Huyu walari mbona mbishiiiGereza la Kifo - 53
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
"Vipi, waandishi wa habari hawakuwepo mahakamani. Wasije kesho wakaandika kwamba nimekufa," akauliza Walari.
"Niliona waandishi wawili pale mahakamani, lakini hawajui kama kulikuwa na hii kesi ya rufaa, kwa hiyo tumejitahidi kuwakwepa. Hakuna mwandishi aliyeingia kwenye chumba cha mheshimiwa hakimu wakati wa hukumu," akajibu Marare.
"Vipi, Masunju alifika kortini kusikiliza hukumu?"
"Alikuwepo ofisa mmoja wa magereza ambaye ndiye nilimsikia nje akiongea na wakili wao kwamba kulikuwa hakuna haja ya kumkatia rufaa mtu ambaye keshakufa," akajibu Marare.
"Nina mashaka, Masunju anaweza akawaambia jamaa wa gazeti la Upekuzi kwamba nimekufa."
"Ngoja tusubiri Jumamosi tuone litatoka na nini," akajibu Marare.
Endelea...
"Sasa tupange namna ya kumlipua Masunju. Ninataka wiki hii hii mambo yake yawe nje," akasema Walari.
"Loh! Usiwe na haraka, Walari. Mimi nilikuwa nashauri kwamba kwanza tusubiri hadi muda wa kukata rufaa upite hapo ndipo uibuke."
"Mimi sioni tatizo kwa sababu mahakama imeshaniachia huru. Sasa kuna nini tena cha kuogopa?"
"Hapana mwanangu," akaingilia mama yake. "Unatakiwa uendelee kujificha. Na kwa kweli utanishangaza sana kama utaendelea kumfuatilia huyu Mkuu wa Gereza."
"Kuhusu kumfuatilia Masunju nimeshamaliza mama. Kila kitu ninacho na nilivyofungwa imeniongezea mengi. Kilichobaki mimi ni kuueleza umma hali halisi tu, basi," akajibu Walari.
"Mwanangu, achana kabisa na huyu mtu. Kama unafahamu mimi ni mama yako tafadhali nisikilize. Achana kabisa na huyu Masunju. Achana naye kabisa. Anachosema mkubwa usikidharau."
"Mama, kwa kweli sitawatendea haki wananchi na mimi mwenyewe sitajitendea haki kama sitayatoa hadharani mambo yanayotokea gerezani. Watu wanataabika. Mama, huko watu wanakufa si mchezo," akajibu Walari.
"Lakini rafiki yangu mimi sikushauri kabisa kujitokeza sasa hivi. Ni mapema mno. Wewe tulia tu hata miezi mitano, halafu utaibuka na kueleza ukweli ulio nao," akajibu Marare.
"Miezi mitano mingi sana, hata mmoja tu naona siwezi. Mwezi ujao huenda Masunju atakuwa ameshateuliwa na chama tawala kama mgombea ubunge. Mimi ninataka niandike habari zake mbaya akiwa bado hajaondoka gerezani kwenda kwenye siasa. Si mnajua siasa zetu siku hizi zinatawaliwa na rushwa. Kwa pesa zake, Masunju anaweza kushinda ubunge. Mimi roho itaniuma sana kama mtu huyu anachaguliwa kuwa mwakilishi wa wananchi. Atawakilisha kitu gani. Anaweza kweli akazungumzia shida za wanyonge? Huyu atakuwa mtu wa kuzungumzia magari ya kifahari kwa ajili ya wabunge na posho zao tu. Kwanza ninahisi kuna anachokitafuta bungeni, kama si kutegemea kupewa uwaziri, basi anataka ubunge uwe ukimpa kinga ya kufanya biashara zake haramu, amini msiamini."
