ametoa bastola. Akina Walari, Marare na Ramla walikua wamezunguka nyuma ya nyuma na kuchuchuma nyuma ya banda la kufugia kuku lililokuwa umbali mfupi kutoka mahala walikokuwa wamesimama Masunju na Bwire kiasi cha kusikia kila walichokuwa wakiongea.

Endelea...

Walijadiliana pale kama ilikuwa inafaa Ramla ajitokeze kama inaweza kumuokoa Bwire, lakini wakaona itaacha maswali zaidi kwa Masunju.

Baadaye waliona kivuli cha Bwire na Masunju wakiongozana kuelekea mahala ambako Masunju alikwa ameegesha gari lake la kifahari huku bado akiwa amemteka nyara Bwire kwa kumwekea basola kisogoni.

Nao walinyatia kuelekea usawa wa gari. Wakasikia Masunju anafungua mlango wa gari na kumlazimisha Bwire kuingia kwenye gari.

Wakati Masunju akitaka kufungua mlango wa gari hilo ili waingie, Marare alikuwa ameshamkaribia na kumpiga ngwara iliyomuangusha chini mwanamume yule mnene na bastola kurika mbali.

Marare aliruka nyuma ya gari haraka na kukimbia huku Bwire naye akikimbia. Masunju alinyanyuka haraka na kufyatua risasi hovyo kuelekea mahala ambako aliona Bwire amekimbilia.

Hali ile ilitia wasi wasi watu wa eneo hilo. Kila mtu akijificha kivyake akihisi mtaa wao ulikuwa umevamiwa na majambazi usiku ule.

Masunju alirudi kwenye mlango wa Ramla na kukuta umefungwa. Alizunguka hadi kwenye banda la kuku hakuona mtu. Happy alikuwa haonekani pia.

*** *** **** *********** **********

Saa 12, jioni, siku ya nne baada ya tukio la kumwadabisha Masunju kuhusu tabia zake za uhuni, Walari alikuwa sebuleni kwake pamoja na wageni wawili, Ramla na mdogo wake Happy wakijipongeza. Marare alikuwa amesafiri asubuhi hiyo kwenda Bandaria kuendelea na kazi, pengine naye angekuwa pamoja nao. Kikubwa walichokuwa wakijadili ni namna walivyomwadabisha Masunju, kwani asubuhi hiyo hiyo magazeti mawili yalikuwa yameandika kisa cha Masunju kufumaniwa huku picha zake akiwa uchi wa mnyama, ingawa zilizibwa sehemu zake za siri, zikichapishwa.

Magazeti pia yaliandika namna mfumaniaji, Bwire, alivyotekwa nyara na Masunju kabla ya kuokolewa na majirani ambao walihojiwa na kueleza kwamba ni kweli Masunju alipiga risasi hovyo na kutisha mtaa.

Walari alikuwa na furaha nyingine. Alikuwa amepokea simu jioni hiyo kutoka gazeti la Upekuzi ambalo lilikuwa limekubali kumlipa shilingi milioni 200 kwa kumkashifu, pesa ambazo yeye aliziona ni nyingi sana. Lakini hakuwa amepanga kuwaambiwa akina Ramla kuhusu hilo. Alitaka atumie muda huo kueleza ukweli wake pia. Alikuwa amempenda Happy na alitaka amweleze kwamba anataka kumuoa.

Kabla Ramla na mdogo wake hawajaondoka, Walari aliamua kueleza ukweli wake. Happy alisema alihitaji muda kidogo wa kufikiria.

“Unajua kaka nina matumaini ya kwenda chuo kikuu. Wasiwasi wangu ni kama nitaweza kusoma sawa sawa huku nikiwa kwenye ndoa,” akasema Happy, baada ya dada yake kuamua kumzungumzia Walari kwamba ni kijana anayemfaa mdogo wake na kwamba hata yeye alikuwa anaombea hilo litokee, yaani wawili hao waoane.

“Ninavyojua miye, masomo ya chuoni hayamzuii mtu kuolewa. Labda kama una mchumba mwingine ama kama hujanipenda. Nadhani hayo ndio mambo muhimu zaidi,” akasema Walari.