"Wewe mwanangu, kuna mbunge hovyo kama yule wa jimboni kwetu? Mbona anashinda tu kila mwaka kwa kuhonga. Hata kama si Masunju atakayechaguliwa, anaweza kuja mbunge mwingine anayeweza kuwa mbovu zaidi," akasema mama yake Walari na kuongezea kwamba yeye Walari hana cha kupoteza wala kufaidi kwa mtu yeyote atakayechaguliwa kama mbunge.
Mama huyo akazidi kusema: "Sidhani kama siku hizi kuna mbunge ambaye anagombea nafasi kwa ajili ya kukerwa na kero za watu. Wengi wanatafuta kura za kula tu."
Walari hakutaka kuendelea kubishana na mama yake kwa sababu alishajua mawazo ya baadhi ya watu kama yeye ambao huamini mbunge hana msaada wowote kwa maisha yao. Wengi pia wanadhani kwamba wabunge wengi wapo kwa ajili ya kula na kusaka maisha yao binafsi.
Lakini Walari aliamini kwamba kama wananchi watakuwa makini na kuchagua wabunge wenye hofu ya Mungu na walio tayari katika kuwahudumia wananchi na siyo matumbo yao, wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya taifa lao.
Baadaye Marare aliaga kuondoka lakini Walari alimuuliza tena ni muda gani mwafaka anadhani atakuwa tayari kumhoji kwa ajili ya kutoa hadharani hali halisi ya gereza la Bulibuli.
"Sikiliza Walari, mbona nimeshakwambia kwamba inatakiwa kwanza utulie na hasa ujifiche ili tuone mambo yanavyokwenda?"
"Lakini si nimekueleza kwamba mimi sioni cha kuogopa hapa kwa sababu mimi tayari ni mtu huru. Kwamba nilifufukaje baada ya kupelekwa chumba cha maiti, hicho ni kitu ambacho tutakitengenezea maelezo baadaye."
"Sikiliza Walari, ni kweli kabisa umeachiwa huru na mahakama, lakini lazima uelewe kwamba hapa kuna masuala mawili ambayo ni vyema kuyazingatia. Mtu anaweza kujenga hoja kwamba ulitoroka ukiwa chini ya kifungo kitu ambacho ni kosa hata kama ulishinda baadaye kesi iliyosababisha kifungo hicho. Mimi ninapata hisia hizo ingawa sina hakika kwa sababu si mwanasheria. Labda vumilia tutawasiliana na Mwanasheria wetu, Dickson Mafuru, ili atupe ushauri wa kisheria. Suala la pili, na hii ninarudia tena, Masunju akiamini kwamba upo hai lazima atakata rufaa kwa sababu siku za kukata rufaa hazijaisha, na kwa silaha yake ya fedha, anaweza akashinda. Lakini hata kama si kupitia sheria, Masunju ni mtu hatari. Anaweza akatafuta mbinu nyingine ya kukumaliza."
"Lakini wewe Walari," akadakia mama yake, "Hivi umechanganyikiwa? Mimi naona kuna walichokufanya huko jela. Kichwa chako bila shaka hakiko salama."
"Wala sina tatizo lolote mama zaidi ya uchungu na hasira nilizonazo dhidi ya hawa wadhalimu. Kwa kweli, kama haya mambo yatakuwa hadharani, wananchi wakajua hali halisi ya gerezani hapo, mimi nitakuwa sasa niko tayari hata kufa."
"Ndiyo maana nasema kichwa chako hakiko salama. Yaani uko tayari kufa kwa kitu ambacho wewe wala familia yako hawatokuwa na faida nacho?"
"Mama, kuna wakati, ili mambo fulani mabaya yanayofanywa na wenye mamlaka yarekebishwe, inabidi watu wengine wajitolee mhanga kuteseka hadi kufa kwa ajili ya kuviletea unafuu vizazi vijavyo."
Alikohoa kidogo kisha akaendelea, "Nchi hii na zingine za Kiafrika kama viongozi waliotuletea uhuru wasingekuwa tayari kujitolea mhanga kupambana na wakoloni na kujiweka katika hatari ya kufungwa na kuuawa, pengine tungekuwa hatujapata uhuru, au tungechelewa sana kuupata. Sasa hivi tuna uhuru, lakini kuna watu wamepewa madaraka ambayo wanayatumia vibaya na kuleta maafa makubwa kwa jamii. Wengine ni wabaya hata kuliko wakoloni. Lazima watu wajitokeze kupambana na watu kama hawa, hata kama ni kwa gharama ya maisha yao."
"Msimamo wako huo ndiyo umesababisha maafa ya mkeo na mwanao. Achana nao mwanangu. Mimi nashauri ukapumzike kwa shangazi yako, Mama Sumuni, hadi hali itakavyokuwa shwari."
"Nikapumzike nini? Mimi siondoki hapa Bulibuli. Ili nitulie lazima kwanza nitumie taaluma yangu kuwaambia wananchi madhambi ya Masunju. Hapo ndipo ninaweza nikapumua na kupumzika. Labda kesho mimi nitakuja nyumbani kijijini kumuona mwanagu, kisha niendelee na mapambano yangu."
Walari alikumbuka jambo lingine ambalo alikuwa akisahau kumweleza Marare, kwamba kwa mujibuwa Ramla, na yeye alikuwa akipania kumfanyiwa jambo baya na Masunjhi na hivyo akamtaka awe akijihadhari.
“Lakini naamini tatizo hapa lilikuwa ni mimi. Kwa kusikia nimekufa, nadhani ugomvi wake kwako pia utakuwa umekoma.”
“Ndio maana tunakutaka kwanza utulie. Hata kwenda kumuona mwanao pia sishauri kwenda. Tulia kwanza Walari,” alisema Marare.
****** ******
Ukumbi wa Idara ya Habari katika mji mkuu, Bandaria, ulikuwa umejaa waandishi wa habari pamoja na wanachi wachache wa kawaida. Walikuwa wamekuja kumsikiliza mwandishi wa habari ambaye kiasi cha mwezi na nusu uliokuwa umepita alikuwa ameripotiwa na gazeti la UPEKUZI alilokuwa akiliandikia zamani kwamba alifia jela alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano cha kuuzia wafungwa bangi.
Gazeti hilo, hata hivyo, halikuandika kuhusu mwandishi huyo kushinda rufaa dhidi ya kesi hiyo na kukanusha habari yake ya kwanza kwamba alifia jela.
Walari, akiwa ameandamana na Madenge Marare waliingia katika ukumbi huo saa nne kasoro dakika nane asubuhi. Afya yake ilikuwa imeanza kurudi kidogo, tofauti na wakati anatoroka jela.
Itaendelea...
lazima raia wamumwage...kapita kwenye chama tawala pekee..asubiri kupambana na ukawa...Kwahiyo masunju anashinda ubunge
Hahaa...lazima raia wamumwage...kapita kwenye chama tawala pekee..asubiri kupambana na ukawa...
Bora iwe hivyolazima raia wamumwage...kapita kwenye chama tawala pekee..asubiri kupambana na ukawa...
Gereza la Kifo - 55
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Saa moja aliyokuwa amepewa na watu wa ukumbi huo ilikuwa imeisha lakini Walari bado alikuwa na mengi ya kueleza na ndipo wahusika wakamuongezea muda. Hata hivyo, masimulizi yake yalikuwa yanasisimua sana na kuwasonenesha wengi. Pengine ilikuwa ni mara ya kwanza kuona waandishi wakifuta machozi kwa kumsikiliza mtoa habari, hata kama alikuwa mwanahabari mwenzao!
Endelea...