“Naomba nikujibu baada ya siku mbili kaka Walari. Lakini usiwe na wasiwasi,” akasema Ramla. Baadaye Ramla na Happy waliondoka.

Saa nne usiku, wakati anajiandaa kupumzika huku akiomba dua Happy amkubali amuoe, Walari alipigiwa simu na mwandishi mwenziye pale mjini Bulibuli. Mwandishi huyo alimpa habari ambazo zilimwacha Walari mdomo wazi. Alimjulisha kwamba alikuwa nyumbani kwa Masunju kwa sababu mkuu huyo wa zamani wa gereza alikuwa amejaribu kujipiga risasi ili kujiua lakini alikuwa hajafa na kwamba alikua amekimbizwa hospitalini.

“Mimi nimepigiwa simu na jirani yake mmoja ambaye ananifahamu. Kajipigia risasi bafuni saa moja jioni na hali yake ni mbaya sana,” akasema yule mwandishi wa habari.

Walari aliona hiyo ni habari ambayo alitakiwa kuifuatilia na kuituma usiku huo huo London yaliko makao makuu ya chombo alichokuwa akikifanyia kazi. Alimuita msichana aliyekuwa akimsaidia kazi na kumuomba alale na mwanae Nadhifu.

Kabla ya kuondoka aliamua kumpigia simu Ramla kumweleza habari hizo za Masunju kujitwanga risasi na hali yake kuwa mbaya.

“Nimeachana na mdogo wangu sasa hivi kaenda kulala. Wakati tunatafakari hilo la huyo mtu muovu naomba ujiandae tu kwa harusi. Mdogo wangu ameniambia amekubali kuolewa na wewe. Mimi nimefurahi sana.”

Walari alijisikia furaha wakati akikata simu. Akatulia kidogo akitafakari kisha akatoka nje kwenda kazini.

************

Walikuwa wanajadili jinsi harusi yao itakavyokuwa. Happy akiwa anataka harusi kubwa lakini Walari akipinga, kwani yeye alitaka ndoa tu ndogo. Hii ilikuwa baada ya Walari kuanza kumbadilisha Happy mtazamo wa kimaisha ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi yanayokubalika katika Uislamu.

Wakati wanaendelea kujadili, simu ya Walari iliita. Akajulishwa na mtu aliyejitambulisha kama msaidizi wa Rais mpya, Makomeo John (MJ), ambaye alikuwa na mwezi tu tangu aingie madarakani lakini akawa ameshafanya makubwa ambayo wengine huyafanya ndani ya miaka mitano, kwamba anahitajika Ikulu mara moja.

“Kesho asubuhi unatakiwa kufika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa hapo Bulibuli ambaye atakupa taratibu za kusafiri kuja Bandaria kwa ndege,” akasema Msaidizi yule wa Rais.

Habari zile zilimshangaza sana Walari na akawa hajui anaitiwa nini na mhesimiwa Rais ambaye katika kipindi kifupi, alikuwa ameshaanza kuwa gumzo nchi nzima na hata nje ya mipaka. Alikuwa amefanya ziara za kushitukiza katika taasisi kadhaa za umma, kurekebisha mambo na kufukuza viongozi wa taasisi zilizoonekana zina matatizo.

Muda mfupi baadaye taarifa kutoka Ikulu ilizagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Rais MJ alikuwa ameagiza Masunju ambaye alikuwa bado hospitalini na hali yake ikiimarika awekwe chini ya ulinzi na mali zake zote kushikiliwa na serikali wakati maandalizi yakifanywa ili kumfikisha mahakamani.

Katika taarifa hiyo ya rais kulikuwa na wakurugenzi wengine kadhaa wa taasisi za umma ambao rais alikuwa amewaondoa madarakani kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za utendaji mbovu na ufisadi.