Huku maneno yake yaliyoambatana na ushahidi yakionekana kuwachoma vilivyo waandishi wa habari waliokuwa wametulia tuli wakimsikiliza, Walari aliendelea kusimulia. Akaeleza namna alivyokwenda kijijini kwao kwa ajili ya kuhani msiba wa mkewe na mambo yaliyomkuta huko, hususani tukio la banda walimokuwa wamelala kuchomwa moto na namna mtuhumiwa wa tukio hilo alivyoachiwa huru na polisi katika mazingira ya kutatanisha. Akaeleza pia jinsi askari aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo alivyohamishwa ghafla.
"Mwandishi yeyote, anaweza akaenda kwenye hiki kituo atakuta ukweli huu, kwamba hii kesi ilikuwa inapelelezwa na askari polisi aitwaye Sumuni lakini alihamishwa ghafla na mfungwa alitoroshwa. Nasema alitoroshwa kwa sababu hakukuwa na juhudi zozote za kumtafuta," akasema, waandishi wa habari wakizidi kumtumbulia macho kwa mshangao.
Kilichowaacha hoi waandishi wengi ni masimulizi yake kuhusu namna alivyokamatwa akienda kukamilisha habari yake ya uchunguzi katika kiwanda cha mafuta na sabuni kinachomilikiwa kwa ubia baina ya Masunju, Mkuu wa jeshi la Polisi wa Bulibuli na gereza.
Akaeleza namna alivyoteswa na hadi kufungwa katika kesi iliyopelekwa haraka haraka sana.
"Hakimu aliyenifunga alidai nimepatikana na hatia ya kuingia kwa jinai na kuongea na mfungwa bila ruhusa kinyume cha sheria, lakini gazeti la Upekuzi, kuonyesha namna lilivyokuwa na chuki na mimi, bila hata kuthamini mchango wangu niliokuwa ninautoa kwa moyo mmoja, lenyewe likaandika kwamba nimepatikana na hatia ya kuuzia bangi wafungwa. Nitalishitaki pia hili gazeti kwa hilo," akasisitiza Walari na kutoa nakala ya hukumu hiyo ambayo baadaye ilitenguliwa na mahakama ya rufaa. Pia Walari akaeleza namna Upekuzi lilivyoandika kwamba 'mwandishi aliyefungwa kwa kuuzia wafungwa bangi kafa' wakati yeye hajafungwa kwa kosa hilo.
Ndipo sasa ikaja sehemu ambayo wengi walitaka kusikia; namna alivyokufa na kufufuka!
Walari aliamua kueleza siri aliyoipata kwamba kulikuwa na mpango wa kumuua kabla ya hukumu ya rufaa yake.
Hata hivyo, kwa kuchelea kumweka kwenye matatizo Ramla na yule mhudumu wa chumba cha maiti, ikabidi alazimike kutoeleza kwa kina kuhusu namna ambavyo alitoroka hospitali huku pia akilazimika kutoleza kwa kina sakata zima kwa kile alichosema ni sababu za kiusalama kwa wale waliomsaidia.
"Nisingependa sana kuzungumzia suala hili lakini ukweli ni kwamba kuna watu walio karibu na Masunju walioamua kunionea huruma na kunieleza mpango uliokuwepo wa kuniua kabla ya hukumu. Ni watu hao hao walionitorosha wodini kwa kughushi kwamba nimekufa. Kuna mtu asiye na ndugu alikufa siku hiyo, kwa hiyo maiti yake ikabandikwa jina langu na kuvishwa nguo zangu. Mimi nikatoroshwa," akasema Walari na kusisitiza kwamba, kama maovu ya Masunju yatakuwa yamefichuka kwa kuwafikia wananchi, yeye hana wasi wasi wa kushitakiwa tena kwa kosa la kutoroka jela katika kesi ya kubambikwa, ambayo hata hivyo, alishinda rufani yake.
Baada ya maelezo marefu ya Walari, baadhi ya waandishi walionekana wakifuta machozi kwa kusikitika kuhusu madhila yaliyompata mwandishi mwenzao huyo.
Wengi pia walimpa mkono wakimpongeza kwa ujasiri wake na kumtakia maisha mema. Viongozi wa chama kimoja cha waandishi wa habari waliahidi kukutana haraka ili kuchunguza adha alizopata mwandishi huyo na kumchunguza mhariri wa gazeti la Upekuzi kwa tuhuma za kupokea rushwa na kumtumbukiza mwandishi wake katika majanga. Waliazimia kukomesha tabia kama hiyo katika vyombo vya habari.
***************** ******
Wiki moja ilikuwa imepita toka Walari alipokuwa ameeleza mkasa wake na kusababisha maongezi ya watu karibu nchi nzima kutawaliwa na tukio la mwandishi huyo. Ukitoa magazeti machache likiwemo la Upekuzi, magazeti mengi yalifululiza kuandika tahariri zilizotokana na kisa cha Walari.
Magazeti mengi yalishauri iundwe kamati kumchunguza Masunju kuhusu tuhuma za kusababisha vifo vya wafungwa wengi katika gereza lake pamoja na kumbambikia mwandishi huyo wa habari kesi, kuchunguza kifo cha mke wa mwandishi huyo na kisha kumchukulia hatua za kisheria.
Pia ilishauriwa serikali kufanya marekebisho katika magereza na vituo vya polisi nchi nzima. Mkuu wa Polisi wa Bulibuli pia aliguswa na tahariri mbalimbali akitakiwa ajiuzulu sambamba na kuchukuliwa hatua.
Hata hivyo, Masunju aliendelea kutoguswa, licha ya wananchi kila kukicha gumzo likiwa ni juu yake.
Masunju alikuwa ametoa taarifa kwenye gezeti la Upekuzi na Radio moja binafsi akikanusha maelezo ya Walari akidai kwamba anatumiwa tu na wapinzani wake wa kisiasa, hususani katika kipindi hicho cha kampeni.
Masunju pia alikuwa ametishia kuvishitaki vyombo vyote vya habari vilivyoandika maelezo ya Walari.
Hatimaye, mgombea huyo wa ubunge aliyekuwa amemwaga pesa nyingi ili achaguliwe katika kura za maoni za chama chake kila alikokuwa anakwenda alikuwa akiangaliwa kwa jicho baya na wakati mwingine kuzomewa, aliamua kusitisha kampeni zake akisingizia kwamba alikuwa anaumwa.
Licha ya serikali kuendelea kutomchukulia hatua Masunju wala kuunda kamati ya kuchunguza mambo yaliyokuwa yakitokea katika gereza la Magamaga, karibu viongozi wengi wa serikali kutoka jijini Bandaria walifurika katika Manispaa ya Bulibuli na kuendesha vikao visivyokwisha.
Marekebisho makubwa yalifanywa katika gereza la Magamaga kimya kimya, huku gereza jipya likijengwa ili kupunguza msongamano. Wafungwa pia walishonewa nguo na adha ya wafungwa kubaki uchi ikawa imetoweka huku kukiwa na habari kwamba chakula na malazi ya wafungwa yalikuwa yameboreshwa maradufu takribani nchi nzima. Nguo za wafungwa ambapo awali zilikuwa kaptula ambazo kimsingi zilikuwa zikiwadhalilisha watu wazima, zilibadilishwa na kuwa suruali.
Wiki ya pili iliingia toka Walari apasue jipu. Katika wiki hiyo maofisa wa gereza la Magamaga pamoja na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Bulibuli walihamishwa. Lakini Masunju ambaye alikuwa amekabidhi madaraka ya uongozi wa gereza kwa ofisa aliyekuwa chini yake ili kugombea ubunge alikuwa hajaguswa, jambo lililoonekana kuwakera wengi.
Pamoja na kashfa hiyo, huku ndugu za watu waliofia gerezani wakijitokeza kila siku kuunga mkono maelezo ya Walari, Masunju, kutokana na pesa alizokuwa amemwaga, alichaguliwa katika kura za maoni kugombea ubunge na kuwashinda watu wawili aliokuwa anapambana nao. Tena alishinda huku siku za mwisho akiwa hafiki kwenye vikao vya kampeni kwa kuona aibu kutokana na kuangaliwa kwa jicho baya na wananchi, huku katika maeneo mengine akizomewa.
Katika mkutano mmoja ulioitishwa na wanaharakati wa haki za binadamu katika manispaa ya Bulibuli ya kutaka kufanyika kwa maboresho ya kanuni za uchaguzi, suala la Masunju ambalo halikuwepo kwenye agenda, liliibuka ghafla na wajumbe wakalaani kitendo cha ofisa huyo mwandamizi wa serikali kufanya hujuma na kusababisha vifo vya mamia ya wafungwa huku serikali ikiwa bao haionyeshi kama ingelimchukulia hatua. Pia wengi walisikitishwa na kitendo cha Masunju kuchaguliwa kugombea ubunge, licha ya kashfa nyingine ya kumwaga pesa kama hongo kwa wajumbe waliomchagua iliyokuwepo. Kashfa hii ilibuuliwa na baadhi ya wagombea waliotupwa katika kura za maoni.
Itaendelea...
Hahahaa...Mimi nikiiona avatar ya Bishop naona imekaa kama walari walari hivi kwa jinsi navyopata picha... Asante Bishop
Sent using Jamii Forums mobile app
Gereza la Kifo - 58
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Happy aliondoa vyombo mezani huku Masunju akimpiga jicho la uchu kwa jinsi alivyokuwa anatamanisha usiku huo akiwa amevaa sketi yake fupi na blauzi fupi iliiyokuwa imeacha kitovu chake nje.
Msichana huyo mrembo alimkaribisha chumbani na kisha akamwambia anatoa vyombo nje kwa ajili ya kuvisafisha baadaye.
Masunju alibaki chaumbani na ndipo Happy akachepuka haraka haraka hadi kwenye dirisha la chumba walimokuwa akina Walari na dada yake Ramla kuwaambia kwamba waje kuvamia baada ya dakika zisizozidi kumi.
Wakati yule kijana aliyejifanya mchumba wa Happy hakuwa na wasiwasi wowote kuanza safari ya kwenda kumvamia Masunju, yule mpiga picha alianza kuogopa.
Endelea...
"Huyu mtu kweli hana bastola? Mimi naogopa bwana," akasema yule mpiga picha.
Wakati dakika kumi alizokuwa amewapa Happy zinaisha bado Ramla, Walari na Marare walikuwa wakimbembeleza yule mpiga picha asiogope lakini ilishindikana licha ya kumwongezea pesa kutoka sh. 40,000 walizokuwa wamemuahidi awali hadi sh. 60,000.
Ingawa Walari na Marare walipanga wawe wakishuhudia kwa mbali, lakini ilibidi sasa Marare aamue kuchukua kamera ya yule mpiga picha wa mtaani kwenda.
Yule kijana aliyepanga kujifanya mchumba wa Happy, akiwa hana wasiwasi alitangulia na alipofika akasukuma mlango wa kuingilia sebuleni na moja kwa moja akasukuma ule wa chumba walimokuwa Masunju na Happy. Happy alikuwa ameacha kuufunga kwa makusudi.
Masunju ambaye alikuwa uchi wa mnyama, huku akiwa amemkumbatia Happy ambaye alikuwa akijifanya yuko katika harakati za kuvua nguo, alishituka sana.
Happy alikurupuka na kwenda kupiga magoti akimwomba samahani yule 'mchumba' wake.
Masunju akiwa amechanganyikiwa alitaka kuchukua nguo zake alizokuwa amezitunduka ukutani haraka haraka, lakini yule 'mchumba' akaziwahi na kuzirusha nje ya chumba huku akimzuia kwa nguvu asitoke.
‘Mchumba’ huyo, akaanza kumhoji inakuwaje anafanya mapenzi na mchumba wake, wakati yeye yuko katika harakati za kufunga ndoa na msichana huyo na sasa walikuwa wanahesabu miezi tu.
Masunju, akiwa bado uchi alimuomba msamaha yule kijana huku akinyanyuka na kumuomba amuache achukue nguo zake na kwamba hilo suala wangelimaliza.
Yule kijana akiwa amekasirika 'sana' alitaka ampe maelezo ya kuridhisha kwa kitendo cha kumrubuni mchumba wake wakati yeye Masunju ana mke.
"Utakuwa mtu mshenzi sana wewe. Bila shaka wewe ni mpenzi wa shemeji Ramla na mimi nilishakuona unakuja hapa hapa mara kwa mara kwa dada yake huyu mchumba wangu. Huwa tunapishana tu. Sasa inakuwaje tena unamchukua mdogo wake ambaye ni mchumba wangu mimi?" Akawa anafoka kijana huyo aitwaye Bwire kwa hasira.
"Kijana samahani sana. Punguza hasira. Tutayamaliza tu kijana. Naomba sana unirudishie nguo zangu nivae," aliomba Masunju.
"Sikubali. Nimeshamhangaikia sana huyu binti. Unajua hasa aliyekuwa akimlipia karo ya shule ni nani? Si unajua hawa mabinti ni yatima?" Akazidi kufoka Bwire huku akina Walari waliokuwa nyuma ya dirisha wakisikia.
"Kijana tutayamaliza tu," akaomba Masunju huku sasa Happy akiwa amemgeukia kwa kumlaumu kwamba amemponza kuhusu mchumba wake na dada yake akipata habari hizo atamfukuza.
Masunju akazidi kumsihi Bwire ampe nguo zake, halafu wamalizane na sasa akamtaka atamke pesa anazotaka. Bwire huku akifunga mlango wa chumba kwa komeo alitoka kama vile anamleta nguo zake alizokuwa amezirusha sebuleni.
Alienda kumchukua Marare ili aje kumpiga picha Masunju. Marare alilazimika kuvaa kofia walioiazima haraka haraka ili kujaribu kuficha sura yake Masunju asimtambue.
Walipoingia mule chumbani ambako Masunju alikuwa bado ameketi kitandani akiwa uchi wa mnyama Marare ambaye alikuwa ameandaa tayari kamera akampiga haraka haraka picha.
Masunju aliposhituka kwamba anapigwa picha alisimama haraka haraka na kujaribu kuficha sura yake huku pia akifunika sehemu zake za siri kwa viganja. Baadaye akafanikiwa kuvuta shuka iliyokuwa kitandani lakini alikuwa ameshachelewa. Marare alikuwa keshampiga picha kadhaa na kutoka nje haraka, akimwacha Bwire akiendelea kuzozana na Masunju ambaye sasa alikua amechanganyikiwa.
Sasa Masunju alianza kugomba kuhusu suala la kupigwa picha, lakini Bwire akamjibu kwa jeuri kwamba ni lazima ampige ili kuweka ushahidi atakapokuwa anadai pesa zake nyingi ambazo ameshamgharimia Happy.
Masunju alizidi kumsihi kijana yule amsamehe, kisha ampe mkanda wa picha alizopigwa huku akiahidi kumpa gari dogo aina ya Toyota Carina pamoja pesa taslimu shilingi milioni moja.
"Mzee, mimi sasa ninakuruhusu uende zako, mambo ya pesa na gari tutaongea siku nyingine kadri tutakavyoafikiana na mchumba wangu kuhusu kadhia hii," akasema Bwire huku akitoka nje ya chumba ambako alichukua nguo za Masunju na kumrushia pale kitandani.
Mwanamume yule menene, Masunju alivaa haraka haraka, tena akiwa amesahau nguo ya ndani ambayo, Happy toka mapema, alikuwa amesukuma uvunguni mwa kitanda bila Masunju kufahamu.
Bwire, huku mawazoni akiingiwa na uchu wa gari, alizidi kumwambia Masunju kwa kiburi kwamba suala la kupeana pesa au gari wangelizungumzia siku nyingine ndipo ampe mkanda wa picha zake.
Masunju alizidi kubembeleza lakini Bwire alikataa na kutoka nje ambako kulikuwa na giza. Happy alikuwa amezima taa ya nje makusudi.
Masunju naye alitoka akizidi kumbembeleza Bwire ambaye alikuwa amesimama nje karibu na mlango. Akamsihi sana ampe mkanda wa picha aliyopigwa.
"Mzee, nimeshakwambia mkanda huupati leo. Kwanza mpiga picha mwenye ameshaondoka zake," akajibu Bwire.
"Kwenda wapi?"
"Kwenda kwake mzee. Wewe huoni huu ni usiku?"
Ghafla Masunju alichomoa bastola ambayo ilikuwa kwenye nguo zake na kumgusisha nayo Bwire kwenye paji la uso. Hicho ni kitu ambacho Bwire alikuwa hakukifikiria.
"Sasa kijana ninakuua ukileta masihara. Nimekupa kila ahadi hutaki kusikia. Mimi siondoki hapa bila kupata mkanda wa picha mlizopiga. Kwanza ninajiuliza huyu mpiga picha katokea wapi?" akafoka Masunju.
Bwire alivaa ujasiri na kumjibu kwamba yeye haogopi kifo wakati anapokuwa anafuatilia haki zake.
"Niue tu kama unataka. Lakini hili si suluhisho na utakuwa unajiweka katika matata zaidi. Niue kama unataka."
"Nyamaza. Mbwa wewe. Weka mikono juu la sivyo nitafumua ubongo wako sasa hivi," alifoka zaidi Masunju.
Bwire sasa alianza kuingiwa na wasi wasi huku akijilaumu ni kwa hakukagua bastola kwenye mifuko ya Masunju. Aliona yule mtu amekasirika kuzidi upeo wa kawaida na angeweza kumuua kweli.
"Sasa tuseme ndiyo unataka nikupe mkanda kwa nguvu halafu ahadi uliokuwa unainiambia ya pesa na gari ndiyo umefuta? Si ninakwambia kwamba hilo tutaliongelea siku nyingine?"
"Siwezi kuondoka hapa bila huo mkanda. Nikishaupata huo mkanda au kufuta hizo picha zote sasa tutazungumza," akasema Masunju akizidi kugandamiza mtutu wa bastola kwenye uso wake.
Bwire alizidi kuogopa.
"Naomba tuwasiliane kesho kwa sababu yule mpiga picha nilimbahatisha tu wakati nimetoka nje, lakini anakwenda kupiga picha katika ukumbi mmoja ambao kuna dansi usiku huu. Kwa hiyo ameshakwenda huko, si rahisi kumpata," akajibu Bwire.
"Bwana mdogo, usinifanye mimi mjinga. Hii inaonekana ni kitu cha kupanga. Inaonekana ulimuandaa huyo mpiga picha wako. Nipeleke kwa huyo mtu kabla sijachukua hatua mbaya kwako."
Muda wote wakiwa wanajibishana pale mlangoni, Happy alikuwa ameshakimbia baada ya kuona Masunju ametoa bastola. Akina Walari, Marare na Ramla walikua wamezunguka nyuma ya nyuma na kuchuchuma nyuma ya banda la kufugia kuku lililokuwa umbali mfupi kutoka mahala walikokuwa wamesimama Masunju na Bwire kiasi cha kusikia kila walichokuwa wakiongea.
Itaendelea...