Habari zile zilimfurahisha sana Walari ingawa aliendelea kutojua nini hasa anachoitiwa na rais mtu mdogo kama yeye. Lakini kutokana na hatua ambayo sasa ilikuwa inachukuliwa na serikali, alihisi Rais alitaka kumsikiliza kwa kina kuhusu habari za Masunju pamoja na vielelezo alivyo navyo.

*************

Walari aliwasili Ikulu saa 11:00 jioni na kutakiwa kwenda moja kwa moja kuonana na Rais Makomeo John. Rais, baada ya kumkaribisha mwandishi huyo kijana na kufanya naye mazungumzo mafupi, alimpongeza kwa ushupavu wake katika fani ya habari na kisha akamjulisha kwamba ameamua kumteua kuwa mbunge katika nafasi zake 10 na pia Naibu Waziri wa Habari. Walari alijikuta amechanganyikiwa kuambiwa nafasi hiyo ambayo hata siku moja hakuwahi kuifikiria.

"Mheshimiwa, ninakushuruku sana kwa hili jukumu unalotaka kunipa, lakini nina mashaka kama ninaliweza kwa sababu mimi siyo mwanasiasa."

"Kijana wangu, nina hakika utaliweza. Katika baraza langu ninataka watu wanaochukia rushwa kwa dhati kama wewe na walio tayari kuitumikia nchi yao kwa dhati hata kama ni kutoa uhai wao kwa jili ya nchi yao. Nimekufuatilia na kugundua kwamba unafaa kutumikia nchi yako katika nafasi hiyo. Kwa hiyo, ili kukidhi matakwa ya Katiba, kama nilivyosema nitakuteua kuwa mbunge kwa nafasi zangu nilizo nazo na pia naibu waziri."

Walari alikubali japo alikuwa bado ana hofu kuhusu jukumu hilo zito la uongozi ambalo Rais alikuwa amedhamiria kumkabidhi. Alijikuta machungu yote aliyopitia kutokana na kadhia ya Masunju yakitoweka.

Vitu viwili vikubwa kwake ambavyo hakuwa amevitazamia vilikuwa vimemtokea kwa muda mfupi; kupata mchumba mrembo, Happy, na kuteuliwa kuwa naibu waziri na mheshimiwa rais.

Alimshukuru Rais kwa kumuona anafaa kuchukua nafasi hiyo na kuahidi kuitendea haki.

Aliondoka Ikulu huku akiwaza sana kuhusu mzigo mkubwa aliokuwa ametishwa. Alijiuliza kama atamudu kuonesha uadilifu na kutenda haki kwa kiwango kinachotakiwa.

Alilikumbuka shairi alilotunga akiwa jela na kulighani huku akitafakari kila msitari hususani beti za mwisho za shairi hilo zilizosema:

Uongozi ni huruma, umma wasaze minofu
Kila anayelalama, tatizole kusanifu
Kutanguliza heshima, kwa watu hata pumbafu
Chagua waadilifu, nchi iende salama.

Uongozi kubwa dhima, kwa Mwenyezi Mtukufu
Siku ile ya Kiyama, tutahojiwa kwa safu
Watatupwa jehanama, waloongoza kwa rafu
Chagua waadilifu, nchi iende salama.

Huacha alama njema, kiongozi mwadilifu
Yule anayesimama, haki kutoikalifu
Mwanga wake unachoma, hata akishastafu
Chagua waadilifu, nchi iende salama.

Nyerere, Gandhi, Nkrumah, walikuwa wanyoofu
Mandela, Karume pima, na wengi watimilifu
Wanakumbukwa kwa wema, siyo kwa zao sarafu
Chagua waadilifu, nchi iende salama.

MWISHO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aseeh!nipo nipoooo siwez kukosa yaan hapa walari ananikumbusha ile methaliiii "baada ya dhiki faraja"maana uzalendo na ujasiri wake unampelekea kula meme ya nchi...Ila mbavu zangu😀😀😀😀 kwenye hili jina la MAKOMEOOOOOOOOO
 
Nimejifunza vitu vingi.sijui Mama yake anajisikiaje?? Ni vizuri kusimamia unachokiamini.
 
Safi sana...

Mwisho mzuri...

Chapter closed...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom